Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 5 | 6 | (Page 7) | 8 | 9 | .... | 3285 | newer

  0 0

  DJ Topspin (Barry Blendiana Jones Gayle) is officially welcomed to Club 327 by the owner Mr. Lawrence Kadri in the Hennessy VIP Suite.
  =======    =======  =======

  DJ Topspin arrives in Dar and Club 327 promises to keep prices affordable for New Year’s Eve.


  It has been a long time since there has been this much anticipation surrounding the arrival of a DJ in Dar es Salaam but Bongo has become a favorite for the American DJ, Topspin, and last night he put his fans at ease announcing his official arrival in country.  Last night after touching down at JNIA, the American, DJ Topspin was taken right away to Club 327 where he was officially welcomed by club owner, Mr. Lawrence Kadri, inside the Hennessy VIP Suite.


  Since Club 327’s announcement of DJ Topspin to be the headliner for the day, there has been great anticipation among music lovers in Bongo, as the American DJ is already a favorite in Dar es Salaam since he came over a year ago to celebrate the two-year anniversary of Groove Theory, a once month soulful house music event.  He was also a co-host of the every popular radio show, The Countdown, on Choice FM for two years.


  Speaking after arriving, DJ Topspin said he is very excited to be here, as Tanzania is a destination that ranks high on his list of global party spots as he even passed on a New year’s Eve party in the Central American country of Panama this year to return to Dar es Salaam.On his side, Club 327 owner, Lawrence Kadri welcomed Tanzanians music lovers to come at Club 327 and celebrate the night on the dance floor.


  “At Club 327 we are firm believers in originality in the market. That is why we have positioned Club 327 as the place to be for anyone who loves music” said Kadri who also added “Club 327 will not raise our prices on New Year’s Eve, we will remain true to our motto of affordable clubbing, so music fans can be assured that at Club 327 they can bring in the New Year without breaking the bank”. It is common practice for clubs to raise admission as high as 500% on New Year’s Eve in Dar es Salaam. However, Club 327 will not be one of them.


  New Year’s Eve festivities kick off at 9pm on the 31st and DJ Topspin is expected to start spinning a little before midnight and continue deep into the morning. 


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akijadiliana jambo kuhusiana na mkutano mkubwa wa kimataifa wa ushirikiano kwa manufaa ya wote, Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013’, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi Mei mwaka 2013 alipokua akiongea na wanahabari jijini la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda na kushoto ni Meneja Mradi wa Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013,’ Rosemary Jairo.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akijadiliana jambo kuhusiana na mkutano mkubwa wa kimataifa wa ushirikiano kwa manufaa ya wote, Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013’, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi Mei mwaka 2013 alipokua akiongea na wanahabari jijini la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda na kushoto ni Meneja Mradi wa Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013,’ Rosemary Jairo.


  0 0

  RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KESHO ANATARAJIWA KUZINDUA RASMI MATOKEO YA AWALI YA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI.

  SHEREHE ZA UZINDUZI HUO UTAKAOAMBATANA NA KUTANGAZA KWA MATOKEO YA IDADI YA WATANZANIA ZITAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM NA ZITAHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA KITAIFA NA WANANCHI.

  KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA AWALI YA IDADI YA WATU,NI HATU YA MWANZO KATIKA UTARATIBU WA UTOAJI WA TAKWIMU ZITOKANAZO NA SENSA YA WATU NA MAKAZI,AMBAPO MATOKEO MENGINE YATAENDELEA KUTOLEWA KWA AWAMU.

  OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU NA OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, INAWATAKA WANANCHI,WANAHARAKATI NA WADAU WENGINE WOTE WA MAENDELEO KUTUMIA TAKWIMU HIZO KWA UFANISI WA MAHITAJI YAO NA MAENDELEO YA TAIFA KWA UJUMLA.

  ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI LILIFANYIKA TANZANIA NZIMA KUANZIA TAREHE 26 AGOSTI HADI TAREHE 8 SEPTEMBA MWAKA HUU.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,ACP David Misime (mwenye Koti jeusi) akiongea na waandishi wa habari Mkoani Dodoma (hawapo pichani) kuhusu Jeshi la Polisi lilivyojipanga kukabiliana na vitendo vya uhalifu na wahalifu katika sherehe za siku ya Mwaka mpya Mkoani humo.

  0 0

  Na Abdulaziz,Lindi

  UPEPO mkali uliombatana na mvua kubwa umeziathiri baadhi ya nyumba huku shule ya sekondari ya Mnacho wilayani Ruangwa ikipata athari kwa kiasi kikubwa baada ya madarasa sita kuezuliwa mabati na baadhi ya wanakijiji kupata majeraha na kusababisha wakazi wengine kukosa mahali pa kuishi.

