Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 659 | 660 | (Page 661) | 662 | 663 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla.

  Globu ya Jamii inaitakia kheri na fanaka Clouds FM katika kusherehekea miaka 15 tangu kuzaliwa kwake.
   Ndafu wa shughuli akiwa mezani
   Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
   Msanii mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
   Mkuu wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty.
   Dj Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo ya kutimizwa miaka 15 ya kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na kwingineko.
   Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.

  0 0

  Mwandishi wetu,Arusha

  WIZARA ya Fedha, imeitaka Bodi ya Wataalam wa Ugavi na Manunuzi nchni (PSPTB), kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kufanya manunuzi bila kuzingatia thamani halisi ya fedha na kuwataka waajiri kuacha mara moja kuwaajiri watu wasio na sifa kufanya kazi hizo

  Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua mkutano wa tano wa mwaka wa Siku mbili unaofanyika kwenye jengo la Mikutano la AICC jijini Arusha ambapo aliwataka Wataalamu hao kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao.

  Amesema katika bajeti ya mwaka 2014/15 serikali imetega bajeti ya Sh trilioni 20 kati ya hizo asilimia 65 hadi za 70 zinatumika kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali,hivyo taaluma hiyo kuwa na umuhimu wa kipee katika kudhibiti mapato ya serikali yasitumike vibaya.

  Awali Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Sr. Dk. Hellen Bandiho, amesema kauli mbiu ya mkutano huo “Thamani halisi ya fedha za Manunuzi” ikilenga kuhakikisha serikali inapata huduma bora kulingana na fedha inazotumia ili kuinua uchumi wa nchi.

  Amesema Bodi hiyo imezalisha wataalam zaidi ya 23,000 katika ngazi mbalimbali ambayo ni sawa na asilimia 47 pekee huku waajiri wengi wakiwa wamewajiri watumishi wasiosajiliwa na Bodi hiyo.
  Naibu Waziri wa Fedha,Adam Malima akiongoza na maafisa wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) katika mkutano wa Siku mbili unaofanyika kwenye kituo cha mikutano cha AICC, jijini Arusha.


  0 0
 • 12/02/14--06:23: YALE YALEEEE.....
 •  Uvunjifu wa Sheria za usalama barabarani hasa kutofuata utaratibu wa Taa za kuongozea magari umekuwa ni kitu cha kawaida kabisa siku hizi hapa jijini Dar es Salaam,Pichani ni msururu wa magari ukikatiza kwenye makutano ya Bamaga mbele kabisa ya pale zilipo Ofisi za Shirik al Utangazaji Nchini (TBC) na ili hali taaza kuongozea magari hayo zikionekana kuzuia.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na watendaji wa kampuni ya DermCappello yenye Ubia kati ya Watanzania na Waitalia waliofika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini ili kueleza nia yao ya kuzalisha umeme wa jua na kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme jua. Kutoka kushoto ni watendaji wa kampuni ya DermCapello, Eng. Steven Chaula, Capello Giuseppe na Giuseppe Capello. Kulia ni Mchumi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Nicolaus Moshi, Mwanasheria wa Wizara, Abbas Kisuju, na Eng. Innocent Luoga, kamishna Msaidizi Nishati anayeshughulikia Umeme.
  Rais wa kampuni ya Capello ya Italia, Capello Giuseppe akizungumza wakati wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini. Kampuni hiyo iliyoungana na watanzania na kuunda kampuni ya DermCapello walifika Wizara ya Nishati na Madini ili kueleza nia yao kuwekeza katika umeme wa jua.

  0 0

  Mdau Ramadhan Hussein ambaye ni Meneja wa Kiota maarufu jijini Mwanza "Villa Park",mwishoni mwa wiki iliyopia aliamua kuachana kabisa na Chama cha Makapera kwa kufunga pingu za maisha na Bi. Husna Salum mkazi wa huko Ukonga jijini Dar es Salaam.Ndoa yao hiyo ilifungwa katika Msikiti Mkubwa wa Ijumaa ulipo Airport,Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Mdau Ramadhan Hussein na Mamsapu wake Bi. Husna Salum wakionekana kuwa na nyuso za furaha mara baada ya kumeremeta kwao.
   
