Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 623 | 624 | (Page 625) | 626 | 627 | .... | 3284 | newer

  0 0
 • 10/29/14--14:20: kishalia hapa usiku huu
 • Muendesha bodaboda (alieshika kiuno) akizungumza na mmiliki wa gari mara baada ya kupigwa pasi na kupiga mweleka barabarani katika eneo la geti kuu la kuingilia Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu.Mwenye gari hiyo alikuwa akiingia Mlimani city huku muendesha bodaboda hiyo akiwa barabara kuu akitokea Ubungo kuelekea Mwenge.

  0 0
 • 10/29/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Soggy Doggy - Kibanda cha simu

  0 0
 • 10/29/14--22:00: NAFASI ZA KAZI
 • Wanahitajika wasichana wa kuuza duka kubwa liliopo posta jijini dar es salaam, wenye uwezo wa kufanya Marketing, na Online Sales. 

  wawe na uwezo wa kuzungumza kiingereza na kiswahili fasaha. elimu kuanzia diploma.

  Wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0756608383 na 0713608383

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya amekuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mheshimiwa Alemayehu Tegenu kuhusu maendeleo ya maji na umeme katika nchi zao
  Waziri Tegenu (kulia) akiwa na Waziri Mwandosya.
  Mawaziri wakisikiliza maafisa wa Ethiopia wakiwasilisha mada mbalimbali.
  Picha ya pamoja baada ya kikao. Wa  tatu kulia ni Ndugu Suma Mwakyusa Afisa Mwandamizi Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, wa nne kulia ni Mheshimiwa Naima Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, wa tano kulia ni Mheshimiwa Alemayehu Tegenu,Waziri wa Maji na Umeme wa Ethiopia akifuatiwa na Waziri Mwandosya na ujumbe wake.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya (wa pili kushoto) na wenyeji wake pamoja na ujumbe wake wakiwa katika mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo nchini Ethiopia

  0 0


  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (Katikati) akionyesha kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.  Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Veronika Kazimoto (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (katikati).

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akimfafanulia jambo Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum mara baada ya kufanya uzinduzi.

  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akimkabidhi chapisho Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira imeendelea na ukaguzi katika Migodi ya dhahabu kufahamu utekelezaji wa Sheri a ya Mazingira. Katika Mgodi wa Bulyanhulu Kamati iliangalia jinsi maji yenye kemikali yanavyohifadhiwa na udhibiti wa taka za plastiki mgodini hapo. Migodi iliyotembelewa mpaka sasa ni Mgodi wa North Mara, Geita na Bulyanhulu. Hii leo Kamati hii itaendelea na ziara yake katika mgodi wa Buzwagi.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi wa kisheria mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Kamati hiyo iko katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mh. James Lembeli (wa tatu kulia), Mh. John Mnyika na Mh. Henry Shekifu wajumbe wa Kamati hiyo. Wa kwanza (kushoto) ni Bw. Peter Burger, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu.
  Pichani ni taka za plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa Bulyanhulu.
  Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
  Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.

  0 0

  Kufuatia kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, kilichotokea tarehe 28 Oktoba 2014, mjini London, na kwa kuzingatia Katiba yake Kifungu cha 38 (1) kinachohusu mamlaka ya Rais, kwamba nafasi ya Rais ikiwa wazi kwa sababu yoyote ile, Makamu wa Rais atakaimu madaraka ya kiti cha Urais hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika ndani ya siku tisini (90), hivyo Serikali imemteua Mhe. Guy Scott (MB), Makamu wa Rais, kukaimu nafasi hiyo katika kipindi hiki cha mpito.

  Tayari aliyekuwa anakaimu madaraka ya Urais, Mhe. Edgar Lungu (MB) ameshamkabidhi madaraka hayo. 

  Hadi sasa kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, bado haijafahamika maombolezo rasmi yataanza lini na kwa siku ngapi au mazishi yatafanyika lini. Haya yote yanategemea maamuzi ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho kinakutana hivi sasa.

  Hizi ni taarifa tunazoendelea kupokea, hivyo nasi tutaendelea kuwataarifu kwa kadri tunavyozipata.

  UBALOZI , LUSAKA , ZAMBIA

  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kusononeshwa sana na taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Michael Chilufya Sata ambacho kimetokea jana, Jumanne, Oktoba 28, 2014 kwenye Hospitali ya King Edward VII, London, Uingereza, ambako alikuwa anatibiwa akiwa na umri wa miaka 77.
  Katika salamu ambazo amempelekea Makamu wa Rais wa Zambia, Mheshimiwa Dkt. Guy Scott kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Kikwete amesema:

  “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi, habari za kusikitisha za kifo cha Mheshimiwa Michael Chilufya Sata, Rais wa Jamhuri ya Zambia. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hakika, kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kukutumia wewe Mheshimiwa salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu, na kupitia kwako familia ya wafiwa na ndugu wa Hayati Rais Sata pamoja na Serikali na ndugu zetu wananchi wote wa Zambia kufuatia msiba huu wa ghafla.”

