Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 684 | 685 | (Page 686) | 687 | 688 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na. Mwandishi Wetu

  Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza itakusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini mikoa ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na Dodoma.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 24 Desemba, 2014 na Katibu wa Tume hiyo, Bw.Frederick Manyanda, Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni na taarifa kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe 21 Januari,2015 katika maeneo mbalimbali ya kanda ya Kaskazini na Kati Nchini.

  Katika kutekeleza jukumu hilo, Bw. Manyanda ameeleza kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4 Januari 2015 mpaka tarehe 8 Januari 2015 na itakuwa Mkoa wa Singida tarehe 9 Januari,2015 mpaka tarehe 10 Januari,2015.

  Aidha Tume itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11 Januari, 2015 mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile, Wakili Manyanda ameeleza kuwa Tume itakusanya maoni Mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 13 Januari, 2015 mpaka tarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha tarehe 16 Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015.

  Mpaka sasa Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza imefanikiwa kukusanya taarifa na kupokea malamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza katika mikoa kumi na tano (15) ya Tanzania Bara ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro.

  Pamoja na mikutano hiyo, Bw. Manyanda ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi na watanzania wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa njia ya barua, simu na barua pepe ambapo ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa maeneo husika wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa namba za simu za Tigo: 0714 826826; Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel: 0773 826826.


  0 0

  Kwa niaba ya jopo zima la blogu ya Lyamba Lya Mfipa inayopatikana kwa anuani ya www.jodanyp.blogspot.com,  mhariri mkuu wa LYAMBA Lya Mfipa Bw.Joachim Nyambo anawatakia heri ya Krismasi na Mwaka mpya 2015.Tunatambua mchango wadau wetu na tunawaahidi kuongeza ubora wa huduma zetu za uhabarishaji.

  J.D.Nyambo.
  Mhariri mkuu Lyamba Lya Mfipa

  0 0

  KESHO ni siku ya Siku kuu, pasi na shaka hakuna mtu ambaye halijui hilo.

  Siku kuu ya Krisimasi na mwaka mpya ni siku kuu ambazo hufuatana na kwa desturi ya ushirikiano tulio nao hapa nchini siku hizi hatubagui hatuchagui kila mtu hufurahi pamoja na mwenzake.

  Furaha hii ni pale wana jamii walio na mirengo tofauti ya kiimani wanapojumuika pamoja na kufurahia, waumini wa dini ya Kikristo walio wengi kesho wanasherehekea kuzaliwa kwa Masia Yesu Kristo.

  Lakini kidoogo tujikumbushe kuzaliwa kwa Yesu Kiristo kulikuaje; Maandiko matakatifu kutoka katika Kitabu cha Biblia Matayo 1:18-21 kunaelezea wazi namna Yesu Kristo alivyo zaliwa.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Simba na mjumbe wa Bodi ya Ligi Kuu, Wakili Damas Ndumbaro (pichani) amesema hatma yake ya kujihusisha na masuala ya soka itajulikana kwenye mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 
   Mkutano huo umepangwa kufanyika mapema mwezi Machi mwakani ambapo ajenda ya mkutano huo ni Kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kusoma nakuthibitisha ajenda, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama, kupitisha taarifa za utekelezaji wa Kamati ya Utendaji, kupitisha taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2015.
   Mkutnao huo utakuwa ni wa kwanza kufanyika tangu rais Jamal Malinzi aingie madarakani ambapo awali ulitakiwa ufanyike mapema mwaka huu lakini haukufanyika huku habari ambazo Mwananchi ilizipata zinasema kuwa ukata unaokabili Shirikisho hilo ndio ulisababisha kutofanyika kwa mkutano mkuu, huku kukiwa na hofu ya uongozi uliopo kuondolewa madarakani kutokana na baadhi ya wajumbe kujipanga kupiga kura za kutokuwa na imani za Rais wa TFF kutokana na makundi yaliyopo ndani ya shirikisho hilo. 
   Dk. Ndumbaro alisema kuwa atatumia fursa hiyo ya mkutano mkuu kujua hatma yake baada ya TFF kuikalia rufaa yake zaidi ya miezi miwili baada ya kufungiwa kwa miaka saba kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi baada ya kuzitetea klabu zisikatwe asilimia tano ya mapato ya wadhamini na TFF. 
  "Mimi nimenyamaza tu, wala sitaki kuongea nao chochote, wasubiri mkutano mkuu mwezi wa tatu, mbivu na mbichi zitajulikana."alisema Ndumbaro Miezi michache iliyopita TFF ilikuwa inashinikiza klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na fedha za wadhamini, kwa kuwa klabu zimekuwa zikipokea udhamini wa Sh73 milioni kutoka Vodacom na Sh110 milioni kutoka Azam TV ambazo asilimia tano yake ni Sh9.15 milioni na kwa klabu 14 za ligi hiyo, TFF ingepata Sh128 milioni iwapo klabu zingeridhia. 
  Hata hivyo, Ndumbaro alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya nidhamu chini ya Profesa Mgongo Fimbo, na wajumbe wake Hamidu Mbwezeleni ambaye ni Makamu . Wengine ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze. 
  TFF imekuwa ikikaririwa mara kwa mara ikisema kuwa tayari ilishawasilisha suala la Ndumbaro kwenye kamati hiyo ya rufaa ya nidhamu lakini kamati hiyo ndio imekuwa ikichelewesha kwa kuikalia rufaa hiyo kwa vile haijapanga muda wa kukutana. Hata hivyo Makamu mwenyektii wa Kamati hiyo ya Rufaa Hammidu Mbwezeleni aliwahi kuimbia Mwananchi kuwa suala hilo bado halijafikishwa kwenye kamati yao.

