Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

Bei ya Madafu leo


Breaking nyuzzz......... :Basi la Simba Mtoto lagongana uso kwa uso na lori Daraja la Wami leo.

$
0
0
Basi la Simba mtoto linalofanya safari zake kati ya Dar na Tanga likiwa limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo katikati ya Daraja la Mto Wami mkoani Pwani,dereva wa lori hilo amefariki papo hapo na wengine kujeruhiwa.tutaendelea kupeana taarifa zaidi hapo baadae.
Baadhi ya wasamaria wema wakijaribu kumchomoa Dereva  wa Lori hilo aliyekuwa amebanwa vibaya,pichani ambalo namba zake za usajili hazikufahamika mara moja.

INTRODUCING Young Killer & Fid Q (Brand New).

CCM YATOA PONGEZI KWA FRELIMO KWA USHINDI KATIKA UCHAGUZI MSUMBIJI

MHE. PINDI CHANA AFUNGUA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA UMATI TAIFA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Pindi H. Chana (Mb.)(katikati) akifuatilia igizo kuhusu kuanzishwa kwa UMATI, mafanikio na changamoto za hutoaji huduma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI Bi. Lulu Ng’wanakilala, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bw. Benidect Misani, Mwenyekiti wa UMATI Bibi Rose Wasira na kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa UMATI Bw. Charles Mngodo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Pindi H. Chana akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya UMATI Taifa ambaye alipata fursa ya kupima afya yake kama sehemu ya huduma zilizotolewa na UMATI sanjari na mkutano katika ukumbi wa Regency Park Hotel jijini Dar es salaam tarehe 30/10/2014.

Rais Kikwete amtumia salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa arusha kufuatia vifo vya watu katika ajali iliyotokea jijini humo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 30 Oktoba, 2014 katika eneo la Makumira Wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha na kusababisha vifo vya abiria 12 papo hapo na wengine kujeruhiwa. 

 “Nimeshtushwa na kusikitishwa sana kutokana na ajali hii mbaya ambayo kwa ghafla imeondoa uhai wa wenzetu 12 wasio na hatia kutokana na kukosekana kwa umakini wa binadamu katika uendeshaji wa vyombo vya moto katika barabara zetu”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake.

Ameongeza Rais Kikwete: “Kutokana na ajali hiyo, naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi, na kupitia kwako, Salamu hizi na pole nyingi ziwafikie wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote mahala pema peponi, Amina”.

Aidha, Rais Kikwete amewapa pole sana wote walioumia katika ajali hiyo akimwomba Mwenyezi Mungu awape ahueni ili wapone haraka na kuweza kurejea katika shughuli za maendeleo yao na yale ya taifa. “Naomba Mwenyezi Mungu awajalie ahueni ya haraka, ili muweze kupona haraka na kurejea katika maisha yenu ya kujitafutia riziki na kuchangia maendeleo ya taifa letu.”

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Oktoba,2014

TFF na Kamati zake hazina mamlaka ya kunifungia - Wakili Ndumbaro

$
0
0
Na Noreen Ahmad Globu ya Jamii

HUKU Dk. Damas Ndumbaro, akiwa amekata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miaka saba kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi iliyotolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema ataendelea kufanya kazi zake za kuwawakilisha wadau wa soka watakaohitaji huduma yake ya uwakili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Ndumbaro alisema kuwa TFF na Kamati zake hazina mamlaka ya kumfungia kufanya kazi za uwakili isipokuwa Jaji Mkuu wa Tanzania na serikali.
Ndumbaro alisema kuwa anashangaa kuona amehukumiwa na Kamati ya Nidhamu kwa kosa la maadili na kuongeza kwamba kamati hiyo haikupaswa kusikiliza tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Alisema kuwa adhabu hiyo aliyopewa ni dalili za wazi za 'chuki' dhidi yake kwa sababu yeye alichokizungumza ilikuwa ni maamuzi ya klabu 12 za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambazo zilikubaliana na kumteua yeye kupitia Kampuni yake ya Uwakili ya Maleta & Ndumbaro ya jijini.

