Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

2014 Hospitality Roundtable in Dar

$
0
0
It is our aim that Hospitality Roundtable will grow into a memorable important conference in the African hospitality industry, and to that end, I am especially grateful to the fantastic network of people who have contributed their expertise, talents, and time to the event this year.

In our inaugural year we welcome over 20 speakers and panelists from across Tanzania and the world, all of whom are sure to inspire and spark debate amongst the participants attending this year.

With international and domestic investors recognizing the rich potential in Tanzania, it really is the time for us all to discuss how Tanzania can best foster a sustainable hospitality industry, build lasting and mutually beneficial partnerships, and build a pipeline for success.

I would like to thank all of our partners, suppliers, and colleagues for taking the time to join us today, including AKO, the JNICC, Southern Sun Hotel, the Sea Cliff Hotel, Man Magazine, and many more.

Thank you. And I sincerely hope that you find 2014 Hospitality Roundtable to be an enriching experience and take hold of the fantastic opportunity to network with so many interesting and engaged people from across the globe.
Hotels Association of Tanzania Chief Executive Officer, Lathifa Sykes adressing participants during the opening ceremony of 2014 Hospitality Roundtable in Dar es Salaam today.
Hospitality Design Partnership CEO, Meelis Kuuskler (L ) talking to one participant, Amit Patel the 2014 Hospitality Roundtable in Dar es Salaam today.
Hotels Association of Tanzania Chief Executive Officer, Lathifa Sykes (C) exchanging views with Peacock Hotels Director, Damas Mfugale (L) during the 2014 Hospitality Roundtable in Dar es Salaam today. Looking on is Skylink Travel Managing Director, Moustafa Khataw.
Some participants exchanging ideas during the conference.
A cross section of participants during the opening ceremony of 2014 Hospitality Roundtable in Dar es Salaam today.

Badilisha fedha za kigeni leo kwa viwango vifuatavyo kutoka NMB

Updates: JK aendelea vyema na matibabu anayopatiwa Marekani

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume. 

Habari kutoka hospitalini hapo ambazo Globu ya Jamii imepata zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. Tutaendelea kuwashirikisha kwa taarifa sahihi za  maendeleo yake mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.

UNDP WAZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NOONDOTO NA ELANG’ATADAPASH

$
0
0
IMG_4156
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro akiongoza gari ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye kijiji cha Elang’atadapash wilayani Longido kuzindua mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na UNDP.

Na mwandishi wetu
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka wananchi wa Longido kwa kushirikiana na viongozi wao kutunza vyanzo vya maji katika wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanafanya maeneo mengi kuwa makame.

Alvaro alisema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash uliosaidiwa na UNDP ambao unahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mratibu huyo alisema kwamba utunzaji wa vyanzo vya maji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 92 utawezesha wanawake kuendelea kushiriki katika kazi nyingine za jamii badala ya kuhangaika kutwa kusaka maji.

Aidha alisema viongozi wanatakiwa kuendelea kutoa elimu wa kutunza vyanzo vya maji na mradi huo ili uwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
IMG_4168
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akiongozana na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (kulia) mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Elang’atadapash tarafa Kitumbeine wilaya ya Longido mkoani Arusha kuzindua mradi mkubwa wa maji uliosaidiwa na UNDP ambao utahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700. 

BALOZI MDOGO WA TANZANIA DUBAI MHE. OMAR MJENGA, AKUTANA NA MTENDAJI MKUU NA RAIS WA FLYDUBAI

$
0
0
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Ghaith Alghaith, Mtendaji Mkuu na Rais wa Shirika la Ndege la FlyDubai katika ofisi za shirika hilo. Katika mazungumzo, Mhe. Omar Mjenga, amemueleza kuhusu maombi ya Serikali ya Tanzania kwa shirika hili ya kuingia ubia na Air Tanzania kwa ajili ya safari za ndani (domestic flights) na zile za kikanda (regional fligjts). Nia ya mpango huu ni kuiwezesha Air Tanzania kuanza safari zake zote za ndani na kikanda zilizosimama kwa kukosa ndege za kufanya safari hizo. Hivyo basi ushirikiano utakuwa ukiitwa: Air Tanzania Operated by Flydubai. Kwa mpango mashirika yote yataingia mkataba wa kugawana mapato kwa asilimia watayokubaliana.
Balozi Mdogo wa Tanzania -Dubai,Mhe. Omar Mjenga akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Flydubai Mhe. Ghaith Alghaith katika ofisi za flydubai.
Balozi Mdogo wa Tanzania -Dubai, Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Ghaith Alghaith, Mtendaji Mkuu wa shirika la ndege la Flydubai ambalo limezindua safari zake kati ya Dubai na Far es salaam kuanzia tarhe 16 Oktoba 2014 kwa nauli ya dola 399 Dubai-Dar-Dubai. 

