Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 660 | 661 | (Page 662) | 663 | 664 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Maafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014.

  Marehemu Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya maziko yake. 

  Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya upata hitilafu katika injini yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa Simba,  Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa Arusha.SOURCE: Father Kidevu Blog
  Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
   Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
   Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita akiwahamasisha baadhi ya vijana na wanafunzi waliotembelea banda la maonesho la kitengo cha kuongozea ndege (hawapo pichani) kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kupata fursa ya kujiunga na fani ya uongozaji wa ndege ndani na nje ya nchi.
   Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere  Bi. Mossy Kitangita (kulia) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka  namna kitengo cha uongozaji wa ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kinavyofanya kazi na changamoto wanazokabiliana nazo.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS),Juma Mgoo wakikagua shamba la miti la Meru jana alipotembelea shamba la miti la mkoani Arusha.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu akikagua ujenzi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Ivume wilayani Siha mkoani Kilimanjaro alipoendesha harambee ya kuchangia ujenzi huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama akizungumza na viongozi wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa mikoa ya Arusha na Kilimanajaro kuhusiana na mgogoro wa katika eneo la Ndarakwayi logde iliyoteketezwa kabisa kwa moto na WANANCHI wa jamii ya wafugaji katika ugomvi wa ardhi ya kwa ajili ya malisho wakati Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu alipotembelea ili kumaliza mgogoro wa wananchi na mwekezaji.

  0 0

  Kamishina wa oporesheni na mafunzo wa jeshi la polisi, Paulo Chagonja akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa pikipiki 10 aina ya boxes kutoka kwa Kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium ya nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kupambana na swala zima la usalama barabarani.Katikati ni Mwenyekiti wa kampuni Hum Dalbit Petrolium Humprey Kariuki na Kushoto ni Mkurugenzi wa maswala ya Uhusiano wa Kampuni hiyo Magaret Mbaka.
  Baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiangalia pikipiki aina ya boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kupambana na swala zima la usalama barabarani.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya jeshi jijini Dar es Salaam
  Kamishina wa oporesheni na mafunzo wa jeshi la polisi Paulo Chagonja akijaribu kuendesha moja ya pikipiki aina ya boxes kati ya 10 zilizotolewa msaada na kampuni ya mafuta ya Dalbit Petrolium nchini kwa ajilia ya kusaidia kikosi cha usalama barabarani kwa kupambana na waalifu wa makosa mbalimbali.Kulia aliyevaa koti ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Humprey Kariuki.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kulifungua Jengo la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Wete Pemba (kushoto) Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu es Hesabu za Serikali Bi Fatma Mohamed Said (kulia kwa Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Wete Pemba jana (kushoto) Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu es Hesabu za Serikali Bi Fatma Mohamed Said.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Hawa Natepe (kulia) wa Kampuni ya STARS CONSTRUCTION LTD ambayo imejenga jingo hilo wakati ufunguzi rasmi wa Jengo la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Wete Pemba (kushoto) Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu es Hesabu za Serikali Bi Fatma Mohamed Said.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuzindua kitabu cha miaka 50 ya Utendaji wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali sambamba na Ufunguzi wa jingo la Ofisi uliofanyika jana Wete Pemba (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini na (kulia) Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Bi Fatma Mohamed Said.(PICHA na IKULU ZANZIBAR).

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kisumba, Jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM katika vijiji vya mkoa huo (Ijumaa 28/11/2014).
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akikumbatiana na mzee ambaye alikuwa mmoja wa wasikilizaji kwenye mkutano wa Operesheni Delete CCM uliofanyika katika Kijiji cha Samazi, mkoani Rukwa. Mzee huyo ambaye alitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba, alisema kuwa aliguswa sana na maneno ya Mwalimu.
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiagana na wananchi wa kijiji cha Kisumba baada ya mkutano huo wa hadhara kijijini hapo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu na msafara wake wakishiriki chakula walichoandaliwa na wenyeji wao katika Kijiji cha Samazi Jimbo la Kalambo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa mikutano mfululizo wa Operesheni Delete CCM mkoani Rukwa.

