Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110108 articles
Browse latest View live

Tanzania adopts the Arusha Declaration on Social Protection

$
0
0
Today Honorable Minister Saada Mkuya Salum (MP), Ministry of Finance, officiated the closing ceremony of the three-day International Conference on Social Protection at the International Conference Centre in Arusha.

Upon closing of the Conference, the Government of Tanzania adopted the Arusha Declaration on Social Protection which provides a strong foundation for advancing the agenda of social protection in Tanzania and in Africa, with a view to make growth and development a reality for all.

The three-day Conference was a historical event, as it was the first ever such international conference on social protection to take place in Tanzania. The Conference, which was organized by the Government of Tanzania through the Ministry of Finance, in collaboration with UNICEF, ILO, UNAIDS and the Economic Policy Research Institute (EPRI) based in South Africa – brought together more than 150 senior government officials, policy-makers, researchers and experts on social protection. Delegates had a unique opportunity to attend presentations from distinguished experts in the field of social protection from many countries, includingAfghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mozambique, South Africa, Uganda, Zambia and Zimbabwe.

Hon. Minister Salum said that the Conference has been very interactive and has explored and deliberated on all important pillars for building sustainable social protection systems in Africa and in Tanzania in particular.

“The final recommendations and Declaration which we have adopted, provide the required knowledge and basis for future work. I am pleased to say that this consensus is a decisive step in pursuance of the social protection agenda in Tanzania and hopefully will serve as an inspiration for the region as a whole. Additionally these recommendations will certainly inform our next growth and development plans and strategies of the various sectors like education, health and social welfare, nutrition, water and sanitation.”

During the Conference, many papers were presented and discussed in six plenary and parallel sessions. The discussions explored issues related to evolution and key trends of social protection; building comprehensive and integrated social protection systems; and designing effective social protection interventions and social protection sustainability and financing. One of the key messages from the discussions was on the importance of coordination, vertically across the central and local government and horizontally across social protection and social services agencies.

As pointed out by H.E. Seif Ali Iddi, Second Vice President during the opening ceremony of the Conference, Tanzania has its vision set high to graduate to a middle-income country by 2025 and the Government has adopted social protection as a key strategy for achieving Tanzania’s growth and development vision.

In order to achieve this VISION, the Government wants to ensure that its citizens, including the poorest and the weakest develop their capacities to realize their rights and make Tanzania stronger and a more equal society. Addressing the needs of children, especially their nutrition, health and education is critical to helping them grow into happy, productive adults and escape from the inter-generational poverty trap.

In conclusion, Hon. Minister Salum felt encouraged that the Conference was able to achieve its objectives.

“As Tanzania moves towards a mineral and gas-rich economy and aspires to move towards a middle-income country, this Conference has been timely in establishing that social protection stands as a key strategy for ensuring a fairer distribution of the nation’s wealth and contributing to measurable improvements in household economic and social development as well as reducing risks by building a peaceful and cohesive society,” She said.