KATIBU MKUU KATIBA NA SHERIA ARIPOTI OFISINI KWAKE LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi ambaye amehamishiwa Wizarani hapo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni akisaini kitabu mara baada ya kuripoti katika ofisini leo (Jumatatu, Novemba 10, 2014).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi (kulia) ambaye amehamishiwa Wizarani hapo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni akifurahi na watumishi wa Wizara hiyo, Bi. Joyce Mtuma (kushoto) na Bi. Fatuma Ngodoki, mara baada ya kuripoti katika ofisini leo (Jumatatu, Novemba 10, 2014).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi (kulia) ambaye amehamishiwa Wizarani hapo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni akiwa katika ofisi yake leo (Jumatatu, Novemba 10, 2014). (Picha na Said Benjamin)

TANZANIA INAHITAJI MASTER PLAN YA NCHI NZIMA - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania kama nchi inapaswa kuwa na mpango wa kuendeleza mipango miji (master plan) wa nchi nzima unaozingatia ukuaji wa miji yetu.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 10, 2014) wakati akifungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa za Miji kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

 “Sasa hivi hapa nchini tuna tatizo la ukuaji mkubwa wa miji yetu na Dar es Salaam ni mmojawapo. Hakuna miundombinu ya majitaka, nyumba zimesongamana, hakuna barabara za uhakika... ukuaji wa miji ni lazima uangaliwe kwa naman ya tofauti na upewe uzito unaostahili,” alisema.

“Lazima tuje na master plan ya miji yote mikubwa kama Arusha, Mwanza na Dar es Salaam hata kama itabidi kutafuta wafadhili ili tuweze kuifanya kazi hiyo. Lazima huo mpango kabambe uwepo kama kweli tunataka kumaliza tatizo hili,” aliongeza.

“Hivi hata ukitaka kupeleka timu ya waokoaji unawapelekaje? Je ukiwapeleka wapite wapi?, watue wapi? Lazima tutafute wafadhili wa kufinance mpango huu,” alisisitiza.

Akitoa mfano Waziri Mkuu alisema kukosekana kwa mipango miji kunaleta matatizo ya wnanchi kupelekewa mahali hata kama hapajaandaliwa. “Kulitokea mafuriko hapa Dar es Salaam, watu wakapelekwa Mabwepande. Je kulikuwa na mpango wowote wa miundombinu ya kuwaweka huko? Je, yakitokea mafuriko mengine, watu watapalekwa wapi?” alihoji.

Alisema kutokuwepo kwa mpango huo kumefanya asilimia 70 ya makazi kujengwa katika maeneo yasiyo rasmi.

Waziri Mkuu pia aliwataka viongozi hao waangalie ni kwa jinsi gani wanaweza kupunguza athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi kwenye maeneo wanakotoka. “Kwangu mimi natamani kuona madhara yanayotokana na tabianchi yakipungua. Jaribuni kujiuliza mtaweka mikakati gani ili kupunguza athari za mafuriko,” alisisitiza.

Aliwataka pia waangalie athari za uchafuzi wa mazingira kwa sababu ni changamoto kubwa katika miji mingi hapa nchini. “Pale Kinyerezi wana dampo na wanaona suluhisho ni kuchoma moto lakini hawaangalii madhara ya ule moshi unaotokana na uchomaji taka,” alionya.

Mapema, akielezea kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty alisema mkutano huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano (Durban Adaption Charter) yaliyofanyika jijini Durban, Afrika Kusini, Desemba, 2011 ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo la mabadiliko ya tabianchi.

“Wakati tulipoenda Durban, tulienda na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke. Sasa hivi ziko Halmashauri 102 ambazo zimeshatia saini makubaliano haya,” alisema.

Lengo la mkutano huo ni kutafuta njia za kutafuta ufumbuzi wa mabadiliko ya tabia kwa kutumia mbinu zinaoendana na mazingira ya hapa nchini (local solutions).

