Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109933 articles
Browse latest View live

Discussion on USAID African Diaspora Marketplace III

$
0
0
Discussion with Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID. Barbara Span, Vice President, Global Public Affairs, Western Union, Eric-Vincent Guichard, CEO, Homestrings and Zelalem Dagne, ​ CEO, Global Tracking before the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADM III), on October 27th 2014 at The Embassy of Tanzania in Washington, DC

WAFANYAKAZI AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAHAMASISHA WATEJA KUFUNGUA AKAUNTI YA DHAMIRA

$
0
0
Meneja Msaidizi wa Benki ya Azania Joseph Msase akikabidhi fomu ya Akaunti ya Dhamira kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo Benjamini Mengi.
Mteja wa Benki ya Azania Benjamini Mengi akionesha fomu yake baada ya kujiunga na Akaunti ya Dhamira ,wengine ni wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe(mwenye kilemba) na familia ya Mengi.
Mtoa huduma kwa wateja katika Benki ya Azania tawi la Moshi ,Happy Msengi akimshawishi Mama Mengi kufungua akaunti ya Dhamira iliyoanzishwa katika Benki hiyo.
Meneja Msaidizi Benki ya Azania Joseph Msese(katikati) akiwa na mtoa huduma kwa wateja Happy Msese wakijaribu kumshawishi kijana Benson Benjamini kufungua akaunti ya Dhamira.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe(kushoto) akiendelea kushawishi wateja wapya kujiunga na Akaunti ya Dhamira iliyoanzishwa katika benki hiyo.
Mtoa huduma kwa wateja katika benki ya Azania Mary Machange akiandika maelezo ya mteja  Benki Dowald Mushi alipokuwa akifungua Akaunti ya Dhamira katika tawi la Benki hiyo la Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA

$
0
0
Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Moshi vijijini  ,Hussein Jamal akizungumza wakati wa kikao cha makatibu kata na makatibu wa matawi kilichofanyika katika hotel ya King Size Himo.
Mwenyekiti wa Makatibu katika jimbo la Vunjo ,Shaban Mwangi akisoma taarifa ambayo inadaiwa kupikwa kwa lengo la kukivuruga chama hicho katika jimbo la Vunjo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakati wa kikao hicho ambacho kilijadili pia tuhuma zilizotolewa dhidi yake.
Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Shirima akizungumza wakati wa kikao hicho kilichokuwa na lengo la kurudisha hali ya amani na umoja ndani ya chama cha mapinduzi jimbo la Vunjo.

KAMPUNI YA PETROGAS YAENDESHA MAFUNZO YA UANDAAJI WA MAPENDEKEZO YA MIRADI KWA WATAALAMU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

$
0
0
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Petrogas inayojihusisha na kutoa mafunzo kwa ajili ya uandaaji wa mapendekezo ya miradi pamoja na usimamizi wake yenye makazi yake jijini Dar es Salaam Bw. Greyson Kiondo akisisitiza jambo kwenye mafunzo yanayohusu uandaaji wa mapendekezo ya miradi na usimamizi wake yaliyoshirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea mjini Bagamoyo katika hoteli ya Stella Maris.
Msimamizi wa mradi unaohusika na kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati na tasnia ya uziduaji (CADESE; Capacity Development in the Energy Sector & Extractive Industries) Bw. Paul Kiwele (kulia) akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga.
Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga ( wa kwanza kulia mbele ), msimamizi wa mradi wa CADESE Bw. Paul Kiwele (katikati) na baadhi ya washiriki wakiendelea kufuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa na mtaalamu mwelekezi Bw. Tom Mitro kutoka Petrogas (hayupo pichani).
Mtaaalamu kutoka Petrogas Bw. Tom Mitro akiwasilisha mada juu ya uandaaji wa mapendekeo ya miradi katika semina hiyo mbele ya washiriki (hawapo pichani).
Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi Hosea Mbise kwenye mafunzo hayo. Kulia ni msimamizi wa mradi wa CADESE Bw. Paul Kiwele.

