Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 632 | 633 | (Page 634) | 635 | 636 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Anitha Jonas, MAELEZO Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Profesa Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha viongozi kumi na moja aliyowateua, ambao ni Makatibu Wakuu wa Wizara ,Wakuu wa Mikoa,Mabalozi na Makatibu Tawala za Mikoa mbalimbali. Viongozi hao, waliapishwa leo jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. 
   Miongoni wa viongozi walioapishwa ni aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando, ambapo amesema katika swala la upungufu wa dawa mahospitalini atajitahidi katika bajeti ijayo kujenga hoja na kutetea manunuzi ya dawa. 
   “Serikali ina mpango mbadala wa utoaji wa vifaa vya afya kwani imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya afya ikiwemo kuangalia kuwepo na usawa wa gharama za huduma afya nchini,” alisema. Naye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba ameapishwa kuwa Katibu wa wizara amesema Wizara ya Maji imefanikiwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN) kwa kufikia 53% kutoka 40% katika kusambaza maji safi maeneo ya vijijini. 
   Aliongeza kwamba Serikali imefanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mitambo ya maji Ruvu chini na kujenga visima ili kuwawezesha wakazi wa jijini Dar es Salaam kupata maji ya kutosha. Aidha aliyekuwa Mtumishi Mwandamizi Ofisi ya Rais, Jack Mgendi Zoka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, ambapo ameahidi kwenda kuiwakilisha vyema Tanzania huko na kuisaidia nchi kupata fursa nyingi na kutafuta wahisani wa kuchangia maendeleo katika taifa. Viongozi wengine, waliapishwa ni Jonny Vianney Mongela ambaye ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
  Hapo awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, ambapo amesema anaamini ushirikiano mzuri atakaoupata kutoka kwa wananchi ndiyo utakao changia mafanikio makubwa katika mkoa huo,pia kwa kupita uzoefu wake na ataenda kusimamia yote yaliyokwisha kuanzishwa ili kuleta mafanikio zaidi. Naye Bi.Amina Juma Masenza ameapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa , amesema ataenda kuweka msisitizo wa vipao mbele vyote vya taifa katika mkoa wake na pia amesema anaamini kufanya kazi kwa ushirikiano ndio njia ya kuleta mafanikio makubwa katika mkoa huo. 
   Wengine waliaopishwa ni Mkuu wa Mkoa Mtwara Bi.Halima Omari Dendego, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga amesema changamoto kubwa katika mkoa wake ni kupandisha pato la mkazi wa Mtwara na kupitia miradi mbalimbali iliyopo mkoa huo ikiwemo gesi kupatikana kwa mafanikio, katika swala hilo pamoja kusimamia maswala ya elimu katika mkoa huo. 
  Aidha naye Samuel Shelukindo aliapishwa kuwa Balozi na kupewa wadhifa wa kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Kidiplomasia,alisema anamshukuru Rais kwa uteuzi huo na ameahidi kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa huku akingalia maslahi ya taifa kwa ujumla. Katika hafla hiyo Makatibu Tawala walioapishwa ni Addo Mapunda na Charles Amos Pallangyo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Samwel William Shelukindo kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais Masuala ya Diplomasia leo Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe Shelukindo anajaza  nafasi iliyoachwa wazi  na Balozi wa Tanzania nchini Marekani  Mhe Liberata Mulamula, na kabla ya hapo alikuwa Afisa mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya hapo Mhe Mongela alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Halima Omary Denengo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya hapo Mhe Denengo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kabla ya Hapo Mhe Msengi alikuwa mkuu wa wilaya ya Moshi
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha  Dkt Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014


  0 0
 • 11/06/14--19:00: ngoma aziepndazo ankal
 • DDC Mlimani Park - Shemeji Issa

  0 0

  World class Information Security training experts of Koening- Solutions, India (www.koenig-solutions.com) in collaboration with Auditec Consulting Company, Tanzanian local partners, welcome all information systems practitioners to attend this unique IT Security career opportunity.

