Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 62 | 63 | (Page 64) | 65 | 66 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta Akimpongeza Mkurugenzi Mkazi Trade Mark East Africa Paulina Elago kwa kuwezesha TANGO kuzindua mtandao wa majadiliano kuhusu Afrika Mashariki kwenye uzinduzi Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta Akisisitiza jambo, wakati wa Uzinduzi wa Mtandao wa Tango utakaojadili mada mbalimbali kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya Serena
   Waziri Sitta Akibonyeza Kitufe Kuzindua Rasmi TANGO Forum. Kulia Ni Mkurugenzi Mkazi Trade Mark East Africa Paulina Elago na Kushoto ni Mratibu Wa Tango Forum David Doya
  Mkurugenzi Mtendaji Wa Tango Nunga Tepani akizungumza na Waandishi wa Habari, mara baada ya uzinduzi Wa Tango Forum uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam

  0 0

   Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkuu wa Utumishi wa MCC Bw.Steve Kaufmann,akiongoza ujumbe wa viongozi wa MCC waliofika Ikulu Mjini
  Zanzibar kwa mazungumzo na Rais 
  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Mkuu wa Utumishi wa MCC Bw.Steve Kaufmann,kiongoza ujumbe wa viongozi wa MCC waliofika Ikulu Mjini Zanzibar baada ya  mazungumzo na Rais jana.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0


  "Mikono Business Consult inakualika kwenye semina ya kutengeneza mfumo bora wa kibiashara tarehe 22 Machi 2013 katika ukumbi wa Holiday Inn. Jumuika nasi kujifunza mengi kuhusu biashara na kutengeneza mitandao na wajasiriamali wengine. Kiingilio Tsh 45,000/= tu pamoja na viburudisho."

  Tiketi zinapatikana Tausi Fashions Mlimani City, Holiday Inn Hotel, Amina Designs Quality Centre, Mayfair Plaza ghorofa ya kwanza au piga simu namba 0717109362.


  Mikono Business Consult

  0 0

   Wajumbe wa Bodi katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chawata Mwanza.
   Mkrugenzi wa shirika la NGOs akiwaeleza wajumbe namna shirika lake linavyofanya kazi
   Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya NGOs Dr. Aisha Kigoda akiongea na wadau wa NGOs wakati wa mkutano
   Katibu na Msajili wa NGOs Bw. Marcel Katemba akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Bodi na wadau wa NGOs


  0 0


  0 0

  Pichani kati ni Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Dina Marios kutoka Clouds FM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo pamoja na Mkurugenzi wa benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha,mapema leo kwenye studio za Clouds FM,Mikocheni jijini Dar.Hafla hiyo imeandaliwa na UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF).
  Mkurugenzi wa benki ya Wanawake Tanzania,Bi.Magreth Chacha ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa hafla ya Tuzo za Mwanamakuka 2013 inayotarajia kufanyika hapo kesho ijumaa ndani ya hotel ya Serena jijini Dar,akifafanua zaidi kuhusiana na mambo mbalimbali yanayofanywa na benki hiyo ya wanawake inayotoa mikopo kwa riba nafuu,kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo akisikiliza kwa makini.Hafla hiyo ya tu zo yakumzawadia mwanamke shujaa aliyepewa jina la Mwanamakuka inafanyika kesho ikiwa pia ni sehemu ya kuadhimisha siku wanawake duniani kote
  Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo,pichani shoto akifafanua jambo kuhusiana na shunghuli nzima ya hafla ya kumzawadia mwanamke shujaa Mwanamakuka siku ya Wanawake Duniani inayotarjiwa kufanyika kesho Duniani kote,Bi.Mariam alisema kuwa katika hafla hiyo kutakuwepo na shunguli mbalimbali ikiwemo burudani kutoka bendi ya Tanzanite,maonesho ya mavazi na zawadi mbalimbali pia zitatolewa ukumbini humo.
  Dina Marios akitaka kufafanuliwa jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa mradi wa Mwanamakuka,Bi.Mariam Shamo kuhusiana na shughuli nzima ya tuzo za Mwanamakuka zitakazofanyika hapo kesho ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.

