Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

UPDATES YA MSIBA WA MAMA KULWA, DOTTO NA NICO MWAIBALE JIJINI DAR

$
0
0
Mwili wa  marehemu,   Bi. Twitikege Mlagha Mafumu utaagwa kesho saa 4 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke kisha kupelekwa katika Kijiji cha Kibumbe, wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambapo atazikwa Desemba 17 alasiri.
Bi. Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake
 Meneja Mkuu  wa Global Publishers Limited Bwana. Abdalah Mrisho akitoa mkono wa pole kwa  Dada mkubwa wa kina Mwaibale Mwalimu Mary Anyitike

Mwanahabari Kulwa Mwaibale (mwenye Fulana nyekundu) akiwatambulisha wafanyakazi wenzake wa Kampuni ya Global Publisher kwa wanafamilia.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Leo wakiwa wamefika kuhani msiba wa Mama yao Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale.
HABARI ZAIDI INGIA HAPA


BASATA YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWANAMUZIKI MKONGWE SHEM KALENGA

$
0
0


National Arts CouncilBASATA

 

Yah: Salaam za Rambirambi

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Shem Ibrahim Kalenga


“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Shem Ibrahim Kalenga ambaye mchango wake katika muziki wa Dansi ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.


Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

 Imetolewa na
Godfrey Mngereza

Kaimu Katibu Mtendaji

Baraza la Sanaa la taifa.







UPDATES: MSIBA WA MAREHEMU SHEM KARENGA WAHAMISHIWA MTAA WA UFIPA, KINONDONI, DAR ES SALAAM

$
0
0
TAARIFA ZILIZOTUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA KWAMBA FAMILIA YA MAREHEMU SHEM KARENGA IMEHAMISHIA MSIBA HUO KINONDONI, MTAA WA UFIPA (JIRANI NA OFISI ZA CHADEMA). 

MIPANGO YA MAZISHI INABAKI PALEPALE YAANI KESHO MAREHEMU ATASWALIWA KATIKA MSIKITI WA MANYEMA, KARIAKOO, BAADA YA SWALA YA ALASIRI NA KISHA KUELEKEA MAKABURI YA KISUTU KWA MAZISHI>

CCM YAONGOZA UCHAGUZI VIJIJI,VITONGOJI NA MITAA MKOA WA PWANI

$
0
0
Na John Gagarini, Kibaha

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani kimeonyesha kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji ambapo kwenye matokeo ya awali kimeonekana kushinda maeneo mengi.

Katika Jimbo la Mafia CCM ilishinda vitongoji  96 kati ya 136 sawa na asilimia 70 Chama Cha Wananchi CUF asilimia 40 sawa na asilimia 29,katika vijiji  CCM ilishinda vijiji 19 kati ya 23 sawa na asilimia 82.6 CUF vijiji 4 sawa na asilimia 17.3.

Katika Jimbo la Kibaha Mjini kati ya mitaa iliyopo 73 ,CCM imeshinda mitaa 62 sawa na asilimia 84.9, huku wapinzani wao Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakishinda kwenye mitaa 10 sawa na asimilia 13.7.

Katika Jimbo Kibaha  Vijijini kwenye Vijini 32 CCM ilishinda mitaa 31 , ambapo kwenye mitaa 10 ilishinda bila kupingwa sawa na asimilia 96.9 ,upinzani ilishinda kijiji kimoja sawa na asimilia 13.1, kati ya vitongoji 106 CCM ilishinda vitongoji 98 sawa na asilimia 92.5,upinzani vitongoji 4 sawa na asilimia 3.8.

Katika Wilaya ya Bagamoyo vijiji vilivyopo ni 75 CCM ilishinda vijiji 67 sawa na asilimia 90.5 na vijiji 8 havijafanya uchaguzi, kati ya vitongoji  610 CCM ilishinda 540 sawa na asilimia 88.5 na vitongoji 45 havijafanya uchaguzi ambapo wapinzani walishinda vitongoji sawa na  asilimia 4.1.

