Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110102 articles
Browse latest View live

Breaking nyuzzz.......: Moto wazuka jengo la Machinga Complex leo

$
0
0
Moto waibuka jengo la Machinga Complex jijini Dar; wazimwa kabla haujaleta madhara makubwa.  
Moshi ukiwa umetanda angani


Smart choice Parenting

BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUARI MOSSI,JIJINI DAR

$
0
0
Bondia Thomasi Mashali (kushoto) akitia saini ya mkataba wa makubaliano ya kuzipiga na Bondia Abbdallah Pazi (kulia) mbele ya promota Kassim Texas (katikati) mpambano utakaofanyika januari mosi katika ukumbi wa friends corner,Manzese jijini Dar es salaam.
Bondia Thomasi Mashali (kushoto) akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano yao ya kuzipiga katika mpambano wao,utakaofanyika Januari Mosi 2015 katika ukumbi wa Friends Corner,Manzese jijini Dar es salaam.Picha na SUPER D BLOG

U.S. GOVERNMENT PROVIDES FUNDING TO DEVELOP SECOND MCC COMPACT FOCUSED ON THE POWER SECTOR

$
0
0
The United States Government, through the Millennium Challenge Corporation (MCC), agreed on November 14, 2014, to provide up to $9.78 million for the development of high-impact investment projects in Tanzania’s energy sector. United States Ambassador Mark B. Childress presided over the signing of the grant agreement at the Ministry of Finance in Dar es Salaam. The agreement was signed by MCC’s Vice President of Compact Operations, Kamran Khan, and Tanzania’s Minister of Finance, Saada Mkuya Salum.

The grant agreement builds on a strong partnership between the United States and Tanzania. Between 2008 and 2013, MCC implemented a compact of investment projects in water, roads, and electric power throughout Tanzania totaling $698 million. That compact program led to the construction of over 3,000 km of power lines, 450 km of trunk roads, two water treatment plants, and an airport runway.

Given its successful implementation of the first compact program – the largest in MCC’s history – MCC designated Tanzania eligible to develop a second compact program with a focus on the power sector, including investments in infrastructure as well as policy, regulatory and institutional reforms. Through the grant agreement signed today, Tanzania will mobilize consultants to undertake detailed feasibility studies and other preparatory work on project ideas that are most likely to stimulate long-term economic growth.

The studies will allow Tanzania to fully develop projects to reform the power sector; improve the technical, financial, and operational performance of the Tanzania Electricity Supply Company Ltd. (TANESCO) and the Zanzibar Electricity Corporation (ZECO); and expand access to electric power in rural areas. These proposed projects are expected to form the basis of a second MCC compact of investments between the United States and Tanzania.

This project development grant marks an important milestone in the development of the second compact program. The grant also marks a significant commitment toward the goals of Power Africa, the U.S. Government initiative to double the number of people with access to power in Africa through collaboration with African governments, the private sector, and other The Millennium Challenge Corporation (MCC) is a United States Government agency that provides assistance to developing countries. MCC is based on the principle that aid is most effective when it reinforces good governance, economic freedom and investments in people that promote economic growth and the elimination of poverty.
U.S. Ambassador Mark Childress (center) presiding over the signing of a grant agreement between the U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) and the Ministry of Finance in Dar es Salaam, while Vice President of MCC (Compact Operations), Mr. Kamran Khan (left) exchanges the grant agreement documents with the Minister of Finance, Ms. Saada Salum Mkuya. The grants total $9.78 million for the development of high-impact investment projects in Tanzania’s energy sector. (Photo by courtesy of U.S. Embassy).

MISS TANZANIA 2013 AAHIDI MAKUBWA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA

$
0
0
Na Benedict Liwenga, Maelezo

MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko nchini Uingereza.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.

Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu mzima.

“Nimejifunza mambo mengi hasa kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.

Naye Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.

Mashindano ya Urembo ya Dunia yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu safari ya Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2013 kuelekea katika Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2014) nchini Uingereza.
Mshindi wa Mashindano ya Urembo Tanzania kwa mwaka 2013, Happiness Watimanywa (kushoto) akieleza jambo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu safari yake ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Urembo wa Dunia yatakayoanza mapema tarehe 14 Desemba, 2014.

