Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 677 | 678 | (Page 679) | 680 | 681 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua Nishati ya Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja leo (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija (kutoka kulia) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiingiza namba katika fungua pazia kuzindua Nishati ya Umeme Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Unguja leo (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija (kutoka kulia) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib na Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZEC) Hassan Ali Mbarouk.


  0 0

   Ujumbe wa wataalamu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) unatembelea Bandari ya Singapore (PSA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ha kuongeza ufanisi na kuimarisha Ulinzi na usalama wa Bandari kwa kutumia Mitambo ya kisasa na Teknolojia ya Habari na mawasiliano (ICT) , Ujumbe wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa , Mkurugenzi wa ICT wa TPA, pia wamo wahandisi wa majengo, wataalamu wa Ulinzi na wataalamu wa  TEHAMA. Ziara hii ni muendelezo wa ushirikiano wa PSA na TPA ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi kati ya TPA na PSA wakati wa ziara ya Mhe. Rais Kikwete alipotembelea nchini Singapore mwaka jana.
    Ujumbe wa TPA ulipotembelea eneo la Bandari ya Singapore linalotumika kwa ajili ya Meli za abiria, starehe na kuvinjari ( waterfront development ). 
   Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye chakula Cha pamoja na Ujumbe PSA
   Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa PSA makao makuu ya PSA
   Mkuu wa msafara Ndg. Magesa akisalimiana na Makamu wa Rais Msaidizi wa PSA anayeshugulikia ICT Ndg. Andrew Gill wakati akiwakaribisha makao makuu wa PSA
  Mkuu wa msafira wa TPA Ndg. Magesa akipokea zawadi toka Makamu wa Rais Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore ( PSA) anayeshugulikia biashara Ndg. Vignes kulia

  0 0

  Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi, Nobert Kahyoza, akifungua semina ya TPDC kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Semina hiyo ililenga kutoa taarifa muhimu zinazo hitajika kwa wadau katika sekta ya mafuta na gesi kutoka sehemu mbali mbali zikiwemo wizara, taasisi na waandishi wa habari, semina hiyo iliyofanyika Bagamoyo.
   Wadau wa sekta ya mafuta na gesi walioshiriki semina wakifutilia kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika semina hiyo Bagamoyo.


  0 0

  Na Bakari Issa,Dar es Salaaam

  Wajasiriamali toka vikundi mbalimbali wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha matibabu wawapo katika shughuli zao za kawaida,leo katika ukumbi wa Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.

  Katika Mpango mpya uliozinduliwa na Mfuko huo ujulikanao kama Mpango wa Kikoa(MATUAL PLAN),Wajasiriamali watakaojiunga na mfuko huo na kuwa wanachama watalipia shilingi 76,800 kwa mwaka ili kupata matibabu kupitia mfuko huo.

  Akizungumza na wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali ambavyo vipo chini ya Muungano wa vikundi mbalimbali vya kuinua jamii(ASE),Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii kutoka Mfuko wa Bima ya Afya,Rehani Athumani amewataka wajasiliamali wanaofanya biashara ndogondogo wasione ngumu kujiunga na Mfuko huo wa Bima ya Afya na amewataka viongozi kuwa na ushirikiano wanapopata matatizo na changamoto katika kufanikisha suala hilo.

  “Wajasiriamali wa biashara ndogondogo nawashauru kujiunga na mfuko huu,na nawasihi viongozi wenzangu kuwa na ushirikiano tunapopatwa na matatizo pamoja na changamoto”,alisema Rehani.

  Kwa upande wake,Afisa Matekelezo na Uratibu(NHIF),Catherine Masingisa amesema kuwa mpango huo ni kwa wote,watoto na wakubwa kwa mjasiriamali kuchangia mfuko huo wa Bima ya Afya,hata hivyo amesema mpango huo utakuwa na matibabu sawa na ule mpango wa Watumishi wa Serikali.

  “Mpango huu wa Kikoa ni utaratibu wa kupata huduma ya afya kwa wajasiriamali wadogowadogo katika vikundi na wanachama watapata huduma ya matibabu kwa unafuu zaidi na kuondoa kabisa suala la unyanyasaji kwa wajasiriamali”,alisema Catherine.

  Naye,Mratibu Mkuu wa ASE,Bi.Sunayritha Mapunda amewataka wajasiriamali hao walioko katika muungano huo wa vikundi mbalimbali vya kuinua jamii kuonyesha mfano kwa wajasiriamali wengine walioko nchini kujiunga na Mfuko huo wa Taifa wa Bima ya Afya.
   Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Rehani Athumani akiongea na vikundi mbalimabli vya wajasiliamali kuhusu umuhimu wa mfuko wa Afya ya jamii pamoja na kuwahamasisha wajasiliamali hao kufungua bima ya afya kwa ajili ya matibabu.
  Mratibu wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii(TNCHF), Camillius Mathew Haule akitoa maelekezo juu ya ujazaji wa fomu za Mfuko wa Afya ya Jamii kwa wajasiliamali hao
  Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Catherine Masingisa akizungumza na wajasiliamali juu ya mfuko wa afya unavyofanya kazi hapa nchini.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  UNIGLOBE Skylink Travel & Tours Ltd based in Dar Es Salaam – Tanzania with branches in Arusha, Mwanza and Zanzibar has been named to the 2015 UNIGLOBE Chairman’s Circle for being among the top-performing TMCs in the UNIGLOBE system worldwide. 

