Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 60 | 61 | (Page 62) | 63 | 64 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Baadhi ya Wakazi wa jiji la Dar wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa mbalimbali  milipuko ikiwemo homa ya matumbo,kufuatia kuwa na tabia ya kula kula vyakula ambavyo haviko katika hali/mazingira ya kiafya na salama zaidi,hasa ukizingatia msimu wa mvua umekwishaanza ambao ni rafiki sana kwa magonjwa ya milipuko.Pichani ni baadhi ya wateja wakila vipande vya samaki aina ya pweza,ambavyo vimeachwa wazi pasi kufunikwa ama kuwekwa tahadhali yote yote ya kulinda afya wateja wake,hali ambayo inaweza kusababisha magonjwa ikiwemo homa ya matumbo.

  0 0

  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi mpya wa Taasisi ya FES ya Ujerumani, Rolf Paasch, wakati Mkurugenzi huyo na Mkurugenzi wa zamani wa Taasisi hiyo anayemaliza muda wake, Dk. Stefan Chrobot (kulia) walipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
  MKURUGENZI Mkazi wa zamani wa Taasisi ya FES ya Ujerumani Dk. Stefan Chrobot (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi mpya wa taasisi hiyo Rolf Paasch, wakizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Oganaizesheni, Dk. Muhammed Seif Khatib (kulia) wakati Mkurugenzi wa zamani anayemaliza mudu wake alipofika kumtambulisha mwenzake mpya, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Machi 5, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0
 • 03/05/13--03:58: KUMBUKUMBU
 • Marehemu Bwana Ali Shariff Mussa Al Shirazi,baba yetu mpendwa alifariki siku ya kama leo tarehe 5/03/1988 ameshatimiza miaka 25 tokea kufariki. Baba yetu tunakukumbuka sana kwa upendo wako na Imani na uchangiaji wako wa kuondosha utumwa na ubaguzi wa makabila Zanzibar .

  Na kuwapa uongozo mwema watoto wako na watoto wa wenzako ambao leo wengi wao ndio Viongozi Wakuu wa Tanzania na Zanzibar. {Hivyo washirazi walianza kujikusanya na kuunda jumuiya yao iliyojulikana Jumuiya ya Washirazi, au Shirazi Association. Jumuiya hii ilianzishwa mnamo mwaka 1940 na washirazi huko Pemba. Muasisi wa Jumuiya hii alikuwa Bwana Ali Sharif Mussa Al Shirazi wa Pandani.

  Wakati akitoa hoja ya kuanzisha jumuiya hii, Bwana Ali Sharif alimuandikia barua mkuu wa wilaya wa serikali ya kikoloni huko Pemba kwamba kati ya wenyeji 73,000 wa Pemba asilimia kubwa yao walikuwa washirazi.

  Hivyo basi alifafanua kwamba jumuiya yao ina malengo ya kujaribu kupata uwakilishi wa kitaifa kwa kuwa jumuiya ya waafrika inayotetea maslahi ya watu wenye asili ya kibantu ilikuwa haiwawakilishi watu wa Pemba kwa kuwa watu wa asili hiyo walikuwa wachache huko Pemba’’ (http://mzalendo.net/habari/dr-shein-enzi-za-wizara-ndogo-ya-kisonge-zimekwisha-chonde-chonde.html)

  Mpaka sasa unakumbukwa sana,Wewe ndio mtu wa mwanzo aliyemuandikia barua Mkoloni na kuwaendea mpaka Mahakama za nyumbani kwao (Lancaster House) kutetea haki za wazanzibari na kuondosha utumwa na ubaguzi wa aina zote. Baada ya kuchaguliwa kuwa Mtunga Sheria 1948.