Wilaya ya Bagamoyo haijafanya uchaguzi katika vijiji 8 na vitongoji 45 kutokana na uhaba wa vifaa ikiwemo katasi husika za viti maalum na kuchanga majina ya wananchi na nembo za vyama vya siasa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Ibrahim Matovu alithibitisha kutokea kwa mabadiliko ya uchaguzi katika maeneo hayo ambapo alisema uchaguzi huo baadhi ya maeneo ulifanyika jana na kwingine utafanyika leo desemba 16.

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAFANIKIWA KWA ASILIMIA 98

$
0
0
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Hawa Ghasia akiwaeleza waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini ambapo umefanikiwa kwa asilimia 98%,kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Hawa Ghasia (hayupo pichani) na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salam ukilenga kueleza hatua zitakazochukuliwa na Serikali kwa wale wote waliosababisha kasoro mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana kote nchini. Picha zote na Maelezo

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI SAMPULI ZA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA MADARASA YA AWALI KATIKA MANISPAA YA LINDI MJINI

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando mara baada ya kuwasili kwenye viwanja wa Shule ya Msingi Rahaleo iliyoko Manispaa ya Lindi Mjini kwa ajili ya kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kupitia taasisi yake kwenye Shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na binti Naida Seleman anayesoma darasa la awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo mara baada ya Mama Salma kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kwenye Shule za Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.

ngoma azipendazo ankal - proudly sponsored by Isumba Lounge

IN LOVING MEMORY of MR CLEMENT G MABINA


Nahodha atembelea ubalzi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

$
0
0
  " Karibu na asante kwa kuja kututembelea" Mwakilishi  wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akimkaribisha Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ( Mb) katika  Ofisi za ubalozi wa Tanzania  Umoja wa Mataifa.
 Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ( Mb) akisaini kitabu  cha  wageni  Ofisini kwa  Mwakilishi wa Kudumu Balozi Tuvako Manongi (kulia). Mhe. Nahodha alikuwa  Nchini Marekani kwa ziara ya kikazi. 

Airtel yazindua ofa kabambe ya simu wakati wa msimu wa sikukuu

$
0
0
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe ya simu kwa msimu huu wa sikukuu ya Krismasi, ambapo itawawezesha wateja wa Airtel kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi, ujumbe mfupi na huduma ya intaneti. Kushoto ni Meneja Masoko wa Bidhaa za Kisasa wa Airtel, Prisca Tembo.
Meneja Masoko wa Bidhaa za Kisasa wa Airtel, Prisca Tembo (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde wakionyesha kwa waandishi wa habari, baadhi ya simu za mkononi zilizo kwenye ofa kabambe ya simu kwa msimu huu wa sikukuu ya Krismasi, baada ya kuzindua ofa hiyo, jijini Dar es Salaam jana, ambapo itawawezesha wateja wa Airtel kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi, ujumbe mfupi na huduma ya intaneti.

Airtel Tanzania leo imetangaza ofa kabambe inayoenda sambamba na kuwazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa sikukuu, ofa hii iliyozinduliwa rasmi leo itawawezesha wateja kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa bidhaa za kisasa Bi Prisca Tembo alisema” tunayofuraha kuzindua ofa hii ya msimu wa sikukuu na kuwawezesha wateja wetu kununua simu kwaajili yao na kwaajili ya wale wanaowapenda kwa bei nafuu zaidi sokoni.

Tembo aliongeza kwa kusema “Ofa hii inaenda sambamba na dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma bora huku tukiwawezesha wateja wetu kufaidika na huduma na bidhaa zetu.  Simu hizi  za kisasa (yaani smart phone) zinapatikana katika maduka yetu ya Airtel nchi nzima kwa gharama  kuanzia  shilingi 125,000/=  hadi 979,000/=. Mteja atakaponunua simu hizi atapata na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na internet vya mwenzi mzima, ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu

Ofa hii si ya kukosa, hivyo Tupenda kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa hii kwa kuwa wakwanza kununua simu ya aina wanayoipenda na kufurahia huduma zetu na kuunganishwa kwenye huduma ya internet ya 3.75G .” aliongeza Tembo

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” simu tulizonazo kwenye ofa ni pamoja na iphone 6, simu za Huawei na Techno. Simu hizi za kisasa ni rahisi kutumia na zitawapatia wateja wetu uzoefu tofauti si kwa bei rahisi tu bali zimewezeshwa na techonologia ya 3G na kuwawezesha kufurahi internet ya kasi.”

