Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

Wameshaezua mabati....!!

$
0
0
Tabia ya baadhi ya watu kuezua mabati kwenye vibanda vya vituo vya daladala katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam imeongezeka kama kibanda hicho cha Kituo cha daladala cha Msimbazi Centre Ilala kinavyoonekana katika picha hii.

kazi na dawa

$
0
0
Mwendesha bodaboda akiwa kauchapa uzingizi mzito juu ya chombo chake maeneo ya Ilala Mchikichini Dar es Salaam.

uchokozi wa Nathan Mpangala leo

TANZANIA TO HOST WIPO AND ECOSOC CONFERENCES ON MARCH 12 TH TO14 TH , 2013

patakuwa hapatoshi tamasha la pasaka

$
0
0

KWAYA ya Kinondoni Revival  (pichani juu) na kundi la Glorious Celebration ni miongoni mwa burudani zitakazokuwepo kwenye Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama jana ilieleza kuwa makundi hayo ya jijini Dar es Salaam tayari yamethibitisha ushiriki wao pamoja na mwimbaji mahiri Upendo Kilahiro ambaye pia atashiriki.



"Niseme mambo yanaenda vizuri na leo (jana) kuna msanii tunamalizana naye kutoka Afrika Kusini, nina imani wakati wowote kuanzia Jumanne (leo) tutamtangaza kwa mashabiki wetu, nia ni kulifanya tamasha liwe zuri zaidi," ilisema taarifa hiyo.

Wasanii wengine wa Tanzania ambao watashiriki tamasha hilo mwaka huu ni Rose Muhando, John Lissu na Upendo Nkone, wakati wa nje ya Tanzania ni Ephraim Sekeleti wa Zambia anayetamba na albamu zake za Acha Kulia na Mungu Mwenyewe. 

Wasani wengine wa nje watakaokuja ni Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, ambapo pia mwaka huu kuna ingizo jipya ambalo ni kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu.
Kundi la Glorious Celebration likiwa kwenye moja ya kazi zake jukwaani.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti, kundi la Glorious Celebration, kwaya ya Kinondoni Revival na Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Airtel yadhamini tuzo za Mwanamakuka 2013

$
0
0
 
Mshindi wa pili wa tuzo za Mwanamakuka bi  Leila Mwambungu  (katikati) akifurahi kwa pamoja  na Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kulia)  wakati wa kukabidhiwa   mfano wa hundi ya shillingi million tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa  tuzo za mwanamakuka . Akishuhudia kushoto ni  Mke wa makamu wa raisi Asha Bilali na wa pili kushoto ni mwenyekiti  wa Unit of women Friends Esther Wakati.i
Mwenyekiti wa Unit of women Friends Esther (kushoto)  akikabidhi Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde cheti cha shukrani kwa Airtel kushiriki na kudhamini tuzo za mwanamakuka kwa mwaka 2013. Akishuhudia ni mtunza fedha Mwate Madinda.
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde(kulia) akikimkabithi mshindi wa pili wa mwanamakuka bi  Leila Mwambungu  mfano wa hundi ya shillingi million tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa  tuzo za mwanamakuka . wakishuhudia  kulia katikati ni mwenyekiti  wa Unit of women Friends Esther Wakati, kushoto ni  msimamizi wa mwanamakuka award Maryam Shamo akifatiwa na Mke wa makamu wa raisi Asha Bilali.
Balozi mstaafu bi Mwanaidi Maajar (katikati) akitoa mkono wa shukrani kwa  Afisa Uhusiano wa Airtel  bi Jane Matinde kuishukuru Airtel Tanzania kwa kudhamini tuzo za Mwanamakuka 2013. Wakishuhudia ni  Mke wa makamu wa raisi Asha Bilali na wa pili kushoto ni mwenyekiti  wa Unit of women Friends Esther Wakati.
Waandaaji na wadhamini wa tuzo za mwanamakuka 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mke wa makamu wa raisi Asha Bilali wakati wa sherehe za tuzo hizo.

