Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 661 | 662 | (Page 663) | 664 | 665 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Nianze kuliandikia hili kwa kuonyesha furaha yangu kuwa huwenda sasa kumekua na uelewa juu ya maswala ya usalama mitandao. Nalisema hili kutokana na uhalisia kwamba Jana nilipata maswali kutoka kwa watu wengi sana huku nikipata jumbe nyingi zilizofanana zikielezea juu ya tukio la benk ya NBC kuingiliwa na wadukuzi.

  Wengi walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza. Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na uelewa wa maswala husika.

  NINI HASA KILITOKEA?

  Kwanza kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.

  Pili, Kulitokea Tahadhari ya Moto iliyosababisha wafanyakazi kuchuukua tahadhari ya kutoka nje.

  Na Tatu, Mifumo ya Mobile banking (Inayotoa huduma za miamala kupitia simu za kiganjani) kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo iliyo sababisha kutoa kiwango kisicho sawa kwa waliokua wakiangalia salio.

  Matukio haya matatu yaliunganishwa na kutengeneza taarifa moja iliyo sambazwa kua kuna mdukuzi aliingilia banki ya NBC na kusababisha mifumo kutofanya kazi na hatimae kuhamisha kiasi kikubwa  cha pesa. Kitu ambapo kilipelekea wafanya kazi kutoka nje ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa.

  Na anaepata taarifa anapo angalia salio anaona kunatatizo katika kiasi chake na kuamini jumbe ile. Panapotoka ufafanuzi wa taarifa hii wengi bado wanahoji bado kuna shaka niendelee kutoa ufafanuzi nini hasa kinaweza kikawa kimesababisha?


  0 0

  Bw. Peragius  Cosmas mwanafunzi aliyehitimu shahada ya Uhasibu na kupata  GPA 4.91 akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.
  Bi. May Issa  mwanafunzi aliyehitimu shahada ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi  na kupata  GPA 4.92 Akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha CBE Prof.Emanuel Mjema.

  Kwa kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  wanafunzi hawa  kutoka kampasi ya Dodoma  wameweza kupata ufaulu mkubwa katika masomo yao.

   Bi. May Issa  Mwanafunzi  aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa  Manunuzi  katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 ametangazwa  kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya  4.92. ambapo  aliweza kupata alama  A  28 , alama  B+ tatu  na  alama  B  moja  kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na  Bw. Peragius Cosmas  aliyepata GPA ya 4.91.

   Kwa upande  wake Mwanafunzi mwingine  Bw, Peragius Cosmas  aliye kuwa akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu   yeye pia alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA ya  4.91  ambapo aliweza kupata alama  A  29 na  alama  B+ tatu    kati ya masomo  32  ya shahada yake ya kwanza  ya  uhasibu.

  Hivi  karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  pia tulishuhudia  Msichana   Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa  Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano.
  PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

   kamishna  wa uhamiaji na usimamazi na uthibiti wa mipaka Abdallah Khamis akipata maelekezo kutoka kwa maofisa wa uhamiaji namna zoezi la kuandikisha raia wa kigeni linavyofanyika.
  Maofisa wa uhamiaji wakichukua alama za vidole
   Moja ya kitambulisho wanachopewa Raia wasio wa Tanzania .
    Raia wa Congo ambaye ameishi nchini isivyo halali kwa miaka kumi na moja akifurahi na familia yake baada ya kupata vitambulisho vya kuishi nchini kihalali.
  Baadhi ya wananchi ambao si raia wa Tanzania ambawaliojitokeza katika zoezi la kuandikishwa ndani ya uwanja wa Lkae Tanganyika

  Na Editha Karlo,wa Blog ya Jamii,Kigoma.

  IDARA ya uhamiaji kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la uhamiaji(IOM) wamezindua zoezi la kuandikisha raia wote wa kigeni wanaoishi nchini isivyo kihalali.

  Kamishna wa uhamiaji Abdallah Khamis, anayeshughulikia usimamizi na uthibiti wa mipaka akiongea wakati wa  uzinduzi wa zoezi hilo katika viwanja vya Lake Tanganyika ,alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuwatambua raia wote wasio Watanzania na kuwapa hadhi ya inayostahili na hili ni zoezi la nchini nzima limeanza Kigoma litaendelea na mikoa yote ya Tanzania.

