Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

Moto wa burudani kuwaka Coco beach mwaka mpya kesho mchana kweupee!

$
0
0
Wapenzi wa burudani  ya muziki wa kizazi kipya  watapata burudani ya fungua mwaka kutoka kwa magwiji wa muziki wa kizazi kipya ambao wanatamba nchini katika tamasha la  wazi la maisha murua na Vodacom katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam.Baadhi ya magwiji hao ni Profesa J,Temba,Chege,Roma Mkatoliki na wengineo wengi.

Tamasha hili  litakalokutanisha magwiji wa bongo fleva ambalo limeanza kuwa gumzo la  jiji kutokana na kuwa na burudani za aina mbalimbali kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenzi wa burudani  limeandaliwa na Vodacom Tanzania.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa Vodacom imeamua kuandaa tamasha hili la”Vodacom Maisha ni Murua” kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na  wananchi kwa ujumla katika sikukuu ya  mwaka mpya vilevile wananchi watapata fursa ya kujinunulia bidhaa mbalimbali za huduma za Mawasiliano kwa gharama nafuu.

“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “Ukiwa na Vodacom maisha ni murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani  hivyo ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya  aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema.

Alisema mwaka huu burudani kupitia matamasha haya imekuwa jijini Dar es salaam  wakati mikakati inafanyika kuhakikisha burudani hii inasambazwa kwa wateja wote nchi nzima “Tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu ambao kwetu ni wafalme hivyo tutahakikisha huduma bora na burudani katika kipindi maalum kama hiki inawafikia katika siku za usoni”.Alisema Nkurlu.

VACANCY ANNOUNCEMENT

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Mmeta Manyala.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) mara baada ya kutoa hotuba fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015.
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu Watumishi wenzao ambao wametangulia mbele ya haki kwa mwaka huu 2014.

Matokeo ya Skolashipu za OAF

WAFANYAKAZI WA PPF IDARA YA UENDESHAJI WAFANYA SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Assumpta Maina Mallya akifungua sherehe iliyoandaliwa na idara yake kwaajili ya kupongezana kwa kazi za mwaka mzima, sherehe iliyofanyika katika hoteli ya Tiffany jijini Dar Es Salaam Jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka idara ya Uendeshaji wakimsikiliza Kwa Makini Mkurugenzi wa Idara hiyo wakati akifungua Sherehe ya Kupongezana kwa Wafanyakazi wa Idara hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Tiffany, Jijini Dar Es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA KIKAMILIFU KUHUSU MKESHA WA MWAKA MPYA WA 2015

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba mkesha kuelekea Mwaka Mpya 2015 unakuwa salama, sherehe za mwaka mpya, kuandamana, baadhi ya watu wachache hasa vijana hupenda kuchoma matairi barabarani, kulipua fataki na vurugu za kila aina kwa lengo la kuonyesha furaha yao ya kuingia mwaka 2015.

Hali kama hiyo haitavumiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu badala ya sherehe hugeuka vitisho, vurugu, na kisha kuwatia hofu wananchi wasiokuwa na hatia. Katika harakati hizo Jeshi limeweka mpango kazi utakaowashirikisha askari wa vikosi vyote pamoja na wadau mbalimbali watakaojihusisha na ulinzi siku hiyo. Watakaojihusisha na ulinzi ni pamoja na kikosi cha Zimamoto, kampuni binafsi za Ulinzi, na katika Jeshi la Polisi kutakuwa na kikosi cha FFU na kikosi cha Mbwa na Farasi.

Kampuni binafsi za Ulinzi zitashiriki kikamilifu katika ulinzi huo ambapo watafanya doria za miguu kwa pamoja, doria za magari, pamoja na askari wa pikipiki. Baadhi ya watu hupenda kusherehekea mwaka mpya katika nyumba za ibada ambapo Jeshi la Polisi litatoa ulinzi. Kutakuwa na ulinzi katika fukwe za bahari pamoja na sehemu zote ambazo zinzkuwa na mikusanyiko ya watu wengi kama vile katika Hotel kubwa kubwa na sehemu za wazi. Uwanja wa Taifa utalindwa kutokana na mikusanyiko mkubwa wa watu utakaokuwepo siku ya mkesha pamoja na viwanja vingine vyote vyenye mikusanyiko mingine kama hiyo.

