Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA POLISI JIJINI DAR: MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA DAR WAKATI WA MAPAMBANO KATI YAO NA ASKARI WA JESHI LA POLISI

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG yenye namba BA172288  na risasi kumi na tatu wakati wa  mapambano makali ya ana kwa ana kati ya majambazi na Jeshi la Polisi.  Aidha katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa  kwa risasi wak ati wakijaribu kuwadhuru askari.  

Tukio hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Livingstone saa 3.00hrs usiku. Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na mlalamikaji alikuwa anatumia taa za kawaida.  Mara baada ya kuanza tukio hilo la uporaji wasamaria wema walijulisha Jeshi la Polisi ndipo kikosi maalum cha kupambana na majambazi (ant robbery squared) kilipofika kwa haraka katika eneo la tukio tayari kwa mapambano. 

Majambazi hao walistuka na kuanza kuwarushia risasi askari waliokuwa katika gari la Polisi na ndipo sasa kukawa na mapambano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa kutumia silaha na kurushiana risasi. Hatimaye majambazi wawili waliuawa mmoja anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya. Jambazi mwingine aliyeuawa ametambuliwa kwa jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB, Miaka 46, Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

Majambazi wengine waliotoroka baada ya tukio hilo wanaendelea kutafutwa na tunaomba raia wema waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili wapatikane.

Pamoja na kuuawa kwa majambazi hawa na kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa pikipiki mbili moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249 CMC, rangi nyekundu. Nyingine ni aina ya BOXER yenye namba za usajili MC350 AM rangi nyeusi ambazo zote zilitumiwa na majambazi hao katika tukio. Aidha, Jambazi ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO  aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya TECNO.  

MAJAMBAZI WENGINE TISA SUGU WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM 

Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

Oparesheni kali bado inaendelea jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha kwamba majambazi wote wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine ambayo ni kero katika jamii yanashughulikiwa kikamilifu. Pamoja na mafanikio hayo tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao za kutoa taarifa mapema zenye kuwa na mafanikio ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee kuwa shwari.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA KUHITIMISHA ZIARA YAKE LEO KISIWANI UNGUJA KESHO KUUNGURUMA PEMBA

0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni, Mh.Jakhu Hashim Ayoub wakielekea kwenye mashamba ya zao la Mwani,ambapo pia Ndugu Kinana alishiriki kupanda Mwani na baadhi ya Wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mwani na baadhi ya Wakulima wa zao hilo la Mwani katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja,kulia kwake ni Muwakilishi wa jimbo la Muyuni ni Mh.Jakhu Hashim Ayoub.

 Baadhi ya Wakulima wa zao la Mwani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman. 
PICHA NA MICHUZI JR-KUSINI UNGUJA

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ASHUHUDIA KUSAINIWA KWA MAKUBALIANO YA MWENDELEZO WA KAMPENI ZA USALAMA BARABARANI BAINA YA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA,JESHI LA POLISI NA VODACOM TANZANIA

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa kwanza toka kushoto) akimweleza jambo Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto) wakati Baraza hili lilipotia saini makubaliano na kampuni hiyo kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani ambazo Vodacom imekuwa ikidhamini tangu mwaka 2014. Akisikiliza pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa pili toka kushoto). Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.) (wa kwanza toka kushoto) akishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano ya kuendeleza ushirikiano katika kampeni za usalama barabarani baina ya Baraza hilo na kampuni ya simu za mikooni ya Vodacom Tanzania. Akitia saini kwa naiba ya Baraza ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga (wa pili toka kushoto) na kwa niaba ya Vodacom ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa watakiwa kujenga utamaduni wa kutekeleza wajibu wao kwa kujitolea zaidi

0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akitoa nasaha kwa wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati akizindua Balaza la 13 la Michezo leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo. Wajumbe waliohudhuria hafla hizo ni pamoja na ,Mkurugenzi wa PSPF Adam Mayingu, Zacharia Hans Pope, Jamal Rwambow, Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF Crescentius Magori ,wajumbe wengine ni Alex Mgongolwa, Jennifer Mmasi Shang’a, Mhe. Zainabu Vulu (MB), Mohamed Bawaziri na Mwl. Zaynab Mbiro.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi akitoa neno lashukrani mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Baraza la 13 la Michezo leo jinini Dar es Salam. Pembeni ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.

