Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 719 | 720 | (Page 721) | 722 | 723 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Wawakilishi kutoka katika Mfuko wa GEPF pamoja na kampuni za PSM Archtect, M/S Interconsult Ltd na Matawana Consulting Group wakijadiliana kabla ya kutiliana saini kwa mkataba wa makubaliano katika Ujenzi wa 'Shopping mallas' katika mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Daud Msangi (alieketi kulia) pamoja na Meneja wa Mradi kutoka PSM Archtect Co Ltd,Peter Matinde wakifurahia jambo pamoja na wawakilishi kutoka taasisi zao,wakati wa kutiliana saini mkataba wa makubaliano katika Ujenzi wa 'Shopping mallas' katika mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Daud Msangi (alieketi kulia) pamoja na Meneja wa Mradi kutoka PSM Archtect Co Ltd,Peter Matinde (alieketi kushoto) wakitiliana saini mkataba wa makubaliano wa Ujenzi wa 'Shopping mallas' katika mikoa ya Morogoro na Kilimanjaro,katika ukumbi wa Mikutano wa Mfuko huo Victoria,jijini Dar es Salaam.Wanaoshuhudia toka kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji (GEPF),Festo Fute, Mkurugenzi wa Fedha (GEPF), Coster Mpagike, Mkurugenzi wa Uendeshaji (GEPF),Anselim Peter, Mhandisi Richard Shumbusho (Inerconsult) na Amedeus Chacky kutoka Matawana Consulting Group
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Daud Msangi (wa tatu kulia) pamoja na Meneja wa Mradi kutoka PSM Archtect Co Ltd,Peter Matinde wakikabidhiana rasmi mkataba wa ujenzi wa ‘shopping malls’ katika mikoa ya Kilimanjaro (Karanga) pamoja na Mkoa wa Morogoro (Kihonda) huku wakishuhudiwa na wawakilishi wao pamoja na Afisa mwandamizi wa kitengo cha manunuzi cha GEPF,Charles Mnyeti.

  0 0


  0 0

  Mapenzi yanamfanya mtoto wa senetor Michael Nsonko kutoka Nairobi Kenya na kuja katika jiji la mwanza Tanzania. Alivutiwa sana na jiji hilo nakujiona ni mwenye bahati. Je kila kiang'aacho ni Dhahabu?. Fuatilia hii kupitia mtandao .......

  Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania mtandaoni iitwayo I LOVE MWANZA au Kununua na iwe yako tembelea tovuti ya 


  Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

  0 0

  Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kushoto akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng. Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
  Kijana Daudi Essau Seme kutoka katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited kushoto akizungumza na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipotembelea mradi wa kikundi hicho wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.


  0 0

  3
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau  akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya shirika hilo na timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk. Dau alisema katika uendeshaji wa kituo hicho, Real Madrid itakua na dhamana ya kushughulikia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.
  2 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
  1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (kulia) wakibadilishana mikataba ya kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
  5
  Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya timu yake  na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kitahusisha wanafunzi 108 watakaogawanywa kwenye timu za chini ya umri wa miaka 13, 15, 17, 19, kikosi cha pili na timu ya wakubwa.
  …………………………………………………

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na klabu maarufu duniani ya Real Madrid ya Hispania wa kujenga kituo cha michezo kwa ajili ya kuzalisha vipaji. 

  Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo wa miaka 18, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema ujenzi huo utagharimu Sh bilioni 16 na unatarajiwa kuanza kujengwa Mei mwaka huu na kwamba utakamilika baada ya miezi 18.Dk Dau alisema kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye kijiji cha michezo cha shirika hilo (NSSF Sports City), kitakuwa eneo la Mwasoga, Kigamboni, Dar es Salaam. 

  “Tuna eneo la zaidi ya ekari 400 ambapo tutajenga viwanja, shule ya michezo, nyumba za kuishi na maduka. Lengo letu tuzalishe na kuuza wachezaji. Tunakusudia kuwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 13, 18, 20, timu B na timu ya wakubwa,” alisema Dk Dau. 

