Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

LAND ROVER FREE LANDER LINAUZWA BEI POA

$
0
0


2003 LAND ROVER FREE LANDER: T373 bas



Make: Land Rover
Model: Freelander

Year: 2003


Price: TZS 7,000,000/-
Negotiable: Yes
Kilometers: 78,540
Fuel: Petrol

Colour: Blue


Transmission: Automatic
Four Wheel Drive: No
Vehicle Current Location: Dar es Salaam
Contacts: 0784587088 & 0712155221

Vehicle is in Good Condition, its Blue in Color...has a RAV 4 3S Engine with Gear Box


Gari lipo katika hali nzuri na linatembea, pia limefungwa injini ya RAV 4 3s Engine.

WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) PAMOJA NA FAMILIA ZAO WAUKARIBISHA MWAKA 2015 KWA MICHEZO

$
0
0
Kaimu Mmkurugenzi wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha akimkabidhi zawadi Khamis Mussa baada ya kuibuka mshindi wa kukimbia wakati wa siku ya familia ya wafanyakzi wa mamlaka hiyo iliyofanyika katika hoteli ya kunduchi beach jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania TCAA wakishindana kukimbia kwenye ufukwe wa bahari ya hindi kunduchi beach wakati wa siku ya family Day iliyowahusisha wafanyakazi na familia zao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania TCAA wakishindana kukimbia kwa kutumia magunia kwenye ufukwe wa bahari ya hindi kunduchi beach ikiwa ni sehemu ya shamlashamla ya family day.

Mwandosya akagua Miradi ya Ujenzi Busokelo,Rungwe Mashariki, mkoani Mbeya

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu) Profesa Mark Mwandosya (wa tano kulia)  akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ntaba, Bi. Rebecca Hyera (wa nne kulia) kuhusu sehemu ya Mradi wa Umwagiliaji maji wa Katela - Ntaba ambapo limejengwa ghala la mazao ya mpunga na kakao.
Ujenzi wa ghala umetokana na upotevu wa mazao baada ya kukosekana hifadhi.Utawasaidia pia wakulima kupata bei nzuri kwa kuamua wao wenyewe wakati mzuri wa kuuza ziada ya mazao. Ghala hilo lililojengwa kwa nguvu ya wananchi lina uwezo wa kuhifadhi  tani 60 za mazao.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya akipita kwenye kivusha maji cha Mradi
wa umwagiliaji Katela - Ntaba wakati akikagua 

 Miradi ya Ujenzi Busokelo,Rungwe Mashariki, mkoani Mbeya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya akipita maelezo ya Banio la mradi wa umwagiliaji wa Katela-Ntaba.

wakati akikagua 

 Miradi ya Ujenzi Busokelo,Rungwe Mashariki, mkoani Mbeya

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya katika picha ya pamoja na watendaji,viongozi na wananchi baada ya kukagua ghala ya mazao ya Mrafi waumwagiliaji wa Kasysbone-Kisegese.


HUYU NA YULE YA KWANZA PRODUCTION NA VIJIMAMBO: Mahojiano na Dr Crispin Semakula

$
0
0
Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dr Crispin Semakla. Daktari wa mahgonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na pia Mwalimu wa Afya katika Chuo Kikuu nchini Marekani. Pia ni mwanzilishi wa Access Medical and Dialysis Center iliyopo Dar Es Salaam
Ameeleza mengi kuhusu maradhi anayoshughulika nayo na pia kituo chake.

Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

REDIO YA JAMII MKOANI YAZINDULIWA KUSINI PEMBA

$
0
0
DSC_0011
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye koti la suti) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili kuhuduria sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba na kupokelewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph (kulia) aliyeambatana na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (aliyeongoza mbele).

Na Mwandishi wetu, Pemba
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa Redio za jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Zainab Omar Mohammed wakati akizundua kituo cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Pemba.

Shughuli hiyo ambayo ilifanyika kama sehemu ya shamra shamra za sherehe za mapinduzi kutimiza miaka 51 zilihudhuriwa pia na wafadhili wa mradi huo ambao ni Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Waziri huyo alisema kwamba uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii katika jimbo la Mkanyageni Mkoani Pemba ni moja ya azma ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapa haki wananchi wake ya kupata habari ikiwa ni sehemu muhimu sana ya maisha ya wanadamu.
DSC_0038
Munekano wa sehemu ya jengo la Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba kabla ya kuzinduliwa rasmi.

