Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 715 | 716 | (Page 717) | 718 | 719 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo Mh. Subira Mgalu (kushoto) akieleza jambo wakati walipoenda kutembembelea miradi ya Maji kanda ya Kaskazini.

  Kamati ya Maji, Mifugo na Uvuvi imeridhishwa na miradi mbalimbali ya Maji iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 ya kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi na kupunguza tatizo la uhaba wa Maji hapa nchini. 

  Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Maji Mh. Selemani Kakoso Wakati wa ziara ya kamati katika kuangalia miradi ya Maji iliyofanikiwa katika baadhi ya mikoa ya kaskazini.


  Katika ziara hiyo wajumbe wa Kamati walitembelea Mkoa wa Tanga kwa kuanzia wilaya ya Muheza na kutembelea mradi wa maji wa vijiji 10 katika kata ya Ubembe ambapo mradi huo wa Maji umeweza kuwanufaisha wananchi zaidi ya 1600 na hivyo kupunguza kero ya Maji na kuwapa wananchi nafasi zaidi ya kufanya shughuli za maendeleo.


  Pia kamati hiyo iliweza kuona uchafuzi wa Vyanzo vya Maji katika mto Zigi na kutoa wito kwa mamlaka ya Maji Tanga pamoja na hifadhi ya bonde la pangani kushirikiana kwa pamoja kuweka usimamizi shirikishi wa pamoja ili vyanzo vya Maji vilindwe kwa ajili ya kizazi hiki na kizazi kijacho.

  Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Muheza, Bi Subira Mgalu aliyekuwepo katika ziara hiyo alitoa wito pia kwa jamiii kuonyesha ushirikiano katika kuwabaini wananchi wanaofanya shughuli za uchimbaji madini katika vyanzo vya Maji kwani wanaojishughulisha na shughuli hizo ni wananchi wa maeneo hayo na si vyema kulindana kwani ili kuleta maana nzima ya ulinzi shirikishi kwa jamii husika

  0 0

  WIZARA ya Habari Utamaduni na Michezo imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutoa adhabu kwa timu ya Ruvu Shooting kutokana na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo dhidi ya mshambuliaji wa Yanga kutoka nchini Rwanda, Hamis Tambwe.

  Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Naibu Waziri wa Habari, Juma Nkamia amesema kuwa TFF isikae kimya kutokana na matamshi ya udhalilishaji juu ya Tambwe na kuiagiza TFF kuchukua hatua za kinidhamu haraka iwapo itathidibitika mshambuliaji huyo alitolewa maneno hayo ya udhalilishaji ili iwe fundisho kwa wengine.

  "Hakuna nchi yoyote duniani inayopenda vitendo vya ubaguzi, kitendo ambacho upendi kufanyiwa usimfanyie mwenzie, nimesikia malalamiko ya Tambwe kama ni kweli Ruvu Shooting wamemuita mkimbiza wajue sio kitu kizuri tena wale ni jeshi, nadhani wanajua madhara ya vita.


  0 0
 • 01/22/15--09:47: Shukrani
 • Familia ya Luteni Kanali Willy John Masoi (Mstaafu) wa Sabasaba Ukonga, Dar es Salaam tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani kwa msaada wa hali na mali wakati wa msiba wa Baba yetu mpendwa Luteni Kanali Willy John Masoi (Mstaafu) aliyefariki dunia Disemba 22, 2014 na kuzikwa Disemba 27, 2014 nyumbani kwake Dar es Salaam. 
  Aidha shukrani za pekee tunatoa kwa Paroko, uongozi na walei wa Parokia ya Mt. Augustino ya Ukonga, Uongozi na wanajumuia wa Jumuia ya Mt. Monica ya Sabasaba Ukonga, Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Uongozi na watumishi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (MAFC), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (NAOT), Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Ofisi ya Umoja wa Mataifa New York. Tunatoa shukrani za pekee pia kwa Dk. Kaushik Ramaiya, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal kwa huduma ya matibabu wakati wa uhai wa Baba yetu Mpendwa. 
  Tunatambua pia michango ya kipekee ya wanaukoo wa Masoi na Minja, familia za Mshanga, Kajiru, Milanzi, Msolla, Msinjili, Leshabari, Mlay na majirani zao. 
  “Raha ya milele umpe ee Bwana, na Mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani”
  Amina 
  “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo
   nimeumaliza, imani nimeilinda”

  (2Tim 4:7)

