Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 669 | 670 | (Page 671) | 672 | 673 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Katika pita pita za kila siku mtaani,hivi karibuni kamera yetu ilikatiza maeneo ya Vingunguti pembezoni mwa bonde la Mto Msimbazi na kukutana na hali kama ionyekanavyo pichani hapa.kiukweli mambo si shwari katika eneo hili hasa usalama wa afya kwa wakazi waliozunguka eneo hilo.ukiangalia kwa makini utabaini kuwa kuna watoto wadogo wakiendelea na michezo katika eneo hilo bila kufahamu kuwa wapo hatarini kiafya.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimfafanulia jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Haji Omar Kheri (kushoto-meza kuu) pamoja na Maofisa wa Watendaji wa wizara hiyo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa mkutano wa ushirikiano wa wizara hizo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Haji Omar Kheri, akimfafanulia jambo Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia-meza kuu) pamoja na Watendaji Wakuu wa wizara hizo mbili wakati wa mkutano wao wa ushirikiano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0  0 0

  Meneja wa Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya Huawei Tanzania, Peter Zhang (kulia) na Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo (kushoto) wakionyesha simu mpya aina ya Smartphone 6-inch Ascend Mate 7 katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa Kampuni ya vifaa vya teknolojia ya Huawei Tanzania, Peter Zhang (kulia) na Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo (katikati) wakionyesha simu mpya aina ya Smartphone 6-inch Ascend Mate 7 katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Masoko wa kampu hiyo, Lydia Wangari.
  Meneja Masoko wa Huawei , Lydia Wangari (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu mpya aina ya Huawei 6-inch Ascend Mate 7 jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo na Meneja wa Huawei Tanzania, Peter Zhang.

  0 0

  Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, na viongozi wa juu wa PSPF,na TPB, wakiwa katika picha ya pamoja.
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, (TPB), Sabasaba Moshingi, (Wakwanza kushoto) na Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, wakishikana mikono kuashiria uzinduzi wa huduma mpya za mikopo kwa wanachama wa Mfuko huo kupitia TPB jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Desemba 11, 2014

   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, akitoa hotuba yake.

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake.  


  Leo Desemba 11, 2014 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua huduma mpya kwa wateja wake, huduma hizo ni Mkopo wa kuazia Maisha na Mkopo wa elimu.

  Kwa upande wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote ile ya elimu, mfano stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 4.

  Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa ana mahitaji muhimu, kwa kutambua hilo PSPF imeanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaweza kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili aweze kujipanga na maisha mapya ya ajira. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.

  Lengo kubwa la PSPF kuanzisha mikopo hii ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kwa kupitia mkopo wa elimu au ndoto yake nyingine kwa kupitia mkopo wa kuanzia maisha, hivyo natoa wito kwa watanzania  wenzetu kujiunga na PSPF ili waweze kufaidika na fursa hizi.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudentia kabaka alisema amefurahishwa na PSPF jinsi ilivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika Kubuni, Kupanga, kuandaa na hatimaye kuteleza utratibu huu, alisema hili ni jambo sahihi na mwafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii duniani kote, kazi za Mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni kuwawezesha wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanastaafu. 


  Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi alisema mwanachama wa PSPF anayetaka kukopa anatakiwa kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Posta lililopo karibu yake. Huduma za utoaji wa mikopo hii ni za haraka sana na bora.

  0 0

   Anchali Seleman Mmoja wa wakulima wa mpunga katika bonde la Madibira akiandaa mbegu ya mpunga katika kitalu chake baada ya kuwezeshwa na udhamini wa Baraza la Uwezeshaji Taifa kupitia bank ya CRDB pamoja na Madibira Saccos.
   Baadhi ya wakulima waliodhaminiwa na serikali kupitia baraza la uwezeshaji la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka baraza hilo.
  Mmoja ya Mkulima aliyefanikiwa kupata udhamini wa baraza la uwezeshaji akielezea mafanikio yake baada ya udhamini huo ikiwa pamoja na ujenzi wa nyumba ya kisasa na kununua trekta na vifaa kazi vingine.(Picha na Denis Mlowe).
   
  NA DENIS MLOWE, MADIBIRA
   
  BARAZA la uwezeshaji Taifa limewanufaisha jumla ya wakulima 400 wa kilimo cha Mpunga wa bonde la Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa kuwadhamini kupitia benki ya CRDB tawi la Iringa na Madibira Saccos baada ya kupatiwa mkopo wa shilingi milioni 400 ambazo zimeweza kuwanufaisha katika kilimo cha mpunga kwa kununua vifaa vya kilimo na kukuza kipato.
   
