Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

CHAMA CHA TENNIS TANZANIA (TTA) KUANDAA TENA MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI

0
0
CHAMA CHA TENNIS TANZANIA (TTA) KUANDAA TENA MASHINDANO YA
AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN JUNIOR ZONAL CHAMPIONSHIPS) KWA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 16, JANUARI 11-19 2015.

Chama cha Tennis Tanzania (TTA) kimepewa nafasi nyingine tena ya kuandaa mashindano ya vijana wa ukanda wa Afrika Mashariki  (East Africa zonal championships) na yatafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 19 Januari 2015. Nchi shiriki kwa mwaka 2015 ni Burundi, Comoros, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Seychelles, Sudan na Tanzania. 

Tunategemea jumla ya washiriki wapatao 72 (pamoja na Tanzania). Tanzania itawakilishwa na vijana 22 ikiwa na team A na B.

TTA inajivunia kuanzishwa kwa mfumo wa renki unaotoa fursa kwa wachezaji kujikusanyia pointi kwenye orodha ya wachezaji wa tennis Tanzania. Hili limesaidia urahisi wa uchaguzi wa timu na kuepuka lawama za kupendelewa watu flani. Kila mchezaji wa chini ya umri 18 ana nafasi sawa ya kukusanya pointi kwa kushiriki mashindano yanayoandaliwa na TTA au watu binafsi yaliyoidhinishwa na chama. Timu ya Tanzania mwaka huu itawakilishwa na:


WANUSURIKA KUFA KUFUATIA AJALI YA GARI KIJIJI CHA MWIDU MKOANI MOROGORO

0
0
 
Camera ya GLOBU ya jamii ikiwa njiani kutoka Morogoro kuelekea jijini Dar,njia ilikutana ajali hii iliyotokea mapema jana kati ya gari ndogo aina ya NOAH ambayo namba zake za usajili hazikufahamika mara moja kufuatia kuharibika vibaya kutokana na ajali hiyo ya kugongwa kwa nyuma na basi la STAMILI kama lionekanavyo pichani lenye namba za usajili T43CJN lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea jijini Arusha,Katika gari ya NOAH hakukuwemo na abiria zaidi ya dereva,ambaye alitoka mzima kama aonekavyo pichani (aliyeshika kiuno).

Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mwidu mkoani Morogoro,Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa gari hiyo ndogo imetokana na basi la Stamili kuwa katika mwendo kasi na hatimae kuligonga gari hilo dogo kwa nyuma na kugonga Lori (halipo pichani).Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa vibaya.

KAMANDA WA POLISI, KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T),MOHAMMED R.MPINGA – DCP amewataka kuwajulisha watumiaji wote wa barabara kuwa  askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki  ambapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekamatwa  akivunja sheria za usalama barabarani. ''Niwaombe tu watumiaji wote  wa barabara watii sheria bila shuruti'' alisema kamanda Mpinga huku akisisitiza kauli mbiu ya usalama barabarani kwa mwaka huu kuwa  

˝Maamuzi yako barabarani ni hatima yetu-Fikiria kwanza”. . 
 Gari hiyo ndogo aina ya NOAH ikiondolewa barabarani
 Basi la STAMILI kama lionekanavyo pichani lenye namba za usajili T43CJN lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea jijini Arusha
 Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye basi la STAMILI wakiwa kando kando ya barabara wakiwa hawaamini kilichotokea.
Polisi wa Usalama barabarani wakifanya kazi yao nzuri kabisa ya kuweka utaratibu wa kupunguza usumbufu kwa magari mengine wakati wa kupishana,huku magari yaliyokuwa kwenye ajali yakiondolewa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mambo mengine ya kisheria za usalama barabarani

MAMBO YA VITOWEO VYA SIKUKUU BEI YAKE HUWA MOTO KIDOGO .!

