Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 658 | 659 | (Page 660) | 661 | 662 | .... | 3278 | newer

  0 0

  MKAZI wa Kijichi Jijini Dar es Salaam, Samson Marwa amejishindia nafasi ya kutembelea hifadhi ya wanyama ya Selous katika droo inayoendeshwa na bia ya Ndovu kupitia kampeini yake ya ‘Ndovu Golden Experience’.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu Victoria Kimaro alisema, mshindi huyu ameibuka kidedea baada ya kuwagaragaza wenzake katika kampeini hiyo na kupata nafasi ya kwenda katika hiyo hifadhi na mtu mmoja.

  Victoria alisema, lengo la kuanzisha kampeini hiyo, ni kuwapa fursa watanzania kujivunia rasilimali zao, hasa kumlinda mnyama Tembo ambaye anaibeba nembo ya bia hiyo.

  “Naimani kuwa, washindi wayafarijika mno kutembelea hiyo mbuga kwani, watapata nafasi ya kuwaona wanyama wengi mno akiwemo Tembo, na pia sisi kama Ndovu tutawagharia washindi Malazi, Chakula pamoja na usafiri,”alisema. Aliongeza kwa kuwataka watanzania kuitumia nafasi hiyo, kabla ya droo hiyo kufikia tamati wiki ijayo, na washindi wanne kupatikana ambao wataambatana na wenzao wanne ambao kila mmoja atachagua.

  Naye Inspekta wa kampuni ya Gaming Board of Tanzania, Humud Semvua ambao ndio wachezeshaji wa droo ya kuwapata washindi aliwapongeza watanzania kwa kuchangamkia fursa hiyo adimu kutokana na wageni wengi kutembelea hifadhi hizo.

  “Watanzania wamejitokeza kwa wingi na kufungua chini ya kizibo, wiki iliyopita tulipompata mshindi watu 3754 walituma meseji na wiki hii ambayo tumempata Samson zaidi ya watanzania 4390 wametuma meseji, hivyo inaonyesha jinsi gani watanzania walivyoamka na kuthamini maliasili zao,”alisema.
  Mwakilishi kutoka Kampuni ya, AIM GROUP LIMITED, Emma Edward akichezesha droo ya tatu kupitia Bia ya Ndovu Special Malt wakati wa kumtangaza mshindi wa tatu atakayetembelea hifadhi ya wanyama ya Selous Dar es Salaam jana (kulia) ni Meneja wa Bia hiyo, Victoria Kimaro na (katikati) ni Ofisa wa Mwandamizi wa Bodi ya inayosimamia michezo ya kubahatisha, Humudi Semvua.
  Meneja wa Bia ya Ndovu, Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati alipokuwa akimtangaza mshindi wa tatu katika droo ya tatu ya bia hiyo (kushoto) ni Ofisa Mwandamizi wa Bodi inayosimamia michezo ya kubahatisha, Humudi Semvua.

  0 0

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland ya Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na uhamasishaji wa uwekezaji na maendeleo ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development). 
  Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja cha “Stadium of Light”, kinachomilikiwa na Sunderland Association Football Club (SAFC).

  Tukio hilo lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe, Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Watanzania waishio nchini Uingereza pamoja na baadhi ya maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania.

  Wakati wa uzinduzi huo katika kingo za kuta za uwanja yalionekana matangazo yanayotangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo kulikuwa na mechi kati ya timu ya Sunderland na Chelsea FC iliyorushwa moja kwa moja na kituo kinachorusha mechi mbalimbali za mpira wa miguu cha DSTV. Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland walionekana wakiwa wamevaa jezi maalum  zilizoandikwa ‘Visit Tanzania’ wakati wakifanya mazoezi kabla ya mechi hiyo.

  Bodi ya Utalii Tanzania imetumia fursa ya mechi hiyo kuhamasisha wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Uingereza pamoja na mashabiki wa Timu hizo wa nchi zote duniani kutembelea vivutio vya utalii wa Tanzania.


