Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

RAIS DK SHEIN AHUDHURIA MAULIDI YA MTUME, TEMEKE JIJINI DAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Sheikh Alhad Mussa Salum,alipowasili katika msikiti Masjid majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho kuhudhuria katika maulid ya Mtume Muhamad SAW.
Sheikh,Dk.Usama Mohammed Esmail,kutoka nchini Misri akitoa mawaidha wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho,yaliyohudhuriwa na Viongozi wa Dini mbali mbali,na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Sheikh Alhad Mussa Salum,wa Mkoa wa Dar es Salaam,akiwatambulisha wageni mbali mbali waliohudhuria katika Maulid ya Mtume S.A.W. yaliyohudhuriwa na maelfu ya waumini wa Jiji la Dar es Salaam,katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.
Sheikh Alhad Mussa Salum,wa Mkoa wa Dar es Salaam,akiwatambulisha wageni mbali mbali waliohudhuria katika Maulid ya Mtume S.A.W. yaliyohudhuriwa na maelfu ya waumini wa Jiji la Dar es Salaam,katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwaongoza Viongozi mbali mbali wa Dini na Serikali katika Maulid ya Mtume Muhammad S.A.W yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.
Wanamadrasatul Az-har ya Koma Kisiwani Dar es Salaam,wakisoma Qaswida Ya swalatu Alan Nabii,katika Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Jijini Dar es Salaam,waliohudhuria katika Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Kumswalia Mtume Muhammad SAW,yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

RICHARD COMMEY NDIYE MFALME WA UZITO MWEPESI KATIKA BARA LA AFRIKA

$
0
0
Richard kulia na Bilal kushoto wakinyemeleana

Richard Commey amedhihirisha uwezo wake wa upigana ngumi wakati alipomtoa kwa TKO bondia Bilal Mohammed na kutangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wills Gym City Engineers katika viunga vya Jamestwon, jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na wapenzi wengi wa ngumi wakiongozwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Ngumi cha Ghana (GBA), viongozi wa Kamati ya Olympic ya Ghana, Meya wa jiji la Accra, pamoja na wWaziri wa Michezo wa Ghana.
Mpambano huo ulianza kwa mbwebwe za aina yake baada ya mabondia wote kuwasili kwenye ulingo wakisindikizwa na mashabiki wao waliokuwa wanacheza ngoma mbalimbali za makabila ya Ghana.
Bilal alianza mpambano katika raundi ya kwanza akikurupuka kutoka kwenye kona yake kama faru na kumfuata Richard kwa nia ya kumsimamisha katika raundi ya kwanza lakini Richard aliweza kuhimili shambulio hilo na kuanza kutoa dozi kwa Bilal.
Katika raundi ya 4 Richard alimpeleka Bilal kwenye sakafu ya ulingo mara mbili kwa ngumi zilizokuwa nzito. Bilal aliweza kuendelea na pambano baada ya kuhesabiwa mara 8! Mashabiki wengi aliuzingira ulingo wakati wote wa mpambano huku wakipiga makalele na ngoma zilizoashia kuwa wawili hao kweli wametawala nyoyo za mashabiki wengi wa ngumi katika nchi ya Ghana.
Mambo yalifikia tamati katika raundi ya saba wakati Richard aliporusha ngumi tatu mfululizo za mchanganyiko na kumpeleka Bilal chini kwa mara ya tatu. Bilal aliamka kwa shida wakati mahesabu ya refarii yalipokuwa yanafikia mwisho na alianza kupepesuka huku refarii akimdaka ili asianguke tena na kuashiria mwisho wa mpambano huo.
Huu ni wakati ambapo Richard Commey alipotangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika na ukumbi mzima kuzizima kwa nderemo na shangwe. Kwa ushindi huo, IBF imempatia Richhard Commey nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito mwepesi mpambano ambao utafanyika tarehe 28 mwezi wa Aprili mwaka huu.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI TUZO ZA MWANAMAKUKA KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na uksherehekea siku ya Wanawake Duniani usiku wa kuamkia leo, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Mamodo wakidundika jukwaani kunogesha siku hii
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, na baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya kutoa tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Wanawake Duniani, katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa kwanza wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume, wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Mmoja wa washiriki wa onyesho la mitindo ya mavazi ya Mwanamakuka,
Mke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wadhamini waliofanikisha kufanyika kwa hafla hiyo ya utoaji tuzi za Mwanamakuka 2013, baada ya kukabidhi tuzo hizo kwenye hafla hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo  kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

MAMA SALMA KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE MKOANI MWANZA

$
0
0
IMG_4139.JPG
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa Jiji la Mwanza wakati wa kilele cha siku ya wanawake iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana.

