Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 650 | 651 | (Page 652) | 653 | 654 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu mwishoni mwa wiki amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mkinga na Pangani kuhimiza wanawake kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa Maabara.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi ya (UWT) kwa Bi. Halima Kassim mmoja wa wanachama wapya katika Kata ya Maramba, Wilaya ya Mkinga.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wapya wa UWT mara baada ya kuwakabidhi kadi zao. Waliosimama kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mkinga, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bi. Mboni Mgaza na Mbunge wa Viti Maalumu Al-Shymaa Kwegyir.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu (Wa nne kutoka kulia) akipata maelezo ya ujenzi wa maabara kutoka kwa Mwalimu Cyprian Taabani kutoka Shule ya Sekondari Daluni, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Daluni Mwanakombo Gobeto.
  Mh. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga akikabidhi bati (50) kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Hafsa Mtasiwa ikiwa ni jitihada za kuunga mkono ujenzi wa maabara.

  0 0
 • 11/24/14--00:00: ze kibonzooo


 • 0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mpango maalumu utakaowawezesha wateja wake wakubwa kufurahia huduma za ziada wawapo kwenye kazi zao.  Mpango huu wenye lengo la  kuwazawadia wateja wa Airtel utakuwa na  kadi maalumu ya kusafirisha yaani (Priority Pass)  itayowawezesha wateja wakubwa wa Airtel kupata huduma ya hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege duaniani na  pia  kupata punguzo la hadi asilimia 30 pindi watakapo nunua bidhaa na kupata huduma nchini

  Kufatia uzinduzi huo wateja wa Airtel sasa wataweza kuunganishwa na huduma za hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege zaidi ya 700 duniani na  hivyo kupata  viburudisho, urahisi wa huduma yaani (VIP services) pindi wasafiripo na kuwawezesha kufurahia safari zao

  Sambamba na hilo wateja hao pia watapata punguzo la hadi asilimia 30 pale watakapopata huduma au kununua bidhaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo hotel, migahawa, maduka makubwa and sehemu nyingine nyingi.

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo,Waziri wa Nchini katika ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu alisema” nawapongeza sana Airtel kwa kuzindua mpango huu maalumu na kuwazawadi wateja na watanzania nchini.  Nafurahi kuona pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano lakini bado tunashuhudia Airtel inajipanga na kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja wake.

  Natumaini kadi hizi maalumu tunazozindua leo zitawaweza watanzania kupata mwanya wa kutengeneza mahusiano na kutanua wigo wa marafiki wa kibiashara na mwisho kuweza kuvumbua fulsa mbalimbali za kibiashara duniani.”

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema “ kupitia huduma hii tunadhirisha lengo letu la kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu. Tunauhakika kadi hii maalumu  ya kupata huduma zenye hadhi katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani hazitarahisha  safari zao tu bali zitawawezesha kufanya mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara kwa wale watakaokutana nao wakati wa safari.

  Ni matumaini yangu kuwa mpango huu utaleta tija na kuwapatia wateja wetu unafuu wa kutanua biashara  zao,

  Katika halfa hiyo Airtel pia ilizindua pia huduma yake ya internet ijulikanayo kama Home Wi-Fi solution,

  kwa kupitia huduma hii ya Airtel Wi-Fi mteja anaweza kuunganisha simu zaidi ya 32 katika kifaa kimoja cha Wi-Fi , kuunganisha hadi simu za mkononi 4 na kuwaunganisha na Wi- Fi ya nyumbani hata kama wakiwa mbali na nyumbani wakati wote mahali popote nchini. Hii ina maana kwamba sasa wateja wa Airtel wanaunganishwa na kifaa kimoja cha familia , kwa kupitia kifurushi kimoja, kupitia huduma hii mpya ya Airtel Wi-Fi
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba wakipiga ngoma baada ya Waziri, kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akionyesha kadi maalum ‘Premier Card’ aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), baada ya kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.

  0 0

   Kijana Datius akiwa katika Picha ya Pamoja na Baba yake Mzazi (nyuma ya babu yake aliyevaa miwani) Babu zake na dada zake wakati alipotunukiwa nondo yake ya elimu kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE hapo jana
   Datius Akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake Mzazi (Kushoto) pamoja na Babu yake mdogo (kulia)
   Akivishwa taji na Dada yake aitwaye Neema
  Akiwa na Dada mara baada ya kulamba nondoz.Picha Zote na Josephat Lukaza wa http://www.josephatlukaza.com

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kikao cha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji walipokutana na Uongozi wa Mkoa wa Pwani.