NHIF YANYAKA TUZO TATU ZA UBUNIFU BARANI AFRIKA

$
0
0
1Bima ya Afyaaa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya mfuko huo wakati walipoonyesha tuzo ambazo mfuko huo ulitunukiwa nchini Morocco na Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni. kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakiwa katika mkutano huo uliozungumzia tuzo hizo.
Bima ya Afya
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili pamoja na wakurugenzi wa shirika hilo kulia Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakionyesha tuzo zilizokabidhiwa kwa mfuko huo kutoka Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni
....................................................................................................................
Kwa miaka mingi sasa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa mwanachama wa mashirikisho mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA), Shirikisho la Hifadhi ya Jamii la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), na Shirikisho la kimataifa la Uchumi wa Afya (IHEA). 
Mashirikisho haya husaidia katika kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali, ushauri wa kitaalamu, viwango vya huduma, miongozo ya kiutendaji pamoja na kutumika kama jukwaa kwa wanachama kujenga na kuhamasisha mifumo endelevu katika hifadhi ya jamii. Taasisi hizi za kimataifa vilevile huhusika katika kutoa tuzo kwa Taasisi ambazo zinafanya vizuri katika ubunifu katika maeneo mbalimbali.
Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) limekuwa na utaratibu wa kushindanisha mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye maswala ya ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo; kuboresha huduma, utawala bora, matumizi ya teknolojia, ukusanyaji wa michango na matekelezo, uwekezaji, kufikisha huduma kwa wananchi waliyo sehemu ngumu kufikika, uhamasishaji wa Afya na uepushaji wa hatari makazini, pamoja na utekelezaji wa tathmini za uhai wa mifuko. Mashindano haya yalianza tangu mwaka 2008 na hufanyika kila baada ya miaka mitatu.
Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi, Mfuko umekuwa ukishinda tuzo katika maeneo mbalimbali. Mwaka 2008 Mfuko ulishinda tuzo moja ya ubunifu katika kuboresha huduma na mawasiliano kwa wanachama kupitia siku ya wadau (Clients Days). Mwaka 2011 Mfuko ulishinda tuzo nne katika masuala yafuatayo; Uboreshaji wa kitita cha mafao yanayotolewa na Mfuko; Usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii: katika kupanua wigo na jitihada za kufikia lengo la afya kwa Watanzania wote; Utoaji wa mikopo ya vifaa tiba na Uboreshaji wa majengo inayotolewa na Mfuko; Ugatuzi wa shughuli za Mfuko kwa kufungua ofisi za mikoa kuwasogezea huduma wananchi: Usimamizi bunifu kuongeza ufanisi katika utendaji. Kwa mara nyingine Mfuko umeshinda tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika katika sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika tarehe 3 Disemba 2014 katika hoteli ya Sheraton mjini Casablanca, Morocco. Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma za matibabu za kibingwa maeneo magumu kufikika, kazi ambayo Mfuko umekuwa ukifanya kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini tangu mwaka 2012.
Tuzo nyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji pamoja na uwasilishaji wa madai ulioanzishwa kwa dhumuni la kupunguza malalamiko ya baadhi ya vituo vya Afya kuchelewa kulipwa madai yao. Kupitia mfumo huu, muda wa ulipaji wa madai hasa katika hospitali kubwa nchini umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Mfumo huu ulianza tangu Januari 2012. Tuzo ya tatu ni juu ya huduma za matibabu kwa wanachama wastaafu ambayo imeanza tangu mwaka 2011. Fao la wastaafu linalenga kuwapa wananchi ambao walikuwa wanachama wa Mfuko na wenza wao uwezo wa kutibiwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kustaafu ajira mpaka mwisho wa maisha
Mfuko utaendelea kufuata miongozo inayotolewa na mashirika ya kimataifa ili kutekeleza shughuli zake kiufanisi na kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wanachama wake. Mfuko vilevile unadhamiria kuendelea kuboresha shughuli zake ili uweze kukidhi viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la viwango la kimataifa (ISO) na hatimaye kuthibitishwa kwa kutimiza viwango hivyo katika kipindi kifupi kijacho. NHIF Mfuko pia unatarajia kwa kipindi kijacho kuweza kukidhi viwango vilivyowekwa na Shirikisho la kimataifa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (ISSA) na kupata ithibati ya kukidhi viwango vya kimataifa.

JIPATIE KITABU CHA TABIA 5 ZA WATU WALIOFANIKIWA

$
0
0
Kitabu kinauzwa shilingi 10,000/- tu na kwa hapa Dar es salaam kinapatikana Posta Mpya ndani ya DAR ES SALAAM BOOKSHOP au nikipigiwa simu namba 0653808032 kitawafikiwa wateja popote walipo, pia natafuta wasambazaji mikoani. 
 Hiki ni kitabu kinachomsaidia mtu kujitambua na kutambua vipaji alivyonayo ili aweze kuvitumia kuchagua maisha anayoyataka na baada ya hapo kimesheheni mbinu nyingi zitakazomwezesha mtu kuishi na kufanikiwa katika maamuzi aliyoyafanya. 
Kimeshawasaidia wengi waliokisoma. Mimi ni mtaalamu wa saikolojia, sosholojia na ujasiriamali, kazi yangu ni kufundisha na kushauri katika maeneo hayo yote napatikana hapa Dar es salaam, nina mtandao wa kiofisi unaitwa www.truemaisha.com.

