Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (kulia), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo.
Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid "Mapara".
Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid "Mapara".
Katibu Msaidizi wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati, Henry Mdimu.
Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha, Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Lounge, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.