RAIS WA TFF JAMAL EMIL MALINZI ATEMBELEA UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA

0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil Malinzi wa pili kutoka (kushoto) akiongozana na Baadhi ya Viongozi wa Mpira hapa Nchini leo hii Mchana alipowasili katika Uwanja wa Kaitaba unaokarabatiwa kuwekwa Nyasi za Bandia. Bw. Jamal Emil Malinzi pia ndie Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) alipowasili hapa Bukoba amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa Kagera na baadae.
Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi pia aliambatana na Viongozi mbalimbali hapo Uwanjani akiwemo Bw. Pelegrinius A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu, Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi kamati ya Waamuzi Nchini.
Doron Mommsen(kushoto) akiongea na Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi(kulia) leo wakati Rais huyo alipotembelea kujionea Ukarabati huo wa Uwanja wa Kaitaba ambao Utachukua Muda wa Miezi Mitatu. Meneja wa Mradi Bw. Doron Mommsen amemweleza Ndugu Jamal Malinzi kwamba Ukarabati unaendelea Vizuri na kinachoendelea kwa sasa ni kusawazisha Udongo katika Uwanja huo.
Meneja wa Mradi Bw. Doron Mommsen akionesha kile kinachoendelea atika Uwanja huo wa Kaitaba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

kumbukumbu

0
0

R. I. P Willy Joseph Minja.

Ni miezi mitano toka umeiaga dunia hii ya tabu na mateso. Familia yako, watoto wako, mke wako, Baba Joseph Minja na mama yako Rose Swai, Kaka, Dada ndugu, Ma-rider  (Tigo Police) jamaa na marafiki tunakukumbuka na tutakukumbuka Daima. 

Raha ya milele upewe eeeWilly...
na Mwanga wa milele uangaziwe...
AMEN

RIP JOSEPH FREDERICK BURENGELO

Mama Tunu Pinda ala nondozzz chuo kikuu huria tawi la dodoma

0
0
 Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Asha-Rose Migiro akimtunuku shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katika mahafali ya 27 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini DODOMA. Kushoto anayeshuhudia ni Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Tolly Mbwete.

Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda  akitoka kupokea shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi. Akiongea baada ya hapo Mama Pinda ametoa wito kwa kinamama wa Tanzania na Afrika kwa jumla kujiendeleza kielimu ili kukomboa mataifa yako kutoka katika dimbwi la umaskini
 Kikundi cha wake wa viongozi kutoka Dar es salaam kikimpongeza mlezi wao Mama Tunu Pinda kwa kutunukiwa shahada ya  uzamili ya usamamizi miradi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika mahafali ya 27 iliyofanyika Mjini Dodoma. Toka  kushoto ni  Mama Mashiba,  Mama Lukuvi na Mama Malima 
Wanafamilia wakimvisha maua Mama Tunu Pinda. Picha na Chris Mfinanga

BREAKING NEWZZZZ: PROFESA SOSPETER MUHONGO ABWAGA MANYANGA

0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Wizara hiyo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es salaam.
Waziri Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo,kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya Bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi yake na wengine kadhaa kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Waziri Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko amesema kuwa yeye sio mla rushwa bali ni mchapa kazi tu na akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo aliyataja kuwa ni Mvutano wa kibiashara, Mvutano wa kisiasa, Mvutano wa uongozi na madaraka pamoja na Ubinafsi.
Hivyo kasema ameamua kujiuzulu ili kuiachia Serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye ndiyo tatizo.Picha/habari na Othman Michuzi.
Sehemu ya Waandishi wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia kwa makini taarifa ya Waziri Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisisitiza jambo wakati akilizungumzia swala la Akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,mchana wa leo.

VIDEO YA MKUTANO HUO ITAWAJIA MUDA SI MREFU

BREAKING NYUZZZZZZ....: RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na manaibu waziri aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue
Moja wa Sura mpya katika baraza jipya la Mawaziri Naibu Waziri wa Elimu Anne Kilanngo Malecela akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, Ikulu,  Jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.

Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.

Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.

Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.

MAWAZIRI
1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
2. Mh. Angela Kairuki -  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU KUMI KISIWANI UNGUJA,KESHO KUWASILI KISIWANI PEMBA.

