Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

MARA FOUNDATION YAJIDHATITI KUIBUA VIJANA WAJASIRIAMALI WATAKAOSAIDIA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA

$
0
0
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi akisikiliza mawazo ya mmoja wa vijana wajasiriamali mwenye nia ya kukataka kukuza biashara yake na kuifanya kuwa endelevu wakati wa uzinduzi wa Mara Foundation ambao uliotoa fursa ya washiriki kuzungumza na wafanyabiashara waliopiga hatua na wenye uzoefu katika kuendesha biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga akimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye ni mjasiriamali anayechipukia aliyetaka kupata uzoefu na mawazo zaidi jinsi ya kuendesha biashara yake.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali akimsikiliza mjasiriamali mdogo mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa.
Ma-Mentors waliokuja kuzungumza na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara na kuwaongoza kufikia malengo yao.
Taasisi ya Mara Foundation ilianzishwa na Ashish Thakkar ambaye ndie mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Mara Group.
Ashish alitumia muda wake mwingi katika kutimiza malengo ya Taasisi hiyo kwa kuwa alikuwa na imani na wajasiriamali na kuendeleza biashara ndogo.
Tangu mwaka 2009 Taasisi hiyo ililenga mtazamo wake na imefanya vizuri sana nchini Uganda, Tanzania, Kenya na Nigeria katika muelekeo huo.
Kuanzia mwaka 2013 mikakati ya taasisi ya Mara Foundation inaendelea kukua katika nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara huku ikiendelea kuongeza wigo wake katika nchi nyingine duniani.
Mara Foundation inafanya kazi ya kubuni na kukuza uchumi endelevu na kufungua fursa endelevu kwa vijana wamiliki wa biashara za kati kwa kupitia vituo vya uwezeshaji vya Mara Launchpad na Mara Launch Fund.
Pichani juu na chini ni Washiriki na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kabla ya mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu kuzindua Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Tanzania Nina Werner (kulia) akizungumza machache kuhusiana na malengo ya Taasisi yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Dkt. Mary Nagu kuizindua rasmi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akizungumza wakati kuzindua taasisi ya Mara Foundation ambapo amewataka vijana wajasiriamali kutumia fursa ya taasisi hiyo kujijenga kibiashara
Taasisi ya Mara Foundation yenye makao yake makuu jijini Dubai sasa imejikita katika nchi za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Kenya na Nigenia kwa lengo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuwezeshwa kimuongozo na kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza kutoa ajira kwa watu wengine.
Washiriki na wageni waalikwa wakifurahi jambo wakati mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu akitoa risala kwenye uzinduzi wa Taasisi ya Mara uliofanyika hivi karibuni kwenye jengo la Mayfair Plaza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akikata utepe kuzindua rasmi taasisi hiyo yenye matawi 28 barani Afrika. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Nina Werner.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Wageni waalikwa wakishangilia kwa makofi.
MC wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Problem Solved Eric Mutta akimkabidhisha Mjasiriamali mdogo Peter Christopher kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (katikati) atakayekuwa mshauri wake wa kibiashara kwa muda wa miezi sita ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali (katikati) akimpokea mmoja wa wajasiriamali waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation kwa lengo la kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga (kushoto) akipata picha ya ukumbusho na kijana aliyemchagua kumsaidia kimawazo na kumwongoza kwa muda wa miezi sita ijayo mpaka kufikia lengo lake.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation uliofanyika hivi karibuni Mayfair Plaza.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) na Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mara Foundation.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha (kulia) na Mkurugenzi wa man Magazine Dismas Massawe (katikati) katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mara Foundation.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI