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha 

   JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili wakazi wa mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kupatikana na magunia 12 ya Bangi. 

   Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na askari waliokuwa doria. 

   Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea huko Desemba 2 mwaka huu majira ya 4.40 usiku kwenye pori la Vikawe kata Pangani wilaya ya Kibaha. 

   Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Sabas Petro (25) na Emily Magomba (21) ambao walikamatwa na askari waliokuwa doria. 

   “Watuhumiwa walikutwa wakishusha magunia hayo kwenye pori hilo kwa lengo la kuyaficha kutoka kwenye gari namba T 773 ELB,” alisema Kamanda Matei.

  0 0
  Today at 09:30am on 3rdDecember 2014, there was a fire threat at NBC Head Office building situated along Azikiwe and Sokoine Drive in the city center. All staff and customers were safely evacuated and accounted for. The NBC technicians and safety officers established an electrical fault at one of the cargo lifts that resulted in the triggering of the fire alarms. The fire brigade and police force responded to the scene.

  “The threat was contained and there was no damage to the people and property. And we assure our customers and the general public that everything is calm and we are back to our normal operations”, said Jimmy Myalize the Acting Chief Operating Officer of NBC.

  Due to the evacuation procedures at NBC, and the arrival of the fire brigade and police, may have caused some traffic congestion and anxiety of pedestrians within Dar es Salaam CBD. NBC sincerely apologizes for the inconvenience caused, and at the same assures customers and the general public that business resumed as usual immediately after the fire threat was contained.

  “We would like to assure our customers that everything is safe and we are committed to serving our customers in the most convenient and innovative manner to help our customers achieve their ambitions – in the right way.

  NBC has introduced exciting and innovative products into the market in the quest to make banking easier for customers in their journey to become the leading bank in Tanzania and to support their ambition of helping customers achieve their ambitions – in the right way. Among other banking services, NBC customers can also send money to their loved ones who do not have banking account through the bank’s Cash Popote product. Recipients are able to withdraw funds from any NBC ATM. 
   NBC is one of the most represented retail bank in the country with over 45 years experience in providing financial services. Apart from offering traditional banking services, NBC also prides itself with an expanded branch network of 52 branches and over 280 Visa enabled ATMs. The bank also services over 250 Points of Sales strategically located throughout the country. NBC has employed over 1300 staff.

  0 0

   
  KAMATI ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kupitia majina ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo. 
  Tuzo itafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee (VIP), Dar es Salaam, ambapo wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014 watakabidhiwa tuzo zao.
   Ni imani yetu kwamba zaidi ya wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo, ambapo kamati imejiridhisha kwamba wanaowania tuzo hiyo wanastahili kulingana na mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia Kamati zao za Ufundi.
   
  Mshindi wa kila tuzo ataingia katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2013/2014, ambapo pia siku hiyo ya sherehe za tuzo itatangazwa zawadi ya Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimichezo hapa nchini. Tuzo hizo ni kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014.
   
   
  OLIMPIKI MAALUM:
  Wanaume: Raphael Kalukula, Pazi Mwinyimkuu na Hatibu Matali
  wanawake: Blandina Blasi, Shida Jaha na Mwanaharusi Risasi.
  MPIRA WA KIKAPU;
  Wanaume:Lusajo Samwel (Oilers), Erick Mchemba (ABC)
  wanawake:Sajda Ahmed Lyamaiga(Don Bosco Lioness), Rehema Silomba (Don Bosco Lioness) na Orlyn Titus (Don Bosco Lioness).
   
  MPIRA WA MAGONGO;
  Wanaume:Yohana Wilson, Focus Paul, Deep Vaja
  Wanawake: Valentina Quarantta, Kidawa Seremala na Mary Mhina

  MPIRA WA WAVU:
  Wanawake: Yasinta Remmy (Jeshi Stars), Hellena Richard (Magereza) na Teddy  Abwao (Jeshi Stars).
  WanaumE: Kelvin Peter Severino (Magereza), Nassoro Sharifu (Jeshi Stars) na Athuman Rupia (Jeshi Stars).
   
