Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live

Viongozi wa Dini Mbalimbali wamuombea dua Rais Kikwete leo Ikulu, Dar es salaam

0
0
 Viongozi wa Dini wakimuombea dua Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati walipomtembelea kumjulia hali na kumuombea jioni hii Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali waliomtembelea na kumjulia hali pamoja na kumuombea dua ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali waliomtembelea na kumjulia hali pamoja na kumuombea dua ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Freddy Maro

TABORA WAZINDUA KAMPENI YA NYOTA YA KIJANI KANDA YA MAGHARIBI

0
0
Baadhi ya wananchi wa wadau wa Afya wakifanya maandamano wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya NYOTA YA KIJANI uliofanyika eneo la kumbukumbu ya Mwl.Nyerere Tabora mjini.
Mmoja kati ya maafisa kutoka Wizara ya Afya Bi.Isabela Nyalusi akisoma taarifa fupi ya hali ya matumizi ya Uzazi wa Mpango kwa kanda ya Magharibi ambapo inaonesha kuwa mikoa ya kanda ya magharibi ina kiwango kidogo cha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa asilimia 19 ikilinganishwa na mikoa ya kanda ya kaskazini yenye asilimia 50.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Dr.Fikiri Martine akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ambapo alieleza kuwa matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango yameanza kupanda katika siku za hivi karibuni licha ya kuwa bado jamii imekuwa ikikabiliwa na dhana potofu juu ya mpango huo.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya akizungumza katika uzinduzi huo amewataka wananchi mkoani Tabora kuzitumia njia za uzazi wa mpango kwakuwa ni njia salama na zinazoweza kusaidia kupanga maisha katka mpangilio mzuri.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Suleiman Kumchaya akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kampeni ya Nyota ya kijani zoezi lililofanyika chini ya sanamu ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere mjini Tabora.







Maalim Hassan yahya Hussein afurahia kurudi kundini CCM

0
0
Maalim Hassan Yahya Hussein amerudi rasmi kundini CCM baada ya kuwa nje ya chama kwa takriban miaka 20 hivi na ushee.
Maalim Hassan alijitosa katika safari yake ya kisiasa kwa kujiunga na CHADEMA ambapo katika  kipindi hicho aliwahi kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya chama hicho na pia udiwani kwa kupitia chama hicho hicho - lakini mara zote kura hazikutosha.
Juzi alipokekelewa kwa shangwe na wanachama wa CCM  katika kata ya Mzimuni, Magomeni, katika mkutano wa kuwanadi wagombea wa serikali za mitaa wakiongozwa na mwenyekiti wa kata ya Magomeni Ndg.  Hassan Dalali na diwani wa kata hiyo Ndg.  Chambuso.
Katika hotuba yake ya shukrani Maalim Hassan amewahakikishia  wanachama wa CCM kwamba atatumia uzoefu wake aliopata kwa wapinzani kukiimarisha chama kuelekea ushindi katika serikali za mitaa, udiwani,  ubunge na hadi urais.
"Upinzani hakuna dili na habari ya sasa ni CCM asikwambie mtu", Maalim Hassan aliiambia Globu ya Jamii, baada ya kukaribishwa tena kule alikokuita kundini baada ya kupotea maboya.
Maalim Hassan Yahaya Hussein akimwaga sera katika mkutano wa kumkaribisha kundini uliofanyika katika viwanja vya Mtambani Magomeni jijini Dar es salaam. Kulia ni mwenyekiti wa kata ya Magomeni Ndg. Hassan Dalali
Maalim Hassan Yahya Hussein akilakiwa kwa furaha baada ya kurudi kundini CCM
Maalim Hassan yahya Hussein akiwa katika  mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM  mtaa wa Mwinyimkuu.
Picha na Sultani Kipingo

RAIS KIKWETE ALIPOTUNUKU NISHANI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM. MUUZA CHIPSI AWEKA HISTORIA KWA KUTUNUKIWA NISHANI YA USHUPAVU

