Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 654 | 655 | (Page 656) | 657 | 658 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Na Beatrice Lyimo- Maelezo.

  GESI asilia ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya wananchi na uchumi wa nchi yeyote ikiwemo Tanzania.

  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadick wakati wa ufunguzi wa taftishi juu ya maombi la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu mapendekezo ya tozo ya uchakataji na usafirishaji wa Gesi asilia uliofanyika.

  Mhe. Sadick amesema  kuwa, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea maombi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu mapendekezo ya tozo ya uchakataji na usafirishaji wa Gesi asilia, hivyo EWURA inatarajia kuandaa mkutano wa wadau wa gesi asilia ili kupata maoni juu ya maombi hayo.

  Alibainisha kuwa, kutokana na upungufu wa maji ya kuendeshea mitambo ya umeme uliosababishwa na ukame nchini Tanzania, zaidi ya asilimia 40 ya uzalishaji wa umeme kwa sasa unategemea hiyo.
  “Gesi asilia inayozalishwa kwa sasa inategemewa katika uzalishaji wa umeme nchini ambapo asilimia 88 ya gesi hii inatumika katika kuzalisha nishati ya umeme”, alisema Mhe Sadick.

  Aliongeza kuwa, mitambo iliyopo inayotumia gesi asilia ina uwezo wa kuzalisha Megawati 441, lakini huzalisha Megawati 300 kutokana na uhaba wa miundombinu ya kuchakata na kusafirisha hiyo.

  Aidha, Serikali inatarajia utendaji mahiri wa EWURA kuwa chachu ya kuboresha utoaji wa huduma za uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia hapa nchini, kwani kwa kufanya hivyo itaongeza upatikanaji na ubora wa huduma na kuleta ufanisi endelevu wenye kuzingatia uboreshaji wa mazingira nchini.

  “Hii ni miongoni mwa juhudi za EWURA katika kushirikiana na wadau na kupata maoni kuhusu huduma zitolewazo na TPDC pamoja na mipango itakayowasilishwa katika sekta hii muhimu ya Gesi asilia”, aliongeza Mhe. Sadick.

  Wito ulitolewa kwa wadau hao kuwa makini, kujenga hoja kushiriki kwa nia njema, pamoja na kutoa maoni yakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa mizania kati ya watumiaji huduma za uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia inawepo, kwani TPDC na Taifa linafikia malengo ya matumizi ya gesi hiyo katika kukuza uchumi wa nchi.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu  wa TFDA , Bw. Hiiti B. Sillo akitoa hotuba ya TFDA kukubali kujiunga na Umoja wa Nchi za Asia katika Udhibiti wa Vifaa Tiba na Vitendanishi (Asian Harmonization Working Party on medical devices and diagnostics - AHWP) wakati wa mkutano wa mwaka wa AHWP uliofanyika Seoul, Korea Kusini kuanzia tarehe 17 - 21 Novemba 2014. Tanzania imekubaliwa rasmi kuwa mwanachama 24 wa AHWP  ikiwa  ni  nchi  ya pili Barani Afrika kujiunga  na  umoja huo baada  ya Afrika Kusini.
   Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo akiwa na Mwenyekiti wa umoja huo Dkt. Saleh Al –Tayyar  kutoka Saudi Arabia baada ya kukabidhiwa mwongozo rasmi TFDA wa kuimarisha mfumo wa udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi kama mwanachama mpya wa umoja huo.

  Mwenyekiti  wa AHWP , Dkt. Saleh Al –Tayyar  kutoka Saudi Arabia akiwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo na Meneja wa Udhibiti wa Vifaa Tiba, TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo, baada ya Tanzania kujiunga rasmi kuwa mjumbe wa Umoja wa Wadhibiti wa Vifaa Tiba katika nchi za Asia (AHWP).
   Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo akisalimiana  na Waziri  anayesimamia Usalama wa Chakula na Dawa nchini Korea na kati yao ni Mwenyekiti wa AHWP  Dkt. Saleh Al –Tayyar .