WAFANYABIASHARA WA KITIMOTO IRINGA WAPINGA KUFUNGIWA BIASHARA

$
0
0

 Wafanyabiashara  wa kitimoto  mjini Iringa  wakionyesha  milango yao  iliyofungwa na mgambo  leo kama njia ya kupinga  uuzaji  wa nyama ya nguruwe (kitimoto)
 Hapa wakiamua  kuchimba barabara  kuzuia  magari kupita eneo hilo 
 Maandamano ya  kupinga  marufuku ya uuzaji  wa kitimoto leo 
 

Na Francis Godwin
Wafanyabiashara  wa  kitimoto katika  eneo la vibanda  vya UVCCM mjini  Iringa  leo wamewatimua mgambo  wa Manispaa ya Iringa ambao  wamefika eneo hilo kufunga biashara  zao kama  njia ya kunusuru wananchi na ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Tukio hilo  limetokea leo  majira  ya  saa 12 jioni baada ya  ofisa mifungo  Manispaa ya Iringa  akiwa na mgambo kufika   eneo hilo  kufunga   biashara  zote za kitimoto eneo hilo.

Wakizungumzia hatua  hiyo  wafanyabiashara  hao  wamesema  kuwa wanashangazwa na uamuzi huo  wa  uongozi  wa afya Manispaa ya iringa  kuwazuia  wao kufanyabiashara  hiyo  wakati maeneo mbali mbali maarufu  nyama  hiyo ikiendelea  kuuzwa kama kawaida .

Hivyo  wameutaka  uongozi  wa Manispaa ya  Iringa  kusitisha mpango huo  kwani  unawatesa wananchi hao  wajasiriamali  wenye kipato cha chini ambao  wanategemea biashara  hiyo.

katika hatua nyingine  wafanyabishara  hao  na  wateja  wao  wamewatimua  mgambo hao na ofisa mifugo  huyo katika  eneo hilo kwa madai  muda  waliokuwa wakifanya kazi ni muda ambao si wa kazi na  kudai kuwa  wanatumiwa na  wafanyabiashara wakubwa .

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN MJINI MAGHARIBI

$
0
0

 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wazee wa Chumbuni  Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi, alipofungua kituo cha Mafunzo ya Kazi za Amali,akiwa katika ziara Mkoa huo,(kulia) Naibu waziri wa Ulinzi Perera Ame Silima,na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abadallah Mwinyi Khamis,na (kushoto)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame 
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea risala ya kituo cha kituo cha Mafunzo ya Kazi za Amali,Chumbuni Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi, kutoka kwa Katibu wa Chuo Iddi Sheha Makame,alipokizindua kituo hicho akiwa katika ziara Mkoa huo
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Hassan Ali Mbarouk,(kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza leo.


Waziri Mkuu wa Denmark Awasili Tanzania, alakiwa kwa shangwe

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt muda mfupi baaday kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt wakipokea heshima za nyimbo za Taifa pamoja na saluti ya mizinga 21  katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt na mwenyeji wake wakifurahia burudani mbalimbali
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akipkea shada l maua
Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akisalimiana na kinamama waliofurika uwanjani kumlaki. Picha na Freddy Maro

WAZIRI MKUU WA DENMARK APOKELEWA KWA SHANGWE IKULU LEO

$
0
0
Chereko Chereko wakati wa kumpokea Waziri Mkuu wa Denmark Ikulu jijini Dar es salaam leo

bei ya madafu

RAIS KIKWETE AMKARIBISHA WAZIRI MKUU WA DENMARK IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0

Mamia ya wananchi wakijiandaa kumlaki Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt kupitia lango la Mashariki la Ikulu Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt  Ikulu Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt wakiingia Ikulu huku wakishangiliwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika maongezi ya faragha na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt leo Ikulu.


Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalon Kibanda apelekwa Afrika Kusini kwa Matibabu zaidi

$
0
0
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd,Absalon Kibanda akipakiwa kwenye ndege ya Kampuni ya Flightlink tayari kwa safari ya kwenda nchini Afrika Kusini kwa Matibabu baada ya kuvamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya,alipokuwa akirudi nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink.
Absalom Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella
Semaya, tayari kuanza safari ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu.
Baadhi ya waandishi na viongozi wa jukwaa la wahariri wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa ajili ya kumjulia hali.
Absalom Kibanda akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kusafirishwa kwenda Afrika ya kusini.




hebu shangaa hii kidogo kama vipi.

neno la leo: Maskini hana Kinyongo

msama promotions yawataja wasanii watakaotumbuiza tamasha la pasaka .

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka kutoka Kampuni ya Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) ,mapema leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa tamasha la pasaka na kuwataja wasanii mbalimbali watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambalo limekuwa liwavutia wengi,ambapo mwaka huu limebeba ujumbe wa kuhimiza suala la amani na utulivu katika nchi yetu,tamasha hilo linatarajia kufanyika Machi 31 ndani ya uwanja wa Taifa na baadae kufanyika kwenye mikoa mingine kama vile Mbeya,Dodoma,Mwanza na Iringa.Kumsikiliza zaidi bofya video hapa chini.

UCHAGUZI MKUU WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MOROGORO WAFANYIKA VYEMA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro ( MOROPC), Wilson Karuwesa , ambaye pia ni Mwanachama wa Klabu hiyo ,ambapo ( mwenye kapero) ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Stephen Mashishanga , ambaye ni mlezi wa MoroPC , na ( wapili kulia) ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa huo, Boniventre Mtalimbo, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo , Machi 2, mwaka huu mjini hapa, hata hivyo wanachama walimchagua Mwandishi na Mtangazai wa ITV , Idda Mushi kuwa Mwenyekiti mpya kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro, Thadei Hafigwa akishikilia kasha ambalo ndani yake zimehifadhiwa simu za wagombea wa uongozi wa MOROPC wakati wa kusehabu kura.
Baadhi ya waandishi wa habari wa Klabu ya Mkoa wa Morogoro wakibadilishana mawazo baada ya upigaji kura wa kuchangua viongozi wa Klabu hiyo.
Mwenyekiti mpya wa MOROPC ,Idda Mushi ( kulia) akiwa na Mwenyekiti za muda aliyemaliza muda wake , Boniventure Mtalimbo ( wapili toka kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wachaguliwa.

DK. SHEIN ZIARANI WILAYANI MAGHARIBI,ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kulifungua Soko la Samaki Mazizini pwani,ikiwa ni mradi wa Tasaf alipokua katika ziara ya Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Tasaf Unguja Shaaban Ali Abdulmalik,wakati alipofungua Soko la Samaki la Mazizini Pwani, ikiwa ni mradi wa Tasaf kupitia Macemp,alkiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Rans CO LTD,inayoshuhukia ujenzi Nassor Salim Said,alipotembelea Kilimo cha Mboga mboga kinacholimwa na kampuni hiyo huko Kombeni Wilaya ya Magharibi alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Magharibi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

JIFUNZE KUTENGENEZA NYAMA SAFI LAINI YA KUKAANGA NA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI


BODI YA UTALII TANZANIA KUWANOA WASHIRIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13

$
0
0
Wakati maandalizi ya Fainali za Taifa za kumpata Miss Utalii Tanzania 2012/13 yakiwa yanaendelea kwa kasi kubwa, Bodi ya Utalii Tanzania itaendesha Semina Maalum ya Mafunzo ya Utalii kwa washiriki wote walioko kambini Ikondolo Lodge Kibamba wakijiandaa na Fainali za Taifa zitakazo fanyika Mwishoni mwa wiki ijayo Jijini Dae es salaam. 

Akithibitisha taarifa hizo kwa waandishi wa Habari Raisi wa Kamati ya Mashindano hayo Erasto G. Chipungahelo alisema kuwa Semina hiyo maalum itakayo endeshwa na Bodi yaUtalii Tanzania itafanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Utalii uliyopo katika ofisi za Bodi ya Utalii jengo la IPS Dar es salaam siku ya Alhamisi Tarehe 7.03.2013 kuanzia saa Tatu asubuhi na kuwashirikisha zaidi ya Warembo 40 wakiwakirisha Mikoa yote ya Tanzania Bara , Kanda maalum za Vyuo vikuu na Zanzibar. 

