Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 645 | 646 | (Page 647) | 648 | 649 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Johary Kachwamba-MAELEZO.

  TAKWIMU zinaonesha kwamba watoto 130000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kati ya hao 39317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo.


  Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la  VVU na UKIMWI kwa watoto linalofanyika  katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam. 

  Dkt . Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata maambukii ya  UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna  umuhimu kwa watoto hawa kupata huduma za tiba mapema.

  Akizungumzia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lengo likiwa  ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto wachanga. “Mama wajawazito na wale wanaonyoyesha wanapatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya VVU mara tu wanapogundulika kuwa na maambukizo, kupitia mpango mpya unaojulikana kama ‘uwezekano namba 2 au (Option B+)”, alisema Dkt.Chana.

  Alisema  kufikia mwezi Juni mwaka huu  jumla ya akina mama 940900 kati ya 1050043 hii ni sawa na asilimia 89.6% ya waliohudhuria kliniki walipimwa UKIMWI kati ya hao 47856 takribani asilimia 5 walikutwa na  maambukizi ya VVU.


  Kwa upande wa watoto 20569 walipima kipimo cha DBS kati ya hao  2063  hii ni sawa na asilimia 10 walikutwa na maambukizo ya VVU. Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mbando, alisema ingawa nchi imepiga hatua katika mapambano ya kudhibiti UKIMWI  hali halisi  inaonyesha  kuwa bado kuna maambukizo yanatokea sio tu kwa watu wazima bali na  kwa watoto pia.

  “Ni jukumu letu kuendelea kuweka mikakati ya dhati na kuisimamia ili kuhakikisha lengo la kutokomeza maambukizo ya VVU tunalifikia kwani mwaka 1986 maambukizi yalikuwa juu kwa asailimia 18 lakini hivi sasa yameshuka na kufikia asilimia 5.3”, alisema Dkt. Mbando.Kwa upande wake  Mkurugenzi wa ufundi kutoka Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF) ambao ni waandaaji wa kongamano hilo  Chrispin Kimario alisema ni muhimu kwa wazazi na jamii kushirikiana kwa pamoja na kulibeba jukumu la  kuhakikisha kila mama mjamzito anapata huduma ya vipimo husika na matibabu kwa wakati.

  Kimario alisema, “Watoto wameachwa nyuma, ni vyema tukumbuke kuwa mtoto hawawezi kujipeleka wenyewe hospitali kupima afya zao, hivyo ni jukumu letu wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma wanazostahili”.


  Kauli mbiu ya kongamano hilo la siku mbili ambalo limehudhuriwa na wadau wa afya kutoka asasi za umma na binafsi za ndani na nje ya nchi ni ongeza kasi: Rahisisha upatikanaji wa utumiaji wa huduma za VVU na Ukimwi, pata matokeo chanya ya afya za mama na watoto wanaoishi na VVU.

  0 0
 • 11/19/14--03:46: REMEMBRANCE

 • The Late Donat Samike Mashiku 1947-2013

  Baba, God saw you struggling and no cure in this world was there to make you stay, he then decided to call you that day of 20th November 2013. They were days, weeks, months and now a year without you. It is true that you are gone.

  Our hearts were hurt but we had no choice, we had to let you go. We miss your smile, your words, and many more that we cannot express .We continue praying for you papa, and on 20th Nov 2014,we will gather at your home Mapinga for remembrance of your great life teachings. 

  A holy mass will be held starting at 1500hrs onward followed by late lunch. Our friends and family please join us when commemorating the life of a beloved HUSBAND,DAD,BABU,UNCLE and a BROTHER.
  May your gorgeous soul continue to Rest In eternal Peace. Amen.

