Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 675 | 676 | (Page 677) | 678 | 679 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Bofya video kumsikiliza Nape Nnauye akizungumza kuhusiana na waliovuruga uchaguzi wa Serikalo za Mitaa.
    Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari,leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutoa tathmini ya matokeo ya awali uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika juzi nchini kote.
  Baadhi ya Wanahabari Wakimsikiliza  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao,leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutoa tathmini ya matokeo ya awali uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika juzi nchini kote.PICHA NA GLOBU YA JAMII.
  =======  =====  =======

  NA BASHIR NKOROMO.


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka watendaji wote waliosababisha kuharibika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya maeneo nchini wachukuliwe hatua kali.

  Kimesema, watendaji hao wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kilichotokea ni uzembe wa hali ya juu uliofanyika huku ikifahamika wazi kwamba tukio la uchaguzi huo ni kubwa na muhimu sana kwa Taifa.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (pichani) amesema, kulingana na kosa lililojitokeza kuwa la wazi hakuna haja ya kupoteza fedha na muda kufanya uchunguzi kabla ya kuwachukulia hatua waliohusika.

  "Kwa mfano, Mkurugenzi wa Halmashauri ana kila kitu na alijua mapema kuwa uchaguzi utafanyika lini kwa kuwa halikuwa jambo la dharura, inakuwaje anaruhusu karatasi ziende kwenye vituo zikiwa zimechapishwa hovyo au mahali pengine vifaa viwe vichache?" alihoji Nape na kuongeza "Sasa hapa unahitajika uchunguzi gani tena kubaini aliyevurunda?".

  "Mahali pengine zimefika karatasi za kupigia kura jina la mgombea wa CCM nembo ya CUF, au mgombea wa CUF nembo ya CCM! huu ni uzembe wa hali ya juu sana na adhabu yake haistahili kusubiri uchunguzi", alisema Nape.

  Akizungumzia matokeo ya awali ya Uchaguzi huo, Nape alisema licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miaka 22 sasa, huku vikifanya harakati za kujaribu kuungana katika umoja wanaouita Ukawa, bado CCM imewagaragaraza vibaya.

  Nape amesema, katika uchaguzi huo, CCM imepata zaidi ya asilimia 80 ya ushindi kwa nchi nzima, huku Dar es Salaam, ikiwa na asilimia zaidi ya 70 licha ya kwamba Chadema wanao wabunge wawili katika mkoa huo.

  "Katika mazingira ya sasa ambayo vyama vya upinzani vina miaka 22, na vinafanya hata harakati za kujaribu kuungana, asilimia 80 si ndogo kwa CCM, na tunaamini huu ni mwanzo mzuri, na hatuoni namna ambavyo asilimia hii itabadilika katika uchaguzi mkuu mwakani, maana uchaguzi huu ni kama kura za maoni", alisema Nape.

  "Wanaosema, asilimia ya CCM imeshuka, wajue kwamba tuliposema tunataka mfumo wa vyama vingi maana yake tulitaka ushindani katika demokrasia, katika demokrasia ya ushindani ni vema kuruhusu vyama vya upinzani vikakua ili ushindani huo uonekane", alisema Nape nakuongeza.

  "Hata hivyo inasikitisha kwamba licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miakaa 22 sasa, bado havijaweza kujenga imani ya kutosha kwa Watanzania kuwa vinaweza kuongoza, lazima wapinzania wazidi kujijenga ili Watanzania wawaamini, asilimia hii 14 waliyopata karika uchaguzi huu wa serikali za mitaa bado ni ndogo sana kwa uhai wa miaka hiyo".

  Amesema, asilimia iliyopata CCM wakati matokeo mengine yakisubiriwa ambako uchaguzi uliahirishwa, ni dalili za wazi kwamba, Ukawa bado ni muungano wa mashaka kwa sababu kama wangeungana na kuachiana maeneo ni kweli wangeweza kufika mbali.

  "Hebu jiulizeni na ninyi, kama kweli UKawa ulitumika vema, ni kwa nini kwenye karatasi za matokeo ya uchaguzi huu, kila chama kina mtu wake na idadi ya kura alizopata? Kwa nini zisiwe za mgombea mmoja wapo wa Ukawa?... Hii inamaanisha ndoa hii ya ukawa bado sana", alisema Nape.

  Nape aliwashukuru wananchi nchini kote kwa kuendelea kuiamini CCM, na kuchagua wagombea wake, huku akivipongeza vyama vya upinzani kwa maeneo waliyochaguliwa, akiwataka kuchapa kazi vinginevyo siku za baadaye wananchi watawahukumu kwa kuwatosa.

