Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 696 | 697 | (Page 698) | 699 | 700 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akisaini nyaraka wakati wa hafla fupi ya kumwapisha, George Mcheche, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi nyaraka za Serikali, George Mcheche, baada ya kumwapisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo mchana.


  0 0

  Balozi wa Tanzania wa Kudumu Umoja wa Mataifa Geneva, Mhe. Modest Mero (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania; Dubai, alipomtembelea ofisini kwake Geneva.
  Wote wawili walilitumikia Taifa kwa pamoja katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York.

  0 0

  Aliyewahi Kugombea Ubunge Tanga Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA mnamo mwaka 2010,Kassim Omar Mbarak almaarufu Makubel,ametangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,baada ya kuvutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza na wakazi wa Mji wa Tanga katika mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 2014 nchi nzima ambapo mkoa wa Tanga umekuwa wa pili kwa kushinda kwa asilimia 97. 

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
  Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.


  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (Trafic), Mohamed Mpinga (pichani), ametoa onyo kwa  baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.

  Kamanda Mpinga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la baadhi ya mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na basi la Kampuni ya Dar Express limepata ajali.

  Alisema, onyo hilo linatokana na kitendo cha baadhi ya mitandao hiyo, jana kusambaza taarifa kuwa kulitokea ajali iliyohusisha gari namba T 640 AXL, huku ikishindwa kutoa ufafanuzi ilikotokea jambo ambalo limezua taharuki kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.

  Mitandao iliyohusika katika kusambaza picha za ajali hiyo ya uzushi ni Bongo Mzuka, Whatsapp, Facebook na Jamii Forum. 

  “Baada ya picha ya basi hilo kusambazwa katika mitandao hii nilipigiwa simu na baadhi ya watu wakitaka kujua kama ni kweli kulikuwa na ajali kama hiyo, iliwaweze kujua majaliwa ya ndugu zao walio kuwa safarini wakitumia mabasi ya kampuni hiyo,”alisema Mpinga.

  Mpinga, aliwatoa hofu wananchi kuwa hakuna ajali yeyote iliyotokea ambayo ilihusisha basi la kampuni hiyo katika siku za hivi karibuni na kwamba gari lililooneshwa katika mitandao ni la uongo kwa vile haliko barabarani. 

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Express,Yudika Mremi
  “Niwashauri wamiliki hawa kuwa wajaribu kuwa makini na waitumie mitandao kwa ajili ya manufaa yao na watu wengune lakini si kwa matumizi kama haya ambayo yanaweza kuwaletea wengine madhara katika maisha yao na ieleweke watu wa aina hiyo wakipatikana watafikishwa katika vyombo vya sheria,”alisema.


  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dar Express, Yudika Mremi 
  alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa ajali hiyo, alisema hata yeye alishtushwa na taarifa hizo, kwa vile gari lililooneshwa katika mitandao hiyo lilipata ajali miaka mitano iliyopita pia haliko tena barabarani tangu kipindi hicho.

  Alisema baada ya kuona picha hizo alichofanya alikwenda Kituo cha Polisi Kinondoni, kufungua jalada kwa ajili ya polisi kufanya uchunguzi ambao utasaidia kujua nia ya watu waliotoa taarifa hiyo ya uongo.

  0 0

  Jengo la Skuli ya Secondary ya Faraja lililofunguliwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kushoto akisalimiana na Muwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan katika ufunguzi wa Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akikunjuwa Kitambaa ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.


  0 0


  0 0

  Na John Gagarini,Globu ya Jamii Kibaha
  WATU wanne wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.

  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa watu hao walikuwa wakimpeleka mgonjwa hospitali.

  Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 5 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana huko eneo la Fukayosi Tarafa ya Msata wilaya ya Bagamoyo.

  Alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari namba T 252 DCB aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na Ramadhana Masapala (32) lilikuwa likitokea kwenye kituo cha afya cha Miono kuelekea hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.

  “Gari hilo lilipasuka tairi la nyuma na kuacha njia kisha kuanguka bondeni na kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao,” alisema Matei.