Mtunzi wa kitabu hicho Bw. Erick Chrispin

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA ZIARA YA KIKAZI DUBAI

$
0
0
 Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akizungumza na Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini, Bi. Devotha Mdachi (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel PSSC ya Dubai, Bw, Ali Lootan wakizungumza katika Mkutano wa Kuitangaza Tanzania na kuvutia wawekezaji wa Dubai  uliofunguliwa na Waziri Mkuu mjini Dubai leo
 Waziri Mkuu Mhe.  Mizengo Pinda akiongozwa na Meneja Mkuu wa Shamba la kufuga ng'ombe wa maziwa la Al Rawabi Dairy la Dubai, Dr. Ahmed Al Mansour (kulia kwake) kukagua shamba hilo akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo leo. Kulia ni Balozi mdogo wa Tanzania Dubai, Mhe Omar Mjenga.
Waziri Mkuuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja mkuu wa shamba la kufuga ng'ombe wa maziwa la Al Rawabi Dairy  la Dubai, Dr. Ahmed Al Mansour (kulia) wakati alipotembelea shmaba hilo akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo leo Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MAONYESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA VIPAJI MPIRA WA MIGUU KWA VIJANA WALIOKO SHULENI NA VYUONI, TANZANIA DESEMBA 19 – 21 2014

$
0
0
Tunayo furaha kukujulisheni kuwa taasisi ya Boko Beach Veterans Sports Club (BBV) itaandaa maonyesho ya kimataifa ya vipaji vya mpira wa miguu kwa vijana wa mashuleni na vyuoni, kuanzia tarehe 19 had 21 kwenye uwanja wao wa kisasa ulioko maeneo ya Boko, Kinondoni , Dar es salaam.  

Maonyesho haya ni nafasi dhahiri kwa vijana wenye vipaji vya kusakata mpira wa miguu, wavulana kwa wasichana, kucheza soka nchini Marekani huku wakisoma katika vyuo vya nchini humo kwa kulipiwa gharama zote. Makocha wapatao watatu (3) kutoka katika chuo kikuu cha Alabama, Chuo kikuu cha Martin Methodist and chuo kikuu cha Lindsey Wilson wamesha thibitisha kushiriki na tunawategemea kufika tarehe 15 Desemba 2014.

 

Maonyesho haya yanatilia mkazo kwa usawa kipaji na mpira wa miguu pamoja na uwezo wa kielimu. 
Pia yanawapa vijana wa kitanzania nafasi ya kupata udhamini wa kusoma katika vyuo vikuu vya Marekani. Ni mpango wa ufadhili ambao unawaunganisha vijana wa kitanzania wenye ndoto ya kucheza mpira pamoja na kusoma na ulimwengu mzima. Boko Beach Veterans Sports Club (BBV)  tayari tumekwisha alike shule mbali mbali kuleta washiriki.

Mkakati wa BBV to ni kuonyesha kile ambacho kimekuwa kikifanywa nan chi nyinngine katika kuinua ujuzi wa kucheza mpira wa miguu kwa vijana wao, kwa kuhakikisha kuwa michezo na elimu vinaenda sambamba. Wakiwa na elimu, wachezaji wa mpira wa miguu wanaweze kutengeneza maisha yao baada ya kustaafu kucheza, kwa kuajiriwa, kuanzisha shughuli zao au kuwa makocha wazuri. 
Pamoja na kuwa na wachezaji wengi walio

wahi kuwika Tanzania, ni wacheche sana wameweza kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu kucheza, sababu kubwa ikiwa ukosefu wa elimu bora. 