  Ni chereko chereko tu kwa kwenda mbele.
  Maharusi wakipokea nasaha kidogo kutika kwa Wazee (hawapo pichani).
  Wakiondoka nyumbani kwa Bi. Harusi.
  Pongezi kutoka kwa Imamu wa Msikiti.


  0 0

  DAWASCO inaomba radhi wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kwa kukosekana kwa huduma ya Maji kutoka katika mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini kwa wastani wa saa 72 kwa siku za Ijumaa hadi Jumatatu ya tarehe 28, 29  na 30 November 2014. 

  Kukosekana kwa huduma hii kulitokana na kazi ya mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Mpiji, Bagamoyo na eneo la Chuo Kikuu Ardhi (Makongo Juu).

  Tunapenda kuwajulisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa huduma ya Maji imerejea na mtambo wa Ruvu Chini umewashwa tarehe 2/12/2014 saa tano asubuhi.

  Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kulisababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; 
  Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. 

  Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.       
  Kumbuka kulipia huduma ya Maji unayotumia kila Mwezi.
  Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.

  0 0

  Mpiganaji Godfrey Monyo wa ITV na RadioOne (kati) akiwa na wahitimu wenzake katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam,wakati alipolamba Nondozz yake.
   Mdau Godfrey Monyo wa ITV na RadioOne (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wenzake mara baada ya kulamba nondozz zao katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam,Mwishoni mwa wiki.
   Monyo na Mdogo Wake.
  Mdau Godfrey Monyo wa ITV na RadioOne akiwa na Baba yake Mzee Zerubabeli Moyo mara baada ya kulamba Nondozz yake.

  0 0

  Rasilimali watu ni changamoto kubwa inayoikabili sekta ya afya nchini Tanzania. Upungufu huu unaathiri mfumo wa utoaji huduma bora na kwa wakati kwa wahitaji. Upungufu wa wahudumu wa afya  wenye ujuzi unaathiri ngazi zote za huduma na hasa vijijini. Kutokana  na wauguzi wakunga kuwa kiini katika utoaji  huduma za afya   vijijini na mijini kwa ujumla,  kuna umuhimu wa  wakunga hawa kupata elimu ya ujuzi  wa kutosha ili waweze kuwafikia wahitaji zaidi ya asilimia  sabini (70%)  ya  jumla ya wananchi wanaoishi vijijini.

  Katika kupambana na changamoto ya upungufu wa wahudumu wa afya hasa katika kulenga  kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, Amref Health Africa imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha taasisi, mashirika na watu binafsi kuchangia mafunzo ya wakunga watalaam   ili waweze kutoa huduma salama, sahihi na kwa wakati ili kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika wakati wa kujifungua.

  Jumla ya Wanafunzi 121 wamehitimu mafunzo ya uuguzi ukunga ngazi ya cheti katika chuo cha Muheza School of Nursing mkoani Tanga.  Miongoni mwa wanafunzi hao 9 walikuwa wakisoma kwa udhamini wa Barclays bank kupitia kampeni ya “Stand up for African Mothers” inayoendeshwa na Shirika la afya la Amref Health Africa Tanzania.

  Barclays Bank ni mshiriki mkubwa katika kampeni hii  na anatoa udhamini wa kusomesha wanafunzi  katika ngazi ya cheti na hivi leo  tumeshuhudia  wanafunzi 9 wamehitimu tayari kwa kwenda kutoa huduma katika jamii zinazowazunguka. Wahitimu hawa wanakwenda kufanya kazi maeneo ya vijijini Kama moja ya lengo na nia ya kampeni ya stand up for African mothers ambayo inalenga kupunguza vifo vya mama na mtoto hasa maeneo ya kijijini na yaliyo magumu kufikika.

