Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

THE BEAT FESTIVAL Friday 7th of November @ Trinini, Oysterbay, Dar es salaam

$
0
0
THE BEAT FESTIVAL 
FRIDAY 7. November - 20.00 - 02.00 
Venue: Triniti, Msasani rd. 26, Oysterbay Dar es salaam
Entrance: 10.000 Tsh. only

This edition of THE BEAT, after a two month break, celebrates the return of a group of Tanzanian musicians from their European tour, which took place in Germany and Denmark in September and October 2014, featuring Mopao Jazz, Malfred, Mzungu Kichaa, Ashimba and backing band Bongo Beat. The aim is to bring the energy from this tour to THE BEAT FESTIVAL in Dar es Salaam. Don't miss this !

Lineup:

DAVID TINNING (Santuri Safari) – 20.00 – 21.30 & 00.30 – 02.00
David Tinning has been DJing for the best part of 2 decades. As the coordinator of Santuri Safari he’s been working to develop platforms for DJ culture in the region through organising workshops, recording sessions, events and festival appearances. As a DJ, David has had a vinyl fixation that first surfaced as a child in the UK. He remains obsessively dedicated to the format - schlepping a bunch from his former home Berlin to Dar es Salaam in 2012. 

MOPAO JAZZ – AfroJazz - 21.30
Mopao is a self-taught Tanzanian Jazz guitarist who is destined for a great future. He is steadily growing on the Dar es Salaam scene and performs with a number of bands and solo artists. Mopao also performs with Mzungu Kichaa and Malfred, so he will definitely own the stage for this edition of THE BEAT.
MALFRED – Reggae – 22.00

Malfred is one of Tanzania’s top dancehall and reggae artists. His album, Hisia Zangu, produced by Alec Burton, won him a nomination at the 2014 Tanzanian Music Awards. The album also features a collaboration with Jamaican reggae singer Lutan Fyah. Malfred will be performing with his full band.
        
MZUNGU KICHAA – World Music – 23.00
Mzungu Kichaa means “the crazy white man”. The real meaning behind this name is many-fold and represents not only his music but also has a deep social-cultural significance. He continues to play an important role on the Tanzanian urban scene and represents Tanzanian music in other countries in Africa and Europe through his tours. His passion and knowledge of Tanzanian music has also led him to teach young aspiring musicians in Dar es Salaam through Caravan Records and the school of Music and Dance. At this edition of The Beat, him and his band will be celebrating the return from their 5th European tour.
ABOUT THE BEAT

The Beat is a monthly festival that takes place on the first Friday of the month, showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is hosted by Mzungu Kichaa andis powered by: Caravan Records, Triniti, and Goethe Institut Tanzania. 


EAC DEPUTY SECRETARY GENERAL HOLDS TALKS WITH MEMBERS OF DANISH CONFEDERATION OF INDUSTRY

$
0
0
A delegation of 18 Members of Confederation of Danish Industry International Market Council including Danish Ambassador to United Republic of Tanzania H.E Johnny Flento today paid a courtesy call on the EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Dr Enos Bukuku at the East African Community headquarters in Arusha, Tanzania. 
 The Confederation of Danish Industry (DI) is a private organisation funded, owned and managed by 10,000 Danish companies within manufacturing, trade and service industry. 
The member companies represent the major proportion of the Danish business community, both in terms of numbers, amount of employees, and volume of exports. 
The EAC Deputy Secretary General briefed the Danish delegation on the major developments taking place in the integration process, notably the operationalization of the EAC Customs Union especially on the Single Customs Territory, status of implementation of the Common Market Protocol, as well as the signed East African Community Monetary Union Protocol and its implementation process. 
Dr Bukuku informed the delegation that the EAC region was undertaking ambitious regional infrastructure development programme in roads, railways, telecommunications and civil aviation. 
He hailed the Danish support to the EAC through the Partnership Fund and other initiatives. 
The EAC Deputy Secretary General reiterated to the Danish delegation that the need to deepen East African integration, and indeed to fulfill the long cherished dream of a united East Africa, cannot be overemphasized. 
The EAC official informed Danish delegation that EAC is people-centered community and the involvement of the private sector, women and youth entrepreneurs, as well as ordinary citizens of East Africa in the integration agenda is critical 
On his part, the Deputy Director General of Confederation of Danish Industry International Market Council, Mr. Thomas Bustrup, who led the Danish delegation thanked his host for the warm reception and hospitality accorded to them and commended the EAC Secretariat for the enormous work done that has led to important milestones in the integration process. 
Later in the day, the EAC Deputy Secretary General Dr Enos Bukuku held talks with Mr. Herve Joly Assistant Director of International Monetary Fund (IMF) Africa and Mr. Thomas Baunsgaard, the IMF Resident Representative to United Republic Tanzania. 
Dr Bukuku and his guests discussed different issues on the region's  economy especially the EAC Monetary Union Protocol and how IMF can support the implementation process.
 Dr Enos Bukuku stressing a point in the discussions
 Members of Confederation of Danish Industry International Market Council in the discussion with EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Dr Enos Bukuku
A group photo opportunity