BBV inakukaribisha sana kushiriki katika maonyesho haya ya kwanza nay a aina yake na yenye mweleleo wa kuleta faida kubwa binafsi kwa washiriki na kwa taifa kwa ujumla. BBV ina nia ya kuandaa maonyesho haya kila mwaka ikiwa ni mchango wake katika kampeini za TFF na serikali ya kuinua kiwango cha soka nchini. 

introducing "Limbwata" by Sam G

WASANII WAKONGWE WAPANIA KUFANYA KUFURU KATIKA UZINDUZI WA KAONE SANAA GROUP NDANI YA DAR LIVE

$
0
0
Mastaa waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyopania kufanya kweli kwenye uzinduzi wa kundi lao jipya la Kaone, Boxing Day ndani ya Dar Live.
Muhogo Mchungu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni msanii Thea. 
Wasanii hao wakongwe wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo na wanahabari. Mkutano huo umefanyika leo katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Dar.
Msanii Thea (kulia) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Msanii Kingwendu akitoa burudani wakati akiongea na mwanahabari wa TBC.

ZIKIWA zimesalia siku chache kuelekea ule Usiku wa Wasanii Wakongwe Desemba 26 ‘Boxing Day’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, mastaa kibao waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole watazindua rasmi kundi jipya linalojulikana kama Kaone.
Usiku huo utakaokuwa wa aina yake, utawakutanisha wale wakali wote kutoka Kaole kama vile Swebe, Davina, Koletha, Zawadi, Nyamayao, Kingwendu, Muhogo Mchungu, Kibakuli na wengine kibao ambao kwa mara ya kwanza watajulikana kama Kaone na kuzindua tamthiliya yao mpya ya Kipusa itakayoanza kuruka hewani Januari 4, 2015 ndani ya Runinga ya TV1.
Usiku huo pia utapambwa na wasanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha pamoja na Isabela Mpanda ‘Bela’ ambapo watatoa burudani mwanzo mwisho.
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Kundi la Masai Worriors litawapagawisha watoto kwa kuwapa chemsha bongo, mazingaombwe sambamba na kutoa zawadi kibao huku watoto wengine wakipata nafasi ya kubembea, kuteleza na kuogelea.

INTRODUCING NEW BOYS ON THE BLOCK - KAZI KWANZA


mhe amos makalla azindua mradi wa maji kijijini Endamaghan, Karatu, leo

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Endamaghan wilayani Karatu leo akiwa amezungukwa na wakaazi wa kijiji hicho ambao wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao wameuita ni mkombozi kwani utawaondolea kabisa shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akihutubia wakati wa kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Endamaghan wilayani Karatu leo akiwa amezungukwa na wakaazi wa kijiji hicho ambao wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao wameuita ni mkombozi kwani utawaondolea kabisa shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji
Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akizawadiwa mgolole baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Endamaghan wilayani Karatu leo akiwa amezungukwa na wakaazi wa kijiji hicho ambao wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao wameuita ni mkombozi kwani utawaondolea kabisa shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji

NAIBU MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI MAHAFALI TAASISI YA MANDELA

$
0
0
DSC_0499
Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack (kushoto) akijadiliana jambo ndani chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri na Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa mipango kitaifa, kitengo cha Sayansi UNESCO,Tanzania, Gabriela Lucas kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida.
DSC_0516
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues akimlaki Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili kuhudhuria mahafali ya pili ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha yanayofanyika kesho. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack na wa pili Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0517
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akimlaki kwa furaha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida (kushoto) aliyewasili jioni hii jijini Arusha na shirika la ndege la Ethiopia. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0518
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akisalimiana na Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
DSC_0524
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akiwa na mwenyeji wake Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues mara baada ya kuwasili wakielekea kwenye chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri.
DSC_0526