  Ameongeza Rais Kikwete: “Hayati Sata atakumbukwa daima kama mmoja wa viongozi wa mfano wa kuigwa katika Afrika. Katika kipindi chake kifupi cha uongozi wa juu wa Zambia, alifanikiwa kuleta mageuzi makubwa katika maisha ya wananchi wengi wa Zambia. Atakumbukwa pia kwa imani yake isiyoyumba ya kupigania uhuru, haki na usawa, sifa ambazo zilimfanya kiongozi mpendwa ndani na nje ya mipaka ya Jamhuri ya Zambia.”

  Ameongeza Rais Kikwete: “Hivyo, huyu ni kiongozi ambaye siyo tu atakumbwa na wananchi wa Zambia lakini atakumbukwa na sisi sote wenzake na watoto wote wa Afrika.”

  “Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na huzuni, tunaungana nanyi kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na subira wana familia ya wafiwa, jamaa na ndugu zetu wote wa Zambia ili waweze kuhimili machungu ya kipindi hiki cha msiba mkubwa. Aidha, tuko pamoja nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema roho ya Marehemu Michael Chilufya Sata.”

  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.

  29 Oktoba,2014.


  0 0

  Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari ya Globu ya Jamii zinaeleza kuwa Msanii wa filamu, Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Globu ya Jamii bado inafuatilia kwa karibu kujua chanzo cha kifo cha Muigizaji huyu mahiri wa filamu hapa nchini.Baadhi ya filamu alizowahi kuigiza Mzee Mnento ni Hero of the church, Dar to Lagos, Fake pastor n.k 
  Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

  0 0  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Dkt. Norman Sigela (wa pili kulia) pamoja na Meya wa jiji la Mbeya Ndugu Athanas Kapunga (kulia) wakipokea kadi ya ushabiki ya Mbeya City Football Club kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndugu Jema Msuya (wa tatu kushoto). Wa pil kushoto kwenye picha ni Mkurugenzi wa masoko wa benki ya Posta Mr Deogratius Kwiyukwa. Chini ni viongozi na wachezaji wa Mbeya City.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kupiga picha ya pamoja na na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma Ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete  kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya tasnia ya muziki nchini. Bendi hiyo kongwe imetimiza miaka 50 mwezi huu. Picha na Freddy Maro


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya utumishi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam .

  Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume yaUtumishi wa Umma lililofanyika jijini Dar es Salaam leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume ya Umma lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) pamoja na makatibu wakuu Kiongozi wastaafu Matern Lumbanga(kulia) na Philemon Luhanjo(kushoto).(picha na Freddy Maro)

  0 0

  cid:image001.png@01CFE2DB.2D4F7150
  East African Legislative Assembly

  East African Legislative Assembly, Kigali, October 30, 2014: EALA has this morning adjourned sine die (indefinitely) on the last day of business owing to a quorum hitch.
   The Rules of Procedure (Rule 13) provide that the quorum of the House shall consist of half of the elected Members provided that such quorum shall be composed of at least three of the elected nine Members from each Partner State.

  Only two Members of the Assembly from the United Republic of Tanzania were present in the House this morning.  Kenya had 8 Members, Burundi 8 Members, Uganda 7 Members and Rwanda 9 Members, during the roll call by the Speaker.

  Hon Susan Nakawuki brought the matter of objection to quorum to the notice of the Speaker, who suspended the House for 15 minutes in accordance with the Rules. Upon resumption, the numbers remained the same.

  As at the time of interruption, the Motion moved by Hon Dora Byamukama on Wednesday, October 29th, 2014, to remove Hon Shy-Rose Bhanji as a Member of the EALA Commission (EALA’s policy organ) by way of secret ballot was on the Order Paper.  Under the Rules of Procedure (Rule 18) any item of business standing on the Order Paper as at time of interruption shall be placed on the Order Paper for the next Sitting.

  The Motion moved under Article 31 (l) avers that the Member had exhibited misconduct while on an EU Benchmarking trip to BrusselsBelgium on October 7-11th, 2014 and attended by Members of the Commission and Chairpersons of EALA’s Committees.

  According to the Motion, the Member in question made derogatory remarks about some EAC Partner States, some Members of the Summit of EAC States and verbally insulted Members of the delegation.  

  The Resolution condemns and expresses displeasure in the mis-conduct of the Honorable Shyrose Bhanji.  