BREAKING NYUZZZZZ.....: Mbunge wa Mbeya Vijijini Mh.Mchungaji Luckson Mwanjale aanguka ghafla bungeni leo

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Vijijini Mh.Mchungaji Luckson Mwanjale akiwa amebebwa na wahudumu wa afya baada ya kudondoka ndani ya Jengo la Ukumbi wa Bunge leo mchana. Chanzo cha kuanguka kwake huko bado hakijafahamika na sasa yuko kwenye uangalizi wa madaktari kwa uchunguzi zaidi.Taarifa zaidi tutatoa kadri zitavyotufikia.
Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii kanda ya kati.

Naibu Mwanasheria wa Serikali afungua mafunzo ya haki za binadamu Kunduchi leo

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo kuhusu masuala ya haki za binadamu wakifuatilia hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (hayupo pichani) iliyotolewa leo Kunduchi Beach Resort. Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) kwa ufadhili wa SIDA.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo ya masuala ya haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (waliokaa, wa pili kutoka kushoto) muda mfupi baada ya kufungua rasmi warsha hiyo Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden, Ms. Janne Holck Clausen (katikati) na Mratibu wa Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI), Ms. Flavia Mwangovya muda mfupi baada ya ufunguzi rasmi wa warsha ya mafunzo ya siku tano kwa taasisi za kitaifa za haki za binadamu Afrika huko Kunduchi Beach Resort leo.

NAIBU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AZUNGUMZA NA MJUMBE MAALUM WA MAREKANI ENEO LA MAZIWA MAKUU

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)  na Mjumbe Maalum wa Marekani kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Russel D. Feingold alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo. Katika mazungumzo yao waligusia mchango wa Tanzania katika suala la amani Mashariki mwa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 
Mkurugenzi wa Idara  ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo  wakifuatilia mazungumzo kati ya Naibu Katibu Mkuu na Bw. Russel (hawapo pichani).
Sehemu ya ujumbe uliofutatana na Bw. Russel wakifuatailia mazungumzo.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa mazungumzo kati ya Balozi Gamaha na Bw. Russel (hawapo pichani) Picha na Reuben Mchome

TAARIFA YA MSIBA WA NDUG.ROBERT VICTOR LENGEJU

$
0
0
Familia ya Lengeju wa Kipera Mkoani Morogoro wanasikitika kutanga kifo cha mdogo wao ROBERT VICTOR LENGEJU kilichotokea mchana wa leo katika Hospitali ya TMJ Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwa kaka yake Charles Lengeju, Njia panda Airport jijini Dar es Salaam.


Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia ya Lengeju na wakazi wa Kipera mkoani Morogoro. 

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

RAIS WA BUNGE LA SADC NA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MHE. ANNE MAKINDA ASHIRIKI MISA MAALUM YA KUMWOMBEA ALIYEKUWA RAIS WA ZAMBIA MAREHEMU MICHAEL SATA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE LA ZAMBIA MJINI LUSAKA LEO

$
0
0
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Sata ukiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia leo tayari kwa misa Maalum iliyoandaliwa kabla ya mazishi kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu wa Zambia Mhe. Lupia Banda akimpokea Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda alipowasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda mara baada ya Kuwasili katika Viwanja vya Bunge kushiriki Misa hiyo.

Akudo Impact, Mashujaa Music na Jahazi Modern Taarab kusindikiza uzinduzi wa Albam ya Tarsis Masela

$
0
0
BENDI mbili za muziki wa dansi, Akudo Impact, Mashujaa Music pamoja na kundi la mahiri la muziki wa taarab la Jahazi Modern Classic vitasindikiza uzinduzi wa albamu mpya wa msanii, Tarsis Masela (pichani katikati) unaotarajiwa kufanyika Novemba 21 kwenye ukumbi wa Ten Lounge jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza jijini Dar es salam leo , Meneja wa mwanamuziki huyo, Ray Matata, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika na bendi zote tatu zimethibitisha kutoa burudani siku ya uzinduzi huo. 

Matata alisema kuwa wameandaa onyesho ambalo litakuwa ni historia katika muziki wa dansi hapa nchini. Masela alisema kwamba amejiandaa kuwapa mashabiki wa dansi wa Tanzania burudani yenye ubora na lengo lake ni kuonyesha kipaji chake katika sanaa ya muziki. 

“Huu ni mwaka wa saba niko Tanzania, nimejiandaa kuwapa burudani bora mashabiki wa muziki na kuwaachia zawadi ambayo hawataisahau kwenye tasnia ya muziki wa dansi,” alisema Masela. 

Aliongeza kuwa albamu yake anayotarajia kuizindua ina jumla ya nyimbo nane na itajulikana kwa jina la Acha Hizo. Alizitaja nyimbo zinazounda albamu hiyo kuwa ni pamoja na Tabia Mbaya, Mwiko, Chaguo Langu, Tusiachane, Penzi Langu Limezidi Asali, Vidole Vitatu na Nimevulimia. 

