Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA

$
0
0
1

Watoto yatima walipokaribishwa kusherehekea Krismasi Giraffe hoteli jijini Dar es salaam

$
0
0
 Meneja Mkuu wa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Evelyn Mwasela akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya Sikukuu ya Krimasi kwa watoto wa Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyofanyika hoteli hapo  ilihusisha pia chakula cha mchana.
 Watoto wa Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Dar es Salaam, wakijihudumiwa chakula  cha mchana juzi kilichoandaliwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyopo jijini ambapo pia walipewa zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kama zawadi ya Sikukuu ya Krismasi.
 Mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Cecilia Ismail (kulia), akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake, baada ya kukabidhiwa mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kama zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyoambatana na chakula cha mchana ilifana asana.
 Watoto wanaolelewa katika Kitu cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, wakiwasili katika eneo la Hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam juzi baada ya kualikwa kwa ajili ya kupewa zawadi ya Sikukuu ya Krismasi pamoja na chakula cha mchana. 
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, wakicheza muziki katika ukumbi wa Hoteli ya Giraffe Ocean View, Dar es Salaam juzi baada ya kualikwa kwa ajili ya kupewa zawadi ya Sikukuu ya Krismasi pamoja na chakula cha mchana
 Meneja Mkuu wa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, Evelyn Mwasela (kushoto), akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya Sikukuu ya Krimasi kwa watoto wa Kituo cha Yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, Dar es Salaam. 
Danielle Taboada raia wa Uswisi (katika), akimsaidia mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Tuwapende Watoto cha Bunju, wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na Hoteli ya Giraffe Ocean View, jijini Dar es Salaam. Hoteli hiyo iliwaalika watoto hao kupata chakula cha mchana pamoja na kuwapa mbuzi, mchele na mafuta ya kupikia kama zawadi ya Sikukuu ya Krismasi.

Msaada kwa yatima kutoka CCM shina la Essex UK

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM shina la Essex UK Bi Maryam Seif akiwakilishwa na Mjumbe na mwanachama hai wa CCM (UK) Bw. Bilal akikabidhi msaada wa Deepfreezer kwenye kituo cha Yatima Magomeni Dar es Salaam. 
Msaada huo pia ulishirikisha Charity ya Sunrise Development Association Limited (UK). Azma ni kusaidia kituo hicho kupata mradi wa kuwawezesha kujikimu katika kulea Yati
 Mama Mlezi kushoto akiwa na mmoja wa Yatima hao na kulia ni kada wa CCM Magomeni.
 Baadhi ya Yatima wakiwa na walezi wao.
Bwana Bilal akiwa na mama mlezi na mmoja wa Yatima katika kutoa msaada wa Deepfreezer pamoja na Voltage Regulator.

mambo ya uswazi

ngoma azipendazo ankal

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
MAREHEMU ANTHONY LUPILYA (R.I.P)

FAMILIA YA MAREHEMU ANDREA CONSTANTINE LUPILYA (R.I.P) WA MJINI MWANZA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTOTO WAO MPENDWA ANTHONY LUPILYA (R.I.P) KILICHOTOKEA JANA ALFAJILI TAREHE 25/12/2014 KATIKA HOSPITALI YA SEKOTURE MJINI MWANZA. 

MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 27/12/2014 NYUMBANI KWA MAREHEMU ANDREA C. LUPILYA YAKIFUATIWA NA IBADA ITAKAYO ANZA SAA NANE MCHANA NA BAADAE KUELEKEA MAKABURI YA KAKEBE - NYAKATO MWANZA. 

HABARI ZIWAFIKIE UKOO WOTE WA MAREHEMU A. LUPILYA, UKOO WA BABU ANDREA, UKOO WA BIBI KADO, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.  BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

KWA MAWASILIANO ZAIDI: PIGA SIMU HII: 255-767-246-233 / 255-657-621-427

IMETOLEWA NA FAMILIA YA MAREHEMU ANDREA CONSTANTINE LUPILYA.

SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA

$
0
0
Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku sita.
Baada ya kupumzika katika eneo la Kisambioni na kupata chakula ,safari iliendelea ya kwenda kituo cha Mandara.
Kila mmoja alikuwa na Morali ya juu wakati wote wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baada ya kuongoza msafara wa Mabalozi kama ishara ya kuanzisha upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa Mabalozi,hatimaye Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe alifika eneo la Nusu njia.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Timu ya Taifa ya Mchezo wa Baseball (U18) yashika nafasi ya tatu mashindano ya Kufaulu kushiriki kombe la Dunia

$
0
0
Timu ya Taifa ya Mchezo wa Baseball baada ya ushindi wa nafasi ya tatu (Bronze Medal) katika mashindano ya Kufaulu kushiriki kombe la Dunia la Mchezo wa Baseball Umri chini ya Miaka 18. Mashindano hayo yalifanyika nchini Kenya katika mji wa Meru tarehe 15 - 20 Disemba, 2014 na yalikuwa kutafuta tiketi kwa Bara la Afrika ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika hapo mwakani 2015 katika jiji la Tokyo, Japan.