NEWS ALERT: FIFA YAICHIMBIA MKWARA SERIKALI YA TANZANIA

$
0
0

Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) limesema litaifungia Tanzania iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

FIFA imesema kumekuwa na shutuma kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari nchini kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeonesha nia ya kuingilia uendeshaji wa TFF.

Kwa mujibu wa barua ya jana (Machi 10 mwaka huu) ya FIFA kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, vyombo vya habari vimemkariri Waziri (Dk. Fenella Mukangara) kuwa Serikali imeiagiza TFF kutumia Katiba ya mwaka 2006 katika uchaguzi wakati tayari imeshafanyiwa marekebisho.

“Pia imeelezwa kuwa TFF imetakiwa kufanya Mkutano Mkuu pamoja na ule wa uchaguzi kwa tarehe ambazo zimepangwa na Serikali. Vilevile imeelezwa kuwa Serikali inakusudia kuunda Kamati ya Muda iwapo TFF haitatekeleza maagizo yake,” imesema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valke.

FIFA imesema iwapo yaliyoripotiwa na vyombo vya habari yatathibitika kuwa kweli, maana yake huo ni uingiliaji wa wazi wa Serikali kwa shughuli za TFF.

“Tunapenda kuwakumbusha kuwa wanachama wote wa FIFA wanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu mwingine kama ilivyoelezwa katika ibara za 13 na 17 za Katiba ya FIFA.

“Hivyo kama maagizo hayo yanayodaiwa kutolewa na Serikali yatatekelezwa, suala hili litapelekwa katika mamlaka za juu za FIFA kwa hatua zaidi ikiwemo kuisimamisha Tanzania kama ambavyo inakuwa pale panapokuwa na uingiliaji wa Serikali,” imesema barua hiyo.

Barua hiyo ambayo nakala yake pia imetumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imeelezea baadhi ya athari ambazo Tanzania itakumbana nazo endapo itasimamishwa ni timu za taifa pamoja na klabu kutoshiriki mechi za kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya FIFA.

Vilevile si TFF au wanachama wake na maofisa wengine watakaoweza kunufaika na programu za maendeleo, kozi au mafunzo yanayotolewa na FIFA na CAF.

“Madai ya uamuzi uliofanywa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni ya kusikitisha kutokana na ukweli kuwa FIFA ilishatangaza itatuma ujumbe wake kuchunguza jinsi hali ilivyo kwa sasa na kutoa mapendekezo yake. Kutokana na hali hii, ujumbe wa FIFA uliokuwa uje kuchunguza (suala la uchaguzi) itabidi usubiri kwa vile ni muhimu kushughulikia tatizo hili kwanza.

“Katika mazingira haya tunaomba ueleze msimamo huu wa FIFA kwa mamlaka zinazohusika (Serikali) na athari ambazo mpira wa miguu wa Tanzania utakumbana nazo. Tunakushuru na tunatarajia utatufahamisha kila hatua inayoendelea katika suala hili,” imesema barua hiyo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

promosheni ya Mahela yaendeshwa na VODACOM eneo la Tabata Mawenz

$
0
0
 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa (kulia)akichezesha droo ya promosheni ya Mahela unayoendeshwa na kampuni hiyo eneo la Tabata Mawenzi,Zaidi ya shilingi Milioni 240 zinaendelea kushindaniwa .
 Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (kulia)akimkabidhi Ramadhani Kibanike mfano wa hundi ya Sh5 milioni nyumbani kweke Tabata Mawenzi mara baada ya kuibuka mshindi   wa promosheni ya Mahela inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Katikati ni mwanaye.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni alipofika Tabata Mawenzi,kumkabidhi Bw.Ramadhani Kibanike(kushoto) alieibuka mshindi wa shilingi Milioni 5 katika  Promosheni ya”MAHELA”inayoendeshwa na kampuni hiyo,mpaka sasa zaidi ya shilingi Milioni 240 zinaendelea kushindaniwa.

mjadala ughaibuni: kushuka elimu Tanzania sehemu ya kwanza

$
0
0
Sehemu ya kwanza ya WanaDMV wafanya mjadala wa kushuka kwa kiwango cha Elimu na matokeoa mabaya ya kidato cha Nne wakianza kuelezea Elimu zamani ilikuwaje na nini kimesabababisha kuporomoka kwa Elimu. Je nani alaumiwe na nini kifanyike kuokoa janga hili WASIKILIZE

KINANA ATUA CHINA NA UJUMBE WAKE LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kulia) akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming (kushoto) baada ya kuwasili leo Machi 11, 2013 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhu, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku kumi nchini China. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai). (Picha na Bashir Nkoromo).

