Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

WANANCHI WAOMBWA KUCHANGIA DAMU

$
0
0
MPANGO Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS) unatoa rai kwa wananchi wote wenye sifa za kuchangia damu wajitokeze kuchangia damu katika vituo vya Damu salama hasa kipindi cha mwezi Novemba mpaka Januari mwakani , kipindi ambacho wanafunzi wa sekondari wanakuwa likizo hivyo kusababisha kuongezeka kwa uhaba wa damu nchini.

Hayo yalisemwa leo na Afisa Habari wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania Bw. Rajab Mwenda (pichani) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ilala mchikichini, Dar es salaam, alisema damu salama kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha Msalaba Mwekundu umekusanya chupa za damu asilimia 97% na kuvuka lengokatika kipindi cha miezi mitatu julai hadi septemba 2014.

Jumla ya chupa 40,974 zilikusanywa , lengo lilikuwa kukusanya chupa 42,500. \“Katika kipindi hicho chupa za damu zilizokusanywa toka vituo vidogo( Blood collection satellite sites) ni 2,886 (8%) ambapo kituo cha Morogoro chupa 1,158, Dodoma-818, M/moja-490, kigoma- 93 na Lindi-327)” alisema.

Alisema katika robo mwaka ya Julai- Septemba 2014 asilimia 32 ya jumla ya chupa zilizokusanywa zilitengenezwa mazao ya damu; Packed Red blood cell, chembe sahani (platelets) na plasma. Lengo lilikuwa ni kutengeneza 40% ya damu iliyokusanywa.


news alert: mchekeshaji wa kimataifa toka nigeria basket mouth aja tanzania mwezi huu - watch this space!

SHEREHE ZA MIAKA 53 ZA UHURU WA TANZANIA -FINLAND

$
0
0
Jumuiya ya Urafiki wa Wafini na Watanzania inayofuraha kukualika kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 53 ya uhuru wa Tanzania. Mgeni rasmi anatazamiwa kuwa balozi wa Tanzania mh Dora Mmari Msechu anaye hudumia nchi za Baltic na Nordic.

Hii itakuwa ziara yake ya kwanza nchini Finland. Karibu kushiriki nasi kwenye mijadala,chakula cha kitanzania,buradani.

Wageni mnaotoka nje ya Finland unaweza wasiliana nasi kwa maelezo zaidi kuhusu malazi kabla ya November 30, 2014. 

Maelezo zaidi ingia kwenye ukarasa wao wa facebook kwa kubofya hapo chini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO KWA WASANII BORA

$
0
0
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii ya Mafanikkio katika maisha ya usanii (LIFE TIME ACHIEVEMENT AWARD) Bibi Martina Edward kwa niaba ya Said George Tingatinga kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii bora katika masuala ya kijamii (HUMANITARIAN AWARD) Bw. Patrick Kungalo kwa niaba ya Fr. Canute Mzuanda kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam. Makamu wa Rais alikutana na jopo la waandaaji wa siku ya Msanii, Kampuni ya Haak Neel Production, Baraza la Sanaa la Taifa na Wizara ya Habari, Vijana Michezo na Utamaduni na kutoa zawadi ya fedha shilingi milioni kumi ambazo aliahidi siku kilele cha siku ya Msanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Oktoba 25,2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha pamoja na washindi wa tunzo ya msanii bora baada ya kuwakabidhi tunzo hizo kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tunzo ya msanii bora na Viongozi wa Wizara ya Habari baada ya kukabidhi tunzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR)

WAWEKEZAJI WAVUTIWA NA KONGAMANO LA BRN

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) na Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima wakifuatilia kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kuhusisha wawekezaji mbalimbali kutoka nje ya nchi. Kongamano hilo lililolenga kuvutia uwekezaji katika miradi ya BRN lilifanya jijini Dar es Salaam Jumatano. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akifafanua kuhusu fursa mbalimbali za uwezekaji zilizopo katika shirika hili wakati wa kongamano la uwekezaji la BRN.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria kongamano la uwekezaji la BRN. Kongamano hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi (PDB) ambayo ndiyo inayosimamia mpango wa BRN lilivutia wawekezaji mbalimbali kutoka nje ya nchi. (Picha na Idara ya Mawasiliano PDB)
Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),David Shambwe akimueleza jambo  mmoja wa washiriki wa kongamano la wawekezaji la BRN juu ya miradi mbalimbali iliyopo sasa katika shirika la nyumba.
Afasa Masoko kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Mariam Ndabagenda akimuonesha mmoja wa washiriki wa kongamano la wawekezaji la BRN juu ya miradi mbalimbali iliyopo sasa katika shirika la nyumba.

Bwana Tariq na Bi. Vumi wameremeta huko jijini Mbeya

$
0
0
Bwana Tariq na Mkewe Bi. Vumi Yassin wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kumeremeta kwao hivi karibuni huko jijini Mbeya.
Bi. Harusi,Vumi Yassin akiwa na dada yake kipenzi Bi. Amina Yassin wakati wa sherehe ya ndoa iliyofanyika hivi karibuni,Jijini Mbeya.
Vijana wa Madrasa wakisoma kaswida na kupiga dufu wakati wa sherehe hiyo.