News alert: Obama announces historic overhaul of relations; Cuba releases American

Balozi marmo akabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa austria mjini Vienna

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Austria ambaye ana makazi mjini Berlin, Ujerumani Mhe. Philip S. Marmo mapema mwezi huu likabidhi Hati za Utambulisho (Letter of Credence) kwa Mhe. Dkt. Heinz Fischer, Rais wa Austria. Shughuli hizi zilifanyika katika ukumbi maarufu wa Maria Teresa uliopo katika kasri ya wafalme wa zamani wa "Austro-Hungarian Empire" mjini Vienna. Gwaride rasmi kwa ajili ya Balozi mpya iliendeshwa katika viwanja vya Hofburg.

mapacha kutoka Tanzania walioungana watenganishwa kwa mafanikio nchini India

$
0
0
Picture1-swahili
Hospitali ya Apollo iliyoko nchini India imefanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike wa Tanzania Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni  katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini humo. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini yaliyounganika.  Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa  utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11.  Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyokuwa vimeungana. Mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Picture2-swahili
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungo husika mahala pake baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”

BREAKING NEWZZZZ: EA LEGISLATIVE ASSEMBLY REMOVES SPEAKER RT HON DR ZZIWA FROM OFFICE

$
0
0
 Hon Frederic Ngenzebuhoro presents the report of the Committee on Legal, Rules and privileges to an attentive House this afternoon in Arusha
The East African Legislative Assembly  has this afternoon voted to remove Rt. Hon Dr. Margaret Nantongo Zziwa from office. This follows overwhelming support of the Motion for removal of the Speaker by 36 to 2 votes (signifying over two-thirds majority in excess of 30 votes) on the floor of the Assembly. Only one abstention was recorded.

Immediately, the Clerk of EALA moved to declare the vacancy and announced that in accordance with Article 7 of the Rules of Procedure, the names of candidates for the election of Speaker shall be obtained within 48 hours from today (Friday at 3.30 pm).

The sitting today was chaired by the Presiding Officer, Hon Chris Opoka Okumu who was elected to preside over the motion for removal of the Speaker on November 26th, 2014 at the sitting in Nairobi. Rt. Hon Zziwa was absent from the Plenary today.

Earlier on in the morning, the Assembly listened through and adopted the Committee on Legal Rules and Privileges on investigation of the complaints raised in the motion for the removal of the Speaker from Office.  The Committee has been receiving and assessing evidence submitted to it.

The Committee also lined up a number of witnesses among them being the Rt. Hon. Speaker of EALA, Members and staff of EALA, and any other witnesses who it deems are necessary for the discharge of their investigative mandate.

The report presented to the House by the Chair of the Legal, Rules and Privileges Committee, Hon Frederic Ngenzebuhoro, cites the inability of the Speaker to perform the functions of the office arising from misconduct in accordance with the provisions of the Treaty and the Rules of procedure.

The report notes that Rt. Hon Zziwa unilaterally made a decision to stop rotation sittings in contravention of the provisions of the Administration of the EALA Act, 2012.  The Speaker is also accused of wasting resources of the Community through poor time management, unnecessary delays postponement of meetings and laisser-faire attitude to Assembly provisions. 

“In August 2013 all members of the Assembly went to Mombasa, Kenya as programmed in the EALA Annual Legislative Calendar for 2013/2014 Financial Year. According to the evidence available the members of the Commission and Chairpersons of all the Standing Committees arrived one day before the workshop for a consultative meeting. The Speaker who was supposed to chair the meeting did not come as scheduled, nor did she delegate responsibility of chairing the meeting”, a section of the report reads in part.

According to the findings, the Speaker continued to be absent from duty station contrary to the terms and conditions and hence giving inadequate supervision to the work of the Assembly.   Other areas include undermining the authority of the Commission by changing the activities for 2013/2014 to suit personal interests and practicing favouritism by denying other Members equal opportunity.