  DATE:1st – 5th December 2014,
  TIMEFrom 0800 to 16OO Hrs 
  VENUENASHERA HOTEL, MOROGORO

  TARGET GROUPChief Information Officers/Heads of IT/Information Security officers
  Auditors/ System Administrators/ System Engineers
  Database Administrators/ Application Administrators
  Network Administrators/ Programmers
  MAJOR COURSE FOCUS
  Information Security  fundamentals, threats and vulnerabilities
  Network scanning and advance sniffing techniques
  System hacking and virus/Trojan/spyware attacks
  Computer and windows forensics investigation process
  AWARDCertificates of Attendance

  TRAINERS. S. Sandhu (CCNA, CEH, ECSA, EDRP, CHFI, CompTIA Security+ Certified)

  FEETshs. 1,500,000 to cover tea break, lunch, training materials, certificates and social gathering events.

  Deposit your fee (cash) to Auditec account number 0150237529000 CRDB Bank and send a scanned copy to Auditec through email or submit original pay in slip to Auditec offices.
  Cheques should be submitted to Auditec at least 1 week before training date.
  Please confirm your participation before November 21, 2014

  All enquiries should be addressed to:
  TRAINING COORDINATOR
  AUDITEC CONSULTING COMPANY
  PLOT 2478/5- OCEAN ROAD/OBAMA DRIVE
  P. O. BOX 34702, DAR ES SALAAM- TANZANIA,
  TEL: 0757 642389.
  EMAIL: info@auditec.co.tz; 

  DON’T MISS THIS CARRER CHANGING OPPORTUNITY!
  LEARN FROM THE BEST!

  0 0  0 0

  Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni Silvery 'Mpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu)
  Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

  Mac Reagan 'Kipara' na Mjuni Silvery 'Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.

  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  IMG_4111
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akitoa nasaha zake kwa jamii ya wafugaji wa wilaya ya Longido mkoani Arusha alipofanya ziara ya siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
  IMG_4075
  Baadhi ya wakazi wa Longido ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
  IMG_4121
  IMG_4077
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akivishwa zawadi ya shuka la kimasai na mmoja wa wafugaji wa wilaya hiyo.
  IMG_4088
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisikiliza maelezo ya zawadi  za asali za Nyuki wadogo na wakubwa kutoka kwa jamii za wafugaji wanaofadhiliwa na shirika la UNDP wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani humo.

  0 0

  The government of the French Republic has accredited its Ambassador to the United Republic of Tanzania, Ms. Malika Berak, to also serve as Ambassador to the East African Community. 
  Her Excellency Malika Berak today presented her accreditation letter dated 9th October 2014 and signed by the Minister of Foreign Affairs and International Development, Hon. Laurent Fabius, to the Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera.
  Amb. Berak informed the Secretary General that her government attaches great importance to regional economic groupings such as the EAC and congratulated the founders of the wonderful regional initiative. 
  “Count on France’s support because the goals of the Community are excellent for the prosperity of the people in the region”, asserted the French Envoy, adding that “regional integration initiatives take time but you need to continue so as to build a strong and powerful bloc”.
  While receiving the French Envoy, the Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera hailed the existing cordial relations between the EAC and France. 
  He said the region was building a firm base to provide space to the over 140 million East Africans to improve the quality of their lives through increased competitiveness, value added production, trade and investments. “Our aim is to fight poverty and establish prosperity and live in permanent peace, not conflict”, noted Amb. Sezibera. 
  The Secretary General welcomed the support from French Government geared towards enabling the Community to achieve its ambitious agenda. He urged the French Government to consider supporting the EAC in three main areas namely; joining and contributing to the EAC Partnership Fund; encouraging the Agence Française de Développement (FrenchDevelopment Agency) to enter into partnership with the East African Development Bank; and lastly to support the EAC in its Energy programmes, especially the Renewable energy.
   Her Excellency Malika Berak presents the letter accrediting to serve to the East African Community to the EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera.

  EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera presents a gift to Amb.Malika Berak
   

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Bw. Witold Karczewski (kulia) ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Mlynpol ya Poland ambayo ina nia ya kujenga maghala ya kisasa ya kuhifadhi nafaka katika kanda hapa nchini wakati alipokagua maghala ya SGR mjini Dodoma Novemba 6, 2014
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana  na Bw. Witold Karczewski (kulia) ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Mlynpol ya Poland ambayo ina nia ya kujenga maghala ya kisasa ya kuhifadhi nafaka katika kanda hapa nchini wakati alipokagua maghala ya SGR mjini Dodoma Novemba 6, 2014. 

