Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

WIKI YA UJASIRIAMALI TANZANIA KUANZA NOVEMBA 17

$
0
0
Mratibu wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania, Lilian Secelela Madeje (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya wiki hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 17 mwaka huu jijini humo. Kutoka kushoto ni mmoja wa wajasiriamali, Mboni Masimba wa kipindi cha Mboni Show na Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa.
Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa (kushoto) akizungumza kuhusu kushiriki kwa DSE katika maadhimisho ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania yanayotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake, ni Mratibu wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania, Lilian Secelela Madeje ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Professional Approach Development na Meneja Mradi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Rukia Lukanza.
Mmoja wa waanzilishi wa asasi ya KINU, Emanuel Feruzi (kulia) akizungumza kuhusu ushiriki wao katika maadhimisho ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania. Kulia kwake ni Rukia Lukanza wa ILO na mratibu wa wiki hiyo, Lilian Secelela Madeje.
Mmoja wa wajasiriamali, Mboni Masimba (kushoto), wa kipindi cha Mboni Show anayetarajiwa kuwa mmoja wa watoa mada katika semina na mikutano wakati wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania akizumguza katika hafla hiyo. Kushoto kwake ni Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa na mratibu wa wiki hiyo, Lilian Secelela Madeje.
Baadhi ya waratibu, wadhamini na waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya utambulisho wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Basi lapiga mweleka huko Kahama leo,watu watano wadaiwa kupoteza maisha

$
0
0
Basi la Wibonela linalofanya safari zake kati ya Kahama - Dar limepinduka na kupelekea zaidi ya watano kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhi vibaya,ajali hiyo imetokea mapema leo katika eneo la Fantom nje kidogo ya mji wa Kahama. Chanzo kinaelezwa ni mwendo kasi uliopelekea kumshinda dereva wa basi hilo wakati akikata kona ya kuingia barabara kuu hali iliyopelekea basi kupinduka.  Taarifa kamili tunaendelea kuifatilia na tutaendelea kujuzana hapa hapa.
Sehemu ya Mashuhuda wa ajali hiyo wakiendele kuchukua taswira mbali mbali wakati jitihada za kulinyanyua gari hilo zikiendelea.

Vacancy announcement

TANGAZO: NAFASI ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WAMA-NAKAYAMA 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAZISHI YA RAIS SATA WA ZAMBIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata Ikulu mjini Lusaka Zambia jana Novemba 11,2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa Rais Michael Sata iliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye Uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika jana Novemba 11,2014. (Picha na OMR)

MWILI WA MAREHEMU ROBERT LENGEJU WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUZIKWA KESHO KIPERA MOROGORO.

$
0
0
Hili ndilo sanduku lililouhifadhi mwili wa Mwandishi/Mchambuzi wa Jukwaa Maalumu la MWALE WA DEMOKRASIA katika Gazeti la Raia Tanzania (Gazeti dada la Raia Mwema), kila Alhamisi. Mwili wa shujaa huyo wa Demokrasia uliswaliwa katika Kanisa Katoliki M<simbazi Jijini Dar es Salaam leo. 

Watu mbalimbali walihudhuria katika misa hiyo ya kumsindikiza Lengeju katika safari yake ya mwisho kabla ya maziko yatakayo fanyika kesho (Novemba 13,2014) Kijijini kwako Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog.
wanakwaya wakiimba katika misa hiyo.
wanafamilia wakiwa Kanisani katika misa.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika misa hiyo leo.
 Kaka wa Marehemu Charles Lengeju akiwa amebeba msalaba wa marehemu.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Mtumie ujumbe wa kumjulia hali na kumpa pole Rais Kikwete kwa kupitia namba yake hii

$
0
0
Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa namba yake maalumu kwa ajili ya Wananchi kumjulia hali na kumpa pole,ambapo atapokea ujumbe wako na kuujibu.