  Alisema utekelezaji wa kituo hicho utaanza hivi karibuni kwa kutumia majengo ya kukodi wakati wakisubiri ujenzi kukamilika.“Hivi hapa baada ya kusaini mkataba, utekelezaji utaanza kwa kutumia majengo ya kukodi ambayo tunadhani yatakuwa maeneo ya Temeke na tutakuwa tukitumia viwanja vya Karume na Uhuru,” alisema. 

  Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF alisema katika kuendesha kituo hicho, kila kitu kitafanywa na Real Madrid kuanzia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu. 

  “Sisi tunachukulia huu mradi ni uwekezaji na hatufanyi hisani, itazingatia misingi ya biashara na faida kubwa ni kwamba NSSF itaongeza kipato, lakini pia kituo kitatumika kuitangaza Tanzania kwa sababu yatakayofanyika yataoneshwa kwenye televisheni ya Real Madrid,” alifafanua Dk Dau. 

  “Lakini pia wakati umefika sasa kwa Tanzania kushiriki Kombe la Dunia Qatar 2022, kama unaandaa vizuri vijana wa miaka 13 sasa mpaka mwaka 2020 wanaweza kuwakilisha vizuri kwenye mechi za kufuzu na mwaka 2022 wakashiriki Kombe la Dunia, wakikosa la Qatar, basi hata hizo zinazokuja, hiyo pia ni moja ya madhumuni ya kituo hicho.” 

  Akizungumzia namna walivyofikia uamuzi wa kujenga kituo, Dk Dau alisema wazo hilo lilipatikana Agosti mwaka jana na kisha likapelekwa kwenye Mkutano wa Wanachama uliofanyika Arusha ambako waliazimia NSSF iwekeze rasmi kwenye michezo kabla ya kuwasilishwa kwenye bodi na utekelezaji kuanza kufanyika. 

  “Tulitembelea sehemu nyingi kuona wenzetu wanafanyaje. Binafsi nilitembelea nchi kadhaa za Ulaya, nilienda kituo cha Manchester United, Sunderland, Real Madrid kwa hapa Afrika nilikwenda Asec Mimosas (Ivory Coast) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC) kuona wanafanyaje, ziara ikazaa matunda kwani tulikubaliana na Madrid na ndio wamekuja kusaini mkataba leo (jana),” alifafanua Dk Dau. 

  Naye Mkuu wa Vituo vya Michezo wa Real Madrid, Rayco Garcia aliishukuru NSSF wa kuwa na mpango huo na kuahidi kufanya kazi ili kuipatia Tanzania mafanikio. “Tukifanikiwa kuwatoa vijana hao, Tanzania itaweza kushiriki kwenye michuano mikubwa kama alivyosema Dk Dau, inabidi tufanye kazi ili vijana wafanikiwe, wafike mbali,” alisema Garcia. 


  Mbali na Garcia ambaye pia ni kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Madrid, wengine walioambatana kwenye msafara huo ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo, Ruben de la Red, Kocha Mkuu wa timu za vijana, Francisco Martin Ramos na Juan Jose San Roman Milla. Mwaka jana, wachezaji wa zamani wa Real Madrid walifanya ziara nchini.

  0 0

   
   Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali Mstaafu Ludovick Utoah akitoa nasaha katika hafla ya kuagwa kwake aliyoandaliwa na taasisi ya wakaguzi wa hesabu binafsi nchini.
   Mwenyekiti wa taasisi  ya wakaguzi wa hesabu binafsi nchinin Bwana Chacha akimpongeza Bwana Utouh baada ya hotuba yake.
  Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma Zitto Kabwe  akimpongeza  CAG mstaafu katika hafla ya kuagwa kwake aliyoandaliwa na taasisi ya wakaguzi binafsi wa hesabu nchini.

  0 0

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kuwatangazia Wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amemteua ndugu Godfrey Lebejo Mngereza kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

  Barua ya Januari 16, 2015 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga imeeleza kwamba uteuzi wa Mngereza unaanza Januari 23, 2015. 

