Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Qaswida


Tuzo za Bodi Bora Katika Sekta ya Kibenki na Bima kufanyika mwezi ujao

$
0
0
 Mratibu wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, Bi Neema Gerald (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo pamoja na wawakilishi kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Matthew Kasonta (wa pili kushoto), na Bw. Kassim Malela (kushoto).
Bw. Matthew Kasonta (katikati), mwakilishi kutoka Capital Plus International (CPI) ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja kati ya wadhamini wa tuzo, Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald (wa pili kulia) na mwakilishi kutoka Capital Plus International (CPI) Bw. Kassim Malela (kushoto).  

TUZO za Bodi yenye Uongozi Bora ijulikanayo kama Best Board Leadership Award (BBLA), ambazo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wagurugenzi katika sekta ya kibenki na bima, zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi ujao. BBLA iliyopangwa kufanyika mwezi Januari tarehe 30 na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini, inaandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa BBLA Bi. Neema Gerald alisema tuzo hizo zinatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam.

Wadhamini wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Capital Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media, wakati wadhamini wengine wakiaswa kujitokeza zaidi kuunga mkono tuzo hizo.

"Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakuwazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.

Bi. Neema alisema kuwa utamaduni unaojulikana ni kuwa ni Maafisa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi Wakuu pekee ndiyo wanaothaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au jamii nzima kwa ujumla. "Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema. Alibainisha kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.

Tathmini hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya Wakurugenzi katika suala la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kuiongoza dira ya taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa hatua madhubuti na  utendaji wake.

Alitaja maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.

Aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka nchini wakati ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa na kujitokeza kwa makampuni mengi ya bima na masoko zaidi kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.

"Kwa mabadiliko haya wakati huu, hasa katika sekta ya fedha ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na mabenki zimekuwa zikifungua biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema, na kuongeza:

"Hili litafanikiwa tu endapo kampuni hiyo ya bima au benki itaendelea kufanya kazi kwa mafanikio. Kwa maana hiyo, bodi ya wakurugenzi itakuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha kampuni hiyo haifi, "alisema.

Introducing HOT BOY REMIX ( SWAHILI VERSION) by Samatwizzy

KUJIAJIRI NI FURSA PEKEE YA MAENDELEO

$
0
0
Beatrice Lyimo -Maelezo

Serikali imewashauri wahitimu kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira kutoka serikalini kwani inatambua ukosefu wa ajira nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar ea Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya  Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Willium Lukuvi alipokuwa akifungua kongamano la mafunzo kwa wajasiliamali wadogo wadogo.

Amesema  kuwa vijana wanatakiwa kuweka mkazo katika suala la ujasiriamali na kujihusisha na mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ili kuwa na fursa mbalimbali kiuchumi.

“Mtazamo chanya, kujitambua, kuwa wabunifu na kusema inawezekana vinachangia kuzidisha maendeleo binafsi hivyo kila kijana afikirie kuwa anaweza”  aliongeza  Waziri Lukuvi.
Mbali na hayo Waziri Lukuvi alisema kuwa vijana hawana mitaji ya kujiendeleza  lakini taasisi za kifedha zinauwezo wa kuwakopesha iwapo watakua na vitambulisho vya Taifa na anwani za makazi hivyo kupelekea vijana kujiajiri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wajiri nchini Bw. Almasi Maige amewaasa wahitimu kuwa na mawazo chanya na kufikiria zaidi kuhusu kujiajiri na si kusubiri kuajiriwa.
“Hakuna ujasiriamali rahisi, inatakiwa kujitoa haswa kwa watu ama vijana wenye nguvu kama ninyi” aliongeza Maige.

Hivyo kuwashauri vijana kuwa wabunifu na kuanzisha shughuli zitakazosaidia kuongeza kipato na si kutegemea kukopi kutoka sehemu nyingine.

Kongamano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Gilgal nchini yenye  kauli mbiu isemayo “wajasiriamali wadogo fursa zilizowazi” lenye lengo la kubadili fikra kwa vijana walio vyuoni kutumia fursa zilizopo.

Mdau Salum Mpenda alamba nondozz yake katika Chuo Kikuu cha South Wales,nchini Uingereza

$
0
0
 Mdau Salum Mpenda akiwa kapozz kwa picha mara baada ya kulamba Nondozz yake ya Mastars of International Law katika Chuo Kikuu cha South Wales,nchini Uingereza.
 Mdau Salum Mpenda (kati) akiwa na Marcina Charles (shoto) na Mariam Ibrahim wakiwa ni wenye furaha tele kwa mufanikiwa kulamza nondozz zao za Mastars of International Law katika Chuo Kikuu cha South Wales,nchini Uingereza.
Furaha ya Nondozz: Mdau Salum Mpenda akiwa kwenye picha ya pamoja na Wazazi wake Dkt. Mpenda na Mama Pili Mpenda pamoja na rafiki yake Bi. Marcina Charles nje ya chuo hicho mara baada ya kulamba nondozz yake ya Mastars of International Law katika Chuo Kikuu cha South Wales,nchini Uingereza.