Mh. Mwanjale arejea Bungeni leo

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Mchungaji Luckson Mwanjale (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi,Mh. David Silinde na Mh. Athuman Mfutakamba wakati akiwasili Bungeni mjini Dodoma leo.Mchungaji Mwanjale alipatwa na ugonjwa wa ghafla uliompelekea kukosa nguvu na kuanguka juzi Novemba 10,2014 wakati vikao vya Bunge vikiendelea,hali iliyopelekea kukimbizwa hospital kwa matibabu zaidi.sasa yuko vizuri na amerejea Bungeni.
 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Mchungaji Luckson Mwanjale (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi,Mh. David Silinde nje ya viwanja vya Bunge,mjini Dodoma leo. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi,Mh. Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari wanaoripoti habari za Bunge, nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Kanda ya Kati.

KUTOKA MAKTABA: TASWIRA YA KIHISTORIA YA GLOBU YA JAMII...

$
0
0
Kutoka kushoto ni: Lwitiko Mwakilasa, Bernard Kakengi, Mapinduzi Mwankemwa, Mzee Kimaro wa JWTZ, Victor Gunze wa TBC, Raymond Mutafungwa. Rupia Lyabandi, Dennis Londo, Ankal Muhidin Issa Michuzi, Fidelis Tungaraza "Mti Mkubwa", Ndesanjo Macha, Magonera Malima na Kisakisa Kiwala.

Taswira hii ni ya Septemba 10, 2005 katika kiota cha maraha kinachopendwa sana na Wabongo cha Chelsea hapo jijini Helsinki Finland. Tukio ni mkusanyiko wa wadau kusherehekea kuanzishwa rasmi kwa Globu ya Jamii takriban miaka 10 iliyopita. Hii ilikuwa ni pembeni mwa mkutano wa Helsinki (Helsinki Conferenceambao Rais Benjamin Mkapa (wakati huo) alihutubia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania (wakati huo) Mhe Jakaya Mrisho Kikwete na mwenzake wa Finland, Mhe Errik Tuomioja, walikuwepo, pampja na Dkt Asha-Rose Migiro (wakati huo akiwa Waziri  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) 
Ni kweli kwamba Ndesanjo Macha (aliyesimama kulia na gwanda la bluu) ndiye aliyefanikisha kuanzishwa kwa Libeneke hili pale jirani na hapo Chelsea, katika ukumbi wa Finlandia, si uwongo kwamba Fide Tugaraza (kifuani pa Ankal, na kulia kwa Ndesanjo, ndiye aliyesababisha yote haya kutokea kwa msimamo wake wa kumcharura Ankal na wanahabari wa Bongo, kwamba kwa nini hawaleti vitu vya nyumbani mtandaoni? 
Yaani kama si yeye (Fide) Globu ya Jamii isingekuwa hai hii leo. Na Kama si Ndesanjo kumpa lekcha Ankal ya nanmna ya kuanzisha blogu, tungekuwa tunaongea nini sijui saa hizi.
Kwa heshima na taadhima Globu ya Jamii inapenda kutoa saluti kwa mkusanyiko huu wa kihistoria ambao mbali na kuwa wadau wa mwanzo wa Libeneke hili, pia wadau hawa ndio waliosimama kidete kuhakikisha hakuna kinachoharibika. ASANTENI SANA SANA FIDE NA NDESANJO pamoja na wadau wote katika taswira hii ya kihistoria. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kusema AHSANTENI AHSANTENI SANA SANA. 

Chadema yaendelea na Mikutano yake Mkoani Kigoma

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (anaeonekana jukwaani) akiwahutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kwenye Uwanja wa Community Cetre mjini Kigoma jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa mji wa Kigoma katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kwenye Uwanja wa Community Cetre mjini Kigoma jana.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 13.11.2014

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA SEKTA HIYO NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)Charles M. Chacha (Kushoto), akiteta jambo na mmiliki wa kampuni ya Tran World ya nchini Dubai Mr. Adil Jadid kulia) wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania. Mkutano huo unatoa fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini . Mkutano ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mjumbe wa Bodi wa TCAA Yussuf Mohammed Ally.
Baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wa sekta hiyo uliotoa fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka yaUsafiri wa Anga(TCAA), Bw. Charles M. Chacha(aliyeshika maiki), akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania. Mkutano huo unatoa fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini Ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania akiuliza swali wakati wa Mkutano huo unatoa fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini Ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti masuala ya Ki- Uchumi, Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Dkt. James Diu (wapilia kutoka kulia) akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa anga Tanzania. Mkutano huo unatoa fursa za kujadili maendeleo ya sekta hiyo nchini, ulifanyika makao makuu ya Mamlaka ya usafiri wa Anga jijini Dar es Salaam .Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti masuala ya ki-usalama TCAA, Bw. Jude Mkai.