  Akizungumza na Tanzania Daima wakati walipowatembelea wakulima hao na kufanya ukaguzi wa udhamini huo mwishoni mwa wiki, Afisa Mwandamizi Mawasiliano ya Umma na Ushawishi kutoka Baraza la Uwezeshaji Taifa, Edward Kessy alisema kuwa lengo la udhamini wa serikali kwa wakulima hao ni kutekeleza mpango wa taifa wa matokeo makubwa sasa kuwawezesha wakulima kuinua kipato chao na kukuza uchumi wa nchi kupitia kilimo.
   
  Kessy alisema kuwa kupita benki ya CRDB tawi la Iringa serikali wamewadhamini wakulima hao fedha hizo ambazo wanazikopa kupitia Madibila Saccos inayofadhiliwa na benki hiyo na wamepatiwa elimu ya kilimo cha kisasa ambacho kimewasaidia kuongeza uzalishaji mazao na kudhibiti tatizo la njaa wilayani humo.
   
  “Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi chini ya mfuko wake wa uwezeshaji mwananchi ambao unatekelezwa kwa kushirikiana na benki ya CRDB imeweza kuwadhamini wajasiriamali mbalimbali  kwa kupitia vyama vya kuweka na kukopa nchini kuweza kupata mikopo ambayo inakuwa mitaji katika kuendeleza biashara zao na kilimo kwa ujumla na itaendelea kutoa udhamini zaidi kwa mwaka wa fedha ujao’ alisema Kessy.
   
  Alisema baraza hilo hadi sasa limeweza kutoa mikopo yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa wajasiriamali mbalimbali na wakulima wa mazao mbalimbali na wakulima wa mpunga Madibira wamedhaminiwa shilingi milioni 400 ikiwa ni awamu ya kwanza kwa wakulima hao.
   
  Awali wakulima hao waliishukuru serikali kwa udhamini huo uliowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato cha familia sambamba na kuongeza mavuno ya mpunga kwa mwaka jana.
   
  Mmoja wa wakulima wa mpunga katika bonge la Madibila, Anchila Seleman alisema kuwa mkopo huo umewawezesha kukuza kipato na mavuno ingawa wanakumbana changamoto ya soko la zao la mpunga hapa nchini.
   
  Alitoa wito kwa baraza la uwezeshaji kuendelea kutoa mikopo kwa wakulima kwa lengo la kuwanufaisha na kuwatafutia masoko nje ya nchi kuweza kuuza mpunga kwa faida tofauti na sasa ambapo soko limekuwa likiwadidimiza wakulima wadogo.
   
  Kwa upande wake,Bruno Theodory Meneja Mahusiano wa benki ya CRDB tawi la Iringa alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima hao kupitia mahusiano mazuri waliyoweka na Madibira Saccos ambapo wakulima hujipatia mikopo kila mwaka kutokana na uanachama waliokuwa nao.
   
  Alisema kuwa msimu wa 2013/2014 wakulima walionufaika na udhamini wa baraza la uwezeshaji ni zaidi ya 400 waliojipatia mkopo wa shilingi milioni 1 kwa kila mkulima na kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao mengi zaidi tofauti na misimu iliyopia. 

  0 0

  In an effort to create employment and increase opportunities to Tanzanians participate fully in economic activities. In 2004, the Government of Tanzania establish National Economic Empowerment Fund, through National Economic Empowerment Act of 2004, section 16. Among other things, the fund is for extending concessionary loans and provision of credit guarantee to borrowers in Tanzania Mainland.

  Furthermore, TIB Development Bank Limited (TIB) has entered into a contract with National Economic Empowerment Council (NEEC) to administer the Credit Guarantee Scheme under the National Economic Empowerment Fund. The Scheme is geared towards promoting and supporting the Young Graduate Entrepreneurs, Small Medium Enterprises (SMEs) and Cooperatives which have a significant role in the economy, by creating enabling environment for expanding and facilitating access to financing requirements.

  In this regard, TIB and NEEC have agreed to collaborate in the Credit Guarantee Programme by providing financial services to the borrowers who meet the criteria to access guarantees through the Fund.