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAZALISHA ZAIDI

$
0
0
Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bw. Ashwin Rana akiwakaribisha wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo nchini. Anayesalimiana naye ni Prof. Longinus Rutasitara (Naibu Katibu Mtendaji Uchumi Jumla). Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua mitambo ya kuzalishia sukari katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni.

Jokate asaini mkataba wa thamani ya Sh8.5 bilioni na kampuni ya Kichina

$
0
0
Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006,  mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano hayo yalisainiwa leo kwenye hotel ya  Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.
 
Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.
 
Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.
 
 “Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.
 
Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania. 

“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.
Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na Tanzania.
 
 “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.
 Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
 Jokate na Guoxun wakibadilishana mikataba baada ya kusaini
 Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo
  Wageni mbalimbali waalikwa wakishughudia hafla hiyo
Meya wa Manispaa ya Ilala akiteta jambo na Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mariam Kisangi katika hafla hiyo. 

SHULE YA MSINGI MISUFINI YAFIKISHA MIAKA 4O,YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA,MBUNGE AZIZ ABOOD AICHANGIA MILIONI 4

$
0
0
 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea kwenye Sherehe za Mazimisho ya Miaka 4o Tangu kuanzishwa Kwa Shule ya Msingi Misufini Iliyopo Manispaa ya Morogoro.Katika Maadhimisho Hayo Mbunge wa Jimbo Hilo alifanya Aliongoza Harambee Nas Jumla ya Shilingi Millioni 5.8 Zilichangwa Ambapo Yeye Alichangia Jumla ya Shilingi Milioni 4.5
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikagua Mazingira Mbalimbali ya Shule ya Msingi Misufini. kwenye Sherehe za Mazimisho ya Miaka 4o Tangu kuanzishwa Kwa Shule ya Msingi Misufini Iliyopo Manispaa ya Morogoro.Katika Maadhimisho Hayo Mbunge wa Jimbo Hilo alifanya Ukaguzi na Kuikuta Shule Hiyo Ikiwa Katika Hali Mbaya Vyumba vya Madarasa ni Chakavu,Havina Milango Wala Madirisha Licha Ya shulie Hiyo Kuafulisha wanafunzi kwa Kiwango Kikukbwa Ndani ya Wilaya ya Morogoro Mjini.
Uchakavu wa Madarasa ya Shule ya Msingi Misufini iliyotimiza Miaka 4O Tangu Kuanzishwa kwake  Ikiwa Katika Hali mbaya sana ya Uchakavu ya Miuondo Mbinu ya Shule Hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Misufini Wakiwa katika Gwaride Maalum la Kumpokea Mh Mbunge ambaye alikuwa Mgeni Rasmi Kwenye Maadhimisho ya Miaka 4o ya Shule hiyo.

Dkt. Bilal kuzindua majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Tanzania Jumatatu

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania) itakayofanyika Jumatatu, tarehe 22 Disemba, 2014 jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo itafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi – saa 6:00 mchana katika eneo lililopo nyuma ya Jengo la Mawasiliano (Mawasiliano Towers), barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam yalipojengwa majengo hayo. Aidha, majengo haya yapo karibu kabisa na kituo kipya cha daladala cha Ubungo.

Majengo yatakayozinduliwa ni Mahakama ya Mafunzo (Teaching Court); Vyumba vya Madarasa (Lecture Theatres); Maktaba (Library); Jengo la Utawala (Administration Block); Mgahawa (Cafeteria); na Nyumba za Watumishi (Staff Quarters).

Pamoja na Makamu wa Rais, viongozi wengine watakaohudhuria ni Mawaziri, Majaji, Makatibu Wakuu, Mawakili, Wabunge, Wahadhiri na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria.

Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilianzishwa na Sheria ya Bunge (Sura 425) mwaka 2007 kufuatia jitihada na mapendekezo ya muda ya muda mrefu ya Tume na Kamati mbalimbali zilizofanya utafiti katika sekta ya sheria nchini na kuona umuhimu wa kuwa na chuo cha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ili kuongeza ujuzi na stadi baada ya kupata mafunzo ya nadharia katika vyuo vikuu.