  0 0

  Kaimu Mwenyekiti wa umoja wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi(TAMONGSCO),Bw.Leonard Mao(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maamuzi ya Serikali kutatua mgogoro wa TAMONGCO,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo,Bw.Mrinde K.Mnzava.
               
  Na Bakari Issa,Dar es Salaam.

  Uongozi wa shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali(TAMONGSCO)  lililokuwa katika mgogoro na kikundi cha waliokuwa viongozi wa kitaifa(National Office Bearers) kilichofanya hujuma za kutaka kuifanya TAMONGSCO kuwa mali yao binafsi.

  Mara baada ya  Katiba kufanyiwa marekebisho kumi(10) na mkutano mkuu(AGM) uliofanyika Mbeya katika ukumbi wa Benjamin William Mkapa,AGM iliagiza kamati kuu ya Taifa (NEC) kuingiza marekebisho hayo kwenye katiba na kuipeleka kwa msajili wa asasi za kiraia(CSO) ambaye ni Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi.

  Akithibitisha uongozi wa shirikisho hilo,Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki na mameneja wa shule  na vyuo visivyo vya serikali,Bw.Leonard Mao amesema uongozi uliokuwa madarakani ndiyo sahihi pamoja na Katiba iliyopita na kuongeza kuwa wanaosema katiba na uongozi uliochaguliwa sio sahihi hao sio wanachama wetu na kuagiza waache kabisa.

  “Uongozi wa waliotaka kuchakachua katiba ya umoja huu,muda wao umekwisha na uongozi uliochaguliwa ndio uongozi sahihi pamoja na katiba iliyopendekezwa,na wanaosema  uongozi pamoja na katiba iliyopendekezwa sio halali hao si wanachama wetu na waache kabisa”,alisema Bw.Mao

  Naye Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo,Bw.Mrinde Mnzava  alisema kuwa umoja huo ndiyo unaoongoza kutoa wanafunzi bora nchini  na kuisaidia Serikali kuweka vizuri miundombinu ya shule pamoja na vyuo.

  Aidha amesema umoja huo utafanya kikao mkoani Dodoma ili kuteua nafasi ya Mwenyekiti ambayo imeachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti Kitaifa,Ally Hassan Mwanakatwe aliyefariki dunia.

  “Umoja huu  unalisaidia Taifa katika kutoa wanafunzi bora na kuipa changamoto Serikali kuboresha miundombinu ya shule na vyuo kwa ujumla na tunatarajia kufanya kikao mkoani Dodoma ili kumchagua Mwenyekiti mpya kitaifa”,alieleza  Mnzava

  Pia Naibu Katibu Mkuu wa TAMONGSCO,Bw.Chelestino Mofuga alitoa pongezi kwa  Serikali  kwa kuweza kusuruhisha suala hilo ambalo kwa sasa limefika mwisho na kuhakikisha kuwa mgogoro huo haupo tena.

  “Pongezi kwa Serikali kwa suala hili,lakini wamiliki wa shule binafsi tunakabiliwa na changamoto ya lugha katika kufundishia katika shule pamoja na vyuo”,alimaliza kusema Mofuga

  0 0

   Jeneza lenye Mwili wa aliewahi kuwa mwanamuziki mkongwe hapa nchini,Marehemu Shem Ibrahim Kalenga ukiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam tayari kwa mazishi.Marehemu Kalenga alifariki Dunia jana katika hospitali ya Amana,Ilala alikokuwa akipatiwa Matibabu.
  Umati Mkubwa uliojitokeza kwenye mazishi ya Marehemu Shem Ibrahim Kalenga wakijumuika pamoja kubeba Jeneza wakati wa Mazishi yaliyofanyika jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
  Picha zaidi bofya hapa


  0 0


  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kagera kujionea maendeleo ya Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja hicho. Waliotangulia mbele ni Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Bukoba, Mhandisi Suleiman Athuman (Katikati) na Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mulungwana (Kulia).
  Ujenzi unaendelea! Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kagera.


  0 0

  1Bima ya Afyaaa
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya mfuko huo wakati walipoonyesha tuzo ambazo mfuko huo ulitunukiwa nchini Morocco na Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni. kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakiwa katika mkutano huo uliozungumzia tuzo hizo.
  Bima ya Afya
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili pamoja na wakurugenzi wa shirika hilo kulia Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakionyesha tuzo zilizokabidhiwa kwa mfuko huo kutoka Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni.


