Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live

MBUNGE WA CHALINZE ATOA WITO KWA MAKAMBUNI YA MAWASILIANO KUSAMBAZA HUDUMA KWA WATEJA WAKE

0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,(kulia)Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard. Hafla hiyo imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kulia)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart kicka Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (katikati) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.


MSUSI WA HK SALOON AFIA GUEST HOUSE,KIFO CHAKE CHAGUBIKWA NA UTATA

0
0

Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume mmoja ambaye ni Msusi katika moja ya Saloon za wanawake hapa manispa ya Tabora inayofahamika kama HK,Mwanaume huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ramadhani amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la SALAMA GUEST ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu na hatimaye kufikwa na umauti.
Mwili ukichukuliwa na Polisi  baada ya kuvunjwa mlango wa chumba katika  Guest House hiyo.
Dada huyu inasemekana kuwa ndiye alikuwa mpenzi wake marehemu huyo Ramadhani
Baadhi ya wananchi waliofika katika Guest house hiyo kushuhudia tukio hilo.
Hii ndio HK Saloon aliyokuwa akifanyia kazi msusi huyo maarufu wa nywele za akinamama ambapo kifo chake kimegubikwa na wimbi la utata kutokana na maelezo kuwa aliondoka Saloon hapo baada ya kufunga milango na kuelekea huko Guest house akiwa mzima wa afya.Habari kwa hisani ya http://kapipij.blogspot.com/

TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MLANDIZI, KIMARA NA TABATA

0
0
Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa KIMARA na TABATA; Miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani  kuwa, Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu umepata hitilafu kuanza siku ya Jumatano ya tarehe 03.12.2014 baada ya kuharibika kwa pampu moja ya kusukuma Maji (Pre-lift pump). 

Hali hii imelazimisha kupungua kwa uzalishaji Maji. 

Mafundi wa DAWASCO wanaendelea na matengenezo na kuhakikisha Pampu hii inafanya kazi na Huduma ya  Maji itarejea katika hali ya kawaida ifikapo siku ya Jumapili tarehe 07/12/2014
Wakazi wa maeneo yafuatayo wataathirika; MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, MSEWE, KIBANGU, RIVERSIDE, BARABARA YA MANDELA, TABATA, NA SEGEREA.

PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022- 2194800/ 0659-574012
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU AMBAO NI WA DHARULA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”

KAMISHNA KOVA AWATAKA ASKARI WALIOMALIZA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO WA JESHI LA POLISI KUTUMIA UJUZI NA MAARIFA WALIYOYAPATA KUONDOA KERO NA KUDUMISHA AMANI KATIKA MITAA YOTE YA JIJI LA DAR

0
0
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akifurahi jambo wakati akizungumza na Askari Polisi waliomaliza Mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar,wakati alipowapokea leo Desemba 4,2014 katika Kituo cha Kati cha Polisi,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Askari Polisi waliomaliza Mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova,wakati akiwaasa maswala mbali mbali yahusuyo Jeshi hilo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam amewapokea askari waliomaliza mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar ambao ni utaratibu wa kawaida na kuwaasa mambo yafuatayo:

Amewataka kutumia ujuzi na maarifa walivyopata katika mafunzo yao ili kuondoa kero za uhalifu katika jiji la Dar es Salaam. “Matukio ambayo ni kero katika jiji la Dar es Salaam ni pamoja na matumizi ya Dawa za kulevya, ujambazi wa kutumia silaha, na kero nyingine, madanguro, grocery katikati ya barabara, na muziki unaopigwa kiholela katika makazi ya watu”. Alisema Kamishna Kova.

Aliwataka washirikiane na askari wenzao katika oparesheni inayoendelea jijini Dar es Salaam kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba ili kuthibiti vitendo vya uhalifu ambavyo kwa kawaida hujitokeza kwa wingi katika kipindi hicho. 

Aidha, wahitimu hao wametakiwa kusimamia na kudumisha nidhamu katika Jeshi la Polisi ili kuwafanya wananchi wapate huduma nzuri pamoja na kuleta  taswira nzuri ya Jeshi la Polisi.

