Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MAHAFALI YA 49 YA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA(CBE) KAMPASI YA MBEYA YAFANA.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Musa Uledi akitoa tamko la kuwatunuku vyeti vya Astashahada katika fani za ununuzi na ugavi, uhasibu na uendeshaji wa biashara Wahitimu 37 katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya yaliyofanyika katika viwanya vya Mbeya Hotel.
Wahitimu wakivaa kofia zao baada ya kutunukiwa vyeti na mgeni rasmi katika Mahafali ya 49 ya CBE.
Picha ya pamoja  ya wahitimu na meza kuu.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MOSES IYOBO, RAMA TONSA NA DJ ROMY JONES WAWASILI WASHINGTON, DC, DIAMOND KUWASILI LEO

$
0
0

 Moses Iyobo, Dj Romy Jones wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa mara tu baada ya kuwasili siku ya Ijumaa Desemba 5, 2014 kwa ajili ya sherehe ya Uhuru itakayofanyika leo Jumamosi Sheraton ya Downtown Silver Spring, Maryland. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SHULE YA AWALI YA ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL SASA KUANZA KUTOA ELIMU YA MSINGI MWAKANI, MAHAFALI YAO YAFANA

$
0
0
Wanafunzi ambao ndio wamehitimu shule ya ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo shule ambayo ipo bunju jijini Dar es salaam hapa wakikata keki pamoja na mwalimu wao ishara ya kufurahia mafanikio waliyoyapata pamoja na mafanikio ya shule hiyo tanghu kuanmzishwa kwake
Wahitimu wakiwa katika pozi za kusubiri sherehe ya kuwaaga rasmi kutoka elimu ya awali kuingia elimu ya msingi
Mgeni rasmi wa mahafali hayo mama NEEMA KIBANGA ambaye ni afisa elimu wa kata ya bunju akikabidhi vyeti kwa wahitimu shuleni hapo

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao baada ya kukabidhiwa vyeti vyao. Kwa habari kamili na mapicha kedekede
BOFYA HAPA

Waziri Membe aanzisha Mfuko Maalum kusaidia Wanafunzi Elimu ya Juu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba  wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika katika Viwanja vya Hoteli ya Kiromo iliyopo Bagamoyo. Wahitimu 99 katika fani mbalimbali walitunukiwa shahada zao. Pembeni yake ni Profesa  Costa Mahalu.
Sehemu ya Wahitimu hao wakifuatilia hotuba ya Mhe. Membe (hayupo pichani)
Baadhi ya wahitimu wa fani mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakiwa wamekaa kwa utulivu huku wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa sherehe za mahafali yao. 
Waziri Membe akiwatunuku  Shahada mbalimbali Wahitimu hao kwa niaba ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Askofu Mstaafu, Dkt. Elinaza Sendoro.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

madereva jihadharini na mambo kama haya....hakikisha ume-lock milango

WANAFUNZI 1,044 WALAMBA NONDOZZZ ZAO CHUO KIKUU CHA ARDHI LEO

$
0
0
 Wahitimu wa digrii ya  elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa  digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu "Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania".
 Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika. Picha zaidi BOFYA HAPA

TAIFA STARS MABORESHO YAREJEA DAR

$
0
0
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.

Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya Airways. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.

Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
 MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

JK APIGA TIZI MARA TATU KWA SIKU KUIMARISHA AFYA YAKE

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazoezi leo katika viwanja vya Ikulu kufuatia ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara tatu kwa siku ili kuendelea kuimarisha afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi uliopita katika hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani. 
Picha na Ikulu

COMRADE MWIGULU NCHEMBA AUTEKA MJI WA GEITA

$
0
0
Muonekano wa Umati wa Wananchi waliotulia wakisikiliza hoja za Msingi kutoka kwa Mwigulu Nchemba.
Comrade Mwigulu Nchemba akisisitiza Jambo kwa Wananchi wa Geita Mjini kuhusu Uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Washindi wa Maonesho ya Keki Wapatikana Dar

$
0
0
Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.Marion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia Mratibu wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maonesho hayo.Marion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia Mratibu wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' akizungumza na wanahabari katika maonesho hayo.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Kutoka maktaba: Ankal akiwa loliondo mwaka 1990

$
0
0
Hapa ni Loliondo Guest House kijijini Loliondo alimofikia Ankal wakati akifuatilia sakata la Loliondogate mwaka 1990.

Wadau Amini Mture Robert Kisanga na Maria Deborah Kimalando wameremeta jioni hii

$
0
0
 Mdau Amini Mture Robert Kisanga na mai waifu wake Maria Deborah Kimalando wakiingia nyumbani Oysterbay jijini Dar es salaam jioni hii tayari kwa mnuso wa nguvu  baada ya kumeremeta katika kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM chapel)
Mdau Amini Mture Robert Kisanga na mai waifu wake Maria Deborah Kimalando wakikaribishwa kimila kwa kunywa Mbege mlangoni wakati wakingia nyumbani Oyster bay jijini Dar es salaam tayari kwa mnuso wa nguvu
Maharusi wakikata keki

Ni wakati wa Ndafu ambapo maharusi na mpambe wao na Jaji Robert Kisanga na Mama Kisanga wanajiandaa kulisha watoto wao 