0
0
Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi waliofika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kumsikiliza.Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Mkutano wa hadhara ukiendelea katika uwanja wa Kizimkazi mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja mapema leo jioni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi majiko ya gesi kwa vikundi vya akina mama wa Makunduchi yaliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Makunduchi,Mh.Samia Suluhu na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh Haroun Ali Suleiman.
Ndugu Kinana akishiriki kupandisha mabomba kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kibuteni-Makunduchi unaosaidiwa na jumuiya ya Milele Zanzibar Foundation.Pichani shoto ni Afisa Maji Mkoa wa Kusini Unguja,Bwana Hafidhi Hassan  Mwinyi,ambaye alisema kuwa lengo la Mradi huo ni kuhuwisha,kuiimarisha na kuikuza miundombinu ya maji safi na salama ya Makunduchi Kibuteni ili iweze kutoa huduma vizuri na kwa ubora unaohitajika kwa walengwa wake.Mradi huo unakisiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 650 na ushehe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na wanachama wengine,wakiwaongoza wanachama wapya wapatao 518 kula kiapo mara baada ya kujiunga na chama hicho sambamba na kukabidhiwa kadi za uanachama.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kwa minajili ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

WAZIRI LUKUVI AMKABIDHI OFISI WAZIRI MHAGAMA LEO

0
0
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (Kulia) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akifafanua jamabo kuhusu masuala ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Waziri wa Nchi aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (kushoto ) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam.
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (mwenye shati) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akiwaeleza wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) kuendelea kutoa ushirikiano wa kutekeleza majukumu ya ofisi hiyo, kwa Waziri mpya wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (katikati) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam (anayeandika) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli .
Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. William Lukuvi (Mb) ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi ambaye wakati wa kumkabidhi Ofisi aliyeshisha wadhifa huo wa Waziri Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akimhakikishia ushirikiano Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (kushoto ), wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam, (kulia ) ni Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (Kulia) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ROBO FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE KUANZA KESHO

0
0
Hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inachezwa kesho (Januari 26 mwaka huu) na Januari 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kwa mechi mbili kila siku.

Mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Televisheni itaanza saa 9 alasiri kwa kuzikutanisha Mwanza na Kigoma. Robo fainali ya pili ambayo ni kati ya Tanga na Pwani itaanza saa 11 kamili jioni.

Ilala na Iringa watacheza robo fainali ya tatu Januari 27 mwaka huu kuanzia saa 9 kamili alasiri, na kufuatiwa na robo fainali ya mwisho saa 11 kamili jioni itakayozikutanisha Temeke na Mbeya.

Nusu fainali za michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitachezwa Januari 29 mwaka huu wakati Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu kuanzia saa 10.15 jioni ambapo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu (play off).

Timu zote zilizoingia hatua hiyo ya nane bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini zimefikia hosteli ya Msimbazi.

Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Januari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Airtel yazindua huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi

0
0
11
Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based solution ya  Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel
1111
Mama elizabeth mshana mmiliki wa duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa na  Airtel Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za mkoni ya airtel.
11111
Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na kadi maalumu ambacho hutumika kukamilisha miamala ya malipo katika maduka mbalimbali. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki mkoani arusha eneo la muromboo wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo inaleta njia salama, ya haraka na rahisi kwa wateja kufanya malipo. 
111
Mfanyabiashara wa duka la chakula katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi akipokea malipo kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field Communication (NFC) ya Airtel Money.  , huduma imezinduliwa na Airtel mkoani Arusha inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi hiyo maalumu kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na kulipa haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akishudia huduma hiyo inavyofanya kazi.  Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZINDUA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA KUZALIWA CCM

0
0
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzinzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.
 Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria katika mkutano wa uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimia miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzinzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo katika uwanja wa wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.

 PICHA NA MICHUZI JR-PEMBA.

ngoma azipendazo ankal

0
0

Tabu Ley Rochereau - Kaful Mayay

Mawaziri wa Afya wa Zanzibar na wa Afya wa Jamuhuri ya Muungano wakutana na waTanzania Ujerumani

0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Jamuhuri ya muungano Mhe.Bw.Seif Rashid na waziri wa afya wa ZanzibarMhe. Rashid Seif Suleiman, Siku ya jumapili 25 januari 2015 walikutana na kuongea na baadhi ya watanzania waishio nchini ujerumani katika hoteli ya Martim Hotel mjini Berlin.
 
Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na  balozi Tanzania nchini Ujerumani mheshimiwa Bw.Philip Malmo,katika mkutano huo mawaziri hao wote walielezea jinsi wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafakia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila Mtanzania atatanufaika na huduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao. 
 