Amewaasa askari hao kufuata maadili ya kazi ya Polisi na kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwani wanaweza kupata vyeo vya juu, kuwa mfano na wakawa viongozi bora Jeshini.
Mwisho amewataka kushirikiana na wananchi katika mitaa mbalimbali na kufanya doria ili kila mtaa jijini Dar es Salaam uwe huru dhidi ya uhalifu.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

MAMA ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE AOMBA MSAADA KWA WASAMALIA WEMA

0
0
WANAWAKE wengi duniani bado wananyanyaswa kijinsia kwa sababu za kijamii, kiuchumi na kipato licha ya kuwepo kwa elimu kuhusu haki zao.


Mwanamama Ester Charles ambaye ni mkazi wa Mwambani wilayani Ilemela ametelekezwa na mumewe aliyetajwa kwa jina la Albinus na kubakizwa na watoto wawili wadogo wanaohitaji uangalizi na usimamizi. Pichani mwanamama Ester akiwa na mtoto wake mdogo anayetaabika na ugonjwa wa kupooza. 



KWA UFUPI

Mumewake alipopata mwanamke mwingine alihama nyumba aliyokuwa akiishi na mama huyu na kupanga eneo jingine kabisa bila kuikumbuka familia yake katika matumizi na mahitaji muhimu.
Alipomfikisha mumewe huyo mbele ya mikono ya Sheria alikubali kutoa huduma lakini ndani ya kipindi kifupi alitorokea kusikojulikana.
Amefika kuomba msaada toka kwa wasamalia wema watakaoguswa na simulizi yake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA. 
Hali ya afya ya kwa mtoto Jr. Albinus si ya kuridhisha na haijafahamika nini kinachomsibu kwani bado hajafika hospitali kupata matibabu ya kina. Mtoto huyu pichani hawezi kutembea, hawezi kuzungumza kwa ufasaha wala kukaa, zaidi ya kulala tu muda wote.


CHANGAMOTO ALIZONAZO MAMA ESTER.

Hana pesa kwaajili ya chakula cha watoto.
Hana nguo kwaajili ya kuwavisha watoto na yeye binafsi.
Anadaiwa pesa ya kulipia nyumba anayoishi kiasi kwamba mwenye nyumba anataka kumfukuza.
Amejaribu kuomba kazi kwenye kaya mbalimbali na kukosa, akipewa majibu kuwa hawezi kuajiriwa akiwa na watoto (atashindwa kufanya majukumu ya mwajiri) naye hana sehemu ya kuwahifadhi iwe ndugu au majirani.
Jeh! Umeguswa tafadhali wasiliananaye kupitia namba 0753804881.

MUNGU AWABARIKI.

MBUNIFU WA MAVAZI,MANJU MSITA KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KATIKA MOZAMBIQUE FASHION WEEK 'MFW-2014'

0
0
Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wake katika Mozambique Fashion Week yatakayoanza desemba 10 mpaka 14 ambapo atakuwa akipeperusha bendera ya taifa
Mwanamitindo Matukio Chuma kulia akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa kutangaza  upeperushwaji wa bendera ya tanzania katika nchi ya mozambique fashion week ambayo mbunifu wa mavazi Manju Msita atashiriki na kupeperurusha bendera ya Tanzania kushoto ni mwanamitindo Vivian Williams ambaye anafanya shughuli zake za uwanamitindo nchini Barcelona,Spain. 

MAREHEMU ELIAS ANTHONY MAPUNDA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI

0
0
1
Kaka wa Marehemu Elias Anthony Mapunda Bw. Nesto Mapunda wa pili kutoka kulia na Mkewe Teddy Mapunda wakiwa wamesimama mbele ya jeneza la marehemu Anthony tayari kwa kiungia katika kanisa katoliki la Mtakatifu Matha Mikocheni kwa ajili ya misa maalum ya mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jana Fullshangwe inampa pole Ndugu Nesto Mapunda pamoja na ndugu na jamaa kwa kuondokewa na ndugu yao mpendwa marehemu Elias Anthony Mapunda. Wao walimpenda lakini mungu amempenda zaidi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN. 
2Mwili wa narehemu Elias Anthony ukiombewa kabla ya kuingizwa kanisani.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Airtel yatoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh mil 15 kwa chuo kikuu cha Dar es saalam