DORIS MOLLEL ACHANGIA VIFAA VYA KUPUMULIA KWENYE WODI YA WATOTO NJITI SINGIDA KWA USHIRIKIANO NA MANIFESTER BRAND

$
0
0
Na mwandishi wetu, Singida.

Katika kuianza safari yake ya huduma za jamii kwa mwaka 2015, Redds Miss Kanda ya kati 2014-2015 Doris Mollel ametoa msaada wa mashine 2 za kupumulia kwenye hospitali ya mkoa wa Singida zenye thamani ya Tsh 1,200,000/=. Mashine hizo huwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida (Pre-mature babies) katika mfumo wao wa upumuaji ambao huhitaji msaada wa juu zaidi mara tu wanapozaliwa.

Doris ambaye pia ni mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2014 ni mwanaharakati wa dhana ya Urembo wenye Malengo endelevu kwa jamii ‘Beauty with a Purpose’. Amefanya kazi kubwa kwenye sekta ya elimu akijikita zaidi kwenye kuchangia Vitabu kwa shule za msingi na sasa, akiwa ni mmoja ya watu ambao walizaliwa kabla ya muda wa kawaida ameamua kupanua wigo wake wa huduma za jamii kuleta mwamko na kusaidia kuokoa maisha ya watoto hawa.

Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo iliyofanyika hospitalini hapo, Mollel alisema. “Kiwango cha vifo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya kukomaa ni karibu 30% vikichangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa vifaa vya kutosha kusaidia mifumo yao ya upumuaji mara tu wanapozaliwa. Nikiwa moja ya watoto hao ambaye nilibahatika kupata msaada na huduma ya kutosha nilipozaliwa, Ninaelewa ni jinsi gani matunzo haya ya awali yalivyo muhimu kwenye kuokoa maisha ya watoto hawa na ninajikita kuwasaidia”.

Bw. Albert Mbepera, Mkurungezi Manifester brand ‘huduma kwa jamii ni eneo muhimu sana kwetu. Tunafurahi kujitolea kufanya kazi na Doris katika maswala ya kusaidia jamii na tunaamini kuwa ushirikiano huu utasaidia kukusanya na kuonyesha matatizo ya wahitaji ili kuongeza uelewa na msukumo wa misaada kutoka kwa sekta binafsi na wanajamii kwa ujumla’

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi Queen Mlozi na ilihudhuriwa na Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Bw. Daniel Tarimo, Daktari bingwa wa watoto wa Hospitali ya Singida, Muandaaji wa Redds Miss Singida 2014 Bora Lemmy na washindi wengine wa Redds Miss central Zone Linda Bureta, blath Chambia, Suzy Wahere.

Doris Mollel na Manifester brand wanapenda kuwashukuru ANUDHA PHARMACEUTICALS LTS kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha shughuli hii.
 Redds Miss Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiongea Maneno machache wakati akikabidi mashine mbili za kupumulia kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa wa Singida, msaada alioutoa kwa ushirikiano na Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikua ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi.
Redds Miss Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiwaona watoto njiti baada ya hafla ya kukabidhi mashine mbili za kupumulia kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa wa Singida, msaada alioutoa kwa ushirikiano na Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikua ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi.(Picha na Albert Manifester).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BENKI YA AZANIA TAWI LA MOSHI, YAWAANDALIA WATEJA WAKE NA WAFANYAKAZI PARTY YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, wakiwa wamejumuika katika sherehe ya kupongezana kwa mafanikio waliyoyapata katika mwaka ulioisha wa 2014 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2015. Sherehe hiyo ilifanyika jana katika Benki hilo, lililoko, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, Bi.Hajira Mmambe, akifungua zawadi katika hafla ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika jana kama sehemu ya kuwapongeza wafanyakazi wa Benki hiyo.  

MEMBE MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA KANISA ANGLIKANA, DAYOSISI YA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akihutubia maelfu ya waumini wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam katika kanisa la Mtakatibu Alban Jumapili.
Waziri Membe akishiriki kusali na waumini wa kanisa la Anglikana Tanzania
Waziri Membe akirekebisha hotuba yake kabla ya kuisoma katika maadhimisho ya miaka 50 ya Jubilee ya Anglikana Tanzania
Sehemu ya umati wa waumini walioungana na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania Mh.Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka 50 ya Jubilee ya Anglikana Tanzania

TPDC yatumia Dola za Kimarekani Bilioni 1.225 kwa ajili ya mradi wa bomba la gesi

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Michael Mwande akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC),James Andilile akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambapo ujenzi huo umefikia asilimia 94. wengine pichani ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Michael Mwande (katikati) na Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO,Kapwalya Mhisomba (kushoto).

UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KITUO CHA POLISI MBWENI,ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati wa Zanzibar,Haji Mwadini Makame akifungua kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wadogo kutoka katika kituo cha Nyerere Shaolin Group wakionyesha umahiri wa kuweza kupambana na uhalifu katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kamishna wa Polisi Zanzibar,Hamdani Omar akitoa maelezo kuhusiana na Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ajali za barabarani zapungua nchini - Kamanda Mpinga

$
0
0
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamanda Mohammed Mpinga(kulia)akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni kuhusiana na maswala ya usalama barabarani,anaeshuhudia kushoto Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamanda Mohammed Mpinga amesema katika mahojiano maalum kuwa madereva wameanza kuelewa kuwa tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (SMS) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto ni uvunjaji wa sheria za barabarani.

Kampeni hii ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani ilizinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mathias Chikawe hivi karibuni na sasa imeanza kuonyesha mafanikio.

MDAU LOOKING FOR A HOUSE TO RENT AT TEGETA, BOKO, UNUNIO & MBWENI AREAS

$
0
0
Kaka Michuzi,
thank you for your good work. Its always a proud moment seeing the good work you do in our social media circles. Keep up and God bless you.
My problem:
Am a young man looking for a suitable house to relocate to (plans of settling down are knocking). Given the housing situation in Dar I have met 'Dalalis' after 'Dalalis' going round looking for a house in  Tegeta, Mbweni,Boko,Ununio & Masiaya areas. 
I think it has to do with my budget. Tsh 250,000/= per month for a simple neat 2 bedroom self contained house in a gated compound (have a car so security is top on the list). Is that too small a figure?Its all I can manage. Jamani nimetafuta wacha masihara!
I think am a relatively wonderful tenant and my current landlord can write a recommendation on that if need be. Could you possibly post for me this ad so that anyone who stays around those areas or along bagamoyo road and has a suitable place that he/she would like a great tenant could contact me? a simple email or pictures of the place to this email will do.  tegetaescrow@yahoo.com . 
Thank you kaka Michuzi!!!!!......

PS:
5 years on you are still the first blog 
I check in the morning at work before my bosses come in!

MAKALA YA SHERIA: UNATAKA NYUMBA/KIWANJA, HAKIKISHA HAYA KISHERIA USITAPELIWE

$
0
0
Na  Bashir   Yakub
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na migogoro ya mashamba, viwanja na nyumba  hasa maeneo ya mijini.  Kwa utafiti wa kawaida utagundua kwa haraka baadhi ya sababu ambazo husababisha hali hii.Uaminifu, tamaa, kutelekeza maeneo kwa muda mrefu, utendaji mbovu wa  baadhi ya watumishi katika mamlaka za ardhi, uzembe na kutojali ni baadhi ya sababu  ambazo huchangia kuwapo  na kukua kwa tatizo hili. 

Baada ya kuwapo  tatizo hili wajibu mkubwa umebaki kwa watu wenyewe kuwa makini na waangalifu  katika mununuzi ya ardhi. Ni uangalifu na umakini pekee ambao waweza kumsaidia mtu kuepukana na  migogoro hii.  Katika kuwa mwangalifu yapo mambo ambayo mtu anaweza kuyafanya . Moja ya mambo hayo ni kuwa makini  kwa kuhakikisha unafuata taratibu zote unapokuwa unafanya mkataba wa manunuzi. 