Ecobank, first bank to support Malaria prevention in Tanzania

$
0
0
Ecobank the pan-African bank celebrated its 27th year of operating in Africa through the annual celebrations, Ecobank Day held on the 8th November 2014. The celebrations, commemorated through Corporate Social Responsibility initiatives, this year focused on the theme Malaria, Dengue and Ebola: Prevention is Better than Cure. Ecobank Tanzania commemorated this anniversary in the Bonde la Mpunga area of Masasani ward, Dar es Salaam at an event graced by the Msasani ward Councilor Hon. Christina Kirigiti and the Chairperson of the Bonde la Mpunga local Government Hon. Philbert Mbepera.

During the event, Ecobank made a donation of free treated mosquito nets and conducted fumigation in the area valued at Tsh. 5,500,000. “We are very happy that Ecobank being the first bank to support malaria prevention initiatives has responded to the dire situation experienced at Bonde la Mpunga, which is an area that experiences water stagnation all year round and is a notorious breeding ground for Malaria. “ Says Hon. Christina Kirigiti. “This area alone has over 17,550 residents who grapple with malaria every day, Ecobank’s intervention is not only timely but very conscious of the urgent need to prevent Malaria infection that greatly affects the livelihoods of households and the overall economic activity and performance of this area.”  Adds Hon. Mbepera.

Ecobank members of staff conducted the fumigation exercise jointly with Malaria corps provided by the Kinondoni District and the residents. This joint fumigation effort aimed to not only kill the mosquitoes and destroy breeding grounds, but to also equip the residents with the know how on controlling and preventing the spread of Malaria in the area.

“Our commitment to the community is solid and we have demonstrated this commitment to developing the overall social and economic wellbeing of Tanzania through various local initiatives.” Says Enoch Osei- Safo Managing Director, Ecobank Tanzania. “ This year, we focused on malaria prevention as it has adversely affected sub-Saharan Africa accounting for 90% of all global malaria cases and causing deaths that are otherwise avoidable. Malaria has affected millions of Tanzanians and Africans as a whole and adversely impacts economic progress and individual livelihoods. We believe that prevention is better than cure, hence our efforts at empowering this community with the requisite tools in promoting malaria and dengue fever prevention as well as creating awareness on prevention of the Ebola virus epidemic that has destroyed the economies of Liberia, Guinea and Sierra Leone in West Africa.” He resounds.

The recently stalled treated mosquito net programme has received support as over 250 residents in the Msasani area will receive free mosquito nets. According to Mr. Abdulla Hemedi the Kinondoni District Malaria Coordinator, “Our clinics had stopped issuing the free mosquito net tokens, but now we shall see another 250 households benefit from the mosquito nets donated by Ecobank. We have decided to distribute these through the Oyster Bay Clinic, a public clinic located near the Oyster Bay police station. Priority will be given to mothers with newborn babies as they are the most vulnerable in contracting malaria.”

Mr. Osei Safo resounds: “ As a pan African bank this initiative is being commemorated today in over 36 African countries in a strong demonstration of a commitment to building Africa, we as Ecobank Tanzania commit to champion initiatives that empower Tanzanians and also demonstrate consciousness to the socio-economic needs of our people.” 

NHIF yakabidhi mashuka hospitali ya wilaya

$
0
0
Na Editha Karlo,wa bog ya jamii Kigoma
MFUKO wa Taifa wa bima ya afya umetoa jumla ya mashuka 100 kwa hospitali ya wilaya ya Kibondo mkoani kigoma ili kukabiliana na upungufu wa mashuka unaoikabili hospitali hiyo.