  0 0


  Kwa habari za kila siku Soma gazeti la Jambo Leo kupitia  www.jamboleo.co.tz 
  Hapa utajipatia habari mbalimbali ambazo zimetokea nyumbani Tanzania na matukio mengine duniani,gazeti la Jambo Leo linatolewa na kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, inayochapisha Jarida la Jambo Brand Tanzania, gazeti la michezo la kila wiki, Staa Spoti na gazeti la matangazo la Dar Metro linalotoka kila baada ya wiki mbili.

  0 0

  Wanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' na Mzee Yusuf (kushoto) wakipozi baada ya kufanya mahojiano na wanahabari leo.
  Wanamuziki hao wakionyesha mbwebwe zao mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
  Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akihojiwa na wanahabari leo katika ofisi za Global Publishers Ltd tayari kwa Tamasha la Wafalme kesho, Dar Live.
  Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akihojiwa na mwanahabari wa Channel Ten, Freddy Mwanjala.
  Mzee Yusuf naye akihojiwa na Freddy Mwanjala wa Channel Ten.
  Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd na Dar Live, Abdallah Mrisho (kulia) akielezea kwa wanahabari jinsi Dar Live walivyojipanga kwa ajili ya kuwapa burudani safi mashabiki hapo kesho.
  Diamond akifurahia jambo na Mzee Yusuf aliyekuwa 'busy' na simu yake baada ya mahojiano.

  WASANII mahiri nchini Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' na Mzee Yusuf wamewaahidi mashabiki wa burudani hususani wa Jiji la Dar es Salaam kutokosa kesho katika Ukumbi wa Dar Live kushuhudia shoo ya kibabe inayotambulika kama Tamasha la Wafalme.
  Wakiongea na wanahabari katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar, wakali hao wamesema wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya shoo hiyo itakayoacha historia katika pande za Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
  Naye Meneja wa Dar Live, Abdallah Mrisho amewataka mashabiki wa burudani kuhudhuria kwa wingi kesho katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live maana kila kitu kiko safi kuanzia ulinzi na huduma zote muhimu.
  Shoo hiyo ya aina yake itaanza asubuhi kwa burudani za watoto ambapo kundi la sarakasi la Masai Worriors litahakikisha linatoa burudani ya nguvu kwa watoto wote kwa kuwapa staili mbalimbali za sarakasi na mazingaombwe.
  Pia watoto wataburudika na michezo kibao kama vile kuogelea, kubembea, kuteleza huku kila mmoja atakayehudhuria kurudi na zawadi kemkem nyumbani kwao.
  Kiingilio cha Tamasha la Wafalme kitakuwa shilingi 10,000 kawaida wakati kwa VIP kiingilio kikiwa shilingi 20,000.
  WOTE MNAKARIBISHWA!