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 40

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAMALIZA ZIARAYAKE KATIKA MGODI WA BUZWAGI

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira hii leo imekamilisha ziara yake kwa kukagua mgodi wa Buzwagi na kuridhishwa na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na usimimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa mgodi huo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Wa kwanza kulia ni Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati hiyo.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana wajumbe wa Kamati katika ziara ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji katika mgodi wa Buzwagi.

Ujenzi wa awamu ya pili wa Kituo cha Afya cha Mwendakulima kinachojengwa na Mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kuwasogezea wananchi huduma bora za afya.
Baadhi nyumba zitakazotumiwa na waganga na wauguzi wa kituo cha afya cha Mwendakulima pindi kituo hicho kitakapoanza kutumika.

Danga chee ndani ya michuzi tv

ngoma azipendazo ankal

APPRECIATION

mkude simba aja kivingine, aangusha single mpya "Kitu Kidogo"


RAIS SATA WA ZAMBIA KUZIKWA NOVEMBA 11, 2014 JIJINI LUSAKA

$
0
0
Serikali ya Zambia imetangaza kuwa mazishi ya Rais Michael Chilufya Sata (pichani) yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 11 Novemba 2014, katika eneo la makaburi lililotengwa rasmi kwa ajili ya kuzikwa Marais  linaloitwa Embassy Park, Lusaka, Zambia.

Mwili wa Rais Sata unategemewa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka, siku ya Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014. Mara baada ya mwili kupokelewa utapelekwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mulungushi ambapo watu wote watapata fursa ya kuuaga. Dkt. Guy Scott, Makamu wa Rais ataweka shada la maua.

 Taratibu za kuaga mwili wa Rais Sata zitafanyika katika Ukumbi wa Mulungushi zitaanza rasmi siku ya Jumapili tarehe 2 hadi  Jumapili tarehe 9 Novemba 2014. Misa ya kuaga itafanyika siku ya Jumannne, tarehe 11 Novemba 2014 katika viwanja vya mashujaa, Lusaka.  na baada ya hapo mwili utapelekwa Embassy Park kwa mazishi.

              
                  MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI, AMINA

UBALOZI WA TANZANIA, LUSAKA 

NEWS ALERT: UFAFANUZI WA TAARIFA ZISIZO ZA KWELI KUHUSU UTEUZI WA KONSELI WA HESHIMA JIMBO LA GUANDONG, CHINA

$
0
0

Hivi karibuni kumezuka taarifa za upotoshaji zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali ya Tanzania imemteua Bw. Salaah, Mkurugenzi wa Home Shopping Centre, (pichani ) kuwa Konseli wa Heshima (Honorary Consul) kwenye mji wa Guangzhou kwenye Jimbo la Guandong. 
Watoa taarifa hizo, hawakutoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yao zaidi ya kutoa picha mbalimbali za Bw.Salaah kutoka kwenye mitandao mingine ya kijamii.
Taarifa hizo sio za kweli. 

Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za mahusiano ya kidiplomasia ya China, nafasi ya Konseli wa Heshima haitambuliki 'mainland' China.  
Kwa maneno mengine hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kuteua mtu kuwa Konseli wa Heshima katika eneo lolote la China isipokuwa Hong Kong ambako kuna mamlaka huru za utawala zinazofuata sheria zake.
Kwa faida ya umma, ni vema kufafanua kwamba Nchi ya China inakubali nchi za Nje kufungua Ubalozi kamili (Embassy) ambao makao yake yanatakiwa kuwepo katika mji Mkuu wa China- Beijing na Konseli Kuu ama kwa lugha iliyozoeleka Ubalozi Mdogo (General Consulate) ambao unaweza kufunguliwa kwenye makao Makuu ya mji wowote ule katika Majimbo ya China.
Watu wengi wamekuwa wakichanganya Ubalozi Mdogo au Konseli Kuu (General Consulate) na Konseli (Ubalozi) wa Heshima  (Honorary Consulate).   Konseli Kuu (General Consulate) ni sehemu ya Ubalozi (ndio maana wengi huuita Ubalozi Mdogo) ambapo kiongozi wake na maafisa wake wote ni watumishi wa Serikali kutokea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Masharti ya kuwa Mkuu wa Konseli 'General Consulate' lazima uwe Afisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje mwenye uzoefu usiopungua miaka 10 ya Utumishi katika Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa muktadha huo, taarifa kwamba Bw.Salaah ameteuliwa kuwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko Guangzhou sio kweli kwasababu Sheria za China haziruhusu uwepo wa nafasi hiyo.  Aidha, Bw Salaah hawezi kuwa Balozi Mdogo (Consul General) kwa kuwa yeye sio mwajiriwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Hivyo habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na zinalenga kuupotosha umma.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA MAMBO YA 
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
OCTOBER 30, 2014

News Alert: mtangazaji mahiri wa RTD Ben Kiko afariki dunia

$
0
0
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko enzi za uhai wake akiwa katika moja ya semina alizohudhuria.

MTANGAZAJI na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Ben Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.

MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA,
AMIN
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kikoakizungumza na Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo mkoani Tabora wakati wa uhai wake.


Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo (pichani akiwa ameshika hati ya Tuzo ya Utumishi uliotukuka wa Maisha April 2012) maarufu kama Ben Kiko,   

 atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.

WANAHABARI KILIMANJARO WATEMBELEA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MOSHI(MUWSA)

$
0
0

Mkurugenzi wa MUWSA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo kwa wanahabari kuhusu uchimbaji wa visima kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa maji katika vyanzo vyake.
Mkurugenzi MUWSA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonesha wanahabari Moja ya tanki lililopo eneo la CCP ambalo linatumika kuhifadhi maji.
Mhandisi Luhemeja akionesha moja ya kisima kilichochimbwa katika eneo la matanki ya kuhifadhi maji ambacho pia kutasaidia kuongeza maji katika matanki hayo kwa ajili ya matumizi. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA







Profesa Mwandosya atembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia

$
0
0
Akiwa ziarani Ethiopia Waziri  wa Nchi (Kazi Maalum) Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya Mwandosya ametembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia (Great Ethiopian Renaissance Dam-GERD).Ujenzi utakapokamilika mwaka 2017 GERD litazalisha MW 6000 za umeme na kuwa mradi mkubwa wa aina yake Afrika na wa nane kwa ukubwa duniani. Mradi unahusu ujenzi wa bwawa kwenye Mto Blue Nile, kilomita 850 kutoka Addis Ababa.
Waziri  wa Nchi (Kazi Maalum) Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya Mwandosya na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Naimi Aziz (wa pili kushoto) wakitembelea mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia (Great Ethiopian Renaissance Dam-GERD).
Waziri wa Maji Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Mheshimiwa Alemayehu Tegenu,kushoto,na Waziri wa Nchi (Kazi Maalum)Ofisi ya Rais,Mark Mwandosya ,kulia,wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi Mhandisi Bekele. 
Waziri Tegenu wa Ethiopia akiwa katikati mwenye kofia ya kijani,kulia kwake ni Mheshimiwa Naimi Aziz,Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, wa kwanza kushoto kwake ni Mama Lucy Mwandosya,mke wa Waziri Mwandosya, wa pili kushoto kwake ni Waziri Mwandosya,wa tatu kushoto kwake ni Mhandisi Bekele,Meneja wa Mradi,wakiwa na wahandisi wa mradi, na ujumbe wa Waziri Mwandosya. 
Eneo la Mradi wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Ethiopia (Great Ethiopian Renaissance Dam-GERD)