Anatafutwa na ndugu zake

$
0
0

Naomba msaada huyu kijana amepotea 
JINA LAKE: ABDILLAHI SAID AHMED 
ni mgonjwa wa akili na nimgeni wa nchi hii
kwa mawasiliano zaidi: 

Mkutano wa Balozi Mh. Dr Deodorus Kamala na waTanzania waishio Uholanzi - Jumamosi tarehe 16 March 2013

$
0
0
Ndugu waTanzania wenzetu,

Tunayo furaha kuwaalika kuhudhuria mkutano kati ya Balozi wetu mpya (Tanzanian Ambassador to the Kingdom of Belgium, the Kingdom of Netherlands, the Grand Duchy of Luxembourg, the European Union and International Organisations based in the BENELUX region)Mhe. Dr. Deodorus Kamala  na Watanzania waishio Uholanzi.

Mkutano huu umeandaliwa na Ubalozi pamoja na Kamati ya Umoja wa waTanzania hapa Uholanzi (TANE). 

Siku na Muda wa Mkutano:
Jumamosi, 16 Machi, 2013; Kuanzia saa  8.00 Mchana

Mahala:
Institute for Social Studies
Kortenaerkade 12, 2518 AX, Den Haag
Dorus Hall
Zuid-Holland, Nederland.

Karibuni nyote kwa kujali muda uliopangwa.

Wenu,

Kweba Bulemo
Mwenyekiti, TANE

Kny. Kamati ya Utendaji.

 TANBIHI:

Kufika eneo la mkutano, unaweza kutumia Bus namba 22 na 24 (Den Haag Central Station), au Tram namba 1 au 17 (Den Haag HS)

Shuka kituo cha Mauritskade. Ni mwendo wa dakika tatu mpaka ISS Dorus Hall.
Chuo cha ISS kipo opposite na Den Haag Hilton Hotel.

Tanzania yasaini makubaliano ya bilioni 34.8 na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kusaidia mradi wa maji Zanzibar

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini makubaliano na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar. Katikati ni Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero na kulia ni Mtaalam wa Benki hiyo anayeshughulikia masuala ya maji Sabas Marandu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero wakisaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akibadilishana hati na Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero mara baada ya kusaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar.

High Quality ICT Services From Mikono ICT Solutions

POLISI KAGERA WAUA MAJAMBAZI SABA

$
0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kagera.

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua majambazi saba wakati wa mapambano makali ya kurushiana risasi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati majambazi hao walipokuwa katika harakati za kuvamia mgodi wa Tulawaka ambapo baada ya kupekuliwa walikutwa na bunduki mbili za kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kurusha kwa mkono, risasi 156, magazine tano, simu mbili pamoja na fedha za Burundi franc 800.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi Philip Kalagi alisema tukio hilo lilitokea tarehe kumi mwezi huu majira ya saa tatu na nusu usiku katika kijiji cha Mavota wilayani Biharamulo.

Kamanda Kalagi alisema kati ya majambazi hao, watano wanasadikiwa kuwa ni raia wa Burundi na mmoja wao ametambulika kwa jina la Minani Luzamba (46) mkazi wa Rwambarage nchini Burundi.

Aidha alisema raia wawili uraia wao bado unachunguzwa ingawa wamekutwa na vitambulisho vya Tanzania vya kupigia kura vilivyotolewa mkoani Kigoma na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Biharamulo.

Alisema kazi hiyo ilifanikiwa kwa kushirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kuzuia uhalifu pamoja na taarifa za raia wema ambapo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za kuwezesha kukamatwa kwa watu wanaojihusisha na uhalifu mkoani Kagera.