  0 0

  Benki ya NMB kwa kuelewa uhitaji wa vifaa vya hospitali na madawati katika jamii inayoizunguka, imetoa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu pamoja na madawati sabini yenye thamani ya shilingi millioni tano kwa Shule ya Msingi Likokona iliyoko Wilayani Nanyumbu, Mkoani Mtwara.

  Msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga,   ni mwendelezo wa sera ya NMB ya kuchangia huduma za jamii ili kukabiliana na changamoto zinazokabili sekta ya elimu na Afya.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa Nanyumbu.Mhe Kiswaga alisema “Msaada huu ambao tumeupokea leo kutoka NMB, utasaidia kupunguza uhaba mkubwa tuliokua nao kwa kipindi kirefu. Vifaa tiba vimekua havitoshelezi katika hospitali yetu lakini pia madawati nayo imekua ni kilio kikubwa katika shule za hapa Nanyumbu. Lakini leo NMB wamekua sehemu ya maisha yetu na hivyo wameweza kujua hitaji letu na kutusaidia. Naomba kutoa shukrani za pekee kwa uongozi mzima wa NMB.
  Meneja wa kitengo cha biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Kusini ,Mr.Haji Msigwa akimkabidhi vifaa vya Hospitali   Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu.
  Meneja wa kitengo cha biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Kusini, Mr. Haji Msigwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga  sehemu ya madawati yaliyotolewa kwa ajili ya Shule ya Msingi Likokona .
  Wanafunzi wa shule ya msingi Likokona walioshiriki hafla ya makabidhiano
  Sehemu ya Madawati yaliyotolewa na NMB.

  0 0

  001

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani akifungua semina ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika Roma Italia, Februari 2015.
  002
  Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.


  0 0
 • 12/16/14--09:05: YALE YALEEEEE........
 •  Moshi mkubwa unasababishwa na uchomaji wa misitu hovyo ukiwa umetanda barabarani na kupelekea watumiaji wa njia hiyo kupita kwa shida kwa kutoweza kuona mbele,hali inayoweza kusababisha ajali mbaya sana.hapa ni kwenye kijiji cha jirani na mji wa Muheza,Mkoani Tanga.


  0 0


  0 0

  KOCHA wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo amewaaga rasmi leo asubuhi wachezaji wa timu hiyo kwenye mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola huku akitarajia kuvuna zaidi ya Milioni 20 ndani ya klabu hiyo ikiwa ni mshahara wake wa dola 1200 na yupo kwenye harakati za kudai fidia ya kuvunjiwa mkataba na kuletwa mrithi wake kabla uongozi wa klabu hiyo haujamaliza nae.

  Hata hivyo, tayari Maximo ameaga wachezaji wake kwenye mazoezi ya asubuhi leo ambapo mazoezi hayo yaligeuka shubiri baada ya Maximo  kuwakusanya wachezaji wake na kuwambia kuwa kuanzia leo  sio kocha wa timu hiyo tena na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa klabu hiyo ambao pia hawajaridhishwa na uamuzi wa uongozi wa klabu hiyo kumuacha mshambuliaji Hamis Kiiza na kumsajili Amis Tambwe.

  Mmoja wa wachezaji hao alisema  "Ni kweli kocha ametuaga asubuhi daa! ndio hivyo tumesikitika lakini hatuna jinsi."

  Naye mchezaji mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Inaumiza sana jana (juzi) tumefanya nae mazoezi vizuri kabisa tena amechangamka kama kawaida kumbe nyuma kuna mambo yanaendelea, leo asubuhi tumeenda mazoezi kama kawaida tukijua tunafanya mazoezi matokeo yake anasema acheni kila kitu kaeni hapo nataka kuzungumza na nyinyi.


  0 0

  Kibao hiki kipo katika Mpaka wa Mkoa wa Tanga na Mkoa wa Pwani,katika kijiji cha Manga.

  0 0
 • 12/16/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Kwenye Chati - Balozi a.k.a Dola

  0 0


  0 0

  Mfalme wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live. 
  Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid 'Suma Ragar' akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga kutoa burudani katika msimu wa Xmas Dar Live wakati wa mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar . Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Benjamin Mwanambuu, Mkurugenzi Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (wa pili kushoto), Mzee Yusuf (wa pili kulia) na Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (wa kw nza kulia).
  Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makamuzi watakayoyafanya Dar Live katika msimu huu wa sikukuu.
  KAMPUNI ya Dar Live kwa mara nyingine imetoa ratiba kamili ya burudani katika msimu huu wa kufungia mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.