MAKOCHA 35 KUSHIRIKI KOZI YA LESENI C YA CAF

$
0
0
Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.

Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).

Washiriki wa kozi hiyo ni Abdulmaliki Nemes (Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented Youth Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids), Amri Saidi (Mwadui FC), Athuman Kambi (Morogoro), Charles Mwakambaya (Burkina Faso FC),  Damian Mussa (Alliance One) na Daudi Sichinga (Kasulu United).

Denis Maneva (Shule ya Msingi Logo), Edgar Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi Mtimbwilimbwili), Henry Ngondo (Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance), Martin Saanya (Magereza Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine University Academy).

Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage Kabange (Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon (Kishoto FC), Nyamtimba Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah (Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers), Safari Nyerere (Elimu Sports Academy) na Said Lyakuka (Kizuka Stars).

Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20), Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting), Swalehe Allawi Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri (Kick Off Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).

Wakati huo huo, kutakuwa na kozi ya wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati (Intermediate) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29 mwaka huu.

Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira yaumwagia sifa Mgodi wa Buzwagi

$
0
0
Migodi ya dhahabu nchini imetakiwa kuiga mfano wa mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama katika kutunza na kuweka mazingira ya uzalishaji salama kwa binadamu na viumbe wengine.

 Rai hiyo imetolewa  na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili  na Mazingira Mheshimiwa James Lembeli, wakati kamati hiyo ilipotembelea mgodi huo tarehe 30 Oktoba 2014 . 

Mhe.Lembeli alisema kuwa kamati yake ilifuatilia kwa kina utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC)  kwa migodi ya dhahabu yote nchini na kukuta mapungufu mengi na dosari za utekelezaji. 

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa hata hivyo ni mgodi  wa  Buzwagi pekee ndio uliozingatia  maagizo ya Baraza hilo katika kuweka Mazingira bora na salama kwa binadamu kwa kiasi kikubwa. 

Lembeli alifafanua kuwa Mgodi wa Buzwagi umeweza  kuharibu maji taka ya sumu aina ya cyanide na mabaki ya takataka zingine kutoka mgodini hapo na kuzihifadhi kwa viwango vya kimataifa kama ilivyoagizwa na NEMC. 

“Taka sumu za kutoka migodi ya dhahabu zikiachwa zikatiririka hadi kwenye vyanzo vya maji zinaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu na viumbe wengine kama mifugo,ndege na wanyama wa porini”Alieleza Mhe.Lembeli. 

Awali akitoa maelezo ya namna mgodi huo unavyohifadhi na kuweka mazingira katika usalama na ubora unaotakiwa kisheria, Meneja Mkuu wa mgodi huo, Bwana Philbert Rweyemamu alisema katika ukaguzi wa dharura uliofanywa na Mkemia Mkuu wa Serikali Agosti 12, 2014 Buzwagi ilitunukiwa usajili kamili Usajili kama muagizaji wa kemikali nchini na usajili huo utadumu hadi Agosti 30, 2019. 

Katika ziara ya mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold, wajumbe walionyeshwa bwawa maalumu ya kuhifadhi maji kwa matumizi ya binaadam na pia bwawa la kuhifadhi maji taka ya sumu na madawa yanayotumika kuchenjulia dhahabu. 