Alieleza kwamba katika albamu hiyo ameshirikisha wasanii wa aina mbalimbali ili kuifanya iwe na ubora kwa kupendwa na wadau wa rika tofauti. Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi ya Mashujaa, Maximillian Luhanga, alisema kwamba wamekubali kusindikiza uzinduzi wa albamu hiyo kwa kuheshimu kipaji cha Masela na kutaka kuendelea wasanii wa muziki wa dansi. 

Luhanga alisema kwamba hiyo itaondoka ile dhana ya wasanii wa dansi hawapendani na amewataka wanamuziki wengine kufuata nyayo za msanii huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya Marekani yaendesha kliniki ya masikio mkoani Arusha

$
0
0
7qDAKTARI, Assay Shibanda(kushoto) na John Yuccas wakimwekea mwanafunzi wa Shule ya Msingi Elbol,Levina Innocent mashine ya kuongeza kiwango cha usikivu kwenye Kliniki inayoendeshwa kwa pamojakati ya Montage Limited na taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation ya kuwawekea vifaa vya kuongeza usikivu inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana
8qMtaalamu wa matatizo ya usikivu kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani, Derek Johson akimfanyia uchunguzi wa awali wamasikio mmoja wa watu wenye usikivu hafifu waliokuja kuhudhuria Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana

9qMratibu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation kutoka Marekani, Derek Johnson akitoa maelezo ya awali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na chuo cha Biashara cha Arusha, (IAA) waliokuja kujitolea kutoa huduma mbalimbali ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwangocha usikivu masikioni kwenye Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jana. Kushoto ni Msimamizi Mkuu wazoezi hilo, Teddy Mapunda.
 1qMMOJA wa wataalamu wa kuchunguza matatizo ya masikio,Stuart Specer kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani inayoendesha kliniki ya masikio aakitaniana na mkazi wa Arusha,Ally Abdulrahman aliyewahi kuishi nchini humo ambaye kwa sasa ana matatizo ya kusikia kwenye kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo PalaceJijini Arusha jana

CAREER AFRICA YAFANA NEW YORK ZAIDI YA WANADIASPORA 400 WAJITOKEZA

$
0
0
Sophia Yona mwanadiaspora wa New York akiuliza jambo kwa mwakilishi wa Exim Bank Bwn. Dinesh Arora kwenye Career Africa iliyofanyika jiji lisilo lala New York City ndani ya hotel ya Hilton iliyopo mtaa wa 1335 avenue of America, New York New York 10019 na wanaDiaspora takribani 400 walijitokeza kwenye Careear Africa hiyo iliyokua imeandaliwa na baadhi ya wana Diaspora wa New York na New Jersey kwa kushirikiana na makampuni makubwa yanayofanya shughuli zake Afrika yaliyofanya kongamano hilo kwa ajili ya kuwatafuta wanaDiaspora wa Marekani wanaopendelea kufanyakakazi kwenye makampuni yao. Makampuni yaliyoleta wawakilishi  ni AXA insurance, Exim bank, national Microfinance Bank (NMB). OCP group, PZ Cussons, Safaricom na Tollow Oil.
Bi. Rokyaya Mane (kulia) mwakilishi wa National Micfofinance Bank (NMB) akitoa maelezo kwa wanaDiaspora waliohudhuria kongamano hilo lililoandaliwa maalum kutafuta wanaDiaspora wanaopendelea kuajiliwa na makampuni hayo Kongamano la Career Africa lililofanyika kuanzia Ijumaa Novemba 7-9, 2014 jijini New York City.
Bwn. Alaoui Banachem (kulia0 mwakilishi kutoka OCP Group akitoa maelezo kwa mwanaDiaspora huku akijaribu kuinadi kampuni yake kwa madau.
WanaDiaspora waliohudhuria kongamano la Career Africa wakibadilishana mawasiliano.
Kushoto ni Bwn. Frederick Kanga mwakilishi kutoka Exim Bank akisalimiana na mwanaDiaspora aliyetembelea meza hiyo kujaribu kupata mawili matatu.
WanaDiaspora wakipata mawasiliano na kuuliza maswali kwa makampuni yaliohudhuria Career Africa jijini New York. 