  RIADHA:
  Wanawake: Zakia Mrisho, Jaqueline Sakilu na Catherine Lange
  Wanaume:Alphonce Felix, Dickson Marwa na Fabian Nelson.
   
  BAISKELI:
  Wanawake:  Salome Donald, Martha Anthon na Sophia Adson.
  Wanaume: Richard Laizer, Hamisi Mskala na  Gerald Konda,
   
  GOFU:
  Wanaume:Nuru Mollel, Abasi Adam na Frank Mwinuka
  Wanawake: Madina Iddi, Hawa Wanyeche na Angel Eaton
   
  GOFU YA KULIPWA:
  Hassan Kadio, Yassin Salehe na Geoffrey Leverian
   
  JUDO
  Wanaume: KOMBO Masoud Amour, MBAROUK MbaroukSleiman
  Wanawake: Grace Alfonce Mhanga, Salma  Omari Othman.
   
  TENISI WALEMAVU:
  Wanaume; Novatus Emmanuel TembaYohana  Assa Mwila, Juma Mohamed Hamisi
   Wanawake; Rehema Selemani Saidi,Bihawa Mustafa Ituji 
   
  TENISI:
  Wanaume: Tumaini Martin, Emmanuel Malya na Omari Sulle
  Wanawake: Rehema Athumani, Edna John, Georgina Kaindoh
   
  NETIBOLi:
  Doritha Mbunda (JKT Mbweni), Berina Kazinja (Magereza Moro), Andressa Andrea (Magereza Moro)
   
  Ngumi za Ridhaa: Fabian Gaudence, Ahmed Furahisha na Ally Abdul Ahmed
   
  SOKA;
  Wanawake:
  Sophia Mwasikili, Sherida Boniface na Amina Ally
   
  WANAUME
  Elias Maguli (Ruvu Shooting-sasa Simba), Erasto Nyoni (Azam FC) na Nadir Haroub (Yanga).
   
  WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
  Kipre Tchetche (Azam), Amis Tambwe (Simba) na Mbuyu Twite (Yanga).
   
  WATANZANIA WANAOCHEZA NJE
             Richard Laizer (baiskeli-Afrika Kusini/Uswisi)    
  Mbwana Sammata (TP Mazembe-soka DRC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-soka DRC).
  NGUMI KULIPWA, Francis Cheka, Ramadhani Shauri na Said Mbelwa.
   
  MPIRA WA MIKONO
  Wanaume: Hemedi Salehe (JKT), Msafiri Makoti (Ngome) na Abinery Kusena (JKT)
  Wanawake: Veronica Mapunda, Subira Omary na Mwajabu Lugato
   
  WANAMICHEZO CHIPUKIZI
  Omari Sulle (tenisi)
  Sheridah Boniface (soka wanawake)
  Aishi Manula (soka wanaume-Azam)
   
  MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2013/2014: ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA KATEGORI.
   
  TUZO YA HESHIMA:
  Itatangazwa ukumbini siku ya sherehe Desemba 12 mwaka huu.
   
  Rehure Nyaulawa
  Mwenyekiti Kamati ya Tuzo
  03/12/2014

  0 0

  A Tanzanian woman performs in the traditional dress of Zanzibar at the East African Urafiki Party in Seoul on Saturday. (Paul Kerry/The Korea Herald)

  The Tanzanians in Korea and the Kenya Community in Korea held their first East African Urafiki Party in Seoul on Saturday. 


  The party, named after the word for “friendship” in the two countries’ common language of Swahili, was a chance for people from both nations to sample some traditional cooking, while members also shared some cultural performances.  The performances included dancing by a group of Daejeon-based students from across Africa, a performance poem and a Tanzanian song and dance. One member even wrote a song for the event.  TANROK chairman Rayton Kwembe said the two groups initially came together informally.   “So then the leaders of TANROK and KCK decided to have a formal thing so we can expand the level of relationships and also try to integrate the East African Community,” he said, referring to an organization made up of the two countries, plus Rwanda, Burundi and Uganda.   The EAC has formed a common market and plans a currency union, and could eventually become a single federal state. South Sudan has sought membership but delayed its formal application.