"Sikuzungumza kwa niaba yangu, nilikuwa na ridhaa ya klabu 12, isipokuwa Stand United na Coastal Union, Kamati hii inatumiwa na Jamal Malinzi, ndio kamati iliyoipa ushindi Stand United kupanda Ligi Kuu," alisema Ndumbaro.

Wakili huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba alisema kuwa alianza kuonekana ni adui mara baada ya kukataa kushiriki katika ufujaji wa fedha ambapo kwa vipindi vitatu tofauti alikataa kusaini hundi za fedha ambazo TFF iliomba kutoka kwenye Bodi ya Ligi Kuu (TPL).

Alisema kwamba kwa sasa shirikisho hilo linakabiliwa na ukata baada ya kutumia kiasi cha Dola za Marekani 696,823 bila ya kupata kibali cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao wamezitoa kwa ajili ya udhamini wake wa timu ya Taifa (Taifa Stars).

Mbali na matumizi hayo, pia Jamal Malinzi anadaiwa kujilipa binafsi Dola za Marekani 159,140 ndio maana sasa wanaamua kufidia fedha hizo katika gharama nyingine ikiwamo makato ya Sh.1,000 kwa kila tiketi," alisema Ndumbaro.

Aliongeza kuwa anashangaa kuona TFF inaendelea kukata Sh. 1,000 katika kila tiketi za mashabiki wanaoingia uwanjani kushuhudia mechi za Ligi Kuu Bara na kutaja kiasi kilichokatwa hadi kufikia jana ni Sh. milioni 193.2 zilizotokana na mashabiki 193,257 walioingia viwanjani kushuhudia michezo ya ligi iliyoanza Septemba 20 mwaka huu.

Alisema pia anashangaa kuona rufaa yake aliyokata tangu Oktoba 21 mwaka huu haijapangiwa siku ya kusikilizwa lakini kikao cha Kamati ya Nidhamu kilichokutana kumjadili kilichukua siku mbili.
Aliongeza kuwa leo Oktoba 31 mwaka huu siku ya 10 na hakuna dalili za kusikilizwa, tutaendelea kuhesabu,  mambo mengi yako katika rufaa.

Alisema kwamba yeye hajawahi kutoa siri za shirikisho na kueleza kuwa kanuni za ligi na mikataba inayoingiwa si siri.

8th NANYUKI SERIES OPENS IN KIGALI

$
0
0
The 8th Inter-Parliamentary Relations Seminar (Nanyuki Series), was officially opened this morning by the President of the Rwanda Senate, Rt. Hon Bernard Makuza.

In his remarks, Rt Hon Makuza called on EALA and the National Assemblies to strengthen their relations and to effectively collaborate to tackle the underlying conditions that give insecurity and terrorism a chance.

“Parliamentarians and all stakeholders must step up real and collective efforts, to enhance mindset, awareness, and contribute to develop policies and legislations to effectively prevent all violent tendencies, negative and destructive ideologies”, Rt Hon Makuza stated.

The President of the Rwanda Senate called on stakeholders to go the extra mile to provide opportunities for the youth as a strategy to combating terrorism. This he noted, includes providing education, employment and real opportunities for the young people.
The Speaker of EALA, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa makes her remarks
Rt. Hon Makuza noted that Rwandans were today re-building the country and had embraced good governance as a pre-requisite to development. “Twenty years ago, under the visionary leadership of H.E. Paul Kagame, Rwandans commenced on the process of re-building the country after the Genocide against the Tutsi”, Rt Hon Makuza said.

“Drawing from this experience, I would like to emphasize that security and peace must be focused on as a foundation for our achievements and aspirations. That is why I want to stress especially that we the leaders, have the duty to prevent and to fight the root causes of insecurity and terrorism, genocide ideology and its denial in the region, in all their forms of manifestations”, he added.