RATIBA YA KUAGA MWILI LEO NA MAZISHI YA ROBERT VICTOR LENGEJU

$
0
0

Familia ya Lengeju wa Kipera Mkoani Morogoro na Dar es Salaam inapenda kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki wote wa marehemu ROBERT VICTOR LENGEJU na Familia ya LENGEJU kuwa kijana wao mpenda aliyefikwa na umauti Novemba 10, 2014 katika Hospitali ya TMJ baada ya kuugua kwa muda mfupi anataraji kuzikwa kesho Alhamisi nyumbani kwao Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro.

Kipera ipo mbele kidogo ya Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Mwili wa marehemu ROBERT LENGEJU, utaagwa leo kuanzaia saa 6:00 mchana baada ya Misa katika Kanisa Katoliki Msimbazi Dar es Salaam na baade jioni kusafirishwa hadi Morogoro.

Kesho Novemba 13 2014, kuanzia saa 5:00 Asubuhi taratibu za mazishi zitaanza nyumbani kwao KIPERA kwa misa takatifu na maziko.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO

$
0
0
Mkutano wa hadhara wa chama cha Tanzania Labour (TLP) uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Agustine Mrema jirani na matanki ya Maji katika kijiji cha Mieresini wilaya ya Moshi vijijini.
Afisa uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Frolah Nguma (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya maji baada ya Mbunge Mrema kumtaka kufanya hivyo muda mfupi baada ya maofisa wa Mamlaka hiyo kufika katika Matenki ya Maji kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Msimamizi mkuu wa (MUWSA) Kituo cha Himo Brucevictor Sangawe akitoa ufafanuzi kwa wananchi mbele ya mbunge wa jimbo la Vunjo ,Agustine Mrema juu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya ukanda wa juu katika mji wa Himo.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

KINUKAMORI WAOMBA DOLA 30,000 KUTENGENEZA AJIRA KWA WATU 300

$
0
0
Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro Executive Wilderness Program (EWP) inatafuta dola za marekani 30,000 kwa ajili ya kuendesha program tatu zenye kutengeneza ajira, ujasirimali, utunzaji wa mazingira na mvuto kwa watalii wanaokwenda kupanda mlima Kilimanjaro.

Kauli hiyo wameitoa kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez wakati alipofanya ziara mkoani Kilimanjaro kuangalia miradi inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Uongozi wa EWP and Kinukamori Enterprises katika taarifa yao kwa Mratibu huyo, iliyosomwa na Mshauri wao wa fedha Grace Shayo wamesema pamoja na nia yao ya kuhakikisha maporomoko ya Kinukamori yanaendelea, kwanza kama taasisi na pili kama mradi wa kuhifadhi mazingira ya Mlima Kilimanjaro ambao ni sehemu ya urithi wa dunia, wakishirikiana na KINAPA wamefikiria miradi kadhaa ambayo ikienda kwa pamoja itaendeleza eneo hilo.

Wamesema fedha hizo zitatumika kutoa elimu ya ujasirimali kwa vijana 300 wanaoishi katika jamii ya Marangu ambao hutoa huduma mbalimbali kwa wenyeji na pia wageni wakiwemo watalii. Kundi hilo linalotakiwa kupewa mafunzo ni pamoja na wapagazi 50, waendesha pikipiki 100, wachuuzi 100 na walima mboga 50.
DSC_0218
Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi (wa pili kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP huku akiwa amembatana na Mratibu wa Kitaifa miradi ya COMPACT mkoani Kilimanjaro, Victoria Nderumaki (wa tatu kulia) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

AFRICA’S REGIONAL NETWORK FOR YOUTH POLICIES EXPERTS LAUNCHED AT THE FIRST GLOBAL FORUM ON YOUTH POLICIES ON BAKU, AZERBAIJAN.

$
0
0
Invest in Youth Logo
Africa made history during the closing session of the just concluded First Global Forum on Youth Policies, held in Baku, Azerbaijan by announcing the birth of African Network of Youth Policy Experts (AfriNYPE) to advance the cause of youth policies in the region.