0
0
 "Hongera kwa ushupavu uliouonyesha...", Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaonekana kumwambia kijana Kassim Saidi Kassim wakati wa kupiga picha ya pamoja, baada ya kumtunuku Nishani ya Ushupavu Ikulu jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumanne, Desemba 9, 2014 ametunuku Nishani ya Ushupavu kwa mfanyabiashara ya kukaanga na kuuza viazi (chips) wa Dare s Salaam , Bwana Kassim Saidi Kassim, kwa kitendo chake cha kuokoa wananchi dhidi ya jambazi. 
Bwana Kassim Saidi Kassim alikuwa mmoja wa watunukiwa 28 wa nishani mbali mbali ambazo Rais Kikwete alitunuku ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 53 ya Uhuru. Katika sherehe ya kutunuku nishani iliyofanyika kwenye Bustani za Ikulu
Rais Kikwete alieleza kuwa amemtunuku Bwana Kassim Nishani hiyo kwa sababu ya kitendo cha ushupavu alichokionyesha cha kujitoa mhanga kukabiliana na jambazi mwenye silaha ambaye angeleta madhara makubwa. 
Katika maelezo yaliyosomwa kabla ya Rais Kikwete kumtunuku Nishani hiyo, ilielezwa kuwa mnamo Julai 7, mwaka jana, 2013, majira ya saa 3:15 usiku, Bwana Kassim akiwa katika eneo lake la biashara, alitokea jambazi akiwa na silaha aina ya bastola na kuanza kuwashambulia wateja kwa kuwapiga makofi na kuwapora mali zao na fedha zao.
 Iliendeleza kuelezwa: “Kwa ushupavu mkubwa ulichukua chepe na kumpiga jambazi huyo mara mbili kichwani, kipigo kilichosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Kitendo hicho kilifanikisha kukamatwa kwa bastola aina ya Glock ambayo nambari zake zilikuwa zimefutwa ikiwa na risasi tano ndani yake na hivyo kuepusha madhara ambayo yangeweza kusababishwa na matumizi mabaya ya silaha hiyo.” 
Bwana Kassim anakuwa muuza chips wa kwanza katika historia ya Tanzania kutunukiwa Nishani ya Ushapavu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Bwana Kassim mwenye umri wa miaka 28 alizaliwa katika Kijiji cha Namwinyu, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma mwaka 1986. 
Alisoma na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2002 katika Shule ya Msingi ya Ilala, iliyoko Wilaya ya Ilala, Dar Es Salaam. 
Baada ya kumaliza elimu ya msingi, alianza kujishughulisha na biashara ya kukaaga na kuuza viazi (chips) katika eneo la Buguruni Malapa. 
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 10 Desemba,2014
 Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Pius Chipanda Msekwa baada ya kumtunuku Nishani.
 Rais Jakaya Kikwete akimvisha Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili Samuel John Sitta. 
 Rais Jakaya Kikwete akimvisha Nishani ya Ushupavu Kassim Said Kassim ambaye ni muuza Chips katika maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, Kassim alitunukiwa Nishani hiyo baada ya kupambana na jambazi aliyevamina na kupora wateja katika eneo la biashara yake na kumpiga chepe na kusababisha kupatikana kwa bastola moja pamoja na risasi tano.
 IGP mstaafu, Phillemon Mgaya akipata Nishani na Tuzo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Ethiopian Airlines Flies Zuriel to Documentary Releases in Africa and Europe

0
0
Zuriel Oduwole on ARISE TV UK December 2014

Mshindi wa Big Brother Africa 2014,idris sultan awasili nchini

0
0
Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa 2014,Idris Sultan akishangilia wakati alilakiwa na Washabiki wake waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere,Jijini Dar es salaam leo akitokea nchini Afrika Kusini yalikokuwa yakifanyika mashindano hayo.Kushoto kwake ni Laveda aliekuwa mshiriki mweza wa Idris.
Idris akionekana ni mwenye furaha kubwa sana baada ya kuwasili nchini.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kati) akijadiliana jambo na Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan pamoja na aliekuwa mshiriki wa shindano hilo,Laveda katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mama Mzazi wa Idris Sultan akijiandaa kumpokea mwanae.
Mshindi wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan akiongea na waandishi wa habari.