  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MWANAMUZIKI mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Bileku Mpasi, atafanya onesho maalum katika utambulisho wa nyimbo mbili mpya za bendi ya Mashujaa utakaofanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Ten Lounge zamani Business Park.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mratibu wa onesho hilo, King Dodoo la Buche, alisema kuwa Mpasi ambaye alitamba katika tasnia ya muziki wa dansi alipokuwa na gwiji, marehemu, Pepe Kale, atakuja na wasanii wengine ili kutoa burudani ya kiwango cha juu. Dodoo alitaja nyimbo hizo mbili ambazo zitatambulishwa ni pamoja na Rafiki Sokoni na My Queen.

  Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi nchini kujiandaa kushuhudia onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria hapa nchini. Rais wa Mashujaa Musica, Chalz Baba, alisema kuwa wamejiandaa kutoa burudani nzuri na kuendeleza heshima yao ya bendi bora kwa mwaka wa pili mfululizo.

  " Napenda kuwahakikishia wapenzi wa bendi yetu tutafanya kazi ya ubora wa juu, ni kawaida yetu kufanya kazi nzuri, tuna usongo," alisema Chalz.

  Katika onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Bear kupitikia kinywaji chake cha Windhoek. Akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo meneja biashara wa kampuni hiyo Joseph Emmanuel, alisema wameamua kudhamini utambulisho huo ili kuendeleza muziki wa dansi nchini kufikia hadhi ya kimataifa.

  Alisema kuwa wapenzi 100 wa kwanza watakaoingia kwenye onesho hilo watapewa bia moja ya Windhoek Drought bure. Mashujaa pia itatumbuiza nyimbo zake zilizotamba katika albamu zake za Risasi Kidole na Ushamba Mzigo.

  Naye Rais wa Mashujaa Chalz Baba amewataka wapenzi wajiandae kupata burudani ya aina yake katika uzinduzi.
  Rais wa bendi ya Mashujaa Chalz Baba, akizungumzia utambulsiho wa nyimbo zao mbili ambao utafanyika Disemba 12 mwaka huuu, kwenye Ukumbi wa Ten Lounge, utasindikizwa na mwanamuziki Bileku Mpasi kutoka nchini Congo, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa Group, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Mabibo Bear, ambao wamedhamini onesho hilo, Picha na Mpiga Picha Wetu.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Novemba 27, 2014.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo akizungumza, Bungeni mjini Dodoma Novemba 27, 2014.
  Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 27, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 27, 2014.
  Waziri Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Maswa Magaribi, John Shibuda, kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 27, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole- Sendeka kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Novemba 27, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati) na Mbunge wa Lshoto, Henry Shekifu kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 27, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam” na kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi chini ya kauli mbiu isemayo “ Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
  Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo kuhusu matumizi ya takwimu sahihi katika kupanga shughuli za maendeleo nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mohammed Hafidh akisisitiza jambo kuhusu athari, madhara na ya matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
  Mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw. Jacques Morisset (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali kuhusu mchango wa matumizi ya takwimu sahihi katika maendeleo ya taifa lolote wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.


  0 0

    Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo huku wakipaza sauti baada Sheikh Ponda kushinda rufaa ya kupinga hukumu ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Mei 9, 2013. (Picha na Francis Dande).
  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kushoto) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kushinda rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuvamia na kujimilikisha kwa nguvu kiwanja cha Markaz Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza wakati  akitoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
   Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam huku wakipaza sauti baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimakabili.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Andrew Chale, Bagamoyo

  CHAMA Cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Public Health Association-TPHA), kipo kwenye mkakati kabambe wa kuendeleza na kuinua mapato ya chama hicho ikiwemo kujenga jengo la kitega uchumi la kisasa litakalo kuwa na zaidi ya gorofa 20, katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

  Hayo yalibainishwa mjini hapa jana kwenye kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, mjini Bagamoyo ambapo wataalamu wa majengo nchini wa kampuni ya K&M Archplans (T)Ltd, walipowasilisha mpango kazi wao huo ikiwemo mchoro wa jengo hilo la TPHA litakavyokuwa.

  Wataalamu hao wa K&M Archplans, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Profesa Arch Livin Mosha alisema kampuni yao imebobea katika ukandarasi wa majengo mbalimbali ikiwemo kuwa na uzoefu wa kutosha katika usanifu na mpanilio wa majengo. Jengo hilo linatarajiwa kujengwa makao makuu ya TPHA, yaliyopo Kinondoni, Victoria Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

  Naye Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alieleza kuwa, Chama hicho kitaendela na mchakato wake ikiwemo kujadiliana kwa kina na wanachama katika kufikia malengo ya utekelezaji wake ambapo mpango wa TPHA kuwa na jengo la kisasa la gorofa 10 ama 25 ambapo itategemea na mchakato wake.