Magari ya Zimamoto yatafanya doria yakisindikizwa na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kwamba yeyote atakayejaribu kuchoma moto matairi au gari atakamatwa na moto unazimwa. 
Kutakuwa na ulinzi wa kutosha ufukweni mwa bahari ambapo Boti za Polisi zitafanya doria ili kuwabaini wahalifu wa aina yoyote kutoka Baharini au nje watakaojaribu kuingia na kufanya uhalifu jijini.

Helkopta ya Polisi itaanza doria kuanzia saa kumi na mbili jioni ili kukagua maandalizi yoyote ya uchomaji moto au uhalifu mwingine wa aina yoyote. Wananchi wanashauriwa kuwa makini na familia zao na hasa watoto wadogo wasiruhusiwe kuingia barabarani wakati wa sherehe hizi kwani ni hatari kwa maisha yao.

Madereva wajiepushe na ulevi ambao wanaweza kusababisha ajali zisizo za lazima pindi wanapoendesha vyombo vya moto katika kipindi hicho. Maafisa, Wakaguzi na Askari watakuwa “standby” kwa shughuli za ziada. Aidha, kutakuwa na mwonekano wa askari wengi wa kila aina kabla na wakati wa sherehe hizo ili kuhakikisha kwamba kuna amani na utulivu wakati wote wa kuingia mwaka 2015.

Wananchi wanaaswa kujihadhari na kufanya vitendo visivyo vya kawaida kama vile kufyatua risasi za moto, kuendesha magari kwa mwendo kasi sana, kupiga honi hovyo, au magari kuwa na milio ya kutisha yenye kero na badala yake wafuate taratibu pamoja na kutii sheria bila shuruti.

Kinyume cha maagazo tajwa hapo, mtu yeyote atakayekaidi na kufanya makosa ya jinai atachukuliwa hatua za haraka na hatimaye kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa mashtaka dhidi yake.

Ni muhimu pia wadau mbalimbali pamoja na wananchi kwa jumla kutoa taarifa wakati ambapo kuna ishara ya uvunjifu wa amani au wakiwaona watu wanaowatilia mashaka watoe taarifa kwa namba zifuatazo:

1.ZCO - Constantine Masawe – SACP:  0713-510 856 / 0658-111 100 
2.RPC ILALA – Mary Nzuki – SACP:     0715-009 980 / 0754-339 558
3.RPC TEMEKE – Kihenya Kihenya – SACP:0715-009 979 / 0754-397 454
4.RPC K’NDON– Camillius Wambura – ACP:  0715-009 976 / 0684-111 111


S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

TAARIFA YA MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JANUARI – FEBRUARI, 2015 NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Februari 2015
Wanahabari wakichukua taarifa inayotolewa na Dkt. Kijazi katika ukumbi wa mikutano TMA.

RAIS WA ZANZIBAR ATOA SALAMU ZA MWAKA MPYA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa salamu za mwaka mpya wa 2015 kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na kuwatakia mwaka wenye Amani na Utulivu pia mafanikio makubwa ikiwemo ya Uchumi wa Taifa letu,hafla hiyo ilifanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]

TUFUNGE MWAKA KWA KUBAKI SALAMA MTANDAONI -

$
0
0
 Mwaka 2014 Umekua Wenye changamoto nyingi sana kwenye upade wa mitandao ambapo wahalifu mtandao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuitikisa anga ya usalama mitandao duniani kote ambapo walifikia kutamba kuwa wameshinda mapambano na wanausalama mitandao.