  Muasisi wa mwanzo( ASP) huko Pemba na (ZPPP).Baba yetu mpendwa tunakuombea dua wewe na wote waliotangulia mbele ya haki Mola azilaze roho zenu mahala pema peponi.(Amin) Watoto wako ( HASANAT,KHALILA,THAMRA,RIDHWANA,AHMED,HABIB,ZAHID,SHARIFF,SALIM, MOHD)

  0 0


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda wa promoshei yake kabambe ya AMKA MILIONEA pamoja na sambamba na kuongeza kiasi kikubwa cha MPUNGA ili wateja wake kuendelea kujizolea mamilioni zaidi

  Meneja Uhusiano wa Airtel ametuhabarisha kuwa promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 hapo awali na kufanikiwa kuzawadia  zaidi ya milioni 400 kwa wateja wameamua kuiendeleza ili wateja waendelee kufaidi zaidi

  “promosheni inaendelea sasa! Kila mteja wa Airtel anaweza akashiriki kwa kutuma neno MILIONEA au SHINDA kwenda 15595 na ataunganishwa bure

  Zawadi zimeongezeka kila siku kutakuwa na washindi 10 watakaojishindia mamilioni kama kawa!!!

  AMKA MILIONEA itahakikisha kila siku kunawashindi 10 kushinda kila siku na watagawana jumla ya shilingi  3,000.000, kila wiki jumla ya shilingi milioni 6,000,000 zitashindaniwa na washindi 10 na kila  mwisho wa mwezi  mshindi wawili watashindania na kugawana kitita cha shilingi milioni 30 wakati milioni  50, 0000Tshs itaenda kwa mshindi mmoja mwisho wa promosheni hii.
  Taarifa zaidi kwa mshiriki 
  Vigezo Muhimu 
  Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 ya kwa zawad ya kila siku .
  Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 yakwa zawadi ya kila wiki Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 zawadi ya kila mwezi.
  Mshiriki mmoja unaweza kushinda mara moja zawadi ya kila siku, mara moja zawadi ya kila wiki  na mara 1 zawadi ya kila mwezi. Lakini pia anaweza akajishindia zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni


  Kujiunga 
  Tuma neno "WIN / Shinda", kwenda namba 15595 ( bure), na kisha utapokea ujumbe wa ukaribisho utakaombatana na maswali utakayojibu.

  Kila jibu sahihi mteja atapata pointi/alama 20 na akikosea atapata pointi 10 zitakazomuwezesha kushinda, ukijibu maswali mengi unajiongezea nafasi ya ushindi.

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Kivuko cha MV Musoma, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara. Kutoka (kulia) kwake ni mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Bw. John
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi uzinduzi wa Kivuko cha Mv Musoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013, kijiji cha Kinesi Wilayani Rorya.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akibonyesha kitufye kupiga alam, kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Musoma, wakati wa uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013 katika kijiji cha Kinesi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akipiga makofi kufurahia uzinduzi huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakiwa ndani ya Kivuko cha Mv. Musoma baada ya kuzinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais, leo Feb 5, 2013 wilayani Rorya kijiji cha Kinesi mkoa wa Mara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa MKoa wa Mara, John Tupa, pamoja na viongozi wa Chama na Serikali, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu baada ya uzinduzi huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Chama na Serikali, wakati akitoka kukagua Kivuko cha Mv. Musoma, baada ya kukizindua rasmi leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi wilayani Rorya. Picha na OMR.

  0 0

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (katikati) akiwa na Mh. Benedict Mwingwa Msajili wa Mahakama Kuu (wa kwanza kushoto) na Mh. Amiri Msumi Msajili wa Wilaya Mahakama Kuu kanda ya Dar eas salaam wakizungumza na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Naibu Waziri katika Mahakama za Mwanzo jana Wilayani Ilala jijini Dar Es Salaam.
  Mh. Ally Katembo Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Ilala Pangani jijini Dar es Salaam akisoma taarifa mbele ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara katika Mahakama hiyo jana.
  Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo na Mahakama ya Wilaya Ilala wakimsikiliza Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki alipofanya Ziara Mahakamani hapo jana jijini Dar Es Salaam.
  Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Buguruni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo kutembelea Mahakama za Mwanzo Wilayani Ilala jijini Dar Es Salaam jana.