Ujenzi huo wa majengo ya kudumu ya Taasisi umeigharibu Serikali zaidi ya Tshs 16.1 bilioni na ulianza mwezi Oktoba, 2010 na kukamilika mwezi Juni, 2013. Ujenzi ulifanywa na Kampuni ya BECG (Beijing Engineering Construction Group) kutoka China na ulisimamiwa na kampuni ya Co- Architecture yenye makao makuu yake hapa nchini. Kampuni hizi ndizo zilizoshinda zabuni za kazi zao.

Wanahabari kutoka vyombo vyote mnakaribishwa katika hafla hiyo.

Imetolewa na:
Wizara ya Katiba na Sheria
Dar es Salaam
Ijumaa, Disemba 19, 2014

BALOZI KAMALA AKAGUA HOTELI YA NYOTA TANO PATAKAPO FANYIKA KONGAMANO LA BIASHARA MWAKA 2015

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Afrika Rise ya Ubeligiji baada ya kukagua Hoteli ya Nyota tano ya Chateau Du Lac patakapo fanyika Kongamano la Biashara na Uwekezaji mwezi Aprili, 2015. Makampuni 500 kutoka Luxembourg, Ufaransa, Canada, Switzerland, Dubai, Ubeligiji, Tanzania, Morocco, DRC na Algeria yanatarajiwa kushiriki. Tanzania imekaribishwa kushiriki katika Kongamano hilo na itapewa fursa ya kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania. Kongamano hilo litafanyika jijini Genval - Ubelgiji.

SERIKALI YAZINDUA RASMI USAMBAZAJI TAKWIMU ZA PATO LA TAIFA, PATO LA MWANACHI LAONGEZEKA

$
0
0
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam.

CHADEMA yakutana na waandishi wa habari kuzungumzia maazimio ya kikao maalum cha kamati kuu ya chama hicho

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao maalum cha kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana wakati wa kujadili taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Bunge na Uchaguzi, John Mrema na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Bara, John Mnyika.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) - Bara, John Mnyika akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao maalum cha kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana wakati wa kujadili taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao jijini Dar es Salaam leo. 

AISHA MADINDA AZIKWA LEO KIBADA,KIGAMBONI

$
0
0
WAKURUGENZI wa bendi hasimu za dansi Tanzania, African Stars, Asha Baraka na Extra Bongo, Ali Choki, leo wameongoza mamia ya waombolezaji kumzika aliyekuwa mnenguaji wa zamani wa bendi hizo, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.

Mazishi ya Aisha Madinda yamefanyika leo kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe, Kigamboni jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kufanyika jana kutokana na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha ghafla cha mnenguaji huyo.

Baada ya uchunguzi huo kufanyika na ripoti kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi na familia, mazishi hayo yakafanyika leo jioni yakihudhuriwa na Asha Baraka na Choki, pamoja na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Salim Omari Mwinyi.

Akizungumza katika mazishi hayo, Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment inayoimiliki Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, alimuelezea Aisha kuwa ni sawa na mwanaye kutokana na muda mwingi aliotumia akiwa Twanga.

Baraka aliongeza kuwa licha ya kutokuwa na Aisha katika siku za karibuni, bado Twanga Pepeta inatambua na kuthamini mchango wa mkali huyo wa jukwaa na kwamba pengo lake halitasahaulika kirahisi ndani ya bendi hiyo kongwe.

Kwa upande wake Choki alisema daima atakumbuka uwajibikaji, usikivu na upendo wa Aisha akiwa na Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ na kwamba kwake yeye marehemu ni sawa na dada yake, huku akimtaja kama mtumishi mwema.

“Alikuwa na Extra Bongo kwa muda mfupi, lakini aina yake ya utumishi utabaki katika kumbukumbu zetu daima. Huu ni mwaka wa taabu kwangu, kwani siku ya arobaini ya marehemu mke wangu, alifariki pia mzee wangu Shem Karenga,” alisikitika Choki.

Choki alienda mbali zaidi kwa kulalama kuwa, siku moja baada ya kumzika Shem Karenga, ndio siku aliyofariki Aisha Madinda, hivyo kuendeleza mfululizo wa majonzi kwake na wadau wa tasnia nzima ya muziki wa dansi nchini.

