Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

ALICHOZUNGUMZA RAIS WA TFF BAADA YA WAAMUZI 11 KUPATA BEJI ZA FIFA


Barafu yaanguka katika maeneo ya DMV

0
0
Embedded image permalink
Na Abou Shatry DMV 


Kama vile matangazo ya hali ya hewa yalivyo tolewa mwazoni mwa wiki hii na National Weather Service, katika maeneo mbali mbali ya hapa DMV kwamba  hali ya hewa itazidi kuwa baridi na kutegemea kuanguka  theluji ya inches mbili hadi tatu  katika maeneo mbali mbali hapa DMV

Theluji hiyo iliotarajiwa kuanguka mapema mapema mida asubuhi 6: AM ya leo Jumanne Jan,6 na kutegemea kusimama kuanguka mida ya 11:AM ya Saa tano mchana . 

Aidha maeneo mbali mbali ya barabara kuu yameonekana kufanyiwa usafi mapema  na magari ya usafishaji kumwagiliaji chumvi maalumu ambazo hupunguza mitelezo inayotokea mara kwa mara wakati theluji hizo zinapotokea kila ifikapo msimu wa baridi.

Pia tunapenda kutoa tahadhari kwa  Madereva wa magari kuwa makini na theluji ambayo husababisha ajali za barabarani  na haswa mnapokuwa katika barabara kuu za Highway na njia za ndani, kwa maana hadi sasa mitelezo na mafoleni baadhi ya maneno mbali mbali yameshaanza kujitokeza katika baadhi ya mabarabara Ndani ya DMV kwa hiyo tunawaomba waTanzania wote wanaoishi maeneo yaliokubwa na theluji hiyo kuwa makini wakati unapoendesha gari lako.

Ujumbe wa JK leo

saida karoli alipotinga hollywood...na mengineyo ya bongo movie na zamaradi mketema wa clouds tv

PROF. LIPUMBA AKIWASHUKURU WANANCHI BUGURUNI

0
0
Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF.  Prof, Ibrahim Lipumba   alipokuwa akiwashukuru wananchi wa Buguruni Dar es Salaam leo kwa  kupiga kura na kukipa ushindi  mkubwa na imani walio ionyesha kwa wagombea wa chama hicho kuwezesha kunyakuwa mita 5 na Chama cha Mapinduzi CCM kunyakuwa mta 1, nakuwaomba wananchi wazidi kuwa na imani na cha hicho.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Mjumbe wa Chama cha Wananchi CUF na Kiongozi wa Sanaa Mshikamano cha Temeke Shamte Mpendaraha  alipokuwa akisoma risala kabla ya mgeni Rasmi kuongea.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MCHEPUKO UNAPOGONGA MWAMBA

0
0
Mara baada ya kutokea kwa tatizo la gari kubwa kuziba njia katika eneo la Kiwangwa Wilayani Bagamoyo,magari mengi yalilazimika kutafuta njia mbadala ya kukwawezesha kuendeela na safari zao,lakini bahati mbaya huku nako kukatokea lingine na lori la mchanga kukwama kwenye udongo na kusababisha adha nyingine kwa wasafiri waliokuwa wakitumia njia hii.
Lori hilo likiwa limekwama kwenye dongo kutokana na uzito mkubwa liliokuwa nao,hali iliyopelekea adha nyingine kwa watumiaji wa njia hiyo.
Sehemu ya Abiria waliokuwa kwenye magari mbali mbali yaliyokwama katika eneo hilo walilazimika kutembea kwa miguu kuelekea barabara kubwa ili kuona kama watafanikiwa kupata usafiri.

SAFARI LAGER YATANGAZA RASMI UPATIKANAJI WA FOMU ZA PROGAMU YA SAFARI LAGER WEZESHWA MSIMU IV

0
0
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi upatikanaji wa fomu za programu yake ya Safari Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati Nchini. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa alifafanuwa ya kwamba “ Fomu za ushiriki zitapatikana kwenye mabohari ya TBL, Mawakali wa kusambaza bia, kwenye mtandao wa www.wezeshwa.co.tz .

Fomu hizo zichukuliwe, zijazwe na kurejeshwa kwenye vituo vilivyotajwa hapo juu au kwa njia ya posta kwa sanduku la posta (Safari Lager Wezeshwa msimu wa nne,Tbl Dar es Salaam,P.o Box 9393 DSM).

Alisema Bi Edith, hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini kwani itarahisisha kazi kwa kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.

Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.

Programu hii itafanyika takribani mikoa yote ambapo itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao alisema Bi Edith.

Meneja wa bia ya Safari Lager, Edith Bebwa alimaliza kwa kutaja tarehe ya mwisho wa kurejesha fomu kuwa ni 20,Februari 2015 hivyo wajasiliamali wanapochukua fomu wakumbuke pia muda wa kuzirejesha walipozitoa.