  Upepo huo uliotokea jana ni mfufulizo wa matukio hayo kwa vijiji vya kata hiyo ambapo awali mwanzoni mwa mwaka huu uliezua madarasa mawili ya shule hiyo.

  Akitoa taarifa ya maafa hayo ya jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ruangwa leo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,Bw Reubern Mfune alieleza kuwa Kufuatia kuwepo kwa tukio hilo lilitokea jana jioni Ofisi yake ilifika eneo la tukio akiwemo na mkuu wa wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira na tayari wamepelekwa wataalamu kutathimini athari hizo ili shule hiyo inayotarajiwa kuanza muhula jan 14 Halmashauri yake itashirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya kuhakikisha hali ya shule inakamilishwa.

  Aidha Mkurugenzi alibainisha katika kikao hicho cha baraza la madiwani kuwa Katika maafa hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliathiri shule hiyo bado ni changamoto katika Halmashauri yake kufuatia kupangawa kupokea wanafunzi 92 wa kidato cha kwanza na inatarajiwa kufunguliwa jan 14,2013 Katika maafa hayo Mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Padri Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi mwangalizi wa mgonjwa huyo, Namsifu Fue.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Padri Ambrose Mkenda, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, leo Desemba 30, 2012 aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kujeruhiwa na risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa getini akisubiri kuingia nyumbani kwake mjini Zanzibar hivi karibuni. Kulia ni Muuguzi mwangalizi wa mgonjwa huyo, Namsifu Fue. Picha na OMR

  0 0

  Mahmoud ahmad Arusha

  Viongozi wa madhehebu mbali mbali ya dini wametakiwa kudumisha umoja na mshikamano sanjari na kuacha kudharaulina kwani hilo litaleta kumong’onyoka kwa maadili na kubomoa amani yetu na badala yake kuhubiri ushirikiano na kuwajenga waumini wao kuwa na hofu ya mungu.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibi mkuu wa ccm ndugu Abdurahaman Kinana kwenye maadhimisho ya siku ya kumbu kumbu imamu Husein yanayoadhimishwa na dhehebu la khoja Ithnasher kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jamii hiyo jijini hapa juzi.

  Kinana alisema kuwa hivi sasa jamii ya watanzania imeingia kwa baadhi ya watanzania kuwauza wenzao huku ni kutaka kuleta mpasuko kiimani na wengine kujenga uadui kwa kudharau madhehebu za wenzao tufike mahali tuheshimu na kujifunza yale yalio kwa mwenzako kwa ustaarabu na kuvumiliana.

  “Ustaarabu wa kuvumiliana na kuweka upendo miongoni mwetu ndiyo silaha ya kuitunza amani iliyopo hapa nchini nawaombeni viongozi wa dini hapa nchini kuwajenga waumini kuwa na hofu ya Mungu ili taifa letu lisikumbwe na mipasuko ya kiimani”alisema Kinana

  Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga alisema kuwa kumekuwa na vikundi vya kiimani ambavyo vimesajiliwa lakini vimekuwa vikichochea uvunjifu wa amani na kuvitaka kuacha kuipoteza amani iliyopo kwani kutafuta ni gharama kuliko kuitunza.

  Kasunga alisema kuwa anatoa wito kwa viongozi wa madhebu hapa nchini kuwajengea hofu ya Mungu watumishi wa serekali na wananchi ilituishi salama kwa amani iliyopo serekali pekee haiwezi kuitunza bila ya kushirikiana nanyi na watanzania.

  Nae Sheikh wa mkoa wa Arusha Shaban bin Simba alisema kuwa nchi kuingia kwenye machafuko ni jamii kumuasi muumba wao na kutokuwa na hofu ya siku ya malipo na kuwataka viongozi wa dini kujenga ushirikiano wa karibu na maskizano