Jaji Robert Kisanga na Mama Kisanga wakilishwa ndafu na mtoto wao Amini
Nasaha za wazazi wa bwana harusi: Jaji Robert Kisanga na Mama Kisanga wakimuasa mtoto wao


SHIRO 2014 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD

Africa Speaks: 6th December 2014 - ICC Chief Prosecutor drops Uhuru Kenyatta's case

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Kijitonyama Choir - Hakuna mungu kama wewe

SERIKALI YAHIMIZA VIJANA KUJITOLEA

$
0
0
DSC_0378
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo, akiongea na Vijana wanaofanyashughuli za kutolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Alisema ingawa kujitolea kunawezesha kupata uzoezi ili vijana waweze kuajiriwa na kuendeleza taaluma,maana ya kujitolea haipo katika kuajiriwa bali katika hali ya kuona maana yake katika kusaidia jamii kujitambua na kujituma na kuwajibika .
“Usaidizi katika jamii ndio muhimu kuliko ajira. Haina maana yoyote kuwa na ajira bila kujua maana yake katika kusaidiajamii,”  huku akisisitiza kwamba haina maana yoyote kama umeajiriwa na ukaendekeza umimi  huku ukiwa hujali maslahi ya umma hata yanapoharibika.
Alisema Serikali ikiwa inaamini kwamba chachu ya kujitolea  ni vijana ametaka watumie njia mbalimbali katika shughuli za kujitolea kwa kuona wenzetu wanafanya nini na kutumia uzoefu wao katika kujenga taifa imara la Tanzania.
Aidha alisema wakati umefika wa vijana kusaidia kurejesha moyo wa kujitolea uliokuwepo kabla ya miaka ya 1970 ambapo shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ulifanywa na wananchi wenyewe kwa namna ya kujitolea kuanzia miaka ya 1970 moyo wa kujitolea umepungua sana.
DSC_0218
Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana kutoka taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali waliohudhuria maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri Mukangara iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (hayupo pichani).
“Nilikozaliwa wananchi ndio walikuwa wanatengeneza barabara, visima vya maji, wananchi ndio wanapeleka wagonjwa hospitali..’” na kusema kwamba sasa hali imekuwa mbaya kwa kuwa inadaiwa kitu kwanza kabla ya kufanyika kwa kazi.
Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kujitolea inayosema; Ushiriki na ushirikishwaji katika kuleta maendeleo katika ngazi zote za kitaifa na za kimataifa, amesema inaangalia  ushiriki wa vijana katika maendeleo.
Alisema Tanzania imetengeneza mikakati kadha aya kuwezesha ushiriki wa vijana ikiwa ni pamoja na kuridhia mkataba wa vijana wa umoja wa Mataifa na kuanzisha baraza la vijana kwa mujibu wa katiba.
Naye Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodrigues, amesema umoja wa mataifa unajisikia faraja kuadhimisha siku hiyo ikiwakumbuka watu mbalimbali waliofanya utu kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za ubinadamu.
DSC_0223
Akiwasilisha neno la katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki moon alisema siku ya kimataifa ya kujitolea ni muhimu kutokana na mahitaji halisi yaliyopo sasa duniani katika ulinzi wa maisha ya binadamu na utamaduni wake.
Alisema maelfu ya wananchi waliokumbwa na madhila mbalimbali wameweza kutulizwa na wafanyakazi wa kujitolea ambao waliondoa umimi na ubinafsi na kusaidia walio katika matatizo.
Alisema Umoja wa mataifa ukiwa unathamini amani , haki sawa na maendeleo ya jamii na kwa kuwa na siku ya kujitolea ya kimataifa kunaonesha umuhimu wa juhudi za umoja huo za kusambaza malengo hayo kufanikisha maendeleo na ushiriki wa vijana katika maendeleo yao , kitaifa na kimataifa.
Katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi, Vuzo alisema kwamba shughuli za kujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini mwaka 1974 katika misingi ile ile ya kufunza jamii kujitolea kwa manufaa yao na maendeleo ya Taifa. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

Diamond Platnumz alamba tuzo nyingine huko Nigeria

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz jana usiku aliweza kunyakua tuzo nyingine kutoka The Future Awards Africa 2014 huko jijini Lagos,Nigeria. Amelamba tuzo ya The Future Awards Africa Prize in Entertainment.

Article 22

BREAKING NEWSSSS.... MTANZANIA IDRIS SULTAN ASHINDA shindano la Big Brother ‘hotshots’ aondoka na dola laki 300 za kimarekani

$
0
0
Mshiriki  wa Tanzania anayewakilisha ndani ya mjengo wa Big Brother ‘hotshots’ , Idris Sultan ndiye ameibuka kidedea leo usiku katika shindano hilo huko Afrika Kusini. Idris amekuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo, baada ya Richard Dyle Bezuidenhout kuibuka kidedea mwaka 2011 katika Big Brother Afrika II.

KATIBU MKUU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI AONGOZA MAHAFALI YA TISA YA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA (MOCU)

$
0
0
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt Richard Sezibera akizungumza wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU)
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) AL-Noor Kassum akiwatunuku wanafunzi wa ngazi mbalimbali waliohitimu masomo yao Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU)
Wakunzi na baadhi ya watumishi wa kada nyingine katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MOCU) wakiwa katika mahafali ya tisa chuoni hapo yaliyofanyika katika uwanja wa Chuo hicho,Ushirika.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images