  Imetolewa na

  BODI YA UTALII TANZANI


  01/12/2014


  0 0

    Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa matembezi ya maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar.
     Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbalimbali  wakiongozwa na Brass band yaJeshi la Polisi,wakiwa kwenye uzinduzi wa matembezi ya maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar.
   Baadhi ya Askari Jamii wakiwa kwenye uzinduzi wa matembezi ya maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar. 
  Baadhi ya Maofisa wa Polisi wakisubiri  kupokea matembezi ya uzinduzi wa maadhimisho  ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto yaliyofanyika katika viwanja vya Oysterbay Polisi,leo Jijin Dar. 

  0 0

  Wa pili kulia ni katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Dkt Omar Dadi Shajak, Kushoto Mkurugenzi wa Mazingira Offisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu, Nyuma KUlia MKurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais ambae pia ni Mtaalamu wa Mabadiliko ya Taibia Nchi wakifuatilia hotuba ya  Ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabia Nchi MJini Lima Nchini Peru. 

  Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia  sehemu nyingine ya ufunguzi wa chombo cha utekelezaji SBI katika mkutano wa 20 wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabia nchi ulioanza rasmi leo Mjini Lima, Peru.
  Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais

  0 0
 • 12/01/14--11:05: Article 6


 • 0 0

  Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa leo amehudhuria maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyoadhimishwa na Manispaa ya Ilala kwenye kata ya Vingunguti na ametumia fursa hiyo kuhamasisha wanaume kupima VVU kwani takwimu zinaonyesha asilimia ndogo ya wanaume wanajitokeza kupima.
  Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akipatiwa maelezo kutoka kwa  mmoja wa wataalamu wa maswala ya VVU wakati alipotembelea maadhimisho hayo.
  Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akipatiwa ushauri nasaha kutoka kwa Daktari kabla ya kuamua kupima VVU.
  Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akipima VVU.
  Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mstahiki Jerry Silaa akizungumza wakati akiwahamasisha vijana na watu mbali mbali kuwa na utamaduni wa kupima afya zao wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyoadhimishwa na Manispaa ya Ilala kwenye kata ya Vingunguti.

  0 0

   By Alex Kajumulo
  To be a legend you have to work with legends. In the pictures I am with my professor, professor Neto, the FIFA technical advisor who's sits on the technical committee. He also taught many many coaches around the world and happens to be my professor. 
  This man is very important for African soccer. He is the one who helped Africans to start their own soccer association. When there was no one who was helping he was fighting to have more African teams in the world cup championship...
  If you read the football soccer association for African is under a Portuguese name. Not English or Dutch. The Portuguese colonized 3 countries, not that many. But the brazilians who care about Africa like professor Neto stepped up. 
  To start the confederation football African. This is where I got my modern coaching certificate diploma and my technical tactical degree under Brazilian soccer. Like I said, to be a legend you have to work with legends. Now he happens to be my best friend. Even today he is the technical advisor of FIFA. It is an honor to work with this kind of man.
  Professor Neto with Alex Kajumulo, Jamhuri Kihwelu 'Julio' and an unidentified player during a training session in Brazil