KONGAMANO LA SIKU TATU ZA MATUMAINI

UTT-AMIS YATOA WITO KWA WATANZANIA KUJITOKEZA KATIKA MASUALA YA UWEKEZAJI

0
0
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza katika masuala ya uwekezaji kwani fursa hiyo wanayo kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutoka nje. Hayo yalisemwa na Ofisa Habari Idara ya Masoko, Waziri Ramadhani, wakati wa maonesho ya kuadhimisha miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema hivyo kutokana na baadhi ya watu hapa nchini kudhani kuwa ili mtu awe muwekezaji ni lazima atoke nje ya nchi wakati sio kweli. “Nawaomba Watanzania wenzangu watambue kuwa wao pia ni sehemu ya wawekezaji hivyo basi wasijitenge wanaposikia fursa kama hizi na baadala yake wajitokeze, waje wawekeze katika mfuko huu wa UTT,” alisema Ramadhani.
Alisema mfuko huo baada ya kuyabaini hayo umeamua kufikisha elimu katika jamii kwa kutumia njia mbalimbali, ambayo anaamini itawajengea uwezo wa uwelewa kuhusu jinsi ya kuwekeza. Ramadhan, alisema Mfuko wa Umoja ulianzishwa mwaka 2005, ni mfuko unaolenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji huku ukitoa faida.
Alizitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni uwekezajiulio wazi kwa kila mtanzania; vipande vinauzwa kwa bei ya soko (hakuna ada ya kujiunga). Nyingine ni mwekezaji anaweza kununua vipande kumi, kuna urahisi wa kujiunga na kujitoa wakati wowote pindi mwekezaji anapotaka kufanya hivyo.
Hata hivyo ofisa huyo, alitoa rai kwa Watanzania kuwa ili kujua mengi zaidi kuhusu mfuko huo wanaweza kufika katika ofisi zao kila mahali zilipo.
 Ofisa Mafunzo na Masoko wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhani akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliofika katika banda lao wakati wa Maonyesho ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi zake kwa lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Kulia ni Ofisa Uendeshajiu wa UTT-AMIS, Justine Joseph.
  Ofisa Mafunzo na Masoko wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhani akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliofika katika banda lao wakati wa Maonyesho ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha Taasisi zake kwa lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 4. Kulia ni Ofisa Uendeshajiu wa UTT-AMIS, Justine Joseph na kushoto ni Ofisa Masoko, Pauline Kasilati.
 Baadhi ya watu waliohudhuria maonyesho hayo wakisikiliza hotuba kutoka kwa mgeni rasmi wakati wa kufungwa kwa maonyesho hayo.
Maofisa wa UTT-AMIS wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonyesho hayo kutoka kushoto ni Ofisa Masoko wa UTT-AMIS, Pauline Kasilati, Ofisa Uendeshaji,  Justine Joseph na Ofisa Masoko, Waziri Ramadhani.

TPDC YACHANGIA UJENZI WA MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA MTWARA VIJIJINI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Ndg, Wilman Ndile akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPDC, Bi. Venosa Ngowi wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya. TPDC imechangia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Mtwara vijijini. 

Makamu wa Rais wa JICA amtembelea Waziri wa Ujenzi Ofisi kwake Jijini Dar es Salaam

0
0
 Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan JICA, Kato Hiroshi  akimueleza jambo Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Sekta ya Ujenzi wa barabara nchini wakati alipomtembelea Ofisini kwake  jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa JICA Kato Hiroshi.

 Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge ( wapili kulia), akimuuliza  swali  Makamu wa Rais wa JICA Kato Hiroshi  (wa kwanza kushoto) kuhusu miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika  hilo la Maendeleo.

 Baadhi ya wajumbe  kutoka  JICA wakiangalia baadhi ya picha za matukio mbalimbali katika Wizara ya Ujenzi kabla ya mkutano wao na Waziri wa Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa JICA, Kato Hiroshi  mara baada ya kumaliza mkutano wao uliofanyika Wizara ya Ujenzi.



PICHA ZOTE KWA HISANI YA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI.

KUMBUKUMBU

0
0

MARY NICEPHORY  MSUYA

10-12-2013 –  10 – 12 -2014.