The network was announced at the closing plenary session attended by over 700 invited delegates constituting of experts, researchers, professors, government representatives across the world, and the United Nations Secretary-General's Envoy on Youth, Mr. Ahmad Alhendawi.

A member of the Steering Committee, Adeola Austin Oyinlade, Human rights lawyer and Youth rights/policy expert from Nigeria described the unveiling as ‘good news from Africa’.

According to Mr. Oyinlade who is also a resource person to the African Union (Youth Division) on the implementation of African Youth Charter, the network’s objectives include establishing a comprehensive research and studies unit, in order to collect reliable data and analyse the current situation of youth policies in order to advise key African Stakeholders on concrete and practical mechanisms, for a more inclusive development and implementation of these policies, while improving legal enabling environment of youth participation in decision making.

Ms. Karima Rhanem, a civil society and youth policy expert from Morocco told the gathering that prior to the global forum, young African delegates to the forum engaged in intensive dialogue, through social media and desk research review to do situation analysis of youth policies in the region, mappings and SWOT analysis, which subsequently produced a concrete strategic document that led to the emergence of AfriNYPE.

According to Ms. Rhanem, AfriNYPE is a collective initiative of experts on youth policies in Africa who shared understanding of the urgent need for concrete development and implementations of youth policies in an African context.

SHIWATA YALIA KUMPOTEZA AMIGOLAS

$
0
0

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)unaungana na watanzania kuomboleza kifo cha mwanamuziki maarufu Hamisi Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki Jumapili na kuzikwa Jumatatu iliyopita katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa marehemu Amigolas atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya akiwa mwanachama wa mtandao huo alishiriki kutafuta eneo la makazi ya wasanii ya kijiji cha Mwanzega na shamba la wasanii lililopo Ngarambe wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Alisema alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele pale  alipowahamamisha wanamuziki wenzake kujiunga SHIWATA kutoka bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'akiwemo Luiza Mbutu,marehemu Abuu Semhando na wengine.

Marehemu Amigolas alifariki kwa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (M.N.H) alipokuwa amelazwa kwa siku tano kabla mauti kumkuta Jumamosi saa tano usiku.

Mkurugenzi wa African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka aliyekuwa mwajiri wake kabla ya kuhamia bendi ya JKT Ruvu alisema marehemu alikuwa mwanamuzi aliyejituma na kufanya kazi kwa juhudi zote kutoka ajiunge na bendi hiyo mwaka 1997.

Hivi karibuni SHIWATA imepoteza wanachama wake maarufu waliofariki akiwemo Abuu Semhando,Amina Ngaluma na Muhidin Gurumo.

Marehemu Amigolas alizikwa na umati mkubwa wa waombolezaji kwenye makaburi ya Kisutu Jumatatu saa 10 jioni. Ameacha wajane wawili na watoto wanne. Mungu ilaze roho marehemu mahali pema peponi. Amen.

DKT International yazindua kondomu mpya

$
0
0
Shirika la DKT International limezindua rasmi kondomu mpya za Bull na Trust. Akizungumza katika uzinduzi huo, rais wa DKT ndugu Christopher Purdy alisema nia hasa ya kuleta bidhaa za kondomu nchini ni kusaidia katika jitihada za kukabiliana na uzazi wa mpango na pia magonjwa ya zinaa.

 Uzinduzi huo ulienda sambamba na usomaji wa ripoti ya utafiti wa tabia za kimapenzi kwa wakazi wa Dar es Salaam iliyofanywa na taasisi ya Data Vision International ambayo mojawapo ya matokeo ni ile iliyoonyesha idadi kubwa ya watu bado inashiriki mapenzi bila kutumia kinga.
Macmillan George toka Data Vision International akitoa ripoti ya tabia za kimapenzi kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini taarifa hiyo.
Rais wa DKT International Christopher Purdy akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa DKT International Davis Kambi akiongea kuhusu bidhaa hizo za kondomu.
Muonekano tofauti wa kondomu mpya za Bull.

MDAU ALALAMIKIA KUCHELEWESHWA UTOLEWAJI WA VYETI VETA.