0
0
Msimu wa Sikukuu mambo ya vitoweo kama Kuku,Mbuzi na Ng'ombe ndio wakati wake wa kununuliwa kwa wingi na pia kuuzwa kwa bei ya juu ama bei ghali.Pichani ni baadhi ya Wauza Kuku katika kijiji cha Mkambarani nje kidogo ya mji wa Morogoro wakisubiri wateja wao Kuku,ambapo kuku mmoja huuzwa kati ya shilingi 12,000/= mpaka 15,000/=

JK AKUTANA NA MSANII NASSIB ABDUL ‘DIAMOND’ IKULU, AWAPONGEZA YEYE NA IDRIS SULTAN KWA KUILETEA SIFA TANZANIA

0
0
unnamed-1
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond”  na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Desemba 23, 2014 . Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, Mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan hakuweza kufika Ikulu kuonana na Rais Kikwete siku hii. 

unnamed-4
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Nassib Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.
unnamed-3
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Nassib Abdul “Diamond”  juu ya ushindi wake wa  tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014. 
Kuona alivyopagawisha Washington DC majuzi BOFYA HAPA

MGENI RASMI WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AWASILI JIJINI MBEYA, TAYARI KWA KUONGOZA TAMASHA LA KRISMAS

0
0
1Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota kushoto na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Tayari kwa kuhudhuria Tamasha la Krismas ambalo linafanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mh, Sumaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji wengi kutoka hapa nchini na nchi jirani.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -MBEYA)2Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama wa pili kutoka kushoto, mwisho kushoto ni MC Mwakipesile wa jijini Mbeya 3Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama  wakimsikiliza MC Mwakipesile mara baada ya kuwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya.4Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama  wakifurahia jambo kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota na MC Mwakipesile.5MC. Mwakipesile kulia na John Melele mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo wakifurahia jambo kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe mkoani Mbeya.

Ibada ya Krismasi – Leo Alhamisi Disemba 25, 2014 Saa 3:30 Alasiri Usikose!

Maulid Kitenge amjulia hali Mdau Mwamad Maulanga alielazwa Moi baada ya kupata ajali

0
0
Mtangazaji wa Radio E FM 93.7,Maulid Kitenge akimjulia hali Mdau Mwamad Maulanga aliyelazwa Moi Muhimbili jijini Dar,baada ya kupata ajali katika eneo la Wami,mkoani Pwani wakati akiwa safarini kuelekea Mjini Moshi hivi karibuni.
Hii ndio gari aliyokuwa akiitumia Mdau Mwamad Mwaulanga.

NMB NA AZAM FC WAZINDUA RASMI KADI ZA UANACHAMA WA AFC

0
0
Benki ya NMB kwa kushirikiana na Azam FC jana wamezindua rasmi kadi za wanachama wa klabu hiyo amabazo zitawawezesha kupata huduma za kibenki za NMB zilizotapakaa nchi nzima.

Naibu Waziri wa Habari ,Vijana ,utamaduni na michezo Mhe. Juma Nkamia ndie alikuwa mgeni rasmi katika hafla hii. Pia aliwataka wanachama kuiunga mkono timu hiyo kwa matokeo yoyote.

“Mashabiki najua kazi zenu ni mbili kushangilia na kuzomea timu pinzani hivyo nawataka muwe na mapenzi ya dhati na timu yenu kwani naamini kuizomea timu ni ishara ya kwamba kuna tatizo mahali na kuishangilia timu ni kuashiria mambo yapo safi” aslisema.

Kwa upande wa NMB, Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Barnabas Waziri alisema kuwa NMB itaendelea kushirikiana na AZAM kukuza mpira hapa nchini na vile vile kuhakikisha kwamba mashabiki wa mpira wanapata nafasi ya kupata huduma za kibenki kwa rahisi na karibu zaidi.
Naibu Waziri wa Habari ,Vijana ,utamaduni na michezo Mhe. Juma Nkamia akiongea na wanachama wa AFC pamaoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kati hii ya uanachama.
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hii katika viwanja vya Azam jana.
Mmoja wa wanachama akionyesha kadi yake aliyokabidhiwa kama mwanachama wa Azam FC.

Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, afanya mahojiano na gazeti la Gulf Today kuhusu kuvutia uwekezaji na kukuza utalii nchini

0
0
Wiki iliyopita tarehe 17-18, Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii, uliandaa kongamano la uwekezaji katika sekta ya utalii, kwa nia ya kuvutia wawekezaji na  watalii ili kuongeza idadi kubwa ya watalii wanao kwenda kuitembelea Tanzania.

Ubalozi Mdogo umejiwekea utaratibu katika mpango wake wa mwaka, kuandaa kongamano za uwekezaji tatu kwa kila mwaka.

Ni imani kuwa mpango huu utasaidia kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na kuvutia idadi kubwa ya watalii kuitembelea Tanzania na vivutio vyake.

SERIKALI YALIFUNGIA SHINDANO LA MISS TANZANIA KWA MIAKA MIWILI

0
0

Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.

Baada ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa'' alisema Mngereza.

Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo. Chanzo cha Habari: Gazeti la Mtanzania, December 25.

Mh. Lowassa ahudhuria ibada ya Krismas Zanzibar leo

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar alipohudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo. Kulia ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Philip Mvungi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa na mjukuu wao, Angelica Freddy wakisoma Biblia katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar walipohudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa na mjukuu wao, Angelica Freddy katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar walipohudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa (kulia) akiwasalimia waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar walipohudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo.

DMK GLOBAL AND COMPANIES WISHING YOU ALL HAPPY HOLIDAYS WITH LOVE !

MSIMU WA EMBE USHAANZA KUMBE.!

Jamii yaaswa kumrudia Mungu - Viongozi wa Dini

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismas  watu wafuate njia ya mungu na sio njia ya Ibilisi ambayo inafundisha maovu.

Akizungumza leo baada ya Ibada ya Sikukuu ya Krismas ,Nzigilwa alisema watu wenye uwezo lazima wasaidie wasio na uwezo kwani Yesu alizaliwa katika pango la Bethelehem lakini watu wenye uwezo walimuacha kutokana na kuwa katika njia ya ibilisi.

Nzigilwa alisema suala la kuingiziwa fedha katika akaunti yake ambazo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow hawezi kulizungumzia kwa  sasa lakini siku zijazo atazungumzia suala hilo.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT),Dk. Alex Malasusa alisema kuwa watu lazima wawe na hofu ya mungu mambo yanayotokea sasa ya ufisadi yanaiweka nchi sehemu mbaya.

Malasusa aliyasema hayo katika Ibada ya Krismas iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front ,alisema nchi ipo katika mambo ambayo hayampendezi Mungu hivyo ni lazima tutoke huko ili wananchi waandokane na kusikia ufisadi kwani sio maendeleo ambayo yanatakiwa kwa sasa.

Mkuu wa Kanisa Kuu la  St.Albano ,Aidano Mbulinyingi alisema  jamii imeingia kufanya vitendo viovu kutokana na kuacha maandiko ya mungu hivyo tunahitaji kujenga msingi upya katika kutokomeza vitendo hivyo ambapo mungu hapendezi navyo.
 Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa akiongoza ibada ya Krismas katika Kanisa la Mt. Joseph,jijini Dar es salaam leo.
"Shkamoo....." Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa akipokea salam kutoka kwa mtoto,mara baada ya Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mt. Joseph,jijini Dar es salaam leo.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dk. Alex Malasusa akiwatakia heri ya Krismas sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front,jijini Dar es Salaam leo.