 Watoa mada wakuu katika semina hiyo, itakuwa ni wataalam walio bobea katika secta ya utalii na masoko ya utalii kutoka Bodi ya Taifa ya Utalii(Tanzania Tourist Board). Kwa niaba na kamati ya Miss Utalii Tanzania, Ninatoa shukurani za pekee kwa Serikali na Bodi nzima ya Utalii kwa kuendesha semina hii muhimu kwa washiriki wa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania ambapo washindi wa kwanza mpaka wa Tano watawakirisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya utalii ya Dunia. Yakiwemo ya Miss Tourism World, International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation World , Miss Tourism university World na Miss Heritage World yatakayo fanyika katika nchi mbalimbali kuanzia mwezi wa nne mwaka huu. 

 Hii ni fursa  pekee kwa washiriki na washindi watakaopatikana katika fainali za Taifa kuweza kujua na kujifunza juu ya utalii Tanzania, mbinu na mikakati ya kutangaza vivutio vya kitalii kitaifa na kimataifa, hivyo kutusaidia kutimiza ndoto na malengo yetu ya miaka mitano ya kutwaa Mataji matatu ya Dunia mwaka 2013. 

 Maandalizi katika kambi ya warembo yanaendelea vizuri , ushindani ni mkubwa ari na dhamira ya kila Mrembo kulinda hadhi na Heshima ya Mkoa wake kwa kutwaa taji la Taifa ni kubwa.

Chipungahelo aliongeza kwamba, ili kuthibitisha hayo, anaomba watanzania wote wakazi wa Dar es salaam na Mikoa ya Jirani, wajitokeze kwa wingi siku ya ya Jumamosi Tar 9.03.2013 usiku katika ukumbi wa Dar Live Mbagala kushuhudia warembo hawa wakipanda jukwaani kuwania Tuzo mbalimbali za Vipaji na Utamaduni. 

Mbali na kupita jukwaani na mavazi mbalimbali washiriki wote pia watashindana kucheza na kuimba nyimbo za Asili za Mikoa wanayo wakilisha. Na hili litakuwa ni tukio la kihistoria la Utalii, Urembo na Utamaduni kuwahi kufanyika hapa Tanzania kabla na Baada ya Uhuru. 

 Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA ) 
www.misstourismorganisation.blogspot.com 

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 201213 wakitoa Burudani ya Nguvu katika Jukwaa la Sanaa (BASATA
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012-13 wakiwa katika mazoezi ya Nguvu ndani ya ukumbi wa Dar Live
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012-13 wakiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Mtwana Catering Service ambaye ndiye anaye walisha Warembo hao.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa Katika Picha ya Pamoja Baada ya kumaliza Mazoezi yao Katika Ukumbi wa Dar Live

Article 13

mwanamuziki mkongwe kabeya badu katutoka

$
0
0
Picture
Mwanamuziki wa siku nyingi Kabeya Badu (pichani), ambaye alikuwa anaimba katika bendi za Wazee Sugu amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Tafia ya Muhimbili jijini Dar es salaam.


Marehemu alikuwa akisumbuliwa na figo ambazo zilishindwa kufanya kaiz.



Wakati wa uhai wake, Kabyea aliwahi kufanya kazi na bendi nyingi zikiwemo za Orchestra Fauvetter, Orchestra Safari Sound, Marquis, Intimate Rhumba, Tancut Almasi na Wazee Sugu



Mola ampumzishe Mahala pema Peponi - Amina

Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwanamuziki, John Kitime.