$
0
0

Lalamiko langu kubwa ni kuhusu VETA kumekuwa na tatizo la ucheleweshaji wa vyeti pindi wahitimu wanapomaliza course zao siju ni kwanini? 

Tukiangaliwa vyuo vingi vinavyomilikiwa na serikali wanafunzi wanapomaliza shule yao na matokeo yao yakatoka uwa wanapewa result
slip inayoonyesha kuwa huyu mtu amemaliza course fulani na ameshinda wakati anasubili cheti chake na cheti hakichelewi sana kutoka kama ilivyo kwa VETA kitu ambacho ni tofauti na VETA.

Mwanafunzi anapomaliza course yake na matokeo yakatoka amefauru anasubili cheti karibu mwaka mzima sasa huyo mwanafunzi au mhitimu kama anatafuta kazi ataipataje bila cheti? au atafanyaje maombi katika vyuo vingine kwa ajili ya kujiendeleza? Jamani tunaomba milifanyie kazi maana sio kawaida kabisa ni uonevu hasa kwa vyuo vya mikoani kazi zenyewe zimekuwa ngumu bila cheti cha uhakika sio rahisi kupata kazi.
TUNAOMBA WAHUSIKA WALIFANYIE KAZI
Nimewasilisha

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA UFUGAJI NYUKI JIJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na wananchi wa jamii ya Wadzabe kutoka wilayani Karatu,mkoa wa Arusha leo wakati wa Kongamano la siku tatu la Wadau wa Ufugaji Nyuki barani Afrika na Mazao ya Asali linalofanyika jijini Arusha.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua mazao yanayotokana na ufugaji wa Nyuki kwenye banda la Wajasiriamali kutoka wilayani Kibondo mkoa wa Kigoma.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu leo wakati akikagua mabanda ya wajasiriamali kwenye Kongamano la siku tatu la Wadau wa Ufugaji Nyuki barani Afrika na Mazao ya Asali linalofanyika jijini Arusha.
Wadau kutoka maeneo mbalimbali nchi wakionesha bidhaa zao zinazotokana na Ufugaji Nyuki na mazao yake likiwa na lengo la kutunza mazingira na kukuza uchumi.
Wadau kutoka maeneo mbalimbali nchi wakionesha bidhaa zao zinazotokana na Ufugaji Nyuki na mazao yake likiwa na lengo la kutunza mazingira na kukuza uchumi.
Banda la Shirika la TBS linalohakiki ubora wa bidhaa mbalimbali likiwa miongoni mwa washiriki ili kuhakikisha ubora wa bidhaa za wajasiriamali.

Rais wa Zanzibar afungua warsha ya Mahusiano ya Kisiasa na Kiutawala

$
0
0
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amefungua warsha ya siku tatu kwa viongozi wa juu wa Mikoa na Wilaya kutoka Zanzibar pamoja na mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara iliyofanyika Hotel ya sea Cliff Zanzibar. Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI umeanza tarehe 10 Novemba, 2014. Lengo la warsha hii ni kutoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mpya ili kuongeza ufanisi katika utendaji. Haya yalisemwa na Profesa Joseph Semboja, Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute.

Kwenye hotuba yake, Rais Ali Mohamed Shein alisisitiza umuhimu wa kuwepo mawasiliano bora baina ya viongozi na watendaji wakuu katika ngazi mbali mbali. “Mawasiliano na uhusiano ni mambo ya msingi katika utawala bora,” alisema Dk. Shein, “Mategemeo yangu ni kuwa warsha hii itakupeni mbinu bora za kuimarisha uhusiano na mawasiliano kwa ajili ya kuyafanikisha majukumu yenu ya kuwatumikia wananchi.”