UJENZI WA BARABARA YA CHUO KIKUU KUTOKEA MBEZI YA KIMARA UKIENDELEA KWA KASI

$
0
0
Pichani juu ni sehemu ya kipande cha barabara ya lami ambacho tayari kimekwisha kamilika,kama kilivyonaswa na Globu ya Jamii wakati ikivinjari katika barabara hiyo jana na kujionea ujenzi huo ukienda kwa kasi,barabara hiyo ambayo imeonekana kuwa na umuhimu mkubwa katika jitihada za kupambana na msongamano wa magari ambao umekuwa kero kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar na kwingineko.Barabara hiyo almaarufu kwa jina la barabara ya chuo kikuu ambayo pia unaweza kwenda Goba ama kuchepuka na kutokea Mbezi ya kimara na kuendelea na safari yako,kwa sasa aghalabu inapitika kwa kiasi kikubwa.


Vodacom Tanzania ilivyowarusha wateja wake kila kona ya jiji la Dar

$
0
0
Mfalme wa muziki wa taarabu na kiongozi wa kundi la Jahazi Modern taarabu Mzee Yusuf akitoa burudani kwa mashabiki wa muziki huo katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Gwiji wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wa muziki wake katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live na kudhamiwa na Vodacom Tanzania hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Linex akiimba kwa hisia kali moja ya nyimbo zake kwa mashabiki wake waliofika kwenye”Tamasha la Vodacom maisha ni murua” lililofanyika katika ufukwe wa bahari Coco-beach hapo jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi.

Balozi Seif Ali Iddi akagua ujenzi wa Bara bara ya Wete hado Konde,Pemba

$
0
0
Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akikagua ujenzi wa Bara bara ya Wete hado Konde ambao uko katika hatua ya lami alipokuwa Kisiwani Pemba kwa ziara ya Siku tatu kuagua shughuli mbali mbali za Maendeleo.
Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Kamati ya Msikiti wa Ijumaa wa Micheweni Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwakumbusha waumini wa dini ya kiislamu kuendelea na ibada zao wakiepuka fitna za kuchanganya na siasa. Picha na Hassan Issa wa - OMPR - ZNZ.

Harakati za ujenzi wa Bara bara ya Wete hadi konde ikiwa miongoni mwa mradi wa Bara bara tatu Kisiwani Pemba zinaendelea baada ya maridhiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na mjenzi wa mradi huo Kampuni ya Mwananchi Contracting Company Engineering { MECCO }.

Ujenzi wa Bara bara hizo wa awamu ya kwanza wenye urefu wa Kilomita zaidi ya 30 ulioanza rasmi Tarehe 15 Mei mwaka 2009 umekuwa ukisua sua kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo uchelewaji wa feha kutoka kwa mfadhili wa mradi huo Benki ya Maendeleo ya Kiislamu { BADEA.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MECHI YA JKT RUVU, SHOOTING KUCHEZWA USIKU

$
0
0
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting itachezwa kesho (Desemba 27 mwaka huu) usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Timu hizo zitapambana kuanzia saa 1 kamili usiku katika mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja (live) na Azam Tv.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa jukwaa la kawaida na sh. 5,000 kwa upande wa jukwaa la VIP.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ambazo ni za elektoniki tayari zimeanza kuuzwa kupitia maduka ya Fahari Huduma, M-PESA kwa kupiga *150*03*02# ambayo utapata namba ya kumbukumbu kwa ajili ya kufanya malipo kupitia hiyo hiyo M-PESA na baadaye kuchapa tiketi yako katika mashine maalumu zilizopo kwenye ATM za CRDB.

Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kupitia CRDB Simbanking.

Mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Abdallah Uhako (Arusha), Godwill Kihwili (Arusha) na Hashim Abdallah (Dar es Salaam).

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina Yahya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.

PINDA AZUNGUMZA NA VIJANA WA MLELE

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na vijana kutoka kata za Kibaoni na Usevya wilayani Mlele mkoani  Katavi waliomtembelea nyumbani kwake Kibaoni  leo akiwa kwenye mapumziko na Krismas na Mwaka mpya. 
Katikati  mwenye miwani ni Mzee Chrisant Mzindakaya
Picha na PMO

TAARIFA YA IBADA TAKATIFU YA KISOMO CHA AROBAINI YA MAREHEMU ANDREA CONSTANTINE LUPILYA

$
0
0
FAMILIA YA MAREHEMU ANDREA CONSTANTINE LUPILYA INAPENDA KUWAJULISHA NDUGU JAMAA NA MARIFIKI KUWA TAREHE 28/12/2014 SIKU YA JUMAPILI KUTAFANYIKA  IBADA TAKATIFU  YA KISOMO CHA AROBAINI  TOKA KUFARIKI KWA BABA YETU  MPENDWA ANDREA CONSTANTINE LUPILYA KUANZIA SAA TANO ASUBHUHI NYUMBANI KWAKE NYAKATO – MJINI MWANZA. 