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Kinondoni Iddi Azzani, akiwapa mazoezi vijana wa Klabu Jogging 12 za maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Kabla ya bonanza hilo kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa nana kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani hadi.
  vijana wa Klabu za Jogging 12 za maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam wakishiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Iddi Azzani akiongoza timu yake ya Klabu ya Jogging ya Barafu ya Magomeni wakati wakishangilia ushindi wao.
  "Hapa lazima waje..." Mh. Iddi Azzan akishiriki kuvuta kamba.
  Iddi Azzani Akizindua bonanza hilo kwa kupiga penati golini.
  Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam ikivutwa na Timu ya Klabu ya Jogging ya Kawe na kuondolewa.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa kampuni ya Vodacom-Tanzania, Matina Nkurlu (Wapili kushoto), akimuelekeza mmoja wa waandishi habari, jinsi ya kununua bidhaa kwa kutumia huduma ya M-Pesa, kwenye duka la Shoppers, Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kampuni ya vodacom kwa kuanzia imeanza kutoa huduma ya kununua bidhaa kwa kutumia M-Pesa kwenye maduka ya Shoppers ya Msasani na Masaki, yote ya jijini.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya Vodacom-Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia), akichagua bidhaa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari ndani ya duka la Shopaz Plaza Dar es Salaam. Waandishi wa habari walifika kwenye duka hilo , kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia huduma ya M-Pesa.
  Mpigapicha Mkuu wa Kampuni ya Free Media Group, inayochapisha gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, (katikati) pamoja na Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Fidelis Felix (kushoto)wakilipia bidhaa zao kwa njia ya M-Pesa walizozinunua ndani ya duka la Shopaz Plaza Msasani. Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.
  Mwandishi wa habari wa Kampuni ya TSN, inayochapisha magazeti ya Dailynews na HabariLeo, Robert Okanda, akinunua bidhaa kadhaa ndani ya duka la Shopaz Plaza Msasani ambazo alizilipia kwa kupitia huduma ya M-pesa, Kampuni ya vodacom kwa kuanzia imeanza kutoa huduma ya kununua bidhaa kwa kutumia M-Pesa kwenye maduka ya Shoppers ya Msasani na Masaki, yote ya jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu , akiwaelekeza waandishi wa habari ndani ya duka la Shopaz Plaza namna huduma ya M-Pesa inavyotumika kwa manunuzi ya bidhaa ndani ya duka hilo. Waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini walifika dukani hapo kupata mahitaji mbalimbali na kulipa kwa kutumia huduma ya M-pesa.

  0 0

  Mahmoud Ahmad Monduli

  IMEELEZWA kuwa Ujirani mwema katika hifadhi za taifa hapa Nchini imepelekea matukio ya ujangili kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na jamii kuwa makini kwa kutoa taarifa kwa wanaohusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu

  Pia katika kuhakikisha zana ya ujirani mwema inafanikiwa katika jamii inazozunguka hifadhi hizo ni pamoja na kutoa elimu kuhusu uhifadhi na kujenga mahusiano mazuri.

  Akizungumza hivi karibuni na jamii Mwansishi wa habari katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Mhifadhi msaidizi hifadhi ya Manyara idara ya ujirani mwema Bw.Goliath Mtawa alisema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali wanazokutananazo katika kutekeleza miradi husika, jamii imeonekana kuithamini miradi hiyo.

  Bw.Mtawa alisema kuwa ili jamii ithamini miradi hiyo ni pamoja na kuchangia asilimia 30 ya pesa au nguvu kazi,mali gafi inayopatikana katika eneo husika na hifadhi kuchangia asilimia 70 ya mradi uliyoibuliwa.

  “Jamii inapochangia kokoto,mchanga,nguvu kazi katika miradi huwafanya wao kuthamini miradi kwa kiasi kikubwa zaidi”alisema Bw.Mtawa.

  Akielezea changamoto wanayokumbana nayo katika kutekeleza baadhi ya miradi ni pamoja na umaskini ndani ya jamii yenyewe hali inayopelekea kushindwa hata kuchangia katika miradi iliyoibuliwa na kupitishwa hivyo kuifanya miradi hiyo kutofanyika kwa wakati.

  Alitaja baadhi ya miradi waliiyotekeleza kwa jamii kwa mwaka wa fedha 2011-12ni pamoja na kuweka mfumo wa umeme wa jua katika shule ya sekondari Silahamo Wilayani Karatu iliyogharimu shilingi Milioni 35,Josho la kuogeshea mifugo katika kijiji cha Moyamayoka Wilaya ya Babati Milioni 17 na laki tano

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishiriki katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Wafanyakazi wa Magic FM Radio Station ya Dar es salaam 
  wakiserebuka kuukaribisha mwaka 2013

  0 0

   Rais wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kukikacha cheo hicho na kuvunja katiba ya kundi lake la Makapera na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa Msasani Makuni. 
   Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akiserebuka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.
   Maharusi, wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya keki.
   Hapa ilikuwa ni muda wa Kwaito..........
   Sehemu ya wageni waalikwa.....
   Wadau kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha.
   Baadhi ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi, wakipozi kwa picha, baada ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya Keki.
   Sehemu ya wageni waalikwa,..

  0 0  0 0

  Mshambuliaji wa timu ya Mikocheni United Keneth Mutta (kulia) akichuana na Jerry Santo wa Mikocheni City katika mechi ya fainali ya kombe la Diwani iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni, Dar es Salaam jana. City waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 4-3.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuf Mwenda akikabidhi kombe la Diwani kwa Nahodha wa timu ya Mikocheni City, Abdul Abdallah baada ya kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa penalti 4-3 katika mechi ya fainali dhidi ya Mikocheni United iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindi, Dar es Salaam jana.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuf Mwenda (mwenye fulaa ya mistari) akikabidhi pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.7 kwa Nahodha wa timu ya Mikocheni City, Abdul Abdallah baada ya kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa penalti 4-3 katika mechi ya fainali dhidi ya Mikocheni United iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindi, Dar es Salaam jana.