Watanzania waishio ujerumani wamefarajika sana na mkutano huo,pia mawaziri wamewataka watanzania waishio ughaibuni  kuchangia kuwekezakatika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi ,mawaziri hao wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.
 Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa(katikati)makam mwenyekiti wa UTU Bw.Peter Kazaura(mwenye kitamba shingoni) mdau Shah wa jiji la Berlin Mwenye kofia nao walikuwapo

 Mkuu wa bendi ya Ngoma Africa Kamanda Ras Makunja akiwa Mhe.Philip Malmo Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ,katika mkutano katika hoteli ya Maritim mjini Berlin.
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii ambaye  pia ni mbunge wa Rufiji Mhe.Seif Rashidi akiwa na Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mjini Berlin,Ujerumani.
 Waziri wa Afya wa jamuhuri ya muungano mhe.Seif Rashidi akiongea na watanzania waishio Ujerumani,
 Waziri wa Afya wa Tanzania Mhe.Seif Rashid akiwa na baadhi ya watanzania nchini Ujerumani. 

MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA, SHERIA NGOWI AMVALISHA RAIS MPYA WA ZAMBIA

0
0
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum  (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish 
 
  Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia  katika sherehe za zilizofanyika  jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akitia saini Hati Maalum Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
 
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa Zambia Guy Scotts Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
  Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi  akiwa na Mkewe Eshter Lungu  Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
-----
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Rais Lungu 58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.

“Hii ni hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu”, alisema Ngowi.

Mbunifu Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake.

Mbunifu huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.

Hii ni changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango.

MAKALA YA SHERIA: JE UMEFUNGUA/UNATAKA KUFUNGUA KAMPUNI, JIFUNZE KAMPUNI YAKO INAVYOTAKIWA KULIPA KODI KISHERIA

0
0
Na   Bashir   Yakub

Vijana wengi  wajasiriamali wadogo wamefungua makampuni. Hakika wote waliofanya  hivi  wamefanya  jambo jema  linaloendana  na  wakati. Niliwahi kuandika wakati  nikielekeza namna nyepesi  kabisa  ya  kufungua kampuni kuwa,  ni  vigumu kwa leo kufanya biashara  na  ukawa  na  mafanikio nje ya  kampuni. Nikasema hata kama unauza maziwa, mama ntilie, unauza mayai, kibanda cha huduma ya fedha kupitia simu,unauza mihogo, haizuiwi kufungua kampuni. 

Kuna kampuni   hata  za mtaji wa milioni moja  na  pesa hiyo si lazima uwe nayo mkononi  ila  ni  katika maandishi   tu. Nikasema anayetaka mafanikio  kwa sasa ahakikishe hiyo biashara yake ndogo kabisa anaifungulia kampuni. 

Kwakuwa wapo wengi ambao tayari  wamefungua  makampuni  basi zipo  changamoto nyingi wanazokumbana  nazo  na kubwa zaidi ni  taarifa au ujuzi wa mambo mbalimbali  ya  namna  ya kuendesha kampuni  ili kampuni  iwe kampuni  kweli. 

Moja ya eneo lenye shida au ambalo  wajasiriamali  wadogo hawana taarifa  nzuri  kuhusu ni taarifa za kodi  zinavyolipwa  na kampuni kisheria. Hawajui  ni kiasi gani, kwa muda gani  na  vipi. Leo hapa nitaeleza kwa  uchache  kuhusu  kodi  za kampuni. Kampuni hulipa  kodi ya mapato,  swali ni  kodi  ya  mapato nini.

1.KAMPUNI  HULIPA  KODI  YA  MAPATO, JE  KODI  YA  MAPATO  NINI ?

Kodi ya mapato Tanzania ni tozo kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inayotokana na vyanzo vitatu ambavyo ni ajira, biashara pamoja na uwekezaji. Aina hii ya kodi inatozwa kwa mamlaka ya Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kama ilivyorekebishwa.Kwa upande wetu wa kampuni  kodi inayolipwa kwa tafsiri hiyo hapo juu ni kwakuwa kampuni ni biashara na pia ni kwakuwa ndani kampuni waweza kuwamo uwekezaji.Hii ndio sababu kampuni hulipa kodi ya mapato.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Huge Asteroid To Fly Past Earth On Monday 26 January (TONIGHT)

0
0
Use binoculars and the sky map below with the path of the ASTEROID 2004 BL86 during its closest approach to Earth on Monday night. East African Time (EAT) is marked on the map. Closest approach is at 3:44 AM but it can be followed from 9 pm onward since it will be half way up the sky when looking east. Visit http://www.astronomyintanzania.or.tz for further follow up.
Dr N T Jiwaji, Open University of Tanzania, 26.Jan.15
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images