  Usiku wa Wafalme
  Kwa mara nyingine shoo bab’kubwa ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ijulikanayo kama Usiku wa Wafalme itagongwa ndani ya ukumbi huo pekee kwa burudani, Desemba 25 ‘Sikukuu ya Krismasi’ ambapo mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atagonga nyimbo zake zote kali siku hiyo.


  Diamond ambaye ni mshindi wa tuzo tatu kutoka Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards (CHOAMVA), siku hiyo atatinga na tuzo zake zote hizo ikiwa ni kuwapa shukrani mashabiki wake wote kwa sapoti waliyoitoa huku akipiga nao picha kwenye ‘red carpet’ na kuongea nao mawili-matatu.

  Mashabiki pia watapata nafasi ya kumshuhudia Diamond kwa mara ya kwanza akipiga nyimbo zaidi ya 20 jukwaani pasipo kusimama huku akiwatambulisha madensa wapya sambamba na kupiga pia na nyimbo zake zote ambazo zilishawahi kuachiwa na hazijawahi kuisha mpaka mwisho.
  Kwa upande wa muziki wa Pwani, usiku huo utafunikwa pia na Mfalme Mzee Yusuf ambaye siku hiyo ataungana na kundi lake la Jahazi Modern Taarab katika kuwaonjesha mashabiki ngoma zao zote zilizopo katika albamu yao mpya ya Chozi la Mama huku wakifunga mwaka na ngoma ambayo ni habari nyingine kwa sasa ya Mahaba Niue.

  Mashabiki watakaofika usiku huo pia watapata bahati ya kushuhudia mshindi wa shindano la kumtafuta mwanaume mwenye mvuto kutoka Gazeti la Ijumaa lijulikanalo kama Ijumaa Sexiest Bachelor ambapo mpaka sasa wamebaki washiriki watatu, Yusuph Mlela, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba.

  Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo watoto wote watakaofika watapata bahati ya kucheza michezo kibao kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea na mingine mingi huku kundi la sarakasi la Masai Worriors likiwapagawisha kwa kutoa michezo kibao ya sarakasi , mazingaombwe sambamba na kumwaga zawadi kwa kila mtoto.

  0 0

  Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic,Mh. Dora Mmari Msechu (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Estonia,Mh. Toomas Hendrik Ilves,wakati alipofika Ikulu ya nchi hiyo kuwasilisha hati utambulisho wake kwa Rais.
  Mhe. Balozi Dora Msechu (wa pili kulia) na timu yake wakiwa kwenye Mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Chuo  cha Tallinn University of Technology. Mazungumzo yao yalilenga kuanzisha ushirikiano na vyuo vya Tanzania (UDSM na UDOM) na pia kutafuta fursa zaidi za masomo ya sayansi ngazi ya Masters na Phd. Estonia ni moja ya nchi iliyopiga hatua kubwa sana katika masuala ya ICT.