  Picha na na habari 
  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekagua maghala ya kuhifadhia chakula yaliyopo Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Alhamisi iliyopita kwamba Serikali inalenga kujenga maghala kwenye mikoa sita kupitia mkopo ambao itaupata kutoka Serikali ya Poland.

  Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo asubuhi (Alhamisi, Novemba 6, 2014) wakati akikagua maghala hayo, Waziri Mkuu alisema katika mkoa huo, Serikali ina nia ya kujenga maghala makubwa (SILOS) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 100,000 za nafaka kwa wakati mmoja.

  “Tukipata maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 100,000 tutakuwa na uhakika wa kuchukua na akiba ya nafaka kutoka mikoa ya jirani ya Singida, Tabora na Manyara,” alisema. 
  Waziri Mkuu alifuatana na Bw. WITOLD KARCZEWSKI ambaye ni mmiliki wa kiwanda kikubwa cha kusindika nafaka nchini Poland ambacho Waziri Mkuu Pinda alikitembelea alipozuru nchi hiyo Oktoba 24, mwaka huu. Bw. KARCZEWSKI anamiliki pia kiwanda kinachotengeneza malighafi za kujengea SILOS. 
  Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kituo cha NFRA Kanda ya Kati, Bw. Ruwaichi Mambali alisema kituo hicho kina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 30,000 lakini kwa sasa kina tani 69,000 ambazo kati ya hizo tani 62,000 zipo Kizota (Dodoma) na tani 7,000 ziko Manyoni (Singida).

  Alisema eneo zima la Kizota lina ukubwa ekari 33 na kwamba kuna maghala matatu yenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 kila moja. “Lakini kwa sasa tumelazimika kuweka mahindi mengine na mtama hapa nje ambayo tumeyafunika kwa maturubali,” alisema. 
  Kwa upande wake, Bw. KARCZEWSKI alitaka kufahamu miundombinu iliyopo kwenye ghala la Kiszota ikiwemo umabli wa kutoka barabara kuu pamoja na reli. Pia alitaka kujua eneo zima lina ukubwa kiasi gani. Na alitaka kufahamu mbinu zinazotumika hivi sasa kuhifadhi chakula kwenye ghala hilo. 
  Alisema wakipata michoro ya eneo hilo (site map), atatuma wataalamu wake Januari mwakani waangalie uwezekano wa kuanza ujenzi mapema iwezekanavyo pindi mazungumzo yakikamilika. 
  Alhamisi iliyopita, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere akitokea Oman, Waziri Mkuu alisema alikwenda Poland kutafuta msaada wa mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu ambao utasaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala  kwa ajili ya kuhifadhia nafaka.

  Alisema Serikali imelenga mikoa sita ya kuanzia ambayo ni Ruvuma, Rukwa, Njombe (pamoja na Iringa) ambako kuna uzalishaji mkubwa wa mahindi. Pia inaangalia Kanda ya Ziwa ambako mara nyingi wana uhaba wa chakula; na kwamba itaweka maghala mkoani Dodoma kwa sababu ni katikati ya nchi ili ikusanye akiba kutoka mikoa ya jirani ya Singida, Manyara na Tabora. 
  “Lengo ni kupata uwezo wa kuhifadhi tani 700,000 hadi 1,000,000 na ujenzi wao siyo kama huu wa kwetu. Tumewaomba watujengee SILOS (maghala makubwa) kwa sababu zina teknolojia ya kujua kiasi gani cha nafaka kimeingia, zina unyevu kiasi gani, unaweza kuweka dawa nafaka zako, kuosha na kukausha na kisha ukasindika kwa kiwango unachotaka,” Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi wa habari. 
  Alisema uzalishaji mwaka huu umetoa ziada ya tani milioni 1.5 za nafaka na tani 800,000 za mpunga ikilinganishwa na ziada ya tani 300,000 iliyokuwepo mwaka jana. “Serikali inakabiliwa na changamoto ya kupata soko la uhakika kwa mazao ya wakulima kwa sababu tulizoea kumtumia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kama mnununzi mkuu na uwezo wezo wake ni tani 240,000 tu kwa mwaka,” alisema.

  0 0

  GU9A7961
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge akisamiana na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD kutoka nchi wadau Dk Chea Sam Ang kutoka Cambodia Naibu Mkurugenzi Mkuu kitengo cha Misitu wizara ya kilimo, Misitu na Uvuvi.
  GU9A8136
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge.