Kwa upande wake, mtoto wa dada wa marehemu, Sheikh Mohamed Mussa, ambaye aliongoza mazishi upande wa familia, aliwashukuru Watanzania kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha mazishi hayo, huku akiwataka kuuendelea kumuombea.
 Mwili wa Aisha Madinda ukitolewa kwenye gari la kubebea maiti mara baada ya kuwasili nyumbani kwao,Kigamboni.
  Mwili wa Aisha Madinda ukiwasili nyumbani kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya mazishi yaliyofanyika  katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jijini Dar es salaam jioni hii.
 Mwili wa Aisha Madinda ukiswaliwa kabla ya maziko huko Kigamboni jijini Dar.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Hyundai Forklift Best Design Award

$
0
0
Hyundai Forklift truck received "2014 Good Design Product Award". HYUNDAI Sales Manager, Mr. Alen Nkya proudly shows the Forklift truck when announcing receiving "Best Design Product Award 2014" in Korea as previously received "Red Dot Design Award 2012" in Germany during press conference held in Dar es Salaam yesterday. Hyundai Heavy Industries has to date received "Good Design Awards" on twelve of its products ranging from Excavator and Wheel Loader to Compactor and Skid Steer Loader

Hans van Der Pluijm na Charles Mkwassa watajwa kuwa makocha wapya wa Yanga

$
0
0
Klabu ya Yanga imemtaja,  Dr Jonas Tiboroha (45) kuwa katibu mkuu wa klabu na kuwathibitisha rasmi Hans van Der Pluijm na Charles Mkwassa kuwa makocha wapya sambamba na kuitaka sekretarieti iliyomaliza muda wake kukabidhi ofisi haraka.

Pluijm na Mkwassa wanachukua nafasi ya makocha wa Yanga, Marcio Maximo na Leonardo Neiva waliotupiwa virago huku Tiboraha akichukua mikoba ya Beno Njovu aliyemaliza muda wake.

Awali mkufunzi wa Fifa, Henry Tandau alipigiwa chapuo kuchukua cheo cha Ukatibu baada ya Njovu licha ya kushindwa kufikia muafaka na viongozi na Tandau kukataa kuajiliwa na Yanga.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo , Jerry Muro alisema Tiboraha ataiongoza sekretarietri mpya ya klabu hiyo.

"Uteuzi wa sekretarieti hiyo umependekezwa kwa kuzingatia vigezo na itaongozwa na Tiboraha ambaye atafanya kazi na mkuu wa Idara ya habari ambaye ni mimi, Omar Kaya yeye anakuwa Mkuu wa Idara ya Masoko,Frank Chacha anakuwa mkuu wa Idara ya Sheria na Baraka Deusdedit anakuwa Mkuu wa Idara ya Fedha," alisema Murro.

Akizungumzia suala la makocha Pluijm na Mkwassa, Murro alisema makocha hao wataanza kazi mara moja na kusisitiza kuwa tayari klabu hiyo imeachana na Maximo na Neiva.


"Maximo na Neiva sio makocha tena wa Yanga," alisema Murro ambaye hakuwa tayari kuweka wazi kama klabu hiyo imemalizana na makocha hao baada ya kuvunja nao mkataba zaidi ya kueleza benchi la ufundi litaongozwa na Pluijm akisaidiana na Mkwassa.

"Mwenyekiti wa Yanga pia anapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Maximo pamoja na Neiva kwa ushirikiano wao katika kufundisha timu ya Yanga kwa muda wa miezi sita iliyopita, na anawatakia kila kheri katika safari yao na Mungu akipenda wataendelea kushirikiana nasi katika siku za mbeleni.

"Pamoja na hayo, Mwenyekiti anapenda kuwashukuru wafanyakazi wa Sekretariati iliyomaliza muda wake, japo bado wapo kwenye mchakato wa kukabidhi ofisi zao, na angependa kuwasihi wamalize haraka makabidhiano yao," alisema Murro katika taarifa hiyo na kuongeza.

"Niwafahamishe wana Yanga kuwa uongozi umeamua kuongeza vijana zaidi kwenye uongozi, ili muda wa kustaafu madarakani ukifika Klabu ya Yanga itakuwa na warithi bora watakaoendeleza mazuri waliokuta.

TUKIO LA UJAMBAZI,MLANDEGE ZANZIBAR LEO

$
0
0
MKUU wa Polisi Wilaya ya Mjini, Ali Makame (wa pili kushoto) akiangalia gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, muda mfupi baada ya kufika eneo la tukio katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar.
ASKARI Polisi wakiwa wameizunguka gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni tano, tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar leo. Mmiliki wa gari hiyo aliegesha gari yake na kuingia msikitini kwa kusali sala ya Ijumaa katika msikiti jirani na maengesho ya gari katika eneo la mlandege. (Picha na Haroub Hussein).

