Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Musalia Mudavadi akubali matokeo, Uhuru Kenyatta bado anaongoza

$
0
0
Mgombea urais Kenya Bw. Musalia Mudavadi 
akitangaza kukubli matokeo leo na kuwatkia heri 
Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kwa kuongoza katika
matokeo hadi sasa.

 Matokeo hadi dakika hii saa 10 na dakika 20 ni:
 Uhuru Kenyatta ana: 5,115,704 
 Raila Odinga ana : 4,513,223

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AKAMILISHA ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA MAHAKAMA ZA MWANZO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh: Angellah Kairuki (mwenye nguo ya njano) akioneshwa kiwanja kitakachojengwa Mahakama ya Mwanzo Kawe wakati wa ziara yake ya kutembelea Mahakama za Mwanzo jijini Dar Es Salaam iliyomalizika jana. Wa kwanza kushoto ni Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Kinondoni Mh. Aniceta Wambura na wapili kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kawe Mh. Mary Katabi.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (katikati) akifafanuliwa jambo na Mh.Sofia Mwaipopo (kushoto) Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Magomeni wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mahakama hiyo jana jijini Dar es salaam.Hapo waliposimama ni jengo la mahabusu la Mahakama hiyo. Aliyeko kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Kinondoni Mh. Aniceta Wambura.

ZIARA YA DK.SHEIN WILAYANI MAGHRIBI UNGUJA YAMALIZIKA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu,Dk.Juma Malik Akili,(kushoto) alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja wa Ndege,unaoendelea,akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi Unguja iliyomalizika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuweka jiwe la msingi ukumbi wa mikutano wa Ushirika wa Meli Nne Saccos,alipokuwa katika katika ziara ya Wilaya ya Magharibi Unguja iliyomalizika leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

taarifa kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF) leo

TUME YA UCHUNGUZI WA KUSHUKA UFAULU KIDATO CHA NNE 2012 YAWAOMBA WATANZANIA KUTOA USHIRIKIANO

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya kuchunguza kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 Prof. Sifuni Mchome akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi hadidu za rejea zitakazotumika kupata ukweli kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya kuchunguza kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 Prof. Sifuni Mchome (katikati)akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kwa zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka wadau mbalimbali. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kushoto) na Bi.Tunu Temu mjumbe wa Sekretarieti ya Tume hiyo.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

WAFANYAKAZI WA VODACOM WALIVYOSHEREHEKEA SIKU YA WANAWEAKE DUNIANI LEO

$
0
0

Wanawake wanaofanya kazi katika kampuni ya mawasiliano ya Vodacom wakibadilishana mawazo wakati wa kusherehekea sikukuu ya wanawake duniani.
Baadhi ya wanawake wanaofanya kazi katika kampuni ya mawasiliano ya Vodacom wakiwa kwenye pozi wakati wa kusherehekea sikukuu ya wanawake duniani.

ABSALOM KIBANDA AANZA MATIBABU AFRIKA YA KUSINI

$
0
0
Mdau Mwanvita Makamba, akiwa katika Chumba alicholazwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd,Absalom Kibanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, wakati alipomtembelea kumjulia hali katika Hospitali ya Milpark baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo jana usiku nchini Afrika ya Kusini.
Mhariri Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd,Absalom Kibanda akiendelea na matibabu katika Chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali hiyo. Picha na Amanitanzania.

The African Court hears the Matter of the Beneficiaries of the late Norbert Zongo and others against the Republic of Burkina Faso


TFF bado yasisiza kukutana na Waziri wa Michezo

$
0
0
ZIKIWA zimebaki siku mbili baada ya Serikali kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hadi Jumatatu Machi 11 kutangaza kutekeleza maelekezo waliyowapa, Rais wa Shirikisho hilo Leodegar Tenga ameomba kuonana tena na Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk. Fenela Mukagara ili kuzungumzia upya suala hilo na sasa watakutana March 19.

March 2 Rais Tenga alitangaza kukutana na Waziri Mukangara jana Alhamasi March 7 kwa lengo la kuzungumza naye kuwa maagizo ya kuikataa katiba yao na kutaka kufanya uchaguzi kwa kutumia katiba ya mwaka 2006 hayatekelezeki na kwamba wanaomshauri Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo wanamshauri vibaya na hawaijui katiba ya TFF.

"Kamati ya utendaji haitaki hata kidogo kubishana na Waziri, tunaamini wakati anatoa maagizo yake hakujua ugumu na madhara yake na waliomshauri hawakumshauri vizuri.....:"Tunaomba kukutana naye tumueleze ajue kabisa agizo alilolitoa alitekelezeki na tutamshauri madhara yake kwa serikali kuingilia TFF madhara yake ni kufungiwa." alikaririwa akisema Tenga mapema wiki iliyopita.