Kamati ya Uongozi ya Bunge yakutana mjini dodoma leo

$
0
0
Mweneykiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (kulia) akiendesha kikao cha Kamati ya Uongozi mara baada kuahirisha kikao cha Bunge. Hapa anatoa ufafanuzi kwa baadhi mambo yalijitokeza ambapo pamoja na mambo mengine amesema taarifa ya IPTL itakabidhiwa kwa Waziri Mkuu naye ataikabidhi kwa Spika wa Bunge.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. William Lukuvi (Mb) (kulia) akifafanua hoja kwenye kikao hicho kilichofanyikaa katika Ukumbi wa Spika wa Bunge.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (mbali-kulia) akitoa ushari wa kitaalam kuhusu mafanikio ya mkutano wa 16 na 17 unaoendelea Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wakimsikiliza Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila alipokuwa akitoa ushari wa kitaalam kuhusu uendeshaji wa shughuli za Bunge.
Mjumbe wa Kamati ya Uongozi na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa akifafanua jambo wakati wa kikao ambapo alilitaka Bunge liendelee kufanya kazi zake za kuishauri serikali kwa umaahisri kama inavyostahiki.
Wajumbe wa kamati ya Uongozi wakimsiliza Mhe. Lowassa. Picha na Prosper Minja - Bunge

Strabag yatangaza mabadiliko makutano ya Morogoro/Kawawa kuanzia Jumatatu

$
0
0
 Mkandarasi mkuu wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka (BRT), Strabag International ametangaza mabadiliko ya matumizi katika makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa.

Mabadiliko hayo yanaanza Jumatatu tarehe 17 hadi tarehe 30 mwezi huu. Akitangaza mabadiliko hayo leo jijini Dar es Salaam, Afisa uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Yahya Mkumba alisema mabadiliko hayo yanatokana na matengenezo yatakayokuwa yanafanyika eneo hilo.

Akielezea zaidi, alisema magari yatakayokuwa yanaelekea Ubungo kutokea Jangwani yatalazimika kutumia mchepuko uliopo kabla ya kituo cha Magomeni Mapipa kwa kuingia barabara ya mabasi yaendayo haraka.

Pia magari yatakayokuwa yanatokea Ilala Boma kuelekea Morocco, Ubungo na Jangwani yatalazimika kutumia barabara moja ya upande wa kushoto. “Wananchi watuvumilie katika kipindi hiki na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea,” alisema.

Mradi wa BRT unalenga kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam. Kilomita 20.9 za mradi huo awamu ya kwanza zipo mbioni kukamilika na kwa mujibu wa ratiba, zabuni za kupata watoa huduma zinatarajia kutangazwa mapema mwakani.

Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa duniani katika mfumo huo ambao unatarajiwa kuwa mfano katika eneo hili la Afrika ya Mashariki na kati.

Katika siku za hivi karibuni, viongozi na makundi ya watu mbalimbali yameeleza kuridhishwa kwao na maendeleo ya mradi huo na kutoa mapendekezo ya kuuboresha zaidi.

MH. PINDA AFUNGUA MKUTANO WA AFYA DAR JIJINI DAR LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Afya (Annual Health Summit) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 14, 2014.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya (Annual Health Summit ) wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba14, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipanue wigo wa utoaji huduma za msingi kwa kuishirikisha zaidi sekta binafsi nchini.

“Ninawasihi Waziri wa Afya na Naibu wake kwa vile ni wapya bado wabadili mtizamo wa wizara hii kwa kushirikisha zaidi wadau wa sekta binafsi kwenye utoaji wa huduma ili wasaidie kupunguza mzigo mkubwa ilionao Serikali,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 14, 2014) wakati akifungua Mkutano wa wa Kwanza wa Kitaifa wa Sekta ya Afya wa mwaka 2014 ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliyeko nje ya nchi kwa matibabu alisema: “Kuna tatizo la kukumbatia utoaji wa huduma ... tunazo hospitali kubwa za wilaya zinazomilikiwa na taasisi za dini. Hivi ni kwa nini kama Wizara msiwasaidie kuwahudumia watumishi wao au kuwapa ruzuku kwenye dawa ili kuwawezesha kutoa huduma kwa ufanisi zaidi?,” alihoji Waziri Mkuu na kushangiliwa na washiriki wa mkutano huo.

“Hata ukiangalia takwimu kwenye utoaji wa huduma za afya kupitia mifumo ya bima ya afya utabaini kuwa ni asilimia 18 tu wananchi wanatumia bima ya afya na kati ya hao, asilimia 15.3 ni mifuko ambayo imeanzishwa na Serikali. Ni kwa nini basi msiwasaidie wadau wa sekta binafsi ili wachangie huduma hii na idadi wa watumiaji wa mfumo huu iongezeke haraka?,” alihoji.

