Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 718 | 719 | (Page 720) | 721 | 722 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anatarajia kuyafutia usajili zaidi ya Mashirika 1000 kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria katika utendaji kazi wake tangu yasajiliwe.

   Hatua hiyo inatokana na maelekezo ya Bodi ya Uratibu ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni mkoani Geita. 

  Kufutwa kwa mashirika tajwa kunatokana na kushindwa kutoa taarifa zake za kila mwaka kama inavyosisitizwa na sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002 hali inayosababisha kazi za mashirika hayo kutofahamika vyema na hivyo kukosa sifa ya kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria. 

  Orodha ya Mashirika tajwa itatolewa kwa umma hivi karibuni na inahusisha pia Mashirika ya Kimataifa.

  0 0

  Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

  Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo KUTAKAPOKUCHA au Kununua na iwe yako kupitia mtandao.

  Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


  Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

  0 0

  Kufuatia mkutano wa Watanzania waishio ujerumani na Rais wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete, Mweyekiti wa umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V Bw, Mfundo Peter Mfundo ameeleza matarajio ya Watanzania waishio Ujerumani.

  Alifafanua kwamba japokuwa Rais Kikwete amebakiza muda mfupi katika uongozi wake lakini Umoja huo unaamini kuwa madam Rais Kikwete ameona umuhimu wa kufanya mkutano na Watanzania wanaoishi ujerumani basi anaweza akatekeleza mahitaji ya Watanzania hao.

  Bw. Mfundo alifafanua pia hoja za msingi ambazo zitaibuka kwenye mkutano huo kuwa ni pamoja na Utekelezwaji wa upatikianaji wa fursa zilizopo Tanzania kwa watanzania wanaoishi Ujermani (Diaspora).

  Aidha aliendelea kueleza kwamba hoja nyingine ya msingi ni kutaka kujua msimamo wa serikali juu ya Uraia Pacha, kwani Watanzania wanaoishi ujerumani wana kiu kubwa ya kujua swala la Uraia pacha limefikia wapi.

   akiendelea kuongea na Mtangazaji Grace Kabogo kupitia sauti ya Radio Deutsche Welle idhaa ya kiswahili Bw. Mfundo alisema kutokana na Vijana wengi wa Tanzania kujiajiri kupitia Muziki na kuupiga vita umasikini, Umoja wa Watanzania Ujerumani Utamuomba rais Kikwete kusaidia kupitisha msamaha wa kodi kwa Vyombo vya Muziki ili kuwawezesha Vijana wa Tanzania kumudu ununuzi wa vifaa hivyo, Bw. Mfundo alieleza moja ya changamoto wanazozipata ni pale umoja huo unapokosa mawasiliano ya moja kwa moja na Idara ya Diaspora Tanzania.

  0 0

  Naibu waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akikabidhiwa ua na mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Christina Nyenga wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu wakati akimkabidhi ofisi leo jijini Dar Es Salaam . kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililofanyika Jumamosi.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki akimkabidhi nyaraka mbalimbali Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi wakati Mhe. Kairuki alipokuwa akikabidhi ofisi leo jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Hii itakuwa ni Sherehe ya aina yake kufanyika katika Jiji la Wajanja Big Apple,Watu wote bila kujali Itikadi zao wanaalikwa kwani hii ni Birthday Bashhh na sio mkutano wa kisiasa,Njoo uburudike na watanzania wenzako kutoka states mbali mbali pamoja na Nje ya nchi,kutakuwqa na Burudani kutoka kwa wasanii maarufu kutoka Tanzania,Habari zaidi za Wasanii na Mgeni Rasmi kufuata. Tuungane Tuiline Tanzania Yetu


  TICKETS PRICE: ADVANCE $40 | DOOR $50
  Inclusive of:
  *3-Course Dinner
  *Soft Drinks
  *Elegant Settings
  *Entertainment
  *Cash - Bar Beer $3| Liqour $5 | Wine $5 | Patron $7
  CALL: 347-663-0781  | 917-698-6943 

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za kuuza za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli na Msimamizi wa mradi huo Bw. Hassan Bendera.
   Hii ni sehemu ya nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kama sehemu ya juhudi za Shirika hilo za kuwezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Nyumba hizi zinajengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.


  0 0
 • 01/26/15--03:10: JOB VACANCY 2015

 • 0 0

  Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Mkuu wa Kongane ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe (Kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory).
  Mtaalamu wa Masuala ya Forodha kutoka TRA, Bw. Stambuli Myovela (Kulia) akizungumza wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.