Aidha Kamanda Kalagi alisema Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na msako mkali kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha mkoa huo unakuwa na usalama na wananchi wanafanya kazi zao bila hofu ya uhalifu na wahalifu.

TAARIFA YA MAZIKO YA NDUGU SAID KHALFANI SHEDHANI - SHEFFIELD UINGEREZA

$
0
0

Tuna masikitiko makubwa ya kuwatangazia maziko ya ndugu yetu Said Khalfan Shedhan hayakuweza kufanyika leo siku ya Jumatatu tarehe 11/3/2013 kama ilivyotangazwa awali kutokana na kwamba mwili wa marehemu umechelewa kukabidhiwa kwa wanandugu


Mazishi yanategemewa kufanyika siku ya Jumanne tarehe 12/ 03/ 2013 mara tu baada ya sala ya Adhuhur,  Inshallah.


Msiba huu upo nyumbani kwa marehemu Address ifuatayo:


3 High Street

Sheffield

Yorkshire

S2  5PZ


SALA YA Maiti itasaliwa msikiti wa address:

3 Ellesmere Road

Sheffield

Yorkshire

S2  7JA


Tunaomba uwasiliane na wahusika wafuatao kwa taarifa zaidi za maziko;


Habibu Swalehe  07904604128 UK

AU

Mohamed Said Khalfan Shedhan 07961014224 UK

AU

Ahmed Mashaka 07876232851 UK


"KWA HAKIKA SOTE NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA "

SIMBA KIMENUKA

$
0
0

Baada ya vigogo wake wawili hans Poppe na Kaburu kubwaga manyanga, hali imezidi kuwa tete katika Klabu ya Simba baada ya kocha wa timu hiyo Patrick Liewing kuwa mguu ndani mguu nje kutokana na kutolipwa mishahara yake ya miezi miwili ikiwa ni pamoja na kupokonywa gari alilokuwa akilitumia.

Gari alilokuwa anatumia kocha huyo ya GX110 linashikiliwa na uongozi wa hoteli ya Spice, iliyopo Kariakoo, Dar es Salaam ambao unaidai klabu hiyo kiasi cha Sh. Milioni 28.

Spice ndiyo kambi kuu ya Simba SC mwaka jana, lakini baada ya deni kuwa kubwa, wakahamia katika hoteli ya Sapphire Court, iliyopo Kariakoo pia ambako nako walifukuzwa jana baada ya deni kuwa kubwa. 

Habari zinasema kocha Liewig amekuwa akilalamikia kufanya kazi katika mazingira magumu na hana matumaini ya kutimiza ndoto zake katkka klabu hiyo.

“Nidhamu ya wachezaji ni mbovu, huo ni mtihani mkubwa wa kwanza alionao, bado na matatizo mengine kibao, usimuone vile yule babu, ni mvumilivu sana kwa kweli,”kilisema chanzo chetu kutoka Simba SC.

Tayari benchi la Ufundi la Simba SC nalo limeanza kumeguka, baada ya aliyekuwa Mtunza Vifaa, Kessy Rajab kuandika barua ya kujiuzulu na daktari wa timu hiyo Cosmas Kapinga naye inadaiwa uwenda akaitema timu hiyo.

Jana usiku Basena, kipa Abbel Dhaira na kiungo Mussa Mudde, wote raia wa Uganda, walifukuzwa kwenye hoteli ya Spice, Kariakoo, Dar es Salaam kutokana na klabu hiyo kulimbikiza deni la Sh. Milioni 27.

Pamoja na kufukuzwa kwa Waganda hao usiku huo, uongozi wa Spice Hotel unashikilia magari mawili ya Simba SC, basi dogo na gari la kocha, aina ya GX110 hadi ulipwe fedha zake.

Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala amesaini hati ya kuahidi kulipa deni hilo baada ya mechi ya leo na kuweka hati yake ya kusafiria kama bondi. Bado Menejimenti ya Sapphire inasistiza kulipwa fedha zake, vinginevyo itachukua hatua za kisheria dhidi ya klabu hiyo.   

