Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: CHOPA YAPIGA MWELEKA LEO NA KUUWA WATU WANNE JIJINI DAR LEO

0
0
Sehemu ya mabaki ya Helkopta aina ya Chopa iliyopiga mweleka mapema leo asubuhi maeneo ya Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam na kuua watu wanne waliokuwemo ndani ya Chopa hiyo hiyo wakiwa ni rubani pamoja na askari watatu.Chanzo cha Chopa hiyo kupiga mweleka bado hakijafahamika mpaka sasa.
Sehemu ya Mashuhuda wakiangalia mabaki ya Chopa hiyo.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia ajali hiyo iliyotokea mapema leo eneo la Kipunguni B,jijini Dar es Salaam.Watu wanne wamepoteza maisha kwenye ajali hiyo.Watu hao ni Rubani mmoja na Askari polisi watatu.

MAHAFALI YA CHEKECHEA SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA NA SIKU YA WAZAZI

0
0
Mkurugenzi mtendaji  wa  Shule za  Southern Highlands Mafinga  Mary  Mungai akishirikiana na mgeni rasmi  kuwalisha  keki wanafunzi wa  shule  hiyo  leo wakati wa mahafali ya  chekechea na siku ya  wazazi.
Wanafunzi  wakionyesha  michezo mbali mbali 
Baadhi ya  wanafunzi wa shule  hiyo  wakifuatilia  michezo mbali mbali.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Mkuu wa shule hiyo pia alitangaza nafasi za masomo kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu wanaotokea kiswahili medium schools na la tano pia wakati ,Darasa la 4 na 6 wanaotoka English medium. 
Kwa la nne na sita wale wanaotoka English medium schools.  

 Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni na kutakuwa na interviews tarehe 13 / 12/2014 maeneo uafuatayo. Shuleni Southern Highlands   Mafinga, Oyster Bay Primary school, Dar es salaam, chuo cha Nursing Ilembula na Misufini primary school, Songea ama  kuwasiliana na  uongozi  wa  shule kwa simu  hii0756749151 au 0754651966 
Pia  alisema  sekondari form one wanazo  nafasi na  jina la sekondari; Mufindi Highlands School


Binti wa Ankal alamba nondozz yake katika Chuo Kikuu cha Dodoma leo

0
0
Binti wa Ankal,Bi. Zahra Muhidin Michuzi akiwa kwenye pozi la picha mara baada ya kulamba Nondozz yake ya BA EC katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo wakati wa Mahafali ya 5 ya Chuo hicho.
Binti wa Ankal,Bi. Zahra Muhidin Michuzi akiendelea kujiachia mbele ya Kamera.
Bi Zahra akiendelea kupata taswira mbali mbali.
Kwa raha zake Binti Ankal.
Pozi la Selfie na mdogo wake.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 16 NA 17 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 29 NOVEMBA, 2014

0
0
I:UTANGULIZI 
                                 
a)Masuala ya jumla

Mheshimiwa Spika,
1. Leo tunahitimisha shughuli za Mkutano wa Kumi na Sita na Kumi na Saba wa Bunge lako Tukufu.  Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

Mheshimiwa Spika,
2. Mkutano huu ulijumuisha kujadili kazi kubwa zifuatazo:

Kwanza: Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/2016;

Pili:Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 [The Tax Administration Bill, 2014];

Tatu:Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani wa Mwaka 2014 [The Value Added Tax Bill, 2014];

Nne:Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2014 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2014]; na
Tano:             Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2014, [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2014].

Aidha, ni hivi mapema leo Miswada 11 ya Sheria ya Serikali kuhusu mambo mbalimbali ilisomwa kwa mara ya kwanza.

Kusoma hotuba kamili BOFYA HAPA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 29, 2014

 Mawaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya  (kulia) na Stephen Wasira  (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bugeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 29, 2014. 
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (kulia) akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mjini Dodoma Novemba 29, 2014. 
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wabunge, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu n Mafunzo ya Ufundi. Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWS FLASH: JK ATUA DAR ES SALAAM LEO AKITOKEA MAREKANI KWENYE MATIBABU

0
0

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru  Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliyeongoza mapokezi hayo ya Ikulu 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu.