Mkataba wa  manunuzi ya  kiwanja, nyumba si jambo jepesi kama wengi wanavyolifikiria. Ni jambo nyeti  hasa ikizingatiwa kuwa  ardhi ni mali ya kudumu . Hii maana yake ni kuwa umri wote wa kiwanja au nyumba yako  itakaoishi iwe miaka mia au mia mbili itakuwa inalindwa na mkataba huohuo. 
Hakika si jambo  jepesi. Nataka nieleze kuwa watu wengi wanafanya  mikataba ya manunuzi ya viwanja nyumba kienyeji na kiholela. Wanafananisha mikataba hii na mikataba ya ununuzi wa vitu ambavyo haviishi hata miaka kumi kama magari. 
Ni hatari sana na wengi wamepoteza nyumba  na viwanja kimchezomchezo. Ubaya zaidi ni kuwa unapokuwa na mkataba wa  kiwanja au nyumba ambao haukidhi viwango vya kisheria  na bahati mbaya ukatokea mgogoro ni rahisi sana kupoteza  eneo lako bila kujali ni kiasi gani  umewekeza katika kulimiliki.

MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 AONDOKA RASMI KUELEKEA JIJINI MIAMI KWENYE FAINALI ZA DUNIA.

$
0
0
Mrembo wa miss Universe Tanzania 2014 Nale Boniface usiku wa kuamkia leo ameondoka rasmi nchini kuelekea nchini Marekani kwenye fainali za  dunia za Miss Universe zitakazofanyika jijini Miami tarehe Jaruari 25, 2015.

kutoka maktaba: Basi la Mbeya-Masasi mwaka 1977

$
0
0
Basi lilikata mbuga likitokea Mbeya kuelekea Masasi. Wenye data watusaidie jina la basi hii iliyoletwa na mdau Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu

Yote Uliyowahi Kutaka Kujua Kuhusu Mkito.com: Mahojiano ya Bongo Celebrity na Mwanzilishi Mwenza,Sune Mushendwa

$
0
0
Sune Mushendwa-Mkito.com  
Sune Mushendwa

Kwa miaka nenda rudi, wasanii wa kitanzania walikuwa na kilio kinachofanana. Ungekaa pembeni bila kuwaona, ungedhani kutokana na mwangwi wa kilio chao, anayelia ni mmoja. Hapana. Wote walikuwa [na pengine bado wanaendelea kulia] kutokana na kunyonywa “jasho lao”. Kimsingi “jasho” wanalolilia limekuwa ni soko na usambazaji. Kipaji unacho na watu wanakubali kazi zako. 
Tatizo utaifikishaje kazi yako kwa mashabiki zako? Ni wazi kwamba unahitaji msaada wa kimasoko na usambazaji. Kusema utaweza kufanya kila kitu peke yako ni kujidanganya.Nani? Yupo wapi na utampa kazi zako kwa thamani gani? Kilio chao kilianzia hapo. 
Wengine wakaamua kuachana na muziki [wengine muziki umewaacha wao] kutokana na ukosefu wa soko la uhakika na kuona kadhaa ya kupanga foleni ukisubiri “hela yako”. 
 Mabadiliko ya masoko ya kazi za wasanii duniani kutoka kwenye mifumo ya ki-analojia kwenda kwenye dijitali na pia kutoka katika mifumo ya vitu kama CD mpaka kwenda kwenye matumizi ya simu na vikabrasha vingine vya mikononi, kulimaanisha kwamba soko la wasanii wa kitanzania [na Afrika kwa upana wake] lilikuwa linazidi kufifia. Hakuna tena shabiki anayetaka kubeba furushi la CD. Inakuwaje? 
 Hapo ndipo baadhi ya vijana wakaona fursa kuthibitisha kwamba penye tatizo ndipo pa kukimbilia.Fursa ni kama dhahabu au almasi.Huwezi kuiokota kando ya bahari ikiwa imetupwa ufukweni na mawimbi ya bahari. Wazo la fursa likazaa Mkito.Com mahali ambapo wasanii sasa wanapumua na huku changamoto pekee ni kuwashawishi mashabiki kupakua kazi zao kutoka Mkito.Com. Kila mara shabiki anapofanya hivyo, msanii ananufaika na kupata nguvu zaidi ya kuingia tena studio kunogesha mambo. 
It’s a win win situation.   Sune Mushendwa [pichani juu] ni mwanzilishi-mwenza wa Mkito.Com. 
Kujua mengi zaidi nilimtafuta na kupiga naye story kidogo. Ameelezea mengi. Nakukaribisha usome mahojiano yangu naye ili ujue yote ambayo umekuwa ukitaka kuyajua kuhusu Mkito.Com .