The report also cites misconduct, the use abusive and derogatory language against Members and staff.

During debate today, Hon Saoli Ole Nkanae remarked that Rt. Hon Zziwa had constantly used unsavory language. “The Speaker created a monster out of this House, we have turned into gladiators. It needs to end today” Hon Ole Nkanae maintained. 
Hon Hafsa Mossi appealed to the Assembly to change the trend and take the right decision. “I have failed to see Leadership in the Speaker, I hope we make the right decision today”, she said.
Hon Dr. Odette Nyiramilimo said it was time for EALA to restore its lost glory.  “I hope we will elect a Member who will restore the dignity of this House”, Hon Dr. Nyiramilimo remarked.

Hon Abubakar Zein told the House to ensure it takes the right path to restore its dignity. “We need to make a decision to do our work with honor, dignity & integrity while putting petty differences aside for the sake of integration”, he remarked.

On his part, Hon Taslima Twaha was emphatic that the region was bigger than any individual. “Let whatever direction we take, lead us to success, and by the will of the Almighty God all through to that of the satisfaction of East Africans”, he stated.

Hon. Dora Byamukama remarked that the truth was key.  “In the next 2.5yrs (balance of the period left to serve the 3rdEALA), I stand committed to what whatever it takes for this House to regain its dignity, honor and glory”, she remarked. 
Hon Hafsa Mossi makes her contribution on the Motion this afternoon
Hon Nusura Tiperu also supported the Motion. “We love the outgoing Speaker, but we love East Africa more”, she said, adding that it had reached the time we make a decision for the people of the region.

Speaking on behalf of the Council of Ministers, the Chairperson, Hon Dr. Abdullah Saadala maintained that the Council had all along respected the rule of separation of powers and the democratic exercise of decision making of the House. 

“We shall continue to do so for the strengthening of the integration process”, he said. Other Members who rose up to speak were Hon Leonce Ndarubagiye and Hon Mukasa Mbidde who termed the process as fair.

The Motion, initially introduced in the Assembly by Hon Peter Mathuki in Arusha during the Fifth Meeting of the Second Session of the 3rd Assembly was cut-short when it was adjourned on April 1, 2014 sine die following two applications made at the East African Court of Justice (EACJ) halting the debate. 
On 3rd June this year, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa ruled on the Motion for her removal to have fallen short of the requirements of signatures of atleast four elected Members from each Partner State and thus collapsed. This followed the withdrawal of signatures of three Members from the United Republic of Tanzania. 
Rt. Hon Zziwa pegged her ruling on Rule 82(2) of Rules of Procedure that grants the Speaker of the Assembly, the final powers on the interpretation and the application of the same. However, prior to that, the Counsel to the Community, Hon Wilbert Kaahwa had maintained that the Motion was “alive”. 
 The third East African Legislative Assembly (EALA) elected Margaret Nantongo Zziwa its first female Speaker in June 2012 when she defeated Hon Dora Byamukama’s in the second round.

Hon Mukasa Mbidde casts his vote on the Motion.   36 members voted in favour of the Motion for the removal of the Speaker, 2 voted against while there was one abstention
-Under the provisions of the Rules, a motion seeking the removal of the Speaker from Office, is referred by the House, to the Committee on Legal, Rules and Privileges for investigation within a specific time frame. Upon conclusion of investigations, the Committee makes a report to the House with clear findings/observations and recommendations.  
-The Speaker against whom proceedings for removal from office have commenced has the right of appeal and recourse to justice through the relevant courts of law if in his/her opinion, there is/has been or appears to be a miscarriage of justice.
-EALA shall elect the Speaker in accordance with Rule 7 of the Rules of procedure.  Under the Rules, the election shall be by secret ballot.  At the same time, all candidates need to present their names  at least 48 hours before the time appointed for which the House is to meet to elect a Speaker.