0
0
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (kushoto) akikabidhi jezi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa pili kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akikabidhi jezi kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga (wa pili kushoto) akikabidhi kikombe kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Yunus Mgaya, wakati Airtel ilipokikabidhi chuo hicho msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya milioni 15/-, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo mbalimbali inayotarajiwa kuanza Jumatatu Desema 08 mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Michezo wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), Stanry Julius (kushoto), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kushoto) na Mratibu wa Michezo wa Chuo hicho, Dk. Crispian Maro.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


KIJANA ANUSURIKA KUAWA BAADA YA KUIBA SHUKA LA KIMASAI.

0
0
Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kifo toka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kukiri kuiba shuka la Kimasai katika moja ya maduka yanayouza bidhaa za aina hiyo lililoko mtaa wa uswahilini katikati ya mji wa Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Membe mgeni rasmi mahafali UB, kufanyika kesho Bagamoyo

0
0
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, kesho Jumamosi Desemba 6 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi Katika Mahafali ya Pili ya  Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo kwa vyombo vya Habari Dar Es Salaam,  na Ofisa Habari wa  ( UB), Happiness Katabazi, inasema Kuwa Membe ndiye Atakuwa mgeni rasmi Katika mahafali hayo ambayo yatafanyika Katika Hoteli ya Kiromo  View Resort  kijijini Kiromo Wilayani Bagamoyo,Mkoani Pwani.


Katabazi alisema jumla ya wahitimu 99 wanatarajiwa kutunukiwa Vyeti Katika ngazi ya Shahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Diploma,  na cheti.


Wakati huo huo , Juzi Makamu wa Rais  Dk.Mohammed Gharib Bilal alishindwa kuhudhuria sherehe za uwekwaji  wa jiwe la Msingi wa makazi ya kudumu ya UB ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa makao makuu ya UB kijijini hapo ambapo ujenzi ukikamilia majengo hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 5000, yaliyopaswa yafanyike Katika kijijini Cha Kiromo ,Bagamoyo Mkoani Pwani kwasababu alikuwa amebanwa na majukumu mengine ya Kitaifa na akaomba apangiwe tarehe nyingine ya kuja kuweka jiwe Hilo la Msingi.


Akizungumza na waandishi wa Habari Katika kijijini Kiromo Juzi wakati akiiarisha sherehe za Utiaji wa jiwe la Msingi , Makamu Mkuu wa UB, Profesa Costa Ricky Mahalu alitoa historia fupi la shamba Hilo lililopo Kijijini Kiromo Alisema  familia yake ililinunua rasmi Agosti 26 Mwaka 2003.

 
Profesa Mahalu alisema Katika shamba Hilo familia yake imeamua kukata heka 100 na kuzitoa kwa UB ili UB iweze kujenga makazi yake ya kufumu katika Kijiji cha Kiromo na kwamba heka nyingine zilizosalia familia yake itazitoa  kwa Taasisi nyingine za elimu ya juu  na kwamba Tayari Taasisi nne za elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu Kimoja Cha kigeni kimeishaonyesha nia ya kutaka Kuja Kujenga Taasisi yake ya elimu Katika shamba Hilo.


Profesa Mahalu Alisema shamba hilo kabla familia yake haijalinunua lilikuwa likimilikiwa na lililokuwa shirika la Serikali la NAFCO na baada ya kufirisika mwaka 1990  lilichukuliwa na LART  ambaye alikuwa na jukumu la kuchukua  kuuza Mashitaka ya serikali yalikuwa na matatizo ya kifedha.


' LART ikamkabidhi  kampuni ya PHLLIP&Ltd  iliyauza mashamba matatu  ya NAFCO  yaliyopo Kiromo. Hayo mashamba matatu ,Moja iliuziwa familia ya Mahalu na mkataba wa mauzo wa shamba Hilo la Mahalu na LART ulisainiwa Agosti 26 Mwaka 2903  na baada ya hapo  umiliki wa shamba  unachukuliwa  na familia ya Mahalu kwa mujibu wa Sheria.' Alisema Balozi Mahalu.