Simba, Kagera vita mpya Taifa jumamosi hii

0
0
Baada ya mapumziko ya karibu miezi miwili, vumbi la Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimka tena kuanzia jumamosi hii kwa pambano moja litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu za Simba na Kagera Sugar. Simba ambayo imelitumia vyema dirisha dogo la usajili kwa kufanya usajili wa baadhi ya nyota kuimarisha kikosi chao itaivaa Kagera ikitokea Zanzibar ilipokuwa imeweka kambi yao tangu Jumapili iliyopita.

Mabingwa hao wa zamani katika dirisha dogo imewaongeza kikosini, nyota kutoka Uganda, Dan Sserunkuma na mdogo wake, Simon Sserunkuma na beki Juuko Mursheed sambamba na beki wa pembeni kutoka Mtibwa Sugar, Hassan Kessy.

Timu hiyo ambayo katika mechi saba zilizopita iliambulia ushindi mmoja tu dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa ni baada ya miezi nane ya kucheza bila kushinda tangu msimu uliopita itakuwa na kazi nguvu mbele ya Kagera ambayo katika dirisha dogo la usajili haikusajili mchezaji yeyote na rekodi yake mbele ya Simba kila wanapokutana jijini Dar es Salaam inawabeba.

Kwa misimu miwili mfululizo timu hiyo imekuwa ikiiwekea nguvu Simba kwenye uwanja wa Taifa, jambo linalotarajiwa kutokea hata katika mchezo huo kutokana na maandalizi iliyofanya timu hiyo chini ya kocha kutoka Uganda Jackson Mayanja.

Katika msimu wa 2012-2013 timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2 na msimu wa mwaka jana matokeo yaliishia kwa sare ya 1-1 na kuibua vurugu kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba waliokuwa hawajafurahishwa na bao la kusawazisha la wapinzani wao.

Katika mechi hiyo, Simba wanashuka dimbani wakiwa nafasi ya saba katika msimo wa ligi wakiwa na pointi tisa mkononi tofuati na mahasimu wao Yanga ambao wanashika nafasi ya tano.

Mechi nyingine zitakazochezwa siku hiyo ni Mtibwa Sugar na Stand United kuonyeshana kazi katika uwanja wa Manungu, mjini Morogoro, Prisons-Mbeya itaikaribisha Coastal Union mjini Mbeya huku JKT Ruvu na Ruvu zitatoshana nguvu kwenye uwanja wa wa Chamazi huku Jumapili Mbeya City ikiikaribisha Ndanda 'Kucheree' uwanja wa Sokoine-Mbeya, Polisi Moro kuialika Mgambo JKT kwenye uwanja wa Jamhuri-Morogoro na wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga na Azam zitaonyeshana ubabe kwenye uwanja wa Taifa.

SUPER D AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA VIFAA

0
0
Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini,Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kushirikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wa kijamii wa whatsapp wamemkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumwi nchini

vifaa hivyo vilivyotolewa na super D kwa kushilikiana na mdau mkubwa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mkumba ambaye ndie muhamasishaji mkubwa katika mtandao huo kwa ajili ya kusaidia mabondia

baada ya kukabidhiwa msaada huo bondia Mussa Chitepete wa Songea aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kumpatia vifaa na kumpongeza kocha Super D kwa kuanzisha Kundi ambalo limekuwa muhimu sana kwake mpaka kupata vifaa hivyo.

nae mdau mkubwa wa masumbwi nchini Rajabu Mkamba amesema kwa kushirikiana na Super D wamefanya mambo mengi kwa ajili ya kuinua mchezo wa masumbwi nchini hivyo hawataishia hapo kwa kutoa sapoti kwa mabondia na wadau mbalimbali ili mchezo usonge mbele na wadhamini wajitokeze kusaidia ili vijana wawe na moyo wa kucheza mchezo wa masumbwi.
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini,Rajabu Mhamila 'Super D' (katikati) akimkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea vilivyotolewa nae kwa kushirikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao. wengine kutoka kulia ni Kiliani Shayo na Rajabu Mkamba ambaye ni mdau mkubwa wa kuhamasisha kusaidia mchezo wa masumbwi na kushoto ni rafiki wa Bondia huyo. Picha na SUPER D BOXING 