Natoa wito kwa wateja kutembelea ofisi zetu na kunua simu na kuunganishwa na huduma zetu nyingi ikiwemo Airtel yatosha, Airtel Money, huduma ya internet na vifurushi vya OMG, Switch On pamoja na huduma yetu mpya ya WiFi ya nyumbani tuliyoizindua hivi karibuni aliongeza Matinde.

SHUKRANI

$
0
0
Familia ya Marehemu Mzee Alexander George Mushema inapenda kutoa shukurani kwa wale wote walio shiriki na kutufariji katika kipindi kigumu cha kuwapoteza wapendwa wetu kaka yetu Robert Deusdedit Kamashaija aliyefariki 26 November 2014 na baba yetu Alexander George Mushema aliyefariki tarehe 13 November 2014. 

Shukurani ziende kwa madaktari wa Hospitali ya Mkoa Bukoba, Serikali ya Tanzania, Chuo Kikuu cha Uppsala Sweden.

Hatuwezi kumtaja kila mmoja lakini tunatanguliza shukurani zetu.

WAZIRI MAKALA AWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WEZI WA MAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuwafichua wale wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.Alitoa wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji

Waziri Makala alisema kuwa serikali inafanya jitihada ya kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na kuboresha miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa wananchi.“Wizi wa kujiunganishia maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni ya kuwasaka wale wote wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria”alisema Makala

Aidha katika moja ya chanzo kikubwa cha maji mto nduruma alisema kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi kwa mamlaka ya maji kwa kuwa wabunifu.
Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni walikuwa na zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kufanikiwa kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo bado ni endelevu.
SAM_0190Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiongea na vyombo vya habaria katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
SAM_0188
 Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga 
SAM_0178

Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
SAM_0191
Askari anayelinda eneo hilo.Na Pamela Mollel wa jamiiblog.

boda boda mwendo mdundo.......

OFISI YA WAZIRI MKUU KUIMARISHA MIFUMO YA UTOAJI TAARIFA ZA TAHADHARI KUHUSU TABIA NCHI NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Harrison Chinyuka (Katikati) akisisitiza jinsi menejimenti ya maafa inavyotekelezwa kwa Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha utoaji wa Taarifa za Tahadhari kuhusu Tabia nchi na Mifumo ya Tahadhari nchini wakati wa mkutano wa wadau wa mradi huo leo Jijini Dar es Salaam, (kushoto) Mwakilishi wa UNDP, Tanzania wa mradi huo, Bw. Abbas Katogo, (kulia) Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Fanuel Kalugendo.

Luizer Mbutu kuimba nyimbo zote alizoshiri katika bendi ya Twanga Pepeta

$
0
0
MWANAMUZIKI mkongwe pia Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amesema katika kupamba usiku wa Luizer Mbutu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 16 ndani ya bendi bila kutoka ataimba nyimbo zote za bendi ambazo alishiriki kwa namna moja ama nyingine.

Akizungumza na Ripota wetu jana Mbutu alizitaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni ‘Kisa Cha Mpemba’, ‘Jirani’, ‘Fainali Uzeeni’, ‘Mtu Pesa’, ‘Safari 2005’, ‘Mwana Dar es Salaam’ , ‘Kuolewa’ pia kutakuwa na wimbo maalum siku hiyo.

Mbutu aliongeza kwa kusema kuwa amefurahishwa na wasanii wa kike kujitokeza katika kutoa sapoti siku hiyo ambapo anamtaja mwanamuziki aliyeongezeka kuwa ni Hafsa Kazinja, ambaye atajumuika na Stara Thomas ‘Stara T’, Siza Mazongera ‘Mamaa wa Segere’.

