Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 649 | 650 | (Page 651) | 652 | 653 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia CCM inasimamia uwajibikaji na kama mtu amekosea awajibike na akishindwa atawajibishwa mapema.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pongezi vijana Lindi waliojiunga na UVCCM mkoa wa Lindi kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini mkoa Lindi.


  0 0

   Mwili wa Mwandishi wa Habari marehemu Baraka Karashani ukiwasili katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
   Mke wa Marehemu, Baraka Karashani, Gloria na watoto wake Bonny na Belinda wakiweka shada la maua katika kaburi wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
  Mzee Phili Karashani akitoa neno la shukrani wakati wa mazishi ya mtoti wake Baraka Karashani.
   Mtoto wa marehemu, Baraka Karashani akiwa ameshika picha ya marehemu baba yake.
   Phili Karashani na mkewe akiweka shada la maua katika kaburi mtoto wao Baraka Karashani.
   Mchungaji akiweka shada la maua.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Amir Mhando akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Baraka Karashani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mtangazaji mkongwe wa radio anaesikika siku hizi kupitia radio EFM 93.7, Dennis Ssebo (pichani), hatimaye amejiunga na mtandao wa kijamii  wa twitter, baada ya miaka yote kuweka msimamo wa kutojihushisha na mitandao ya kijami kwa kuwa alikua haoni faida zake.

  Alipo ulizwa na Globu ya Jamii  kwanini ameamua kujiunga, Ssebo alijibu, "Radio yangu ya EFM na hususani Manager wa Radio, Bwana Geoffrey Ndawula amenifungua macho juu ya faida za twitter, 

  "Hata hivyo najiunga na twitter tu. Sintojiunga na mitandao mingine kama facebook na instagram kwa sababu Bado sijaona faida zake", alisema Ssebo ambaye kitaaluma ni wakili pia.

  Unaweza kumufollow Ssebo kupitia @ssebodennis

  0 0

   Waziri wa Nchi(Kazi Maalum) Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya,Rev Dr Thadeus Mkwama,Makamu Mkuu wa SAUT,na Mwadhama Baba Askofu Desderius Rwoma,Mkuu wa Chuo,wakiwa kwenye maandamano ya ya taaluma, ya Maprofesa. 
   Maandamano yakiendelea
   Profesa Mwandosya,Rev Dr Thadeus Mkwama,Makamu Mkuu wa SAUT,na Mwadhama Baba Askofu Desderius Rwoma,Mkuu wa Chuo,wakiwa kwenye maandamano ya ya taaluma, ya Maprofesa. 
   Waziri Mwandosya akisalimiana na wakufunzi wa SAUT.
   Picha ya pamoja ya Prof. Mwandosya na wahadhiri wa SAUT baada ya mahafali.
   Waziri Mwandosya akitoa mhadhara kwenye mahafali hayo
   Mgeni Rasmi katika Mahafali,Profesa Mark Mwandosya,Waziri wa Nchi(Kazi Maalum) Ofisi ya Rais, akipokea shukrani za Chuo Kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Rev.Dr Thadeus Mkamwa.Anayeangalia kushoto ni Baba Askofu Desderius Rwoma, Mkuu wa Chuo Kikuu hicho
   Mgeni Rasmi Prof. Mark Mwandosya akiwa na Uongozi wa Chuo na Uongozi wa Mkoa.Kutoka Kushoto kushoto ni Prof. Cathian Magori,Mkuu wa Chuo Kikuu cha Saut tawi la Ifakara,Dr Dominic Negussie,Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo,Mhandisi Evarist Ndikilo,Mkuu wa Mkoa, Rev.Dr Thadeus Mkamwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu,Saimon Filbert Rais wa Serkali ya Wanafunzi SAUT.Waziri Mwandosya,Mhe Baraka Konisaga,Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,Baba Askofu Rwoma,Mama Lucy Mwandosya,na Marygoreth Gervas,Makamu wa Rais Serikali ya Wanafunzi SAUT
  Waziri Mwandosya na Mkuu wa Mkoa Eng.Ndikilo (wa pili kulia) wakiwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Picha na Freddy Maro.