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini. Kutoka kulia ni  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mhe Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD). 
  Nyuma yao ni mjane wa marehemu John Garang aliyekuwa Mwenyekiti wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng de Mabior na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Thobias Makoba. Meza kuu toka kushoto  wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wwa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Naibu Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol

  baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia  sehemu ya wakazi wa Nungwi na Wafuasi wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.Kinana amewataka Wananchi hao kuwa makini na baadhi ya viongozi wenye tamaa ya madaraka kwa kuahidiwa mambo ambayo hayatekelezeki,pia amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi siku ikifika ya kupiga kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa,kwani imejaa mambo mengi na mazuri kwa Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla.
   Sehemu ya umati wa wakazi wa Nungwi na Wafuasi wa CCM wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipowahutubia mapema leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Skuli,Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Nae amewataka vijana kuacha tabia  yakushabikia vyama ambavyo havina msaada kwao
   Sehemu ya Meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Nungwi akiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,aliwahutubia mapema leo jioni kwenye uwanja wa Skuli,jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.
   Baadhi ya Wanachama wapya wapatao 284 waliojiunga na chama CCM wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama
  Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.

  0 0
 • 01/22/15--13:40: bwawa la maini


 • 0 0
 • 01/22/15--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Mayaula Mayoni "Mbongo"

  0 0

  Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania
  Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage.
  Amezungumza mengi kuuhusu
  Karibu usikilize hapa chini

  Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja

  0 0

     Katibu wa Mbunge viti maalum, Tumaini Mwakatika akizungumza jambo katika hafla ya utolewaji wa madawati 84 kwa shule za msingi Ivumwe na Itiji jijini mbeya kwa niaba ya mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya,Dkt. Mary Mwanjelwa kwa kushirikiana na Benki ya NMB.

  Baadhi ya viongozi wa Benki ya NMB, walimu pamoja na Katibu wa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Msingi Ivumwe Jijini Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kukabidhi madawati hayo. 


  0 0

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. George Masaju ameahidi kutumia uzoefu wake alioupata katika ngazi ya Taifa na Kimataifa katika kuhakikisha jukumu alilokabidhiwa na Taifa analitekeleza katika misingi ya uadilifu. 
  Mhe. Masaju alitoa ahadi hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kushika wadhifa huo.
   Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa  V.I.P  uliopo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar mazungumzo ambayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis Bakari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Fatma Abdulhabib Ferej pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh. Said Hassan Said. 
  Mhe, Masaju alisema yeye kama wakili wa Serikali atakuwa kiungo wa kuunganisha uhusiano unaohitajika kuendelea kuwepo kati ya Serikali mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  “ Naahidi kusimamia ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania { SMT } na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar {SMZ } nikitumia uzoefu wangu nilioupata katika masuala ya kisheria “. Alisema Mwanasheria Mkuu huyo.
  Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimpongeza Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. George kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. 
  Balozi Seif alisema Rais wa Kikwete hakufanya makosa Kumteua Mh. George kutokana na umakini wake wa kutekeleza jukumu analokuwa akikabidhiwa na umma. Alimkumbusha Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuzingatia maadili yanayosisitiza uwajibikaji uliotukuka ambao hutoa fursa kwa kila mwananchi kupata haki zake kwa mujibu wa sheria. 
  Balozi Seif alieleza kwamba wadhifa wa uanasheria Mkuu wa Serikali sio kazi nyepesi kwa vile unasimama kwa kazi moja ya kuunganisha pamoja kati ya Serikali na ile mihimili mengine ya Nchi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba wanasheria wakuu wote wawili wa Zanzibar na Tanzania wataendelea kufanya kazi kwa kusaidiana. 
  Balozi Seif alimuhakikishia Mwanasheria Mkuu huyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar muda wote itajitahidi kumpa ushirikiano mzuri ili awe na uwezo madhubuti wa kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akimpongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. George Masaju  aliyekaa upande wa kulia kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.
  Aliyepo upande wa Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria wa Sewrikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis Bakari.
  Mhe. Masaju  amefika Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kushika wadhifa huo.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. George Masaju akitoa ahadi kwa Balozi Seif ya kufanya kazi zake kwa uadilifu wakati akijitambulisha rasmi kushika wadhifa huo. Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Katibu Tawala Wilaya ya Ileje Bw. Francis Mbenjile katikati akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo walipomtembelea ofisini kwake jana wakati wa ziara ya kuhamasisha vijana wa Ileje kuhusu Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Wilaya ya Ileje Mkoa wa Mbeya.
  Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akitoa mada ya Stadi za Maisha kwa vijana wa Wilaya ya Ileje walioudhuria semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Ileje Mkoa wa Mbeya.
  Baadhi ya Vijana wa Wilaya ya Ileje wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyokua yakiendelea wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Ileje Mkoa wa Mbeya. (Picha na Genofeva Matemu – Maelezo)