Nae kiongozi wa wataalamu wa ushauri wa biashara kutoka kampuni ya TAPBDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa “Zoezi hili linahusisha wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo na kubwa.

Hivyo aliomba wajasiriamali wote kuitumia fursa hii kushiriki kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye fomu ya ushiriki. Wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati kutangaza upatikanaji wa fomu za kuomba ruzuku za wajasiliama kwa msimu wan ne wa program ya Safari Lager Wezeshwa uliofanyika Dar es Salaam jana.Kulia ni Jaji wa Programu hiyo, Joseph Migunda.

Wastaafu watakiwa kushirikiana kwa karibu katika kutumia ujuzi na Taaluma zao za muda mrefu

0
0
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyakazi wastaafu Pemba Bwana Majid Moh’d akimkabidhi risala Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya hiyo hapo ukumbi wa Tasaf Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Chake chake Pemba.
Baadhi ya Wajumbne wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Wafanyakazi Wastaafu Pemba akifutilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akiizindua rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiizindua rasmi Bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Wafanyakazi Wastaafu Pemba hapo ukumbi wa Tasaf uliopo Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Chake chake Pemba. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Wastaafu wa Taasisi za Umma za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na zile za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapaswa  kushirikiana kwa karibu katika kutumia ujuzi na Taaluma zao za muda mrefu ndani ya Jumuiya wanazozianzisha baada ya kustaafu kwao  ili waendelee kuchangia Maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiizindua rasmi Bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Wastaafu Pemba hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Tasaf  uliopo katika Majengo ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar yaliyopo Chake chake Pemba.

Balozi Seif alisema mashirikiano hayo yatatoa nafasi nzuri kwa wastaafu hao kuondoa shaka ya kuendeleza maisha yao kwani baadhi yao hupata wakati mgumu  kabla na baada ya kustaafu kwa vile wanakuwa bado hawajajipanga.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

HONGERA MWENYEKITI MPYA

0
0
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,Mh. Mboni Mhita (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa Serikali ya Mtaa wa Masaki,Kinondoni Jijini Dar es Salaam,Ndg. Kimweri Mhita wakati wa hafla fupi ya kumpongeza mara baada ya kuapishwa kwake,Kimweri ni mmoja wa Wenyeviti wapya waliochagulia katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini kote. 
Mwenyekiti Mpya wa Serikali ya Mtaa wa Masaki,Kinondoni Jijini Dar es Salaam,Ndg. Kimweri Mhita (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake,Dkt. Mohamed Mhita (kushoto) na Mh. Zabein Mhita (Mbunge wa Jimbo la Kondoa Kaskazini) wakati wa hafla fupi ya kumpongeza mara baada ya kuapishwa kwake,Jijini Dar es Salaam jana. 

MBUNGE WA MOROGOR MJINI ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 20 KUTATUA KERO YA MAJI KATA YA MLIMANI

0
0

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kwenye Ofisi ya Mtendaji  kata ya Mlimani Katika Mfululizo wa Ziara zake katika Kata mbalimbali Jimbo la Morogoro mjini.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Vifuko vya mndihira na Mwere Vilivyo Kata ya mlimani Ambavyo Vimegarimu Kiasi cha Shilingi Milion 3 Zilizotolewa na Mbunge Huyo.bofya hapa kwa picha zaidi

VIJANA Kilimanjaro watakiwa kusimama imara na kudai fursa mbalimbali zikiwamo za kupewa kipaumbele katika ajira zinazotokana na mlima Kilimanjaro

0
0
VIJANA wa mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kusimama imara na kudai fursa mbalimbali zikiwamo za kupewa kipaumbele katika ajira zinazotokana na mlima Kilimanjaro.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini na Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Moshi Vijijini, Innocent Melleck alipokuwa akizungumza na waandishi wahabari juu ya mkakati wa kupambana na wimbi la vijana walio mitaani kwa kukosa ajira katika mkoa wa Kilimanjaro .
  Melleck alisema anatarajia kuitisha mkutano maalum kwa ajili ya kuwakutanisha vijana kujadili namna watakavyoweza kufaidika na fursa zitokanazo na mlima Kilimanjaro hususani katika sekta ya utalii.

Tunatarajia mwishoni mwa mwezi huu kukutanisha vinjana wote wanajishugulisha na shuguli za kupandisha watalii mlimani wakiwepo wabeba mizigo,wapishi na wasimamizi wao ambao ni wazawa ili kuweza kujadili njia sahihi ya kufuata kuweza kushinikiza uongozi wa KINAPA kutoa nafasi kwa vijana wazawa.


Alisema pindi mlima huo ukiwaka moto vyombo vya usalama kutumika kuwakamata wazawa kwenda kuzima moto huo tena kwa kutumia nguvu wakati katika swala la ajira rasmi na zisizo rasmi wazawa wameonekana sii lolote kitu na nafasi kuwewa wageni.