  0 0

  Na Woinde Shizza, Arusha 
  Baraza la ushauri la chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii (VHTTI) limetakiwa kuhakikisha linaandaa wanafunzi vyema na wenye viwango vya kimataifa ili kukabiliana na ushindani mkubwa ulioko katika sekta ya hoteli na utalii duniani. 
   Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa wakati akizindua baraza hilo jana ndani ya chuo cha hoteli na utalii cha VHTTI kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha . 
   Alisema kuwa kutokana na changamoto kubwa ya hoteli zetu kuajiri watu kutoka nje ya nchi ikiwemo kenya na hata nchi za bara ya ulaya kwa kile kinachodaiwa vijana wazawa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na sekta ya hoteli na utalii hivyo ni wajibu wao kuakikisha wanafundisha wanafunzi ili waweze kuwa na elimu ya kiwango cha kimataifa . 
   Alibainisha kuwa wanatakiwa wahakikishe wanachuo ambao wanawafundisha wanakuwa na sifa zinazotakiwa huku akiongeza kuwa mafunzo wanayofundishwa yawe bora yanayokidhi maitaji ya ajira .
   Aidha alisema kuwa iwapo watawafundisha wanafunzi hao vyema na kuwapa elimu inayoitajika kuoendana na soko hii itawasaida kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira kwani wanafunzi hawa pindi watakapo maliza elimu yao itakuwa raisi kupata kazi kulingana na elimu walikuwa nayo. 
   ''Pia napenda kuwashauri kuanzisha lunga zote za kimataifa katika chuo chenu ili mwanafunzi anaetoka katika chuo hichi aweze kuwasiliana na mgeni yeyote ambaye atakuja kutoka katika nchi yoyote huko kazini kwake anapoenda kwakweli inachekesha sana kuona mgeni anakuja alafu mwanafunzi anaanza kuongea lugha mfano ya Kingereza kwa kukosea kosea au anaongea Kifaransa  kwa kukose kosea''alisema Munasa 
   Kwa upande wa Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kuwa wao kama Veta wameamua kuanzisha chuo hichi cha hoteli na utalii ili kuweza kupunguza tatizo la ajira ambalo linaendelea kwa vijana wengi. 
   Aliesema kuwa chuo hichi kitatoa mafunzo ya hoteli na utalii katika ngazi ya cheti na shahada kwa wasimamizi na waangalizi wa hoteli zetu. Naye mkuu wa chuo hicho Flora Hakika alisema kuwa wataji taidi kuwafundisha wanafunzi vyema na wataanza kwa kuaandaa mitaala mipya huku wakiwa wanaangalia zaidi jinsi wenzetu wa nchi za nje wanavyo fanya pia watajitaidi kulenga kupata maitaji ya soko linavyoitaji ili kuweza kuinua zaidi utendaji kazi wa vijana wa kitanzania
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa akiwa anaongea wakati wa uzinduzi  wa baraza la ushauri wa chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii cha mamlaka ya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (VHTTI) Kilichopo Njiro mkoani Arusha
  Bw. Mattasia, Mwenyekiti wa Chuo cha hoteli na utalii cha VHTTI akiongea 
  wadau mbalimbali wakiwemo wajumbe wa chuo hicho wakiwa wanafatilia uzinduzi huo wa baraza la chuo kwa makini


  mkuu wa wilaya ya Arumeru akiwa anamkabidhi nyaraka ya kutendea kazi mmoja wa wajumbe wa baraza la chuo cha VHTTI ambaye ni mwakilishi wa chama cha wamiliki wa makampuni ya utalii(TATO) bw, Peter Lindstrone
  Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi (kulia) akifuatiwa na mwenyekiti wa bodi  Bw. Mattasia pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru  Mhe. Nyerembe Munasa na wakwanza kushoto ni mkuu wa chuo cha VHTTI Flora Hakika wakibadilishana mawazo

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu  Madame Rose Abdallah akitoa shukrani kwa wageni waliofika kwenye mchaparo wa kusherehekea kutimiza Miaka 20 ya Antelope Tours& Travel Services Ltd iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam

   Mkurugenzi Mkuu Eckhardt Mtasiwa akiongelea machache kuhusu kampuni kwa wageni waalikwa

   Bwana Davis Mosha akiongea machache baada ya kupokea tuzo ya mteja wa Antelope Tours & Travel Services Ltd wa miaka mingi

   Meneja Mkuu Bwana Harry Chopeta akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Rose Abdallah na wakurugenzi Bwana Eckhardt Mtasiwa na Bi Lysa John

   Mkurugenzi mkuu Rose Abdallah akikata keki huku  na wafanyakazi wa Antelope na Meneja mkuu wa Amadeus Juan Tores wakiisubiuri kwa hamu.