WANASIASA WATAKIWA KUTOSHIRIKI KATIKA USHAWISHI WA UHARIBIFU WA MISITU NA MAZINGIRA NCHINI

$
0
0
Na Abdulaziz Ahmeid-Dodoma 
Wanasiasa wameombwa kutoa ushirikiano kwa taasisi na wadau mbalimbali wanaoshughulika na uhifadhi wa misitu na mazingira badala ya wao kuwa ni miongoni mwa watu ambao wanaoshiriki na kusababisha uharibifu wa mazingira unaondelea kwa kasi hapa nchini. 
Wito huo umetolewa leo mjini Dodoma na mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania(MJUMITA)Bi Rahima Njaidi Wakati wa ufunguzi wa warsha na mkutano mkuu wa 14,ambao umeshirikisha wanachama wajumuia hiyo na wadau mbalimbali wanaoshughulika na uhifadhi wa misitu na mazingira toka kanda sita Nchini. 
Bi Njaidi alibainisha kuwa ili kufaniwa katika mapambano na harakati za kuhifadhi misitu na mazingira ni wajibu kwa wanasiasa kushirikiana na taasisi mbalimbali zilizopo katika mapambano na harakati hizo zenye lengo la kuokoa misitu inayoharibiwa kwa kasi nakutishia ‘ kupitia mpango huo Wanajamii wamediriki kuwahoji viongozi wao katika mchakato mzima wa usimamizi endelevu wa rasilimali misitu ambapo suala la Mapato ya vijiji vya uhifadhi ni moja ya changamoto iliyoonekana katika warsha hii’ alibainisha Njaidi 
Akimalizia taarifa yake katika warsha hiyo Njaidi aliviomba vijiji kuachana na baadhi ya wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wana katika jamii na pia ni washiriki wakubwa uharibifu wa misitu na mazingira kwa kuwaruhusu wananchi wanaowaongoza kuishi na kufanya shughuli za kibinadamu zinazoharibu maliasili kwa lengo la kuwafurahisha wanaowaongoza au kwa maslahi binafsi Nae Bw Musa Mkoyage,
Diwani wa kata ya Likongowele wilayani Liwale aliitaka MJUMITA iwaelimishe wanajamii juu ya ugawanaji wa mapato kama vile ilivyoainishwa katika vijiji vingine ambavyo tayari vimeishaanza kupata faida za misitu huku mapato yote yakibaki kijijini na kuweza kuendeleza shughuli mbali mbali za maendeleo. 
Mkoyage pia alieleza kuwa katika kuokoa misitu inayoharibiwa kwa kasi na kutishia uwepo wake hapa nchini na kusababisha hofu ya nchi kugeuka jangwa Akifungua Warsha hiyo ya siku mbili,Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Bw Lefy Gembe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Bi Chiku Galawa Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kufanya tathmini ili kujua ni kwa kiasi gani taratibu na kanuni za uvunaji endelevu zinasimamiwa na kufanikiwa ili kila mwananchi ashiriki kulinda na kuhifadhi misitu na mazingira kwa manufaa ya jamii ‘Uvunaji endelevu ni suala la kisheria hivyo ni muhimu kwa wananchi kutekeleza taratibu na sheria zilizopo ili misitu iweze kuwa endelevu na Iwe yenye tija kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. 
Warsha hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa MJUMITA na kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Jumuiko la maliasili Tanzania(TNRF) ikiwa na lengo kuu la kutafuta mbinu za kupambana na uharibifu wa misitu na mazingira na kufanya usimamizi na uvunaji endelevu
 kutoka kulia ni mkurugenzi wa Mjumita Bi Rahima Njaidi;Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Mpingo Bw Gasper Makala;mkurugenzi wa Tfcg na mwanamtandao wakijadili jambo kuhusiana na uhifadhi wa misitu
Washiriki katika warsha
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Lephy Gembe akiongea kwemye warsha hiyo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mjumita,Bi Rahima Njaidi akitoa utangulizi wa warsha ya ya siku mbili ya wadau wa mtandao huo inayoendelea Mkoani Dodoma