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha UPDP na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba Mh. Fahmi Dovutwa akitoa taarifa ya ushirikiano wa Vyama sita vya siasa visivyokuwa na wambunge katika uchaguzi wa Serkali za Mitaa, Wabunge na Rais unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu mpaka mwaka 2015 ambapo uchaguzi wa Wabunge na Rais utafanyika.

   Mhe Dovutwa amesema vyama hivyo vimeamua kushirikiana kwa sababu vipo vyama vilivyounda kundi lisilokuwa la kisheria linaitwa Ukawa, lakini  hakuna sheria inayoturuhusu kuunganisha vyama ila tunaweza kushirikiana tu ndiyo maana tunasema tumekubaliana kushirikiana”. vyama vilivyokubaliana kushirikiana ni SAUT, DEMOKRASIA MAKINI, JAHAZI ASILIA, UMD, UMD, UPDP NA AFP ,  Katika picha wanaofuatia ni Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Rashid Lai Katibu Mkuu AFP na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
   Rashid Lai Katibu Mkuu AFP akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Sinza jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha SAUT  Yusuf Manyanga , Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa na Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini
  Mwenyekiti wa Chama cha SAUT  Mhe Yusuf Manyanga  akifungua mkutano huo kabla ya Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa kutoa tamko.

  0 0


  0 0

  MIFUKO ya hifadhi ya Jamii ya NSSF na PSPF imejitokeza kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania ambazo zitafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP), Dar es Salaam, zikiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
  Udhamini wa PSPF katika tuzo hizo ni Sh. Milioni tano, wakati NSSF imetoa Sh. Milioni mbili, hivyo kufanya fedha taslimu ambazo hadi sasa TASWA imepata kufikia Sh. Milioni 37. 
  Wadhamini wengine ni Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group Limited iliyotoa Sh. Milioni 10 na Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL iliyotoa Sh milioni 20. 
  Uongozi wa TASWA unaendelea na mazungumzo na kampuni mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo, ambapo licha ya walioahidi kutoa fedha taslimu, lakini wapo wengine tunaendelea kuzungumza nao kwa ajili ya kudhamini kwa njia ya huduma zinazoambatana na tuzo hizo. 
  Ni imani ya TASWA kwamba hadi kufikia Novemba 20 mwaka huu kampuni na wadau mbalimbali walioahidi kutusaidia watakuwa wametekeleza ahadi zao kulingana na mazungumzo tuliyofanya nao, hivyo kuwatangaza rasmi.
   Wanamichezo zaidi ya 100 wanatarajiwa kuwania tuzo kwa michezo mbalimbali, ambapo Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora wa TASWA, inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujiridhisha kwa mara ya mwisho orodha ya mapendekezo ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali vya michezo kwa ajili ya kuwania tuzo hizo.
  MEDIA DAY BONAZA
  TASWA kila mwaka inaandaa bonanza la vyombo vya habari linalojulikana kama Media Day Bonanza, ambalo hushirikisha wadau mbalimbali kutoka vyombo vya habari. 
  Lengo la bonanza hilo ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja. 
  Lakini  mwaka huu bonanza hilo limechelewa kutokana na na suala la wadhamini ambao awali TASWA ilikubaliana nao, lakini baadaye walisema wamepata matatizo ya kifedha. 
  Hata hivyo kutokana na umuhimu wa bonanza hilo, uongozi wa TASWA umezungumza na wadau wengine na mazungumzo hayo yanaendelea ili Media Day Bonanza ifanyike mwezi ujao likiwa ni maalum kwa ajili ya kufunga mwaka 2014. 
  Tunajua maswali kuhusu Media Day yamekuwa mengi pengine kuliko majibu, pia wasiwasi kwa baadhi yenu ni mkubwa kuliko uhakika, lakini tunawahakikishia mambo yanaenda vizuri na ni imani yetu yanakaribia kuiva. 
  Kwa hili la Media Day, tuliona ni bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama tuendako. Tutambae, lakini macho njiani na mbele tunakoelekea na hiyo ndiyo dhamira yetu.
  Ahsanteni,

  Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA
  07/11/2014

  0 0


  When: 07th November 2014

  Where: ESCAPE ONE
  Time: 10pm Till late tulivu ( Saa NNE usiku na kuendelea)
  Live band by DAMIAN SOUL together with his friends from all over the WORLD.
  Lots of surprise guests to be featured on.
  Don't afford to miss this LAUNCHING in the coming Friday...There also gonna be HIP HOP, JAZZ, SOUL & AFRO FUSSION...All LIVE with the Band
  Y'ALL WELCOME

  Damage 10K (10,000) 

  0 0
 • 11/07/14--00:03: GADO LEO


 • 0 0

   Valerian Luzangi (kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo  ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.
   Valerian Luzangi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo ya kuoshea mbwa ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.
   Mmoja wa wafanyakazi walioajiriwa na kiwanda hicho akiweka maji kwenye pipa tayari kuchanganywa na dawa wakati wa kutengeza shampuu.

  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limeuda kamati ya pamoja baina ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo na maafisa wa Jeshi hilo ili kuwa na utaratibu sahihi wa kushughulikia kero za uhalifu miongoni mwa wafanyabiashara wazalendo na wageni zinazojitokeza katika soko hilo. 

  Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kamati hiyo alipokuwa akijibu hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na baadhi ya wafanyabiashara wa sokoni hapo juu ya baadhi ya kero zinazowakabili  katika mkutano na wafanyabiashara hao uliofanyika katika mtaa wa Kongo na Mchikichini jijini Dar es Salaam jana.

  Kamati hiyo itawahusisha maafisa wa Polisi na baadhi ya wafanyabiashara na itaongozwa na Naibu Kamishna wa Polisi SIMON SIRRO kama mwenyekiti. Kaimu Mwenyekiti ni bwana JONSON MINJA ambaye pia ni kiongozi wa wafanyabiashara huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mary Nzuki atakuwa mjumbe maalum wa kamati hiyo pamoja na wajumbe wengine. 

  Awali katika mkutano huo baadhi ya wafanyabiashara walipata fursa ya kutoa dukuduku/kero zanazowakabiri ili zipatiwe ufumbuzi. Baadhi ya kero zilizoianishwa ni pamoja na Kituo cha Polisi Msimbazi kugeuzwa sehemu ya kukusanyia mapato; kutokuwepo na huduma bora kwa mteja toka askari polisi; n.k.

   Mmoja wa wafanyabiashara HUMFREY SAMBO alihoji uhalali wa mgambo wa jijini kufanya kazi zao bila kufuata sheria za nchi na serikali haichukui hatua? Huku weginne wakitaka wahalifu sugu wanaojulikana kama “KAPERO” wakamatwe kwani wamekuwa kero kwa wafanyabiashara na wateja.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara bwana JONSON MINJA amesema hakuna mfanyabiashara asiyependa kulipa kodi bali ameomba pawe na mfumo shirikishi utakaosaidia kuleta uelewa wa pamoja kwa maslahi ya wafanyabiashara na uchumi wa nchi kwa jumla. Pia ameiomba serikali ione sasa kuwa ni muda muafaka kwa wafanyabiashara wazawa kupewa fursa za kuwekeza nchini hasa katika miradi mikubwa ya kiuchumi ili kujenga uchumi imara wa nchi na kukuza uzalendo miongoni mwa watanzania ambao kwa sasa ni kama haupo.

  Akijibu hoja mbalimbali toka kwa wafanyabiashara hao Kamishna Kova amesema mbali na kuunda kamati tajwa pia ametoa maagizo yafuatayo:

  Kituo cha Polisi Msimbazi kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na si kituo cha kukusanya kodi/ushuru. 

  Kikundi cha Polisi jamii kinacholalamikiwa kimevunjwa na kitaundwa kingine kinachohusisha watu makini watakaopatiwa mafunzo ya kuifanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu.

  Kushauriana na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam kuona namna ya kuboresha huduma inayotolewa na askari wa jiji kwa kushirikisha Polisi ili iwe ni yenye tija na inayofuata sheria za nchi kuliko ilivyo sasa.

  Pia nawataka vibaka maarufu kama KAPERO kujisalimisha wenyewe vinginevyo watasakwa kwa namna yoyote ile mpaka wapatikane na hatua zichukuliwe dhidi yao. Nia ni kuwafanya wafanyabiashara wa ndani na nje kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu 
  Aidha, nawaasa wafanyabiashara kuacha mtindo wa kubeba pesa nyingi kiholela kwa sababu ni hatari kwa maisha yao hasa katika kipindi hiki kinachotawaliwa na utandawazi na badala yake watumie mifumo ya kisasa ya kibenki ya usafirishaji fedha ikiwa ni pamoja na kuomba eskoti toka Jeshi la Polisi. 