Mh. Dk. Shein aliongezea kwamba zimekuwepo baadhi ya changamoto za mahusiano na muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa viongozi wa kisiasa na Watendaji Wakuu wa Mikoa na Wilaya, kwa hivyo ni muhimu kwa viongozi hawa kufahamu mipaka ya majukumu yao na kuwa na uhusiano mzuri kwa ajili ya utawala bora, ukuaji na maendeleo ya nchi.
Mh. Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya viongozi wa juu wa mikoa na wilaya ya Zanzibar pamoja na Ruvuma, Lindi na Mtwara ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi. “Huu utakuwa ni mwanzo tu wa ushirikiano wa Taasisi ya UONGOZI, Wizara ya Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Taasisi zetu mbali mbali,” alisema Dk. Shein.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI akifungua warsha ya Mahusiano ya Kisiasa na kiutawala – Zanzibar “Warsha hii imezingatia umuhimu wa mwingiliano kati ya siasa na utendaji katika kuleta maendeleo ya nchi,” Profesa Semboja alisema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Haji Omar Kheir, akipokelewa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI.
Mh. Dk. Ali Mohamed Shein na Mh. Hawa Ghasia (MB) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, wakizungumza kwenye ufunguzi.
Baadhi ya washiriki katika warsha ya “Mahusiano ya Kisiasa na kiutawala ” 
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Dk. Gordon McIntosh akiendesha mafunzo haya.

Nishati na Madini yatakiwa kushirikisha jamii kwenye uanzishaji wa miradi

$
0
0
Mtaalam Mwelekezi kutoka Kampuni ya Petrogas Bw. Tom Mitro (kushoto) akielekeza namna ya kuandaa mapendekezo ya miradi ( project proposals) mbele ya washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na Bw. Tim Mitro kutoka kampuni ya Petrogas (hayupo pichani).
Mtaalam Mwelekezi kutoka Kampuni ya Petrogas Bw. Tom Mitro akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.

Na Greyson Mwase, Bagamoyo

Wataalamu wa Nishati na Madini wametakiwa kushirikisha jamii inayozunguka miradi inayoanzishwa ili kuzuia migogoro inayoweza kutokea kutokana na wananchi kukosa uelewa na miradi mipya.

Wito huo umetolewa na mtaalamu kutoka kampuni ya Petrogas Bw. Tom Mitro katika mafunzo ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yanayoendelea mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TDGC).

Bw. Mitro alisema kuwa katika nchi nyingi za Afrika hususan zenye rasilimali nyingi kumekuwepo na migogoro mikubwa katika uanzishwaji wa miradi kutokana na jamii kutoshirikishwa kabla ya kuanzishwa kwa miradi.

Alisema katika hatua za awali za maandalizi ya miradi, wadau mbalimbali muhimu wamekuwa wakishirikishwa ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha, serikali, wanasiasa, wahisani huku kundi la jamii inayozunguka miradi husika likisahauliwa kabisa.

Akielezea athari za kutowashirikisha jamii inayozunguka miradi Bw. Mitro alisema kuwa ni pamoja na migogoro inayopelekea kukwama kwa miradi hali inayopelekea miradi kutokamilika kwa wakati.

“ Wananchi wengi wanapokosa uelewa wa miradi yenye manufaa kwa taifa, matokeo yake ni kuipinga hali inayopelekea kukwama kwa miradi hiyo.” Alisema Bw. Mitro. Bw. Mitro alisema kuwa jamii inayozunguka miradi pamoja na asasi za kiraia zina umuhimu mkubwa sana katika ushirikishwaji katika uanzishaji wa miradi kwani ndio walinzi wa miradi husika hususan miundombinu yake.

Akilelezea jinsi jamii inayozunguka miradi inavyoweza kushirikishwa Bw. Mitro alieleza kuwa ni pamoja na mikutano ya mara kwa mara na wananchi ikiwa ni pamoja na wawakilishi wao na kusisitiza kuwa wanaposhirikishwa katika kila hatua ya mradi wanakuwa mabalozi kwa wananchi wenzao.

Aliongeza kuwa ushirikishwaji wa jamii unaifanya jamii kuwa sehemu ya umiliki wa miradi na kulinda miundombinu yake.