Akizumgumzia kuhusu uwiano kati ya daktari na mgonjwa, Waziri Mkuu alisema uwiano uliopo ni mbaya na kwamba hakuna njia ya haraka ya kupunguza tatizo hilo isipokuwa kwa kuishirikisha sekta binafsi kwenye ujenzi wa vyuo vikuu vya elimu ya tiba na sayansi za jamii.

“Uwiano wa sasa hapa nchini ni daktari mmoja kwa wagonjwa 75,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka daktari mmoja awahudumie wagonjwa 7,000. Kwa wauguzi, hapa nchini muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa 6,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka muuguzi mmoja ahudumie wagonjwa 500,” alisema.

“Kwa uwioano huu safari bado ni ndefu. Tunapaswa tuangalie tutafanyaje ili watu binafsi waje kuwekeza kwenye elimu ya juu ya sayansi na tiba, wajenge vyuo vya tiba, wajenge hospitali kubwa, na sisi pia kwa upande wa Serikali ni lazima tuseme tunawapa vivutio gani hawa wawekezaji hadi wakubali kuwekeza kwenye eneo hilo,” alisema.

“Tunataka mkutano huo uje na mapendekezo ambayo mnataka Serikali iyafanyie kazi na hatimaye isaidie kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi,” alisema Waziri Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kudhibiti ugonjwa wa ebola kwenye vituo vya mipakani na kwenye viwanja wa ndege.

“Mpaka sasa hatujapata kesi ya ugonjwa wa ebola hapa nchini... changamoto kubwa ni ukubwa wa mipaka yetu. Si wageni wote wanaoingia nchini wanapita kwenye vituo rasmi, wapo wanaotumia njia za vichochoroni. Rai yangu ni kuwaomba Watanzania wawe waangalifu kutambua ni wageni gani wanaingia kwenye maeneo wanayoishi,” alisema.

Mkutano huo wa siku mbili unamalizika kesho (Jumamosi, Novemba 15, 2014).


Waziri Mkuu amerejea mjini Dodoma kuendelea na kikao cha Bunge.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) afanya ziara kwenye vitengo vya Mawasiliano Serikalini

$
0
0
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi akimueleza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mikakati ya ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika vitengo cha mawasiliano.
Afisa Habari wa Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim Nyaki (kulia) akieleza kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mafanikio ya kitengo cha mawasiliano cha ofisi hiyo katika kutoa taarifa kwa umma ambapo alisema hadi sasa tovuti yao ina zaidi ya watu Elfu 8 wanaotembelea kwa siku.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia mwenye Kaunda Suti) akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma. Katikati ni Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila.
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kujionea utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano serikalini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo Bw. Gerard Mwanilwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia) akisisitiza kwa Maafisa Habari wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu utoaji wa taarifa kwa umma kwa wakati. Kushoto ni Afisa Habari wa Ofisi hiyo Bi. Evelyne Thomas. Picha na Fatma Salum-MAELEZO

Mh. Lukuvi atoa taarifa ya Hali ya Madawa ya Kulevya nchini kwa Mwaka 2013

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge),Mh. William Lukuvi akisoma taarifa ya Hali ya Madawa ya Kulevya nchini kwa Mwaka 2013,wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari (hawapo pichani) Mjini Dodoma leo.
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Kitabu cha Kurasa 56 chenye taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya kwa Mwaka 2013.
Baadhi ya picha za vielelezo ndani ya taarifa hiyo.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii,Kanda ya Kati.

TASWIRA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

$
0
0

Waziri Mkuu Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na sehemu ya viongozi wa jamii ya wafugaji kutoka katika baadhi ya mikoa hapa nchini waliotembelea bungeni leo.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Kanda ya Kati.
Katibu wa Bunge,Dkt. Thomas Kashilila (katikati) akiteta jambo na Mchungaji Luckson Mwanjale (kushoto) na Mh. Godfrey Zambi katika Viwanja vya Bunge,Mjini Dodoma leo.
Waziri wa Afrika Mashariki,Mh. Samuel Sitta (katikati) akisalimiana na Baadhi ya Wachungaji wa Mkoa wa Dodoma waliotembelea Bungeni hapo leo.
Waziri wa Afrika Mashariki,Mh. Samuel Sitta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wachungaji wa Mkoa wa Dodoma waliotembelea Bungeni hapo leo.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Kanda ya Kati.