  0 0


  0 0

  Mflame Abdullah bin Abdul-Aziz wa Saudia (pichani) aliyefariki usiku wa kuamkia leo anatarajiwa kuzikwa leo baada ya swala ya Ijumaa. Taarifa iliyotangazwa na televisheni ya nchi hiyo imesema kuwa, uongozi umechukuliwa na Salman bin Abdulaziz ndugu wa Abdullah. 
  Mfalme huyo aliyekuwa anakaribia umri wa miaka 90 alipelekwa katika hospitali moja ya mjini Riyadh mwanzoni mwa mwezi huu kwa ajili ya matibabu baada ya hali yake ya kiafya kuzorota ambapo alikuwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji. 
  Habari zinasema kuwa, Mfalme Abdullah amefariki dunia saa saba za usiku wa kuamkia leo kwa majira ya Saudia. Ofisi ya ufalme ya nchi hiyo imetangaza kuwa, sala ya maiti itasaliwa baada ya sala ya alasiri ya leo katika chuo cha Imam Turki bin Abdullah mjini Riyadh. 
  Aidha habari zimeongeza kuwa, Salman bin Abdulaziz Aal Saud amepata baiya ya kuwa mfalme kwa mujibu wa katiba ya utawala wa Saudi Arabia ambapo naye amemteua Muqrin bin Abdul-Aziz, ndugu wa baba mmoja wa Mfalme Abdullah kuwa mrithi wa kiti cha ufalme baada yake. 
  Mfalme Abdullah aliyezaliwa mjini Riyadh, alikuwa mtoto wa 13 wa mfalme Abdul-Aziz, mwasisi wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo. Baadhi ya duru zinasema kuwa, bado kuna mivutano ya kuwania madaraka kati ya watu wa ukoo wa Aal Saud. Kupata chanzo BOFYA HAPA

  0 0

  Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel yuko nchini katika ziara fupi kusaidia kumaliza tatizo la Ndoa za utotoni kupitia programu na miradi mbalimbali atakayoifadhili ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu hatimae kujikomboa na umaskini.

  Katika ziara yake mama Machel, amekutana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ambapo, alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa jitihada kubwa inayofanya wizara hiyo kupambana na tatizo hilo la mimba za utotoni.

  Vilevile, aliitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na wadau mbalimbali hususan viongozi wa mila/jadi na dini kushirikiana nae na kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya kupitia program hizo anazotarajia kuzianzisha, na kuongeza kuwa, “Mkoa wa Mara ndio utakaokuwa wa kwanza kuanzishwa kwa program hiyo kwani bado mkoa huo una mila gandamizi. (mfumo dume)”,alisema Machel.

  Naye Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akiongea katika kikao hicho, alieleza kuwa, ni kweli tatizo hilo lipo nchini lakini Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari, wanapambana kikamilifu kumaliza tatizo hilo.

  Aidha, Waziri Simba alitumia fursa hiyo kumshukuru Mama Machel kwa jitihada anazozifanya kuwawezesha watoto wa kike kuondokana na umaskini.
  Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba (katikati) akimsikiliza Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Gracia Machel (wa pili kushoto) aliyefika Wizarani hapo kujadili program maalum ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu.
  Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Gracia Machel (wa pili kushoto) aliyefika Wizarani hapo kujadili program maalum ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu. Wengine pichani toka kulia ni Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Nuru Millao na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Benedict Missani.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara.
  Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo katika shuleni hiyo.
  Akipokea msaada huo Diwani wa kata ya Central wilayani Kiteto Mh Yahya Masumbuko, amesema shule nyingi wilayani hapo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.
  “Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Kiteto hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Mh Masumbuko.
  “Uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pia ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa wilayani” aliongeza Mh Masumbuko.
  Aidha Diwani huyo ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel  kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo  ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.
  “Msaada huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa vitabu vya sayansi” alieleza Mh Masumbuko.
  “Sisi wa Kiteto tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wanafunzi wetu wanajifunza masomo hayo na ndio maana hata mgao wa walimu tulioupata tumeuelekeza katika ufundishaji wa masomo ya Sayansi. Alimalizia Mh Masumbuko. 
  Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwawezesha kupata vitabu vitakavyowasaidia katika masomo yao.
  Msaada huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo ya wilayani Kiteto mkoani Manyara.
  Airtel shule yetu ni mpango endelevu uliodumu kwa takribani miaka 10 iliyopita mpaka sasa zaidi ya shule za sekondari 1300 nchini zimeidika na msaada wa vitabu chini ya mradi huu. Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha sekta ya elimu na kutoa kipaombele kwenye masomo ya sayansi ili kuwa na wanasayansi wengi nchi ambao kwa sasa ni changamoto katika shule nyingi na nchi kwa ujumla alisema Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kati Bwana  Hendrick Bruno
   Wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto mkoani Manyara wakionesha vitabu baada ya kukabidhiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wake wa "Airtel shule yetu" wenye lengo la kuchangia katika sekta ya elimu nchini.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Damien Thuriaux alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa IOM alifika ofisini kwa Waziri Chikawe kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji pamoja na ushirikiano kati ya Wizara na shirika hilo. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Damien Thuriaux alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa IOM alifika ofisini kwa Waziri Chikawe kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji pamoja na ushirikiano kati ya Wizara na shirika hilo. 
  Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  THE BEAT FESTIVAL “Unplugged” at a NEW VENUE
  TONIGHT - 17.00 - 23.00 
  Venue: Makuti / Vipaji Gallery, Mtwara Rd (see signboard between Club Maisha and Oysterbay Shopping Center).
  Entrance: 10.000 TSH only