Kubwa zaidi ni uelewa mdogo wa watumiaji mtandao juu ya kujiweka salama kimtandao iliyo ambatana na wana usalama mitandao kuwa wachache sana katika ngazi ya kidunia huku baadhi ya mataifa kutotoa kipaumbele katika maswala ya usalama mitandao.

Aidha, Mengi katika jitihada yameweza kufikiwa ikiwa ni pamoja na Kikao cha funga mwaka cha tathmini ya hali ilivyokuwa kwa mwaka 2014 ambapo iliweza kutabiri hali ya uhalifu mwaka 2015 na kuweka mikakati ya dhati ya kukabiliana na hali hiyo kwa mwaka 2015 inayotegemewa kuwa na matokeo chanya. Kwenye hili unaweza kulisoma kwenye  “TAARIFA FUPI INAYOSOMEKA HAPA"

Wamarekani nao kupitia “US department of Justice” wameamua kuazisha kitengo maalum kitakachotoa msaada kwa mataifa yote duniani katika upande wa maswala ya usalama mitandao ikisisitiza itaangazia zaidi katika kuzuia matatizo kabla hayajatokea.

Tanzania nayo haikubaki nyumba kwenye hili, Tumeshuhudia warsha, semina, kongamano na mikutano mingine yenye malengo thabiti ya kukuza na kuongezea uwezo wa uelewa wa matumizi salama ya mitandao paoja kukuza uwezo wa kukabiliana na hali ya uhalifu mtandao nchini.

Sheria za usalama mitandao zimeweza kupaziwa sauti na kutoa matumaini makubwa kwa mwaka ujao, Huku vyombo vya habari kuw na jitihada ya dhati katika kampeni ya kutoa elimu na kuhabarisha jamii kuhusiana na janga la uhalifu mtandao linaloweza kuleta athari zaidi kwa taifa.

Nikumbushe tu, Uhalifu Mtandao umeendelea kuja kwa kasi ya juu na njia ambazo watanzania wengi wameweza kuwa waathirika. Kubwa nililoliona ambalo kueleke mwisho wa mwaka limeweza kukamata kasi ni pamoja na uhalifu aina ya “Phishing kama unavyo onekana kwenye picha nilizo tumiwa na baadhi ya raia wema ambapo wengi wameendelea kuathiriwa na uhalifu huu wa kimtandao.

Umakini zaidi unahitajika na tumalize mwaka kwa kuwa salama kimtandao.

MASTAA SIMBA WATAKA PESA, SI MALI KAULI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Dar 

MASTAA nane wa klabu ya Msimbazi wamekacha timu hiyo iliyoandoka leo kwenda Zanzibar kwa kile wanachoshinikiza kulipwa fedha zao. Habari za kuaminika zinasema kuwa mastaa nane wa klabu hiyo wameingia mitini wakiwemo waganda watano na wabongo watatu mpaka hapo watakapomaliziwa fedha zao za usajili.

Wabongo waliokacha timu hiyo ni Shaban Kisiga, Jonas Mkude na Ivo Mapunda hata hivyo kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola jana alikiri kutokuwepo kwenye kikosi chake wachezaji hao na kuweka wazi kuwa Ivo amekwenda Mbeya kwenye arobaini ya mama yake mzazi aliyefariki hivi karibuni, huku akiwa hana taarifa za Kisiga na Mkude.

Pia mbali na wachezaji hao wa kibongo, wachezaji waganda ambao wameingia mitini ni Emmanuel Okwi ambaye alikuwa wa kwanza kutimka mara baada ya kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Kagara. Wengine ni Joseph Owino, Dan Sserunkuma, Juuko Murshid na Simon Sserunkuma.

"Ninaondoka na wachezaji wachache, nina taarifa za Ivo tu ambaye ameenda kwenye harobaini ya mama yake, wengine sina taarifa zao." alisema Matola ambaye hata hivyo ameaidi kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Kikosi hicho cha Simba kimeondoka leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kutimua vumbi keshoJanuari Mosi hadi Januari 13 kwenye uwanja wa Aman visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hanspope alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema kwa kifupi "Nipo Iringa, sijui chochote kinachoendelea Simba kwa sasa, hayo mambo waulizeni viongozi waliopo huko, mi mwenyewe nasikia tu lakini sijui chochote."

