Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 655 | 656 | (Page 657) | 658 | 659 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Arusha(ATC)Dk Richard Masika akizungumza kwenye tamasha la kuwahamasisha wasichana wanaosoma Shule za Sekondari kusoma masoma ya Sayansi na Ufundi inayofadhiliwa na serikali pamoja na serikali ya Ubalozi wa Italia. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji Safi na Maji Taka jiji la Arusha (Auwsa) akiwahamasisha wasichana kusoma masomo ya Sayansi na Ufundi hadi kufikia hatua za juu,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha ATC ,Dk Richard Masika na Mwakilishi wa Ubalozi wa Italia nchini,Daniel Christian.
  Wanafunzi kutoka Shule za Sekondari 10 kwenye mikoa ya Arusha na Manyara wakifatilia tamasha hilo ambao waliahidi kusoma masomo ya ufundi ambayo yana uhakika wa ajira. 
   Mmoja wa wanafunzi kutoka Shule ya Arusha Sekondari aliyefanya vizuri kujibu maswali ya kisayansi akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi. 
   Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali. 

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donald Mmbando (kushoto)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo baada ya kupokea msaada wa magari manne na vifaa vya afya  kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya la Dunia(WHO),Dk. Rufaro Chotaro(kulia).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donald Mmbando (kushoto)akipokea moja ya funguo kati ya magari manne kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Afya la Dunia(WHO),Dk. Rufaro Chotaro(kulia).
  Magari manne na vifaa vya afya yaliyotolewa na Shirika la Afya la Dunia(WHO) kwa Wizara ya Afya.

  0 0

  The Ambassador of Tanzania to the United States H.E. Liberata Mulamula together with H.E. Dr. Faida Mitifu, Ambassador of the Democratic Republic of Congo and the Women Ambassadors in Washington, DC co-hosted a dinner at Vidalia restaurant in honor of H.E. Dr. Tebelelo M. Seretse, Ambassador of Botswana who has completed her tour of duty in Washington. Ambassador Seretse was well known for her distinguished service and was admired by all the women Ambassadors.
  Members of the Women Ambassadors in Washington, DC co-host a dinner at Vidalia restaurant in honor of H.E. Dr. Tebelelo M. Seretse, 
  Members of the Women Ambassadors in Washington, DC discussing matters arising during a dinner the co-hosted  in honor of H.E. Dr. Tebelelo M. Seretse, 
  H.E. Amb. Mulamula handing H.E. Dr. Amb. Tebalelo Seretse a gift from the Women Ambassadors of Washington DC.
  H.E. Amb. Mulamula and H.E. Dr. Amb. Tebalelo Seretse hug after the former has handed a gift from the Women Ambassadors of Washington DC.
  Members of the Women Ambassadors in Washington, DC in a group photo during the dinner at Vidalia restaurant in honor of H.E. Dr. Tebelelo M. Seretse, 

  0 0

   Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya  MaxCom Africa, inayotoa huduma za Max Malipo,  Juma Rajabu  na Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula wakikata utepe kuzindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo, katika hafla iliyokutanisha uongozi wa kampuni hiyo ya Jukwaa la Wahariri, leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Mkurugnezi Mtendaji wa MaxCom Africa, watoaji wa huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akizindua muonekano mpya wa huduma ya Max Malipo itakavyokuwa sasa kwenye ofisi za mawaakala wake.
   Mkurugnezi Mtendaji wa Kampuni ya Max Com Africa, watoaji huduma za Max Malipo, Juma Rajabu akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 10, kwa Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, Richard Chagula, kuashiria kampuni hiyo kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule zilizomo katika Manispaa hiyo, wakati wa hafla ya kampuni hiyo kutimiza miaka mitano ambapo uongozi ulikutana na wadau wakiwemo Jukwaa la Wahariri katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.

  0 0

  The New Vision [Uganda] of this Friday November 28, 2014 has run a news story on Page 49 titled ‘CECAFA SHOW OFF’ under which the author indicated that this year’s CECAFA edition won’t take place.


  As much as the author doesn’t clearly indicate the source of his information for the alleged call-off of the regional event, he somewhere claims to have spoken to me yesterday [Thursday] which never happened.