  0 0

  Kampuni yetu ya Rex Energy, wataalamu wa Solar, tulitoa msaada wa chakula kwaajili ya Christmas na Mwaka mpya kwa watoto yatima kutoka vituo vinne vya kulelea watoto vilivyoko hapa Dar: 

  Msimbazi Center Children Home, Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Buguruni Viziwi na kituo cha watoto cha Tanzania Mitindo House kilichoko Magomeni. Tulitoa vyakula mbali mbali ili watoto hawa waweze kusherehekea Christmas angalau kwa kupata chakula kizuri. 

  Tulitoa (kwa kila kituo) gunia la mchele (kilo 100), sukari (kilo 50), mafuta ya kupikia madumu mawili (ya lita 50 na 25), pamoja na mbuzi mnono kwaajili ya kitoweo.
  wafanyakazi wa Rex Energy wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa vituo vinne vya kulelea watoto vya Msimbazi Center Children Home, Buguruni Viziwi, Uhuru Mchanganyiko na Tanzania Mitindo House nje ya kituo cha Msimbazi Center.
  wafanyakazi wa Rex Energy (toka kulia) Diana Mokiwa, Medard Rweikiza, Vera Bosco na Meneja wao Vincent Mughwai wakiwa na watoto yatima wa kituo cha Msimbazi Center Children Home.
  Vincent Mughwai na timu yake wakiwa na watoto yatima wa Msimbazi Center Children Home.
  Kiongozi mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Msimbazi Center Children Hom, akipoea vyakula toka Kampuni ya Rex Energy.
  Mlezi wa shule ya viziwi Buguruni akitoa shukrani kwa kampuni ya Rex baada ya kupewa vyakula.
  Vincent Mughwai, Meneja Uendelezaji Biashara, Rex Energy akiwashukuru walezi wa vituo hivyo na pia kutoa salamu za Christmas na mwaka mpya kwa watoto yatima kwa niaba ya kampuni yao.

  0 0


    Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani. Mbali ya kukabidhi vyakula hivyo, Msama pia alikabidhi hundi ya sh milioni 1.5 kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Msaada huo  umetokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula 
   Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 1.5 Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani kwa ajili ya kulipia ada za wanafunzi waliofukuzwa shule. Mbali ya kukabidhi hundi, Msama alikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vikiwa na thamani ya sh milioni 3 zilizotokana na mapato ya tamasha la Pasaka, hafla hiyo ilifanyika Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
  Dua ya kumshukuru mungu ikisomwa.Picha zaidi Bofya hapa

  0 0

  The Board of Directors of Tanzania Standard (Newspapers) Limited (TSN) has appointed Mr Gabriel Nderumaki (pictured), the company's Acting Managing Editor effective December, 24, this year.

  Mr Nderumaki (46) takes over from Mr Mkumbwa Ally whose contract with the company expired on December 15.

  The new acting Managing Editor has been with TSN for over 20 years and served in senior editorial positions including Sports Editor, News Editor and Business Editor.

  "I am ready for the new challenge and looking forward to getting maximum co-operation from readers, government, private sector and all other stakeholders," Mr Nderumaki.

  He pledged that under his leadership, TSN who are the publisher of Daily News, Sunday News, Habari Leo, Habari Leo Jumapili and SpotiLeo, will continue to publish well researched educative and informative, as opposed to unreasonable sensational articles.

  "We will continue to publish informative stories in support of the government's initiatives to improve the lives of Tanzanians and when necessary provide constructive criticism, as opposed to unreasonable sensational articles.

  "To investors and the private sector, we will continue writing balanced and educational stories about their role in national development," he said.

  TSN is a registered company and has been in the newspapers industry for more than 70 years. The company is currently wholly owned by the government.

  The company also owns state-of-the-art printing press.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimjulia hali Baba yake mzazi Mzee Savere Kayanza Pinda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Moi kwa matibabu ya Maradhi yanayomsumbua.Mzee Pinda yupo hospitalini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo la nyonga.kulia kwa waaziri mkuu ni Muuguzi mkuu wa zamu wodi hiyo Edna Mhina na kushoto kwa waziri mkuu ni Donatila Kwelukila ambaye ni afisa muuguzi chumba cha wagonjwa mahututi


  0 0
 • 12/31/12--00:17: Article 8


older | 1 | .... | 5 | 6 | (Page 7) | 8 | 9 | .... | 3285 | newer