NI MWAKA MMOJA SASA TANGU MUNGU AKUCHUKUE GHAFLA BILA MATEGEMEO  YETU,TULIKUPENDA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI,UNAKUMBUKWA NA MUME WAKO NICEPHORY SUDI MSUYA, WATOTO WAKO,  WAJUKUU, WAKWE ZAKO, NDUGU ZAKO, JAMAA , WANAJUMUIYA NA MARAFIKI WOTE, TUNAZIDI KUENZI UPENDO ULITUACHIA,



BWANA ALITOA ,BWANA ALITWAA , JINA LAKE LIHIMIDIWE.

MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA COLLEGE NA SCHOOL ZA UDSM YAPAMBA MOTO

0
0

Wachezaji wa timu ya COSS (College of Social Science) ya chuo kikuu cha Dar es salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kujiandaa kucheza mechi. Kikosi hiki ndicho kinachoongoza kundi B la wanaoshindana chuoni hapo.


*       SJMC (School of Journalism & Mass communication)  wanaongoza kilele cha group A
*       COSS (College of Social Science)  wanaongoza kilele cha group B
*       Mechi zingine nne kuendelea leo hadi Jumamosi



Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yanayojulikana kama Airtel UNI255 yanayoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo chuoni hapo yameendelea kwa  kasi ikiwa leo yameingia siku ya tatu toka kuanza kwake huku baadhi ya washiriki wakijichukulia ushindi na kuongozo msimamo wa mchezo huo na wengine kuendelea kusuasua.

Akiongea kuhusiana na mwenendo wa mashindano hayo kwa sasa Waziri wa michezo wa jumuiya ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema "Mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na wadhamini wetu Airtel kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja yameongeza hari sana kwa washiriki wote


Hadi sasa kinara wa kundi A ambao mechi zao zinachezwa pale katika viwanja vya ndani chuo kikuu cha Dar es salaa ni SJMC (School of Journalism and Mass Communication) alicheza mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea pointi 6 na huku akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.

Kundi B ambao mechi zao zinazochezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama Mabibo Hostel linaongozwa na COSS (College of Social Science) ambapo imecheza mechi 3 ikashinda moja na kutoa sare ya bila kungana mechi 2. Kwa matokeo hayo wanapointi 5 na goli 2.

Mashindano haya ya Airtel UNI255 yanaendelea tena leo na yatafikia tamati siku ya jumamosi kwa fainali itakayokutanisha mshindi wa kundi A na kundi B na baadae Airtel imeandaa tamasha maalum la vipaji maalum kwa wanafunzi wa  chuo hicho litakalofuatiwa burudani kali toka kwa wasanii maarufu wa kizazi kipya nchini akiwemo shilole, Ney wa Mitego, Roma na wengineo. Aidha katika kilele cha tamasha hilo Airtel itazindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa gharama nafuu.

KATIBU WA CCM MKOANI IRINGA AWAONYA WANAVYUO KUJIHUSISHA NA MASWALA YA SIASA

0
0
katibu wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa, HASSANI MTENGA akiwahutubia wananchi wa mataa wa semtema mjini iringa
 wananchi wa mtaa wa semtema wakimsikiliza katibu wa  ccm mkoa HASSAN MTENGA
 hapa wakiwa makini wakisikiliza maneno matamu wakati wa mkutano huo

Na Fredy Mgunda, Iringa.
 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa semtema  mkoani Iringa.

Akiwahutubia mamia ya wananchi wa mtaa wa semtema MTENGA aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi katika uchaguzi utakao fanyika tarehe 14/12/2014.

MTENGA alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo yanaanzi chini ndio yanaenda juu,hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na kumchagua kiongozi anayefaa.

 aidha MTENGA aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa kuacha kuiga siasa chafu ambazo waiga kutoka kwa wapinzani wao kwa kuwa wanaiga kitu ambacho hawakijua ambacho kitawaletea madhara baadae.