  “Annually, we award UNIGLOBE Chairman's Circle membership to travel management companies who meet or exceed our highest performance and operating standards, based on established criteria," says UNIGLOBE Travel International president and chief operating officer Martin Charlwood. 
  “We are pleased to welcome Moustafa H. Khataw, owner of UNIGLOBE Skylink Travel & Tours Ltd to our 2015 Chairman’s Circle for delivering exceptional performance over the past year. 

  Chairman’s Circle members are invited to join UNIGLOBE founder and chairman, U. Gary Charlwood and Martin Charlwood in an annual meeting to discuss trends and issues in the travel industry which was also the topic of a session by ACTE Executive Director Greeley Koch. New technologies, service delivery tools and flexibility make UNIGLOBE the brand of choice for business and leisure travelers. 
  This year, senior executives from Delta, United and Amadeus participated and shared their views on today’s dynamic travel environment. Additionally, Brian Terwilliger, Film Producer/Director shared his passion and latest film adventure about the history of aviation scheduled to be released in 2015. 

  Khataw attended this year’s event at the Beverly Hills Hotel in Beverly Hills, California. 
  Khataw is upbeat on this nomination and stated that this is a clear manifestation of the upbeat thrust UNIGLOBE Skylink Travel & Tours Ltd has shown during the year 2014 being the only ISO 9001:2008 Certified Travel management Company in Tanzania.
  UNIGLOBE Travel International Limited Partnership is the leading international travel management system specializing in providing travel services to small to mid-size enterprise (SME) and leisure clients through its network of franchised and member agencies. 
  With global oversight, The UNIGLOBE organization presently comprises locations in more than 60 countries across the Americas, Europe, Asia/Pacific, Africa and the Middle East operating under a well-recognized brand, common system and services standards. 
  UNIGLOBE has its world headquarters in Vancouver, B.C., Canada with an annual system-wide sales volume of $5.0+ billion. UNIGLOBE Travel International Limited Partnership is a subsidiary of the Charlwood Pacific Group, which also owns Century 21 Canada Limited Partnership, Century 21 Asia/Pacific, Centum Financial Group Inc. and other interests in travel, finance and real estate. -30-

  0 0
  0 0

  Yatima wanaolelewa katika nyumba ya watoto katika hospitali ya Nkoaranga wamepewa misaada mbalimbali iliyotolewa na wafanyakazi wa Lake Duluti Serena Hotel, mkoa wa Arusha katika kusherekea siku kuu za Krismas na mwaka mpya ikiwa ni njia ya kuyakumbuka makundi maalumu katika jamii. 
   Meneja wa hoteli hiyo, Gerald Macharia amesema wameguswa na hali ya maisha ya watoto hao ambao wazazi wao walifariki dunia wakati wa kujifungua na wengine walitelekezwa baada ya kuzaliwa.
  Amesema kwa miaka iliyopita walikua na utaratibu wa kutumia gharama kubwa kupamba hoteli wakati wa Siku kuu za mwisho wa mwaka ila kwanzia mwaka jana waliamua kuwa watakua wanatoa misaada kwa jamii zenye mahitaji maalumu. 
   “Wafanyakazi na marafiki zetu tulitoa misaada katika Shule ya Msingi yenye mahitaji maalumu ya Patandi iliyopo wilaya ya Arumeru, tuliguswa sana na kuona tuna wajibu wa kushirikiana na wadau wengine kuifikia jamii kwa misaada mbalimbali”amesema Macharia 
   Nkoaranga Hospital Children’s Home ina jumla ya watoto zaidi ya 70 na ilianzishwa mwaka 1965 ikiwa na watoto wenye umri wa miezi 3 hadi miaka 8 huku wakipata elimu katika viwango tofauti.
   Wafanyakazi wa Lake Duluti Serena Hotel wakitoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao.
  Meneja wa Lake Duluti Serena Hotel Bw. Gerald Macharia(kulia)akitoa zawadi ya jiko la gesi kwa mlezi wa Nyumba hiyo Bi Damari Mbisse.

  0 0

  Kaimu Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Karatu, Wende Lyimo (wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya bodaboda kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya weka upewe, Mchungaji Christopher Kingo katika hafla iliyofanyika tawini hapo, Arusha hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wateja wa benki hiyo na mfanyakazi wa benki hiyo, Kalist Masika (kulia).