RT HON KIDEGA ELECTED SPEAKER OF EALA: Undertakes to reconstruct EALA and take it to the next level

$
0
0
 New EALA Speaker Rt. Hon Dan Kidega
 Rt. Hon Kidega is congratulated by Hon Chris Opoka Okumu
Rt. Hon Kidega been sworn in by the Deputy Clerk Obatre Lumumba
The East African Legislative Assembly sitting in Arusha, Tanzania, has this afternoon elected Rt Hon Dan Fred Kidega as Speaker. Rt. Hon Kidega becomes the fourth Speaker of EALA, replacing Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa who was removed from Office on Wednesday this week.

Rt. Hon Kidega was elected unopposed after his main contender, Hon Chris Opoka- Okumu stepped down.   The two were the only ones validly nominated. 


At exactly 3.56 pm, the Clerk to the Assembly declared Rt. Hon Dan Kidega duly elected and proceeded to administer the oath of the Office of the Speaker.



In his acceptance speech, the new Speaker pledged to uphold the dignity of the House at all times and to apply the Rules without fear or favour.
"You will note as a House, we have a big and challenging task ahead of us to legislate and represent a Community whose activities and Membership is expanding fast," Rt. Hon Kidega said.  
 

" I have no doubt we shall deliver.  I will pick up from where my predecessors left and continue to promote the good ideals of our mandate of widening and deepening the integration process.  In doing so, I will give the majority their way but respect and protect the rights of the minorities at all times" Rt. Hon Kidega added.
 Rt Hon Kidega, 41, is serving as a Member of Parliament of East African Legislation Assembly for a second stint having been a Member in the 2nd EALA (2007-2012). He has prior, been a Member of Parliament in Uganda for a period of five (5) years (2001-2006) representing the youth. Rt. Hon Kidega has been active in NRM politics and was a member of President Yoweri Kaguta Museveni's national campaign taskforce in 2001, and the Party's National Executive Committee (NEC) member.
 Rt. Hon Kidega has also worked as a Private Secretary to the Vice President of the Republic of Uganda. Prior to joining legislative work, he was a youth leader at different levels; including being Chairman of the National Youth Council (NYC), National Representative to the Commonwealth Youth Forum (African Region). Rt. Hon Kidega is remembered in his days in school as a strong student activist.
 The Speaker is an entrepreneur and has been engaged in the struggle against HIV/AIDS and Women Empowerment in Uganda. Rt. Hon Kidega obtained his first degree in Business Administration from Uganda Christian University.  He holds a Master of Science Degree in International Trade Policy and Trade law. He is also a Diploma holder in Bio-Chemistry.

Katibu Mkuu Kiongozi atembelea ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA)

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue (wanne Kulia) akitoa neno la shukrani kwa watu wa Kenya baada ya  mazungumzo kwa njia ya mtandao , alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni  Mkuu wa Chuo cha IFM  Pro. Daniel Mjema, wa kwanza kushoto ni  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bwana George Yembesi na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo.

 Wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLa) wakifuatilia mazungunzo  kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) akifurahia jambo baada ya kupata maelekezo namna mitambo ya mawasiliano inavyofanya kazi kutoka kwa Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto,na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA ,Bwana Charles Senkondo(katikati) leo jijini Dar es Salaam.
Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA.

CHANGE OF VENUE of the 5th Annual East African Health and Scientific Conference

$
0
0
The EAC Secretariat would like to inform you that the venue for the 5th Annual East African Health and Scientific Conference has been changed from Commonwealth Speke Resort Hotel, Munyonyo, Kampala, Uganda to SERENA  HOTEL, KAMPALA, REPUBLIC OF UGANDA.

The EAC Secretariat is requesting you to put a notice of the change of venue at the front page of your National Ministries of Health website, and you are also requested to help in circulating widely the information about the change of the venue and conference at large to other stakeholders in your country. 
 
The link of the conference is unchanged. The conference details are:
  • Conference name: 5th Annual East African Health and Scientific Conference & International Health Exhibition and Trade Fair
  • Dates: 25 - 27 March 2015 
  • Venue: Serena Hotel, Kampala, Uganda.
  • Conference Website: http://eahsc.eac.int

BONGO MOVIE WALIA NA MAHARAMIA, FILAMU KUSHUSHWA BEI

$
0
0
Wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie wakiwa katika mkutano na wanahabari jijini Dar es salaam kulalamika jinsi maharamia wanavyowaibia kazi zao na pia soko la filamu kujaa kazi za nje zinazouzwa bei chee 

Wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie wakiwa katika mkutano na wanahabari jijini Dar es salaam 

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images