Alisema kuwa IRINGA ni ya watu wa iringa hivyo kuwaambia wanafunzi wa vyuo vyote mkoani iringa kuwaachia siasa wana iringa na wao waendelee na walicho kifuata hapa na sio isasa.

kwa upande wake wanafunzi waliohudhuria mkutano huo walimsifu katibu huyo wa chama cha mapinduzi kwa kuwa na sera zinazotekeleza na kuwaambia ukweli vijana waliopo vyuoni kwqa kuwa wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga mambo mengi bila kujua nini kipo mbele yao.
lakini wananchi waliojitokeza eneo hilo walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya muarobaini kwa maneno aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi huyo kuwa ni kiongozi ayefaa kuigwa hapa mkoani iringa.


 pia kunabaadhi ya wananchi walisikika wakisema kwa sera za katibu MTENGA mbunge wa jimbo la iringa mjini atake asitake ataondoka tu na kumwomba aanze kukusanya kilicho chake. 

MIUNDOMBINU YA BANDARI YA KIGOMA KUBORESHWA NA KUPANULIWA

0
0
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Serikali imeazimia kuendelea kuboresha miundombinu ya bandari hususan miradi iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa ikiwemo kuanza kufanya upanuzi wa Bandari ya Kigoma  na kuendelea kuboresha miundombinu na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena katika Bandari ya Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku katika bandari hiyo.
Ahadi hiyo imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Bandari ya Kigoma.
Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Bandari nchini nchini ipo kwenye mkakati wa kuiendeleza bandari hiyo ili iwe ya kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa bandari hiyo.
“Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka huu wa fedha ilipanga kuiendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini na anga ili kuongeza ufanisi wa sekta hizi, ambapo Bandari ya Kigoma ni mojawapo ya bandari zilizopewa kipaumbele kwa ajili ya uendelezaji,” alisema Bibi Mwanri.
Kwa mujibu wa Bibi Mwanri, upanuzi wa bandari hiyo upo kwenye hatua za upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuboresha bandari ya Kigoma na kutwaa maeneo zaidi kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya Bandari hiyo, Mkuu wa Bandari hiyo Bw. Athuman Malibamba alisema kuwa mpaka kufikia Juni 2014 hatua ya utekelezaji iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya uthamini wa mali eneo la Kibirizi lenye hekta 10 kwa ajili ya upanuzi wa bandari hiyo. “Pia, Mamlaka imempata Mtaalam Mshauri (M/S Royal Haskoning H.D.V Nederland, B.V) atakaefanya kazi ya Upembuzi Yakinifu. Aidha, kazi ya uthamini wa mali imekamilika kwa eneo la Katosho lenye hekta 69 kwa ajili ya kujenga bandari kavu,” alisema.
Kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika nchi za jirani kunatoa fursa ya kuimarisha miundombinu ya bandari ya Kigoma ili kuwa na uwezo wa kuhudumia shehena inayoongezeka na kukuza uchumi katika mkoa na Taifa kwa ujumla. Aidha kuanzishwa kwa Eneo Maalum la Kiuchumi, katika mkoa wa Kigoma ni kichocheo muhimu kwa Mamlaka ya Bandari (TPA) kuimarisha huduma katika bandari ya Kigoma na hivyo kuweza kuzitumia fursa zitakazojitokeza mara baada ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kuanzishwa. 
 Sehemu ya chelezo zinazotumika kwa ajili ya matengenezo ya meli na boti katika Bandari ya Kigoma.
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Katikati mbele) akifafanua jambo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara walipofika kujionea shughuli za maendeleo kiwanjani hapo.
 Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni (Wapili kushoto) akiuliza jambo kwa Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Athuman Malibamba (Wapili kulia) walipofanya ziara bandarini hapo.

KATIBU MKUU UVCCM KUAANZA ZIARA YA SIKU 14 KANDA YA ZIWA

0
0
Katibu Mkuu wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ndugu Sixtus Mapunda anategemea kufanya ziara ya siku kumi na nne (14) katika mikoa minne ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera kuanzia kesho tarehe 12 Dec 2014.

Ziara hii ya kikazi ya Katibu Mkuu inalenga kukagua na kuhimiza ujenzi na uimara wa jumuia ya Vijana katika maeneo husika lakini pia kushiriki kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 14th Dec 2014.