  0 0

   Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa tatu kushoto) sehemu ya msaada wa vifaa tiba vya hospitali vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania vyenye thamani ya shilingi Mil. 20 vitakavyotumiwa katika hospitali hiyo leo Novemba 19,2014,Zanzibar. Makabidhiani hayo yamefanyika kufuatia muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania ya TRA yenye Kauli mbiu isemayo Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" .Wa pili ni Kaimu Kamishna wa TRA (Zanzibar),Mcha Hassan Mcha akiwa pamoja na maofisa wengine wa TRA.Picha na Othman Michuzi.
  Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vya hospitali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib,leo Novemba 19,2014,Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa pili kushoto) akizungumza wakati akitoa shukrani zake kwa Uongozi mzima wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutoa msaada wa vifaa tiba kwenye Hospitali hiyo ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo Novemba 19,2014.
  Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa hospitali ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo Novemba 19,2014.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Taarifa ya Chama Wilaya Amani kutoka kwa Katibu Abdalla Mwinyi katika mkutano wa Mabalozi wa Mkoa wa Mjini Unguja akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mikoa ya Unguja.
  Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Mjini Mhe,Borafya Silima Juma akiwapa nasaha Mabalozi wa CCM Mkoa wa Mjini katika wilaya ya Amani wakati mkutano wa kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa ni mfululizo wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
  Mjumbe wa Mkutano wa Mabalozi wa Wilaya ya Amani CCM kutoka Mpendae Gabriel Mlekwa akitoa mchango wake katika mkutano maalum wa Mabalozi wa Wilaya hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mfululizo wa ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja.
  Balozi kutoka Shehia ya Kwawazee jimbo la Magomeni Juma Ameir Jecha akitoa mchango wake katika mkutano maalum wa Mabalozi wa Wilaya ya Amani ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja.
  Balozi kutoka Shehia ya Chumbuni Bibi Nunuu Khatib Hamad akitoa mchango wake katika mkutano maalum wa Mabalozi wa Wilaya ya Amani ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi wa Majimbo mbali mbali ya wilaya ya Amani Unguja akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani leo.Picha na Ikulu.

  0 0

  United States Ambassador Mark Childress giving remarks at the Fourth National Pediatric HIV conference. The conference focused on improving children’s access to HIV testing and treatment, and was held at the Julius Nyerere International Convention Center (JNICC) in Dar es Salaam. In his remarks, the Ambassador highlighted the critical need to close the gaps in treatment overall, and especially for children. The conference was attended by national, regional and district health managers, health care providers and communities involved in pediatric HIV care, policy makers and implementing partners. Listening is the Deputy Minister of Community Development, Gender and Children Dr. Pindi Hazara Chana (Far right seated). (Photo by courtesy of U.S. Embassy).

  0 0

  Habari wadau, kwa masikitiko makubwa nawajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya jeshi Lugalo alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.  Pia mwandishi mahiri wa zamani wa habari za michezo nchini Innocent Munyuku, naye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

  Hilo ni pigo kwa waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla, maana wote wameondoka wakati bado mchango wao ukihitajika sana. Taarifa zaidi tutaendelea kupeana kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

  Nawasilisha,
  Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA
  19/11/2014

  0 0

  Taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Forum CC imeandaa kongamano la siku moja kwa vijana kutoka  Asasi za kiraia lililojadili msimamo wa Tanzania juu ya masuala ya Mazingira, hususan Mabadiliko ya Tabianchi  kuelekea Mkutano Mkubwa wa Mazingira Duniani utakaofanyika katika jiji la Lima nchini Peru, Desemba 2014.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari  (hawapo pichani) mara baada ya kufungua kongamano hilo.
   Sehemu ya Washiriki walioshiriki katika kongamono hilo la siku moja lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Forum CC wakifuatilia mjadala kwa makini.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akijibu maswali ya washiriki katika kongamano la vijana jijini Dar es Salaam katika Hotel ya JB Belmont. Kongamano hilo la siku moja lililenga kukusanya maoni ya vijana na kuainisha changamoto katika suala zima la Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.


   Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. Wengine katika picha, (waliokaa) ni Bi. Grace Munna, Mkurugenzi wa Program kutoka Forum CC.

  0 0

  Moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha likishushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), leo limepokea mabehewa 50 ya kubebea makasha ambapo mradi huu unatekelezwa chini ya Mpango wa Matokeo makubwa sasa(BRN).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk . Shaaban Mwinjaka(mwenye tai ya blue), akiangalia behewa moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha yalishuhushuwa katika bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuniya reli Tanzania(TRL), Mhandisi Amani Kipalo Kisamfu. Kuwasili kwa mabehewa hayo kutasaidia kupunguza msongamano wa mizigo ya makasha na kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Aman Kipalo Kisamfu, kabla ya kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha katika bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kulia kwa Mhandisi Kipalo Kisamfu ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Alois Matei.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akisisitiza jambo wakati wa kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha, leo katika Bandari ya Dar es Salaam. Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba Menejiment ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuyatunza lakini pia na wananchi wanaokaa pembezoni mwa reli kusaidia Serikali kutunza miundombinu ya reli.(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi).

  0 0

  MKURUGENZI WA SERIKALI ZA MITAA BWANA KHALIST LUANDA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) JUU YA KUKAMILIKA KWA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MJINI DODOMA LEO AMBAPO ALITANGAZA RASMI TAREHE YA KUANDIKISHA KUPIGA KURA . (PICHA NA HABARI KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI).

  ======  ========  =====

  Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema  wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014. 