TANGAZO LA MSIBA WA KEPTENI-SP. KIDAI SENZALA KALUSE

0
0
Mrakibu wa Polisi-Captain Kidai Senzala Kaluse enzi za uhai wake. 

Familia ya Mzee Senzala Kaluse wa Kimara Mwisho Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao KIDAI SENZALA KALUSE kilichotokea Novemba 29, 2014 Saa 4 asubuhi kwa ajali ya Helkopta huko Kipunguni B, Moshi Bar Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa baba yake Mzee Kaluse, Kimara Mwisho. Habari ziwafikie, Ukoo wote wa Warutu, Ukoo wa Kaluse, Ukoo wa Mroki, Familia yote ya Timothy Nathan, Ukoo wa Kajiru na Taluka, Wakamba wote wa Ugweno Msangeni, Bibi wa Marehemu Mary Nathan wa Kinyenze- Morogoro, Familia ya Tarimo ya Ukonga Mombasa, Omary Msuya wa Moshi, Abdalh Mgonja wa Gonja Maore, Hosea wa Arusha.

Taarifa pia ziwafike maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Kikosi cha Polisi Anga, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

Misa ya kuaga Mwili wa Marehemu itafanyika mnyumbani kwao leo Jumapili kuanzia Saa 6:00 kabla ya safari ya kuelekea Gonja Maore, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kuanza. Mazishi yatafanyika Jumatatu Kijijini Kwao Gonja Maore.  

Mawasiliano zaidi: Mroki Mroki- +255 717002303. 
 MATAYO 5: 4 HERI WENYE HUZUNI; MAANA WAO WATAFARIJIKA

ngoma azipendazo ankal

0
0
Safari Trippers -Pole sana

KUMBUKUMBU

0
0

Late Col. Godfrey K. Makaya          

Leo tarehe 30/11/2014, baba yetu mpendwa umetimiza miaka saba tangu 
ututoke, unakumbukwa sana na familia yako, ndugu, jamaa na marafiki. Still in  our heart, continue to rest in peace dad GK. Amen.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi  wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati  wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana Novemba 29, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi 
wengine walioshiriki katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kifurahia jambo na Makamu wa Rais wa  Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana Novemba 29, 2014. Picha na OMR.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NBC yazipiga jeki shule sita za msingi wilayani Kilombero

0
0
  Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Morogoro, James Ndimbo (kushoto) akikabidhi sehemu ya msada wa madawati 150 kwa Meneja Fedha wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Mark Roe Scott (kulia) yaliyotolewa na NBC kwa ajili ya shule sita za msingi wilayani Kilombero. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kilombero, Morogoro jana. Wa pili kushoto ni Ofisa Mauzo na Masoko wa NBC Morogoro, Mary Mwansele na mwalimu wa shule ya msingi Lyahira, Sara Mwanukuzi.
 Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Morogoro, James Ndimbo (kushoto) akikabidhi sehemu ya msada wa madawati 150 kwa Meneja Fedha wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Mark Roe Scott (kulia) yaliyotolewa na NBC kwa ajili ya shule sita za msingi wilayani Kilombero. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kilombero. Wa pili kushoto ni Ofisa Mauzo na Masoko wa NBC Morogoro, Mary Mwansele na mwalimu wa shule ya msingi Kantui, Prisca Kasanga. 
Shule ya Msingi Kilombero wakipokea moja ya madawatri kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, James Ndimbo (kushoto).
Shule ya Muungano wakipokea moja ya madawatri kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro, James Ndimbo (kushoto).

Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai afanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia Dubai

0
0
 Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga amekutana na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu wa Mabalozi wadogo nchini humo (Dean of Diplomatic Corps)  Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia. 
Mhe. Mjenga alienda kumtembelea ili kuomba ushiriki wake pamoja na Mabalozi Wadogo wote kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii nchini Tanzania, litakalofanyika tarehe 17 Disemba 2014. 
Mhe. Emad Madani amesema atashiriki vikamlifu kwenye kongamano hilo huku akisema kuwa Tanzania na Saudi Arabia ni nchi rafiki wa siku nyingi, na hivyo basi wapo tayari kuomba taasisi ya utalii ya Saudi Arabia kushiriki pia.
Aliahidi kuwaomba Mabalozi Wadogo wote washiriki. Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga akiagana na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu wa Mabalozi wadogo nchini humo (Dean of Diplomatic Corps)  Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia.