Tupo tayari kwa Uhurumarathon 2014

0
0

 Mratibu wa Uhurumarathon Tanzania Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kukamilika kwa maandalizi yam bio hizo zinazotarajiwa kufanyika jumapili hii jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Leders Club kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la Riadha la Taifa Selemani Nyambui.

MAANDALIZI ya mbio za Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7  (jumapili) jijini Dar es Salaam yamekamilika, huku wanaridha kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi wakithibitisha kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuulinda uhuru wetu, kudumisha umoja, amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, maandalizi yote yamekamilika, huku wanariadha wa hapa nchini kutoka nje ya Dar es Salaam wakiwa wamewasili tayari kwa ushiriki wao.
 
Melleck pia alisema, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ulinzi umeimarishwa kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha usalama unakuwa mkubwa kwa washiriki wote na barabara zitakazotumika zitafungwa katika kipindi hicho.
 
“Kila kitu kimekamilika na washiriki kutoka nje ya Dar es Salaam wameanza kuwasili kwa ajili ya mbio hizo na tunawahakikishia usalama utakuwa mkubwa mno katika kipindi chote cha mbio hizo n mpaka kufikia jana (juzi) tayari washiriki waliojitokeza walikuwa 4000,” alisema.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, wanariadha maarufu wa hapa nchini watakaoshiriki ni pamoja na Fabian Joseph na Dickson Marwa, huku Jacqueline Sekini aliyeshinda mbio hizo kwa upande wa wanawake mwaka jana, naye akiapa kutetea ubingwa wake.
 
“Wapo wanariadha wengi watakaoshiriki, lakini nataka kutoa angalizo kwa wanariadha kutoka Kenya, sisi tumetumwa mwaliko kwa wa chama husika na wao ndio watutumia majina ya wanariadha kumi, watano wa kiume na waliobaki wa kike, hatutapokea mwanariadha kutoka nchi hiyo ambaye hatujapewa jina lake,” alisema.
 
Nyambui alisema, tayari waamuzi watakaosimamia mbio hizo wapo tayari na akasisitiza ni lazima taratatibu zote zitafuatwa ili kupata mshindi halali.
 
Mbio hizo zinatarajiwa kuanzia viwanja vya Leaders Club na zitakuwa za kilomita 21, kilomita 5 na kilomita 3 ambazo ni maalumu kwa ajili ya viongozi wa kitaifa, dini na taasisi mbalimbali.
 
 
Aidha Melleck alisema, tayari namba kwa washiriki zimeanza kutolewa na wanaweza kuzipata katika viwanja vya Leaders Club.
Mgeni rasmi katika mbio hizo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.

Balozi Seif Idd awaasa wana CCM Zanzibar kuacha tabia ya kupuuza mambo yanayowahusu,ili wasije jutia baadae

0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif kizungumza na Viongozi wa Kamati ya Siasa ya Tawi la CCM Upenja.Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ B” Nd. Hilika Khamis na kulia yake ni Mwenyekiti wa Tawi la CCM Upenja Nd.Daudi Hasnuu Khamis.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa na Mabalozi wa Nyumba Kumi wa Tawi la CCM Upenja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani alipokuwa akizungumza nao kwenye ukumbi wa Tawi la hilo Upenja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Zanzibar Nd. Said Sarboko Makarani akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hatua zilizochukuliwa za kuheshimu hifadhi ya urithi wa Kimataifa wakati wa ujenzi wa Hoteli ya Park Hyatt iliyopo Forodhani Mjini Zanzibar. Nyuma ya Nd. Sarboko ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Ardhi, Maji Nishati na Madini Mh. Haji Mwadini pamoja na Mratibu wa Mradi wa Hoteli ya Park Hyatt Bwana Yaqoub Osman.