  Generally, the Scheme shall target issuance of guarantees in respect to credit facilities granted by TIB for manufacturing, agriculture, trading and service provision projects that are geared to promote the growth of the economy. Therefore, the following specific criteria shall apply;-
   
  Executive Secretary of the National Economic Empowerment Council (NEEC),Dr. Annacleti Kashuliza (L) exchanged MoU with Managing Director of TIB Development Bank,Mr. Peter Noni.

  0 0

  Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa bwana Kharist Michael Luanda akitangaza idadi ya watanzania waliojiandikisha kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili ijayo.

  Jumla ya Watanzania 11,491,661 sawa na asilimia 62% ya watanzania 18,587,742 ambao walitarajiwa kujiandikisha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili ijayo wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo. 

   Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa mikoa ambayo imeandikisha idadi kubwa ya wapiga kura ni Katavi 79% na Kagera (78%) na mikoa ambayo iliandikisha idadi ndogo ya wapiga kura ni Dar es salaam 43% na Kilimanjaro 50% .


  0 0

  Flaviana Matata Mwanamitindo wa kitanzania afanyae shughuli zake za Mitindo Nchini Marekani, Jana alijiunga na rafiki, mshauri, mwekezaji na hip- hop legend , Russell Simmons na kuitambulisha rasmi Flaviana Matata Foundation 'FMF' nchini Marekani katika hafla fupi ilofanyika jijini New York City kwenye mgahawa wa Beautique. 
   Nia ikiwa ni kusaidia suala la FMF katika - kuhamasisha , kuwawezesha na kuwasaidia watoto wa Tanzania katika masomo yao - wageni walioudhulia waliburudishwa na cocktail; wengi wakiwa ni models Wilhelmina Models. 
  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo7_400
   Kwa habari zaidi juu Flaviana Matata Foundation na jinsi ya kuchangia , bonyeza hapa.   #unamfuatilia Flaviana MatataInstagram: @FlavianaMatataFoundation Twitter: @FMFound flavianamatatafoundation.orgtumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo1_1280  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo2_400  tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo3_400      tumblr_ngdxj7AcPp1swsaplo5_400       

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa mikoa waliowawakilisha wenzao kwenda ikulu leo kumjulia hali na kumpa pole kufuatia upasuaji alifanyiwa mwezi uliopita nchini Marekani.Picha na Freddy Maro

  0 0

  Kaimu Mgukurugeni wa Uhuru FM, Angela Akilimali (katikati) akiwa na wahitimu wenzake wa Shahada ya Mawasiliano ya uma ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali yaliyofanyika hivi katibuni mkoani Kibaha mkoani Pwani.  Kushoto ni Hemed Mbaraka na Mganwa Nzota.
   Wanahabari wa morogoro nao walikula nondo zao katika mahafali hayo.
   Angela Akilimali akiwa na mumewe Hassan Hemedi Chamshama baada ya kumkabidhi shada la maua wakati akimpongeza.
   Toka kushoto ni Idda Mushi wa ITV/Redio One - Morogoro, Angela Akilimali wa Uhuru FM na Hana Mayige  wa TBC wakipozi kwa picha wenye furaha baada ya kula nondo zao. PICHA ZAIDI BOFYA>>>>KIDEVU BLOG.

  0 0

  Afisa mdhamini shirika la biashara la taifa Zanzibar ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi(kuli), akiwa na mkulima wa zao la karafuu Khatib Suleiman Amour, ambae anadaiwa kuchanganya karafuu na makonyo na kugundulika na watendaji wa ZSTC Finya wilaya ya Micheweni.
  MPIMAJI karafuu wa kituo cha mauzo ya zao hilo, Wete Pemba Kitwana Salim Kitwana, akipima karafuu hizo, kama alivyokutwa na mpiga picha wetu kituoni hapo.
  WANANCHI waliokodi shamba la mikarafuu la serikali eneo la Makuwe wilaya ya Micheweni Pemba, ambao kwa sasa wamekosa majamvi maalumu ya kuanikia na kusababisha kuanika kwenye maturubali ya plasitiki, ambayo husababisha kupoteza ubora wake. 
  OFISA MDHAMINI ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi akikagua karafuu za wananchi waliokodi shamba la mikarafuu la serikali, ambapo wananchi hao kwa sasa wanahitaji kupatiwa majamvi ya kuanika ili kuepusha karafuu zao kuharibika.(picha na Haji Nassor, Pemba).