Hata hivyo Waziri Mukangara aliwaita viongozi wa TFF wakiongozwa na Katibu mkuu Angetile Osiah Jumanne wiki hii na maagizo waliyopewa viongozi hao wa TFF ni kuhakikisha hadi kesho kutwa Jumatatu TFF itangaze kutekeleza maagizo waliyopewa na serikali ikiwemo kuitisha mkutano wa marekebisho ya katiba ndani ya siku 40 kuanzia Juzi na wahakikishe wamefanya marekebisho hayo hadi ifikapo Aprili 15.

Pia serikali iliwataka TFF kuhakikisha inaanza upya mchakato wa uchaguzi na hadi Mei 25 uchaguzi huo uwe umefanyika kwa kutumia katiba ya mwaka 2006 ikiwemo na marekebisho yote hadi ya mwaka 2010.

Hata hivyo, Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah leo aliwambia waandishi wa habari kuwa, Tenga ambaye alikuwa nje ya nchi amerejea juzi na kwamba tayari amewasiliana na Waziri Mukangara na kumuomba asitishe maamuzi yote ambayo ameshayatoa na anayotarajia kuyafanya.

"Katika barua pepe ambayo amemuandikia Waziri ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi, Rais Tenga ameeleza kuwa alikwenda ofisini kwake tarehe 7 March kujaribu kumuona lakini akaambiwa amesafiri, hivyo kuomba kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara, ambaye pia hakuwepo ofisini na hatimaye akakutana na Naibu Katibu Mkuu.

" Katika barua hiyo pepe, Rais Tenga amemshukuru Waziri kwa kuonana na ujumbe wa TFF juzi March 6 na kukubali kukutana naye tena March 19 kwa ajili ya mazungumzo juu ya maagizo yake pia kumuarifu amepokea maagizo yake aliyoyatoa kupitia kwa mjumbe wetu wa kamati ya utendaji kwa njia ya barua.

"Kwa heshima na taadhima, kukuomba usitishe hatua yoyote ile unayodhamiria kuchukua hadi hapo tutakapokutana na kupata maelezo yetu, TFF, juu ya maamuzi na maagizo uliyoyatoa.” alisema Angetile akinukuu waraka wa Tenga.

Tenga, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) aliondoka jana (Machi 7 mwaka huu) kwenda Marrakech, Morocco kuhudhuria kikao cha kamati hiyo na pia Mkutano Mkuu wa CAF ambao umepangwa kufanyika Machi 10 mwaka huu ukihusisha pia ajenda ya uchaguzi wa rais.

Rais Kikwete amjulia Hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda,pia ahudhuria Mkutano wa Viongozi wa vyama vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika nchini Afrika ya Kusini leo

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini leo jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).
Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Freeedom Park mjini Pretoria Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyioshiriki katika harakati za ukombozi Kusini Mwa Afrika.
Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(Katikati) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa vyama vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika leo mchana.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa FreedomPark,Jijini Pretoria Afrika ya Kusini. Kushoto ni Rais Jakaya Kikwete mbaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni kiongozi wa ZANU PF.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ambaye pia ni kiongozi wa ANC(Watatu kushoto),Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC.(picha na Freddy Maro).

MBIO ZA URAIS KENYA, NGOMA BADO MBICHI

$
0
0
Ngoma bado mbichi katika lala salama za uchaguzi mkuu wa Kenya, japo mgombea wa Jubilee Mhe. Uhuru Kenyatta (shoto) anaongoza kwa kura 6,035,582 dhidi ya Mhe Raila  Odinga ambaye kapata kura 5,285,771 hadi kufikia wakati huu ambapo ni saa saba na robo za usiku kwa saa za Afrika Mashariki. 

Wagombea wote wawili wameshatimiza asilimia 25 zinazohitajika kutoka kwa angalau majimbo 24.  Uhuru Kenyatta anahitaji kura za asilimia 0.1 tu kujinyakulia ushindi, ingawa kura toka za majimbo yaliyosalia yanaweza kumpaisha Mhe Odinga pia. Matokeo rasmi ya mwisho yanategemewa kutangazwa saa tano asubuhi leo. 
Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia mambo.....

Tawi la Simba la Mpira Pesa la magomeni lafunguliwa

$
0
0
SIKU moja baada ya kung'atuka madarakani kwa viongozi wawili wa Simba, Zacharia Hans Poppe na Godfrey Nyange Kaburu, Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, imetangaza kulifungulia Tawi la Mpira Pesa la Magomeni.

Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Kaburu, Makamu Mwenyekiti walitangaza kujiachia ngazi katika klabu hiyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo timu kufanya vibaya katika mechi zake za kitaifa na kimataifa.

 Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alitangaza kulifungia Novemba 26, mwaka jana. Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho kilichofikia uamuzi huo, Joseph Itangare 'Kinesi' alisema kuwa sababu kubwa ni kuleta umoja ndani ya klabu.

"Hatuhitaji tena mpasuko katika Simba,ni wakati wa kushirikiana na kuleta hamasa kwa wachezaji, tunataka kuleta umoja kwa kuwa bado tuko katika mapambano ya kuinusuru timu," alisema Itangare.

Hata hivyo, Rage ambaye ndiye aliyekomalia kufungwa tawi hilo, hakupatikana kwa kuwa yuko nje ya nchi  kwa matibabu.

Kiongozi wa tawi hilo, Masoud Awadh alipotafutwa kuzungumzia hali hii alisema kikubwa wao wanataka mkutano mkuu ufanyike March 17 ili waweze kutoa madukuduku yao na kama tawi lao limefunguliwa inabidi pia wanachama wao watatu nao wafunguliwe.

"Sasa ivi timu imeyumba lazima waone umuhimu wetu,sisi hatuna kinyongo kwa sababu tunafanya kazi kwa maslahi ya timu na si wachezaji wachache,kwanza tunataka mzee kilomoni atambue kesi ipo mahakamani na yeye anatakiwa kuhudhuria Machi18 kama anavyotakiwa kwani kila anapoitwa anakaidi tunamtaka afanye ivyo mara moja,"alisema Kundi la mpira pesa lilimfungulia kesi Hamis Kilomoni baada ya kuwakashifu wanatumiwa na matajiri wa klabu katika kuihujumu timu na kwa sasa kesi hiyo ipo mahakamani na itasomwa tena Machi18.

Katika hatua nyingine Kinesi alisema kwa kuwa ligi bado inaendelea na Simba ina mechi ngumu mbele yao Kamati ya utendaji ya wekundu hao wa Msimbazi imeunda kamati ndogo ya ushindi ambayo itaongozwa na Rahma Al Kharoos maarufu kama 'Malkia wa Nyuki, lengo likiwa ni kuhakikisha Simba inashinda katika mechi zilizosalia.

Kwa upande wa Kocha msaidizi wa wekundu hao Jamhuri Kihwelo 'Julio' amewaonya wachezaji wake kuacha kujihusisha na mgogoro unaoendelea ndani ya klabu hiyo iliyopo mtaa wa Msimbazi na badala yake waelekeze nguvu na akili zao katika Ligi inayoendelea na kesho Simba itashuka dimbani kumenyana na Coast Union ya Tanga kwenye uwanja wa taifa.

Article 1

$
0
0


Tunapenda kuwatangazia wanachama na wakereketwa wote wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Uingereza kwamba Shina jipya la CCM katika jiji la Coventry UK linafunguliwa rasmi leo siku ya Jumamosi tarehe 09/03/2013 kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 12 jioni saa za Uingereza.


Uzinduzi huo utafanyika katika anuani ifuatayo;

 Cheylesmore Community Centre
Arundel/Poitiers Road,

Coventry, CV3 5JX


 

Kwa maelezo zaidi wasiliana;

 

Ahmed Mashaka  - 07876232851
Simba Fundikira -  07853311241


WOTE  MNAKARIBISHWA.

 

IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI
CCM - UK

WAZIRI MKUU WA DENMARK ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA AFRIKA MASHARIKI ARUSHA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Africa Mashariki Dk. Richard Sezibera (kulia) akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Mh  Helle Thorning-Schmidt alipotembelea makao makuu ya jumuiya Arusha,Tanzania.
Picha ya pamoja na Waziri mkuu wa Denmark, Waziri  Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu,Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  pamoja na maofisa wa juu wa jumuiya 

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
The winners walikuwa washindi kwa kila ngoma waliyotoa. Mfano ni hii 'Love Station'

Balozi Tuvako Manongi akisaini kitabu cha maombolezo ya Hugo Chavez

$
0
0
 Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, jana  Ijumaa aliungana na  Mabalozi wengine katika kutia saini kitabu cha Maombolezo  kufuatia kifo cha Rais wa Venezuela,  Hugo Chaves, aliyefariki siku  ya jumanne wiki hii kwa ugonjwa wa  kansa. Kitabu hicho  kilifunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa  Venezuela katika Umoja wa Mataifa. 