KANUSHO LA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO KWENDA NCHINI NORWAY

TFF YATANGAZA RASMI RATIBA YA MASHINDANO YA KOMBE LA WANAWAKE TAIFA

0
0
 Rais Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mh Jamal Malinzi akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za TFF kuhusu kampuni ya Proin Promotions ltd kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Disemba kwa kushirikisha timu kutoka Mikoa yote ya Tanzania. Mashindano hayo yatazinduliwa Mkoani Mwanza kwa kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara. Kushoto kwa rais wa TFF ni Rose Kissiwa ambae ni mwakilishi wa Chama cha Mpira wa wanawake Tanzania.Na Kulia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Wanawake Tanzania.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza akizungumzia jinsi kampuni ya Proin Promotions Ltd ilivyoona umuhimu wa kuchangia katika kuinua soka la wanawake nchini na kuamua kudhamini Shindano hilo lijulikanalo kama Kombe la Wanawake Taifa ambalo litaanza rasmi tarehe 28 kwa mechi ya uzinduzi kati ya Mwanza na Mara huko Mkoani Mwanza
Bi Rose Kissiwa, Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania akizungumzia juu ya udhamini uliotolewa na kampuni ya Proin Promotions Ltd katika kufanikisha Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo uzinduzi wa Mashindano hayo yatafanyika Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha TImu za Mwanza na Mara.Picha zote na Josephat Lukaza. 

Tanzania Seeks Out Sunderland FC to Promote Its Tourism.

0
0
As Kenya grapples with insecurity and the consequent ailing tourism, her neighbor Tanzania is confidently striding across the borders to replenish its parks with international visitors.

A closer look at the once vibrant industry, the number of international tourists’ arrivals has plummeted owing to the incessant terror threats and attacks from the Al-Shabaab militant group thereupon scaring the visitors away.
The Tourism Recovery Taskforce, which is charged with the responsibility of instituting turnaround strategies to reanimate the ailing sector. On its list ‘Global Terrorism Index 2014’, the Institute for Economics and Peace ranked Kenya 12th most at risk of becoming less peaceful on its list of countries most affected by terrorism. The country also sits 132 on the Global Peace Index score and this insecurity setback has seen the numbers of tourist arrivals plummet.

When the task force took charge, Chairperson Lucy Karume revealed that the private sector has used over KES 14.7 million in local and international media familiarisation trips to showcase Kenya as a safe destination.

Amid the lukewarm reception, the government has set out to hire a foreign PR company to restore Kenya’s image abroad. During the World Travel Market held in London in August, Tanzania Tourist Board (an equal of Kenya Tourism Board) seized the chance to secure Sunderland FC’s services to “promote their beautiful country to a wider audience” and “develop sports tourism in Tanzania”. The ties are not new: they are deep-rooted.

Since then, the club has labeled all its flash tops “VISIT TANZANIA”. The club, in partnership with Tanzania Tourist Board and South African Airways, launched a competition whereby four lucky fans are set to jet off to Tanzania and experience the African savannah for a whole week this holiday.

What if Kenya employed such a strategy? In fact, Kenya has more elite sportsmen than Tanzania contracted in top class leagues in the world like Victor Wanyama who plays for Southampton FC in England. What if Kenya Tourism Board turned to such clubs whereby they are assured of reaching a wider audience than just an international PR firm? It’s up for debate.


Mahafali DIT kufanyika Januari 2015

0
0
Mahafali ya nane ya Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), yanatarajiwa kufanyika Januari 31 mwaka huu katika viwanja vya chuo hicho na yatatanguliwa na utoaji wa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wahitimu ambao wamefanya vizuri katika masomo yao. 

 Taarifa ya DIT kwa vyombo vya habari imesema kuwa tuzo kwa wanafunzi zitatolewa Januari 23 mwaka huu ikiwa ni wiki moja kabla ya mahafali hayo ambayo wahitimu katika ngazi na masomo tofauti watatunukiwa. Wahitimu watakaotunukiwa ni siku hiyo ni pamoja na wa Stashahada ya Uhandisi (Ordinary Diploma), cheti cha awali cha TEHAMA (IT) mwaka wa masomo 2013/2014.

 Wahitimu wametakiwa kusoma utaratibu wa kuthibitisha kushiriki mahafali hayo katika tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz na “Rehearsal” itafanyika Ijumaa tarehe 30 Januari 2015. 