  0 0

  Na Freddy Macha, London
  Watalii na wageni Tanzania wamehakikishiwa kwamba kasheshe ya Ebola inayousakama uwanda wa magharibi ya bara haitaidhuru Bongo. Akizungumza nami katika ofisi ya kampuni ya Safari Hub yenye makao makuu Arusha na London, Mkurugenzi, Navraj Hans alisema ingawa kitakwimu idadi ya watalii barani imeshuka kwa asilimia 50 hakuna haja ya kuhaha. 
  “Ebola inasambaa kirahisi zaidi kuelekea Ulaya kutoka Afrika Magharibi kuliko kuja kwetu. Sisi tuko mbali sana.” 
  Bwana Hans ambaye pia ni dereva na mshindi wa mbio za magari Tanzania, alisema ni muhimu kuzingatia si Ebola tu nuksi iliyolipaka bara, masizi. “Hebu tazama Afrika Kusini yenye mauaji makubwa sana, kitakwimu, duniani. Utalii unaendelea kama kawaida, maana wenzetu wanasisitiza kuwa kuna mabaya machachena mazuri mengi zaidi. Matokeo,” aliendelea kufafanua Bwana Hans ambaye ni mzawa wa Arusha, 
  “Watalii wanaendelea kutiririka Sauzi bila shaka yeyote.” Mkurugenzi huyu wa Safari Hub aliendelea kusisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa mandhari nzuri duniani. 
   “Watanzania wanasifika kwa ukarimu wao na amani. Hivyo tujitangaze zaidi. Tujifunze toka kwa nchi kama Singapore na Indonesia wanaojua kujitangaza.” 
   Kuonyesha namna Tanzania inavyohusudika, Bwana Hans alisema karibuni kampuni ya kimataifa ya Kili Villa imeamua kujenga uwanja wa mchezo wa Golf eneo la Maji ya Chai wilaya ya Arumeru. Ili kutimiza lengo lake, kampuni hiyo iliwasiliana na Safari Hub. Uwanja huo utakaokuwa na ekari 7,000 na mashimo 18, umeshawekwa katika ya orodha ya viwanja kumi bora vya golf Afrika. 
  Mandhari ya uwanja inaonyesha milima Meru na Kilimanjaro, moja ya vivutio vikuu vya Kitanzania. Bosi wa Kili Villa, Bwana Wilhem Kurpers alinieleza kwamba mcheza Golf mashuhuri, Tiger Woods, ameshakubali mualiko kuitembelea Tanzania kwa kuvutiwa na viwanja hivyo vya Maji ya Chai. 
  Mapema mwaka huu Safari Hub ikishirikiana na shule maarufu ya Eton College na Ubalozi wetu Uingereza ilipeleka timu ya vijana kuendeleza mpira Arusha.
  Mandhari ya uwanja mpya wa gofu utaojengwa eneo la Majani ya Chai Arusha na kampuni ya Kili Villa
  Mandhari ya uwanja mpya wa gofu utaojengwa eneo la Majani ya Chai Arusha na kampuni ya Kili Villa
   Mkurugenz wa Safari Hub Bw. Navraj Hans akiwa ofisini kwake na Bosi wa kampuni ya Kili Villa Bw. Wilhem Kurpers
   Bw. Navraj Hans akiwa  na Bosi wa kampuni ya Kili Villa Bw. Wilhem Kurpers mbele ya picha za vivutio vya Tanzania
   Mkurugenzi wa Safari Hup Dilip Navapurkar  akizungumza, akisema Tanzania inaweza kuendelezwa ikafikia kiwango cha timu nyingine bora Afrika katika kandanda.

  0 0

  Na Woinde shizza, Arusha 
   Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai mkoani Arusha ameahirisha hadi  Desemba 24, 2014  kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru  Mashariki Mh. Joshua Nassari (pichani), kwa tuhuma za kuharibu mali ya umma  yenye dhamani ya shilingi laki mbili, pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya Desemba 15, mwaka huu 
  Mahakama hiyo imemuachia Mbunge huyo baada ya kutimiza masharti ya dhamana,  ikiwa ni wadhamini watatu ambao wana mali zisizohamishika zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja. 
   Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki Bw. James Ole Milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haihitaji mashariti makubwa hivyo . 
   Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhusu kuweka wakili. 

  0 0

  http://2.bp.blogspot.com/-i2-4osDY9qY/UWP7jkUdnlI/AAAAAAAAZlU/Kl-V8X24-g4/s1600/IMG_0134.JPG
    WATU watano wamekufa na wengine 36 kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kwenda msibani kupata hitilafu katika mfumo wa breki na kisha kutumbukia kwenye korongo.

  Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Bw. Ahmed Msangi zilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nane mchana katika mteremko wa Kanyegele, Kata ya Ntokela wilayani Rungwe.

  Kamanda Msangi alisema lori hilo aina ya Mitsubishi Fuso yenye namba za usajili T143 ACR lilikuwa likitokea Ilemi jijini Mbeya likiwa limebeba maiti na waombolezaji kuelekea wilayani Rungwe.

  Alisema baada ya kufika katika mteremko wa Kanyegele dereva wa gari ambaye hakufahamika jina lake mara moja alipojaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake ghafla lilijitokeza gari jingine mbele yake na alipojaribu kuminya breki lilimshinda na hatimaye kutumbukia kwenye korongo na kusababisha vifo na majeruhi hao.


  Alisema kati ya majeruhi 36, wawili walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi, tisa wakapelekwa hospitali ya Wilaya ya Rungwe ya Makandana na 25 walipelekwa katika kituo cha afya Igogwe.

older | 1 | .... | 675 | 676 | (Page 677) | 678 | 679 | .... | 3272 | newer