Mkasi | S11E03 With Alain Mulumba

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASHUKURU WAKAZI WA TANGA KWA KUFANYA VYEMA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0
 Wananchi wa Tanga mjini wakimpa mkono wa kumuga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuwashukuru Watanzania kwa kuichagua CCM na kuwashukuru kwa imani yao kwa kutambua chama kinaweza kuongoza.
  Wananchi wakiwa wamefurika uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba 2014.
  Wananchi wakiwa wamefurika uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba 2014.  
  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa kushukuru wananchi kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa January Makamba,Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Abdalah Kigoda na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mheshimiwa Mboni Mgaza.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Tanga,katika uwanja wa Tangamano jioni ya leo,baada ya aliyewahi Kugombea Ubunge Tanga Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA mnamo mwaka 2010,Kassim Omar Mbarak almaarufu Makubel,alipotangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,baada ya kuvutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza na wakazi wa Mji wa Tanga kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa mwenyekiti wa chama CUF-Pongwe,Bwa.Mbaraka Saad Mbaraka kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
 Wakazi wa mji wa Tanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alizungumza nao kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.
PICHA NA MICHUZI JR-TANGA

JK ALIPOTUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WA JESHI MONDULI

MEMBE APONGEZA KANISA LA ANGLIKANA KUPINGA USHOGA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa kusimama kidete kupinga ndoa za jinsia moja, hata pale makanisa mengine ya Anglikana duniani yalipounga mkono suala hilo.
Akizindua sherehe za Miaka Hamsini tangu kuanzishwa kwa Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa hilo jana, Mhe. Membe alisema msimamo huo wa Kanisa na Watanzania uliipa serikali nguvu kukataa shinikizom kutoka nchi za Magharibi kwamba iidhinishe ushoga hapa nchini.
"Mlinitia nguvu sana pale niliposimama kidete kuwaambia rafiki zetu wa nje kuwa katika hilo la ndoa za jinsia moja, Tanzania tunaomba tukubaliane kutokukubaliana," alisema Mhe. Waziri, wakati wa uzinduzi huo uliofanyikia kwenye kanisa la Mtakatifu Albano, jijini Dar es Salaam. Sherehe za Miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam zitafikia kilele Julai, mwaka huu.
Mhe. Membe alisema serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Anglikana na madhehebu mengine ya dini kuboresha maisha ya Watanzania. 
"Naomba muendelee kushirikiana na serikali katika kutoa huduma kwa wananchi," aliwaambia waumini na waalikwa wengine waliohudhuria misa maalum ya uzinduzi iliyoongozwa na Askofu Valentine Mokiwa.
Aliwataka viongozi wa dini kuombea nchi umoja na  amani, na kuhimiza waumini wao kushiriki kikamilifu katika matukio mawili muhimu yanayolikabili taifa mwaka huu -- Kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Uchaguzi wa Rais ni muhimu kwa sababu "Rais wa Awamu ya Tano atategemewa kuendeleza mema ya Awamu ya Nne na awamu zilizopita, na kutoa majawabu kwa changamoto za sasa na zijazo na kutusogeza karibu zaidi na Tanzania njema tunayoitamani, Tanzania yenye neema tele. Hatuko mbali na nchi yetu hiyo ya ahadi," alisema.
Mhe. Membe alishambulia rushwa na Ufisadi kuwa ndivyo vinavyodidimiza nchi na kuongeza umasikini kwa wananchi licha ya Tanzania kuwa na rasilimali lukuki.
 "Tuchague viongozi waadilifu, wazalendo, wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi na marafiki zao," alisema.
Alitaka vijana waandaliwe vyema kushiriki ujenzi na ulinzi wa taifa kwani ndio warithi. "Tukiwaandaa vyema,mustakabali wa taifa letu na watu wake utakuwa kwenye mikono salama. Tukishindwa leo, tutalia na kusaga meno kesho," alionya.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamillius Membe akizindua sherehe ya miaka 50 ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano, jijini Dar es salaam jana Jumapili, Januari 4, 2015, akishuhudiwa na  Dk. Valentine Mokiwa, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.
Waziri Membe akizungumza katika sherehe hiyo


Waziri Membe akikaribishwa na Askofu Mokiwa kwaajili ya utoaji wa vitabu vya kuchangishia fedha kwa ajili ya miradi ya Dayosisi
Waziri Membe akimkabidhi kitabu cha Harambee Askofu Mokiwa.
Picha zote na Reginald Philip. Kwa picha zaidi na BOFYA HAPA


Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images