Pia, Katibu Mkuu anatarajia kufanya mikutano ya ndani na viongozi wa Jumuiya na Chama, pia kufanya mikutano ya hadhara inayolenga kuingiza wanachama wapya ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla.

Kuhimiza wanachama wa chama cha mapinduzi na viongozi kuwaandaa wananchi katika kuipigia kura katiba mpya iliyopendekezwa wakati ukifika.

Ziara hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kumalizika tarehe 25th Dec 2014.

MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA KUFANIYIKA JIJINI DAR DESEMBA 31,2014

0
0
 Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi  ya Mkesha Mkubwa wa kuliombea Kitaifa ,Askofu Godfrey Emmanuel Malassy (wa Nne  kutoka kulia) akiongea  na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkesha huo utakaofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Desemba 31,2014.Dhima ya mkesha wa mwaka huu ni kumshukuru Mungu kwa awamu 4 ya uongozi wa Taifa letu na kuliombea Taifa katika kipindi chote cha mchakato wa uchanguzi mkuu wa mwaka 2015.Kutoka kulia ni Askofu Nickson Kallinga, Mchungaji Derrick Luhende, Askofu William Mwamalanga, Makamu Mwenyekiti wa mkesha huo, Askofu Keneth Dismas, Mchungaji Debora Mallasy (Mjumbe), Mama Mchungaji Olivia Mallongo (Mjumbe) na Debora Elisha (Mjumbe) 

 Mchungaji  Olivia Mallongo  Akizungumza jambo na wandishi wahabari(hawapo pichani) kuhusu Maandalizi ya mkesha utakaoo fanyika uwanja wa taifa Desemba 31, 2014
Baadhi ya wandishi wa habari wakifatilia na kuchukuwa habari

MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI YAFANYIKA MKOANI DODOMA

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime akiongea jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake na watoto yaliyofanyika Bwalo la polisi Dodoma.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Amina Mfafaki akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea wakati wa kufunga maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili kwa wanawake na watoto katika ukumbi wa Bwalo la polisi Dodoma.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TAPSEA YATANGAZA VIONGOZI WAKE WAPYA

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Songambele (kulia), akionesha katiba ya chama hicho wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kupata viongozi wapya na mambo mengine. Kushoto ni Katibu wa TAPSEA, Festo Melkiory.
 Makamu Mwenyekiti wa TAPSEA, Janejelly James (kulia), akizungumza katika mkutano huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

UTT-PID YATOA HATI YA VIWANJWA KWA WATEJA WAKE

0
0
NA  ANDREW CHALE, BAGAMOYO

NAIBU  Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ametoa rai kwa Taasisi za Kiserikali na zisizo za Kiserikali kuona umuhimu wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi katika shughuli za upimaji ardhi ili kuwaepusha na adha zinazoweza kuwapata pale yanapotokea maafa.

Hayo alisema mjini hapa siku Desemba 8, wakati wa ufunguzi wa mradi na ugawaji wa hati kwa wanunuzi wa  Viwanja katika Kijiji cha Mapinga- Bagamoyo ulioratibiwa na Taasisi ya Maendeleo ya Miundombinu chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT -PID).

“Wananchi wapewe elimu ya kutosha katika shughuli za upimaji ardhi na umuhimu wa kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa. Hii itasaidia serikali kutoingia gharama hususani pale yanapotokea maafa kama vile mafuriko nikitolea mfano wa eneo kama Jangwani Jijini Dar es Salaam ambapo serikali imekuwa ikiingia gharama mara kwa mara katika uokoaji wa watu katika eneo hilo kipindi mafuriko yanapotokea,” alisema Nchemba.

Naibu Waziri huyo wa Fedha ambaye aliwakilishwa na  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene alieleza pia kuwa  migogoro ya ardhi nchini ni moja ya matatizo makubwa yanayotokana na watu wengi kununua viwanja au ardhi ambazo hazijapimwa.