  0 0

  NANI zaidi kati ya wakongwe na mahasimu wakubwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra (Sikinde) itajulikana leo wakati miamba hao wa muziki wa dansi watapambana kwenye ukumbi wa TCC Club Chang’ombe. 
  Mashabiki wa bendi hizo wanatarajia kumiminika kwa wingi kushuhudia mtanange huo ambayo pia itatumika kusherekea Sikukuu ya Krismasi. 
  Pambano hilo linatarajia kuanzia mchana, linafanyika siku chache tu baada ya mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga kwa mchezo wa soka, hivyo bendi hizo nazo kuamua kuweka Nani Mtane Jembe yao kwa upande wa muziki wa dansi. 
  Mratibu wa pambano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni mpambano huo ambao umeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi. 
  Mratibu huyo amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2014. 
  Kapinga alisema waamuzi katika pambano hilo watakuwa ni wanamuziki wa zamani ambao hawajawahi kupigia bendi hizo ili kuzuia upendeleo wowote. 
  Mmoja wa wanamuziki wa Sikinde Ngoma ya Ukae Hassan Rehani Bitchuka amesema kuwa wamejiandaa kuachia makombora makali ambayo yatawasambararisha kabisa Msondo Ngoma na wasirudie tena kupambana nao. 
  Hata hivyo, mwanamiziki mkongwe na bendi ya Msondo Shaaban Dede amesema kuwa siku zote Sikinde ni watoto wao, kwani imetoka ubavuni mwao, hivyo hawaoni sababu ya kushindwa kuibuka wababe kwenye pambano hilo. Kabla ya mtifuano huo bendi ya kongwe nyingine, Vijana Jazz Wana ‘Saga Rhumba’ itatumbuiza. 
  Bendi hiyo itakuwa chini ya binti wa aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo Hemed Maneti, Komweta Maneti ambaye ataimba nyimbo zote zilizokuwa zikiimbwa na baba yake. Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka huu wa 2014. 
  Mratibu Kapinga alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa malalamiko ya kuhujumiwa. 
  “Tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto kwa ajili ya kusherehekea Krisimasi,” alisema Kapinga. Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi liamba. Wadhamini wengine wa shindano hilo ni pamoja ni Fredito Entertainmernt na Saluti5.

  0 0

   Na Anitha Jonas – Maelezo, Kagera
   Kikundi cha vijana cha Ngara Youth Foundation chenye wanachama wapatao kumi na moja waliomaliza elimu ya juu wamenufaika baada ya kupata mkopo wa Milioni tano kupitia mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuanzisha miradi miwili ikiwemo mradi wa kuuza mbao na mradi wa kuosha magari. 
  Hayo yalisemwa jana na Katibu wa kikundi hicho Bw. Jason Athanas alipotembelewa na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutathimini miradi inayoendeshwa na vikundi baada ya kupatiwa mkopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na changamoto ya ajira iliyopo nchini. 
  Kikundi hicho kimeishukuru Serikali kwa kuwapatia mkopo uliopelekea kuongeza kipato kwa kila mwanachama hivyo kuboresha hali ya maisha baada ya kukosa ajira na kuwafanya kuwa wabunifu katika jamii. 
  “Tuliamua kuanzisha kikundi hiki baada ya kumaliza chuo na kutafuta ajira kwa muda mrefu hivyo tuliamuamu kuungana kuanzisha kikundi chetu ambapo tulibuni mradi tulioona unafaa na kuomba mkopo, kwa sasa tuna miradi miwili ambayo ni mradi wa kuuza mbao na wakuosha magari (Car Wash)”,alisema Bw. Athanas. 
  Naye Mkurugenzi Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Habari, Vjana, Utamaduni na Michezo Bibi.Verdiana Mushi, aliwapongeza vijana hao kwa juhudi kubwa wanazozifanya na kutoa wito kwa vijana wengine kuiga mfano wa vijana hao kwa kuanzisha vikundi vyao na kuomba mkopo katika mfuko wa maendeleo ya vijana unaosimamiwa na Wizara. 
  Aidha Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliakim Mtawa aliwashauri vijana wa Ngara Youth Foundation kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu huku wakizingati matumizi mazuri ya mapato yanayotokana na miradi yao pamoja na kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kukua kiuchumi na kukuza miradi ya kikundi.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Ufutiliaji na Tathimini  kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.Verdiana Mushi akikagua mradi wa kikundi cha vijana kutoka Ngara alipowatembelea kwa ajili ya kutathmini maendeleo ya mfuko wa maendeleo wa vijana. Kulia ni Mwenyekiti  wa kikundi cha vijana cha Hekima Group Ngara  Bw.George  Kessy
  Katibu wa Ngara Saccoss Bw.Joackim  Jordan (wapili kushoto)   akiwaonyesha Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipowatembelea hivi karibuni baadhi ya tofali aina ya "vibrated blocks" zinazotengenezwa kwa udongo na simenti ambazo vikundi kumi vya vijana vilipata mafunzo ya kutengeneza matofali hayo kama sehemu ya  miradi wanayofanya. Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Hekima Group Ngara  Bw.George  Kessy.