  This edition is dedicated to the singer-songwriter tradition of acoustic guitar and vocals. The event features a long list of performers and we break the rules here and there by replacing the guitar with a traditional Gogo bowed fiddle called the Zeze. Get ready to lounge, listen and enjoy a wide range of unplugged performances.

  Vitalis Maembe – 18.00
  Vitali Maembe is a singersongwriter based in Bagamoyo, where he completed his music studies at the Bagamoyo School of Arts. He is known for his socially conscious song writing which comments on daily life in Tanzania. He has a way of captivating his audience with his socio-political and powerful lyrics both live but also through his studio album “Bagamoyo”.

  Lea and Grace – 18.45
  Grace and Lea are Gogo musicians from the Zawose family. They are known for their work with Msafiri Zawoze, son of the esteemed late Hukwe Zawose who was signed to Peter Gabriels record label ‘Real World’. When performing with Msafiri, Lea and Grace will usually play “hour-glass” shaped drums, which are traditionally played by women. Tonight they will be performing Zeze and Marimba which are traditionally only performed by men.

  Jim Kroft – 19.30
  Jim Kroft is an eclectic singer-songwriter originally from the UK, but based in Berlin who has embarked on an artistic and physical journey where he fuses music, photography and film with travel. Journey #1 took him to China and Journey #2 has brought him to East Africa where he has immersed himself in the local culture through his art. It is a pleasure to host him at this special edition of THE BEAT, which in fact might have been born through his presence.

  Samwel Hokororo – 20.15
  Samuel Hokororo, was born in 1990 in Temeke, Dar es Salaam. He started singing when he was eight years old, at school, at home and in the church choir. In 2006 he went to the Dogodogo center – a center for street children – and received training in theatre, dance and music. It was there that he learned to play the guitar. Samuel was an excellent student and since he left the Dogodogo center in 2008 he has been working full time with music.

  Mzungu Kichaa – 21.00
  Mzungu Kichaa plays guitar and sings in Swahili and English. Debuting in 2009 with his album Tuko Pamoja, Mzungu Kichaa and his band Bongo Beat have created a unique style of Congolese inspired Bongo Flava. For this unplugged edition he will be performing his songs accompanied only by his acoustic guitar.

  ASHIMBA – 21.45
  Ashimba is a talented singer and songwriter. He has a passion for intricate and complex compositions. His sound borrows from the West African griot traditions fused with his own unique style of guitar playing and traditional Tanzanian music.

  ABOUT THE BEAT: The Beat is a monthly festival that takes place on the first Friday of the month, showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is hosted by Mzungu Kichaa and is powered by: Caravan Records, and Goethe Institut Tanzania. 

  0 0  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahya  akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-Maelezo. Balozi Yahya aliwaomba wanahabari hao kuwafikishia ujumbe Watanzania wote ili wachangamkie fursa za ajira katika Shirika la Ndege la Emirates. Wengine katika picha, kulia ni Konseli Mkuu wa Konseli ya Tanzania nchini Dubai Bw. Omar Mjenga na kushoto ni Kaimu Mkuu Mtendaji kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA) Bw.  Boniface Chandaruba. Emirates ni moja ya Shirika la Ndege tajiri duniani.
  Balozi Yahya akiendelea kuzungumza.

  bofya hapa kwa habari na picha zaidi

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Afrika (OAU),Dkt. Salim Ahmed Salim akizungumza na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika DRC Balozi Said Djinit ambaye alimtembelea nyumbani kwake jana kusalimiana naye. Balozi Djinit aliwahi kuwa Msaidizi wa Mheshimiwa Salim Ahmed Salim wakati akiongoza OAU.

older | 1 | .... | 715 | 716 | (Page 717) | 718 | 719 | .... | 3348 | newer