IMG_4158.JPG
  Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

WAKAZI ZAIDI YA 160,000 JIJINI MWANZA KUNUFAIKA KWA MRADI WA MAJI KUTOKA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI(SBL)

$
0
0

Mke wa rais mama Salma Kikwete akisaidiana na Meneja miradi wa

SBL Nandi Mwiyombela wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji la Mwanza
Getrude Ngonyani kuashiria kuanza kutumika kwa kisima kwa ajili ya wakazi wa Mwanza.


 Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria
uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa ajili ya wakazi zaidi ya 160,000 waishio jijini Mwanza, kushoto kwake ni 
Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Pascal K. Mabiti na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Jaji Mark Bomani.
Meneja miradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL) Nandi Mwiyombela
akitoa maelezo kwa mke wa Rais mama Salma Kikwetejuu ya kisima
kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti katika Hospitali ya
mkoa wa Mwanza - Sekou Toure.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akihutubia wakazi wa jiji la
Mwanza(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti katika eneo la  hospitali ya Sekou Toure ulifanyika Alhamisi ya wiki hii.
Meneja miradi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela
katikati akisalimiana na mke wa rais mama Salma Kikwete mara baada
yakuwasili katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kwaajili ya
uzinduzi wa kisima cha maji na pembeni yake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mwanza Patrick Kisaka.

MICHUANO YA NSSF CUP 2013 YAZINDULIWA RASMI LEO

$
0
0
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akipa mpira wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF leo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akikagua timu ya Changamoto kabla ya pambano lao na timu ya Habari Zanzibar. Changamoto iliwavua ubingwa wa michuano hiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Habari Zanzibar kwa kuitandika 3-0.
 Waamuzi wa mchezo wa ufunguzi wakisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka kabla ya mchezo.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na wachezaji wa Habari Zanzibar.
 Golikipa wa Habari Zanzibar akipatiwa matibabu baada ya kuumia.
 Kocha wa timu ya Changamoto, Mawazo Lusonza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (katikati) akifuatilia mchezo wa netiboli kati ya NSSF na Mlimani Tv, katika mchezo huo NSSF ilishinda 46-1 Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa Bodi, Abubakar Rajabu.
 Meneja Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu akitoa maelekezo kwa Ofisa Uhusiano Kinongozi wa NSSF, Eunice Chiume wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo.
 Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa wa ufunguzi wa mashindano ya NSSF Media Cup dhidi ya NSSF uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Changamoto imeshinda 3-0
 Mshambuliaji wa timya Habari Zanzibar, Amour Mohamed akimtoka beki wa Changamoto, John Robert 
 Kiungo wa timu ya Changamoto, Andrew Faustin akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa Habari Zanzibar, Thani Mfamau.
 Beki wa timu ya Changamoto, Emmanuel Balele akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.
 Timu za Nertiboli za NSSF na Mlimani Tv zikichuana ambapo NSSF imeshinda 46-1

JUMUIYA YA FAWE ZANZIBAR YAKABIDHI FEDHA KWA WANAFUNZI MAYATIMA

$
0
0
 Wakushoto Katibu wa Jumuiya ya Fawe Zanzibar Dkt.Mwatima,wa katikati Kaimu Mratib Fawe Arafa Yahya na wakulia ni Bi Mwaka Sleiman Mlezi wakiwa katika Picha ya pamoja na wanafunzi waliopatiwa msada huko Ofisini kwao Vuga. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Katibu wa Jumuiya ya FaweZanzibar Dkt.Mwatima Abdalla Juma akimkabidhi msada wa fedha mwanafunzi Halima Vuai Issa uliotolewa na Al-Amana ya Dubai kupitia Jumuiya ya FaweZanzibar.
  Katibu wa Jumuiya ya Fawe Zanzibar Dkt.Mwatima Abdalla Juma akimkabidhi msada wa fedha mwanafunzi Abushiri Abdalla uliotolewa na Al-Amana ya Dubai kupitia Jumuiya ya FaweZanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya FaweZanzibar Dkt.Mwatima Abdalla Juma akifafanua kitu kwa wanafunzi mayatima waliofika kupokea msada wa fedha uliotolewa na Al-Amana ya Dubai kupitia Jumuiya ya  FaweZanzibar,hawapo pichani kulia Kaimu Mratibu Fawe Arafa Yahya hafla hiyo imefanyika ofisini kwao Vuga Mjini Zanzibar.
 Katibu wa Jumuiya ya FaweZanzibar Dkt.Mwatima Abdalla akizungumza na wazee na wanafunzi kabla ya kuwakabidhi msada wa fedha zilizotolewa na Al-Amana ya Dubai kupitia Jumuiya ya FaweZanzibar.