  Aidha aliwataja watu waliokufa kuwa ni pamoja na dereva Masapala, Mnamisima Semhoro, Stamili Semhoro na Nemganga Semhoro wote wakazi na wakulima wa Miono.

  Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo ni pamoja na mama mjamzito aliyekuwa akipelekwa hospitali Shukuru Jaba (30) na muuguzi wa kituo cha afya cha Miono Mariamu Omary.

  Kamanda Matei alisema kuwa miili ya marehemu hao ilipelekwa hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo huku majeruhi wawili wakipelekwa kituo cha afya cha Miono huku mama mjamzito akiandaliwa kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

  0 0

   Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na baadhi ya waamuzi waliopata hadhi ya kuwa waamuzi wenye beji za FIFA katika hafla fupi ya kukabidhi Beji hizo,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Jumla ya waamuzi 11 wamepata Beji ya FIFA mwaka huu na kupelekea idadi ya waamuzi wote nchini wenye Beji hizo kufikia 18.Picha zote na Othman Michuzi.
   Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akisisitiza jambo kwa waamuzi waliopata beji za FIFA wakati akiwaonyesha kitabu cha Maadili ya FIFA katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Jonesia Rukyaa katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
  Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Kiongozi Mujuni Mkongo katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wamuzi Tanzania,Salim Chama.


  0 0

  Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza 7171 Josephine (kushoto), akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva Alex John wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
  Dereva wa kampuni ya mabasi ya Mohamed Trans, Soud Nassoro (katikati) akitumia kifaa maalum cha kupima kilevi huku askari wa kikosi cha usalama barabara jijini Mwanza, F4278 PC Luge na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa, Domicien Mkama akishuhudia wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo.Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
  Dereva Lucas Kibogi akipuliza kifaa maalum cha kupima kilevi mwilini ili kuangalia kama ana kilevi mwilini wakati wa zoezi maalum la usalama barabarani lililofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo. Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
  Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Koplo Jeremia akimpima kilevi kwa kutumia kifaa maalum dereva Nyange Migoko (katikati) wakati wa zoezi maalum la usalama barabarani lililofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo. Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.

  0 0


  0 0

  Na Abdulaziz Lindi,Globu ya Jamii - Lindi

  Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zilizopo katika mkoa huu wahakikishe shule zote za sekondari ambazo hazina vyoo kwa ajili ya matumizi ya walimu wa shule hizo zijenge kabla hazijafunguliwa.

  Mahiza alitoa agizo hilo katika kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea katika ziara yake ya siku tatu wilayani Nachingwea.Ambapo alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari.

  Agizo la mkuu huyo wa mkoa lilitokana na hali aliyoiona katika shule ya sekondari ya kutwa ya Kilimarondo ambayo ina matundu mawili pekee ya vyoo ambavyo ni kwa ajili matumizi ya wanafunzi wa shule hiyo ambayo inatarajia kufunguliwa mwaka huu.

  Alisem a nijambo lisilokubalika shule ambazo hazina vyoo zifunguliwe bila kuwa na vyoo,hivyo aliwataka wakurugenzi watendaji kuhakikisha tatizo hilo linashugulikiwa kabla ya muhula wa masomo kuanza.

  "naagiza shule ambazo hazina vyoo vya waalimu zisifunguliwe hadi vitapojengwa,nanikatika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kwani bila kufanya hivyo nikuwadhalilisha na kuwatesa waalimu kitendo ambacho hakikubaliki," alisisitiza Mahiza.Alisema huduma bora kwa waalimu ndizo zitakazo waongeza ari ya kufanya kazi moyo na bidii nakusab matokeo mazuri katika shule wanazofundisha.

  Sambamba na agizo hilo,mjuu h uyo wa mkoa amewataka viongozi na watendaji wa serikali katika mkoa huu kuwa karibu na miradi inayojengwa ili waweze kusimamia kikamilifu ujenzi wa miradi hiyo,badala ya kuicha inajengwa bila usimamizi.