Kivuko kipya cha Msangamkuu chawasili Mkoani Mtwara

$
0
0
Kivuko cha Msangamkuu( MV Mafanikio) chenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 50 pamoja na abiria 100 kikiwasili Mkoani Mtwara tayari kwa kuanza kazi rasmi ya kutoa huduma kati ya upande wa Mtwara Mjini na Msangamkuu.
Kivuko kipya cha (MV Mafanikio) kama kinavyoonekana mara baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwaletea wananchi wa Mtwara Kivuko hicho kipya.
Wananchi wakikimbia kuingia ndani ya Kivuko hicho kipya cha (MV Mafanikio) huku wakishangilia kuonyesha furaha yao mara baada ya kivuko hicho kuwasili mkoani Mtwara.
Baadhi ya kina mama nao walipata fursa ya kukaa na kufurahia ndani ya kivuko hicho kipya.
Usafiri huu wa Mitumbwi ndio uliokuwa unategemewa na wananchi hao wa Mtwara kabla ya ujio wa Kivuko kipya cha Msangamkuu.
Mkurugenzi wa Ufundi na Umeme (DTES) Dkt. Wiliam Nshama kutoka Wizara ya Ujenzi akipita kukagua Kivuko hicho kipya cha Mv Mafanikio. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

malenjendari wa disco waalikwa rasmi isumba lounge kesho jumamosi

$
0
0
Tukiwa tumebakiza siku moja tu kabla ya THE LEGENDS 2ND ANNIVERSARY kesho Jumamosi 1/11 ndani ya Isumba Lounge jijini Dar es salam; mimi  John Dillinga na mwenzangu DJ Fast Eddie tunapenda kutoa heshima kubwa na mwaliko rasmi kwa malejendari hawa pamoja na patners wao hiyo kesho. 
Kama unamfahamu au uko karibu na yeyote kati ya hawa naomba nisaidie kufikishia taarifa: John Peter Pantalakis, Ommy jr, DJ Seydou, DJ Paul master G, DJ Sweet Francis, DJ Gerry kotto, DJ Neagre Jay a.k.a Masoud Masoud, DJ Young Millionaire a.k.a Jakoub Usungu, DJ Master Funky, DJ Luke Joe, DJ Joe Johnson Holela, DJ TNT tito, DJ Ebonity Woo Jacky,  DJ Agib show,  DJ Junior Challenger Amani na DJ Richie Dillon, DJ Emperor. 


AND THE BEAT GOES ON WANAKWAMBIA THE WHISPERS....

Caroline Bernard anyakua taji la Miss Universe 2014

$
0
0
 Mrembo Caroline Bernard akipungia mkono muda mfupi baada ya kutangazwa rasmi kuwa ndio Miss Univerce 2014,katika hafla iliyofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.Picha na Othman Michuzi
Mrembo Calorine Bernard akipongezwa na washiriki wenzake.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
ALBERT MANGWEA (RiP) FT Mchizi Mox

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU MRS MAUA MPANKULI 

KWA KILA JAMBO KUNA MAJIRA YAKE NA WAKATI KWA KILA KUSUDI CHINI YA MBINGU.

MHU 3:1

LEO TAREHE 1 NOVEMBA 2014 UMETIMIZA MWAKA MMOJA KAMILI TANGU UITWE NYUMBANI KWA BWANA. INGAWA TUPO MBALI NA WEWE, LAKINI UMETUTOKA KIMWILI TU, KIROHO TUKO NA WEWE.

UNAKUMBUKWA SANA NA MUME WAKO MPENDWA MARTIN MPANKULI, WATOTO WAKO WAPENDWA JOYCE, ANGELA, GEOFREY, JACKSON, ANTONY, KANALI NA ALEX, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

RAHA YA MILELE UMPE EEH BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI.
AMINA!

President Jakaya Kikwete Mourns Sata- Signs a Condolence Book at Zambia High Commissioner’s Residence.