Semina ya wakuu wa Mikoa na Wilaya Bara na Visiwani yamalizika Zanzibar

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji katika Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa Bara na Visiwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kuhusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania bara ufungaji huo ilifanyika jana Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja.
Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji katika Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja jana.

WAZIRI MKUU AAGANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNIDO NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNIDO nchini aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwakilishi Mkazi wa UNIDO nchini aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NHIF yasaidia ujenzi wa wodi ya watoto ya hospitali teule ya Dr. Artiman,Sumbawanga

$
0
0
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Ramadhani Mhina (kushoto) akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya hundi ya sh. mil. 1 kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya ujenzi wa wodi ya watoto ya hospitali teule ya Dr. Artiman memorial hospital (Kristo mfalme) iliyopo Sumbawanga,Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Mb) akizungumza na baadhi ya watendaji wa mkoa wa wakati wa kikao cha kikazi cha kujadili maendeleo ya kisekta mkoani Rukwa.
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Ramadhani Mhina akitoa maelezo baada yakukabidhi hundi hiyo kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya ujenzi wa wodi ya watoto ya hospitali teule ya Dr. Artiman memorial hospital (Kristo mfalme) iliyopo Sumbawanga,Mkoani Rukwa.
Sehemu ya wauguzi wa hospitali hiyo pampja na Wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wakisikiliza maelezo kwa makini

Huduma ya Treni ya Jiji yaahirishwa kuanzia leo hadi Jumatatu Novemba 17, 2014

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL unasikitika kuwatangazia kuwa kuanzia leo jioni saa 10 hakutakuwepo huduma ya usafiri wa treni ya Jiji maarufu kama ' treni ya Mwakyembe' hadi siku Jumatatu Novermba 17, 2014 huduma itakaporejea kama kawaida.

Ufafanuzi wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya Jumapili.Novemba 16, 2014 baada ya kukamilika zoezi hilo la ukarabati.

Huduma zitarejea tena siku ya Jumatatu saa 12:30 asubuhi kuanzia kama kawaida kituo cha Ubungo Maziwa.

Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake!
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza!

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL
kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
Dar es Salaam,
Novemba 13, 2014

HAPA VIPI KAMA LIKIINGIZWA KWENYE VAZI LA TAIFA??

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU SIKU YA KISUKARI DUNIANI ITAADHIMISHWA KESHO NOVEMBA 14-2014.

$
0
0
Na Dotto Mwaibale wa Habari za Jamii Blog

SERIKALI imesema gharama za kutibu mgonjwa wa kisukari kwa mwaka hapa nchini ni sh.408,000 na kuwa watu wengi wamekuwa wakiugua ugonjwa huo bila ya wao kujitambua.

Imeelezwa kuwa utafiti uliofanya mwaka 2012 katika wilaya 50 nchini ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya watu huugua ugonjwa huo bila wenyewe kujua.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Afya Kebwe Stephen wakati akitoa tamko la serikali kuhusu siku ya ugonjwa huo ambayo itaadhimishwa duniani kote kesho alisema ugonjwa huo umekuwa na changamoto kubwa kwa vile hutokana na ulaji usiofaa.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa watoto wenye kisukari mwaka huu 2014 ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wote kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki nchini.

"Maadhimisho ya siku ya kisukari yataadhimishwa katika  hospitali zote za Rufaa, mikoa na ngazi  za wilaya kwa wananchi wote  kupima bure sanjari na kupata dawa,"alisema Kebwe.

Alisema watu wengine wanakuwa na dalili lakini huwa hawachukui hatua za mapema ili kuweza kuuzia ugonjwa huo kuendelea.

Alisema dalili za ugonjwa wa kisukari ni rahisi kuzitambua nazo ni kusikia njaa kila wakati,kukojoa mara kwa mara,kupungua uzito, na mwili kukosa nguvu. 


Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka 2014 ni "Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi" na kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya ulaji unaofaa ili kuepuka matatizo mbalimbali yanyotokana na ugonjwa wa kisukari katika jamii. 


 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Stephen (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana , wakati akitoa tamko la serikali kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa duniani kesho.
 Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk.Ayoub Magimba (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Stephen kuzungumza na wanahabari.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk. Sijenunu Aaron (kushoto) na Mratibu wa Kisukari wizarani hapo, Dk.Auson Rwehumbize wakiwa kwenye mkutano huo.
 "Hii picha ni lazima niipate" ni kama anaongea Halima Kambi mpiga picha wa Kampuni ya The Guardian Limited wakati Naibu Waziri Kebwe Stephen alipokuwa akitoa tamko hilo kwa wanahabari.

WAZIRI WA AFYA DKT SEIF RASHID AZINDUA KONGAMANO LA TISA LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI DODOMA LEO.