Meneja Mkuu Rweyemamu aliekuwa akiongoza ziara hiyo alisema bwawa la Buzwagi la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya binaadamu ni bwawa pekee la aina yake hapa nchini ambalo limejengwa kwa teknolojia ya hali ya juu ili kuweza kuhifadhi maji. 

Alisema bwawa hilo litakua raslimali kubwa kwa jamii ya Kahama hapo mgodi utakapofungwa kwani wataweza kulima mazao kwa mwaka mzima kwa kutumia njia ya umwagiliaji. 

 Rweyemamu alisema serikali kupitia mkemia  mkuu wa serikali imekuwa ikifanya uchunguzi wa kina kwa vyanzo vya maji kuzunguka mgodi huo na kuridhika kuwa hakuna sumu inayovuja kutoka katika mgodi wa Buzwagi.

 “Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mfanyakazi hapa Buzwagi na idara ya Mazingira ipo tu kwa ajili ya kusimamia utekelezaji ” alisema Meneja huyo. Kwa upande wake Mheshimiwa Lembeli alisema kazi ambayo imefanyika katika mgodi wa Buzwagi katika miaka miwili iliopita imekuwa ya kusifika hata katika mahusiano yake na jamii inayozunguka mgodi.

 Wajumbe wengine wa kamati hiyo ya bunge walioshiriki katika ziara hiyo ya mgodi wa Buzwagi ni pamoja na Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) Mazingira, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ambae nae pia uliumimBus la Simba mtoto na Lori zimegongana uso kwa uso, dereva wa lori amefariki na majeruhi kadhaainia sifa mgodi wa buzwagi kwa kuwa kinara katika utunzaji wa mazingira. 

 Katika ziara hiyo pia alikuwepo Sazi Salum Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira NEMC Mhandisi Boniaventura Baya ambae aliudhibitisha mgodi wa Buzwagi kuwa wa kwanza kwa utunzaji wa mazingira
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Philbert Rweyemamu akiwaelezea Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira jinsi bwawa la uhifadhi wa maji kwa matumizi ya binaadamu lilivyojengwa kitaalam wakati walipotembelea bwawa hilo.
Mhandisi Bonaventura Baya akiusifu mgodi wa Buzwagi baada ya maelezo yaliyotolewa na Meneja Mkuu wa Mgodi kuhusu jinsi mgodi huo unavyozingatia utunzaji wa mazingira.
Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) Mazingira, Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipewa ufafanuzi zaidi na Meneja wa Idara ya Mazingira wa Buzwagi John Murray.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa mameneja wa mgodi wa Buzwagi mbele ya bwawa la kuhifadhi maji taka ya sumu.
Wajumbe wakionyeshwa kituo cha afya cha kisasa cha Mwendakulima kilichojengwa na mgodi wa Buzwagi.

TUTASHIRIKIANA NA WAPENDA AMANI KUISAIDIA DRC KUWA NA AMANI - TANZANIA

$
0
0
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa iliyokuwa ikijadili ajenda kuhusu tathmini ya jumla ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi zinazochangia wanajeshi wake katika operesheni hizo za ulinzi wa amani.
Sehumu ya wajumbe wa Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakifuatilia majadiliano ya ajenda kuhusu Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.

news alert: Gadner G. Habash atinga EFM, kuanza kusikika hewani Jumatatu saa tisa alasiri

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Mtanganzaji mahiri nchini Gadner G. Habash amejiunga na kituo cha redio kinachiokuja kasi sana nchini cha EFM 93.7, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha. 
Gadner, ambaye alikuwa akipiga jalamba katika kituo cha Time FM baada ya kuondoka Clouds FM, pia hupasha-pasha mambo katika Michuzi TV, kwenye makala zake za kusisimua za "NAJUA WAJUA". 
"Ni kweli kaka. Sikiliza mambo kuanzia Jumatatu saa 9 alasiri hadi usiku. Kipindi kitaitwa 'Ubaoni". Gadner kaiambia Globu ya Jamii mchana huu. 
Gadner anakuwa mtangazaji mahiri wa pili kuhamia EFM, baada ya Maulid Baraka wa Kitenge kujiunga nao hivi karibuni akitokea Radio One Stereo. 
Globu ya Jamii inamtakia kila la heri Gadner G, Habash kwa kibarua hicho kipya ambacho hatuna shaka atakitendea haki kama ilivyo kawaida yake.