  I therefore wish to clarify as follows:

  1.    It’s true, this year’s CECAFA challenge Cup had been scheduled for Ethiopia but the intended Member Association later showed inability to host the event.

  2.    The CECAFA Executive Committee headed by Eng. Leodgar Tenga and the Secretary General Mr. Nicholas Musonye are still working out the possible measures to ensure that a late championship is at least organized.

  3.    CECAFA will later officially communicate its position on this matter.

  4.    CECAFA therefore wishes to ask all journalists and Media Houses to consult the relevant authorities before running personal opinions attributed to CECAFA officials.


  Anticipating your continued cooperation as we jointly work together for the development of our game.


  ROGERS MULINDWA

  CECAFA MEDIA MANAGER

  +256 772 751 829/ +256 701 520 115


  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Juma Yakout Juma kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Khadija Bakari Juma kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt. Juma Yakout Juma kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi Madina  Mjaka Mwinyi kuwa Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Wananachi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Mtwara Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 


   Kinana akizungumza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kibaoni, Mtwara Vijijini leo.

   Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Katika Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya Mtwara Vijijini.

  0 0  0 0

  Chief Park Warden for Lake Manyara National Park Mr. Domician Njau (right) explain a point to Hon. Lazaro Nyalandu, Minister for Natural Resources and Tourism as they walk through the Lake Manyara Hot springs boardwalk way yesterday.
  Director General of TANAPA Allan Kijazi giving out welcoming remarks during the official launching of the hot springs boardwalk way and hippo view point at Lake Manyara National Park yesterday.
  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (2nd right) cuts a ribbon to officially launch the Lake Manyara hot springs boardwalk way and hippo pool view point in Lake Manyara. Others in the picture from left are Manyara Regional Commissioner Hon. Elaston Mbwilo; Director General of TANAPA Allan Kijazi and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli.
  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu unveils the foundation stone of the Lake Manyara hot springs boardwalk way yesterday. For full story and more pictures CLICK HERE

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha  kwa Rais baada ya kuteuliwa rasmi.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha  kwa Rais baada ya kuteuliwa 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana  na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka baada ya mazungumzo  alipofika   kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibarbaada ya kuteuliwa. Picha na Ikulu, Zanzibar

  0 0
 • 11/28/14--12:37: UNCDF VACANY ANNOUNCEMENT
 • vacancies
  Basically, professionals with this background:
  Required Skills and Experience
  Education:
  At least a Master’s Degree in Business Administration, Finance, Banking or related areas, plus preferably a Bachelor Degree in engineering, finance or economics.
  Experience:
  Preferably a minimum of 5 years of relevant experience;
  Ability to build partnerships and deliver results that meet the needs and long-term interest of clients within and outside the institution;
  Demonstrated experience in preparation of project financial analysis and creation/evaluation of advanced and complex Ms Excel spread sheet financial models;
  Demonstrated experience with private equity/venture investments, credit and risk assessment, with solid financial modelling and risk assessment skills. Project financing experience in the private sector is a plus;
  Demonstrated experience in preliminary evaluation of project proposals for assessing their feasibility for private sector funding and/or technical support by LFI.
  Here is the link with more information


  0 0


  Sintofahamu iliyotokea kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma Ijumaa Novemba 28, 2014 imepelekea Spika Anne Makinda (pichani) kulazimika kusitisha shughuli za Bunge mpaka hapo watapojadiliana tena. 

  Hii ni baada ya majadiliano makali kuhusu kuwajibishwa ama la kwa viongozi wanaohusika na sakata la akaunti ya Escrow. Hali hii iliibuka baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA na kambi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe kuinuka na kusema kuwa Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, na kwamba kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kutoka maamuzi kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. 
  "Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi", alisema Mhe. Mbowe.