kwa picha zaidi Bofya Hapa

MWANAMUZIKI MKONGWE WA TWANGA PEPETA,AMIGOLAS AZIKWA MAKUBURI YA KISUTU JIJINI DAR LEO

$
0
0


Waombolezaji wakiuswalia mwili wa marehemu Hamis Zayumba, maarufu kama AMIGOLAS, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Jumatatu kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Amigolas ambaye alikuwa mtunzi na mwimbaji mashuhuri wa bvendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, alifariki Jumapili jijini.
Mwimbaji na mtuzni, Ali Choki, akiwa na uso wa huzuni wakati wa mazishi ya AMIGOLAS, ambaye kipindi gulani walikuwa bendi moja ya Twanga Pepeta
Waombolezaji wakiwemo wasanii maarufu, wakiwa kwenye mazishi.
Waombolezaji na wasanii wakiwemo wanamuziki wakiwa nyumbani kwa marehemu AMIGOLAS, kabla ya mzishi yake.PICHA KWA HISANI YA K-VIS BLOG

SWAHILI FASHON WEEK 2014 ON 5-7 DECEMBER

$
0
0
 SWAHILI FASHON WEEK 2014
For the SEVENTH year in a row, we are all set to bring you the best of the Designer Collection showcase from Tanzania and Beyond.

UPDATES:
Emerging Designers Competition on 5th December
AWARD NOMINEES to be announced soon
Tickets will be available for sale from 18th November
Open Model Casting on 22 November in Dar es Salaam
Shopping Festival booking - NOW OPEN
2nd Sunday POP UP SHOP - more info Coming Soon
5-7 December 2014
HOTEL SEA CLIFF
DAR ES SALAAM


CONTACTS:
General
+255757828832
Fashion+255785630007
Sponsorship+255787747918
Advertising: +255789954307
Shopping Festival:+255789954319
Follow us @swahilifashion

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Zaiko Langa Langa - Dede sur mesure

JK ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA AMIGOLAS WA TWANGA PEPETA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Profesa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kuomboleza kifo cha Mwanamuziki Muasisi wa Bendi Maarufu ya Twanga Pepeta, na baadaye Kiongozi wa Bendi ya Ruvu Star, Khamisi Kayumbu maarufu kama Amigolas (pichani).

“Nimehuzunishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha MwanamuzikiKhamisi Kayumbu kilichotokea tarehe 9 Novemba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.

 Rais Kikwete amesema anatambua mchango mkubwa wa Marehemu Amigolas, katika kuhamasisha maendeleo ya nchi yetu, kupitia sanaa ya muziki katika kuwafikishia wananchi ujumbe muhimu wa masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. Amesema kuwa Hayati Kayumbu alikuwa mfano  unaofaa kuigwa na Wasanii wengine  kote  nchini.

“Kutokana na msiba huu, naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa Wanamuziki Mahiri hapa nchini, na Rambirambi hizi ziwafikie pia Wanamuziki wengine kote nchini kwa kumpoteza mwenzao”.


Aidha, Rais Kikwete amemwomba Dkt. Fenella Mukangara kumfikishia Salamu zake za Pole kwa Familia ya Marehemu Khamisi Kayumbu kwa kupotelewa na Kiongozi na Mhimili madhubuti wa Familia.

Mwisho.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.


10 Novemba,2014

WAFANYAKAZI AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAHAMASISHA WATEJA KUFUNGUA AKAUNTI YA DHAMIRA.

$
0
0
Meneja Msaidizi wa Benki ya Azania Joseph Msase akikabidhi fomu ya Akaunti ya Dhamira kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo Benjamini Mengi.
Mteja wa Benki ya Azania Benjamini Mengi akionesha fomu yake baada ya kujiunga na Akaunti ya Dhamira ,wengine ni wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe(mwenye kilemba) na familia ya Mengi.
Mtoa huduma kwa wateja katika Benki ya Azania tawi la Moshi ,Happy Msengi akimshawishi Mama Mengi kufungua akaunti ya Dhamira iliyoanzishwa katika Benki hiyo.
Meneja Msaidizi Benki ya Azania Joseph Msese(katikati) akiwa na mtoa huduma kwa wateja Happy Msese wakijaribu kumshawishi kijana Benson Benjamini kufungua akaunti ya Dhamira.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe(kushoto) akiendelea kushawishi wateja wapya kujiunga na Akaunti ya Dhamira iliyoanzishwa katika benki hiyo.
Mtoa huduma kwa wateja katika benki ya Azania Mary Machange akiandika maelezo ya mteja  Benki Dowald Mushi alipokuwa akifungua Akaunti ya Dhamira katika tawi la Benki hiyo la Moshi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images