  0 0   Msikilize Afande Kenyela akiongelea tukio zima la moto huo eneo la tukio.
   Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security wakiendelea kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo,ambao tayari ulikwisha teketeza mali nyingi.
  Moto mkubwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo kama uonekanavyo pichani.
  Moto mkubwa umezuka na kuteketeza mali mbalimbali zilizokuwemo kwenye moja ya ghala kubwa la kuhifadhia vitu mbalimbali ikiwemo vikombe vya udongo,Pampas,vigae na vitu vingine,sehemu ya maghala ya kuhifadhia vitu Shekilango,jijini  Dar,aidha kufuatia tukio hilo mpaka Globu ya Jamii inaondoka eneo la tukio,hasala naa gharama za mali zilizoteketea haikuweza kufahamika mara moja,aidha kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Wilaya ya Kinondoni,Afande Kenyela alieleza kuwa mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika isipokuwa juhudi za kuuzima moto zilikuwa zikiendelea kwa juhudi kubwa.Picha zaidi bofya michuzijr.blogspot.com

  0 0

  Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael akiongea kwenye simu na mmoja wa washindi aliejishindia shilingi Milioni 5 katika Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu na Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw. Abdallah Hemedy,ambapo wakazi ya jijini Dar es Salaam Bw.Ramadhan Kibanike(62)na Bi.Maselina Apolinali wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano tano kila mmoja.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (katikati)akiwasiliana na Bi.Maselina Apolina,mkazi wa jijini Dar es Salaam ukonga magereza alieibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni tano katika Promosheni ya"MAHELA"inayoendelea kuchezeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom,zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Bw.Benjamin Michaelna kulia ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy.
  Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael akiongea na waandishi wakati wa kuchezesha droo ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo wakazi ya jijini Dar es Salaam Bw.Ramadhan Kibanike(62)na Bi.Maselina Apolinali wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano tano kila mmoja.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu na kulia ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw. Abdallah Hemed.

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Solomon Mukubwa ameibuka kidedea kwa wasanii wa nje watakaoshiriki Tamasha la Pasaka mwaka huu.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa mashabiki wengi wamempigia kura Mukubwa kuomba ashiriki kwenye tamasha la mwaka huu kama ilivyokuwa matamasha yaliyopita.

  “Kwa hiyo leo naomba kumtangaza Mukubwa, ambaye ni raia wa DRC lakini anayeishi Kenya kwamba ni mwanamuziki wa kwanza nje ya Tanzania ambaye tayari kamati imeafiki ashiriki tamasha letu,” alisema Msama. Alisema maandalizi yanaenda vizuri na idadi ya wasanii kutoka nje ya Tanzania waliopendekezwa ni kubwa, lakini wanachokiangalia si kupendekezwa tu lakini pia nafasi ya msanii husika kuja kwenye tamasha hilo.

  “Msanii akishapendekezwa vya kutosha kwa njia ya kura za maoni ambazo ni kupiga simu au kutuma ujumbe wa simu ya mkononi kwa kamati,  kinachofuata ni mazungumzo kati ya sisi waandaaji na msanii na tukifikia makubaliano ndiyo tunamtangaza,” alisema Msama.
  Mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu mwenye ulemavu wa mkono mmoja, anatamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

  Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Wasanii ambao mpaka sasa wameshatangazwa kushiriki ni Rose Muhando, John Lissu na Upendo Nkone ambao wote ni Watanzania.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0

  Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akitoa pole kwa mama mzazi wa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana CCM,Marehemu Benson Mollel aliyefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha katika hoteli moja jijini Arusha.
  Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapa pole baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu Benson Mollel wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu,Daraja Mbili Jijini Arusha jana.

  Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akiwa na mwenyekiti wa CCM Monduli  Ruben Kunei (kulia) na mjumbe wa halmashauri kuu taifa NEC Mathias Manga (kushoto) wakati walipohudhulia msiba huo.

  0 0

  SAKATA la serikali kuikataa katiba ya TFF imechukua sura mpya baada ya katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah kumtaka Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amos Makala kujiweka pembeni na kuacha kuzungumzia masuala ya uchaguzi wa shirikisho hilo.

  Angetile aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa Makala alishaonyesha kuwa ana upande anaoupendelea ndio maana alitoa maoni yake kama mdau alipokuwa jimboni kwake Mvomero na alipofika Morogoro mjini akadai lazima Serikali itoe tamko zito.

  "Katika suala hili tunamuomba Makala akae mbali ameshaonyesha interest, Waziri (Dk Fenela Mukangara) bado tunaimani naye, tumeomba kikao kifanyike kesho kutwa (kesho) Alhamis na kama itashindikana basi kifanyike baada ya tarehe 13 kwa kuwa hapa katikati kuna vikao vya CAF (Shirikisho la Soka Barani Afrika).

  "Serikali sio Wizara peke yake ni pamoja na sisi kwa hiyo ikitoa maagizo itoe yanayotekelezeka sio maelekezo ambayo ni vigumu kutekelezeka."alisema Osiah ambaye pia aliwataka waliopoteza sifa za kuingia TFF kuacha kuongea ongea ovyo kwenye vyombo vya habari kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mpira hali kadhalika kwa waliofungua kesi Mahakamani kupinga mchakato wa uchaguzi.

  Akizungumzia kauli hiyo ya Angetile, Makala alisema anaheshimu kauli iliyotolewa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga wiki iliyopita ya kuomba kukutana na Waziri kujadili suala hilo lifike mwisho na kudai kuwa kauli ya katibu huyo wa TFF ni yake binafsi na si msimamo wa shirikisho.

  " Angetile anaupande ndio maana mimi nilipotoa maoni yangu kama mdau ilimuathiri yeye na mgombea wake, niliwaudhi, alafu hawezi kusema nikae pembeni wakati michezo ni eneo langu katika kazi, wapende wasipende suala lao mimi ndio ninayelisimamia.

  Mapema mwezi uliopita kamati ya rufaa chini ya Idd Mtiginjola ilimuengua mgombea wa nafasi ya urais Jamali Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 kwa madai ya kukosa uzoefu, na Naibu Waziri Amos Makala alikaririwa akitoa maoni kama mdau wa michezo alisema ameshtushwa kwa Malinzi kuenguliwa na kudai kamati ya rufaa imenunua dharua kwa gharama ndogo.

  "Bila kupepesa macho wala kuumauma maneno, nikiwa mdau wa soka na kuuvua wadhifa wangu wa unaibu waziri, hapa kuna tatizo kwani kamati haijamtendea haki Malinzi," alikaririwa Makalla.

  Hata hivyo jana alisisitiza: "Kwa taarifa yao Waziri kasafiri kwa siku 10 nina maelekezo yote ya suala lao hivyo waje nilishasema milango ipo wazi, wasichague nesi wakati wapo leba, kwanza aliyefikisha suala hili kwenye matatizo ni Angetile mwenyewe baada ya kufanya makosa yake ya kiutendaji nilidhani angekaa kimya na kutafakari makosa aliyofanya badala ya kuongea ongea."alisema.

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mkwakyembe(mwenye tai nyekundu), akiangalia mataruma 35 yaliyoibiwa kutoka katika stesheni ya Reli ya Pugu na kusafirishwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuja kuuzwa kama chuma chakavu . Kulia kwa Waziri wa Uchukuzi ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa tai ya mistari).
  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba akipata maelezo na mataruma yaliyobiwa kutoka kwa ACP Saada Haji ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi Cha Polisi Reli, wakati walifanya ziara ya kuangalia mataruma ya reli yalyibiwa katika vipindi tofauti tofauti yaliyopo katika eneo la Mivinjeni kurasini. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini Uchukuzi).