 “Malipo ya Tshs 30,000/= kwa ajili usajili yatafanyika kwenye tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.ac.dit.tz” Inasema taarifa hiyo. Malipo yanatakiwa klufanyika kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu iliyotolewa kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na dhumuni la malipo mf. 

Ada, transcript na graduation. Kulingana na taarifa hiyo, mwisho wa kujisajili ni tarehe 31 Desemba, 2014 na wahitimu wametakiwa kufahamisha kuhusiana na mahafali hayo.

MAKAMU WA RAIS DKT BILALI ABARIKI KANISA LA KIASKOFU LA ROHO MTAKATIFU LA JIMBO LA KONDOA MKOA WA DODOMA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilai akizungumza na waumini wa Dini ya kikiristo wakati washerehe za kutabaruku Kuweka wakfu, kanisa la Kiaskofu la Roho mtakatifu jimbo la kondoa  jana 4/12/2014 iliofanyika Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipongezwa na Askofu wa kanisa katoliki Jimbo la kondoa Baba  Bernadin Mfumbusa mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la kiaskofu la Roho mtakatifu jimbo la Kondoa juzi 4/12/2014 iliofanyika walaya ya kondoa mkoa wa Dodoma.
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu na mashekh wa Wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma Mara baada ya kuzungumza na waumini wa Dini ya kikiristo jana tarehe 4/12/2014.
Makamu wqaa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania Kardinali Polcarp Pengo wakati wa Sherehe za Kutabaruku kuweka wakfu ,kubariki kanisa lakiaskofu la roho Mtakatifu la jimbo la kondoa iliofanyika wilayani kondoa mkoa wa Dodoma juzi tarehe 4/12/2014.                                                

Naibu Katibu Mkuu afungua Mkutano wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akifungua Mkutano wa 6 wa Kamati ya Ukaguzi kwa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika katika Hoteli Harbour View, Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kudhibiti uvunaji haramu wa maliasili ikiwemo madini ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa kichocheo cha vikundi vya uasi na migogoro katika Eneo la Maziwa Mkuu hususan katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Balozi Dora Msechu awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Finland

0
0
 "Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic,  na Baltic Mheshimwa Dora Mmari Msechu aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Finland, Mheshimiwa Sauli Niinistö  jijini Helsinki Alhamisi 4 Desemba, 2014"
 "Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic,  na Baltic Mheshimwa Dora Mmari Msechu katika picha ya pamoja na   Rais wa Finland, Mheshimiwa Sauli Niinistö  baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho jijini Helsinki Alhamisi 4 Desemba, 2014. Kulia ni Afisa wa Ubalozi ni Yusuph Mndolwa
 "Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic,  na Baltic Mheshimwa Dora Mmari Msechu akipeana mikono na Rais wa Finland, Mheshimiwa Sauli Niinistö  baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho Alhamisi 4 Desemba, 2014.

ICC yatupilia mbali kesi ya Kenyatta

0
0
Mahakama ya kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Mwendesha Mashtaka mkuu, Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008 nchini humo.

Mahakama ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya Kenyatta au la ingawa alisema muda huo haukutosha kwake yeye kuandaa ushahidi zaidi dhidi ya Kenyatta.

Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni Naibu Rais wa nchi hiyo ya Kenya kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.

Zaidi ya watu elfu moja waliuawa wakati wa ghasia hizo. 

Uhuru alikuwa mtu maarufu zaidi kufikishwa mahakamani na pia mshukiwa mkuu kwani alifikishwa mahakamani akiwa Rais aliye mamlakani.

Hili ni pigo kubwa kwa upande wa mashitaka, wengi walioana kesi dhidi ya Kenyatta kama mtihani mkubwa katika historia ya mahakama hiyo.

Upande wa mashitaka ulitaka mahakama kuupatia muda zaidi ili upate ushahidi zaidi,dhidi ya Kenyatta kama vile taarifa za akaunti yake ya benki.
Upande wa utetezi ulisema kuwa ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha kesi hiyo inapaswa kutupiliwa mbali.

CHANZO: BBC SWAHILI
Viewing all 109581 articles
Browse latest View live




Latest Images