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete signs a condolence book at Zambia’s High Commissioner residence in Dar es Salaam today following the death of Zambia’s President Michael Sata early this week at a London hospital where he was receiving treatment. Seated left is First Lady Mama Salma Kikwete and standing second left is Zambia’s High Commissioner to Tanzania H.E. Judith Kapijimpanga.Photo by Freddy Maro-State House

Kiluvya United yaitungua Sinza Star bao 3-0

$
0
0
 Kikosi cha Kiluvya United kikifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi yao ya Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 katika Uwanja wa Makurumla dhidi ya Sinza Star. Kiluvya United ilishinda 3-0.
 Wachezaji wa Sinza Star wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mchezo wao na Kiluvya United.
 Wachezaji wa Kiluvya United wakisalimiana na wachezaji wa Sinza Stara kabla ya mchezo wao wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla jijini Dar es Salaam. Kiluvya United ilishinda 3-0 na kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 
 Kikosi cha Kiluvya United kikiwa katika picha ya pamoja.
Kikosi kamili cha timu ya Snza Star kikiwa katika picha ya pamoja.
Beki wa tmu ya Kiluvya United, Mwita Enoshi (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Sinza Stars katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla Dar es Salaam. Kiluvya ilishinda 3-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya mchuano hiyo.
Mshambuliaji wa timu ya Kiluvya United, Haji Zege (kushoto) akichuana na beki wa Sinza Stars Charles Kaembe katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Makurumla Dar es Salaam. Kiluvya ilishinda 3-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya mchuano hiyo.

MwanaFA atembelea kituo cha watoto yatima kabla ya kuangusha bonge la shoo ya"Vodacom Life is better"Tanga

$
0
0
Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Diana kilichopo jijini Tanga Tatu Chamchuo Akipokea zawadi ya jezi kutoka mwanamziki wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva Mwana FA alizozikabidhi kwa niaba ya Vodacom Tanzania,Mwanamziki huyo alitembelea kituo hicho kabla ya kufanya shoo yake ya"Vodacom Life is better" katika ukumbi wa Lacasachika mjini Tanga hapo jana.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva MwanaFA akipiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi pamoja na mshindi wa wa simu ya Vodafone Smart Kika Martin Joseph wa mjini Tanga mara alipotembelea duka la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya tatu jiji Tanga hapo Jana ambapo baadae shoo kali ya kukata na shoka ya''Vodacom Life is Better'iliyofanyika katika ukumbi wa Lacasachika hapo jana .
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva Mwana FA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa duka la Vodacom Tanzania barabara ya tatu mjini Tanga alipotembelea duka hilo na baadae akafanya shoo yake ya"Vodacom Life is better" katika ukumbi wa Lacasachika mjini Tanga hapo jana.

TFF YAJIBU SHUTUMA ZILIZOTOLEWA NA WAKILI NDUMBARO DHIDI YAKE

$
0
0
Oktoba 31 mwaka huu kupitia vyombo vya habari Wakili Damas Ndumbaro alitoa shutuma mbalimbali dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Tunapenda kuueleza umma wa Watanzania yafuatayo;

1.Hukumu dhidi ya Wakili Ndumbaro ilitolewa na chombo halali kwa mujibu wa Katiba ya TFF. Hivyo, TFF inatoa tahadhari kwa wanafamilia wa mpira wa miguu kutomhusisha Wakili Ndumbaro katika masuala ya mpira wa miguu katika kipindi hiki anachotumikia adhabu.

2.Hadi sasa TFF haijapokea rufani yoyote kutoka kwa Wakili Ndumbaro. Hii ni kwa kuwa kupitia barua yake kwa TFF aliagiza asikabidhiwe nyaraka yoyote kutoka TFF hadi Oktoba 30 mwaka huu, hivyo hukumu ya Kamati ya Nidhamu dhidi yake alikabidhiwa Oktoba 30 mwaka huu. Alichokifanya Wakili Ndumbaro ni kuleta TFF barua ya kusudio la kukata rufani.

3.Tuhuma za ubadhirifu wa TFF zilizotolewa na Wakili Ndumbaro si za kweli. TFF inatafakari hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua dhidi ya tuhuma hizi.
4.Mkataba wa TFF na TBL:
TFF inapenda kuwahakikishia wadau wa mpira wa miguu kuwa hakuna ubadhirifu wa aina yoyote katika matumizi ya fedha za mkataba wa TFF/TBL. TFF ingependa itoe kwa umma ufafanuzi wa vipengele vya mkataba huo na jinsi unavyoendeshwa lakini masharti ya mkataba huo (confidentiality clause) yanatuzuia kufanya hivyo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikutana na klabu za Ligi Kuu na kuzielekeza zikae na kujadili kanuni za Ligi, kisha zipendekeze maboresho ili yajadiliwe katika kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji.