  0 0

    Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo cha mabadiliko ya tabianchi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CCCS),  Prof. Pius Yanda akifungua semina ya kikanda ya athari na changamoto zitokakanazo na mabadiliko ya tabianchi inayoshirikisha wajumbe kutoka maeneo kame inayofanyika mjini Singida. 
   Mhadhiri na mtafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Emma Liwenga akitoa mada kuhusu maenedelo ya mradi wa mazingira kwenye maeneo kame  unaonedeshwa na kituo cha mabadiliko ya tabianchi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
   Wadau wa mazingira wakifutilia mada zianazotolewa.
   Mtaalam wa mabadiliko ya tabianchi Bw. Edmund Mabhuye kutoka CCCS akitoa mada kuhusu tafiti zilizofanywa na viashiria vya mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa semina hiyo. Picha na Obeid Mwangasa

  0 0

   Ofisa Masoko wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF, Albert Kitunga, (kulia) akimsajili mwanachama mpya wakati wa maonesho ya elimu ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam, kushoto ni Ofisa mwenzake wa Mfuko huo, Jacob Ondara
  Wateja wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF wakijisajili sanjari na kupewa vitambulisho vya uanachama wa mfuko huo katika maonesho  hayo.

  0 0

   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi umoja wa vikundi vya wama katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha Usafirishaji tarehe 
   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akisoma maandishi baada ya kuzindua rasmi umoja wa vikundi vya wama katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha Usafirishaji tarehe 
    Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo huko Chuo Cha Usafirishaji. Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Happy Holidays from the
  United Nations Association of Tanzania

  Like
  Follow
  Circle
  www.una.or.tz

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya heshima ya Uzamivu PhD Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika Jamii, kitaifa na kimataifa pamoja na kufanikisha kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya pili  iliyofanyika leo  jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya PhD ya Sayansi Uhandisi na Hesabu Bw. James Philip kwenye Mahafali ya pili ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo jijini Arusha.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Mahafali ya 2 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyofanyika leo jijini Arusha.
   Sehemu ya wahitimu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela 
   Wahadhiri katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanmzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika maandamano na viongozi wa Taasisi hiyo pamoja na wahitimu, wakati wa Mahafali ya 2 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo  jijini Arusha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Shahada ya Uzamili na Uzamifu kwenye Mahafali ya 2 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyofanyika leo jijini Arusha. 
  Picha na OMR


  0 0  0 0


  "Ndugu Meneja wa Kanda, napenda kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF ambao unatekeleza mojawapo ya sera zake ya kuhakikisha sekta isiyo rasmi inafikiwa kama ilivyo kwa sekta nyingine za uchumi hapa nchini. Hii itaongeza pato la Taifa hivyo kuzidi kuboresha maendeleo ya Watanzania kwa ujumla na kupunguza umaskini. Napenda kuwaambia kuwa kwa kuandaa semina hii muhimu katika eneo ambalo mimi mwenyewe nalisimamia imenipa faraja sana kwa kuona jinsi Mfuko huu wa PPF unavyowajali sekta zote za uchumu wa nchi. Hongereni sana."
  Kwa mujibu wa Meneja wa Kanda ya Ziwa Ndugu Meshack Bandawe (pichani aliyesimama) alisifia Mahudhurio ya semina hiyo akisema kuwa yanadhihirisha kuwa kuna mwamko wa jamii ya watanzania kuhusiana na masuala ya hifadhi ya jamii unaendelea kukua na kuimarika. 
  Wanasemina wakichukuwa data muhimu. Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).


  Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.

  Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-


  ELIMU:-

  ·        Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)

  ·        PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)

  ·        MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)

  ·        BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994


  UZOEFU WA KAZI:-


  ·        Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA

  ·        2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu

  ·        2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  ·        1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)

  ·        1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.


  Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.


  Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.


              Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu.

  Dar es Salaam.


  18 Desemba, 2014


  0 0

  NA CHALILA KIBUDA WA GLOBU YA JAMII.

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka amesema kuwa hawezi kujiuzulu katika nafasi  ya uwaziri kutokana fedha ya Tegeta ESCROW. 
  Akizungumza  na Waandishi na Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency, Profesa Tibaijuka  alisema kuwa udalali wake wa  fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi katika shule  za Taasisi ya  Barbo Johansson  Girls Education Trust, na kwamba fedha aliyoipata ni  Bilioni  Tshs. 1.66 ambazo zilitoka katika kampuni ya James Rugemalira kama msaada kwa shule hiyo.
  Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James  Rugemalira  ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi. 
  "Nikijiuzulu hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani fedha nilizopata ni za shule na kwa ajili kukomboa elimu nchini  hasa kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za shule’’alisema.

  Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta  fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai hata Mwenyekiti wa Makampuni  ya IPP  Dkt Reginald Mengi alitoa sh.milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.

  Profesa Tibaijuka  alisema kuwa  wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi kufanya hivyo na kama angetaka fedha hiyo angeweza kufuata hata katika shule na kuchukua.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
   Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka.

  0 0

  Courtesy of NTV

  0 0


older | 1 | .... | 677 | 678 | (Page 679) | 680 | 681 | .... | 3272 | newer