  Picha na Anitha Jonas - Maelezo

  0 0
 • 12/24/14--13:18: KUMBUKUMBU
 • Marehemu WILLIAM JOSEPH MINJA
  Leo ni miezi mitano na siku nne toka uiage Dunia hii ya tabu na mateso. Ntakukumbu mimi Mama Minja, Mama, Father na wanao Minja na Marco, Glory, Father na Enjoy. Upunzike kwa amani na Maraika wa Mbingu wakurunde. Raha ya milele upewe hee bwana....

  0 0


  0 0

  Bendi ya Muziki wa dansi Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibu,
  yenye makao nchini Ujerumani ,inawatakia wadau wote popote
  pale MERRY X-MASS,msherehekee kwa Amani na Upendo.

  0 0
 • 12/24/14--13:39: SHIMOZZZ
 • Mkazi wa jijini Dar akikatisha kando ya shimo la chemba lililopo katika barabara ya Umoja wa Mataifa,Upanda jijini Dar es salaam.Mifuniko mingi ya chemba hizi imekuwa ikipotea siku hadi siku na haifahamiki ni kwanini imekuwa ikipotea kwa kasi kubwa namna hiyo.!!

  0 0


  Na Yusuph Kileo
  Swala la kukuza uelewa wa matumizi mtandao salama maarufu kama “Cybersecurity Awareness programs” imekua iki himizwa sana kwani uhalifu mtandao unaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa sana pale watumiaji watakapo pata ufahamu wa kina wa matumizi salama wa mitandao. 

   Swala hili limekua liki imizwa sana na mataifa mbali mbali ili kuhakiki matumizi salama ya mitandao yanakuwepo na hatimae kupunguza wimbi kubwa la uhalifu mtandao unao endelea kukua hivi sasa. 
  Katika kuonyesha umuhimu wa swala hili Mwezi Wa Kumi umekua ukitumika kama mwezi maalum wa kukuza uelewa wa matumizi salama katika mataifa mengi. Kujua zaidi katika Hili Fatilia Taarifa inayoweza kusomeka "HAPA" 
   Kwa kutambua umuhimu Huo Chuo cha Teknolojia cha Dar-es-salaam (DIT) kiliandaa semina maalum ambapo wanafunzi wa vyuo mbali mbali waliweza kualikwa kuhudhuria semina hiyo ambayo ilikua na lengo la kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao.


  0 0

  NA CHALILA KIBUDA WA 
  GLOBU  YA JAMII, DAR

  SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo na Elimu ya Juu Nchini wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa maamzi kwa wale ambao walihusika katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow na kwa kutengua uteuzi wake kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi , Profesa Anna Tibaijuka, kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema  pamoja na kusimamishwa kazi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliackim Maswi.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,jijini Dar es Salaam, Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo na Elimu ya Juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ngubiagai, alisema maamuzi magumu ya Rais Jakaya Kikwete ni jambo la busara kwani Watanzania walikuwa wakisubiri kwa hamu maamuzi yake katika sakata la Tegeta Escrow.
  Ngubiagai alisema nchi inajengwa na viongozi walio bora kuchukua maamzi pale ambapo linatokea jambo, kuweza kuchukua hatua kwa wale ambao wamekwenda tofauti ambayo ndio demokrasia imara kwa wananchi.
  Aidha alisema katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alipokutana na Wazee wa Jiji la Dar es Salaam Desemba 18, mwaka huu a kuwa hakuna sababu ya kutaifisha mali za muwekezaji kutokana na mfumo uliopo sasa ni ushirikiano wa Sekta Binafsi (PPP).
  Wananfunzi  hao waliwataka Watanzania kuwa na imani na Rais Kikwete kutokana na utendaji wake unaoonekana katika maamzi mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kuweza kuondokana na umasikini ambayo ndio ilani ya CCM.
  Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu nchini wa Chama cha Mapindizi (CCM), Ndugu Christopher Ngubiagai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya maamzi aliyochukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sakata la Tegeta Escrow. Wengine ni Katibu wa Mkoa Dar es Salaam wa Shrikisho hilo David Zenda (Kulia), Mwenyekiti wa UWT Chuo Kikuu Huria Tawi la Ilala Evelyne Chack (kushoto).