Mkutano wa Mawaziri wa Mifugo wafunguliwa leo jijini Nairobi,Kenya

$
0
0
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Dr. Titus Mlengeya Kamani (katikati) akishiriki kwenye mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya Mifugo,Mkutano huo umefanyika Katika ukumbi wa mikutano wa AU-IBR Jijini Nairobi, Kenya. Lengo la mkutano ni kujadili Mkakati wa Maendeleo ya Mifugo Afrika kwa kipindi cha 2015-2035
Sehemu ya Mawaziri wenye dhamana ya Mifugo wakiwa kwenye Mkutano huo.
Picha ya pamoja ya Mawaziri wenye dhamana ya Mifugo.

UWEKEZAJI KATIKA RASILIMALI WATU: GOOGLE KWA ELIMU (EDU) KUIPATIA TANZANIA NJIA MBADALA KWA AJILI YA KUBORESHA ELIMU KUPITIA TEKNOLOJIA.

KINANA KUANZA ZIARA YA SIKU 16 MIKOA YA LINDI NA MTWARA, KESHO NOV 15

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana kesho November 15, 2014 anatarajia kuanza Ziara katika Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara). Ziara hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kuanza kesho katika wilaya ya Kilwa iliyopo Lindi na Kisha kuendelea katika wilaya zingine kwa takribani siku kumi na sita za kutembelea majimbo, kata, matawi na mashina ya Chama Cha Mapinduzi.

Ziara hii ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana ni muendelezo wa Ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambazo zimekuwa zikiendelea kote nchini tangu Sekretarieti hiyo ilipoteuliwa mwanzoni 2012.

Malengo ya ziara hii ni kukagua uimara wa Chama katika mikoa hiyo pamoja na kujenga na kuhimiza Uhai wa Chama katika kanda ya kusini ambayo kwa muda wote imeendelea kuwa ngome muhimu kwa Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Lakini pia ziara hii inalenga Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 - 2015 ambayo imeendelea kutekelezwa kwa mafanikio na Serikali katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Tunawaomba wananchi wa Mikoa ya Kusini kuwa tayari kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na kusema kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kufanyiwa kazi na kutekelezwa mara moja.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ataongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, ndugu Nape Nnauye.

UMOJA NI USHINDI.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

VYAMA VITANO VYA SIASA VISIVYO NA WABUNGE VYAOMBA SAKATA LA IPTL LIMALIZWE

$
0
0

 MAKATIBU wakuu wa vyama vitano vya kisiasa visivyo na wabunge bungeni wameomba suala la utata wa ufisadi zaidi ya sh.bilioni 300 zilizowekwa katika akaunti ya Tegeta Escrow zilizokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limalizwe ili kuendelea kwa mambo mengine ya kitaifa.

 Katika hatua nyingine makatibu hao wamepinga hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru) kukabidhi ripoti ya uchunguzi kwa Waziri Mkuu na kudai ipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DDP) mwenye uwezo wa kuchukua hatua za kisheria.

 Makatibu hao ni kutoka Chama cha Kijamii (CCK), Sauti ya Umma (SAU), Union For Multiparty Democracy (UMD), Alliance Farmaers Party na Demokrasia Makini (DM) ambavyo vimetoa tamko hilo Dar es Salaam leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo linaloendelea bungeni mjini Dodoma. 

 Tamko la makatibu hao limekuja siku moja tu baada ya kuwepo taarifa kuwa Waziri Mkuu, Pinda atakabidhi kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda ripoti ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow kufuatia madai ya uchotwaji wa Dola za Marekani milioni 200 (Sh. bilioni 320). 

 Makatibu wakuu wa vyama hivyo,Renatus Muabhi (CCK), ,Ali Kaniki (SAU), Rashid Rai (AFP),Dominick Lyamchai (Demokrasia Makini)na Kibaya Kiahira (UMD) walisema Takukuru kupeleka ripoti ya uchunguzi wa suala hilo bungeni siyo sahihi kwasababu ina utaratibu wake wa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria. 

 “Kiutaratibu Takukuru wakikamilisha uchunguzi wa jambo lolote inatakiwa kisheria kupeleka ripoti hiyo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP) na baada ya DPP kuipitia atatoa maoni yake ya kisheria kama kuna umuhimu wa kufungua mashtaka,”alisema Ali Kaniki Katibu Mkuu wa chama cha SAU. 