  0 0
 • 11/22/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Upendo Nkone - Upendo wa Yesu

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa tatu kutoka kushoto) akizindua Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 20 Novemba 2014. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sammy Mollel (kulia).
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (kushoto) akihutubia wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, washiriki (exhibitors) na wanunuzi wa madini ya vito ambao wamehudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yanayofanyika jijini humo kuanzia tarehe 18 hadi 20 Novemba, 2014.
  Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,wakifuatilia majadiliano uendelezaji endelevu wa madini ya Tanzanite nchini. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, John Nayopa, Kamishna Msadizi wa Madini-Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane, na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim.
  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara, nchini Thailand, Tony Brooks akionesha machapisho mbalimbali kuhusu madini ya Vito kwa mgeni rasmi wa maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kushoto), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa kwanza kutoka kushoto). Nchi ya Thailand ina uzoefu mkubwa katika uandaaji wa maonesho ya Vito ambapo wameshafanya maonesho zaidi ya 50 na wafanyabiashara wa madini ya Vito kutoka Tanzania wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo.
  Wachimbaji wadogo wa madini ya vito kutoka ukanda wa Umba mkoani Tanga waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha wakiwa kwenye banda wanalouzia madini hayo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Pamoja nao ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Tanga, Mjiolojia Elias Kayandabila (wa nne kutoka kushoto).
  Watendaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bruno Mteta, (wa pili kutoka kulia), Meneja Mipango na Utafiti, Julius Moshi (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Eng. Yisambi Shiwa (wa tatu kutoka kushoto) waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito Arusha, wakisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Eng. Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto) aliyetembelea banda la Wakala huo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
  Washiriki kutoka nchini Rwanda wakiwa na mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kulia), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa nne kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sammy Mollel, (wa nne kutoka kulia_mstari wa mbele).
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa kwanza kulia) akizungumza na mfanyabiashara wa madini nchini, Peter Pereirra mara alipotembelea banda la mfanyabiashara huyo katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha. Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja.

  0 0

   Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma,  jana Jumamosi Novemba 22, 2014
   Mhe David Kafulila akiwa kanisani  na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa  kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
   Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi 
  Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba  harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe  Zitto Kabwe na Mhe David  Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma

  0 0

  Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Muhitimu aliyefanya vizuri Shahada ya Kwanza ya Jinsia na Maendeleo, Nyamambara Simon katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika Dar es Salaam leo. W apili kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila.
   Wimbo wa Taifa ukiimbwa- Kutoka kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph na Mjumbe wa Bodi Dk.Terezya Huvisa (MB).
   Vyeti vikiendelea kutolewa.
  Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na viongozi wa chuo hicho.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia CCM inasimamia uwajibikaji na kama mtu amekosea awajibike na akishindwa atawajibishwa mapema.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pongezi vijana Lindi waliojiunga na UVCCM mkoa wa Lindi kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini mkoa Lindi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.
  KWA BICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Nusu ya fainali ya kwanza ya mashindano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP imepigwa hapo jana kwenye uwanja wa Bandari maeneo ya Tandika Mwembe Yanga kati ya Tabata FC na Black Six,mchezo ulimalizika kwa tabata kushinda bao 1-0 na kukata tiketi ya kucheza fainali hapo tarehe 29/11/2014 kwenye uwanja huo huo wa Bandari.mchezo huo uliweka rekodi ya mashindano ya NDONDO kwa kuhudhuliwa na mashabiki wengi.10553574_836086276455319_1176921432347220072_n Mashabiki wa BLACK SIX ya Buguruni.......... 1960140_836086329788647_6126915949753505475_nMshambuliaji wa YANGA Jerry Tegete alikuwa anaongoza mashambulizi ya timu yake ya nyumbani TABATA FC....... 10350425_836086403121973_4713464705511470346_nMkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Bwana Ruge Mutahaba,Fauzia Abdi pamoja Ibrahim Masoud 'Maestro' walikuwepo kushuhudia mpambano huo..... 
  10382399_836086466455300_4570599094018049969_o
  Nyomiiiii.....10408076_836086479788632_905767488845041078_nMpambano kati ya Tabata FC na Black Six ukiendelea kwenye uwanja wa BANDARI maeneo ya Tandika Mwembe YANGA ukiendelea...... 


  0 0


  0 0

  SERIKALI kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kuongeza ufanisi zaidi katika Tamasha la Krismasi mwaka huu kwa sababu  kupitia matamasha yake anafanikisha matakwa ya jamii yenye uhitaji maalum. 

  Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza alisema  kwa mwenendo huo bora unaofanywa na Msama anatoa wito kuendeleza mwenendo huo ili kuisaidia jamii.
   
  Mungereza alisema Msama anafanikisha hayo kwa sababu anaipenda jamii ambako alitoa wito kwa wadau wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 hapa nchini ili kufikia malengo stahili.
   