  0 0

  Timu ya Abajalo ya Sinza jijini Dar es Salaam imefanikiwa kukata tiketi ya fainali ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 baada ya kuifunga Burudani FC ya Temeke mikoroshini mabao 3-1. Mabao ya Abajalo kwenye mchezo huo yalifungwa na Idd Kulachi ‘Kleberson’ aliyefunga mabao mawili kati ya matatu. Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulipigwa kwenye uwanja Bandari uliopo maeneo ya Tandika Mwembe Yanga. Kwa ushindi huo sasa Abajalo itacheza na Tabata FC kwenye fainali itakayopigwa siku ya jumapili ya tarehe 30/11/2014 pale pale kwenye uwanja wa Bandari,huku timu za Black Six ya Buguruni na Burudani zikipambana kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo iliyovutia mashabiki kibao mpaka sasa,Bingwa mwa mashindano hayo atapata pesa taslim shilingi milioni tano huku mshindi wa pili akipata milioni tatu na mshindi wa tatu akiambulia shilingi milioni mbili.Capture7

  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira,Mh Gaudentia Kabaka akifungua rasmi semina maalum kwa wamiliki wa hoteli ya nyumba za kulala wageni wa Mkoa wa Dodoma,iliyofanyika kwenye katika ukumbi wa mikutano wa Dodoma Hotel.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Bw. Daud Msangi akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya ufunguzi wa semina maalum kwa wamiliki wa hoteli ya nyumba za kulala wageni wa Mkoa wa Dodoma,liyofanyika kwenye katika ukumbi wa mikutano wa Dodoma Hotel.
  baadhi ya washiriki wa semina hiyo ya wamiliki wa hoteli pamoja na mameneja wa hoteli hizo
  Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF,Bw. Aloyce Ntukamazina akiwasilisha mada maalum juu ya sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kujiunga na GEPF.
  Meneja wa Kanda Mkoa wa Dodoma,Bw. Josephat Mshana akielezea faida za kujichangia katika mpango wa hiari uliobuniwa na GEPF (VSRS)
  Mkurugenzi wa hoteli maarufu mjini Dodoma Royal Village,Bw. Merley Shabiby akikabidhiwa cheti maalum cha ushiriki na msaidizi wa Waziri wa Kazi,Bw. Simon Mwanjali.

  0 0
 • 11/24/14--01:53: YALE YALEEEEE.....


 • 0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo, mkutano huo ulifanyika leo Novemba 23-2014 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.
  Washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji wa Sekta ya kilimo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua mkutano huo leo Novemba 23-2014 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo leo Novemba 23-2014 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo leo Novemba 23-2014 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha. (Picha na OMR)

  0 0
 • 11/24/14--03:25: Taarifa ya msiba
 • Ndugu Richard Kilimbe anasikitika kutangaza kifo cha Binti yake Doris Richard Kilimbe wa Mwanza kilichotokea tarehe 20/11/2014 na kuzikwa tarehe 23/11/204.Nawashukuru wote walioshiriki msiba huu na Mungu awabriki.

  0 0

  Mbunge Ritta Kabati
  Na MatukiodaimaBlog

  MBUNGE  wa   viti maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) amewakata   wananchi  kutokubali kudanganywa na  vyama  vya  siasa  vinavyounda umoja wa katiba  ya  wananchi (UKAWA)  juu ya mchakato  wa  katiba  iliyopenekeshwa  na badala yake  kuungana na  watanzania wapenda maendeleo  kuikubali  katiba   hiyo  muda  utakapofika.

  Mbuge Kabati  alitoa  kauli   hiyo kwa nayakati  tofauti juzi na  jana  wakati  wa  semina  zake za  ndani na wanawake  wanachama  wa UWT  katika wilaya ya  Iringa , Kilolo na Mufindi semina  iliyolega  kuwajengea  uwezo  wa  kujiamini kwa  wanawake  waliojitokeza  kugombea nafasi  mbali  mbali  za  uongozi wa  serikali  za mitaa na  vijijini .

  " Mimi  kama  mbunge  wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa   wajibu   wangu  ni pamoja na kukutana na  wananchi  wa  Iringa na  kuwajengea  uelewa   mpana  wa  katiba  hiyo  iliyopendekezwa  ila  muda  ukifika  wa  serikali  kutangaza mchahato  wa  kupokea maoni ya  wananchi   juu ya katiba   hiyo  iliyopendekezwa  basi   viongozi hao  waweze  kuelewa  zaidi  pamoja na  wananchi  wanaowazunguka..... hivyo  nitaendelea  kutoa  elimu  kwa  viongozi  wa chama katika  semina  mbali mbali"

  Kabati  alisema   kumekuwepo na  upotoshwaji  mkubwa ambao  umeendelea   kufanywa na UKAWA  kwa  kuzunguka  huku na kule  kujaribu  kupotosha  ukweli    juu ya katiba   iliyopendekezwa  kwa madai  kuwa  ni katiba ya  CCM jambo ambalo  ni upotoshaji mkubwa na  kuwa  mchakato  wa katiba    hiyo  ulifanywa na vyama vyote  na makundi  maalum.