Tiwa Savage, Olamide, Diamond win at Channel O Music Video Awards 2014 (Full list of winners)

0
0

Diamond and Cassper Nyovest took home the most plaques, by the time the 2014 edition of Channel O Music Video Awards ended on Saturday night. Davido missed out on all the categories he was nominated for, but other Nigerian acts like Tiwa Savage, KCee and Olamide won.

The event was staged in Johannesburg, South Africa. 

Here is the list of all the winners:
MOST GIFTED MALE

CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA*** Winner

DAVIDO – AYE
RIKY RICK FT OKMALUMKOOLKAT – AMANTOMBAZANE
K.O. FT KID X – CARACARA
SARKODIE – ILLUMINATI

MOST GIFTED FEMALE
THEMBI SEETE – THUNTSHA LEROLE
BUCIE FT HEAVY K – EASY TO LOVE
LIZHA JAMES FT UHURU – QUEM TI MANDOU

TIWA SAVAGE FT DON JAZZY – EMINADO** Winner

SEYI SHAY – IRAWO

MOST GIFTED NEWCOMER
DREAM TEAM FT TAMARSHA, AKA & BIG NUZ – TSEKEDE
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
EMMY GEE FT AB CRAZY & DJ DIMPLEZ – RANDS AND NAIRAS

DIAMOND – NUMBER ONE** Winner

PATORANKING – GIRLIE O (REMIX)

MOST GIFTED DUO, GROUP OR FEATURING
UHURU FT OSKIDO & PROFESSOR – Y-TJUKUTJA
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
R2BEES FT WIZKID – SLOW DOWN
K.O. FT KID X – CARACARA

KCEE FT WIZKID – PULL OVER** Winner

MOST GIFTED DANCE
UHURU FT OSKIDO & PROFESSOR – Y-TJUKUTJA
DAVIDO – SKELEWU
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
P SQUARE – PERSONALLY

BUSISWA FT VARIOUS – NGOKU** Winner

MOST GIFTED RAGGA DANCEHALL

BUFFALO SOULJAH – BASAWINE** Winner

OREZI – RIHANNA
JESSE JAGGZ FEAT WIZKID – BAD GIRL
PATORANKING – GIRLIE O (REMIX)
SHATTA WALE – EVERYDOBY LIKES MY TING

MOST GIFTED AFRO POP
DAVIDO – AYE
MAFIKIZOLO FT MAY D – HAPPINESS

DIAMOND – NUMBER ONE** Winner

FLAVOUR ADA ADA
IYANYA – JOMBOLO

MOST GIFTED KWAITO

UHURU FT OSKIDO & PROFESSOR – Y-TJUKUTJA** Winner

CHARACTER FT MONO T & OSKIDO – INXEBA LENDODA
BIG NUZ FT KHAYA MTHETHWA – INCWADI YOTHANDO
DJ VETKUK VS MAHOOTA – KHABA LENJA
DJ CNDO – YAMNANDI INTO

MOST GIFTED R&B
2FACE FT T PAIN – RAINBOW
JIMMY NEVIS FT KWESTA – BALLOON
GB COLLECTIVE FT BRIAN TEMBA & REASON – CHOCOLATE VANILLA

DONALD – CRAZY BUT AMAZING** Winner

NIYOLA – TOH BAD

MOST GIFTED HIP HOP
CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA
KHULI CHANA FT DA L.E.S & MAGESH – HAPE LE HAPE 2.1
PHYNO – ALOBAM
K.O. FT KID X – CARACARA

AKA – CONGRATULATE** Winner

MOST GIFTED SOUTHERN
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)

CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA** Winner

AKA – CONGRATULATE
ZEUS – PSYCH
K.O. FT KID X – CARACARA

MOST GIFTED WEST
R2BEES FT WIZKID – SLOW DOWN
DAVIDO – AYE
BURNA BOY FT D’BANJ – WON DA MO

OLAMIDE – TURN UP** Winner

DR SID FT DON JAZZY – SURULERE

MOST GIFTED EAST
SAUTI SOL – NSHIKE

DIAMOND – NUMBER ONE** Winner

NAVIO – NO HOLDING BACK
EDDY KENZO – SITYA LOSS
ELANI – KOOKOO

MOST GIFTED VIDEO OF THE YEAR
EMMY GEE FT AB CRAZY & DJ DIMPLEZ – RANDS AND NAIRAS
DAVIDO – AYE
K.O. FT KID X – CARACARA
BURNA BOY – RUN MY RACE
TIWA SAVAGE FT DON JAZZY – EMINADO
DR SID FT DON JAZZY – SURULERE
RIKY RICK FT OKMALUMKOOLKAT – AMANTOMBAZANE

CASSPER NYOVEST – DOC SHEBELEZA** Winner

SARKODIE – ILLUMINATI
DJ CLOCK FT BEATENBERG – PLUTO (I REMEMBER)
AKA – CONGRATULATE
DIAMOND – NUMBER ONE

yale yaleeeee....Gatepass ya Mlimani City, dar es salaam

Taarifa ya benki ya biashara ya Mkombozi juu ya sakata la Escrow

0
0

Utangulizi


Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering 


and Marketing (VIP)


Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.

Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.

2.0 Mauzo ya hisa za VIP

Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.

3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali

Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).

TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.

Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.

4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali

4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu

Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.

Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.

Benki ya Mkombozi haijihusishi na utakasishaji wa fedha chafu na haramu katika uchumi wa Tanzania.

4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP

Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.

Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.

4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia

Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.

Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.

4.4 Malipo kwa mfanyakazi wa benki ya Mkombozi

Gazeti la Mawio la tarehe 20-26, Novemba, 2014 tolea namba 0122 liliandika kuwa mwanasheria wa benki ya Mkombozi ajulikanaye kwa jina la Rweyengeza Alfred alipokea malipo toka akaunti ya VIP ya shilingi milioni 40.2.

Benki inatoa tamko kuwa haina mfanyakazi anayetambuliwa kwa jina hilo na wala hakuna mfanyakazi yeyote wa benki aliyelipwa fedha toka kwenye akaunti ya VIP.

Wito kwa umma

Benki ya Mkombozi inachukua fursa hii kuwatarifu wateja wake na umma kutopotoshwa na taarifa au tuhumma zilizofafanuliwa hapo juu na kuwataka wateja wake wote kutokuwa na hofu yeyote kwani benki ipo imara na inafanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhumma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja tunajenga nchi na uchumi wa nchi yetu.

Hitimisho

Benki ya biashara ya Mkombozi haijihusishi na haitajihusisha na utakasishaji wa fedha chafu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI

Wakazi wakaskazini wanufaika na Gulio la Vodacom Tanzania

0
0
 Afisa Mauzo wa Duka la Simu la Bei nzuri la jijini Arusha,Martha  Meena akitoa maelezo kwa wateja waliofika katika banda la duka hilo  wakati wa gulio la punguzo kubwa la bei za bidhaa za Mawasiliano   lijulikanalo kama Vodacom Expo linalofanyika siku mbili katika uwanja wa Sheakh  Amri Abeid jijini Arusha.
 Afisa huduma kwa wateja wa Duka la  Vodacom jijini Arusha,Samya Ulimwengu  akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika katika banda lao   kujipatia huduma za mawasiliano ambazo zinapatikana katika Gulio la Vodacom Expo kwa punguzo kubwa la bei lililofanyika katika uwanja wa Sheakh Ami Abeid jijini Arusha. 


Mamia ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa katika Gulio la Vodacom Expo kupata   huduma mbalimbali za mawasiliano ambazo zimeuzwa kwa punguzo kubwa la bei lililofanyika kwa siku mbili katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CCM KASKAZINI UGUJA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi katika Mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa katika jitihada zake za kuimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Mkoa huo,(kulia) Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, na  wa kwanza (kushoto) Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Khadija Hassan Aboud akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM Kaskazini A Unguja  Ali Makame Khamis, sambamba na jitihada hizo leo anatarajiwa kuanza kuzungumza na Viongozi mbali mbali wakiwemo Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani wa Chama hicho katika Mikoa  ya Pemba.  [Picha na Ikulu.]