   Shehena ya mataruma ya zaidi ya Tani 15 yaliyokamatwa na askari wa kikosi cha reli yakiwa katika eneo la reli Mivinjeni baada ya kukamatwa tarehe 14/2/2013 na dreva wa Lori hilo kukimbia. Waziri wa Uchukuzi na Naibu Waziri wamefanya Ziara katika eneno hilo leo kujionea mzigo wa Mataruma yaliyobiwa katika vipindi tofauti tofauti.
  Waziri wa Uchukuzi.Dkt Harrison Mwakyembe (mwenye tai  nyekundu),akipata maelezo kutoka kwa ACP Saada Haji Mkuu wa kikosi cha Polisi (Reli)(aliyevaa hijabu) ya namna wezi wa Mataruma hayo walivyoiba na kukamatwa na askari wake tarehe 14 Februari 2013. Kulia kwa ACP Saada Haji, ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba.


  Magunia yaliyotumika kufunikia mataruma ya Reli ambayo yaliibiwa na kusafirishwa kutokea Tabora tarehe 14/2/2012 na kubebwa kwenye Lori la Mizigo la Kampuni ya Unga ya Azania (linaloonekana mbele) kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuuza kama chuma chakavu. Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba wamefanya ziara ya kuangalia mataruma hayo leo mchana jijini Dar es Salaam. Mataruma hayo yamehifadhiwa katika yadi ya Reli iliyoko Mivinjeni Kurasini, Dar es Salaam.


  0 0


  0 0
 • 03/05/13--08:01: Article 10


 • 0 0

  Wakazi wa mikocheni, eneo la Regent Estate jijini Dar es salaam wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu katika kipindi hiki cha kuelekea mvua za masika kutokana na maji ya taka ikiwemo kinyesi, yanayotoka kwenye nyumba zote zilizoko mtaa wa Mgombani, kutiririka juu ya mtaro uliokuwa ukitumika kupeleka takataka hizo baharini kama inavyoonekana katika picha. 

  Wakazi hao hasa waliopo katika makutano ya mtaa wa Mgombani na njia ya kuelekea mtaa wa Chwaku (nyuma ya Shoppers Plaza) wameieleza Globu ya Jamii kwamba wamepitia njia zote za uongozi kuanzia kwa serikali ya mtaa, diwani hadi uongozi wa juu wa manispaa ya Kinondoni bila mafanikio. 

  Uongozi wa DAWASCO ambao ndio wanahusika na suala hili walipoambiwa na wakazi wa maeneo hayo walidai kwamba pump ya kunyonya maji hayo kuyapeleka baharini imeharibika na hawana namna nyingine ya kufanya ingawa Ankara zao za kila mwezi zinalipiwa huduma hiyo. Hali hii imekuwa hivyo toka mwezi wa nane 2012 hadi leo. 

  Na jambo la hatari zaidi ni kwamba maungio ya mabomba ya maji masafi yapo katikati au yamefunikwa na kinyesi hicho. 

  Wadau mnaombwa ushauri. Kama vipi tumepanga kuandamana...
   Mkazi wa mtaa wa mgombani.
  Mtaa huo pia ni makao makuu ya taasisi za utafiti maarufu nchini, ikiwemo REPOA na 
  IPSOS SYNOVATE ambazo bila shaka zitatoa tafiti kuhusu madhara ya mitaro hiyo iliyojaa kinyesi....
  Mtaro mchafu
  Maji yaliyojaa kinyesi kutoka katika vyoo vya mitaa yote ya hapo
  Hatari kwa wakaazi na hata wapita njia


  0 0
 • 03/05/13--08:21: Article 8


 • IMED invites applications for admission into the above course.

  Why choose our Certificate Program over others?