  Mwisho nawataka watanzania kuacha mtindo wa kujichukulia sheria mikononi kwa sababu tabia hii imekuwa ikikatisha maisha ya watu ilihali sheria za haki za binadamu zinakiukwa jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo. Ni vema kuachia vyombo husika vikasimamia sheria kwa wale wanaokiuka sheria hizo kuliko kujichukulia sheria mikononi.


  0 0

  SAM_1076
  Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Bw. Allan Kijazi (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha.

  0 0

  Contact specialists Jossekazi Auto Garage & General Supply located at Kinondoni, Dar es salaam  behind Best bite.
   Call 0718-437828 or  0765-743122.
  We also sell spare parts and diagnosis machines.
  Visit TEAM TZ at:
   http://teamtz.com/?xg_source=msg_mes_network

  0 0

    On 3 November, a delegation of three Air Force Officers from the Tanzania Peoples’ Defence Forces (TPDF), headed by Colonel R K Kapinga, arrived in the Seychelles for an official two day visit to the Seychelles Air Force (SAF). The purpose of the visit was to explore the air surveillance capability of the SAF that has been developed in the past year in close cooperation with EUCAP Nestor.

  Technical briefing on capabilities of air crafts and surveillance systems

   

  The official visit started on 4 November when Colonel Kapinga and his delegation met with the Chief of Seychelles Peoples’ Defence Forces (SPDF) Brigadier-General Payet at the SPDF Headquarters. Colonel Kapinga expressed his appreciation for this cooperative and collegiate approach which will greatly assist the future Tanzanian Air Surveillance Capabilities.


  Meeting at SPDF HQ with TZ Delegation and CO-SPDF Brigadier Payette
  “We do not yet have any air surveillance capability like this in Tanzania, hence the importance to come here to the Seychelles and see the capability of the surveillance systems and learn from the experience gained within SAF in terms of air surveillance operations, technical systems and the training of personnel to become professional in Air Surveillance operations. Air Surveillance will not only help us for maritime purposes but also to assist in border monitoring and to support combatting poaching of wildlife. It will allow us to make recommendations for implementing air surveillance capabilities in Tanzania.” said Colonel R K Kapinga. 


  The delegation has followed a comprehensive programme with SAF initially receiving various briefings on air surveillance operations, technical systems, training courses and experience gained during operations conducted by SAF. Among others: air patrolling, counter-piracy, search and rescue, medical evacuation and VIP transport as tasked by various national agencies.

  The visiting officers also participated in an “operational” flight to see first-hand the capability of the surveillance systems and processes linking the air-patrolling with mission preparation, in-flight reporting, mission debriefing, reporting and analysis of information and imagery by the SAF imagery and intelligence section.


  “I am glad to welcome our colleagues from Tanzania here. It is the very first time that we are exchanging on this subject and I am glad to share the experience we gained over the years with regard to air operations with them. They will take valuable information and key knowledge back home. I hope that we will have many more occasions in the future to exchange and that we can further support them in establishing air operations” said Capt. R. Zarine, adjutant at SAF.


  “This is the first time that two countries within the mandated area of EUCAP Nestor engage in knowledge-sharing on development of air surveillance capabilities and I am proud to say that it is done on the initiative of EUCAP Nestor” said Bo Holtse, EUCAP Nestor’s Head of Country Office in the Seychelles. “The enthusiasm by both Air Forces is proving just how vital it is to form regional links, to share information and experiences by regional counterparts. This visit reflects the regional engagement of EUCAP Nestor. Assisting the sustainable development of capabilities and facilitating of the transfer of knowledge between countries of the region is in the core of its mandate.

  Group photo; TZ Delegation and 2IC SAF, Capt. Zarine and EUCAP Nestor ASE Bjorn Erlandsson
  This Furthermore demonstrates the professionalism and commitment by SAF developing this capability to a high standard and willingness to share such knowledge and experience with their Tanzanian counterparts” said Bo Holtse, EUCAP Nestor’s Head of Country Office in the Seychelles. 


  0 0older | 1 | .... | 632 | 633 | (Page 634) | 635 | 636 | .... | 3285 | newer