Pichani ni Gadner G. Habash (kulia) na Maulid Baraka wa kitenge wakiwa na Da'Mboni wa The Mboni Show TV talk show  wakijiandaa kurekodi kipindi kitachorushwa hivi karibuni.

mambo ya Comedian MC ZIPOMPAPOMPA leo

CCM YATOA PONGEZI KWA FRELIMO KWA USHINDI KATIKA UCHAGUZI MSUMBIJI

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,makao makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.

NA BASHIR NKOROMO

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa furaha Chama cha Frelimo kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu.
Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Frelimo, Mhe Filipe Nyusi ameibuka kidedea na sasa ndiye Rais Mteule wa Msumbiji ambaye baada ya kuapishwa atashika mikoba itaakayoachwa na Rais anayemaliza muda wake, Armando Gwebuza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (Pichani), amesema, CCM imepokea ushindi huo kwa furaha kubwa kutokana na undugu wa damu uliopo baina yake na Frelimo kwa mikaka mingi.

"Chama Cha Mapinduzi kilifuatilia kwa karibu kwa kuwa CCM na Chama cha Frelimo ni vyama ndugu vyenye historia moja na ya pamoja ya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Historia hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Mteule wa nchi hiyo Ndugu Filipe Nyusi mara baada ya kuteuliwa kwake na Frelimo kugombea Urais, nchi ya kwanza kuitembelea kuwa Tanzania", alisema Nape na kuongeza;

"Ikumbukwe kwamba huyu si mgeni hapa Tanzania. Kama wanaharakati wengine wa ukombozi, Ndugu Nyusi aliishi Tanzania, anaongea vizuri Kiswahili na anaichukulia Tanzania ni nyumbani".
Alisema kwa mnasaba huo, Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa ujumla wana kila sababu ya kushangilia ushindi walioupata ndugu zao wa Frelimo, kwa kuwa ushindi huo ni wa wote.

"Tunampongeza sana Rais Mteule Filipe Nyusi kwa kupeperusha vema bendera ya Frelimo. Matokeo ya Uchaguzi yamedhihirisha imani kubwa waliyonayo wana-Msumbiji kwa Frelimo na kwa Rais Mteule Filipe Nyusi", alisema Nape. 

Nape amesema CCM ina imani kwamba chini ya uongozi imara wa Mwenyekiti wake Dk. Jakaya Kikwete, na Rais Mteule Filipe Nyusi, uhusiano kati ya vyama vya CCM na Frelimo utaimarika na kustawi.
Kadhalika Chama Cha Mapinduzi kimempongeza  Armando Guebuza kwa kuiongoza Frelimo na Taifa lake vema na kukamilisha uongozi wake kwa mafanikio makubwa.

"Anapoanza kipindi hiki cha uongozi wa Taifa lake, sisi wana-CCM tunamtakia Ndugu Nyusi afya njema, busara, maarifa na uongozi uliotukuka", alisema Nape. 
Alisema, CCM itasimama pamoja na Frelimo katika kuendeleza urithi ulioachwa na waasisi wa vyama vyao, Mwalimu Julius Nyerere na  Samora Machel. 

Kongamano la Ufugaji nyuki Barani Afrika kufanyika Jijini Arusha

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii (Kitengo cha Misitu na Nyuki),Bi. Gladnes Mkamba akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu uwepo wa Kongamano la Ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Novemba 11 - 16,2014 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC),jijini Arusha.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu kutoka Wakala wa Misitu Tanzania,Bw. Zawadi Mbwambo.Picha na Othman Michuzi.
Kaimu Mkurugenzi Mwandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii (Kitengo cha Ufugaji Nyuki),Bi. Monica Kagya akichangia machache kuhusu Kongamano hilo na umuhimu wa wadau kushiriki.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images