  Kabla ya Uteuzi huo Bwana Mngereza alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kwa kipindi cha kutoka Februari 2013 hadi 2015 mwanzoni akitokea Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii ya BASATA aliyokuwa akiiongoza kama Mkurugenzi wake.

  Godfrey Mngereza ni msomi mwenye shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amepata kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu hicho katika Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) hadi mwaka 2008 alipoajiriwa rasmi na BASATA kama Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari ambayo kwa sasa inafahamika kama Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii.  

  Aidha, shahada yake ya kwanza ilikuwa katika masuala ya Sanaa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
  Imetolewa na Kitengo cha Habari- BASATA


  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Chung Il kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Ujenzi pamoja na mchakato wa Ujenzi wa Daraja jipya litakalopita baharini pembezoni mwa daraja la Selander.Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na uwezo wa kupitisha magari zaidi ya 61,000 kwa siku. Ujenzi wa Daraja hilo utaanza muda wowote kuanzia sasa. Daraja hilo litakuwa na njia nne za magari pamoja service road njia za waenda kwa miguu kila upande.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Chung Il mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi huyo wa Jamhuri ya Korea Chung Il pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe na Mkurugenzi wa Barabara Eng. Ven Ndyamukama. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Ujenzi

  0 0

  Na Anitha Jonas - MAELEZO.

  SERIKALI imedhamiria kupunguza msongamano wa magari  ndani ya jiji la Dar es Salaam kwakujenga barabara sita zitakazo ambazo ujenzi wake utasimamiwa na TANROADS. Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu sh. trilioni moja ambapo lengo barabara hizo ni  kupunguza adha ya msongamano wa magari  katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es saalam.

  Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara hizo. “Barabara hizi zinajenga kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na lengo kubwa la mradi huu ni kupunguza msongamano ndani ya jiji” alisema Magufuli.

  Magufuli aliendelea kusema “Rai yangu kwa Watanzania  wote ikiwemo madereva wa magari yenye uzito mkubwa  kuacha kupita barabara zisizo stahimili uzito wa magari hayo na kuwaasa wananchi wa maeneo jirani waache  kugeuza  barabara hizo kuwa maduka au fremu za biashara”.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Said Mecky Sadick aliwaasa wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na wakandarasi pale watakapoombwa wasogee  nje ya barabara ili kufanikisha ujenzi huo kwani barabara ni sehemu ya maendeleo na ni vyema kila mmoja kuwa mzalendo na kuacha itikadi za vyama .

  “Nikiwa kama mdau mkubwa wa maendeleo ya jiji la Dar es Salaam nitahakikisha wakandarasi hawa wanamaliza kazi ya ujenzi huu  kwa wakati na nitakuwa nikiwafuatilia kwa karibu katika kuhakikisha  viwango  vinazingatiwa  ili barabara hizi ziweze kuwa mkombozi wa tatizo la msongamano katika jiji,” alisema Sadick.

  Kwa upande wake Mtendaji  Mkuu Wakala wa Usimamizi wa Barabara (TANROADS) Mhandisi  Patrick Mfugale alizitaja barabara zinazotarajiwa kuanza kujengwa katika mradi wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam ni Ubungo Msewe hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 2.6, Ubungo Externo hadi Kilungule kilomita 3, Kigogo hadi Tabata Dampo kilomita 1.6.

  Mfugale alisema kuwa barabara nyingine ni Kinyerezi hadi Kifuru kilomita 4 kwa awamu ya kwanza na badae ni Kifuru hadi Maramba Mawili kilomita 10, pamoja na Mbezi Mwisho hadi Goba Tangi Bovu ambayo ni kilomita 20.
  Katika Ziara hiyo ya kuweka jiwe la msingi Waziri Magufuli aliambatana na watendaji na viongozi wa TANROADS, wabunge wa maeneo hayo, watendaji wa wizara.                                    

  0 0

  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (katikati) akielezea maendeleo ya mradi wa Kinyerezi I. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene. Kushoto kabisa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kulia) akitoa maelekezo kwa wataalamu wanaosimamia mradi wa Kinyerezi I.
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima ( aliyetangulia mbele) akiongoza msafara wa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene kwenye eneo la mradi.