AIDHA, IBADA HII ITAJUMUISHA IBADA TAKATIFU YA KUMUOMBEA MTOTO WA MAREHEMU BWANA ANTHONY LUPILYA ALIYEFARIKI LEO TAREHE 25/12/2014.

FAMILIA YA MAREHEMU KWA HESHIMA KUBWA INAWAKARIBISHA UKOO WOTE WA MAREHEMU ANDREA C. LUPILYA, UKOO WA BABU ANDREA, UKOO WA BIBI KADO; NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI  KUSHIRIKI KATIKA IBADA HII .  

KWA TAARIFA ZAIDI UNAWEZA KUWASILIANA NA MTOTO MKUBWA WA MAREHEMU BWANA DEOGRATIUS LUPILYA KUPITIA NAMBA YA SIMU HII: 255765-246-233 / 255657621427. 
NYOTE MNAKARIBISHWA 


Alipukiwa na Bomu alipotaka kuwadhuru Polisi Mkoani Ruvuma

$
0
0
Mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka amefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu huku utumbo wake ukiwa nje na mkono wake kukatika alipotaka kuwarushia askari polisi waliokuwa doria usiku wa kuamkia leo na kujeruhi askari polisi wawili ambao hali zao zinaendelea vizuri.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa watu wa nne waliokuwa na mtu huyo wamekimbia huku polisi wakikamata simu za watu hao pamoja na ya marehemu huyo na kwamba hili ni tukio la tatu la mabomu dhidi ya askari Polisi na amasema kukamatwa kwa simu hizo ni mwanzo mzuri wa kuwabaini walipuaji mabomu kwa askari polisi mjini Songea.
Mkuu huyo amesema kuwa kutokana na uzito wa tukio hilo mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini CP Isaya Mungulu anafanya safari kuja Songea leo na atazungumza na vyombo vya habari.
Mwandishi wa habari hii aliyekuwepo eneo la tukio aliweza kushuhudia mabaki ya bomu hilo pamoja na mzula wa kuziba sura aliokuwa akiutumia mtu huyo.

CHANZO: ITV

DK. SHEIN AFUNGUA MASHINDANO YA RIADHA ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati aliupowasili katika Uwanja wa Amaan Studium kufungua Mashindano ya Riadha ya Wilaya kumi za Unguja na Pemba leo.
Wachezaji wa riadha wa wilaya ya wete Pemba wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi Rais wa wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Zanzibar na Mwenyekiti Mohamed Shein kabla ya kuyafungua mashindano ya mchezo huo kwa Wilaya kumi za Unguja na Pemba leo katika uwanja wa Amaan Studium.
Rais wa wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Zanzibar na Mwenyekiti Mohamed Shein akipiga bastola juu kuzindua rasmi mashindano ya mchezo wa riadha ya Wilaya kumi za Unguja na Pemba leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja (kushoto) Naibu wa Waziri wa Habari,Utalii ,Utamaduni na Michezo Bi Hindi Hamad Khamis.

HERI YA MWAKA MPYA TANZANIA NA SOUTH AFRICA TOKA KWA MAMA BISHANGA NA MUMEWE NA WAJUKUU

$
0
0
Wapendwa wanangu Sizelina, Kilian, Henrich/Kenny, Frolence na wajukuu Kilian /Mzungu na Maria Henrick, ndugu zangu na wa Tanzania wote na wa South Africa wote sisi Bwana na Bibi Marolen na wajukuu zetu Maria Kilian Kamota na Lailai Johnson tunawatakia furaha na amani ya mwaka mpya wa 2015 uwe wa baraka, mafanikio na upendo na amani kwenu wote. 

 Watoto Maria Kilian Kamota na Lailai Johnson wanasema next year, new year we will be there with dady Kilian and Henrick and aunt Size, and our young brother Mzungu and sister Maria. We love you all Tanzanians and South Africans and karibuuuuu to Canton Ohio!
Wajukuu wa Mama Bishanga Maria Kilian Kamota na Lailai Johnson
Christina Marolen - Mama Bishanga Bashaija
Bw. Marolen
Mama Bishanga

Mwl.Mwakasege kumwaga Zege Jumamosi

KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA - MH. SUMAYE:

$
0
0
1Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi yanayofanyika kuombea taifa la Tanzania yapokelewa na Mungu , Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha mungu kwa njia ya uimbaji 
7Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa akitunzwa na mashabiki wake wakati akiimba jukwaani. 10Tumaini Njole na wacheza shoo wake wakiwa angani wakati wakifanya vitu vyao jukwaani. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images