  Alisema tabia ya kutokuwa karibu na miradi inayojengwa inasababisha ubadhirifu na kujengwa chini ya viwango.Hivyo kuisababishia serikali hasara ambazo zingeweza kuepekwa.

  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha kwamba zahanati ya kijiji cha Kipara, kata ya Kipara inaanza huduma mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Mohd Gharib Bilal akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Mohd Gharib Bilal akipata maelezo kuhusiana na Compyuta kwa Balozi mdogo wa china alieko Zanzibar Mr.Xie Yunliang katika ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


  0 0


  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii ,Dar

  Wanafunzi Chimbukizi wa Sayansi wameitaka serikali kuwekeza katika masomo ya sayansi ili nchi kuweza kupata watalaam ambao watasaidia kutatua changamoto katika jamii.

  Hayo waliyasema leo wanafunzi wa Sayansi Chimbukizi walioshinda mashindano ya utafiti kwa kutumia malighafi asili ya kutengeneza dawa ya kuua Nzi na Mbuu ambao wamepewa udhamini na Mfuko wa  Karimjee Jivanjee  (KJF)wa kwenda kusoma nchini Ireland.

  Wanafunzi hao ni Dharia Amour Ali na Salma Khalfan Omari kutoka shule ya Sekondari Lumumba  iliyopo Unguja Mjini Zanzibar

  Mkurugenzi wa Wanasayansi Chipukizi ,Dk.Gosbert Kamugisha alisema wataendelea kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili nchi kuweza kuwa watafiti wa kisayansi.

  Kamugisha alisema utafiti wanasayansi Chipukizi kwa kutafuta dawa ya kuua nzi na mbu kwani dawa ambayo wengi wanaweza kutumia kuliko inayozalishwa na viwanda.

  Mwenyekiti wa Mfuko wa Karimjee Jivanjee (KJF),Hatim Karimjee alisema wamekuwa wakitoa udhamini kwa wanafunzi kwa muda mrefu kwani nia ni kutaka taifa liwe na wataalam watafiti watakaotatua matatizo ya wananchi.
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Karimjee Jivanjee (KJF),Hatim Karimjee (wa pili kulia) pamoja na Muwakilishi wa Balozi wa Ireland Tanzania,Carol Hannon wakiwakabidhi Vyeti wanafunzi wawili walioshinda mashindano ya utafiti kwa kutumia malighafi asili ya kutengeneza dawa ya kuua Nzi na Mbuu ambao wamepewa udhamini na Mfuko wa  Karimjee Jivanjee  (KJF)wa kwenda kusoma nchini Ireland,Wanafunzi hao ni Salma Khalfan Omar (kushoto) na Dhariha Amoor Ali.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Egon Kochanke alipofika Ikulu Mjini Uguja leo asubuhi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Egon Kochanke (katikati) alipofika Ikulu Mjini Uguja leo asubuhi akifuatana na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Tamasha la Afrika Stefan Oschman (kushoto).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Misri nchini Tanzania Hossam Mohamram alipofika Ikulu Mjini Uguja leo asubuhi kwa mazungumzo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Hossam Mohamram alipofika Ikulu Mjini Uguja leo asubuhi.[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Na: A. Othman

  Mshairi nguli na mwalimu mzoefu wa Kiswahili ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe kutoka nchini Kenya, Bwana Abdilatif Abdalla amemtembelea mwandishi chipukizi kutoka Zanzibar, Bwana Yussuf Shoka ofisini kwake jijini London mapema wiki hii. Katika ziara yake hiyo fupi Bwana Abdalla alifanya mazungumzo mafupi na mwandishi huyo kuhusu kitabu chake kipya cha ‘Paka wa Binti Hatibu’.

  Gwiji huyo ambaye ametumia muda mwingi kufundisha Kiswahili nchini Uingereza na Leipzig, Ujerumani amejinyakulia umaarufu mkubwa zaidi katika tasnia ya ushairi kwa kazi yake iitwayo ‘Sauti ya dhiki’ (1973)’.Sambamba na kazi hiyo Bwana Abdilatif Abdalla ambaye ni Profesa mstaafu wa chuo kikuu cha Leipzig Ujerumani, kwa sasa amekuwa akitembelea sehemu mbali mbali duniani na kutoa mihadhara yake kufuatia mialiko anayoipata.