  Katibu huyo alisema mbali ya kuchangia jamii pia kupitia tamasha hilo wananchi  wa maeneo husika wanapata fursa nyingi katika maeneo yao kama madereva bodaboda, texi na biashara nyingine.
   
  “Wananchi wa mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo watambue kwamba ni lao, hivyo wajitokeze kwa wingi kwani viingilio vitakavyopatikana vinasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, wajane, walemavu na wengineo,” alisema Mungereza.
   
  Kuhusu waimbaji, Mungereza alisema waichukulie sanaa kwamba ni kazi  watumie vipaji vyao hasa wakifikiria jamii kwani wanahitajika kutoa elimu ya uraia kutoka kwao.
   
  Katika hatua nyingine, Kampuni ya Msama imepokea kibali cha kufanikisha Tamasha la Krismasi mwaka huu ambako kampuni hiyo imejipanga kufanya tamasha hilo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
   
  Naye mmoja wa Watendaji wa Kampuni ya Msama, Jimmy Rwehumbiza aliyepokea kibali cha Tamasha la Kriamsi aliishukuru Basata kwa kufanikisha kibali sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo yanayotolewa mara kwa mara yanayofanikisha matamasha hayo.

  0 0


  The NBC Head of Corporate and Investment Banking, Theobald Sabi (left) signs documents with Executive Director for MTT Limited which is the sole authorised dealer of JCB products in Tanzania, Mr Andrew Fimister (right) at an event where the two signed Preferred Supplier Agreement on behalf of their two organisations in Dar es Salaam on Friday. The agreement allows the facilitation of the origination of financing of JCB goods with NBC as the preferred financier and MTT as the supplier. Other are: NBC Head of Global Corporates, Wilson Nkuzi (behind Mr. Theobald) and MTT Limited General Manager, Yogesh Tripathi.
   The NBC Head of Corporate and Investment Banking, Theobald Sabi (left) exchange documents with Executive Director for MTT Limited which is the sole authorised dealer of JCB products in Tanzania, Mr Andrew Fimister (right) at an event where the two signed Preferred Supplier Agreement on behalf of their two organisations in Dar es Salaam on Friday. The agreement allows the facilitation of the origination of financing of JCB goods with NBC as the preferred financier and MTT as the supplier. Other are: NBC Head of Global Corporates, Wilson Nkuzi (second left) and MTT Limited General Manager, Yogesh Tripathi.

  0 0

   TAREHE 22 NOVEMBER 2014 UMOJA WA WANAFUNZI WA KITANZANIA WANAOSOMA JIJINI WUHAN CHINA (WUHAN TANZANIAN STUDENTS ASSOCIATION) ULIWAONGOZA WATANZANIA WANAOISHI JIJINI HUMO,KATIKA KUITANGAZA NCHI YA TANZANIA KATIKA MAONESHO HAYO YA KITAMADUNI YALIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU CHA WUHAN(WUHANI UNIVERSITY) NA KUSHIRIKISHA MATAIFA MBALIMBALI YA AFRIKA,ULAYA ,AMERIKA YA KUSINI,AMERIKA YA KASKAZINI NA ASIA.
  AMBAPO WUTASA ILITUMIA FURSA HIYO KUITANGAZA TANZANIA IKIWEMO MBUGA ZA WANYAMA,VYAKULA VYA KITANZANIA,MUZIKI NA MAVAZI PIA.
    MWANA MAMA WA KICHINA NA MWANAYE WAKIWA WANASUBIRI MUDA WA KUPATA HUDUMA UANZE.
   KATBU MKUU WA WUTASA(KULIA) NDUGU HASSAN MKOKO NA NDUGU NOEL ERNEST WAKIWA WANATOA HUDUMA KWA WAGENI WALIOTEMBELEA BANDA LA TANZANIA 
   WAGENI WAKIPATA HUDUMA KATIKA BANDA LA TA NZANIA
   SEHEMU YA MAELFU YA WATU WALIOKUWEPO KWENYE MAONESHO
   WAGENI WAKIENDELEA KUPATA HUDUMA KWENYE BANDA LA TANZANIA 
   HATA VYAKULA VYA KITANZANIA NAVYO VILIKUWEPO. HAPA WAGENI WAKIJIPATIA MLO WAO WA MCHANA WA KITANZANIA
   MHASIBU WA WUTASA ELVIS MULOKOZI AKIWA ANATOA HUDUMA KWA WAGENI,HUKU MWANADADA MARY NAFTALI AKIWA UPANDE WA KUGAWA MSOSI(CHAKULA CHA KITANZANIA 
  BAADHI YA WANAFUNZI WA KITANZANIA KWENYE MAONESHO HAYO