  Naye Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii hususani sekta ya afya hapa nchini. Kongamano hilo la kisayansi lililoanza Jumatatu ya Novemba 24, wiki hii, linatarajia kumalizika Ijumaa ya Novemba 28 wiki hii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K&M Archplans (T) Ltd, Profesa Arch Livin Mosham akifafanua jambo juu ya jengo hilo la kisasa linalotarajiwa kujengwa na TPHA (Linaloonekana kushoto kwake pichani), kwa wajumebe wa mkutano huo (Hawapo pichani) juzi, katika kongamano la 31 la kisayansi na mkutano mkuu wa mwaka, unaoendelea, katika ukumbi wa Stella Maris, Mjini Bagamoyo, Pwani.
  Mkurugenzi wa K&M Archplans (T)Ltd, Arch Albert Mwambafu akifafanua jambo kwa wajumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Public Health Association-TPHA), (Hawapo pichani) wakati wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, mjini Bagamoyo. ambapo jengo ni mradi wa kuinua mapato ya TPHA kwa ajili ya kuendelea kuelimisha jamii kuhusiana na mambo ya afya.
  Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa TPHA, akiwemo Dk. Anna Nswilla (Treasure of TPHA), (katikati) akifuatiwa na Dk.Faustine Njau (TPHA Life Member).
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K&M Archplans (T) Ltd, Profesa Arch Livin Mosha (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe, mara baada ya kuwasilisha mada na kuonesha shughuli za kitaalamu za usanifu wa nmajengo hapa nchini.

  0 0


  0 0  0 0  0 0  SERIKALI Kuu kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Handeni na Mkoa mzima wa Tanga, wameombwa kuingilia kati mgogoro mzito wa ardhi katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, ili kuepusha hatari inayoweza kutokea, ikiwamo vita ya wenyewe kwa wenyewe.

  Hayo yamesemwa juzi na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Handeni Kwetu Foundation inayofanya ziara katika maeneo mbalimbali, hususan ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, baada ya kuzinduliwa Mei 8 mwaka huu.

  Wakizungumza kwa uchungu mkubwa, wananchi hao walisema kuwa hali ni mbaya, maana kijiji chao kimeendelea kutekwa na kubaki eneo dogo lililoanza kuibua chuki za wazi kwa wananchi.

  Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Alhaj Ally Yasin Ling’ande, alisema kiuhalisia hakuna kijiji cha Komsala, kwakuwa hawana eneo la ardhi, hasa baada ya wilaya Korogwe kuingia kwenye eneo lao kwa kufikia hata kujenga mnada wa ng’ombe.

  “Ukiaangalia usawa palipojengwa mnada, utaamini kuwa hata kwenye shule ya Msingi Komsala pia patakuwa ni eneo la Korogwe, ingawa si sahihi kulinganaa na ramani ya mwaka 1978, jambo linaloonyesha kuwa huu ni mzozo utakaoweza kumwaga damu,” alisema.

  Naye William Seif alisema mbali na mipaka hiyo kuwa tata, pia kumekuwa na idadi kubwa ya wageni kumiliki heka zaidi ya 130 na bado wanaingia kwa wenye heka tatu wakiamini kuwa uwezo wao kifedha unawafanya wamudu kesi zinazoendeshwa kwenye mabaraza ya Kata na wao kupata haki.

  “Masikini akionewa anakimbilia kwenye Bazara la Kata, lakini huko kumekuwa na danadana nyingi, ukizingatia kuwa siku zote mkono mtupu haulambwi, ndio maana tunaoimba serikali ya wilaya ya Handeni, mkoa na wadau wengine wa ardhi kuja kujionea bomu hili linalosubiriwa kuripuka hapa kwetu,” alisema.

  Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bashiri Wabu, alisema kuwa ardhi katika kijiji chao imeuzwa kiholela kwa watu wenye nazo bila kufuata sheria za ardhi, ikiwamo ya kuandaa mkutano wa wananchi wote.