  Juhudi za Amref Health Africa na Barclays bank  ni endelevu  na wito unatolewa  kwa mashirika, makampuni ya umma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi  kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga  kwa miaka miwili  yanagharimu dola 3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia

  Bank  account at Bank M, Kisutu Branch , Akaunti Namba  0250027331
  Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548
  Mpesa Namba 0762 22 33 48
  Tigo pesa Namba 0716 032 441
  Airtel money Namba 0685 506306.

  Stand Up For African mothers ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuelimisha na kutoa taarifa juu ya umuhimu na mchango wa wakunga wenye ujuzi katika kupunguza viofo vya mama na watoto wakati wa kujifungua.  Kampeni hii inayoendeshwa na Amref Health Africa inalenga kusomesha wakunga 15,000 katika nchi kumi na tatu za Africa wakati Tanzania ikitarajia kusomesha wakunga 3800.
  Dr. Pius Chaya,mkuu wa kitengo cha kujenga uwezo Amref Health Africa Tanzania akimuwakilisha Mkurugenzi , Dr. Festus Ilako wakati wa mahafali Chuo hapo.


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kisumba, Jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM katika vijiji vya mkoa huo
   Naibu akikumbatiana na mzee ambaye alikuwa mmoja wa wasikilizaji kwenye mkutano wa Operesheni Delete CCM uliofanyika katika Kijiji cha Samazi, mkoani Rukwa. Mzee huyo ambaye alitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba, alisema kuwa aliguswa sana na maneno ya Mwalimu.
   Naibu Katibu Mkuu akiagana na wananchi wa kijiji cha Kisumba baada ya mkutano huo wa hadhara kijijini hapo.
  Naibu Katibu mkuu na msafara wake wakishiriki chakula walichoandaliwa na wenyeji wao katika Kijiji cha Samazi Jimbo la Kalambo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa mikutano mfululizo wa Operesheni Delete CCM mkoani Rukwa.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Kulia akimsikiliza Aliyekuwa Mwenyekiti Baraza la Vijana la Chama cha wananchi CUF Wilaya ya Morogoro Ndugu Mariam Iswili aliyeamua Kurudisha Kadi ya Cuf na Kujiunga na Chama cha Mainduzi.Katika Tukio Hilo jumla ya wanacha 167 Kutoka Vyama vya CUF CHADEMA na NCCR MAGEUZI Walirudisha kadi zao na kusema vyama hivyo havina sera Mya zaidi ya Majungu na Maneno Mengi yasiyo na Tija kwa wananchi.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Kiwa na Kadi ya Cuf aliyoiokea.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akionyesha kazi alizokabidhiwa kuto kwa wanachama waliohama kutoka vyama vya CHADEMA  na CUF na Kuhamia CCM
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Za vyama vya chadema CUF na Nccr Mageuzi alizookea Kutoka kwa wanachama wa Vyama Hivyo na Kuamua Kujiunga na chama cha Mapinduzi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Kichama ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amewahakikishia wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwamba uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 unatarajiwa kuwa wa utulivu na amani. 
  Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya dola vitahakikisha kuwa vikundi vya kihuni vinavyoanza kuandaliwa kwa ajili ya kuvuruga uchaguzi huo itapambana navyo kwa nguvu zake zote. 
  Balozi Seif Ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza hayo wakati akihutubia Mkutano wa hadhara baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ndani ya Mkoa wa Magharibi Kichama akiwa mlezi wa CCM Mkoa huo uliofanyika katika uwanja wa Kwamabata Magogoni. 
  Alisema wananchi walio wengi wameshuhudia vitendo vya kihuni vilivyofanywa na vikundi vya Vijana kujaribu kuvuruga zoezi la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu mambo ambayo alisema hayatokubalika kutokea tena kwenye uchaguzi Mkuu ujao hapo mwakani. 
  Aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kujiepusha na wimbi la vikundi vilivyojikubalisha kujiingiza katika vitendo vya ugaidi ambayo kamwe havikubaliki Kitaifa wala Kimataifa. 
  Katika Mkutano huo wa hadhara Balozi Seif ambae pia ni Naibu Kamanda wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania aliwatawadha makamanda wa Vijana wa Majimbo na Wilaya zilizomo Mkoa wa Magharibi Kichama baada ya kuteuliwa na Baraza Kuu la UVCCM.
  Mapema asubuhi akizungumza katika Kikao cha Majumuisho ya ziara yake ya siku mbili akiwa mlezi wa CCM wa mkoa wa Magharibi hapo Tawi la CCM Mbweni Balozi Seif aliwataka Viongozi wa kamati za siasa za Matawi hadi Mkoa kutoogopa au kusemwa wakati wanapotekeleza majukumu yao. Akimkaribisha Mlezi wa CCM Mkoa huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf aliwaasa wananchi wa Majimbo ya Magogoni na Mtoni
   Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo la Kituo cha Afya cha Jimbo la Mtoni ambalo lililoanzishwa kwa mchango wa Wananchi na Viongozi waliopita wa jimbo hilo.
   Vijana wa matambuizo wa Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Mtoni wakifanya vitu vyao wakati wa mkutano wao na Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Balozi Seif aliyefanya ziara kukagua maendeleo ya Chama Mkoani humo.
   Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif akimkabidhi kadi mwanachama Thuwaiba Jeni Pandu akiwa miongoni mwa wanachama wapya wa CCM na Jumuia zake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Tawi la CCM Pangawe Jimbo la Fuoni.
  Wanachama wapya 50 wa Chama cha Mapinduzi na Jumuia zake wa Jimbo Jimbo la Fuoni wakila kiapo cha utii baada ya kukabidhiwa kadi kwenye mkutano wa hadhara hapo Tawi la CCM Pangawe. Picha na Hassan Issa wa  OMPR – ZNZ.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph ole Lenku (kulia), na Mkuu wa Polisi, David Kimaiyo ambae  amejiuzulu  muda mfupi leo  