$
0
0
Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akizungumza katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto akifafanua jambo kwenye kongamano la tisa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Waandishi wa habari lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahya Nawanda akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mmpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya
Pichani ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima (RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee na pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid wakifuatilia na kusikiliza kwa makini baadhi ya maswali na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Kongamano hilo.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali walioko mezani mbele wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo la tisa la NHIF,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid ndiye aliyezindua kongamano hilo lililohudhuriwa na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.

MTAA KWA MTAA YA MICHUZI TV JIJINI MBEYA LEO

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda (UN-ICTR) Yaadhimisha Miaka 20

$
0
0
Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda mwaka 1994 juzi iliadhimisha miaka 20 tokea ianzishwe. Maadhimisho hayo yalihusisha maonyesho ya kazi zake pamoja na mikutano. Siku ya mwisho Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal alikuwa mgeni wa heshima. Mhakama hiyo inamaliza kazi zake mwakani. Chini hapo ni baadhi ya picha za shughuli hiyo.
 Mpiganaji Danford Mpumilwa, ambaye ni Afisa Habari wa Mahakama hiyo akisoma hotuba ya Wafanyakazi wa Mahakama hiyo. 
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Bwana Miguel de Serpa Soares akiangalia maonyesho hayo.
 Mgeni wa heshima Dr. Bilal akiangalia maonyesho kuhusu kazi za mahakama hiyo. 

makamu mwenyekiti wa UVCCM Mboni Mhita atembelea ubalozi wetu marekani

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.Liberata Mulamula akiwa katika picha pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Umaaja wa Vijana wa CCM  Mhe.Mboni Mhita (kulia)  na Bi. Loveness Mamuya  kabla (juu) na baada (chini) ya Mhe.Mulamula kufanya mazungumzo na Mhe.Mboni ubalozini Washington DC

ngoma azipendazo ankal

BURUDANI FC YAINGIA NUSU FAINALI, YAIONDOSHA KILUVYA UTD KWA PENATI KWENYE DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP

$
0
0
4Michuano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP hatua ya robo fainali imeendelea  kwenye uwanja wa bandari maeneo ya Tandika Mwembeyanga kwa kuzikutanisha timu za Burudani Fc ya Temeke mikoroshini dhidi ya Kiluvya Utd kutoka mkoani Pwani
Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana baada ya dakika 90 ikabidi changamoto ya mikwaju ya penati itumike kumpata mshindi na timu ya Burudani ikafanikiwa kupata mikwaju minne dhidi ya miwili ya kiluvya,golikipa Abraham Abdallah wa Burudani alipangua penati moja ya kiluvya. 10KIKOSI CHA BURUDANI FC 11KIKOSI CHA KILUVYA UTD......... Capture SEHEMU YA MASHABIKI WAKITAZAMA MPAMBANO MKALI KATI YA BURUDANI NA KILUVYA UNITED. 

NHIF YAJENGA KITUO KIKUBWA CHA KISASA CHA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA BINADAMU MKOANI DODOMA

$
0
0

1
Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi na Matibabu ya magonjwa ya binadamu kinachojengwa katika Chuo Kikuuu cha Dodoma (UDOM)  kikiwa katika hatua za mwisho mwisho za kukamilika.

Kituo hiki kitahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya jirani ya na mkoa wa Dodoma na kinajengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 ambazo zimetolewa na mfuko huo kwa  silimia 100.

 Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli ya Dodoma mjini humo walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mlacha Shaaban amesema “Kituo hiki kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi na utafiti  pia kitatoa wataalamu kutoka katika kitivo cha afya cha Chuo kikuu cha UDOM na wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa wakifundisha wanafunzi na kuhudumia wagonjwa. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Januari 2015"
2
Jengo la kituo cha Utafiti na tiba cha UDOM kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
3
Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha UDOM Profesa Mlacha Shaaban akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali walipotembelea ujenzi wa kituo cha Tiba na Utafiti kinachojengwa katika chuo kikuu cha UDOM.
4
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamotoakizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo hicho
5
Waandishi wa habari wakisubiri kupata  maelezo ya kituo hicho.

KONGAMANO LA TISA LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI LAENDELEA LEO MKOANI DODOMA.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya,lakini pia alieleza kuwa Wilaya yake ya Igunga ina vijiji 98,vijiji 78 vimejengwa zahati,lakini mpaka sasa zahanati 31 hazijasajiliwa,hivyo ameiomba Serikali kupitia wizara ya Afya kuhalakisha suala la usajili wa zahanati hizo katika kuwasaidia wananchi.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akifafanua jambo katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel,ikiwa ni siku ya pili ya hitimisho la Kongamano hilo,Kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza akifafanua jambo  katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.   
  Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
 Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda pamoja na  Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani kwa pamoja wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
 Pichani shoto ni Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza na Mdau wakifuatilia mada mbalimbali ndani ya kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.   
 Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu pamoja na Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda  wakijadiliana jambo.
Washiriki katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel ikiwa ni siku ya pili ya kilele chake huku likiwa limebeba kauli mbiu ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images