Aliongeza ajira katika mlima Kilimanjaro imeendelea kunuka rushwa na ubaguzi mkubwa jambo ambalo linahita mshikamano wa pamoja kwaaji ya ukombozi wa kizazi cha wazawa wa mkowa wa Kilimanjaro,Aliongeza mkoani Arusha katika mlima meru hakuna mtu ambae sii mmeru anayeweza kupandisha watalii katika mlima huo Zaidi ya wameru jambo ambalo ni kinyume mkoani kilimanjaro

"Lazima vijana wetu wafaidike na fursa hizi za kupata ajira badala ya watu kutoka mikoa mingine kuchukua nafasi hizo na wao kubaki kama watazamaji," Kada huyo wa CCM ambaye ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo mwaka huu, alisema unapotokea moto katika mlima huo, vijana ndiyo wanaojitokeza kuuzima hivyo lazima wafaidike nao moja kwa moja.

Alisisitiza kuwa ajira kwa vijana itakuwa ajenga yake namba moja na atahakikisha analipigania hilo kwa nguvu zake zote. "Mlima Kilimanjaro peke yake ukitumiwa vizuri unatosha kutoa ajira za uhakika kwa vijana wetu wa mkoa wa Kilimanjaro hususani jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi vijijini ambao kwa sasa hawana ajira," alisisitiza Melleck

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, Melleck alisema amejipanga kulikomboa jimbo la Vunjo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Augustino Mrema kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP).

Gusa Gusa Min band ndani ya Usiku wa Old is Gold Safari Carnival kila Jumapili

0
0

Na Andrew Chale
Bendi ya taarab ya 'Gusa Gusa Min Band,'  inatarajiwa kurindima kila Jumapili katika usiku wa Old is Gold Taarab ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, kila Jumapili bendi hiyo ya Gusa Gusa itakuwa ikitoa burudani ya kipekee kwa  nyimbo za taarab zikiwemo za zamani na zile za kisasa.
"Kila jumapili  kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao  watafurahia bendi ya Gusa Gusa ndani ya Usiku wa Old is Gold katika ukumbi wa Safari Carnival” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous amewasihi wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia bendi hiyo pamoja na kukumbushana yale ya zamani na kubadilishana mawazo.
Mdau huyo Asia Idarous aliongeza kuwa, usiku huo uliodhaminiwa na  Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo, utakuwa wa aina yake kwa kila atakayefika ukumbini.

FLORA MBASHA: NAKUSHUKURU WEWE UNAYENIOMBEA KUNIUNGA MKONO KATIKA HUDUMA YANGU

0
0
Nina kila sababu ya kukushukuru wewe mdau wangu ambaye umekuwa bega kwa bega nami katika kuiombea huduma yangu hii ya uimbaji. Ninakushukuru sana maana nimeona matunda kutokana na maombi yako. Mungu azidi kukubariki na kukulinda katika shughuli zako za kila siku pamoja na familia yako. 

Flora Mbasha

Maombi yako yamefanyika baraka katika kazi yangu hii mpya ambayo iko sokoni kwa sasa inayoenda kwa jina la NIPE NGUVU YA KUSHINDA. Nimemuona Mungu akinipa Nguvu za kushinda katika maisha yangu, hata ninapopitia magumu lakini Mungu huyu ninayemwamini kila siku ananishindia.

Ningependa kukutia moyo rafiki yangu ya kuwa Mungu yupo na Mungu huyu huyu tunayemwabudu ni mwenye huruma na upendo. Unaweza ukaamuka asubuhi na usijue nini utaenda kukumbana nacho kazini kwako au mahali unapoenda, lakini ukashangaa Mungu anafungua milango ya kujipatia riziki yako. Una heri wewe unajipatia hata sh. 100 kwani kuna watu wengine hata hiyo unayopata hawapati. 

Tuzidi kumtumikia Mungu kwani Mungu wetu wa huruma zana na ni mwema sana kwetu. Kukaa katika uwepo wake kuna faida sana kwani unakuwa umelindwa na malaika wa Bwana.

Nina mengi sana ya kuzungumza na wewe lakini kwa kupitia albamu yangu hii mpya, naamini Mungu atakuinua kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Ninachokuomba ni wewe kwenda kununua nakala hii na ukishanunua mwite na mwenzako mkae na kuisikiliza kwa makini na baada ya hapo chukua ho ujumbe na ufanyie kazi.

Mungu wangu na akubariki sana.

SERIKALI YATAKIWA KUKOMESHA UBABE KWENYE UKEKETAJI

0
0
DSC_0300
Mratibu wa kituo cha TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).

Na Mwandishi wetu, Tarime-Mara
SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.

Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.

Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.