  Kufuatia  shambulio  lililofanywa na  kundi la wanamgambo wa Al Shabaad  nchini Kenya kwa  kuwaua   watu  36 yaliyotokea  leo  ,mkuu wa polisi  nchini humu  David Kimaiyo anadaiwa  kutangaza  kujiuzulu nafasi  yake  hiyo.

  Mkuu   huyo wa  polisi amelazimika  kujiwajibisha  mwenyewe kwa  kujiuzulu  kutokana na mauwaji ya mara kwa mara  yanayofanywa na kundi  hilo la Al shabaad nchini  humo kwa  kipindi  cha siku takribani 8  ni  watu zaidi ya 60  wameuwawa  na kundi hilo wakiwemo  wale  waliotekwa katika basi na kumiminiwa  risasi na Al Shabaab .

  Suala  hili  la kujiwajibisha  kwa  wenzetu  Kenya  wanaweza  hasa  wakitambua kuwa  cheo ni  dhamana  ila ingekuwa  kwetu Tanzania kwa  kiongozi  kujiuzulu bila  kuundiwa  tume ni  vigumu  sana   

  0 0


  Watanzania tuungane na kumchagua mwenzetu Idris Sultan aweze shinda mashindano ya Big Brother Africa.Wiki hii ndio wiki ya mwisho na kinyang'anyori ni kikali kweli .Ila Idris ana nafasi nzuri ya kushinda
  tukimpigia kura.Ameweza kuonyesha ni mtu mwenye vipaji lukuki na kuweza kwenda mbali kwa vipaji alivyonavyo

   Mpe kura yako kwa  kupiga

   1.Kura ya bure kupitia mtandao na simu mara 100 bila gharama
  yoyote.Unachohitaji ni kuweka namba yako kwenye link ya DSTV na
  ku-press Idris mara 100 .Pitia hapa

   haichukui zaidi ya dakika tano

   2.Download  WeChat app kwenye smartphone yako, ongeza ID
  BigBrotherAfrica na  piga kura mara 100 bure !