  “Kuna watu hawana maeneo kabisa ya kulima, wakati watu wachache wanamiliki maeneo makubwa ambayo hata kuyalima yote hawana uwezo huo, jambo linalokera na kuudhi mno kila tunapoliangalia suala hili katika kijiji chetu,” alisema Wabu, akiungwa mkono pia na Hemed Ngona, Kombo Twaha, wakisisitiza kuwa sheria za ardhi na utawala bora hazifuatwi katika kijiji chao.

  Katika mkutano huo ulioanza saa 9 alasiri na kumalizika saa 12 jioni, ulihudhuriwa na watu wengi, huku idadi kubwa ikiegemea katika kero ya ardhi na mipaka.

  Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Komsala anayemaliza muda wake, Mwanaidi Said, alisema kero kubwa katika kijiji hicho ni mipaka iliyoshindwa kutatuliwa na viongozi wa juu, licha ya kupeleka malalamiko yao mara kadhaa.

  “Kijiji cha Komsala sasa ni kama kitongoji tu, maana kimechotwa katika pembe zote na ndio maana hata wenzetu wa Korogwe wamekuja kujenga mnada wa ng’ombe kwa madai kuwa ni kwao, jambo ambalo hata mwenyekiti atakayefuata litamuumiza kichwa,” alisema na kuwafanya wananchi wapatwe na hofu.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo aliyetumia muda huo kuaga wananchi wake, sekeseke la mipaka limeshindwa kutatuliwa, huku akiwataka viongozi kulipa kipaumbele kabla ya matatizo hayajakikumba kijiji chao pale wananchi hao watakapotafuta haki yao.

  Naye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, aliwashukuru viongozi wa serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa kuwapa ushirikiano, ikiwamo kuruhusu kutembelea katika vijiji mbalimbali kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha utawala bora.

  “Naomba niwatoe hofu Watanzania wote kuwa mikutano hii ya hadhara hairatibiwi na chama chochote cha siasa, hivyo tunaomba tushirikiane kwa ajili ya kufanikisha maendeleo, hasa kama wananchi watahudhuria mikutano wanapoitwa na viongozi wao,” alisema.


  Ziara ya Handeni Kwetu Foundation ilianzia Kata ya Misima, ambapo wananchi wengi wameiunga mkono taasisi hiyo yenye lengo la kuwakomboa wananchi kwa kutoa elimu na kuhamasisha maendeleo ya jamii.

  0 0


  Na. Leonard Mwakalebela, Norway
   
  UJENZI wa mtambo wa kuchakata gesi asili kwa ajili ya matumizi mbalimbali (LNG) mjini Mtwara unakadiriwa kuchukua miaka takriban saba.

  Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Statoil Tanzania Bw. Thomas Mannes amesema kuwa, mambo yakienda kama yalivyopangwa, mtambo huo utakuwa tayari kwa uchakataji kati ya mwaka 2022 au 2023.

  Akizungumza na viongozi wa dini wa Tanzania waliotembelea mtambo wa uchakataji gesi wa Statoil uliopo Karsto, Bw.Mannes amesema kuwa mradi huo mkubwa utagharimu mabilioni ya dola za Marekani.

  "Tunakadiria itachukua kama miaka saba, mmoja kwa utafiti wa eneo kujua uimara wake kiufundi, miaka miwili ya utafiti wa kiuhandisi na michoro na miaka minne ya ujenzi wenyewe" alisema. Kwa mujibu wa Bw. Mannes,tayari wameishapendekeza maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa mtambo huo na hivi sasa wabia wa mradi wanateua timu ya pamoja itakayosimamia mradi huo.

  Mradi huo utakuwa wa pamoja kati ya Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini (TPDC) na kampuni za Statoil, BG, ExxonMobil, Ophir na Pavilion. Mradi huo utaenda sambamba na miradi mingine ya mafuta ya vitalu 1,3 na 4 inayoshirikisha TPDC, BG,Ophir na Pavilion na mradi wa gesi wa kitalu 2 wenye ubia kati ya TPDC, Statoil na ExxonMobil.

  Bw. Mannes alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na manufaamakubwa kwa Tanzania kwani kutoongeza mapato na nafsi za ajira, kutachochea biashara za bidhaa na huduma, kutoongeza mchango katika Pato la Ndani la Taifa (GDP) na kutaleta uwiano mzuri wa biashara.