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Za EAC Wakamilika Nairobi

0
0
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (kulia) na Naibu Waiziri wa TAMISEMI (Elimu) Mh. Kassim Majaliwa wakizungumza nje ya Ukumbi wa Mkutano wa Kenyatta kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Miundombinu Nov 29, 2014,Nairobi
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo (kushoto) akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu uliofanyika leo Novemba 29, 2014 Nairobi Kenya

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki Bw. Amantius Msole (kulia) na Naibu Mwanasheria Mkuu Mh. George Masaju walifuatilia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya

Makamu wa Rais wa Kenya Bw. William Ruto akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Miundombinu leo Novemba 29, 2014 Nairobi, Kenya.

ELIMU HAINA MWISHO...BRIGEDIA JENERALI (RTD) LIGATE ALAMBA NONDOZZZ ZA SHERIA LLB CHUO KIKUU HURIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 74

0
0
Brigedia Jenerali i Mstaafu P.S.Ligate Baba Mzazi wa akina Phanuel, Obed, Vupe na Guy Ligate akiwa Mwingi wa Furaha na Mkewe Mama Ligate mara tu baada ya kutunukiwa Shahada ya Sheria (LLB) katika  Chuo Kikuu Huria (Open Univeristy of Tanzania) Jijini Dar es salaam wikiendi hii. Globu ya Jamii inatoa pongezi sana kwa baba yetu huyu ambaye ni mfano wa kuigwa.

HONGERA MWALIMU WANGU DR NELSON ISHENGOMA KWA KUHITIMU MASOMO YA SHAHADA YA UDAKTARI

0
0
Dr Nelson Ishengoma akiwa katika pozi mara baada ya kutunukiwa shahada yake ya udaktari katika Mahafali ya Tano ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Chimwaga vilivyopo Chuoni hapo.
 Hongera sana Mwalimu wangu na sasa Mwanzo wa Jina linaanza na Dr. Sio kazi rahisi lakini Mungu ameweza kukusimamia na kukuongoza. Nakuombea kwa Mungu ufanikiwe zaidi na zaidi. 
Kutoka Kwa Mwanafunzi wako  Josephat Lukaza

kinana na ujumbe wake wateka mji wa mtwara

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini Mtwara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye  viwanja vya Mashujaa mjini humo akihitimisha ziara yake ya siku 16 aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi wenyewe na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM.
 Katika ziara hiyo Katibu mkuu huyo aliongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Katika kutano huo Kinana amempa wiki mbili Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe kutoa maelezo kwanini bidhaa mbalimbali hazisafirishwi kwenda nje kupitia bandari ya Mtwara
Pia Kinana amewaagiza Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ni kwanini wawekezaji wenye kampuni zinazofanya shughuli zao mtwara wanalipia kodi zao jijini Dar es salaam badala ya kulipia mkoani Mtwara ambako wanafanya shughuli zao
Pia waziri wa Ofisi ya Mkamu wa Rais Mazingira amepewa mwezi mmoja kuhakikisha dampo la taka za sumu zinazotupwa na wachimbaji wa gesi na viwanda kuacha mara moja kwa sababu zinahatarisha maisha ya wakazi wa Mtwara
 Mwisho akaagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa kibali cha kugawa viwanja katika manispaa ya Mtwara kwani viwanja vimeshapimwa, Fedha za kulipa fidia zipo ila kibali kutoka ofisi ya Waziri mkuu ndiyo kimkwama kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
 Wananchi wakinyoosha mikono yao juu kufurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiwahutubia.
 Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji akiwahutubia wapiga kura wake ambao walifurahia sana hotuba yake kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
 Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakati wa mkutano huo.
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
 Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape nnauye wakiingia katika uwanja wa mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangali vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia Nape Nnauye na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakiwasili katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara leo.
Picha na John Bukuku wa Full Shangwe.
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images