   3.Tuma sms Vote Idris kwenda namba 15426 kupitia mitandao yote
  Tanzania.Unaweza fanya hivyo hata kwa mara 100 kwa siku haina noma!

   4.Sehemu nyingine Africa tuma sms Vote Idris kwenda 2783142100414 mara 100

   Asanteni


  How to Vote

  1.Vote for free up to 100 times on the website and again up to 100
  times on the mobile site

       FIRST register here
       https://connect.dstv.com/4.0.863/en-ZA/Login/?returnUrl=http%3A%2F%2Fbigbrotherafrica.dstv.com%2Fvote

       It will take you 5 minutes only to send 100 free votes to Idris
  2.Download the WeChat app on your smartphone, add ID BigBrotherAfrica
  and vote up to 100 times  FOR FREE !

  3.In Tanzania through sms " VOTE Idris" and send to 15426  Vote up to
  100 times by SMS (Vodacom,tiGO,Zantel,Airtel).You are charged Tsh 600
  only

  4.In Rest of Africa sms " VOTE Idris " and send to 2783142100414  Vote
  up to 100 times by SMS

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho kikwete katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na wafanyakazi wa ofisi ya CAG  Ikulu jijini Dar es salaam leo
   Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa  Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad na CAG Mstaafu Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo.  0 0  0 0

  DSC_0341
  Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000 Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

  Tanzania imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa wote (EFA).Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani imeweza kukaribia kufikia malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala la wastani wa waalimu kwa wanafunzi.

  Amesema kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi 47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 27. Mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya mpango huo ni kuboresha wastani wa wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania Bara wastani umetoka kuwa wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi 65 huku Zanzibar wastani ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
  DSC_0288
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA ulioshirikisha wadau wote wa sekta ya elimu uliofanyika jijini Dar Es Salaam. Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuiandaa Tanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mashauriano ya kiserikali baina nchi mbalimbali na kuhakikisha wadau wakuu wa elimu kitaifa wanapata taarifa juu ya mapendekezo ya agenda zitakazoanza mwaka 2015.

  Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.

  Bi. Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha , wadau, usimamizi na uwajibikaji.
  DSC_0224
  Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa elimu kutoka bara na visiwani wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kutekeleza malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote –EFA.

  Katika mkutano huo imeelezwa kwa sasa hakuna tatizo la uwiano wa wanafunzi wa kike na wa kiume kwa kuwa jinsia zote zipo darasani katika uwiano unaoridhisha unaokaribia wastani wa 50/50, lakini pia kigezo kingine ni uwiano wa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari ambapo bado kumeonyesha kuwa na mapungufu hivyo kazi ya ziada inahitajika.

  Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa nchi wahusika kujitathimini zimefikia wapi katika utekelezaji wa malengo waliyojiweke ya Mpango wa Elimu kwa Wote-EFA kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi 2015 na kujiwekea mikakati mipya.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  SONY DSCKaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Aliyenyanyua mikono) akitoa maelezo juu ya sehemu zitakazoendelezwa kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.SONY DSCKiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia tabaka za udongo uliotumika katika kujengea Kiwanja cha Ndege Kigoma. Anayemuonesha ni Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende (Kulia).
  SONY DSCMeneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha (Wapili kulia) akionesha eneo likaloboreshwa katika Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma.
  ………………………………………………………………………………………
  Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
  Serikali imeazimia kuanza kufanya utanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ili kuweza kukidhi mahitaji yanaongeza siku baada ya siku ya kiwanja hicho.
  Azma imetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
  Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini ipo kwenye mkakati wa kuuendeleza uwanja huo ili uwe wa kiwango kizuri kwa kuhudumia watumiaji wa wa kiwanja hicho.
  “Kama munavyokumbuka Serikali katika mwaka ujao wa fedha imepanga kuendeleza na kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi; na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati ikiwamo Kiwanja cha Ndege cha Kigoma,” alisema.
  Kwa mujibu wa Bibi Mwanri, uendelezaji wa Kiwanja hicho utajumuisha ujenzi wa jengo la abiria pamoja na miundombinu yake (maegesho ya ndege, maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka) na kurefusha barabara ya kuruka na kutua ndege.
  Akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya uwanja huo, Meneja Mradi wa Utanuzi wa Kiwanja cha Kigoma, Mhandisi Neema Mwasha alisema kuwa mpaka sasa Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini imekamilisha taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa usalama na eneo la maegesho ya ndege.
  “Kwa sasa tunaendelea na kazi ya utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya kazi za ujenzi wa barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari, na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa maegesho ya ndege pamoja na usimikaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege,” alisema.
  Mhandisi Neema aliongeza kuwa wapo kwenye mchakato wa kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya usanifu wa jengo la abiria uwanjani hapo.
  Naye Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege Kigoma, Bw. Joseph Nyahende alisema kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini kwa kushirikiana na Mkoa wa Kigoma vimeainisha na kufanyia tathmini eneo litakalotumika kwa ajili ya kazi hiyo.

  0 0

   Ujumbe wa Watalaamu wa masuala wa ICT, Ulinzi na Ujenzi kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) uko kwenye ziara ya mafunzo ( Study tour ) katika Mamlaka ya Bandari Ghana (GPHA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ya kuongeza ufanisi wa utekelezaji na kuimarisha Ulinzi wa Bandari, ujumbe wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa Mkurugenzi wa ICT - TPA .

  Kwa sasa TPA inatekeleza miradi kadhaa ya kuongeza ufanisi kwa kutumia ICT, kuboresha  Ulinzi kwa kufunga Mitambo ya kielektroniki na kuongeza vifaa na maeneo ya operations ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari za Dar, Mtwara na Ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo na Mwambani Tanga.
   Ujumbe wa TPA ukiongozwa na Ndg. Magesa wakiwa kwenye mazungumzo na wenyeji wao kutoka Mamlaka ya Bandari ya Ghana kufanya majumuisho ya ziara .
    Watalaamu wa TPA wakiwa kwenye chumba Chenye vifaa vya kielektroniki Cha kuangalia matukio ya kuilinzi na ki usalama katika Bandari ya Tema
  Watalaamu wa TPA toka idara za Ujenzi, TEHAMA na Ulinzi wakiangalia Ujenzi wa Magati manne ya kisasa katika Bandari ya Tema , Ghana
  Watalaamu wa TPA wakiangalia lango la kuingia bandarini ambazo lina vifaa maalumu vya ki electronic vya kutambua magari, makasha na dereva bila kusimamia.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto), akipokea ripoti ya maoni inayohusu mabadiliko ya Tabianchi kutoka kwa Uester Kibona ambaye ni mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (FORUM CC).
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge  (wa kwanza kushoto) na Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), wakisikiliza kwa makini ripoti ya maoni inayohusu mabadiliko ya Tabianchi itakayowasilishwa huko Peru hivi karibuni ,ikitolewa na  Uester Kibona ambaye ni mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira  (FORUM CC).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto) pamoja na  Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira  (FORUM CC). 

  0 0

  Sumai Kazi (with white dress) akiwa na dada ake wakiingia eneo la ukumbi kwa kutumia boat maalum ili kujumuika na ndugu jamaa na marafiki waliofika Jembe Beach kushuhudia Send Of Party yake.
  Wakishuka kwa kutumia ghati tayari kuingia ukumbini.
  Sumai (L) akiwa na dadayake (R) sanjari body guard wake. 
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 659 | 660 | (Page 661) | 662 | 663 | .... | 3278 | newer