  ·         We have passionate, well trained and experienced teachers, including practicing entrepreneurs and professionals;

  ·         We have a strong focus on building confidence, creativity, assertiveness, responsibility, independence, persuasiveness and honesty among learners

  ·         We develop practical skills. Our students create and operate businesses as part of their study. Our student run companies that won the 1st and 2ndrunners up award in 2012 Junior Achievement Company Program in Tanzania.

  Duration and starting date of the Programme

  ·         The classes will start on 8th April 2013 and the program takes one year

  Admission Requirements

  ·         Form 4 with passes in at least any four subjects OR Level 3 Vocational Certificate in any occupational subject (NVA Level 3).

  Application Procedure

  Collect, complete and submit Application Form from our offices (see below) or download from our website before 20th March 2013.

  Contacts.  Principal IMED, 7th Floor, Mwalimu House, Uhuru Street, Ilala, P.O.Box 35036,

  Dar es Salaam, Tanzania, Mobile: (+255) 765 111100/718 400884, 

  0 0


                                           Mr. Kenneth Wanyoto

  Tanzania Breweries Limited (TBL) Human Resources Director, Kenneth Wanyoto, has been recently promoted and appointed to the post of Human Resources Director for SABMiller Africa with effect from 1st May 2013, and will based in Johannesburg, South Africa.

  Kenneth joined TBL on 1st October 2011 as Human Resources Director. Prior to this, he held the position of Human Resources Director at Nile Breweries in Uganda from 2003.

  Ken started his career as a brewer in 1992 and in 2001, he joined Nile Breweries as the Training Manager and his career progressed swiftly to becoming the Human Resources Director in 2003.

   In 2007, he expanded his knowledge of the business in the role of Operations Director, returning to the position of HR Director in 2009 supporting both the Beer and a newly acquired Water business of Rwenzori Bottling Company in Uganda.

   He holds a BSc. Industrial Chemistry and a Post Graduate Diploma in Brewing and Distilling.