  0 0

  Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi
  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6. 
  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabithi kombe  captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6
  Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)  kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke. 
  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akimtambulisha  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na  Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima ambaye  wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.

  0 0


  Vodacom Tanzania inakuletea video ya Harlem Shake! Unaweza kumtambua nani katika Video hii?

  0 0

  Wakala wa Vodacom, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akimuelimisha mteja wa Vodacom eneo la Kigogo-Mburahati Dar es Salaam faida za matumizi ya teknolojia itokanayo na minara ya 3G iliyofungwa na Kampuni hiyo kuzunguka jiji lote la Dar es Salaam hivi karibuni. Minara hiyo inatoa fursa kwa mteja wa Vodacom Tanzania kupiga simu na kupata huduma mbalimbali kulingana na vifurushi vilivyomo katika simu yake, ikiwemo intanet kwa kasi na viwango.
  Wakala wa huduma za mtandao wa Vodacom Tanzania, Elizabeth Stephen,() akimuelimisha mkazi wa Kigogo-Mburahati, Dar es Salaam, namna atakavyonufaika baada ya kutumia vifurushi vilivyopo katika mtandao huo, kufuatia kampuni hiyo hivi karibuni kufunga minara ya 3G kuzunguka maeneo yote ya Dar es Salaam, minara hiyo inatoa fursa kwa mteja wa Vodacom kupiga simu na kupata huduma mbalimbali zikiwemo za intanet kwa kasi na viwango.


  0 0
 • 03/07/13--05:11: In Loving Memory
 • THE LATE ALFRED DADI MDACHI 

   12.02.1932-11.03.2008 

   Five years look like today since you left us to be with the Lord, Your heart brought great joy to many, Those hearts can never truly forget you for you were indeed God's gift to us, Life has never been the same. We dearly miss your presence, love, understanding, guidance, kindness and rich legacy, Remembering you is easy, we do it every day,missing you is the heartache which never goes away. 

  We are comforted by the great moments you shared with us which have become our treasure, Our consolation each day is that you are in a better place where there is no pain and that one day we shall be reunited with you 

   We remain grateful to all who stood with us and continue to do so. Greatly missed by your dear wife Bernadette, your children Maria Triphonia, Fortunata Kabula, Regina Kwigema and Richard, Devota Kasanda, John Mutahanwa and Savera ,Stella Matutina ; Grandchildren Ambonisye, Irene, Joseph, Norman, Wilfred, Rafaella, Renee, Rhona, Bernadette, Alfred Dadi and Daniel, family and friends .

   In God's hands you rest, but in our hearts you live forever!

  0 0
 • 03/08/13--00:47: Article 24


 • 0 0


  KILA IJUMAA NI SIKU YA SHANGWE , WADAU WOTE WALA BATA MNAKARIBISHWA USIKU WA BEAT DOWN .

  KUTANA NA MANDHARI NZURI KWENYE LOUNGE YA KISASA NA WAJANJA WA TOWN TUJICHANGANYE HUKU( DJ BIKE WA RADIO 1) AKISABABISHA NA NGOMA ZA UKWELI.
  KIINGILIO NI ELFEU KUMI (10,000/=) 

  TUNAANZA ILE MIDA YETU YA SA 3 MPAKA ASUBUI.
  TUKO MTAA WA ZAMBIA NA MKWAWA . KATA KUSHOTO BAADA YA KCB BANK, NENDA HADI ZAMBIA AMBAYO NI KONA YA PILI KUSHOTO ALAFU KATA KULIA MTAA WA MKWAWA NA UTATUONA NYUMBA YA 5 KULIA. 

  BASI HIYO NDIO MASKANI YA WAJANJA WA TOWN
  KARIBUNI.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa kipindi kingine Balozi Christopher Liundi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa-Arusha (AICC).


  Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-


  1.         Bw. Aggrey Mlimuka


  2.         Bw. Dash-Hood Mndeme


  3.         Dkt. Ali Mndali


  4.         Mhe. Balozi Abdi Mshangama (Mstaafu)


  5.         Mhe. Faith Mtambo (Mbunge wa Viti Maalum)


  6.         Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (Mbunge wa Nzega)


  7.         Mhe. Mary Chatanda (Mbunge wa Viti Maalum)


  8.         Mhe. Ali Mzee Ali, (Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi - Zanzibar)


  9.         Bw. Wilson Masilingi (Mbunge Mstaafu)


   Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 06 Machi, 2013.
      
  IMETOLEWA NA: 
  WIZARA YA MAMBO YA NJE

  NA 
  USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

    8 MACHI, 2013

  0 0

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania.Airtel,Tigo,TTCL kuweka saini makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
  Baadhi ya wawakilishi wa kampuni za simu za mkononi wakimpigia makofi ,Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,mara baada ya kumaliza kutoa spichi yake wakati wa kuweka saini makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania,Airtel,Tigo,TTCL kuhusiana na makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
  Mwakilishi wa Vodacom Tanzania Bw.Nguvu Kamando, (Kulia), akiweka saini makubaliano ya pamoja ya kampuni nne za simu za mkononi, kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma jijini Dar es Salaam . Katika mkataba huo makampuni ya Tigo, TTCL, Airtel ambapo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,(Watatu kulia waliosimama), alishuhudia.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura (Kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Nguvu Kamando mara baada ya hafla ya kusaini mkataba wa ushiriki wa mfuko wa mawasiliano ya umma, jijini Dar es Salaam, ambapo makampuni manne ya simu za mkononi yameshiriki. Makampuni hayo ni Vodacom Tanzania, Tigo, TTCL na Airtel .

  0 0

  Weruweru river lodge hotel ya mjini Moshi imebainika kutumia umeme wa wizi mchana huu. Kikosi toka Tanesco makao makuu pamoja na mafundi mkoa Kilimanjaro wamebaini hotel hiyo kutumia umeme usiopitia kwenye mita. 
  Mhandisi Francis Maze amesema hotel hiyo inamatumizi makubwa sana hivyo ni wazi kwamba Shirika limekuwa likipoteza mapato makubwa sana kupitia wateja hao. Meneja mkuu wa hotel na fundi mkuu wamechukulia na polisi kwa taratibu za kisheria.
  Weruweru river lodge hotel ya mjini Moshi

  Hivi ndiyo njia iliyowezesha Weruweru river lodge hotel kutumia umeme bila kupitia kwenye mita.  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana jioni amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bharti Airtel ya India Bw. Sunil Mittal aliyemtembelea na ujumbe wake kuzungumzia maswala mbalimbali ya sekta ya Mawasiliano. 

  Bw. Mittal aliongozana na Bw. Manoj Kohli, CEO Internationa wa kampuni hiyo, Bw. Jayant Khosla, CEO Anglophone Africa, Bw. Sam Elangallor, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania anayemaliza muda wake, Bw Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania pamoja na Bi Beatrice Singano, Corporate Affairs Director wa Airtel Tanzania.

  Katika mazungumzo hayo ujumbe wa serikali ulikuwa ni pamoja na Waziri wa Sanyasi, Mawasiliano na Tekenolojia, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CHC Profesa Marcelina Chijoriga, Kaimu Mtendaji wa CHC Bw. Dome Malosha, Msajili wa Hazina Mama Mlaki na Mhandisi Clarence Isokeleza.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso.
  Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Sam Elangallor.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


   Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Vivian Shalua akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Semina ya Mawakala wa Mashindano ya Urembo ya Redd's Miss Tanzania 2013 inayofanyika kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga na Kushoto ni Afisa Habari Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Agnes Kimuage.
   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akitoa Mada kwenye Semina ya Mawakala wa Mashindano ya Urembo ya Redd's Miss Tanzania 2013 inayofanyika kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini Wakuu wa Redd's Miss Tanzania,Fimbo Butallah akitoa ufafanuzi juu ya Mada ua Udhamini na Wadhamini wakati wa Semina ya Mawakala wa Mashindano ya Urembo ya Redd's Miss Tanzania 2013 inayofanyika kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam leo.
   Muandaaji wa shindano la Urembo la Redd's Miss Temeke,Benny Kisaka akichangia Mada katika Semina hiyo inayoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
   Muandaaji wa shindano la Urembo la Redd's Miss Chang'ombe,Tom Chilala akichangia Mada katika Semina hiyo inayoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.
   Muandaaji wa shindano la Urembo la Redd's Miss Mbeya City Center,Anitha Audax akijitambulisha kabla ya kuanza kwa Semina ya Mawakala wa Mashindano ya Urembo ya Redd's Miss Tanzania 2013 inayofanyika kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam leo.
   Muandaaji wa shindano la Urembo la Redd's Miss Kanda ya Kati,Mama Salome Kiwaya akichangia Mada katika Semina hiyo inayoendelea leo kwenye Ukumbi wa Jetty,uliopo ndani ya Hoteli ya Girrafe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki michuano ya NSSF Media Cup 2013. 
  Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto) akimkabidhi nahodha wa Free Media FC, Salum Mkandemba sehemu ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya NSSF Media Cup 2013 yanayoanza kutimua vumbi Jumamosi Machi 9 kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa timu ya TBC, Chacha Maginga akipokea jezi pamoja na viatu kutoka kwa Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume. Katikati ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF Juma Kintu.
  Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akikabidhi sehemu ya vifaa vya michezo kwa wawakilishi wa timu za vyombo vya habari kwa ajili ya mashindano ya NSSF Media Cup 2013 yanayoanza kutimua vumbi Jumamosi Machi 9 kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akimkaribisha Balozi wa Rwanda hapa nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ben Rugangazi, wakati Balozi huyo alipomtembelea Spika ofisini kwake Dar es Salaam leo. Katika mazungumzo yao, Balozi Rugangazi alimuomba Spika kupitia Bunge nchi mbili hizi zizidi kuimarisha mahusiano mzuri yaliyopo.

  Spika Makinda alimhakikishia Balozi Rugangazi kulisimamia jambo hilo huku akimweleza kwa muhtasari nia ya mabadiliko ya Bunge ya kuanza mkutano wake wa Bajeti mwezi Aprili badala ya mwezi Juni kama ilivyozoeleka. Mkuu huyo wa mhimili wa Bunge amesema hatua hii itaisaidia serikali kuanza kutumia fedha za mapato na matumizi mara tu mwaka wa fedha wa serikali (Julai Mosi) unapoanza. "Siku ya kusomwa bajeti kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itabakia kuwa ni ile ile ila sisi tutaanza kujadili wizara zote za kisekta isipokuwa wizara ya Fedha hadi mwezi Juni," alisema Spika na kuongeza.

  Balozi Rugangazi aliifurahia hatua hiyo huku akisisitiza kuwa Rwanda inayo mengi ya kujifunza kutoka Tanzania. Aidha Balozi huyo alitoa mwaliko na taarifa ya maadhisho ya siku ya 'Utu wa Binadamu' ambayo taifa la Rwanda huadhimisha kila tarehe 7 Aprili kwa ajili kuwakumbuka wale wote waliouawa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu takriban milioni moja waliuawa kikatili kufuatia mchafuko baina ya kabila la Wahutu na Watutsi.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa Tamko kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Afya ya Figo Duniani itakayoadhimishwa tarehe 14, Machi. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Figo Tanzania ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Figo Tanzania Mh. Frederick Werema akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kunywa maji safi na salama kama moja ya njia za kukinga figo kuathiriwa na magonjwa mbalimbali na kutoa wito kwa watanzania kuepuka tabia hatarishi kwa afya ya figo zikiwemo za utumiaji wa pombe kupita kiasi, madawa ya kulevya, utumiaji wa dawa za binadamu kupita kiasi na uvutaji wa sigara. 
  Katibu wa Taasisi ya Figo Tanzania Dr. Linda Ezekiel akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mikakati ya Taasisi ya Figo Tanzania katika kutoa kwa elimu wananchi na mchango wake katika kupambana na ugonjwa wa Figo nchini.
   Picha na Aron - MAELEZO.

older | 1 | .... | 62 | 63 | (Page 64) | 65 | 66 | .... | 3272 | newer