  Bwana Abdalla alifika chuo kikuu cha London, SOAS majira ya mchana wa Jumatatu (5-01-2015) na kukaribishwa na mkuu wa Idara ya lugha na Tamaduni za Afrika ambaye pia ni mwalimu wa Fasihi ya Kiswahili Chuoni hapo, Dr. Alena Rettova ambapo pia alikutana na kufanya mazungumzo mafupi na Mwalimu wa Lugha ya Kiswahili na Tafsiri wa chuo hicho Dr. Chege Githiora.

  Katika ziara yake hiyo fupi, Bwana Abdalla alikutanishwa na kutambulishwa kwa mwandishi wa ‘Paka wa Binti Hatibu’ na mwenyeji wake Dr. Rettova ambapo kimsingi mwalimu huyo alitaka kujua kwa kina fasili ya msemo huo na jinsi mwandishi huyo alivyoutumia katika kazi yake hiyo ya sanaa.

  Naye, Mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni mwalimu wa lugha na Fasihi chuoni hapo, Bwana Yussuf Shoka alijadiliana na mtaalamu huyo kwa kina juu ya fasili ya msemo huo na kuhitimisha kwa kusema; ‘Unajua katika utangulizi wa kitabu hiki, mwandishi wa utangulizi Bi Asha Khamis Hamad amesema – ukitaka kujua uhondo wa ngoma ingia ucheze, na ukitaka kujua uhondo wa kitabu hiki kisome’.

  Wakati huo huo, Bwana Abdilatif Abdalla alitumia fursa hiyo kumshauri mwandishi huyo chipukizi kuandika kwa kutumia lugha yake ya kawaida yaani lugha ya kimazungumzo:

  ‘Hakuna haja ya kung’ang’ania usanifu. Andika Kiswahili unachokizungumza katika mazingira ya kawaida. Kiswahili unachozungumza nyumbani na watu wako’. Akiongezea na kutetea hoja yake, Bwana Abdalla alitoa mfano wa Profesa Said Ahmed Muhammed kwa kusema;

  ‘Watu wengi wanashindwa kufahamu uandishi wa Said Ahmed eti kwa sababu anaandika kwa lugha ya kawaida. Lugha ya kwao. Nami siku zote humwambia endelea kuandika hivyo hivyo, kwani hicho ndicho Kiswahili kinachotumiwa na watu wako.’

  Bwana Abdalla pia alimalizia kwa kusema kuwa Kiswahili kimekuwa lugha ya watu wote. Hivyo hakuna haja ya kusema huyu hivi na huyu vile kwani wenye lugha ni watumiaji wa lugha yenyewe.

  Mwandishi huyo pia atatembelewa na mwalimu mkongwe na gwiji wa uandishi wa tamthiliya za Kiswahili visiwani Zanzibar, Bwana Farouk Topan mapema wiki hii. Bwana Topan ni profesa mstaafu wa Kiswahili wa chuo kikuu cha London, SOAS ambaye anajulikana zaidi kwa kazi zake za sanaa ya maigizo kama vile Mfalme Juha (1971), Aliyeonja Pepo (1973) na Siri (2000).
  Profesa Abdilatif Abdalla akiwa pamoja na Bwana Yussuf Shoka. Kushoto ni Mhadhiri wa Kiswahili na Tafsiri, SOAS Dr. Chege Githiora.
  Bwana Yussuf Shoka (Kushoto) akijadiliana jambo na Profesa Abdilatif
  Profesa Abdilatif Abdalla akiwa pamoja na Mkuu wa Idara ya Afrika, SOAS Dr. Alena Rettova. Kushoto ni mwandishi wa Paka wa Binti Hatibu Bwana Yussuf Shoka.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.
  Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
   Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

older | 1 | .... | 696 | 697 | (Page 698) | 699 | 700 | .... | 3282 | newer