  ''Kuna raia wakigeni hawana sifa za kuishi nchini ila tayari wamelowea huku na wameishi miaka mingi,na pia wapo wanaoishi nchini kwa vile wameolewa au wameoa Watanzania,kwakweli zoezi hili litasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa utata ambao umekuwepo kwa muda mrefu wa nani raia na nani si Raia wa Tanzania''alisema Kamishna Abdallah

  Kamishna huyo alisema pia zoezi hilo halina uhusiano wowote na uchuguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani pamoja na uchaguzi wa serekali za mitaa.

  ''Hii itasaidia sana kuondoa wahamiaji haramu waliokuwa wakijiingiza katika masuala ya siasa na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kitu ambacho si sahihi''alisema Kamishna

  Naye Ofisa uhamiaji wa Mkoa wa Kigoma Ebrossy  Mwanguku alisema kuwa lengo hasa la zoezi hilo pia ni kuondoa raia kutoka nje ya nchi wanaoishi nchini bila ya kuwa na vibali halali vya kuishi nchini.

  Alisema kuwa sehemu kubwa ya wahamiaji waliojitokeza katika zoezi hilo ni raia kutoka nchi za Burundi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya  Congo(DRC)Uganda na Rwanda.

  Aliwataka Raia wote wanaoishi nchini isivyo halali kujitokeza katika zoezi hilo kwani baada ya kukamilika kwa zoezi hilo desemba 21 kwa Mkoa wa Kigoma yeyote atakaye kamatwa sheria zitachukua mkondo wake.

  Kiongozi wa shirika la IOM Tamara Keating alisema kuwa hayo ni matokeo ya oparesheni kimbunga iliyobaini kuwepo nchini kwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu,

  0 0  0 0


  0 0

  Salam kwako Ankal na timu nzima ya Globu ya Jamii,

  Tunawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kutujuza mambo mbali mbali yanayoendelea hapa nchini na nje ya mipaka ya nchi yetu,tunawapa BIGI APU sana kwa kweli.

  Kupitia libeneke la Globu ya Jamii,naomba nifikishie kero yangu hii kwa wahusika wa Halmashauri ya Jiji,maana leo nilifika pale kwenye stendi kuu ya mabasi (Ubungo Bus Terminal) na kukutana na  utaratibu wa kulipisha kiasi cha sh. 300 ikiwa ni gharama ya maegesho ya magari ndani ya stendi hiyo,hali ambayo haiendani kabisa na malipo yanayolipishwa getini pale.

  Kiukweli pale haki haitendeki kabisa maana hakuna huduma yeyote ya maana ndani ya Stendi ile kwa hivi sasa,hasa baada ya kituo kicho kuvunjwa vunjwa na hayo maegesho yenyewe tunayolipia hata hayapo na pia bado kuna utaratibu wa kuwalipisha kiasi cha sh. 200 kila mtembea kwa miguu anayeingia kwenye stendi hiyo.

  Naomba wahusika wa Halmashauri ya Jiji hasa Manispaa ya Kinondoni kuliangalia swala hili kwa jicho la pili,maana hicho kiasi kinaonekana ni kidogo lakini ni kikubwa sana.

  Mdau Mzalendo wa Jijini Dar.

  0 0
  0 0


  0 0

  Mdau Anne Kivembele ambaye ni Mhariri na Mchanganya picha wa Kituo cha Televisheni cha ITV akiwa kapozi kwa picha mara baada ya kulamba nondozz yake ya Uzamili ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii katika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki iliyopita.
   Mdau Anne Kivembele akiwa na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondooz zao katika Chuo Kikuu Huria,jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0
 • 12/04/14--03:24: NMB YAWAFIKIA WAKAZI WA SIHA
 • Benki ya NMB jana ilizindua rasmi tawi Jipya katika wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro. Tawi hili linakadiriwa kuhudumia Zaidi ya wateja Mia moja kwa siku. Tawi jipya la NMB Siha litakuwa linatoa huduma zote za kibenki kunzia kufungua akaunti mbali mbali za akiba, huduma za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya mahitaji yote kwenye soko, huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipa kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali, kuweka na kutoa fedha. 