Mafunzo hayo yameandaliwa na mradi unaohusika na kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati na tasnia ya uziduaji (CADESE; Capacity Development in the Energy Sector & Extractive Industries) lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu kutoka sekta za nishati na madini katika uandaaji wa mapendekezo ya miradi mbalimbali ( project proposals) na sera na hivyo kuepusha gharama ya kutumia wataalamu kutoka nje na kukuza umiliki.

Mafunzo hayo yatakayochukua wiki tatu yatashirikisha washiriki 60 ambapo kila kundi la washiriki 20 litajifunza kwa muda wa wiki moja. Kundi la kwanza litajifunza juu ya uandaaji wa mapendekezo ya miradi na kufanya tathmini yake ( project proposals preparations and evaluations ), kundi la pili litajifunza juu ya uandaaji wa sera na kundi la tatu litajifunza juu ya usimamizi wa miradi.

Mradi wa CADESE unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Maendeleo (UNDP) ulianzishwa mwaka huu unatekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wadau wengine kama vile Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Taasisi ya Uogozi na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Serikali kudhibiti ukimwi hadi kufikia maambukizi sifuri

$
0
0
Na Genofeva Matemu – Maelezo

Serikali imepanga mikakati na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau wa ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanapungua hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti mtendaji kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt. Mrisho amesema kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua ukilinganisha na miaka 10 iliyopita kwani idadi imepungua kutoka waathirika laki moja na elfu themanini hadi kufikia waathirika elfu sabini na mbili kwa sasa.

Akitoa mfano Dkt. Mrisho amesema kuwa Mkoa wa Njombe, Shinyanga, Dar es Salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa ambayo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ukimwi hivyo kuwataka wadau wa ukimwi kutoka mikoa hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pamoja na magojwa ya zinaa.

Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa serikali imedhamiria kuanzisha mfuko utakaokua unashughulikia masuala ya ukimwi wakati wa bajeti ya mwaka 2015/2016 wenye lengo la kuondoa maambukizi mapya ya ukimwi nchini.

Aidha Dkt. Turuka ameitaka jamii kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi bali wawapende na kuwapa moyo ili waendelee kuwa na afya bora kwani serikali inawapigania na kuhakikisha kuwa wanatumia dawa za kuongeza maisha ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi ulianzishwa mwaka 2003 ukifuatiwa na ule wa mwaka 2006 na kuendelezwa kila baada ya miaka miwili ambapo mkutano wa mwaka huu ni wa sita na umebeba kauli mbiu inayosema “Kwa yale mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa tunayaendeleza”.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akifungua Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa wadau wa Maendeleo kwenye sekta ya ukimwi Dkt. Michelle Roland akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Chadema aunguruma mikoa ya KIGOMA na KATAVI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwakabidhi kadi za Chadema waliokuwa viongozi wa CCM wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katija jimbo la Mpanda Vijijini, baada ya kujiunga na Chadema katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.

ZAIDI YA WANARIADHA ELFU KUMI NA TANO KUSHIRIKI UHURUMARATHON 2014

$
0
0
ZAIDI ya wanariadha 15,000 kutoka ndani na nje wanatarajiwa kuthibitisha kushiriki katika mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Desemba 7 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alisema kuwa maandalizi yako katika hatua za mwisho huku akimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuongoa mbio hizo.

Melleck pia alikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Chama cha Raidha Tanzania (RT) na Sh. Milioni moja kwa wenyeji Chama cha Raidha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), ili kupata kibali cha kuendesha mbio hizo.

Mratibu huyo alisema kuwa fomu kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zimeanza kutolewa jana na jijini zinapatikana katika maduka yote ya TSN, huku pia zikitolewa kwenye mikoa ya Arusha, Moshi mkoani Kilimanjaro na Leaders.

“Tunawashukuru wadau wote walioshiriki katika kujiandaa kushiriki mbio hizo hasa klabu za jogging ambazo zinahamasisha wanariadha kushiriki mbio hizo zenye kuhamasisha Amani, ushirikiano na mshikamano,” alisema Melleck.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema kuwa chama kimeialika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Afrika Mashariki na mataifa mengine ambayo yako tayari kushiriki mbio hizo zitakazofanyika sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania.