  Aidha amewataka Watanzania hususani wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kujipanga izuri kwa ajili ya kufanya biashara ya bidhaa na huduma kwani kampuni yake itatoa kipaumbele wa kufanya biashara na wazawa.
  Bw. Mannes aliongeza kuwa mkataba kati ya Statoil na serikali ni wa manufaa kwa pande zote mbili na kuwa ni wa viwango na taratibu zote za kimataifa. Naye Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Bw. Ove Tungesvik alisema kuwa mtambo wa Karsto ndio mkubwa kuliko yote barani Ulaya.

  Kwa upande wao, viongozi hao wa dini wameishauri kampuni ya Statoil kuwajengea uwezo watanzania, kupitia mafunzo na programu nyingine, kama Wanorway walivyosaidiwa na wamarekani katika miaka ya 1970, ili watanzania nao waweze kuisimamia sekta ndogo ya mafuta na gesi katika miaka michache ijayo.

  Viongozi hao wa dini wapo mjini Stavanger, nchini Norway katika ziara ya mafunzo ya sekta ndogo ya mafuta na gesi. Ziara hiyo imeandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Serikali ya Norway kupitia kwa Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.

  0 0

   Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji Dkt. Diodorus B. Kamala akielezea lengo la ujio wa wawekezaji kutoka Ubelgiji kuja kuwekeza nchini Tanzania alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ujio wa wawekezaji wa nchi hiyo Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
   Waziri wa Miundombinu na Mawasilino Juma Duni Haji akiwa na watendaji wake wakuu wakimsikiliza Meneja mauzo  wa Kampuni ya ujenzi ya Anglo Belgian Corporation ya Ubelgiji walipofanya mazungumzo Ofisini kwake Kisauni.
   Wamiliki wa makampuni  toka Ubelgiji wakimsikiliza Mkurugenzi Uenezi wa Mamlaka ya Uendelezaji  Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Bi. Nasria Mohd Nassor (hayupo pichani)  walipofika ofisini kwake Maruhubi Mjini Zanzibar.
   Afisa Mipango wa Shirika la Bandari Zanzibar   Ali Haji akizungumza na wamiliki wa makampuni  kutoka Ubelgiji walipotembelea bandari ya Malindi mjini Zanzibar .
   Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akizungumza na ujumbe wa Wafanyabiashara  wa Makamupuni ya uwekezaji kutoka Ubelgiji walipomtembelea Ofisini kwake  Vuga Mjini Zanzibar.
  Picha ya pamoja ya wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na viongozi  wa Mamlaka ya Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar  (ZIPA).(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).


  0 0

  MSANII wa vichekesho (komedy) kutoka Nigeria,Okopcha Bright Onyekere maarufu kama Basket Mouth amewasifu wasanii wa Tanzania kwa juhudi wanazofanya kuelimisha jamii kutumia vipaji vyao.

  Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kuwasili kutoka Nigeria kwa ajili ya onesho maalum kushirikiana na wasanii wa Tanzania juzi Dar es Salaam alisema kutoka aanze sanaa ya vichekesho miaka 16 iliyopita amekuwa akipata sifa za wasanii wa Tanzania wakiwika katika fani za muziki, sanaa za filamu, michezo ya kuigiza na vichekesho.

  Onyekere aliyetamba nchini Nigeria na Bara la Afrika katika fani hiyo amekuja kufanya onesho moja lililopangwa kufanyika jana hoteli ya Golden Tulip, aliongeza kuwa sanaa ni utajiri mkubwa kama vipaji walivyopewa vitatumika ipasavyo na kutawala jukwaa .

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku alisema lengo la kumleta msanii huyo wa komedy ni kuimarisha sanaa ya vichekesho kwa wasanii chipukizi wa Tanzania ambao wanahitaji kuandaliwa kwa soko hilo nchini na nje ya nchi.

  Alisema Kampuni ya Vuvuzela imejitolea kusaidia wasanii wa vichekesho nchini na kuwafundisha namna watakavyoweza kuendeleza fani hiyo kazi iliyoanza miaka minne iliyopita kampuni ilipoanzishwa.