   Tawi la NMB Siha lipo maeneo ya Boma Ng’ombe bara bara ya Sanya Juu.Tawi hili linatoa huduma kwa wakazi wa Lawate, Ngare Nairobi, Kibong’oto,Sanya Juu na Halmashauri ya wilaya ya Siha kwa ujumla.
  Naibu Waziri wa nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.  Aggrey Mwanri   akikata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Siha mkoani Kilimanjaro.  Wa Pili kutoka kushoto  ni Meneja wa NMB Kanda ya kaskazini - Bi.Vicky Bishubo pamoja na maofisa wengine wa NMB na serikali wakishuhudia.
  Meneja waTawi la NMB Siha Bw.Jovin Twesige akimsubiri Naibu Waziri wa nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.  Aggrey Mwanri  ambaye anaweka saini kwenye Kitabu cha wageni wakati   alipowasili katika tawi la NMB Siha Kwa ajili ya uzinduzi rasmi


  0 0

  Napenda kupitia blog hii ya jamii kuwakaribisha watu wote katika jiji hili la Dallas,Texas katika semina kubwa ya neno la Mungu itakayofanyika katika jiji letu. Mtumishi wa Mungu anaeheshimika ndani na nje ya nchi yetu Dr.Daniel Moses Kulola ndie atakae tuhudumia. 

  Daniel Kulola ni mtoto wa marehemu mzee Moses Kulola,mtumishi ambae ametoa mchango mkubwa  sana wa injili katika Taifa letu kabla hajaenda kukaa na Bwana. Ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kuhudhuria semina hii; kanisa lako la Umoja limetoa basi maalumu litakalo wahudumia watu wote ambao wanahitaji usafiri. Dr. Daniel pichani atatuhudumia siku siku zifuatazo;

  Ijumaa kuanzia 12 jioni -2 jioni (6:00 Pm-8:00Pm)
  Jumamosi Kuanzia 10 jioni-12:30 Jioni (4:00Pm-6:30Pm)
  Jumapili kuanzia 11:30 jioni- 2 jioni (5:30 Pm-8:00 Pm)
  Tunaomba kila moja wetu azingatie muda haswa siku ya Jumamosi kwani ndio jumuia yetu inasherekea siku ya uhuru wa Taifa letu.

  Anuani: Umoja International Outreach Church
  6411 LBJ Freeway,Dallas Texas,75240
  Simu: 214 554 7381, 682 552 6402

  Pastor Absalom Nasuwa

  0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo,(kushoto), akimkabidhi Kamanda Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Mohammed Mpinga. Ripoti ya Upimaji wa afya za madereva, wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika Novemba 22 hadi 28 katika vituo vya mikese, mkoaniMorogoro. Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam juzi.
    Kamanda Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Mohammed Mpinga. akitoa shukrani kwa TBL baada ya kukabidhiwa  Ripoti ya Upimaji wa afya za madereva,
   Mganga Mkuu wa Polisi akisoma ripoti hiyo.

  0 0

   Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo akitoa ufafanuzi wa tatizo la huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya tatizo hilo hakuna hata senti moja ya mteja wao iliyopotea. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa.
   Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu tatizo lililojitokeza jana katika huduma zao za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya wateja kutoona salio katika akaunti zao hakuna hata senti moja iliyopotea. Kushoto ni Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Jimmy Myalize.
  Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini kurekodi mkutano wa menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam leo walipokuwa wakitoa ufafanuzi juu ya tatizo lililojitokeza jana Desemba 3, 2014 ambapo wateja wa benki hiyo walishindwa kutumia huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking).

  0 0


  0 0  The showcase will be from 5-7 December from 8 PM on wards

  NORMAL Tickets available ONLY @ EPIDOR in Masaki @30,000TZS
  Tickets at entrance is priced at 40,000TZS
   
  VIP FRONT ROW Tickets SMS: +255767222441
  5-7 December 2014
  HOTEL SEA CLIFF
  DAR ES SALAAM


  CONTACTS:
  General: +255757828832
  Shopping Festival:+255787747918

  Share
  Tweet
  Forward
  +1
  Share
  Copyright © 2014 Swahili Fashion Week, All rights reserved.
  you are receiving this email due to your patronage to our event