Hata hivyo jana uongozi wa Simba kupitia kwa ofisa habari wake Ezekile Kamwaga ulitoa tamko na kudai kuwa uongozi wa Simba, umesikitishwa na hatua ya uongozi wa hoteli a Saphire kwani ilikuwa ni ya gafla sana.

"Ifahamike kwamba kabla ya hatua hiyo, uongozi wa Simba ulikuwa umemlipa mmiliki huyo kiasi cha zaidi ya Sh milioni 30 katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.

"Mara baada ya mechi dhidi ya Libolo ya Angola, Saphire walilipwa Sh milioni 15 na Simba. Hii maana yake ni kwamba klabu yetu ina utaratibu wa kulipa madeni yake na si watu wasiolipa kama hatua hiyo ya wamiliki wa Saphire inavyotaka kueleza.

Alisema Uongozi wa Simba tayari ulitoa ahadi ya kumaliza deni lote inalodaiwa baada ya kulipwa fedha zake inazodai zinazotakiwa kulipwa wakati wowote mwezi huu au ujao. Simba inadai zaidi ya Sh milioni 500 kwa wadai wake wawili (Etoile du Sahel ya Tunisia na Push Mobile) na inataraji kulipwa fedha hizo.

"Tutakapolipwa fedha hizo, Simba itakuwa na uwezo wa kulipa madeni yake yote inayodaiwa na watu binafsi na makampuni bado ikabaki na fedha za kufanya mambo mengine ya kimaendeleo.

Alisema Wakati ikisubiri ilipwe fedha zake inazodai, Simba itaendelea kulipa madeni yake taratibu kwa kadri itakavyoweza na kwamba chanzo kikuu cha mapato ya klabu ni fedha za mapato ya milangoni na za udhamini wa bia ya KILIMANJARO ambazo hazikidhi mahitaji yote ya timu.

"Kwa kuzingatia nakisi hii ya mapato na matumizi, Simba SC imeanza mchakato wa kutafuta wafadhili na wadhamini kokote walipo duniani ili kuongeza mapato yake na tayari awasiliano yameanza na wenzetu wa Sunderland ya England kupitia mradi wao wa Invest in Africa ili Simba nayo ifaidike.

"Simba inaomba pia umma ufahamishwe kwamba klabu ya soka kudaiwa si dhambi. Iwapo klabu kubwa na tajiri duniani kama vile Manchenster United, Real Madrid na Liverpool zina madeni, inakuaje madeni ya Wekundu wa Msimbazi (tena ambayo klabu ingeweza kuyalipa yote iwapo wadeni wake nayo wangewalipa kwa wakati) yaonekane kama kitu kigeni?

"Uongozi unaahidi kwamba utalipa madeni yake yote kwa kadri utakavyojaaliwa. Kwenye lugha ya kibenki, credit worthiness ya mteja inamaanisha mteja ambaye anakopa na kulipa. Simba inapenda kusisitiza kwamba ni taasisi ya kuaminika na yenye heshima kubwa na bado inavutia watu na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Simba ni CREDIT WORTHY INSTITUTION !

Hata hivyo, Kamwaga alisema uongozi wa wekundu hao wa Msimbazi unafikiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wamiliki wa Saphire Court Hotel kwa kitendo chake cha kuwazuia wachezaji na viongozi wa Simba hotelini kabla ya mechi ya jana dhidi ya Coast Union ambapo Simba ilitoka kifua mbele kwa kuinyuka Coast mabao 2-1.

xxxxxxxxxxxxxx

Simba inachukulia kitendo kile kama hujuma na kisheria kinaangukia katika kundi la FORCED IMPRISONMENT  kwa wamiliki kuwazuia watu kinguvu hotelini kwao. WAMILIKI hawakutoa notisi kwa uongozi au taarifa yoyote ya mdomo au maandishi kabla ya kuchukua hatua hiyo.