Akikabidhi mashuka hayo kwa uongozi wa hospitali ya wilaya ya Kibondo, meneja wa NHIF mkoa kigoma,Elius Odhiambo alisema kuwa kutolewa kwa mashuka hayo ni sehemu ya mpango wa mfuko huo katika kuboresha utoaji huduma katika sekta ya afya.

Odhiambo alisema kuwa mashuka hayo yaliyotolewa kwa hospitali ya wilaya ya Kibondo ni sehemu ya vifaa ambavyo vimekuwa vikitolewa kwa vituo mbalimbali vya utoaji wa huduma ya afya ambavyo vinanufaika na huduma za mfuko wa taifa wa bima ya afya.

Akipokea mashuka hayo kwa niaba ya hospitali ya wilaya ya Kibondo Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo,Emanuel Mwasulama alisema kuwa kupokewa kwa mashuka hayo kutapunguza upungufu mkubwa wa mashuka unaoikabili hospitali hiyo.

Alisema kuwa kwa sasa hali ya upatikanaji wa mashuka hospitalini hapo haiendani na mahitaji na kuomba kwamba kutolewa kwa mashuka hayo na mfuko wa Taifa wa bima ya afya iwe chache kwa wadau wengine kujitolea katika kuisadia hospitali hiyo.

Sambamba na kutolewa kwa mashuka hayo Mganga huyo wa wilaya ya kibondo alisema kuwa kumekuwa na maboresho makubwa katika utoaji wa huduma ya afya kupitia mfuko wa taifa wa bima ya afya na watu wengine wamekuwa wakieleza kuridhishwa kwao na huduma zinazotolewa hospitalini hapo  kupitia mfuko huo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanaopata huduma kupitia mfuko wa Taifa wa bima ya afya wamelalamikia kukosekana kwa dawa katika hospitali ya wilaya na hivyo kulazimika kufuata katika maduka ya dawa au kununua kwa pesa zao.

Akizungumzia jambo Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya kibondo, Laurean Kanaganwa amesema kuwa madawa ya shilingi milioni 44.2 yamenunuliwa na yameanza kusambazwa katika vituo vya afya na zahanati wilayani humo.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa Kigoma Elius Odhiambo (kushoto) akizungumza katika kampeni ya uhamasishaji jamii kujiunga na huduma za mfuko wa afya ya jamii (CHF) kampeni inayofanyika kwa muda wa siku 10 kwenye vijiji mbalimbali vya wilaya ya kibondo.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa Kigoma Elius Odhiambo (kulia) akikabidhi kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Kibondo Emanuel Mwasulama (kati kati) moja kati ya mashuka 100 ambayo mfuko huo imetoa kwa hospitali hiyo ya wilaya (kushoto0 ni Meneja wa Taifa wa mifuko ya jamii kutoka NHIF Constantine Makala (picha na Editha Karlo)

INTRODUCING DOTTO GIDI - Mapenzi Ya Twitter


Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake waanza ziara ya siku 10 nchini China

$
0
0
Mkuu wa Kijiji cha Maeneo huru ya uwekezaji katika Mji wa Chengmai aliyevaa shati jeupe Bwana Yang Si Tao akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kushoto yake wakati ujumbe wa Zanzibar ulipoangalia maeneo hayo ukiwa katika ziara ya siku 10 Jimboni Hainan. Kushoto ya Balozi ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji,Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana Abdullrahman Shimbo na Mkewe Mama Mary Antoni Tairo. Nyuma ya Bwana Yang Si Tao ni Waziri wa Habari Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk, Katibu Mkuu Fedha Nd. Khamis Mussa,Mye wa Manispaa ya Zanzibar Msitahiki Khatib Abdulrahman, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala wa Mikoa na Idara Maalum Nd. Joseph Abdulla Meza, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalis Salum Mohamed, Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Mhudumu wa Balozi Seif Hassan Ali pamoja na Mkurugenzi Manispaa Nd. Abeid Juma Ali.
Balozi Seif na ujumbe wake wakifuatana na mwenyeji wao Mkuu wa Kijiji cha Uwekezaji wa Mji wa Chengmai Bwana Yang Si Tao wakielekea ukumbi wa mkutano kwa mazungumzo. Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd. Salum Nassor Khamis, Mkurugenzi Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo haji.
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ule mwenjeji wa Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo Bwana Jian Dingzhi ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano hapo katika Hoteli ya Le Meriden Mjini Haikou.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi wa Kasha lililojaa vyakula vya viungo { spices } Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian Dingzhi mara baada ya kumaliza mkutano wao rasmi wa ushirikiano.
Gavana wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan Bwana Jian Dingzhi akibadilishana mawazo na Mgeni wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