Video chini ikimuonesha marehemu Kabeya Badu (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Wazee Sugu ukumbi wa La Prima jijini Dar.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Odyssey walipoibuka na ngoma ya 'Going Back To My Roots' walitesa sana

WATOTO WANAWEZA KUTUFUNDISHA KUIENZI AMANI KUPITIA MICHORO YAO

$
0
0
  Na Mwandishi Maalum
Imeelezwa kwamba  ujumbe wa amani unaweza kuenezwa kwa njia nyepesi na rahisi   kama ile ya kuwatumia vijana na watoto kutumia vipaji vyao kuchora michoro inayobeba ujumbe unaosisitiza  umuhimu wa  amani duniani.

 Hayo yameelezwa na Tuvako Manongi,  Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya miaka mitano ya  “Jioni ya  Amani”, ambapo  Asasi isiyo ya kiserikali  ijulikanayo kama CITYarts Pieces for Peace ilionesha  kwa wageni waalikwa michoro mbalimbali iliyochorwa na watoto kutoka nchi 62 zikiwamo za Afrika.

 Madhumuhi ya hafla hiyo ambayo  Ubalozi ulikuwa mwenyeji yalilenga katika kuonesha ni kwa namna gani watoto wanavyoweza kuhuburi  na kuienzi amani kupitia sanaa  ya uchoraji na kwa njia  hiyo pia kukuza vipaji  vyao.

CITYarts Pieces for Peace ambayo makao yake yako  New York, imekuwa ikitembelea nchi mbalimbali, na kuwahamasisha watoto na vijana kuchora iwe kwenye makaratasi, mabango au hata kuta kwa lengo moja  tu la kueneza   ujumbe wa amani.

Balozi  Manongi amewashukuru waandaaji wa hafla hiyo kwa kubuni wazo hilo jema  la kuwahamasisha   watoto  kutumia vipaji vyao vya uchoraji kuhubiri amani hasa kwa kuzingatia kwamba mara nyingi mawazo wanayotoa watoto yanakuwa hayajachakachuliwa.

Naye  Mkurugenzi wa CITYartsPieces for Peace, Bi Tsip Ben-Haim pamoja na    kuushukuru  Ubalozi wa Tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa hafla hiyo, amesisitiza  haja na umuhimu kwa jumuia ya kimataifa kuienzi amani kwa  hali na mali.

Akasema kwamba uamuzi wa Asasi yake  wa kuanzisha  program hiyo ya kuwashirikisha watoto  kupitia sanaa  kueneza ujumbe wa amani, imekuwa na mafanikio sana na kwamba  program hiyo imesambaa  katika nchi nyingi.

Michoro wanayochora watoto na vijana hukusanywa na kuwekwa katika mabango ambayo waandaaji wa michoro hiyo  husafiri nayo kila nchi wanayokwenda  na kuionesha kwa watu wengine na kwa namna hiyo kueneza ujumbe wa amani kutoka  taifa moja hadi taifa jingine. 


 watoto hawa Linda, Maria,  Stephen na Alex  nao walipata fursa ya kutoa ujumbe wao wa amani kwa njia ya michoro, michoro  hapa wapo bize kila mmoja akichora ujumbe wake alioubuni mwenyewe. 
  Na utamduni wetu ulikuwapo, watanzania hawa,  Eri Fungo na Amiri Koba hawakuwa nyuma kurindimisha midundo iliyosherehekesha hafala hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa CITYart akielezea madhumuni ya hafla hiyo na kubwa zaidi ushirikishwaji wa watoto katika kueneza ujumbe wa amani
 Wageni
 Balozi Tuvako  Manongi akiwashukuru waandaji wa hafla hiyo pamoja na wageni waliofika, katika mazungumzo yake mafupi, Balozi alisititiza kwamba watoto na ambao mawazo yao hayajachakachuliwa.
 Wageni waalikwa wakisoma  ujumbe wa amani
Wageni waalikwa wakipata kitu kidogo walichangamkia sana  Maandazi
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live


Latest Images