  The Motion was supported by Hon Abubakar Zein, Hon Christophe Bazivamo, Hon Bernard Mulengani and Hon Dr. Martin Nduwimana.  Others were Hon Hafsa Mossi, Hon Abdulkarim Harelimana, Hon Peter Mathuki, and Hon Mike Sebalu.

  Those who opposed the Motion were Hon Makongoro Nyerere, Hon Taslima Twaha, Hon Mumbi Ngaru and Hon Susan Nakawuki.

  In her contribution, Hon Shyrose Bhanji denied the allegations terming them as character assassination.  She urged the House that all allegations be put in writing to afford her an opportunity to formally respond.

  The Speaker has also announced in the House of the resignation of 5 Commissioners from the EALA Commission. The Members are Hon Abubakar Ogle (Kenya), Hon Christophe Bazivamo (Rwanda), Hon. Patricia Hajabakiga (Rwanda), Hon Hafsa Mossi (Burundi) and Hon Jeremy Ngendakumana (Burundi).

  This now means that for the Commission to transact any business it needs to be re-constituted according to Article 3 of the Administration of the East African Legislative Assembly Act.

  0 0


  0 0


  Right is Nahid Hirji, Facebook Head of Growth and Partnerships; David Zacharia, Tigo Head of Data and Devices and Miss Iku Lazaro, Shule Direct Communications Director.
   Kwa mara ya kwanza, wanafunzi Tanzania wanaweza kujipatia nyenzo za kujifunzia masomo ya sekondari bila gharama yoyote kupitia mpango wa Facebook wa Internet.org.

  Mfumo wa masomo ya digitali wa Shule Direct ni mpango wa kwanza wa aina yake Tanzania, mfumo huu unawapatia wanafunzi na walimu nyenzo za masomo zenye ubora wa hali ya juu zilizotengenezwa kufuata mfumo wa elimu ya Sekondari ya Tanzania.
   
  Watengenezaji wa nyenzo zinazopatikana Shule Direct ni mabingwa katika fani ya elimu, hii inahakikisha kuwa nyenzo zipatikanazo Shule Direct ni sahihi, zinapitiwa na kuhakikiwa mara kwa mara kwa ajili ya maboresho, hivyo zina ubora wa hali ya juu.

  Mfumo wa masomo wa kidigitali wa Shule Direct unampa mwanafunzi uhuru wa kujisomea, kujadiliana na kubadilishana mawazo na wanafunzi wenzake wakati wowote na mahali popote.

  Kupitia Shule Direct wanafunzi wanaweza kujisomea matini (“notes”), kujibu maswali ya majaribio, pia wanaweza kushiriki mijadala mbali mbali na wanafunzi wenzao na walimu. Mijadala hii inasimamiwa na msimamizi kutoka Shule Direct kuhakiki matumizi salama ya mtandao wa Intaneti na kuwa haki za wanafunzi na watu chini ya umri wa miaka 18 zinahifadhiwa.

  Ushirikiano wa Shule Direct na Internet.org ni hatua madhubuti katika kuhakikisha teknolojia iliyopo inatumika kuboresha elimu Tanzania. Ushirikiano huu umekuja wakati muafaka, na ni faida kubwa kwa Shule Direct kwa vile kwa mpango huu nyenzo zetu sasa zitawafikia wanafunzi wengi zaidi.

  Internet.org ni mpango wa Facebook ambao unalenga kuwezesha watu wengi zaidi ambao hawana namba ya kuunganishwa na Intaneti, kuweza kupata namna ya kutumia Intaneti, na kujipatia huduma mbali mbali muhimi k.v. tovutu ya Shule Direct na nyinginezo nyingi zipatikanazo kupitia Intaneti.

  Mpango huu wa Internet.org unapatikana kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kwa sasa.  Jifunze. Jadiliana. Wakati wowote. Mahali Popote.


  0 0
 • 10/30/14--11:14: Taswira ya leo


 • 0 0


  0 0

  Marehemu Meja Jenerali (mst.) Aidan Isidore Mfuse 
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa akipata matibabu.

  Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo.

  Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe                  01 Novemba 2014, kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe  02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.  

  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


  Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963


  0 0

   Mashabiki wa timu ya  Sifa Politan wakishangilia timu yao kwenye uwanja wa Bandari, Tandika, jijini Dar es salaam.
   Mashabiki wa timu ya Tabata FC wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Sifa Politan kwa mikwaju ya penalti 4-3.
   Kipa wa Sifa Politan akiruka bila mafanikio kujaribu kuokoa penalti iliyopigwa na Kudura Shaban wa Tabata FC. 
  Heka Heka katika lango la timu ya BOOM FC.
   Mashabiki  soka wakifuatilia pambano la Sifa Politan na Tabata FC kwenye Uwanja wa Bandari. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 623 | 624 | (Page 625) | 626 | 627 | .... | 3284 | newer