  0 0

  Naibu Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Mtokeo Makubwa Sasa! (BRN), Peniel Lyimo akizungumza katika mkutano wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na taasisi ya ACT na kuhusisha wadau zaidi ya 100 wa sekta ya kilimo nchini ambapo alieleza jinsi BRN inavyosaidia kuboresha mazingira ya uwekezaji katika biashara na kilimo.
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Kilimo Tanzania (ACT), wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na taasisi ya ACT, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani (katikati waliokaa mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano huo Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Mawasiliano PDB).

  0 0

  Aliyekuwa Mtangazaji wa vipindi vya Michezo wa redio Clouds Dar es Salaam,Ibrahim Masoud 'Maestro' (pichani kushoto) leo amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Kituo maarufu hivi sasa cha radio hapa jijini Dar es Salaam cha E FM 93.7.

  Maestro ameungana na magwiji wengine katika utangazaji wa vipindi vya michezo nchini Maulid Kitenge na Omary Katanga ambao wapo katika radio hiyo inayokuja kwa kasi jijini.
  Pichani Maestro akitambulishwa rasmi na Mkuu wa kipindi cha michezo cha E. sports cha E FM 93.7 Maulid Baraka Kitenge leo.

  0 0

  Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mh Ummy Mwalimu akimkabidhi Naibu Waziri mpya Ofisi hiyo Mh. Stephen Masele.
  Naibu Waziri mpya Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Stephen Masele akiwa katika Ofisi yake aliyokabidhiwa na Mh. Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.Angeline Madete akitoa maelezo mafupi wakati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Stephen Masele akikabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Naibu Ofisi hiyo Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Chiku Galawa jana wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoendelea Mkoani Dodoma.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mathias Chikawe (katikati) wakiongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Chiku Galawa kuingia ukumbini kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoendelea Mkoani Dodoma.
  Baadhi ya maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya ofisa wa polisi jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu hao unaoendelea Mkoani Dodoma.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza washiriki wa Mkutano huo umuhimu wa kuelimisha umma kuelekea upigaji kura ya maoni na kuwataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza suala hili la kitaifa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti Bw. Theophil Makunga akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pia aliwataka Maafisa Mawasiliano kutengeneza mazingira yatayowezesha kufanya kazi na wanahabari.


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

  Waziri wa Nishati na Madini ,George Simbachawene amesema kuwa watanzania wamuamini ataendeleza kwa kasi ile ile katika kuwafikishia wananchi maendeleo kupitia sekta za nishati na madini.

  Hayo ameyasema leo wakati alipoanza kazi rasmi katika Wizara hiyo akichukua nafasi ya Profesa Sospeter Muhogo aliyejiuzulu wiki iliyopita,amesema kila mtu sio mkamilifu hata mitume watu wengine hawakumuamini.

  Simbachawene amesema ana uzoefu wa kufanya kazi na kuachana na vyeti kwani vyeti ni ziada lakini kalama ya uongozi ndiyo inayohitajika.

  Aidha amesema wanaotilia shaka uteuzi wake watakuwa na kigezo lakini kila mtu hawezi kuamini kila binadamu ana mapungufu kwa namna anavyoona mtu.

  Simbachawene amesema atafuatilia usiri wa mikataba lakini sasa anasoma mazingira kwanza na kuweza kuweka bayana suala hilo.

  “Niko hapa watu waniamini kutokana na kazi zangu na watanzania waniamini niweze kufanya kazi niliyoaminiwa kwa niaba ya watanzania wenzangu”amesema Simbachawene.
  Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na uongozi wa Wizara hiyo mapema leo asubuhi. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini kama mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari mada baada ya kuwasili Wizarani hapo mapema leo asubuhi.
  Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo.

  0 0

  Picha ya pamoja ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika baada ya Mkutano wao kufunguliwa rasmi jijini Addis Ababa leo.

  Na Ally Kondo, Addis Ababa
  Kamati ya Uongozi ya NEPAD imekutana leo Jumatatu jijini Addis Ababa, Ethiopia kutathmini utekelezaji wa programu mbalimbali wa chombo hicho. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shuguli za NEPAD kwa mwaka 2014, Mtendaji Mkuu wa NEPAD, Dkt. Ibrahim Mayaki alieleza kuwa Chombo hicho kimepiga hatua kubwa katika maeneo ya kipaumbele iliyojiwekea.

  Kwa upande wa miundombinu, Dkt. Mayaki alikumbusha Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Darker, Senegal ambao ulijadili njia za kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya miuondombinu barani Afrika. Mkutano huo uliweka msingi wa kuainisha miradi 16 ya miundombinu yenye kukopesheka na yenye lengo la kupunguza tatizo la miundombinu barani Afrika. NEPAD kwa kuzingatia ushauri wa Wakuu wa Nchi, imeanzisha chombo maalum ambacho jukumu lake ni kutoa msaada wa kiufundi katika hatua za mwanzo za maandalizi ya miradi ya miundombinu.