  0 0

  Mheshimiwa Dkt Pindi Chana (Mb.), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Tarehe 10-12/12/2014 alifanya ziara ya kikazi ya chama Mkoani Njombe kwa kushiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

  Katika ziara hiyo pamoja na shughuli nyingine Mhe. Mbunge aliwanadi wagombea uongozi kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji vya Mkoa wa Njombe. Kupitia mikutano hiyo ya kampeni wagombea walipata fursa ya kueleza sera na ahadi zao kwa wananchi, endapo watawapa ridhaa ya kuwaongoza.
  Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Serikali ya Kijiji cha Mbugani – Ludewa, Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mbugani, Wilayani Ludewa.
  Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Mtaa wa Kihesya - Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika Njombe Mjini.
  Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Serikali ya Kijiji cha Mavanga – Ludewa, Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mavanga, Wilayani Ludewa.
  Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Mtaa wa Kwivaha - Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika Njombe Mjini.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mqwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Nchini Tanzania Dr.Jama Gulaid alipofika Ikulu Mjini Unguja akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
  Rais wa Zanzibar na Mqwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa UNICEF Nchini Tanzania Dr.Jama Gulaid alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Na Bashir Nkoromo 
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa. 
   Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300. 
   Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi. 
   Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009. 
   "Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia 96, sasa kutokana na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka kabisa kwamba wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja", alisema Nape. 
   Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi. "Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema Nape. 
   Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura. 
   "Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi fujo na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa napigilia msumari tu". 
  Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri. 
   Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga. Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi. 
   Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu Tambaza
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioni
  Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
  Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
  Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo
  Lwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili Nape kwe ye mkutano huo. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa Wanajeshi katika  uboreshaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kupiga kura.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tume inasema kutakuwepo na wanajeshi 6 wa Jeshi la Wananchi katika kila kituo ambao kazi yao ni kusaidia shughuli za lojistiki kama vile kuhamisha vifaa kutoka kata moja kwenda nyingine.

  Pia wanajeshi hao watasaidia katika shughuli za kufanya matengenezo madogo madogo ya vifaa yanayoweza kujitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.

  Taarifa inasisitiza kuwa Wanajeshi hao hawatakuwepo kwenye vituo vya uboreshaji wala hawatahusika na zoezi la uandikishaji kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoiti hivi karibuni.

  Aidha katika mkutano na Vyama vya Siasa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ulifafanua kuwa watendaji watakaohusika katika zoezi hilo ni maafisa waandikishaji na wasaidizi wao, waandishi wasaidizi, wataalamu wa fani ya TEHAMA na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  0 0

  Mama wa Mitindo Asya Idarous wa Khamsin akipongezwa na wadau kwa kupokea tuzo  ya LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD katika kiota cha MOG Bar (Zamani Nyumbani Lounge) jijini Dar es salaam 
   Mama wa Mitindo Asya Idarous wa Khamsin akipokea tuzo yake ya LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
   Mama wa Mitindo Asya Idarous wa Khamsin akitoa neno la shukrani kwa Mwenyezi Mungu baada ya kupokea tuzo yake ya LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
    Mama wa Mitindo Asya Idarous wa Khamsin akiwa haamini macho yake baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa tuzo yake ya LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
   Mamodo mbalimbali wakiwa katika mavazi ya Khanga ya
   Fabak Fashions ya Asya Idarous-Khamsin.

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akimkabidhi Mkataba wa Makubaliano ya mradi uchimbaji madini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges. Shirika la Magereza limeingia ubia katika mradi huo na Kampuni ya Twiga Cement katika eneo la Jeshi la Magereza, Wazo Hill lililopo jijini Dar es Salaam ambapo hafla hiyo imefanyika leo Desemba 12, 2014 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
    Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges(hayupo pichani) kabla ya makabidhiano rasmi ya Mkataba wa Makubaliano ya mradi wa ubia wa uchimbaji madini ya chokaa. Shirika la Magereza limeingia ubia katika mradi huo na Kampuni ya Twiga Cement katika eneo la Jeshi la Magereza, Wazo Hill lililopo jijini Dar es Salaam ambapo hafla hiyo imefanyika leo Desemba 12, 2014 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges(kushoto) akifuatilia majadiliano kabla ya makabidhiano rasmi ya Mkataba wa Makubaliano ya mradi wa ubia wa uchimbaji madini ya chokaa.Shirika la Magereza limeingia ubia katika mradi huo na Kampuni ya Twiga Cement katika eneo la Jeshi la Magereza, Wazo Hill lililopo jijini Dar es Salaam(kulia) ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Twiga Cement.
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohuhuria hafla hiyo ya makabidhiano rasmi ya Mkataba wa Makubaliano ya mradi wa ubia wa uchimbaji madini ya chokaa(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga(wa kwanza kushoto) ni Afisa Ugavi Mkuu wa Shirika la Magereza,  Mrakibu wa Magereza, George Wambura.
  Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