 Kaniki alisema ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ripoti yake ya uchunguzi kujadiliwa bungeni ni sahihi kwasababu utaratibu kama huo umekuwa ukitumika hata katika uchunguzi wa mambo mengine lakini siyo ripoti ya Takukuru. 

 Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha CCK,Renatus Muabhi, alisema inashangaza bunge kuendelea kung’ang’ania suala la IPTL wakati halina tija kwa Watanzaia katika kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na matatizo mengi. 

 “Bunge nalo linatoa hadithi tu,wabunge wanapiga kelele kuhusu sakata la IPTL na hatuoni mwisho wa jambo hili,hospitali hazina dawa,kuna suala la katiba ambalo ni muhimu limefunikwa,nchi inakwenda wapi,”alisema. 

 Muabhi alisema Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea anapaswa kuwajibika kutokana na uamuzi wake wa kupeleka ripoti ya uchunguzi wa sakata la IPTL kwa Waziri Mkuu. “Dk.Hosea anapaswa kuwajibika sababu ameshindwa kuzingatia sheria katika suala hili,kwanini apeleke hiyo ripoti kwa Waziri Mkuu wanakati anafahamu fika kuwa Waziri Mkuu hahusiki na masuala ya jinai,”alisema Muabhi. 

 Muabhi alisema danadana inayofanywa na serikali katika jambo hilo ni kutaka kuficha ukweli ili wawe waliotajwa katika ripoti ya CAG na Takukuru wasiweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akizungumza kwa niaba ya vyama vitano visivyo na wabunge Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko la vyama hivyo kuhusu kumalizwa kwa utata wa ufisadi zaidi ya sh.bilioni 300 zilizowekwa katika akaunti ya Tegeta Escrow  zilizokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kutoa fursa kuendelea kwa mambo mengine ya kitaifa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Dominick Lyamchai na Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Ali Kaniki.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Ali Kaniki (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance Farmaers Party,Rashid Rai (kulia), naye alipata fursa ya kuchangia jambo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

KAMPUNI YA MAFUTA YA ENGEN YAANDIMISHA MIAKA 21 TANGU KUANZISHWA KWAKE

$
0
0


Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania leo Novemba 14,2014 wameungana na wafanyakazi wenzao Barani Afrika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo.Engeni ni Kampuni iliyojikita katika uuzaji wa Mafuta bora ndani na nje ya Tanzania,huku ikiendelea kujivunia kwa Ubora wake.Pichani ni Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Engen hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo lao Kurasini jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania,Mubita Akapelwa (wa pili kulia) akikata keki wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo.

Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo akichua kipande cha Keki iliyokatwa vyema na Dada Jullieth Lwato (alieshika sahani) wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

CBE YATOA TUZO KWA WANAFUNZI BORA

$
0
0
Na. Aron Msigwa – MAELEZO

Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam kimetoa tuzo kwa wanafunzi bora 12 waliohitimu na kufanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka wa masomo 2014/2015 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa chuo hicho kuenzi na kuthamini mchango walioutoa katika maendeleo ya taaluma chuoni hapo.

Akikabidhi tuzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mwenyekiti wa sasa wa wanafunzi  waliomaliza chuo cha CBE, Bw. Harry Kitilya amesema kuwa wahitimu hao wanayo nafasi kubwa ya kutumia elimu waliyoipata na kuwa mfano katika kuleta mabadiliko nchini.

Amesema chuo hicho tangu kuanzishwa kwake  mwaka 1965 kimekua mfano wa kuigwa kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu  ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Biashara nchini kwa kuongeza  nafasi za ajira kwa kujiajiri wenyewe  kupitia shughuli za ujasiriamali,uanzishaji wa makapuni na miradi mbalimbali.

Bw.Kitilya amewataka wahitimu hao kujiendeleza zaidi kielimu ili waweze kukabiliana na ushindani wa ajira uliopo hususan katika soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya rushwa na uzembe pindi wanapoingia katika ajira.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu wa mwaka 2014 wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo ulioshuhudiwa na wanafunzi waliosoma miaka ya nyuma ni utaratibu wa chuo hicho kuenzi na kuthamini juhudi walizozionyesha katika taaluma.

 Amesema utoaji wa tuzo hizo umehusisha  fani za Uhasibu,Udhibiti wa Biashara, Usimamizi wa Masoko,Manunuzi na Ugavi na kuongeza kuwa utafanyika katika kampasi nyingine za chuo hicho zilizoko Zanzibar, Mbeya, Dodoma na Mwanza.