  0 0  0 0

   Waziri  Lukuvi  akimkabidhi  mwanafunzi  wa shule ya Msingi Kipera Rahel Mwikonzi cheti  cha ushiriki mzuri wa siku ya  walemavu
  mwenyekiti wa baraza la watu wenye ulemavu Prof Edward Bagandashwa
  Kamishina  wa ustawi  wa jamii Bw Dunford Makala akitoa salam zake
  Walemavu  nchini  wakiwa katika maandamano  leo  wakati wa kilele  cha siku ya  walemavu duniani kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika  mkoa  wa Iringa,kushoto ni mkalimani  wa  kujitolea  ambae ni Mtangazaji wa radio  Nuru Fm Bw  Clement akisaidia  kuwaelekeza  walemavu hao. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya ametunukiwa Shahada ya Sayansi ya Jamii katika Siasa, Uongozi na Utawala (Political Science and Public Administration), baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya juu. 
  Mkotya pamoja na wahitimu wengine walitunukiwa shahada zao mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika eneo la Bungo, Kibaha mkoani Pwani. 
   Wahitimu wote walitunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Asha Rose Migiro, ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria. Katika mahafali hayo, mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd. Wengine ni Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Profesa Samuel Wangwe.
  Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya akipongezwa na wadau wenzie wa habari
  Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya na wahitimu wenzie. Kulia ni Bi Maura Mwingira ambaye ni Afisa Habari katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania New York  na kushoto ni Jane Maswe
  Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya akihojiwa na mtangazaji wa ITV ambaye naye kala nondozzz siku hiyo

  0 0

  Na Deusdedit Moshi
  Misiba ya vijana wawili, Marehemu Matei John Mmassy, Mfanyabiashara na mmiliki wa Klabu maarufu mjini hapa ya Matei Lounge na Wakili wa kujitegemea na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha St.John, Marehemu Joseph Joshua Oguda waliofariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ranchi ya mifugo, Narco iliyopo Kongwa mapema wiki hii wakitokea Mjini Morogoro vimetikisa mji wa Dodoma na Viunga vyake. 
  Miili ya marehemu hao imeagwa leo kuanzia mchana katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika Uwanja wa Nyerere mjiji Dodoma.Marehemu watasafirishwa jioni hii.Matei atasafirishwa kuelekea maziko Moshi Mkoani Kilimanjaro na Joshua atasafirishwa kuelekea Musoma.

   Baadhi ya mahakimu,wanasheria na mawakili waliojitokeza kushiriki kuagwa kwa marehemu Joshua na Matei
   Baadhi ya mahakimu,wanasheria na mawakili waliojitokeza kushiriki kuagwa kwa marehemu Joshua na Matei
   Baadhi ya mahakimu,wanasheria na mawakili waliojitokeza kushiriki kuagwa kwa marehemu Joshua na Matei
  Wakili wa kujitegemea Mhe. Anthony Mavunde ambaye alihitimu siku moja na marehemu Joshua.
  Majeneza yenye miili ya marehemu Joshua na Matei wakati wa ibada Uwanja wa Nyerere Dodoma.
   Mamia ya waombolezaji waliofurika katika Uwanja wa Nyerere mjini Dodoma kuaga miili ya marehemu Matei John Mmassy(mfanyabiashara) na marehemu Joseph Joshua Oguda Wakili wa kujitegemea na Mkufunzi katika Chuo Kikuu Cha St John wakiwa katika harakati za kutoa heshima za mwisho kwa miili nya marehemu.
  0 0  0 0

   Waziri  wa Biashara,  Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe: Nassor Ahmed Mazuri akipokea maandamano ya watu wenye ulemavu wakati wakipita mbele yake kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa kwa Zanzibar yaliofanyika mjini Chakechake, Pemba 
   Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri wa biashara na viwanda Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazuri aliekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye duniani ambayo kitaifa kwa Zanzibar yalifanyika mjini Chakechake Kisiwani Pemba
   