Aliipongeza  Taasisi inayoratibu miradi hiyo ya maendeleo ya UTT PID kwa jitihada kubwa inayofanya na kueleza kwamba kupitia mifumo ya kisasa ya upimaji wa maeneo unaofanywa na taasisi hiyo ya serikali ndio utakaokuwa msingi utakaoziwezesha Halmashauri, Miji na Majiji ya nchini kuwa na maendeleo ya kasi kutokana na mipango hiyo ya kisasa.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, miongoni mwa mambo yanayochangia umaskini kwa wananchi ni pamoja na kutopimwa kwa ardhi wanayomiliki na kueleza kuwa inakadiriwa kuwa asilimia 10 tu ya ardhi yote ya nchini ndiyo iliyopimwa huku nchi ikikadiriwa kuwa na zaidi ya kilometa za mraba milioni moja.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UTT PID, Elpina Mlaki alisema katika mradi huo wa Mapinga ambao ni wa awamu ya pili utahusisha uuzaji wa viwanja 246 vilivyo na huduma zote muhimu kama vile maji ya Dawasco mpaka eneo la mradi na ujenzi wa tanki la kutunzia maji ya dharura lenye ujazo wa lita 150,000 , umeme pamoja na huduma nyinginezo.

Alisema kutokana na uhitaji mkubwa wa viwanja katika eneo hilo taasisi hiyo iliyo chini ya serikali inatarajia kuwekeza zaidi katika miundombinu na kuongeza wigo wa viwanja zaidi ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka siku hadi siku kutoka kwa watu mbalimbali katika eneo la Mapinga.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiwahutubia wananchi (Hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo.
Beatrice Ngode akipokea hati ya kumili ardhi kutoka kwa Naibu Waziri Mbene, ambapo alipokea kwa niaba ya Kezia Pallangyo.

FM Academia, Yamoto, Sylight, Mapacha jukwaa moja katika Beach Band Bonanza

0
0
BENDI nne nyota nchini, FM Academia, Yamoto, Mapacha na SkyLight zitatumbuiza katika jukwaa moja kwenye tamasha la Beach band Bonanza lililopangwa kufanyika Desemba 20 kwenye ufukwe wa Azura, Kawe darajani.

Bonanza hilo limeandaliwa na kampuni ya Team Mamba na mbali ya bendi hizo nyota, wasanii wa bongo fleva wakiongozwa na Dully Sykes, CPWAA na Damian Soul ambaye atakuja na bendi yake.

Msemaji wa kampuni ya Team Mamba, Doris Godfrey alisema kuwa bonanza hilo lililodhaminiwa Coca-Cola na bia ya Windhoek, limepangwa kuanza saa 6 mchana mpaka alfajiri.

Doris alisema kuwa wameandaa bonanza hilo kwa ajili ya kuwakutanisha wadau wa muziki na familia zao kwani siku hiyo kutakuwa na michezo ya watoto mchana na baadaye usiku kwa ajili ya wakubwa.

Alisema kuwa pia kutakuwa na michezo ya watoto, kupanda farasi na michezo mingine ambayo ni ya kuvutia. “Hili ni bonanza la kwanza la muziki linalokutanisha bendi nyingi ambazo zitafanya shoo katika jukwaa moja, hivyo tunatarajia kuwa na burudani aina yake kwani bongo fleva nao watakuwepo kwa lengo kutoa burudani safi,” alisema Doris.

Kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Sadaat alisema kuwa wamejiandaa vizuri kutoa burudani katika bonanza hilo la aina yake. “Tuna nyimbo mbalimbali mpya, staili mpya ambazo siku hiyo zitakuwa zinaonyeshwa mara kwanza jukwaani,” alisema Nyoshi.

Kwa upande wake, Dully Sykes alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo na kuwaomba mashabiki wa muziki kufika kwa wingi.
Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo kuhusu Beach Band Bonanza litakalofanyika Desemba 20 katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Ilunga Khalifa (Cpwaa) na Mratibu wa Bonanza hilo, Dorice Godfrey.
Mratibu wa Bonanza la Beach Band, Dorice Godfrey akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo kuhusu Bonanza hilo litakalofanyika Desemba 20 katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.Kulia ni Msanii Dully Sykes na kushoto ni Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat
Viewing all 109610 articles
Browse latest View live




Latest Images