NEWS ALERT: UHURU KENYATTA AELEKEA KUSHINDA URAIS KENYA

$
0
0
Ankal akisalimiana na Mhe Uhuru Kenyatta Mei 22, 2006  wakati  alipotembelea Tanzania. Picha hii ya kutoka maktaba ya Globu ya Jamii haihusiani na uchaguzi mkuu Kenya.

Leo saa tano asubuhi  Tume ya Uchaguzi ya Kenya inatazamiwa na wengi kumtangaza Mhe Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho cha Urais wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Hii ni baada ya Uhuru Kenyatta kupata kura 6,173,433  (50.03%) dhidi ya mpinzani wake wa karibu Raila Odinga aliyepata kura 5,340,546 (43.28%) katika majumuisho yasiyo rasmi baada ya kura zote kuhesabiwa, ikiwa ni tofauti ya kura 4,100 tu. Jumla ya watu 12,338,667 walipiga kura.

Na tusubiri hiyo saa tano tuone....




Orodha ya Vyuo vikuu bora ya mwaka 2013; vya afrika havimo...

$
0
0

Kwa mara nyingine tena chuo kikuu cha Harvard kilichopo nchini Marekani, kimechukua nafasi ya kwanza katika orodha ya vyuo vikuu vyenye hadhi na ubora duniani. Orodha hiyo ambayo inatolewa na jarida la Times ya Uingereza ilitolewa hivi karibuni.

Katika idadi ya vyuo mia duniani Marekani imendeleea kuongoza ikiwa na takribani ya vyuo zaidi ya arobaini. Kwa bahati mbaya bara la Africa halina mwalikishi katika idadi hiyo.

1. Harvard - USA
2. Massachusetts Tech- USA
3. Cambridge -UK
4. Oxford -UK
5. U. of California, Brrkeley -USA
6. Stanford -USA
7. Princeton - USA
8. U of California, LA -USA
9. U of Tokyo - Japan
10. Yale University -USA

Tanzania Yashiriki vyema Maonyesho ya Utalii nchini Canada

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Canada,Mhe. Alex Massinda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) ambayo hufanya safari zake za Anga kutoka Toronto hadi Ethiopia (Wawili walio upande wa kulia) , anayefuata ni, anayefuata ni Bw. Rashid Adam wa Kampuni ya Zara Tours iliyoko Toronto na wa mwisho in Bw. Paul Makelele, Afisa Ubalozi wa Tanzania, Ottawa, Canada wakati wa maonyesho ya Utalii yaliyofanyika nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini Canada,Mhe. Alex Massinda akiwa na Afisa wa Ubalozi Bw. Paul Makelele.
kutoka kulia ni Bw. Peter Makutian kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, anayefuata ni Balozi wa Tanzania Canada Mhe. Alex Massinda, anayefuata ni Bw. Macon Dunnagan, mtaalam wa kupanda Mlima Kilimanjaro, ambaye amepanda Mlima mara 26 kwa mara ya mwisho mwezi Januari, 2013, anayefuata ni Bw. Rashid Adam wa Kampuni ya Zara Tours iliyoko Toronto, na wa mwisho ni Bw. Paul Makelele, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Kanada.

JIFUNZE MAPISHI KWA VIDEO ZA CHEF ISSA

$
0
0
NAJARIBU KUAANDAA MAFUNZO KWA NJIA YA VIDEO KAMA MAOMBI YA WATU WENGI KWANI NI NJIA RAHISI YA KILA MMOJA KUELEWA KWA URAHISI ZAIDI KWANI UNAONA MAFUNZO YANAVYOKWENDA HATUA KWA HATUA MAHITAJI YAKO...KARIBU SANA

RECIPE SAFI KABISA YA CHAKULA HIKI CHA VIAZI PAMOJA NA SAMAKI WA KUKAANGA
 1 pc ya pili pili hoho chop chop 
10 gram ya kitunguu swaumu 
400 gram fileti ya samaki 
1 pc kitunguu maji kikubwa kata kata slice 
500 gram viazi ulaya chemsha viive visipondeke 
150 gram cheese 
200 gram maziwa au fresh cream 
5 gram chumvi 1 pc limao kubwa 
30 gram mafuta ya kupikia
Video ya kwanza
Video ya pili
Video ya tatu 

CHAKULA HIKI NI RAHISI SANA KUANDAA NIMETUMIA DAKIA 13 TU PIA NAFUU KWA GAHARAMA LADHA SAFI WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE 
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images