  Pia  alisema  kuwa  kitendo  cha  baadhi  ya  wanasiasa  wasilolitakia  mema  Taifa hili kwa  kupotosha   juu ya katiba   hiyo ni  sawa na  kutaka  kuona  nchi haitawaliki   na   hivyo  kuamua  kuanza  upotoshaji  huo.

   Alisema  kuwa  si  kweli kama katiba  hiyo  iliyopendekezwa  haina jambo  lolote la msingi kama  ambavyo  UKAWA  wamekuwa  wakizunguka na  kupotosha  ila alidai kuwa ndani ya katiba   hiyo  kuna mambo  mengi  yamezingatiwa  kwa  ajili  ya  wananchi  na  Taifa   kwa   ujumla.

  Akielezea  kuhusu  mchakato  wa uchaguzi  wa  serikali  za  mitaa ,vijiji na vitongoji  unaotaraji  kufanyika  hivi karibuni  alisema  kuwa  upande  wa  mkoa  wa  Iringa  wanawake  baada ya  kuhamasishwa  wamepatika  kujitokeza  kwa   wingi  kuchukua  fomu  za  kuwania nafasi mbali mbali  za  uongozi na kuwa  baadhi ya maeneo  wamepata  kushinda kwa  kishindo nafasi  walivyoomba ndani ya CCM wakisubiri  uchaguzi  rasmi wa serikali .

  Hivyo aliwataka  wananchi wa  mkoa  wa Iringa  kujitokeza  kuwapa kura  zao  wanawake hao  waliogombea nafasi mbali mbali na  kuwa  imani  yake  kuona kunakuwa na uongozi mchanganyiko.

  0 0

  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Kodi Tanzania (TAWNET) umeipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuwa moja kati ya walipa kodi bora wakubwa wa pili kwa mwaka 2014.

  Sambamba na kampuni ya Vodacom, TAWNET pia imeipongeza kampuni ya bia Tanzania (TBL) na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kuweza kushika nafasi katika makampuni matatu bora. Mwaka huu, mchango wa Vodacom katika pato la taifa umeongezeka na kuisukuma kampuni hiyo katika nafasi ya pili kutoka ya tatu waliyoshika mwaka jana. 

  Mkurugenzi Mtendaji wa TAWNET Judica Tarimo aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, Vodacom imeshika nafasi ya pili bora kwa mara ya kwanza haijawahi kutokea na 
  Kodi ni chanzo kikuu cha mapata kwa serikali na ndiyo inaiwezesha kutoa huduma kwa wananchi. Kwa niaba ya wana TAWNET napenda kutoa pongezi za dhati kwa Vodacom kwa kulipa kodi kwa uaminifu na pia makampuni mengine yafuate mfano huu, alisema.

  Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, Vodacom imekuwa mdau mzuri wa maendeleo kwa Watanzania na kuongeza kuwa uwekezaji wake umekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi kwani pamoja na kuwa mlipa kodi mzuri wa pili, pia kupitia mfuko wake wa jamii kusaidia wa Vodacom Foundation kampuni hiyo imeweza kusaidia watanzania wenye matizo mbali mbali

  Alisisitiza kuwa nchi inaweza kuondokana na utegemezi wa ufadhili endapo kila mtu na makampuni yatalipa kodi kwa uaminifu na kuzitaka mamlaka zinazohusika kuwa macho dhini ya watu na makampuni yanayotumia mbinu mbali mbali kukwepa kulipa kodi ahalali za serikali

  Kuhusu kodi zilizolipwana Vodacom katika kipindi cha miaka miwili na kuifanya kampuni hiyo kuwa miongozi mwa walipa kodi bora Mtendaji wake Mkuu, Mkuu Rene Meza anasema“katika kipindi cha miezi sita cha mwaka wetu wa fedha kuanzia mwezi Aprili mpaka Septemba 2014,tumelipa kodi serikalini shilingi 27.6 bilioni/- kwa Kodi ya mapato,na tulikusanya shilingi bilioni 141.5 kwa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi ya zuio kwa niaba ya serikali”.

  Pia aliongeza kuwa mwaka jana Vodacom ililipa kodi ya shilingi 47.1 bilioni/-kwa kodi ya mapato pia ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 262.8 za kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) ,kodi ya zuio na kodi nyinginezo zinazolipa serikalini. “Tunatimiza taratibu za kulipa  kodi kulingana na sheria za serikali na kuendelea kutimiza matakwa ya serikali.Ushindi huu tulioupata kwa mara ya pili ni uthibitisho wa kutosha”.Alisema.