  Bukuku alisema kila mwisho wa mwezi kuna onesho maalum ambalo hutumika kuonesha vipaji vya wasanii wa vichekesho na jinsi msanii anavyoweza kutawala jukwaa kuwaburudisha watazamaji.

  Alisema kampuni yake inatarajia kufanya maonesho kama hayo mikoa mbalimbali ya Tanzania kuibua wasanii wengine wenye uwezio katika fani hiyo.

  Mkurugenzi Bukuku alisema katika onesho la karibuni Watanzania walikongwa nyoyo zao pale wasanii wa Tanzania washirikiana na wasanii wa vichekesho kutoka Kenya ambaye ni Mdomo Baggy na Dick Omondi kutoka Uganda anayejulikana kama Uncle Bob kufanya onesho kali nchini.

  Bukuku aliwashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia kufanyika kwa onesho hilo ambao ni Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA),Hoteli ya  Golden Tulip, Gazeti la Mwananchi Communications, Clouds Media Group, Ultimate security, Simu TV, Prime Advertising, Dar insites, Advertising Dar, Bongo 5, Eventlites, Hugo Domingo na Michuzi Blog.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi- Dodoma
  28/11/2014.
   
  Serikali imesema kuwa VICOBA ni taasisi binafsi inayomilikiwa na wananchi wenyewe vikiwa ni miongoni mwa tasisi ndogo za kifedha ambazo ni za kibinafsi na huanzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa ama kijijini, kitongojini na hata kwenye kata.

  Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rungwe Magharibi Prof. David Mwakyusa (CCM) ambaye alitaka kujua kama Serikali inatambua VICOBA  kama mkombozi wa wanyonge.

  Mwigulu amefafanua kuwa taasisi hizo zimo kwenye sekta ya fedha isiyorasmi na zinatoa huduma za kifedha mijini na vijijini.

   “Uwepo wa taasisi hizi, umewezesha kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi waliombali na huduma za sekta rasmi ya fedha na hivyo kuwa mkombozi wa wanyonge” alisema mwigulu.

  Aidha, kwa kutambua suala hilo, ili kusaidia na kuimarisha taasisi hizo, Mwigulu amesema kuwa Serikali baada ya kupata ushauri kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa masuala ya uchumi na tafiti za kijamii, inafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Taasisi ndogo za huduma ya fedha ya mwaka 2000 ili kuihuisha iweze kukabili na kuzingatia mabadiliko na maendeleo yanayojitokeza katika sekta hiyo.

  Vilevile Mwigulu amesema kuwa Serikali inakamilisha uhuishaji wa sera ya taasisi ndogo ndogo za kifedha ambapo hatua inayofuata ni kuandaa mapendekezo ya muswada ambayo yatapelekwa Baraza la Mawaziri mara baada ya kupata idhini na maelekezo ya Baraza hilo na muswada huo utafikishwa bungeni.


  Taasisi ya VICOBA ilianzishwa nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo imekuwa na manufaa kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini hususan wanawake waishio vijijini wamefanikiwa kuboresha kipato chao na maisha yao kwa ujumla kwa kujiunga na taasisi hiyo.

  0 0

   Eng. Ahmed Dau akila pozi baada ya kulamba Nondozzzz ya Masters of Science Degree in Petroleum, Energy, Economics and Finance katika Chuo Kikuu cha Aberdeen
   Eng. Ahmed na Wazazi wake Dr Ramadhani K Dau na Mrs Zeinab Dau Kwenye mahafari Chuo Kikuu cha Aberdeen 
  Waliosimama kutoka kushoto Meya wa London Haruna Mbeyu, Abdul Dau, Mohamed Janguo, Kheri Mahimbali (MSc oil and gas class of Feb 2014 Aberdeen). Walioketi kutoka kushoto Dr Ramadhani K Dau, Eng. Ahmed Dau na Mrs Zeinab Dau.

  0 0


  0 0  0 0

  Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48  kwa siku za Ijumaa na Jumamosi ya tarehe 28 na 29 November 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Mpiji, Bagamoyo na eneo la Chuo Kikuu Ardhi (Makongo Juu) 

  Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; 

  Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. 

  Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.  
       
  Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.

  Au piga simu huduma kwa wateja namba 022- 2194800
  Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

  Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.


older | 1 | .... | 654 | 655 | (Page 656) | 657 | 658 | .... | 3272 | newer