MEYA MANISPAA YA KINONDONI AKABIDHI MSAADA WA VYAKULA KWA VITUO VYA YATIMA

0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda amekabidhi msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima vilivyopo kwenye Manispaa yake, Dar es Salaam ambavyo ni Missionary of Charity cha Mburahati, Almadina Children Home na Mwandaliwa Orphanage Centre cha Mbweni na kuwataka watu wenye uwezo kujitokeza kuvisaidia vituo hivyo ikiwemo kuasili watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Missionary of Charity.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akisalimiana na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Missionary of Charity kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa kituo hicho katika hafla iliyofanyika kwenye Manispaa yake, Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akikabidhi msaada wa vyakula kwa mtoto Anitha Consantino wa kituo cha Missionary of Charity kwa niaba ya watoto wenzake wakati wa hafla iliyofanyika kwenye Manispaa yake, Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa Mlezi wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Almadina Children Home, Kurthum Yusuf kwa niaba ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati wa hafla iliyofanyika kwenye Manispaa hiyo, Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa mtoto Mwajabu Juma wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa Orphanae Centre kwa niaba ya watoto wenzake wakati wa hafla iliyofanyika kwenye Manispaa hiyo, Dar es Salaam.

FROLA MBASHA: DVD MPYA YA NIPE NGUVU YA KUSHIDA SASA IKO MADUKANI

0
0
Mungu amekuwa mwema kwangu tangia nilipomkubali kuwa mwokozi wangu na nguzo yangu. Nimeona Mungu akinishindia na magumu ninayopitia na niliyoyapitia katika maisha yangu. Nimeona Mungu huyu unayemwabudu kila siku akinivusha na kunitia moyo pale ninapoona akili yangukufikiri jinsi ya kutatua yale yaliyombele yangu. Mungu huyu ni waajabu kwangu, kaniwezesha katika uaandaji wa albamu hii mpya ya "NIPE NGUVU YA KUSHINDA". Nazidi kumshangaa Mungu huruma zake na fadhili zake kwangu - Flora Mbasha

kadhia ya kocha Marcio Maximo yaibua mambo mazito Yanga!

0
0
Timua timua ndani ya Yanga imeibua kadhia kubwa ambapo zaiodi  ya TSh  bilioni 3 ndani ya klabu hiyo zikidawia kuchotwa na kwamba uchunguzi unaendelea. 
Mwanasheria wa Yanga George Chacha ameiambaia
Globu ya Jamii kwamba  pamoja na kuwa ukaguzi bado unaendelea lakini huenda kuna mabilioni ya fedha yakawa yameyeyuka  ndani ya klabu hiyo. 
Alisema: "Kwa haraka haraka kuna fedha kiasi cha dola 2500 za tiketi ya mke wa aliyekuwa kocha msaidizi  Leonado Neiva, aliyetakiwa atumiwe ili aje, hizo hela zimetoka lakini hazikufanya kilichokusudiwa, na makocha ndio kama hivyo wametimuliwa. 
"Kuna fedha pia za Marcio Maximo kiasi cha dola 21 milioni (sawa na 35,700,000 za Tanzania) ambazo ni kodi ya nyumba na masuala mengine. Hizo hela pia Maximo hakupewa. Sasa wakati wanakatishiwa mikataba ndio ikagundulika -  fedha zimetoka lakini hazikufikia walengwa wala kufanya kilichotakiwa."alisema Chacha. 
"Yanga kama sio kufukuzwa makocha hao sidhani kama ingebainika mapema hivi kuwa kuna hela zimepigwa. Kuna watu wanapiga hela. Hela zinatolewa lakini hazifiki zinapostahili." 
Yanga iliwatimua Maximo na msaidizi wake Neiva mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni pamoja na kiungo mkabaji Mbrazil, Emerson Oliveira Neves Roque baada ya mchezo wa Nani Mtani Jembe ambapo Yanga ilinyukwa mabao 2-0.
"Kuna mambo mengi sana. Ukaguzi unaendelea. Utakapokamilika kila kitu tutaweka wazi na watakaogundulika wamehusika kwa namna moja au nyingine hatua zitachukuliwa,"alisema.
 Kuhusu kushikiliwa kwa mahojiano kwenye kituo cha Polisi Central kwa aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga Benno Njovu na mkuu wa idara ya fedha Rose Msamila, Chacha alisema "Ni kweli juzi Ijumaa saa 11 jioni ndio walichukuliwa kwa mahojiano na kuruhusiwa, kama ninavyokwambia uchunguzi bado unaendelea,"alisisitiza.
Juhudi kubwa za kuwasaka Njovu na Rose lakini hawakupatikana baada ya simu zao za kiganjani kutokuwa hewani.