Mwenyekiti wa Simba Evans Aveva hakupatikana kuzungumzia suala hilo, hata hivyo mmoja wa viongozi wa klabu hiyo aliiambia Mwananchi kuwa wachezaji hao waliondoka kwa vile Simba hawakuwa na uhakika wa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

"Unajua barua ya kuthibitisha yenyewe imetumwa juzi tu, hatukuwa na uhakika wa kushiriki ndio maana tuliwaruhusu wachezaji kuondoka na warudi tarehe moja, wote wana ruhusa maalum."alisema mmoja wa viongozi wa wekundu hao wa Msimbazi.

SSRA EMERGED AN OVERALL – ATE WINNER UNDER THE CATEGORY OF WORKFORCE FOCUS

$
0
0
In a jovial mood the Director General of SSRA,Irene Isaka receiving a certificate of participation from the Prime Minister Hon. Mizengo Peter Pinda during the Employer of the year Award, where SSRA emerged an overall winner under the category of Workforce Focus. From left is Ms. Zuhura Muro Vice Chairperson of Association of Tanzania Employers (ATE); Hon. Gaudentia Kabaka Minister for Labour and Employment; on right is Mr. Almasi Maige ATE Chairperson.
Very proud with her team the Director General Mrs. Irene Isaka holding a trophy as an overall winner of the Employer of the year Award under the category of Workforce Focus. On left is Ms. Lightness Mauki Director of Compliance and Registration.

HALI ILIVYOKUWA BAADA YA MVUA YA JUZI JIJINI DAR

GORAN AMWAGA WINO KWA MWAKA MMOJA KUINOA SIMBA

$
0
0
KOCHA mpya wa Simba raia wa Serbua Goran Kopunovic amemwaga wino wa mwaka mmoja kuinoa timu hiyo ya Msimbazi.

Mmoja wa viongozi wa Simba aliiambia blog ya jamii kuwa kocha huyo aliyewasili leo asubuhi na kufikia kwenye hotel ya Double Tree Masaki ataondoka kesho kwenda Zanzibar kujiunga na timu hiyo ya wekundu wa Msimbazi inayoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Naye Kopunovic akizungumza muda mfupi baada ya kukanyaga hardhi ya Tanzania alisema "Nimekuja kufanya kazi, naamini nitapata ushirikiano kutoka kwa viongozi wa Simba, wachezaji na mashabiki, Simba ni timu kubwa, naamini nitawapa mafanikio."alisema

Kocha huyo, amechukua mikoba ya Patrick Phiri aliyefungashiwa virago baada ya uongozi wa Simba chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva kufanya tathmini ya mwenendo wa timu ambapo ametoka sare mechi sita, ameshinda mechi moja na kupoteza moja hivyo kuona hastaili kuendelea kuinoa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi huku akidaiwa kukaidi agizo la viongozi la kutowachezesha Waganda katika mechi dhidi ya Kagera walionyukwa bao 1-0

ngoma azipendazo ankal

SERIKALI YAITAKA KAMPUNI YA STEPS KUSITISHA USHUSHWAJI WA BEI ZA FILAMU

$
0
0
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment. 

Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa  na pia haina tija katika tasnia ya filamu. 

Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ALIHUTUBIA TAIFA KWENYE TAMASHA LA MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA,JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi alipowasili Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana usiku Disemba 31, 2014/2015 kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la mkesha wa Mwaka Mpya na Dua maalum ya kuliombea Taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Taifa kwenye Tamasha la Mkesha wa mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika Disemba 31, 2014/2015 usiku wa kuamkia mwaka mpya Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Viongozi na Wananchi kupeperusha bendera ya Taifa wakati ulipoingia mwaka mpya wa 2015 kwenye Tamasha la mkesha na Dua maalum ya kuombea Taifa lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana usiku Disemba 31, 2014/2015.
Wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam wakishangilia kwa furaha wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akihutubia Taifa kwenye Tamasha la Mkesha wa mwaka mpya wa 2015 iliyofanyika Disemba 31, 2014/2015 usiku wa kuamkia mwaka mpya Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwatakia heri ya mwaka mpya wa 2015 Viongozi na Wananchi baada ya kumalizika kwa Tamasha na Dua maalum ya kuliombea Taifa lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Disemba 31, 214/2015. (Picha na OMR)

SIKU YA PILI ILIVYOKUWA KWA MABALOZI WAKATI WAKIPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Mabalozi ,Waandishi pamoja na waongoza watalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea kwa umbali mrefu kueleka Horombo.
Safari ya kuelekea kituo cha Horombo ikaendelea kwa pamoja bila ya kuacahana.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

WAKAZI WA TEMEKE NA VITONGOJI VYAKE WALIPOKEA VYEMA TAMASHA LA TUO8JANUARY, JIJINI DAR

$
0
0
  Hii ilikuwa ni picha ya pamoja ya wasanii na mashabiki waliojitokeza kuunga mkono tamasha hilo la bure ambalo lina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika maamuzi yenye mustakabali wa nchi.

WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya aina yake pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Wakiongowa na  Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili, wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu hiyo.
Akizungumza kabla ya kuimba nyimbo zake kali,Mwana FA akitumia tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuchagua viongozi wanaowataka.
“Vijana wenzangu.., tusisubili watu wengine watufanyie maamuzi.., ni sisi wenyewe tunatakiwa kuamua tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema Mwana FA.
Mara baada ya kusema hayo, alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa sasa ukiwemo, mfalme ambao uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani hapo.
Mbali nma Mwana FA, pia Niki wa pili alipata mapoekzi makubwa viwanani hapo kwa nyimbo zake kali huku pia akisisitiza vijana kuchakua maamuzi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Wanamuziki wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni pamoja na Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and kenzo, Dogo Janja, Madee, Chegge, Temba, mwasiti na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya mashabiki waliojitokeza kuimba nao sambamba.
Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na Morogoro ambapo linalengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba mwaka huu.
Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro. 
 Mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk' akichana mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
 Baadhi ya wakazi wa Temeke waliojitokeza kwenye onesho hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar hapo jana.

Wasanii Chegge na Temba kutoka TMK Wanaume Family wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MBUNGE WA MOROGORO MJINI ATOA WIKI MBILI KWA MTENDAJI WA KATA KURUDISHA FEDHA ZA WANANCHI

$
0
0
 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiongea Kwa Msisistizo Akimtaka Mtendaji wa Kata ya Luhungo Iliyopo Mzee Makame Kai Kurudisha Fedha za Wananchi wa Kata Hiyo Shilingi Milioni 1.4 Ndani ya Muda wa Wiki Mbili lasivyo atangulie Polisi.Mh Mbunge Ametoa Kauli Hiyo katiaka ziara yake aliyoifanya kata ya Luhungo Kwajili ya Kusikiliza Kero za wananchi na Ndipo wakazi wa Kata Hiyo walipotoa Malalamiko kwa Mbunge wao Kuhusu Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata Hiyo Aliyefahamika kwa Jina la Mzee Makame Kai. Wananchi walimweleza Mbunge kuwa Mtendaji huyo amechukua fedha za Maendeleo ya Kata Hiyo Kinyume na Utaratibu na Alipotakiwa kuzirudisha amekuwa na Maneno Mengi Bila Kuzirudisha ia Kufuja Pembejeo za wakulima Ndipo Mbunge Abood Alipotoa kauli ya Kumshugulikia kwa Kumpa wiki mbili fedha za Wananchi ziwe zimerudi.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwasikiliza viongozi wa Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia Jumla ya Shilingi Milioni 2

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images