  Kuhusiana na uwekezaji mtendaji huyo Mkuu wa Vodacom anasema kampuni   hadi kufikia sasa Vodacom imewekeza nchini zaidi ya shilingi trioni 1.7/- na bado ina dhamira ya kuendelea kuwekeza na kukuza sekta ya mawasiliano nchini.

  TAWNET ni asasi isiyokuwa ya Kiserikali inayojitegemea ambayo inaundwa na waandishi wa habari wenye mapenzi ya kuandika habari za kodi ikilenga kuwajengea  uwezo waandishi wa habari ili kubobea katika uandishi wa masuala ya kodi.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King, akitoa shukrani kwa kampuni ya ALAF  kwa kujitolea mabati kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Wilaya ya Mbeya.
   Meneja wa Kampuni ya ALAF Tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kabla ya kumkabidhi msaada wa mabati 384 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara.
    Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigallah King na Meneja wa ALAF tawi la Mbeya, Greyson Mwakasege wakikabidhiana mabati 284 kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Kata.
   Fundi umeme na mtaalamu wa Mashine wa Kiwanda cha kuzalisha mabati, Himid Mwenzegule akiendelea kuendesha mitambo ya mashine ya kuzalisha mabati kiwandani hapo.
   Mashine ya kuzalisha mabati ya migongo ya kawaida aina ya Corrugator ikiendelea na kazi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0
 • 11/24/14--11:13: Article 6


 • 0 0


  Imagen M-bet
  logotipo M-Bet
  BETI HEWANI (ONLINE) SASA NA M-BET NDANI YA TANZANIA
  www.m-bet.co.tz
  Furahia mpira na ushinde pesa kwa Tuvuti (Website) mpya ya M-Bet.
  Fungua akaunti ya M-Bet na upate kubeti bure.
  Kulipa na Mpesa , na Tigo pesa ita kuja hivi karibuni.
  Boton


  0 0

  Only a four days remaining before Africa's King of Standup Comedy sets foot in Tanzania for the very first time!! It's a show NOT to be missed.


  0 0

  Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.

  SARATANI NI NINI?
  Saratani ni jina la gonjwa ambao hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo.  Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.

  NINI KINATOKEA
   Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takriban miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake.  
  Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. 
  Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya '50 Plus Campaign' anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini humo, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.

  VIHATARISHI VINAVYOCHANGIA SARATANI YA TEZI DUME

  ·         Umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.
  ·         Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.
  ·         Suala jingie ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.
  ·         Vilevile wataalamu wanatuambia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
  ·         Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.


  0 0

  "NAMSHUKURU MUNGU KWA KUCHAGULIWA KUSHIRIKI KAMA MSIMAMIZI KWENYE WORLD CUP YA WAPISHI INAYOFANYIKA KILA BAADA YA MIAKA 4 NITAPEPERUSHA BENDERA YA NCHI YANGU TANZANIA NI JAMBO LA KUJIVUNIA SANA".

  Mpaka sasa Chef Issa Kapande mbali ya kushinda tuzo nyingi tofauti ndani na nje ya nchi katika fani yake ya upishi pia anashikilia rekodi ya kua Chef Mtanzania Msomi na mdogo kuliko wote aliewahi kufungua na kuongoza hotel ya nyota tano ( Certified Executive Chef) akiwa na umri wa miaka 25 tu. Hili ni jambo la kujivunia sana.

  Mola ajaliapo anatamani sana mwaka 2018 aipeleke Tanzanian chefs national team kwenye mashindano haya na anaimani atafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonyesha uwezo wao Mungu ibariki Tanzania.
  Chef Issa Akiwa na Mr Wyne aliekua FB manager wakati huo.
  Tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wa chef Issa kwa chakula cha kiafrica ndio tuzo ya mwisho aliopata mwaka jana mwezi wa 10
  Chef issa akiwa na jaji mkuu wa mashindano ya kumpata mpishi bora wa mwaka wa Sweden.
  Chef Issa Akiwa kazini anamuwekea kuku wa kuoka viungo tayari kwa kuliwa.
  Hapa chef Issa Kapande akiwa na management team ya East African All suits hotel alipofungua hotel ya nyota tano na kuandika historia ya kua certified Tanzanian Executive chef katika umri wa miaka 25 tu. Hotel ilifunguliwa na aliekua Makamu wa Rais wakati huo ambaye sasa ni Rais wa Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati walioketi). 

  kwa habari zaidi za kombe la dunia la wapishi unaweza zipata hapa http://www.vatel.lu/competitions.php

  kwa habari zaidi za mapishi na za chef Issa unaweza like facebook page https://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534

  0 0older | 1 | .... | 650 | 651 | (Page 652) | 653 | 654 | .... | 3272 | newer