  0 0

  EAC Deputy Secretary General in charge of Productive
  and Social Sectors Hon. Jesca Eriyo
  The 1st East African Community (EAC) Youth Conference themed The EAC Youth: Think. Speak. Participate is scheduled to take place 5 to 6 December 2014 at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. 
   According to the EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors Hon. Jesca Eriyo, the 1st EAC Youth conference is the first formal process of engaging the Youth in the region following the adoption of the EAC Youth Policy by the EAC Council of Ministers In August 2013. 
  The Policy guides the Community in planning, implementing, monitoring and evaluating programmes geared towards the youth in the region while ensuring sustainable social, economic and political development. 
   The theme of the Youth Conference will be realised through discussions on a number of interrelated sub themes including; entrepreneurship, employment, skills development and innovation; leadership, governance, peace building, human rights and conflict management; creativity, expression and transformation; youth and sexual reproductive health and substance abuse; and youth: environment, climate change adaptation and mitigation. 
   The EAC Youth Conference is expected to bring together over 200 youths drawn from diverse backgrounds taking into account gender, marginalised youth, rural youth, youth living with disabilities, youth in slum dwellings, among others. 
  Other participants include Government officials, Young Parliamentarians, PSOs, CSOs, professional bodies, Academia/Universities, Media and EAC Organs and Institutions, Development Partners and other interest groups. 
   Youth participation in EAC affairs is provided for under Article 120 (c) of the EAC Treaty, which provides for adoption of a common approach for the participation of youth in the integration process through education, training and mainstreaming across EAC policies, programmes and projects as one of the strategic interventions towards the realization of a fully integrated Community. 
  Youth participation is also grounded in the EAC Youth Policy, the 4th EAC Development Strategy (2011 – 2016) and the EAC Strategic Plan on Gender, Youth, Children, Social Protection and Community Development (2012-2016). 
   In furtherance of the aforementioned provisions, the EAC Secretariat has undertaken a series of interventions aimed at ensuring a more meaningful involvement of the youth in the integration process. Recent initiatives include the convening of the EAC Youth Summit in Arusha, Tanzania 2007 and the 1st, 2nd and 3rd EAC University Students Debates on regional integration in August 2012, August 2013, and September 2014 respectively. 
  The 2nd EAC University debate resulted into the formation of the EAC Youth Ambassador’s Platform as an information infrastructure that would accelerate a youth-focused integration through knowledge and experience sharing from the EAC and within the youth communities across the region. 
   The youth civil society fraternity in the EAC has also been active through different initiatives to create opportunities for their own engagement with the EAC processes with the recent establishment of the East African Youth Network (EAYN) as a positive step towards a platform to amplify their voices for collective advocacy and engagement. 
  The EAYN is composed of youth CSO’s and National Youth Councils in the Partner States. The EAC interventions as well as those of the youth civil society in the region have focused on addressing the contemporary youth challenges such as unemployment, high HIV-AIDS prevalence rate, drugs and substance abuse, low participation of the youths in development among others. 
   Therefore, the 1st EAC Youth Conference is convened as a platform to disseminate the Youth policy, strengthen existing pillars as well as set new strategies for more sustained and meaningful engagement of the youth in the overall EAC integration agenda.

  0 0


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi, kwa pamoja wakisimama kupokea maandamano wakati wa sherehe za Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika leo Desemba 1, 2014 Kitaifa kwenye Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo, Desemba 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo, Desemba 2014. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
 • 12/02/14--02:57: TAARIFA YA MSIBA
 • Familia ya Captain Narcis Mapunda wa Mikocheni B (TPDC) Dar es salaam, kwa masikitiko na huzuni wanatoa taaifa ya msiba wa mtoto wao mpendwa; ELIAS NARCIS MAPUNDA Kifo hicho kilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 28 November 2014 hapa jijini Dar es salaam. 

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Baba mzazi Captain Narcis Mapunda, pale mikocheni, Nyumbu Street (pandisha mtaa wa mikocheni Wariob tokea Mwai Kibaki Rd, baada ya Kanisa la Mt Martha ingia mtaa unaofuata kulia).

  Maandalizi ya awali yanalekea kuwa na ratiba ifuatayo ya mazishi; mazishi yatafanyika kinondoni Makaburi ya Jumuiya ya Madola (ndani ya ukuta) siku ya alhamisi tarehe 4 December 2014 majira ya saa 10 jioni (1600 hrs).

  Awali ya hapo kutakuwepo misa fupi, chakula pamoja na za heshima za mwisho nyumbani kwa Capt Mapunda, ikifuatiwa na misa maalum pale jirani kanisa la Mt Martha. Ratiba ya shughuli zote inatarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi ya siku hiyo (1000hrs).

  Habari za msiba huu ziwafikie wana-Mapunda popote pale walipo pamoja na nduguwote na marafiki.

  Waweza kumpigia Mama Suzanne Mapunda kwa kujua taarifa zaidi - 0754 884104.

  0 0

  Na Saidi Mkabakuli, Mpanda

  Kufuatia kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali imewaasa watumiaji wa uwanja huo kutunza miundombino ya uwanja huo ili kuweza kuhudumia wakazi na wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.

  Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi.

  Bibi Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imekamilisha kazi ya kuufanya uwanja huo uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara, hivyo uongozi wa uwanja huo hawana budi ya kuhakikisha miundombinu ya uwanja huo inatunzwa ipasavyo.

  “Kama munavyofahamu Serikali imekuwa ikiwekeza sana katika uendelezaji wa miundombinu ya usafiri nchini hasa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri wa anga ili kuongeza ufanisi na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati, hivyo kuna haja ya kuunga mkono jitihada hizi za Serikali,” aliasa Bibi Mwanri.

  Akitoa taarifa ya uendelezaji uwanja huo kwa msafara wa timu ya ukaguzi, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.

  “Uwanja huu umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30,” alisema Bw. Lyatuu.

  Kwa mujibu wa Meneja huyo, kukamilika kwa uwanja huo kumevutia idadi ya abiria wanaoutumia uwanja huo kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.

  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16),  Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na TEHAMA.

  Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. 

  Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.

  Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo uwanjani hapo.
  Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia). Anayefuatilia mazungumzo ni Bw. Omary Abdallah ambaye Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango).


  0 0

  Mratibu wa Uhurumarathon Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam wakati akielezea juu ya udhamini wa kampuni ya startimes kudhamini kwa kutoa matangazo na vifaa vyenye Zaidi ya shilingi milioni nne na laki tano.Kushoto kwake ni meneja huduma kwa wateja wa startimes Jackson Ngowi

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari,Wengine katika picha maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari kushoto ni Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,kulia Mkurugenzi Mtendaji Andrew Mboma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti ya Vinjari Andrew Mboma(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari, Wengine katika picha Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(katikati) kushoto ni Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji.
  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kushoto)akipongezana na maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari (katikati ) Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,(kulia )Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti hiyo Andrew Mboma wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti hiyo.


  0 0

  Msimu wa pili wa tamthilia ya Siri ya Mtungi itazinduliwa rasmi Desemba 7 kupitia televisheni ya Taifa (TBC). Akizungumza jijini leo mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza. 
  Kamin alisema kuwa kukamilika kwa hatua ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins University Centre for Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii na MFDI. Alisema kuwa sehemu hii ndiyo inatoa majibu ya msimu wa kwanza na kuwataka mashabiki watamthilia hii kuangalia TBC kuanza saa 12.30 jioni kupitia TBC. “Msimu wa kwanza wa tamthilia ya Siri ya Mtungi uliwavutia watu wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki na kuwaachia maswali kibao na hii imetokana na tamthilia kubeba vionjo halisi vya maisha katika jamii na hasa kwa wakazi wa mikoa ya Pwani ya Tanzania,” alisema Kamin. 
  Alisema kuwa mapokeo mazuri kutoka kwa watazamaji kuliwapa nafasi ya kuingia katika vipengele saba vya tuzo za M-Net Africa Magic Viewers Choice Awards mwaka 2014 ambavyo ni TV Series, Make Up, Wardrobe, Art Direction, Sound Editor, Acting, and Indigenous Language Series.
   “Msimu wa kwanza ulikuwa hewani katika vipindi vya miaka miwili tangu mwezi Desemba mwaka jana kupitia vituo vya televisheni vya ITV/EATV na baadaye kurushwa hewani kupitia DTV, TV1, MNet Africa Magic, Maisha Magic kabla ya msimu huu kupitia televisheni ya TBC,” alisema. 
  Kwa mujibu wa Kamin, mpaka sasa wanajivunia kupata mapokeo mazuri kwenye mitandao ya kijamii na hasa facebook kwa kupata mashabiki 200,000 na kwenye YouTube ambapo tumepata watazamaji zaidi ya 500,000 kwani tamthilia hii imepata umaarufu mkubwa kwa kutazamwa na mashabiki wengi kuliko vipindi mbali mbali vya televisheni hapa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki. 
  Alisema kuwa Siri ya Mtungi ni hadithi ya Kitanzania ambapo wametumia siku 86 kukamilisha kurekodi. Alisema mbali ya kuwashirikisha waigizaji maarufu kama yvonne Cherie maarufu kwa jina la Monalisa, pia imewashirikisha warembo maarufu kutoka Miss Tanzania kama Richa Adhia na Jokate Mwegelo. 
  “Tumetoa ajira kwa waigizaji 60 ambao walipatikana baada ya mchujo wa watu 2,500,” alisema.
   Mtayarishaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi  Louise Kamin kutoka  Shirika Lisilo la Kiserikali la  Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa pili na wa mwisho wa tamthilia hiyo. Kutoka kulia kwa Kamin ni Karabani (Muongozaji), Cheche (Muigizaji), Jordan Riber (Muongozaji). Kutoka kushoto ni Goldliver Gordian (cheusi) na David Michael (Duma).
   Cheche akizungumza katika mkutano huo.
   Muongozaji wa tamthilia hiyo, Karabani akisisitiza jambo katika mkutano huo.
  Muongozaji , Jordan Riber akifafanua jambo katika mkutano huo.