  0 0

  Tanzania leo imekabidhiwa rasmi Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki baada ya Kenya kumaliza muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja. 
  Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta na Katibu Mkuu Bi. Joyce Mapunjo walipokea Uenyekiti huo katika Mkutano wa Baraza wa Mawaziri uliofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC), Jijini Nairobi, Kenya. 
   Rais wa Tanzania anatarajiwa kupokea Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki siku ya Jumapili katika Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya utakaofanyika pia hapa KICC.
  Waziri Samuel Sitta akizungumza baada ya kupokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki leo 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo akisoma taarifa ya Kamati ya Makatibu Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Baraza la Mawaziri. Wengine kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera, Waziri Mh. Samuel Sitta na Mwandishi wa Taarifa za Mikutano Mpya kutoka Uganda Bi. Mary Nankabirwa.
  Mwenyekiti anayemaliza muda wake Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Kenya Bi. Phyllis Kandie (katikati) kabla ya kukabidhi uenyekiti kwa Waziri Samuel Sitta wa Tanzania. Kushoto ni Bw. Mugisha Kyamani kutoka Tanzania ambaye alikua ni Mwandishi wa Taarifa za Mikutano kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita

  Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akliwa na  Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).
  Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughilikia Miundombinu Dkt. Enos Bukuku walipokutana Jijini Nairobi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki leo. Wengine ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora Mh. George Mkuchika (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Abdullah Juma Saadalla (kulia).

  0 0


  Na Andrew Chale

  USIKU maalum wa kuenzi vazi la Khanga na magwiji wa taarab nchini 'Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab' unapotarajia kulindima usiku wa leo Novemba 29 ndani ya Ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B, karibu na daraja la Kawe, na kusindikizwa na gwiji wa mipasho Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi. 
  Kwa mujibu wa Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin amebainisha kuwa kwa ushirikiano wa Fabak Fashions na Safari Carnival wameandaa usiku huo maalum kuenzi vazi la Khanga.
  "Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab ni maalum kuenzi vazi hili la khanga ambapo pia watu wote watakaofika watavaa vazi maalum la khanga. Hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P." alisema Asia Idarous Khamisin.
  Aidha, alisema wadau watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi.
  Amesema  leo usiku  pia kutakuwa na zulia jekundu  (Red Carpet)  ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maarufu watakaojitokeza, ambao pia The Legend Dj John Dilinga wa nIsumba Lounge atasimamia muziki Old School.
  Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival.

  0 0

   Executive Chef Issa Kipande  tunayemfahamu kama Chef Issa (aliyeshika kombe) wiki hii amefanya makubwa kwa kuwa mmoja wa ma-Chef  wa timu ya Stockholm, Sweden, kushiriki na hatimaye kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Mapishi  2014 yajulikanayo kama  Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014  yaliyofanyika nchini Luxemborg. Mshindi wa jumla alikuwa Singapore.

  Kushinda kombe la dunia si mchezo katika tasnia yoyote ile nasi hatuna budi kumpongeza Chef Issa kwa kuwakilisha vyema Watanzania na Waafrika kwa jumla.
   Mtanzania huyu anayefanya kazi huko Sweden na Mtwara kuliko na hoteli yake aliyoifungua hivi karibuni, ameshiriki katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika kila baada ya miaka minne na yaliyoshirikisha ma-Chef zaidi ya 3000 kutoka nchi 56 za mabara yote matano ya dunia.

  Mpaka sasa Chef Issa Kapande mbali ya kushinda tuzo nyingi tofauti katika fani yake ya upishi pia anashikilia rekodi ya kuwa Chef Mtanzania Msomi na mdogo kuliko wote aliyewahi kufungua na kuongoza hotel ya nyota tano  akiwa Internationally  Certified Executive Chef  akiwa na umri wa miaka 25 tu. Hili ni jambo la kujivunia sana.
  Chef Issa anasema kuwa Mola ajaliapo anatamani sana mwaka 2018 aipeleke Timu ya Taifa ya Tanzania mashindano haya. "Na nina imani tutafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonyesha uwezo wao. Mungu ibariki Tanzania", anasema.
   Executive Chef Issa Kipande  tunayemfahamu kama Chef Issa (aliyeshika kombe) akiwa na  timu yake ya  Stockholm, Sweden,
   Executive Chef Issa Kipande alipoitwa mbele kwenda kupokea tuzo akiwa mtu  mweusi peke yake
   Executive Chef Issa alipata heshima kubwa sana ya kuhudhuria executive lunch kwa watu maalumu tu iliofanyika  wakati wa kutoa kombe la dunia kushoto ni Raisi wa mashindano hayo na kulia ni mtoto wa mfalme wa nchi ya Luxembourg Crown Prince Guillaum
  Executive Chef Issa akiwa na Raisi wa chama cha ma-chef dunia nzima 

  0 0


  Afro 70 Band - Week End

  0 0  0 0


  Na Mwandishi wetu,Mara.