Wengine ambao watanogesha onyesho hilo kuwa ni bendi ya Utalii inayoongozwa na Komandoo Hamza Kalala ‘Mzee wa Mdaongo’, bendi ya Msondo Ngoma .

Wakati huohuo Mbutu alisema kwamba naye waliokuwa wanenguaji wakali wa bendi ya hiyo Lilian Tungaraza ‘Lily Internet’ na Aisha Madinda nao watakuwepo siku hiyo ambapo wataudhihirishia umma kwamba bado wako gado.

Mbutu alisema kwamba pia mwanamuziki ambaye aliwahi kufanya kazi katika bendi hiyo Roggert Hegga ‘Caterpiller’ , Bob Gaddy Wai na Ramadhan Masanja wamethibitisha kuwepo katika maadhimisho hayo yatakayofanyika Desemba 20 katika ukumbi wa Mango Garden Kindoni Jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh.10,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Asha Baraka alisema kuwa wameandaa onyesho hilo ambalo litakua maalum kwa Kiongozi wa bendi hiyo ambaye anaetimiza miaka 16 ndani ya bendi bila kuhama tangu ilipoanzishwa hivyo wanafanya hayo ikiwa ni katika kuenzi mchango wake ndani ya bendi.

“Uongozi wa ASET umeamua kuandaa usiku maalum wa kumuenzi Luiza kutokana na kua na msimamamo wa kukaa katika bendi kwa muda wote huo bila kuhama hilo ni jambo la kujivunia” alisema Mkurugenzi wa bendi Asha Baraka.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa wao kama ASET wanatambua mchango wa Luiza ndani ya bendi hiyo hivyo kutakuwa na tukio la aina yake ambalo mashabiki na wadau wa bendi hiyo pamoja na wapenzi wa Luiza wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia litakalojiri sambamba na kupata burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 16.12.2014.

DKT. SHEIN AFUNGUA MKUTANO WA 8 WA BARAZA LA BIASHARA ZBC,ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja kushiriki katika Mkutano wa 8 wa Baraza la Biashara la Zanzibar (ZBC) lililofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Baraza la Biashara la Zanzibar (ZBC) ulilofanyika leo Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja (kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko  Nassor Ahmed Mazrui na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee(kulia).

MAALIM SEIF ZIARANI NCHINI UTURUKI

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili nchini Uturuki kwa ziara ya siku tatu ya kiserikali.

Ziara hiyo inafuatia mwaliko rasmi wa serikali ya Uturuki kupitia kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo  Mhe. Ahmet Davutoglu.

Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa mjini Istanbul, Maalim Seif alipokelewa na Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Mhe. Mevlut Cavusoglu.

Mbali ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake ambaye ni Waziri Mkuu wa Uturuki, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar pia anatarajiwa kukutana na viongozi wa jumuiya ya watembezaji watalii ya nchi hiyo.

Aidha Maalim Seif ambaye ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Bw. Ali Saleh Mwinyikai, anatarajiwa kuhudhuria kwenye maadhimisho ya sherehe kubwa za kimila nchini humo ambazo pia zitahudhuriwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Recep Tayyip Erdogan.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni kadhaa mashuhuri kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Imetolewa na 
Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Zanzibar.

DEREVA WA BODA BODA KAPITA HAPA.!

$
0
0
Dereva wa Boda boda akiwa amepenya katikati ya magari mawili bila kujali usalama wake kama aonekanavyo pichani,mara baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii iliyokuwa ikijivinjari mtaa wa Jamhuri,jijini Dar mapema jioni ya leo.Pichani Kulia ni  dereva akitoa maneno ya kumuonya dereva huyo wa boda boda kuacha tabia ya kulazimisha kupita sehemu ambayo inahatarisha usalama wa maisha yao,lakini hata hivyo  Dereva huyo wa boda boda alionekana kutojali kwa kile alichokuwa akiambiwa badala yake aliendelea na safari yake.

MSAFARA WA KIGAMBONI

$
0
0
Foleni ya magari kuelekea Kigamboni ikiwa imechanganya jioni ya leo kama ionekavyo pichani mara baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii .
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images