haya tena,yale yaleeee.....

Tanzia

$
0
0
Marehemu Eng. John Said Kimbe


Jumuiya ya Watanzania Mozambique (JUWAMO) inasikitika kutangaza kifo cha Ndugu yao Mpendwa Eng. John Said Kimbe, kilichotokea ghafla usiku wa tarehe 10 Novemba, 2014 nyumbani kwake Maputo, Mozambique.

 Wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa Mwenyekiti wa JUWAMO, Tawi la CCM Maputo, Mozambique na Mfanyakazi; Mtaalamu wa Miundombinu ya Mawasiliano “Telecommunication/ICTs expert” kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), kitengo cha “Southern Africa Telecommunications Association (SATA) tangu Juni 2001.  


Jumuiya ya Watanzania Mozambique inawafahamisha Watanzania wote waishio Jiji la Maputo na vitongoji vyake kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa “Memorial Service” tarehe 13 Novemba, 2014 katika Kanisa la Roman Catholic “Paroquia Nossa Senhora das Victoria” Karibu na Soko la Janet – Maputo, saa 9. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Tanzania kwa mazishi tarehe 14 Novemba, 2014.


JUWAMO inawaomba Watanzania wote kujitokeza kumuaga mpendwa wetu na kuwafariji wafiwa kama mila na desturi zetu zinavyotuelekeza.


Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Katibu wa JUWAMO Ndugu Annuar Aziz Simu No. +258824034391 au +258842337117 na Katibu wa CCM –Tawi la Maputo, Mozambique Ndugu Gesona Ngabo Simu No. +258821403433.

Imetolewa na JUWAMO


12/11/2014

NHIF YAJENGA KITUO KIKUBWA CHA KISASA CHA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA BINADAMU UDOM MKOANI DODOMA.

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na ujenzi wa mradi mkubwa wa kituo cha  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umegharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zimetolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.

Kwa mujibu wa Profesa Shaban Mlacha,amesema kuwa kituo hicho kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi /Utafiti na Tiba, yakiwemo ya figo,akaongeza kusema kuwa kina maabara ya kisasa na vifaa vya kisasa huku kukiwa na vyumba 40 vya madaktari.


Profesa Mlacha amesema kuwa ,kuwapo kwa kituo hicho kitakachojengwa na kukamilika, kitachangia si tu katika kufanya utafiti wa magonjwa na kutibia lakini pia itatoa nafasi kwa wanafunzi wa kitivo cha tiba UDOM na walimu wao kufanya mazoezi yanayostahili na kuonesha ubingwa wao.  

Baadhi ya Wahariri wa Habari kutoka nyombo mbalimbali hapa nchini,wakitoka nje ya Jengo la kituo cha  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),kama kionekanavyo pichani.Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Chuo  hicho  cha  Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha amesema kuwa Ujenzi wa kituo hicho uko katika hatua za mwisho kukamilika na kuwa kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mnamo januari 2015  mwakani .Mradi huo umegharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36 zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa kituo hicho cha kisasa kilichopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa kituo hicho cha kisasa kilichopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

ajali kazini

$
0
0
Ankal akiwa katapakaa vumbi mwili mzima baada ya kula mwereka na kamera yake katika harakati za kazi kwenye soko la nafaka la Kibaigwa mkoani Dodoma hivi karibuni. Ankal anakwambia kwamba katika maisha lazima mtu ujiandae kwa lolote, mahali popote na wakati wowote... 

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images