RAIS KIKWETE AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS MTEULE WA KENYA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.

Katika salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:

“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa kwako.”

Ameongeza Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa ambao umeutoa katika nafasi mbali mbali za uongozi katika siku za nyuma katika jitihada zako za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi wake.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa  kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa kwamba pamoja tutaweza kuendelea kusukuma mbele zaidi maendeleo ya nchi zetu – Kenya na Tanzania na pia utengamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake.”


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU

DAR ES SALAAM


9 Machi, 2013



MASHABIKI MISRI WACHOMA OFISI ZA SHIRIKISHO LA SOKA

$
0
0

Ofisi ya Shirikisho la Soka nchini Misri likiwaka moto baada ya kuchomwa na mashabiki kufuatia hukumu ya mahakama ya kifo kwa watu 21. 

Mashabiki wa soka wa klabu ya Al-Ahly katika jiji la Cairo nchini Misri wamezua balaa katika jiji hilo ikiwa ni pamoja na kuichoma moto ofisi ya shirikisho la soka nchini humo kufuatia mahakama jijini Cairo kutoa hukumu ya kifo kwa mashabi 21 wa soka.

Maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoa wa Arusha

$
0
0


Naibu waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Goodluck Olemadeye akiongea na wananchi wa Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arumelu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, tarehe 08/03/2013. Kulia kwake ni Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo, mhe. Ummy Ally Mwalimu ( mb.) Naibu waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Arumelu, mhe. Nyerembe Munasa.


Mhe. Ummy Ally Mwalimu (mb.), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akihutubia wananchi na wanawake wa Mkoa wa Arusha, wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoadhimishwa kimkoa katika wilaya ya Arusha.


Safari ya Uhuru Muigai Kenyatta kuingia Ikulu ya Kenya yaiva

$
0
0
 Mhe Uhuru Muigai Kenyatta akionesha hati aliyokabidhiwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya jana katika ukumbi wa Bomas na kutangazwa kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo. Mpinzani wake Mhe Raila Odinga amekataa kukubali matokeo hayo na kuonesha nia ya kwenda kuyapinga mahakamani. 
Walinzi wakiwa wamelizingira gari lililombeba Rais mteule wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta alipokuwa akiwasili Bomas of Kenya mara baada ya kutangazwa mshindi.

Mhe Raila Odinga aongea baada ya matokeo

TASWIRA ZA UZINDUZI WA SHINA LA CCM KATIKA JIJI LA COVENTRY UINGEREZA

$
0
0


Ndugu Haji Mallesa wa tatu kutoka kulia akitazama kadi yake mpya aliyokabishiwa kutoka kwa Katibu wa CCM UK ndugu Mariam Mungula. Na wa kwanza kushoto ni ndugu  Simba Fundikira Mwenyekiti wa muda Shina la Coventry.


 Bi Saida Mashaka (Chui) wa pili kutoka kushoto akikabidhiwa kadi ya uanachama mpya wa CCM kutoka kwa Katibu wa CCM UK ndugu Mariam MUngula wa pili kutoka kulia.


 Ndugu Mariam Mungula Katibu wa CCM UK (wa pili kulia), akimkabidhi mwanachama mpya ndugu Athuman Mchujuko (Achu) Kadi ya CCM katika uzinduzi wa Shina la CCM Coventry UK.
 Ndugu Dessa Makoko (katikati) ambaye ni Katibu wa muda wa Shina la Coventry akipokea baadhi ya vitendea kazi vya chama kutoka kwa Katibu wa CCM UK ndugu Mariam Mungula wa pili kulia.

 baadhi ya waliokuwepo katika uzinduzi wa shina la CCM katika jiji la Coventry.