  0 0

  Wazazi nchini Tanzania wametakiwa kuzungumza na watoto wao umuhimu wa elimu na hali halisi ya maisha ili kuepuka kujiingiza kwenye vitendo viovu  ikiwamo mimba za utotoni na maambukizi ya ukimwi.

  Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) Lulu Ng'wanakilala katika maadhimisho ya kupinga unyanyasajji kwa watoto pamoja na maambukizi ya ukimwi nchini.

  "Wazazi na jamii kwa ujumla wanapaswa kukemea tabia ya unyanyasaji hasa wanafunzi wanaofanyiwa na makondakta wa dala dala, wanapowasukuma kuwazuia kupanda na huku wengine wakitumia fursa hiyo ya shida  ya usafiri kuwahadaa watoto wa kike kwa kuwataka kimapenzi.

  "Kuna wanaume watu wazima lakini wana kazi ya kuwatongoza watoto wadogo kwa kuwahada na pesa, zawadi kwa lengo la kuwashawishi na kujaamia nayo, makonda wa dala dala nao ndio usiseme, jamii inapaswa kukemea kwa nguvu zote jambo hili, kwa kuwachukulia hatua bila hivyo vitendo hivyo viovu haviwezi kuisha.

  "Watu wazima wanashuhudia wanafunzi wanavyosukumwa na makondakta na kuambiwa wasipande dala dala, wao wanapanda wanawaacha wanafunzi chini, si haki kabisa, kupitia  mradi huu wa jamvi la vijana tunapiga vita unyanyasaji wa vijana kwa nguvu zote." alisema Ng'wanakilala.

  Alisema pia kupitia mradi huo wa Jamvi la Vijana, wamekuwa wakitoa elimu kwa vijana ikiwemo kupima kwa hiyari maambukizi ya VVU, saratani ya shingo ya kizazi kwa kuwa moja ya sababu ya ugojwa huo ni kujiingiza kwenye vitendo vya ngono zisizo salama katika umri mdogo.

  "Tanzania hii kuna maeneo mtoto wa miaka tisa ana mtoto, wazazi wanawafukuza nyumbani huu ni ukatili wa hali ya juu, ukatili kwa kupewa mimba akiwa na umri mdogo, na ukatili kwa kufukuzwa nyumbani  ndio chanzo kikuu cha watoto wa mitaani na wengine kuamua kuwatupa na hata kuwaua, ndio maana tumeamua tutoe elimu hii kwa vijana.

  Alisema kupitia mradi huo wa Jamvi la Vijana ambao wanazunguka sehemu mbalimbali lengo lao ni kuwafikia vijana 200 kila mwezi na vijana 1,000 kwa mwaka.
  Mkurugenzi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Lulu Ng'wanakilala (kushoto) akizungumza katika tamasha la Jamvi la Vijana lililofanyika kwenye ofisi za Umati Temeke,jijini Dar es Salaam. kulia ni ofisa habari wa Umati, Upendo Daud.
  Sehemu ya vijana waliojitokeza kwenye tamasha hilo
  Sehemu ya washiriki kwenye igizo linalopinga unyanyasaji kwa vijana.