  0 0


  Bw. Lopez akiwasilisha hotuba jijini Addis Ababa


  Na Ally Kondo, Addis Ababa
  Uchumi wa Bara la Afrika umeelezwa kuwa unakua kwa kasi zaidi ukilinganisha na mabara mengine duniani. Hayo yamesemwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Afrika, Bw. Carlos Lopez wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa AU jijini Addis Ababa, Ethiopia siku ya Jumatatu tarehe 26 Januari 2015.
  Bw. Lopez alithibitisha kauli yake hiyo kwa kunakili ripoti mbalimbaliikiwa ni pamoja na ripoti ya Ernst & Young inayosema kuwa Bara la Afrika ni la pili kwa kuvutia uwekezaji baada ya Asia ya Kusini-Mashariki.

  Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa uwekezaji baina ya nchi za Afrika umeongezeka na kwa sasa unakua kwa asilimia 32.4 kwa mwaka. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, jumla ya akiba ya fedha katika Bara la Afrika itafikia Dola za Marekani trilioni 23 kutoka trioni 12 ifikapo mwaka 2030.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mh Egon Kochanke akitoa historia fupi ya wahanga wa maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi katika maadhimisho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia na kuandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania.
   Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi Usia Nkhoma akiwakaribisha wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar ambavyo Kuna Klabu za Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa utamaduni wa Russia wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na kuwakumbuka wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Spika wa Bunge, Anne Makinda akiongozwa na Mpambe kuingia kwenye ukumbi wa Bunge leo Januari 27, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama,Bungeni mjini Dodoma leo Januari 27, 2015.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akiapa Bungeni mjini Dodoma leo Januari 27, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju (wapili kulia) baada ya mwanasheria huyo kuapishwa Bugeni mjini Dodoma leo Januari 27, 2015.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakisaini mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 182.
  Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 182.
  Picha ya Pamoja.


  0 0


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 27, 2015(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisaini katika kitabu cha wageni mapema leo alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kwenye ziara ya mafunzo kuhusu uendeshaji wa Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani).


  0 0

  Hayawi hayawi yamekuwa , Dk. Neema Nalitolela (kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na mpambe wake Winne Temu (kulia) wakifurahia jambo wakati wa sherehe ya kumuaga (Send off) iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
  DK. Neema Nalitolela akikata keki wakati wa sherehe ya kumuaga (send off ) huku akishuhudiwa na wazazi wake Mr &mrs Nalitolela( kushoto) na upande wa wazizi wa mmewake mtarajiwa Mr&mrs Kabyemero( kulia) sherehe hiyo ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam, Neema ni Daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Dk. Neema Nalitolela akipongezana na mpambe wake Winne Temu wakati wa sherehe ya send off yake iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam. Neema ni Daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona(Katikati) akikata utepe, kuashilia uzinduzi Rasmi wa nyumba aliyokabidhiwa Salome Mhando ambaye alitelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo hadi kufikia sita na kukosa Mahali pa kuishi, Covenant Bank imemkabidhi nyumba hiyo ambayo ataimiliki yeye mwenyewe pamoja na thamani za ndani na Bima ya Matibabu kwa Mwaka mzima. Anaeshuhudia ni mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sabetha Mwambenja (wa kwanza kushoto) na Salome Mhando (wa kwanza kulia).
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank Balozi, Salome Sijaona (kushoto), Pamoja na Mkurugenzi wa benki Hiyo, Sabetha Mwambenja, wakimkabidhi hati ya kiwanja na Umiliki wa nyumba Salome Mhando, Mama alietelekezwa na mume wake baada ya kujifungua watoto mapacha mfurulizo, hadi kufikia sita, Benki hiyo imemkabidhi nyumba hiyo pamoja na Bima ya Matibabu kwa mwaka mzima.


  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga(katikati) akitembelea katika katika eneo la Mradi wa kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant wakati wa ziara ya Maafisa Mawasilano Serikalini katika eneo a mradi huo leo Mkoani Mtwara.


older | 1 | .... | 719 | 720 | (Page 721) | 722 | 723 | .... | 3282 | newer