  KIKUNDI cha Wanaume  wapiga kasia cha JJ Buda kutoka Nyarusurya Mkoani Mara kimeibuka na ubingwa katika fainali za Mkoa za mashindano yambio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya  Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na kuwakilisha Mkoa wa Kagera kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.

  Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Benedict Chamba ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Tumaini Maendeka kutoka Kisorya ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Bernard Charles kutoka Nyarusurya ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=


  Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Siagi Siagikutoka Kinesi, Chuma Musa kutoka Kinesi, Matiku Nkoba kutoka Kuruya, Paul Mwita kutoka Nyarusurya, Ostadhi Magori Kutoka Kuruya na Emmanue Jemes kutoka Resti


  Upande wa Wanawake kikundi cha Nyamizi Deokutoka Kisorya kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza. 

  Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Maria Sarige ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindi wa tatu ni kikundi cha Edina Peterkutoka Bwai ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Rosalina Johanes kutoka Nyarusurya  ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Khadija Simon kutoka Nyarusurya, Debora Malima kutoka Bweri, Winfrida Majinge kutoka Bukabwa, Tatu Siagi kutoka Kinesi, Justina Kambarage kutoka Kinesi,  na Siwema Doto kutoka Majengo.  Jumla ya vikundi 90 vilijitokeza kushiliki mbio hizo za makasia chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja matukio wa wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela aliwashukuru wakazi wa Mara kwa kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ambapo pia aliwapongeza walishinda na kupata nafasi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za Kanda Desemba 6, Mwaka huu na kuwaomba ambao hawakufanikiwa wakajipange kwa mwaka ujao.

  Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika  Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.

  0 0

  Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina akiongea na vyombo vya habari juu ya mipango ya Mfuko huo kutoa misaada kwa jamii hasa kwa wale wenye mahitaji kama walemavu wa ngozi (Albino)
  Mtoto Maria Mwingira akipokea msaada wa mafuta maalum ambayo hukinga ngozi yao wakati wa jua kali kutoka kwa Meneja Masoko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina.
  Kijana Salum Iddi akitoa neno la shukurani kwa Mfuko wa GEPF kwa niaba ya watoto wenzake huku akisikilzwa kwa makini na Meneja Masoko wa GEPF, Bw. Aloyce Ntukamazina pamoja na Afisa Uendeshaji wa Mfuko huo,Bi. Zuwena Rajabu.
  Afisa kutoka GEPF,Bw. Gaudence Mkoba akikabidhi misaada hiyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Matumaini.
  Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Matumaini Bw. Chacha akizungumza na baadhi ya watoto wa shule hiyo huku mwenyekiti wa umoja wa Albino wilaya ya Ilala Bw Seif Ulate akifuatilia kwa makini.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kushoto akizungumza na watu kutoka Jamhuri ya watu wa china (hawapo pichani) walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Sanaa Bibi Leah Kihimbi.
  Mkuu wa masuala ya Utamaduni, Utangazaji, Habari na Uchapishaji kutoka Nanjing China Bw. Yan Yiping kushoto akifafanua jambo walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
  Baadhi ya wageni kutoka Nanjing China wakifuatilia mazungumzo yaliyokua yakiendelea walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni yake. Kushoto ni Mkurugenzi msaidizi Mila Bibi Lily Beleko.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Haabari, Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akipokea zawadi kwa niaba ya Wizara kutoka kwa Mkuu wa masuala ya Utamaduni, Utangazaji, Habari na Uchapishaji kutoka Nanjing China Bw. Yan Yiping walipofika katika ofisi za Wizara kuonana na uongozi wa Wizara kabla ya Maonyesho ya Miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yaliyofanyika jioni Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

older | 1 | .... | 655 | 656 | (Page 657) | 658 | 659 | .... | 3284 | newer