Nyambui alisema kuwa wanariadha wamejiandaa kuonyesha vipaji vyao na wanaamini yataendelea kukuza vipaji vyao kulitangaza jina la Tanzania. Naye Mjumbe wa DAAA, Tullo Chambo, alisema kwamba chama kimeshiriki kuanzia hatua ya awali na wanawahakikishia wadau kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na mafanikio. Chambo alisema kuwa wanazipongeza klabu na makundi yote yanayoendelea kujiandaa kushiriki mbio hizo na kila kitu kitafanyika kwa kufuata taratibu za kiufundi.

Melleck alitoa rai kwa makampuni na mashirika pia watu binafsi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kudhamini mbio hizi kwani bado nafasi ipo kwa wale wote wenye nia ya kudhamini kwa mwaka huu.

Mbio za Uhurumarathon kwa mwaka huu zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake Grandmalt,Maji ya Uhui,Azam Tv,Tbc 1,Mwananchi Communications Ltd,Magazeti ya Uhuru,Jambo Leo,Michuzi media,CxC Africa,Kitwe General Traders,Samsung,Cokacola,Tindwa Mediacal Service,Gazeti la TABIBU,Konyagi,na TSN SUPERMARKETS.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akionyesha moja ya fomu za kujiunga na mbio hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambazo zinataji kufanyika Desemba 7,2014,huku Mgeni rasmi akitazamiwa kuwa ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete huku Zaidi ya wanariadha elfu kumi na tano kukadiriwa kushiriki kwa mara ya kwanza.kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambapo zinataji kufanyika Desemba 7,2014.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui akizungumzia namna mbio hizo zitakavyokuwa ikiwa ni pamoja na njia zitakazokuwa zikitumika kwa washiriki wa mbio ndefu.Kulia ni Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Raidha Tanzania (RT),Suleiman Nyambui (kulia) huku Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo akizungumza machache akishuhudia.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akikabidhi ada ya Sh. Milioni moja kwa Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo.

WATU WATANO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA BASI LA WIBONELA KUPINDUKA MJINI KAHAMA LEO

$
0
0


 Basi la Wibonela linalofanya safari zake kahama Dar limeua watu zaidi ya watano na kujeruhi wengi leo asubuhi eneo la Fantom Kahama. Chanzo ni mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo kukata kona ya kuingia barabara kuu hivyo kuruka nje na kusababisha basi hilo kupinduka. Na pia kibaka aliyekuwa anapekua na kuchomoa fedha na Vitu kwa majeruhi wa ajali hiyo amepigwa na kuchomwa moto hadi kufikia na watu wenye hasira kali. Mpaka sasa haijajulikana majeruhi ni wangapi na waliokufa ni wangapi.

Mkutano wa Fidic Business Day wafunguliwa leo jijini Dar

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Eng. Mussa Ibrahim Iyombe akizungumza wakati wa Kufungua Mkutano wa siku ya Biashara (Fidic Business Day) katika Ukumbi wa hoteli ya Serena,Jijini Dar es salaam leo. 
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano huo wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Eng. Mussa Ibrahim Iyombe (hayupo pichani).
Picha ya pamoja.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wanufaika na semina ya maswala ya udhibiti wa kipato

$
0
0
Mshauri wa maswala ya uchumi na fedha Consultant Service Excellence,Joy Nyabongo akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania jinsi ya kuweza kudhibiti matumizi ya kipato binafsi.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa sinema mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania wa kitengo cha IT Josephat Kyando akichangia hoja wakati wa semina ya jinsi ya udhibiti wa matumizi ya kipato binafsi iliyofanyika katika ukumbi wa sinema mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza mshauri wa maswala ya uchumi na fedha Consultant Service Excellence,Joy Nyabongo(hayupo pichani) wakati wa semina maalumu kwa wafanyakazi hao ya jinsi ya kudhibiti matumizi ya kipato binafsi.Semina hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa sinema mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Viewing all 109933 articles
Browse latest View live




Latest Images