“Hii sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
DSC_0480
Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (wa pili kushoto) akiwasili kwenye mahafali hayo pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem.

MAKAMU WA RAIS MHE. DKT. BILAL AWATEMBELEA NA KUWAFARIJI WAZEE WAASISI WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Machano Mjombo (102) mmoja kati ya Waasisi wa TANU na ASP wakati alipomtembelea kijijini kwake Gamba Mabatini Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kumjulia hali leo Januari 07,2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafamilia ya marehemu Mzee MtumwaKassim, wakati alipowatembelea kijijini kwao Gamba Sokoni Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya kuwafariji leo Januari 07,2015.


Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea waapishwa leo

0
0
 Baadhi ya Wajumbe wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele Wakili wa Serikali kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
 Baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele Wakili wa Serikali (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Wenyeviti na Wajumbe wao wakiwa nje ya Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo wakisubiria kuitwa majini yao kwa ajili ya kwenda kula viapo.
 Sehemu ya Wenyeviti na Wajumbe wao wakijaza fomu za viapo kabla ya kuapishwa.

BANK M KUBORESHA ZAIDI HUDUMA KWA WATEJA WAKE

0
0
 Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Bank M,Allan Msalilwa akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Hayyat Regency ,jijini Dar es Salaam juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu Biashara wa Bank M,Jacqueline Woiso akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.
======= ======== ======== ===========
Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii,Dar.


Benki M imesema imeendelea kuboresha huduma kwa wateja katika uendelezaji wa viwanda pamoja na mikopo katika miradi ya jamii ikiwepo kudhamini maji.


Akizungumza na waandishi leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency Jijini Dar es Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Benki M,Jacqueline Woiso ,alisema kufanya hivyo kuboresha hivyo ni kutaka wateja wa benki M kuendelea kunufaika.


Alisema mikopo waliositisha ni ya nyumba pamoja na elimu na kufungua milango ya mikopo kwa taasisi kwa ajili ya maji na viwanda ili kuweza wananchi kunufaika katika viwanda pamoja na maji.


Jacqueline  alisema benki inawakaribisha wateja wapya kujiunga na benki hiyo ili kuweza kunufaika na huduma mpya zitakazoweza kusaidia jamii kupata  maendeleleo.


Aidha alisema huduma nyingine ni uwekaji wa mashine ya kukusanyia fedha kutoka kwa wateja ili kuondoa usumbufu kutoka sehemu moja kwenda nyingine

ZIARA YA WAZIRI MKUU PINDA KATIKA JIMBO LAKE LA UCHAGUZI

0
0
 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea  silaha za jadi, upinde, mishale na usinga kutoka kwa  Machifu wa kabila la Wakonongo  katika mji wa Inyonga wilayani Mlele akiwa katika ziara ya jibo lake la uchaguzi Januari 7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Halmashauri hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Januari 7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanawake wa  Nsimbo wakati alipowasili kwenye viwanja vya Halmashauri hiyo kuhutubia mkutano wa hadhar akiwa katika ziara ya jimbi lake la uchaguzi Januari7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SERIKALI YAMPONGEZA PROFESA MBWETE KWA KUANZISHA MAKTABA BINAFSI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalum), Prof. Mark Mwandosya akizindua maktaba ya kisasa binafsi iliyoanzishwa na Prof. Tory Mbwete nyumbani kwake Mavurunza B. jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia uzinduzi huo ni Mama Halima Mbwete. Waziri Mwandosya amewataka wasomi hasa maprofesa kuiga mfano wa mwenzao ilikuweza kukuza elimu hapa nchini.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria wa kwanza kilipo anzishwa, Prof. Geoffrey  Mmari walipokutana katika uzinduzi wa maktaba ya kisasa iliyo anzishwa na Makamu Mkuu chuo kikuu huria Prof Tory Mbwete (wa pili kushoto). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji TCU Bw.  Yunisi Mgaya. Maktaba hiyo ipo Mavurunza B nyumbani kwa Profesa Mbwete.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na masoko wa Chuo kikuu huria Tanzania,Dr. Heriet Heller pamoja na wana kamati wenzake walio weza kufanikisha hafla hiyo ya uzinduzi.
Wageni waalikwa wakishuhudia uzinduzi.

Dkt. Magufuli aagiza kufungwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini

0
0
Na JOHN DOTTO,  Mwanza 
 WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo. 
 Mbali ya hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi. 
 Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania. 
 "Tulianze pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo) tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki...vivuko vyote nchini," aliagiza Dkt. Magufuli. 
 Alisema mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo. 
 Hata hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi mapato hayo yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza kwenda na kufanya uhalifu. 
 Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa. "Kama mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao. 
 Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa ya kuvutwa. 
 Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakifurahia baada ya kukata  utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Mfanyakazi wa  kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images