“Siku ya leo mbali na zoezi hili la utoaji wa tuzo, wahitimu wote wa sasa na wa zamani wanakutana kujadili namna ya uendelezaji wa chuo chetu, siku hii ni muhimu sana kwa kuwa inaongeza ushiriki wao katika kujadili masuala mbalimbali ya kukiendeleza chuo” Amesema Prof. Mjema.

Ameongeza kuwa lengo la kuwakutanisha wahitimua wa miaka iliyopita ni kujenga umoja imara na kupata mrejesho kutokana na huduma wanazozitoa kwa jamii, mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mwaka 2014 na wale miaka iliyopita wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo, wameiomba Serikali kendelea kupanua wigo wa Elimu ya Biashara kwa kuongeza matawi mengi zaidi kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi katika maeneo yao.

Wameiomba Serikali kupitia wizara ya Viwanda na Biashara kuwaendeleza na kuwawezesha wahitimu wanaoonyesha nia ya kujiajiri wenyewe na kuanzisha makampuni yao hapa nchini.

Aidha ,wametoa wito kwa walimu kutoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea duniani ili kuwawezesha kukidhi soko la ajira  huku wakitoa wito  kwa wahitimu wa vyuo kujenga utamaduni wa kujitolea ili waweze kupata uzoefu. 

Rais Kikwete atoka Hospitalini Baada ya kupata nafuu

$
0
0

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.(picha na Freddy Maro)

BINTI ALIYEPOTEA TANDIKA MWEZI OKTOBA APATIKANA AKIWA SALAMA SALIMINI

$
0
0
Mtoto Mwasiti Abdulrazack Kakurwa, miaka 14 (pichani), aliyetoweka nyumbani kwao Tandika, Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es salaam, mnamo tarehe 31/10/2014, katika mazingira ya kutatanisha, amepatikana jana.
Mwasiti ameletwa nyumbani kwa wazazi wake na bibi mmoja ombaomba anayesema kuwa binti huyo aliletwa maeneo ya kitumbini wanakolala ombaomba na Wanawake watatu Usiku na baadae wanawake hao wakatoweka katika mazingira ya ajabu!
 Baadae huyo bibi alimchukuwa Mwasiti na kukaa naye. Alipomuuliza huyo binti anatokea wapi, binti alisema hajui kwao ni wapi. Ila baadae huyo binti alipata ufahamu na kusema kwao ni tandika na kumuelekeza huyo bibi ni wapi wanapooishi wazazi wake. Asubuhi ya jana ndiyo bibi akamleta huyo binti nyumbani kwa wazazi wake.
Huyo bibi aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi  na kuhojiwa sana. Na baada ya kujiridhisha na maelezo ya huyo bibi polise wameishauri familia kumuachia huyo bibi na familia imekubali aachiwe!
 Binti alipelekwa hospitali na kufanyiwa checkup na kuonekana yuko salama. 
Tunamshukuru Mola kwa kumrudisha salama binti yetu. Tunawashukuru watu wote waliokuwa karibu nasi wakati wote wa kuhangaika kumtafuta binti yetu.
Mimi Mubashiry Kakurwa, 
kwa niaba ya familia ya binti aliyekuwa amepotea.

Ajali katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi Rodi Usiku huu

$
0
0
 Gari aina ya Toyota Rav4 yenye nambari za usajli T 141 AHS likiwa katika mtaro wa katikati ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi,Maeneo ya Namanga mara baada ya kugongana kwa ubavuni na Gari nyingine aina ya Toyota Vits yenye nambari za usajili T 551 CUP.Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wasi waliokuwa nao Madereva wa magari hayo,hali iliyopelekea hiyo Vits kuigonga kwa hiyo Rav4 na zote kutoteza mwelekeo na kwenda kuingia mitaroni.Madereva wa Magari yote walitoka salama salimi.
 Gari aina ya Toyota Vits yenye nambari za usajili T 551 CUP na lenyewe likiwa mtaroni upande wa ng'ambo ya barabara baada ya kuigokwa hiyo Rav4.
 Wazee wa Break Down wakiskilizis.
"Yaani imekuwa kama sinema vile"
 Askari wa Usalama Barabarani akizungu na watu waliokuwa wakiendesha magari hayo.

Viewing all 110102 articles
Browse latest View live




Latest Images