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kuchukua fomu za kugombea kuanzia tarehe 16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Bwana Luanda aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kushiriki katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaowataka.

  Alisema sifa za mtu anayestahili kujiandikisha kushiriki uchaguzi huo ni lazima awe raia wa Tanzania, mwenye umri wa miaka 18 au zaidi, mkazi wa eneo hilo na mwenye akili timamu.
  Pia alisisitiza kuwa uandikishaji huo utafanyika katika vituo maalum vilivyoandaliwa ambavyo vipo katika majengo ya umma, isipokuwa sehemu ambazo hazina majengo hayo, uandikishaji utafanyika katika vituo maalum kutokana na makubaliano ya Msaidizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa.Bwana Luanda amesisitiza kuwa vituo hivyo vitafunguliwa saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 10:30 jioni.

   Aidha alisema kuwa vyama vya Siasa vitaruhusiwa kuweka mawakala wao wakati wa uandikishaji wa wa wapiga kura lakini gharama  za kuwalipa zitakuwa juu ya chama husika. Kuhusu  sifa za mtu anayetaka kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mtaa Mkurugenzi huyo alisema kuwa ni lazima awe  mtanzania mwenye umri wa miaka 21 au zaidi na awe mkazi wa kudumu wa eneo husika.

  Vile vile alisema  kuwa wasimamizi wasaidizi wa kila kituo wanapaswa  kubandika orodha ya wapiga kura tarehe 30/11/2014, endapo mkazi yeyote au chama cha siasa kitakuwa na pingamizi au maoni juu ya orodha hiyo basi awasiliane na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ili kuweza kufanyia marekebisho na orodha ya mwisho itabandikwa siku tatu kabla ya uchaguzi.

  Uchaguzi wa serikali za Mitaa Tanzania Bara umepangwa kufanyika disemba 14, 2014, ambapo wananchi watawachagua wenyeviti wa vijiji, vitongoji, Mitaa, Wajumbe wa Halmashauri za vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.  Viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni pamoja na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji wasiopungua 15 na wasiozidi 25, wenyeviti wa Mitaa na wajumbe wa kamati za Mitaa wasioziidi 6 na wenyeviti wa vitongoji wa kila kitongoji.

  0 0
 • 11/19/14--07:18: Shinda na Vodacom Kabumbu


 • 0 0

  Lady Jaydee anatarajia ku release single mpya aliyomshirikisha Dabo inayoitwa "Forever' hapo Jumatatu tarehe 24 Novemba. Hii ni baada ya Kimya cha muda mrefu kidogo na siku ya Ijumaa ndio itakuwa official launch day pale M.O.G bar & Restaurant ambapo video ya wimbo huu ita premier for the first time. Wimbo umetayarishwa na producer mahiri Man Water wa Combination Sounds, na video ya wimbo huo imefanywa na muongozaji mkongwe Adam Juma wa Next Level. 


   Instragram: @jidejaydee @dabomtanzania 
  Twitter: @jidejaydee @dabomtanzania

  0 0

  Bismillah Rahman Rahim. 
  Umoja wa misikiti ya Ilala unawaomba/unawaalika kushiriki katika Dua maalum ya kumuombea Mh. Rais Alhaji Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kupona maradhi yake, siku ya Alhamis tarehe 20/11/2014 saa mbili usiku ( baada ya swalatul isha'a). 

  Dua itafanyika masjid TAQWA Ilala-Bungoni. Nyote mnakaribishwa. 
  Imetolewa na Sheikh Abdul Wakati- Mwenyekiti wa umoja wa misikiti ILALA.
  Rais Kikwete akiendelea na kazi ndogo ndogo,wakati akiwa kwenye matibabu,nchini Marekani. 


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Balozi wa kudumu wa Umojawa Mataifa(mstaafu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,New York,Marekani Mhe,Augustine Maiga alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa kudumu wa Umojawa Mataifa(mstaafu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,New York,Marekani Mhe,Augustine Maiga alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.)

  0 0

  Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Buguruni,Dk. Mwajuma Mbaga (kushoto) akipokea msaada wa mabechi ya kukalia wagonjwa wakati wakisubiri huduma kutoka kwa Kaimu Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL),Bw. Edwin Mashasi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano,iliyofanyika leo Novemba 19,2014.
  Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Buguruni,Dkt. Mwajuma Mbaga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa kituo hicho.Kulia waliokaa ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TTCL Bw. Edwin Mashasi.
  Sehemu ya mabenchi yaliyotolewa na kampuni ya simu Tanzania (TTCL). Msaada huo umegharimu shilingi milioni moja na laki saba.
  Wafanyakazi wa kituo cha afya Buguruni katika picha ya pamoja.