  0 0

   Furaha ilishika nafasi pale mwanadada shilole alipowasili uwanja wa kimataifa wa ndege wa Zaventem jijini Brussel.
   Msanii Shilole akiwa na furaha baada ya kupokelewa na wenyeji wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem jijini Brussel.
  The Big Boss Mohammed akiwa na msanii Shilole muda mfupi tu baada ya kuwasili uwanjani Brussel. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
  Theme: Prevention Beyond Mother-to- Child Transmission (PbMTCT)

  Collaborating with: Mildmay Uganda and Profam Royal Domiciliary Clinic

  Description: In order to achieve " Getting To Zero", CSI joins the global community in the fight against HIV and AIDS by strengthening efforts to prevent future mother-to child transmissions and reaching out to adolescents and youth with educational materials and information to protect themselves. 

  The CSI theme "PbMTCT" is to engage more parents, guardians, teachers, healthcare providers, community and religious elders to protect, help, and teach the future generation about HIV and AIDS. Unable to join?, click here to learn how you can support - Thank you.

  0 0
  Nyumba ya Maarifa (NIP) mkabala ATCL House, Ghorofa ya Kwanza, Mtaa wa Ohio,
  S.L.P. 79868, Dar es Salaam. Simu: +255 22 2127464, Nukushi: +255 22 2126399
   Barua pepe: info@tapsea.org, Tovuti: http://www.tapsea.org
   
  VIONGOZI WAPYA WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA WATAMBULISHA OFISI MPYA ZA CHAMA

  MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA – TAPSEA ANAWAJULISHA MAKATIBU MAHSUSI WOTE TANZANIA KUWA OFISI YA TAPSEA IMEHAMIA KATIKA JENGO LA NYUMBA YA MAARIFA (NIP) MTAA WA OHIO.  WANACHAMA WOTE MNAOMBWA KUKAMILISHA UANACHAMA IKIWA NI PAMOJA NA KULIPIA ADA YA MWAKA KUPITIA AKAUNTI NAMBA 0150031411800 CRDB AZIKIWE BRANCH, AU AKAUNTI NAMBA 2236600363 NMB HOUSE.  

  NA WALE AMBAO HAMJAJIUNGA NA CHAMA MNAOMBWA MJIUNGE, FORM ZINAPATIKANA KWENYE MTANDAO WA TAPSEA, KATIKA OFISI ZA CHAMA NA KWA WAWAKILISHI WA MIKOA.

  OFISI ZIKO WAZI KUANZIA SAA 1:30 ASUBUHI MPAKA SAA 11:00 JIONI. 
  WOTE MNAKARIBISHWA KUPATA HUDUMA ZA CHAMA.


  IMETOLEWA NA

  ZUHURA S. MAGANGA
  MWENYEKITI – TAPSEA


  0 0

   
  Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry  na Ernest Napoleon
  Blog ya swahilivilla imepata furasa ya kufanya mahojiano na muigizaji, muongozaji na muandishi wa  filam ya kwanza Afrika Mashariki kukubalika kuuzwa kupitia iTunes ‘Going Bongo Ernest Napoleon a-filamu-ya-kwanza-afrika-mashariki-kukubalika-kuuzwa-kupitia-itunes-07-2014/
  Pata filamu hiyo ya kihistoria kwenye iTunes bit.ly/goingbongoitunes ama DVD bit.ly/goingbongodvd. Check trailer hapa bit.ly/goingbongotrailer, share na wenzio.
  Jiunge nasi ka kusikiliza
   
  Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry  na Ernest Napoleon
  Blog ya swahilivilla imepata furasa ya kufanya mahojiano na muigizaji, muongozaji na muandishi wa  filam ya kwanza Afrika Mashariki kukubalika kuuzwa kupitia iTunes ‘Going Bongo Ernest Napoleon a-filamu-ya-kwanza-afrika-mashariki-kukubalika-kuuzwa-kupitia-itunes-07-2014/
  Pata filamu hiyo ya kihistoria kwenye iTunes bit.ly/goingbongoitunes ama DVD bit.ly/goingbongodvd. Check trailer hapa bit.ly/goingbongotrailer, share na wenzio.
  Jiunge nasi ka kusikiliza
  Angalia Trailer ya Filam Going Bongo 

older | 1 | .... | 649 | 650 | (Page 651) | 652 | 653 | .... | 3270 | newer