Katibu wa CCM UK wa tatu kutoka kushoto ndugu Mariam Mungula akiwa pamoja na wanachama wa Shina jipya la Coventry. Kutoka kushoto ni ndugu Saida Mashaka (Chui), Ndg. Amina Suleiman, Katibu Mungula, Arua Yusuph Chunda, Mrs Simba Fundikira na Bi. Safina Omary Rashid.

IJUE HALI YA ABSALOM KIBANDA AFRIKA KUSINI

$
0
0


Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Absalom Kibanda nchini Afrika Kusini
Nachukua fursa hii kuwapa maendeleo ya tiba ya Mwenyekiti wa TEF Absalom Kibanda ambaye amelazwa Hosipitali ya Millpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini.

1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.
-- 
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Jumapili njema na Solomon Mukubwa na wimbo wake wa 'Mfalme Wa Amani'

Umoja wa Mataifa waishukuru TANZANIA

$
0
0

Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Katibu Mkuu,  kuhusu maendeleo ya  maandalizi ya Ujenzi wa  Majengo ya Kimataifa  Tawi la  Arusha yatakayotumika kushughulikia umalizaji wa mashauri ya Masalia ya  iliyokuwa  Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) pamoja na utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za mahakama hiyo.  
Majengo hayo yatajengwa katika eneo la Laki Laki Jijini Arusha, ujenzi wake unagharamiwa na Umoja wa Mataifa ambapo makadirio yanaonyesha  yatagharimu dola za Kimarekani 8.79  milioni.  Tayari dola za kimarekani 3 milioni za kuanzia  zimekwisha kutengwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.  
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Tano, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na  Bajeti ya UN, Bw.  Johannes Huisman ameishuruku Tanzania kwa kutoa eneo hilo la Laki Laki.Akizungumza baada ya kuwasilisha wa  taarifa hiyo, Balozi Manongi alisisitiza kwamba  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti katika kutoa ushirikiano na kuunga mkono kazi ya  utekelezaji wa mradi huo muhimu ili uweze kukamilika kwa wakati. Na kusisitiza kwamba  jambo  la muhimu ni kwa pande hizo mbili yaani  Tanzania na Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba zinashirikiana  na kuwasiliana kwa karibu katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi huo

Mbowe Avunja Kamati ya Utendaji CHADEMA Wilaya ya Tarime

$
0
0

Mwenyekiti wa Chademan,Mbunge wa Hai na  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe akiongea na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani.Picha na Habari na CHADEMA
---
Baada ya kikao cha ndani kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya Utendaji).

Uamuzi huo uliofanyika jana mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao hicho.

Baada ya kikao hicho cha Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani, ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha chama.

Uongozi wa chama katika ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kwa hatua hiyo, uchaguzi wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja ukisimamiwa na ngazi ya juu

Mwenyekiti Mbowe amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi, ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu kusalimiana..."mambo...kama Tarime..."

kocha athumani kilambo kuzikwa leo kisutu

$
0
0
Kocha Athumani Kilambo (kanzu ya kijani) enzi za uhai wake akiwa na vijana wake wa Yanga Kids na baadaye wakaja kuchezea Yanga na Pan Africa  mwaka jana wakati wa mkusanyiko wao kumkaribisha nyumbani mwenzao Kassim Manara (kushoto) aliyerejea Tanzania kwa mapumziko baada ya kuishi Ulaya kwa takriban miaka 25 mfululizo.

Marehemu Kilambo, ambaye alifariki usiku wa kuamkia leo kwa maradhi ya Saratani ya koo, anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaaam baada ya Salat Alaasiri katika msikiti wa Manyema.

tuzo za mwanamakuka zilivyofana ndani ya serena hotel jijini dar.

$
0
0
Wageni waalikwa wakiburudishwa huku wakijimwaya mwaya na muziki safi kabisa kutoka kwa msanii wa kizazi kipya Shaban Katwila a.k.a Q-Chilla, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Mwanamakuka zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Mwanamke Duniani,mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Wageni waalikwa wakijimwaya mwaya.

Wamachinga:Supa maketi zinazotembea

$
0
0
Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga wakiwa kwenye shughuli yao ya kujitafutia rizki katika foleni ya magari Barabara ya Kawawa,jijini Dar es Salaam kama walivyonaswa na Kamera ya Globu ya Jamii.kikweli ukweli jamaa hawa wanasaidia sana kufunguza safari za kwenda kwenye masupa maketi kila siku,maana wanamahitaji ya kila aina yanayopatikana kule.
Korosho za Mtwara hizooo....

Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images