Lengo lilikuwa ni kuchafua heshima na hadhi ya Simba kwa hoteli ambayo imetoka kulipwa Sh. milioni 15 wiki mbili tu zilizopita. Uongozi wa Simba SC unaapa kuilinda na kuitetea hadhi ya klabu yetu kwa nguvu zetu zote, akili zetu zote na maarifa yetu yote.

2. WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI KUFUKUZWA

KUNA taarifa zimeenezwa pia kwamba kuna wachezaji wa Simba wamesimamishwa au kufukuzwa kuchezea Simba. Habari hizi nazo hazina ukweli wowote

Ukweli ni kwamba, uongozi wa Simba umetoa ruksa kwa benchi la ufundi kupanga timu ambayo litaona inafaa kwa mechi husika. Uongozi hautaingilia, kwa namna,njia au aina yoyote ile utendaji wa benchi la ufundi.

Hakuna mchezaji yeyote aliyesimamishwa hadi sasa. Pia uongozi unakanusha taarifa kuwa Daktari Mkuu wa Klabu, Cosmas Alex Kapinga, kuwa naye ameachia ngazi. Habari hizi hazina ukweli kwani daktari huyo ana ruhusa ya kikazi ya wiki mbili inayojulikana

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA WILAYANI NKASI PAMOJA NA SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Kata ya Wampembe kujibu kero zao alipotembelea kata hiyo tarehe 09.03.2013. Moja ya kero kubwa za wananchi wa kata hiyo wapatao alfu kumi na tisa (19,000) ni ukosefu wa huduma muhimu ya mawasiliano ya simu za aina zote, umeme, barabara, na Zahanati katika vijiji viwili vya kata hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiangalia daraja la muda lililoharibika katika kijiji cha Ng'unde Kata ya Wampembe Wilayani Nkasi tarehe 10.03.2013 alipotembelea Kata hiyo kuzungumza na wananchi kujua kero zao. Alimuagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi kwa kushirikiana na wananchi kujenga daraja hilo katika kiwango kinachostahiki.  
Godfrey Mwanansao Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi akitoa maelezo ya ubunifu wa kinyago kinachoonyesha baadhi ya michezo kwa kinamama kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akikagua mabanda ya wadau wa siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa Wilayani Nkasi tarehe 08.03.2013. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Kimanta.
Meneja wa PSI Mkoani Rukwa Issa Ismail akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya juu kazi za shirika hilo Mkoani Rukwa na katika maonyesho hayo. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta, Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ramadhan Juma, Mbunge wa Nkasi Kaskazini CCM Ali Kesi na Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Jakob Mwaruanda.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla akijionea baadhi ya bidhaa zilizokuwa zikionyeshwa na kuuzwa katika mabanda hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wananchi katika viwanja vya sabasaba Mjini Namanyere katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwishoni mwa juma.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi Wilayani Nkasi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyika Wilayani humo kimkoa tarehe 08.03.2013. Aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kujikwamua kiuchumi kwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali na kujiunga kwenye vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo, aliwataka pia kuzingatia uzazi wa mpango katika kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Nkasi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilayani humo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

AFRICAN FILM AND TV TALENTSHINE AT THE INAUGURAL AMVCAs!

Balozi wa Marekani nchini azindua muonekano mpya wa Bidhaa za American Garden jijini Dar

$
0
0
Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt (kushoto) akizindua rasmi muonekano mpya wa Bidhaa za American Garden wakati wa hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Kingsway International Limited, Murtaza Faizal.
Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt (kushoto) na Mwenyekiti wa Kingsway International Limited, Murtaza Faizal wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa Bidhaa za American Grden wakati wa hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt akizungumza na wageni waalikwawakati wa hafla ya muonekano mpya wa Bidhaa za American Garden iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Bidhaa za American Garden iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Kingsway International Limited, Murtaza Faizal.
Wasanii wa Integreted Comunication Limited wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Bidhaa za American Garden iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Kingsway International Limited, Murtaza Faizal.
Balozi wa Marekani, Alfonso Lenhardt akizungumza na waandishi wa habarimara baada ya uzinduzi wa muonekano mpya wa Bidhaa za American Garden iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images