  0 0  0 0

   Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.
   Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijionea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60.
   Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

  PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

  0 0

   Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza hotuba , Kushoto ni mjumbe  toka Afrika kusini katikati ni Mkurugenzi wa ICT TPA Ndg. Phares Magesa, na kulia ni Mkurugenzi Mkuu TPA Eng.Madeni Kipande
    Ndg. Magesa akifuatilia mkutano huo
   Gavana wa County ya Kwale akitoa hotuba kwenye ufunguzi na kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mkutano huo
   Waziri wa Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Adan Mohamed akitoa hotuba rasmi ya ufunguzi wa mkutano huo.
  Baadhi ya wajumbe kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA , Mwenyekiti wa bodi TPA, Katibu Mkuu wa PMEASA , na Mkurugenzi Mkuu TPA wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko

  0 0

  Mhe. Dr. Mary Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji (wa pili kutoka kushoto) akijiandaa kuzindua ziara ya Wafanyabiashara kutoka Ubeligiji iliyoanza leo Dar es salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Ubeligiji Tanzania Mhe. Adam Koenraad. Waziri Nagu kazindua ziara hiyo ya siku saba katika Hoteli ya Serena.

  0 0
 • 11/20/14--01:30: Article 21
 • TURKISH ENVOY TO TANZANIA , H.E. ALİ DAVUTOĞLU SPEAKS ON TURKISH AFRICAN PARTNERSHIP IN REFERENCE TO AN ONGOING SUMMIT THE  SECOND TURKEY - AFRICA PARTNERSHIP SUMMIT ONGOING IN MALABO, EQUATORIAL GUINEA, ON 19-21 NOVEMBER 2014.
  Africa is now in an impressive surge of growth, urbanization and modernization. The natural and human resources are abundant and diverse. One can easily see Africa re-emerging with many promising developments. Africa has an average annual growth rate of 5 percent over the last decade and is expected to continue this trend in the coming years. 6 out of 10 fastest growing economies in the world are in now Africa.

  In terms of Turkish Foreign policy Relations with Africa constitutes one of the prime orientations of Turkish foreign policy, which is not based temporary political and economic considerations. On the contrary, it is the process of strong historical and cultural ties that we have with Africa.Following a multi-faceted policy in Africa, establishing close political relations and intensifying bilateral high level visits. Also economic field is another area that we help African nations overcome their challenges through more trade, investment, technical and humanitarian assistance.

  Turkey is doing its level best to contribute through diplomacy to the peaceful settlement of conflicts and disputes in Africa. Therefore, we do not consider ourselves as outsiders to the continent, rather a strategic partner. Turkey-Africa relations have gained a substantial momentum since the declaration of Turkey as a strategic partner of the Continent by the African Union in January 2008. Turkey-Africa relations have gained a substantial momentum since then. For example, in the year of 2009 there were only 12 Turkish Embassies in Africa. There is now 39. It is not one sided. We see, today, a growing number of African Embassies in Ankara. It reached 30 while it was merely around 10 five years ago.

  For Turkey it is not just about diplomatic representation and developing political relations. People-to-people contacts have intensified tremendously as a result of direct flights between Turkey and African countries as well as ever growing numbers of students, business people and tourists travelling both ways. Turkish Airlines has become major international airline connecting the continent to the world with a total number of flights to over 40 destinations in 28 African countries. 

  Direct flights of Turkish Airlines had an immense effect on bilateral trade volume reaching 23,4 billion USD in 2013 with all Africa. It is 7,5 billion USD with Sub-Saharan Africa. When we compare the figures in 2000 which was about 750 million USD and those of 2013, we see an increase of almost tenfold. When people get to know more about each other, they stand ready to deepen their relations. More than 200 thousand people travel mutually between Turkey and the African countries for business, tourism and cultural purposes. Turkey provides around 500 scholarships annually for students from Africa.

  Besides, Turkey has become a leading country in humanitarian activities all over the continent. Turkish International Cooperation and Coordination Agency (TİKA) has a central role in organizing and funding humanitarian projects that many people can benefit. TİKA currently operates 11 Program Coordination Offices in Africa and the number is expected to increase.

  After the first Summit in Istanbul in 2008, Second Turkey-Africa Partnership Summit will be held on 19-21 November 2014 in Malabo, Equatorial Guinea. We preferred to name it as Partnership Summit not just because we want to further develop our relations with Africa, but also we want to surpass what we achieved after the First Summit. That’s why the theme of the Summit is called “a new model of partnership to enhance a sustainable development and integration of Africa”.

  0 0older | 1 | .... | 645 | 646 | (Page 647) | 648 | 649 | .... | 3286 | newer