Mkuu wa wilaya Dodoma(suti nyeusi)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Mjumita

Afisa wa polisi kenya aua wenzake 5 kwa kuwapiga risasi kisha kujiua

ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Mr II aka Sugu -  ft Dola Soul Sema Nao (1998)

Benki ya NBC yakabidhi bodaboda kwa mshindi wa Weka Upewe Karatu

$
0
0
Kaimu Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Karatu, Wende Lyimo (wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya bodaboda kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya weka upewe, Mchungaji Christopher Kingo katika hafla iliyofanyika tawini hapo, Arusha hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wateja wa benki hiyo na mfanyakazi wa benki hiyo, Kalist Masika (kulia).

Watanzania wengi hawana uelewa kuhusu tatizo la usonji - Mama Salma Kikwete

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo

Watanzania wengi hawana uelewa  wa tatizo la usonji (Autism)  kwa watoto hivyo basi uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa jamii unahitajika  ili watu watambue  tatizo hilo na kuweza kuwasaidia watoto hao.

Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma kikwete wakati akiongea na Prof. Andy Shih ambaye ni Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mambo ya kisayansi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Autism Speaks katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) zilizopo jijini Dar es Salaam. 

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo alisema  jamii ikiwa na uelewa kuhusu watoto hao kutakuwa na mabadiliko kwa wazazi na walezi hivyo basi ni jukumu la jamii nzima kuungana na kuweza kuwasaidia watoto hao ili waweze kupata elimu na mafunzo maalum.

Mwenyekiti huyo wa WAMA alimpongeza Prof. Shih kwa kazi anayoifanya ya kuwasaidia watoto wenye usonji Duniani na kwa kitendo chake cha kuamua kuwasaidia watoto wa Tanzania.

Kwa upande wake Prof. Shih alisema tatizo la usonji linatibika kama watoto watapewa mafunzo mapema na  jamii ikipata elimu na kulifahamu tatizo hilo itaweza kuwasaidia watu wenye matatizo hayo kupata huduma.

Alisema alitembelea shule ya msingi Msimbazi Mseto ambacho ni kitengo mama cha kutoa huduma ya watoto wenye usonji na kujionea hali halisi na kuahidi kushirikiana na wadau wengine ili waweze kutatua changamoto zilizopo.
Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na wadau wa Afya nchini na Taasisi ya kimataifa ya Autism Speaks  yenye makao yake mjini New York Marekani  watafanya kazi kwa pamoja  ili kutumia vitendea kazi na utaalam wao ambao wameukusanya kwa miaka mingi kuwasaidia watoto wenye matatizo ya usonji nchini. 

Kazi watakazozifanya ni pamoja na  kuunda timu ndogo ya wataalam wa mitaala na mafunzo ambao watapitisha miongozo na mitaala iliyopo pamoja na ile ya Autism Speaks na kupendekeza utaratibu wa mafunzo ya makundi mbalimbali wakiwemo watoa huduma.

Timu hiyo inaandaa utaratibu wa mafunzo ya wazazi, walezi na familia ya mtoto mwenye matatizo ya usonji, kuandaa mwongozo unaokubalika wa kuwapima na kuwatambua watoto wenye usonji, kuandaa mitaala na miongozo ya ufundishaji wa watoto wenye usonji na kutumia jukwaa na program za kitaifa kuwalinda watoto.

Wakati wa Mkutano wa  69 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa tisa mwaka huu mjini NewYork Marekani Mama Kikwete alikutana na Prof. Shih ambaye aliahidi kufanya kazi na WAMA ili kuwasaidia watoto wenye tatizo la usonji ambao wataweza kupata elimu na huduma ya afya kama watoto wengine.

TANAPA YAZINDUA TUZO ZA TANAPA ZA HABARI ZA 2014

Viewing all 110108 articles
Browse latest View live




Latest Images