Simba SC , Kagera Sugar vita mpya uwanja wa Taifa leo

0
0
Kagera Sugar FC
Simba FC
Na Sultani Kipingo
Baada ya mapumziko ya karibu miezi miwili, vumbi la Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza kutimka tena kuanzia leo kwa pambano moja litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa kuzikutanisha Simba SC na Kagera Sugar FC. 
Simba ambayo imelitumia vyema dirisha dogo la usajili kwa kufanya usajili wa baadhi ya nyota kuimarisha kikosi chao itaivaa Kagera ikitokea Zanzibar ilipokuwa imeweka kambi yao tangu Jumapili iliyopita. 
Mabingwa hao wa zamani katika dirisha dogo imewaongeza kikosini, nyota kutoka Uganda, Dan Sserunkuma na mdogo wake, Simon Sserunkuma na beki Juuko Mursheed sambamba na beki wa pembeni kutoka Mtibwa Sugar, Hassan Kessy. 
Timu hiyo ambayo katika mechi saba zilizopita iliambulia ushindi mmoja tu dhidi ya Ruvu Shooting ikiwa ni baada ya miezi nane ya kucheza bila kushinda tangu msimu uliopita itakuwa na kazi nguvu mbele ya Kagera ambayo katika dirisha dogo la usajili haikusajili mchezaji yeyote na rekodi yake mbele ya Simba kila wanapokutana jijini Dar es Salaam inawabeba. 
Kwa misimu miwili mfululizo timu hiyo imekuwa ikiiwekea ngumu Simba kwenye uwanja wa Taifa, jambo linalotarajiwa kutokea hata katika mchezo huo kutokana na maandalizi iliyofanya timu hiyo chini ya kocha kutoka Uganda Jackson Mayanja. 
Katika msimu wa 2012-2013 timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2 na msimu wa mwaka jana matokeo yaliishia kwa sare ya 1-1 na kuibua vurugu kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba waliokuwa hawajafurahishwa na bao la kusawazisha la wapinzani wao. 
Katika mechi ya leo,  Simba wanashuka dimbani wakiwa katika nafasi ya saba katika msimo wa ligi wakiwa na pointi tisa mkononi tofuati na mahasimu wao Yanga ambao wanashika nafasi ya tano. Mechi nyingine zitakazochezwa kesho ni Mtibwa Sugar na Stand United ambao wataoneshana kazi katika uwanja wa Manungu, mjini Morogoro, Prisons-Mbeya itaikaribisha Coastal Union mjini Mbeya huku JKT Ruvu na Ruvu zitatoshana nguvu kwenye uwanja wa wa Chamazi.
Jumapili Mbeya City itaikaribisha Ndanda 'Kucheree' uwanja wa Sokoine-Mbeya, Polisi Moro kuialika Mgambo JKT kwenye uwanja wa Jamhuri-Morogoro na wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga na Azam zitaonyeshana ubabe kwenye uwanja wa Taifa.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images