  Our mailing address is:
  Swahili Fashion Week
  Plot 48B Drive inn
  Dar Es Salaam
  Tanzania
  0 0

   Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Patrobas Katambi. Ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na mwanadiplomasia mahiri Profesa Abdalla Safari, uko nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Safari Abdalla akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP) Rainer Wieland wakati ujumbe wa CHADEMA ulioko nchini Ubelgiji, ulipofika ofisi za bunge hilo mjini Brussels kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri John Mrema.
   Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demoikrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, wakati ujumbe wa CHADEMA ulipofika Ofisi za EP kuanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Jumbe Safari akiwa na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, walipokutana jana mjini Brussels, Ubelgiji kwa mazungumzo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa CHADEMA kufuatia mwaliko wa bunge hilo.

  0 0

   Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
   Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilishana hati ya  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.
   Baadhi ya waandishi wa habari na watumishi wa wizara ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia wakiwashuhudia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kwa serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo)
   
  Eleuteri Mangi- MAELEZO
  04/12/2014
  Serikali ya Tanzania imesainiana  mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya  shilingi bilioni 45.2 na Shirika la Maendeleo la Saudia kwa lengo la kuboresha miradi wa maji kwa wilaya ya Same, Mwanga na ujenzi na ukarabati wa barabara Visiwani Zanzibar.

  Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas.

  Akiongea na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Waziri Saada alisema kuwa kati ya mkopo huo shilingi bilioni 41.25 ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani milioni 25 zitagharimia mradi wa maji katika wilaya za Same na Mwanga na  shilingi bilioni 3.96 kwa ajili ya maradi wa barabara Pemba, visiwani Zanzibar.

  Waziri Saada alilishukuru Shirika la Maendeleo la Saudia kwa jitihada zao za kuisaidia Serikali ya Tanzania katika kautatua tatizo la maji wilaya za Same na Mwanga pamoja na uboreshaji wa barabara katika visiwa vya Pemba.
   
  Aidha, mradi wa maji wa Same- Mwanga utagharimu Dola za Kimarekani milioni 110.34 ambazo benki ya BADEA, Shirika la Maendeleo Kuweit, OPEC na mashirika mengine wamekubali kukamilisha sehemu ya fedha iliyobakia.

  Mradi wa maji wa Same- Mwanga baada ya kukamilika utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji vijijini amabapo utasaida kuboresha hali ya maisha wa wananchi wa maeneo hayo, upatikanaji nwa maji safi na salama kwa maendeleo ya afya za wakazi hao na kuboresha uchumi wao kwa kutumia muda mwingi kwa shuighuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Saudia Mhandisi Hassan Al-Attas amesema kuwa makataba waliosaini leo unaonesha kuwa Saudi Arabia iko mstari wa mbele katika kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi wake kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo.

  Hafla hiyo ilihudhuriwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa wizara ya Fedha na wawakilishi wa Serikali ya Saudi Arabia.

  Mwisho

  0 0

  Timu kutoka Bandari za Maziwa ikiingia uwanjani.
  Mashabiki wakiwa uwanjani.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Ponsiano Nyami akiikagua timu ya Bandari ya Dar es Salaam kabla ya kuwavaa Bandari Mtwara.
  Timu ya kuvuta kamba kutoka Bandari ya Dar es Salaam wakimenyana na wenzao wa Bandari Mtwara.


  0 0

   Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti mmoja ya washiriki wa mafunzo ya D.H.I.S  Osama Al Zubair  kutoka Sudan wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi, Kaskazini Unguja.
   Mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya D.H.I.S Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo kutoka Nchi za Afrika, Marekani, Ujerumani na Mashirika wahisani katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
   Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) Suleiman Salum  Ali  akieleza mafanikio  ya mafunzo hayo  yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi, wa kwanza (kulia) ni Profesa Kristin Braa kutoka Chuo Kikuu cha Oslo ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo kwa kushirikiana  na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar. (kati) ni Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliefunga mafunzo hayo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar)
   Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa akiyafunga mafunzo ya siku 10 yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
   Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya Suleiman Salum Ali akizungumza na waandishi wa Habari walioshiriki ufungaji wa mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
   Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) wakiwa na mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar).

older | 1 | .... | 661 | 662 | (Page 663) | 664 | 665 | .... | 3278 | newer