  0 0

  Mwenyekiti Mteule wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Richard Ndassa (Mb) akiwashukuru wajumbe wa Kamati hiyo baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo baada ya Mwenyekiti wa awali Mhe. Victor Mwambalaswa kujiuzulu kufuatia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la Account ya Tegeta ya Escrow. Mhe. Ndasa alimshinda mpinzani wake Mhe. Jerome Bwanausi (Mb) katika uchaguzi huo.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Jerome Bwanausi akitoa neno la shukrani mbele ya wajumbe wa kamati hiyo baada ya kuchaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Picha na Owen Mwandumbya

  0 0

  Na   Bashir     Yakub

  Katika  makala  iliyopita  nilisema  kuwa  vijana  wengi   wajasiriamali  wanaofungua   biashara  za  makampuni   wanao  uwezo  mkubwa   wa kufika mbali   isipokuwa  tatizo  lao  ni  taarifa za  mambo  mbalimbali   kuhusu uendeshaji  wa  kampuni   hizo. 

   Mambo  ya uendeshaji   wa  kampuni  ni  mepesi sana  na  yanawezwa   na  mtu  yeyote isiopokuwa   tatizo   ni   taarifa   na  elimu ya  namna  ya  uendeshaji  kisheria   ili   kampuni   ionekane  ni kampuni.  Nilieleza  namna   kampuni  inavyolipa kodi   na  taratibu  za   kikodi  za kampuni.

    Leo tuangalie  kipengele  kingine  cha  uendeshaji  wa kampuni  ambacho  ni namna  ya   kupata   leseni  ya   biashara.

  1.KAMPUNI   ULIYOSAJILI   HAIWEZI   KUANZA   KAZI   BILA   LESENI    YA BIASHARA.

  Wajasiriamali   wengi   wanaofungua kampuni   wanajua   kuwa   ukishapata usajili   wa   kampuni   basi    unakuwa umemaliza   kila   kitu   na   unaweza  kuanza   biashara.  Wazo  hili  si   la  kweli kwakuwa  baada  ya  kampuni  kuwa  imepata usajili  na    unataka   kuanza biashara   ni   lazima  uwe   na   leseni   ya biashara (business  licence).  Kwa   maana   hii   kumbe  mchakato   wa kuanza   biashara   na   kampuni   hauishii kwenye  kupata     usajili   wa   kampuni. Cheti  cha  kuzaliwa  kwa  kampuni  yako ( certificate  of  incorporation)  ni  tofauti na  leseni   ya   biashara.Na   ili  biashara  ya  kampuni  ianze  kisheria  lazima  uwe  navyo  vyote  viwili.


  0 0
 • 01/26/15--21:48: KIJIWE CHA UGHAIBUNI


 • 0 0

  A plow truck clears snow off South Church Street, in Hazleton, Pennsylvania on Monday. The area received another three-inches of snow overnight
  Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliyoenea katika barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk

  By Abou Shatry Washington DC

  Zaidi ya watu 60 million wataathirika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki ya Marekani.

  Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na dhoruba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.

  Imetaja baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo viongozi wakuu wamajimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.

  Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango chengine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine.

  Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo katika viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.

  0 0

  The government decision of January 23rd to suspend the circulation of "The East African", a long- established regional newspaper, gives rise to concerns about freedom of press in Tanzania.

  It is the duty of the media to work within the law and to make every effort to adopt and adhere to professional standards. But Press Freedom and freedom to express opinions are fundamental rights of the people, which call for circumspection and proportionality in the application of the law.

  The Delegation of the European Union expresses its concern that modern media legislation in Tanzania, including on the citizens' Right to Information, has not yet been promulgated despite the longstanding requests of the media profession and the repeated commitments of the Government.

  It is recalled that in October 2010 the EU's independent Election Observation Mission recommended expediting modernisation of the media laws, taking into account stakeholders' views.

  The Delegation of the European Union calls upon the Government to make every effort to preserve the freedom of expression in Tanzania and it urges all stakeholders to prioritise constructive dialogue as the primary means to resolve differences. It also reiterates its commitment to monitor, support promote and monitor media freedom as a shared value of the EU partnership with Tanzania.

  The High Commission of Canada and Embassies of Norway and Switzerland associate themselves with this statement.

older | 1 | .... | 718 | 719 | (Page 720) | 721 | 722 | .... | 3272 | newer