  0 0

  Taswira za kuwasilisha Hati za Utambulisho za Mhe. Balozi S Marmo kwa Baba Mtakatifu Francis, mjini Vatican-Roma, Italia. Mhe. aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francis katika makao yake ya Vatican, Roma. Katika sherehe hizo kulikuwepo pia na Mabalozi wengine 12, watatu kutoka Afrika, nao ni Mali, Rwanda na Togo. Anakuwa Balozi wa Tanzania Holy See mwenye makazi yake Berlin, Ujerumani.
   Mhe. Balozi S Marmo kwa Baba Mtakatifu Francis, mjini Vatican-Roma, Italia.
  Mhe Marmo na Mke wake Nuruana Sulle wakiwa na Baba Mtakatifu Francis
  Mhe Marmo na mke wake Nuruana Sulle Marmo na Maofisa wa Ubalozi wakipata picha ya kumbukumbu na Baba Mtakatifu Francis
  Mhe. Balozi S Marmo na  Baba Mtakatifu Francis, mjini Vatican-Roma, Italia.
  Mhe Marmo na Mke wake Nuruana Sulle Marmo na Maofisa wa Ubalozi wakiondoka Vatican baada ya hafla hiyo

  0 0

  Mwezi huu wa Disemba 2014,EFM redio ilianza kuwashukuru wasikilizaji wake kwa kuanzisha “Kapu la sikukuu project”. Madhumuni ya project hii ni kuwashukuru wasikilizaji wa redio ya 93.7 EFM kwa upendo walio uonyesha tangu kufunguliwa kwa redio hiyo mpaka sasa.

  Meneja uhusiano ambae pia ni mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Joto La Asubuhi,Kanky Mwaigomole alisema kuwa makapu hayo ya sikukuu yalikua yamejaa hasa vitu vya nyumbani.

  “Tumehakikisha ya kwamba kapu hili litakalo muendea mshindi na familia yake,iwe ni furaha tosha kwani kapu mmoja limewekwa nyama,kuku,mafuta ya kupikia,mchele,unga wa ngano na wa sembe,nyanya,vitunguu na kadhalika”, alisema Mwaigomole.

   Kanky Mwaigomole alisema kuwa utaratibu wa kushinda kapu hilo wala halikuwa na masharti magumu.

  “Tulitumia mziki mfupi bila maneno wa "merry christmas ya jingle bells" na msikilizaji alitakiwa kusikiliza redio yetu mda wote,endapo pale angesikia mwimbo huo wa jingle bells,anaandika ni mda gani umepigwa na ni watangazaji gani waliupiga”,alisema.

  Kanky aliendelea kusema kwamba kwa yule ambae alipatia jibu ndio alipigiwa simu siku ya leo na kuelekezwa kufwata kapu lake la sikukuu.

  Washindi 30 walifanyikiwa kuitwa katika ofisi za EFM na kukabidhiwa makapu yao rasmi siku ya tarehe 24 mwezi wa Disemba 2014.
  Meneja Uhusiano wa EFM,Kanky Mwaigomole,akimsaidia mmoja wa washindi wa Kapu la sikukuu,kuingiza kwenye usafiri.

  Mtangazaji wa kipindi cha gurudumu,Swebe,akimsaidia mmoja wa washindi wa kapu la sikukukuu bwana Darisudi wa Bunju.


  0 0


  0 0
 • 12/24/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Juma Nature Ft Inspector Haroun - Mzee wa busara

  0 0

   Wasanii wa Hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Faridi Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Stamina wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la wazi la Tuo8January,hapo jana katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.

  Tuo8January ni kampeni maalum iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi  wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.

  Kama vile haitoshi kampeni hiyo inatumika kuwahamasisha vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi kuchukua hatua sasa za kufanya hivyo,pia kupata vijana wen,vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu na kuwa vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha mambo ya msingi yanajadiliwa na wagombea na yanapewa kipaumbele. 

  Katika tamasha hilo Fid Q aliwahamasisha vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye tamasha hilo,kuwa imefika wakati wa vijana kujitokeza kushiriki mambo mbalimbali ya kimsingi kwa manufaa ya nchi yao na si kukaa chini na kuanza kulalama,wakati kwenye mambo ya maamuzi wakishirikishwa hawataki kujitokeza,hivyo ni wakati wao wa kuamka na kuchagua kiongozi kijana wa kisasa na si kiongozi wa kisiasa.
   Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.
   Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.

  Kampeni hiyo ilizinduliwa jijini Dar hivi karibuni na kufanyika tamasha la kwanza mkoani Njombe na sasa Mkoani Morogoro.Baadhi ya Wasanii mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa vijana wameonesha kuiunga mkono kampeni hiyo,akiwemo Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto,G-nako,Fid Q,Shilole,Yamoto Band,Stamina na wengineo.

   Baadhi ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana katika viwanja vya Sabasaba,mjini Morogoro.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

older | 1 | .... | 684 | 685 | (Page 686) | 687 | 688 | .... | 3286 | newer