  0 0

  Kampuni ya Bima ya REAL Tanzania sasa imekuwa ni moja kati ya makampuni makubwa  rasmi chini ya Kampuni ya Britam ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha. Hii inafuatia kununuliwa wa Kampuni hiyo ya Bima na Kampuni ya Britam kutoka Kenya. 

  Kufutia hatua hiyo Kampuni ya REAL itakuwa na wigo mpana wa kutoa huduma za bima zikiwemo bima za Afya na Bima za maisha  ambazo tayari kampuni ya Britam imekuwa ikitoa kwa muda mrefu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Muungano huu utaboresha huduma za bima nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambayo kwa sasa Britam inanguvu ya kifedha, kiteknolojia na rasilimali watu. 

  Kufutia hatua hii, Britam sasa inaongoza kwa ukubwa wa kijografia kuliko Kampuni zoter za Bima Afrika Mashariki, pia Kampuni hiyo inashikilia nafasi ya pili kulingana na pato la ziada.

  Mchakato wa ushirikiano na muungano wa Kampuni hizo mbili umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa sasa na kufuatiwa na kupata kibali  kutoka kwa mdhibiti wa Mamlaka ya Masoko na  Mitaji ya nchini Kenya na kutekelezwa na washiriki  kutoka Britam na REAL kwa kusaidiwa na Kampuni ya Usimamizi wa Kimataifa ya Mckinsey na washauri wengine.

  “Kutokana na muungano wa Kampuni hizi mbili, uwepo wetu umekuwa kwa sehemu kubwa sana,” alisema Bwana Peter Munga, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REAL na Britam Tanzania.

  Bwana Munga  aliendelea kusema kwamba muungano huo ni moja kati ya makampuni ya kutoa huduma za Bima katika Afrika Mashariki, kwani sasa Kampuni hizo zinatoa huduma katika nchi 7 tofauti ambazo ni; Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini, Malawi na Msumbiji.

  Pia aliwahakikishia wamiliki wa hisa, wauzaji, watoa huduma za bima na wadau wengine kwamba wote wenye mikataba na Kampuni hizo mbili bado zitaendela kudumu hadi mwishoni mwa mwaka na kila Kampuni itawajibika kwa madeni yeyote wanaodaiwa kwa kipindi kilichobaki.

  Kuungana kwa Kampuni hizo mbili ni fursa kwa Britam kuongeza uwepo wake katika soko la kitaifa na Afrika Mashariki na pia kuongoza soko katika biashara zote ambazo inazifanya.

  Muungano wa Kampuni hizo mbili pia unaonekana kama hatua ya kwanza ya kuimarisha sekta ya Bima Tanzania ambayo ina ushindani mkubwa. Soko la Bima Tanzania lina zaidi ya makampuni 29 yanayofanya kazi katika soko hilo.

  Muungano huu inaiwezesha Britam kutekeleza mkakati wake we kupanua biashara yake ya Bima na pia kutoa huduma zingine mbalimbali katika maeneo muhimu ya kijografia kama Tanzania ambayo yameonyesha uwezo mkubwa wa kukuwa kiuchumi barani Afrika.

  0 0

   Jacquline Shija Mazemle, aliyewezeshwa na TBL na kufanikiwa kuanzisha mghahawa maarufu wa FACEBOOK, ulioko karibu na Chuo Kikuu cha Kampala, Gongo la Mboto, Dar es Salaam. Akiandaa chakula na wenzake Ramadhan Seleman kushoto na Hans Shija
   Akiwahudumia na wateja wa Facebook
   Dorren Asey aliyewezeshwa na TBL kutengeneza mikate, keki na maandazi kupitia kampuni yake ya Dee Bakery,Doreen akiandaa mikate.

  0 0
 • 12/02/14--05:33: Congratulation Note


older | 1 | .... | 658 | 659 | (Page 660) | 661 | 662 | .... | 3278 | newer