  0 0

  Mkuu wa dawati la uangalizi wa chaguzi na bunge LHRC KHAMIS MKINDI akizungumza na wnahabari juu ya mfumo huo ambao watautumia katika uchaguzi huo unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki huu siku ya jumapili

  Na Exaud mtei

  Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya mwisho wa wiki hii,kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC leo kimetangaza kufanya uangalizi wa uchaguzi huo kwa njia ya TEHEMA yaani ICT-election monitoring katika mikoa yote nchini Tanzania baada ya kufanya hivyo kwa mafanikio makubwa mwaka 2009.
  Akizungumza na wanahabari muda huu makao makuu ya LHRC mkuu wa dawati la uangalizi wa changuzi na bunge bwana KHAMIS MKINDI amesema kuwa kituo chao kimesambaza waangalizi nchi nzima katika mikoa 25 na wilaya 165 za Tanzania bara na visiwani ambapo hadi kufikia sasa wawakilishi wao wapo kila kona ya Tanzania kwa uangalizi wa hatua kwa hatua ya uchaguzi huo,ambapo amesema kuwa uchangalizi huo umeanza kipindi cha kampeni na utaendelea kipindi cha uchaguzi na baadae baada ya uchaguzi.
  Wataalam mbalimbali wakiwa tayari kufanya uangalizi wa uchaguzi huo 
  Aidha pamoja na wawakilishi hao katika mikoa na sehemu mbali mbali nchini kituo hicho kimeweka timu maalum ndani ya makao makuu ya LHRC ambapo ndio taarifa zote za uchaguzi zitafikia na kupokelewa na wataalam mbalimbnali waliobobea katika Nyanja mbalimbali.

  Amesema kuwa pia wako na kitengo maalum cha kupokea taarifa kupitia mitandao yote ya kijamii ikiwemo facebook ambapo account yao ni www.facebook/chaguzitanzania pamoja na mitandao yoote ya kijamii kama twitter ambapo ni @chaguzitanzania pamoja na namba ya simu ya 0684472896ambayo mtu yoyote anawezakutuma taarifa mbalimbali kuhusu matuio ya chaguzi katika maeneo yao.
  Huu ndio mfumo utakao kuwa unatumika kuleta taarifa zoote za uchaguzi huo wa serikai za mitaa ambapo taarifa zote zitakazoripotiwa zitaonekana hapa
  Pamoja na hayo amesema kuwa kituo cha sheria LHRC ni commanding center ambapo lengo lao ni kupokea taarifa za uchaguzi na kuzifikisha katika mamlaka husika kwa lengo la kuzifwatilia

  0 0

  The Guest of Honour; the Deputy Minister for Finance Hon. Adam Malima (MP) presenting the award of the Best Presented Financial Statements under the category of Regulators applying IPSAS to the Social Security Regulatory Authority, Director General Mrs. Irene Isaka .
  The Guest of Honour; the Deputy Minister for Finance Hon. Adam Malima (MP) congratulating SSRA for emerging the 1st Winner of the Best Presented Financial Statements under the category of Regulators applying IPSAS. 2nd left is the Chairman of the Board NBAA Prof. Isaya Jairo and the 3rd right is the Accountant General Madam Mwanaidi Mtanda, the rest are members of staff of SSRA.
  Director General Mrs. Irene Isaka posing with her members of Staff; Mohamed Nyasama Director of Finance Planning and Administration, and staff of the directorate of Finance.
  Proudly with his team Director of Finance, Planning and Administration Mr. Mohamed Nyasama (Centre). From left Athumani Halfani; Latifa Mazengo; Athumani Juma and Naiserian Mainoya after receiving the award in Arusha.

older | 1 | .... | 669 | 670 | (Page 671) | 672 | 673 | .... | 3272 | newer