TFF inapenda kuchukue fursa hii kusisitiza umuhimu wa kufuata mifumo tuliyojiwekea katika kutatua matatizo/kero zetu mbalimbali, utulivu ni muhimu katika kuendeleza mpira wa miguu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Nakala: Mkurugenzi Mtendaji TBL

TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA MRADI WA RUSUMO

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Mhe. Come Manirakiza wakitia saini mkataba wa miaka 50 wa  usafirishaji wa umeme kutoka Mradi wa Rusumo kwenda nchini humo katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Mradi huo unazihusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto), akibadilishana hati na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Mhe Come Manirakiza, baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka 50 wa  usafirishaji wa umeme kutoka Mradi wa Rusumo kwenda nchini humo katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Mradi huo unazihusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
 Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe Issa Mtambuka  (wa pili kushoto mbele) akiwa na maofisa wengine kwenye sherehe hiyo.

JUMUIYA YA WAZAZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE

$
0
0
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto) na Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje wakionesha daftari hilo baada ya kuzinduliwa.
 Viongozi wa meza kuu wakipiga makofi wakati wakiimba wimbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kuzindua daftari hilo. Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mavela, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu,Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje ,  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed, Katibu wa Elimu na Malezi Taifa, Masoud Bwire na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Dar es Salaam, Nicolaus Msemo.
 Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
  Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kushoto), akiteta jambo na wajumbe wa kamati ndogondogo zilizoundwa ili kurahisisha utendaji kazi wa jumuia hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu na mjumbe Angelina Malembeka.

MDAHALO WA KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA KWENYE HOTELI YA BLUE PEARL, UBUNGO PLAZA DAR ES SALAAM JUMAPILI TAREHE 2 NOVEMBA 2014 KUANZIA SAA 9.00 MCHANA MPAKA SAA 12.00 JIONI

$
0
0
      Taasisi ya Mwalimu Nyerere inapenda kutoa taarifa kwamba imeandaa mdahalo wa Pili wenye lengo la kujadili umuhimu  wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba. Mambo ya msingi  yaliyomo katika Katiba hiyo yataainishwa  na kujadiliwa na washiriki wa Mdahalo.  Taasisi ya Mwalimu Nyerere inapenda kusisitiza kuwa lengo la mdahalo si malumbano au makatazo:

 Lengo ni kutoa fursa kwa washiriki wa mdahalo na wananchi kwa ujumla kujielimisha kuhusu Katiba inayopendekezwa ili waweze kuielewa vizuri, na hivyo kujiandaa kuipigia kura katika mazingira ya uelewa kwa kuzingatia dhamira yao, bila kulazimishwa, kutishiwa au hata kulipwa fedha na mtu au kundi lolote.  Hakuna kiingilio katika mdahalo huo, na watu wote wanakaribishwa.   

Mdahalo  utafanyika kati ya saa 9.00 mchana na saa 12.00 jioni  kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.  Washiriki wote wawe wamefika Blue Pearl  Hoteli  saa 8 mchana.

2.         Washiriki katika mdahalo huo ni baadhi ya waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiwamo  Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph S. Warioba,  Mzee Joseph W. Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bibi Mwantumu Malale, Mtumishi wa Umma Mwandamizi Mstaafu, ,   

 Ndugu Awadh Ali  Saidi, Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar na Ndugu Humphrey Polepole, Mdau wa Maendeleo),  Profesa Baregu, Jaji Mstaafu Mzee Ussi (Zanzibar) na Ndugu Muhammad Mshamba (Zanzibar).wananchi  na viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya wafanyakazi,  n.k. wanakaribishwa kushiriki.

3.         Mdahalo utarushwa moja kwa moja na ITV.  Kwa kupitia TV na Redio zao  na TV Sibuka Maisha.  Wananchi  po pote walipo wanaombwa kushiriki katika mdahalo huo.
Imetolewa na:

Mkurugezi Mtendaji,
Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
S.L.P. 71000,
Fax No. 255 22 2119216/2118354
India/Makunganya/Bridge Street
1 Novemba,  2014
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images