   Waziri  wa Biashara,  Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe: Nassor Ahmed Mazuri akiwapungia mkono watu wenye ulemavu wakati wakipita mbele yake kwa njia ya maandamano kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa kwa Zanzibar yaliofanyika mjini Chakechake, Pemba 
    Wanafunzi kutoka  Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba wakitumbuiza mshindo wa dufu kwenye maadhimisho ya siku ya watuwenye ulemavu duniani ambapo kitaifa kwa Zanzibar yaliofanyika mjini Chakechake, Pemba. 
   Afisa tawala mkoa wa kasakazini Pemba Khamis Salim Mohamed akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya watuwenye ulemavu dunia ambapo kitaifa kwa Zanzibar yaliofanyika mjini Chakechake Pemba. 
  Waziri wa Biashara, Viwanda na masoko Zanzibar Mhe: Nassor Ahmed Mazurui akizungumza na wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye duniani ambapo kitaifa kwa Zanzibara yaliofanyika kisiwani Pemba  Picha zote na Haji Nassor, Pemba

  0 0


  0 0

  Jumatatu tarehe 1-12-2014 Excutive Chef Issa Kipande maarufu kama Chef Issa alipata heshima kubwa sana ya kuonana na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe.  Dorah Msechu pamoja na Wafanyakazi wote wa ubalozi ambao walimpokea kwa furaha sana na kumpa pongezi nyingi wakijivunia ushindi alioupata nchini Luxembourg kwenye Mashindano ya Chef's World Cup 2014.
  Chef Issa ameiambia Globu ya Jamii leo kuwa  alifarijika sana kwa upendo, heshima na ushirikiano alioupata toka kwa Mheshimiwa balozi na wafanyakazi wote wa ubalozini hapo.
  "Inatia hamasa sana ya kuendelea kufanya mambo mazuri zaidi kutokana na mchango wa mawazo pamoja na kutambulika na kuheshimika kwa juhudi na mafanikio binafsi yanayoiletea sifa nchi yetu Tanzania. 
  " ASANTE SANA MAMA MHESHIMIWA BALOZI DORA MSECHU MOLA AKUJAALIE WEWE NA WAFANYAKAZI WOTE HAPO  UBALOZINI MAISHA MAREFU YA FURAHA NA AFYA NJEMA AMEEN UENDELEE KUTUWAKILISHA WATANZANIA TUNAOISHI SWEDEN " alisema Chef Issa.

  Akaongezea: "Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaliia kushiriki chef's world cup inafanyika kila baada ya miaka mnne kama football  world cup.

  "Ni heshima kubwa sana kwa nchi yangu nimeitendea haki nchi yangu kwa kupata tuzo ya mafanikio na badges ya utambuzi na first world touch smartwatch ooohhh baada ya timu nilivyokua nayo kushinda kombe la dunia la mapishi pia nimeandika historia ya kuwa Mwafrika  na mweusi pekee kushiriki mashindano haya. Nawashukuru sana wote mnaoniunga mkono kwa namna moja ama nyingine. Tupo pamoja ndugu zangu. Na ninaahidi kuwa sitawaangusha kamwe..."

  Ili kusoma habazi zilizopita pamoja na taarifa ya ushindi wa Chef Issa alioupata akiwa na Timu ya Stockholm iliyonyakua nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda (Regional teams) BOFYA HAPA

  Executive Chef Issa Kipande akiwa nje ya Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden.
  Executive Chef Issa Kipande akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipotembelea Ubalozini hapo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dorah Msechu baada ya kumpokea shujaa huyu hapo ubalozini.
  Executive Chef Issa Kipande akiwa pamoja na Balozi Dorah Msechu anayeshikilia kwa furaha na fahari medali ya ushindi  ya Chef Issa.

  Kupata mambo mengine kibao hebu M-Like 
  Chef Issa kwenye Facebook page yake hapa chini...
  https://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534?fref=ts

  0 0

older | 1 | .... | 660 | 661 | (Page 662) | 663 | 664 | .... | 3272 | newer