  0 0

  Benki za Biashara Nchini zimetakiwa kuzingatia mahitaji ya wananchi katika kuchukuwa sarafu na noti zenye kuleta uwiano kwenye matumizi ya kibiashara. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito huo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Benki Kuu cha kutunzia na kusambazia sarafu katika Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ } Tawi la Chake chake Pemba. 
  Balozi Seif alisema yapo mafanikio miongoni mwa Wananchi kuhusu uhaba wa sarafu na noti za thamani ndogo kwa mahitaji ya chenji, uchakavu wa noti na kupeleka hisia za wasi wasi kuhusu ubora wanoti zilizopo kwenye mzunguuko. 
  Aliwataka Wananchi kuacha kutumia noti zilizomaliza uhai wake katika mzunguuko na badala yake wazirejeshe Mabenki kwa lengo la kubadilishwa. Aliupongeza Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa kazi kubwa unaofanya na kujituma kwao hadi kuinua hadhi ya Benki ya kwa kufikia kiwango kinachokubalika. 
  Alisema kufunguliwa kwa Kituo cha Benki Kuu cha kutunzia na kuchukulia sarafu katika Benki ya Watu wa Zanzibar ni ushahidi wa wazi kuwa PBZ iko imara na kuaminiwa na Benki Kuu ya Tanzania {BOT }. 
  Balozi Seif alisisitiza kwamba Kituo hicho hivi sasa kitawezesha Benki ya Watu wa Zanzibar kupunguza gharama za usafirishaji wa noti na sarafu sambamba na kuzuia uwezekano wa kupata majanga kwenye zoezi hilo. 
  “ Benki imekuwa ikisafirisha wastan wa shilingi Bilioni nne hadi Tano kwa mwezi kwenda Pemba kwa miezi ya kawaida lakini usafirishaji unakuwa mara tatu kwa wiki wakati wa msimu wa Karafuu”. Alisisitiza Balozi Seif. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alielezea matumaini yake kwamba Benki ya Watu wa Zanzibar itazingatia mahitaji ya wateja na kuwapatia wanachokihitaji kwa wakati hasa ikizingatiwa ishara ya kukua kwa uchumi wa Kisiwa cha Pemba uliosababishwa kufunguliwa kwa Kituo hicho. 
  Akitoa Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania { BOT } Naibu Gavana wa Benki Kuu Sera za Uchumi na Fedha Dr. Natu Mwamba alisema uamuzi wa akuanzishwa kwa Vituo kama hivyo umelenga kupunguza ao kuokoa kabisa usumbufu wa upatikanaji wa Farafu hapa Nchini. 
  Dr. Natu alieleza kwamba ili kuhakikisha huduma hizo zinawafikia Wananchi walio wengi hasa Vijijini vituo zaidi vitaongezwa katika maeneo mbali mbali Nchini. 
  “ Benki Kuu ya Tanzania { BOT } tayari imeshafunguwa Vituo vya kutunzia na kusambazia noti na sarafu katika kanda za Mbeya, Mwanza, Arusha na Zanzibar na mipango iko katika hatua za mwisho kufungua chengine sumbawanga”. Alifafanua Dr Natu. 
  Naibu Gavana huyo wa Benki Kuu ya Tanzania alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana lakini bado zipo baadhi ya changamoto kama baadhi ya watu kuzitumia noti wakiwa na uchafu . 
  Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Nd, Juma Amour Mohammed ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuichagua PBZ kuwa na Kituo cha kutunzia na kusambazia sarafu na noti baada ya kuridhika na vigezo vyote ilivyovitoa. 
  Nd. Juma Amour alieleza kwamba uwekaji wa Kituo hicho Kisiwani Pemba ni ishara ya kukuwa kwa uchumi wa Kisiwa cha Pemba ikiwa pia miongoni mwa huduma za maendeleo kwa kusogeza huduma karibu na Jamii. 
  Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Watu wa Zanzibar alifahamisha kwamba Benki zilizopo Zanzibar hivi sasa zitaweza kutoa huduma kwa urahisi kwa kukitumia kituo hicho. 

  Imetolewa na Othman Khamis Ame.
   Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 5/3/2013.

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  sambamba na Viongozi wa Taasisi za Fedha akisalimiana na Wananchi wa Chake chake katika sherehe za uzinduzi wa  kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha BOT katika jengo la People's Bank of Zanzibar (PBZ) mjini Chake Chake, Pemba, leo
   Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania { BOT } Dr. Natu Mwamba akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa Kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha BOT kiliopo katika Jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ } Chake chake Pemba.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikizindua rasmi kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha Benki Kuu ya Tanzania katika jingo la Benki ya Watu wa Zanzibar Chake chake Pemba.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa JUU WA Benki Kuu ya Tanzania BOT, PBZ na Wizara inayosimamia Fedha Zanzibar mara baada ya kukizindua Kituo cha kutunzia na kusambazia fedha kwenye jingo la PBZ Chake chake Pemba.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongezana Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ } Nd. Juma Amour Mohammed alipowasili jingo la PBZ Chake chake Pemba kukifungua kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha BOT. Pembeni yao ni Naibu Ghavana wa Benki Kuu ya Tanzania { BOT } Dr. Natu Mwamba. 
  Picha na Hassan Issa wa  OMPR  -  ZNZ.

  0 0

   Maya Azucena delivers remarks during a press conference announcing her visit held at the U.S. Embassy in Dar es Salaam today March 5, 2013. Pictured left to right are Public Affairs Officer Dana L. Banks, Maya Azucena, Chedi Ngulu and Gaidi Faraj from Mega Mark Entertainment.
  Ambassador Alfonso E. Lenhardt welcomes Maya Azucena to the U.S. Embassy in Dar es Salaam and presents her a Coin of Excellence today March 5, 2013.


  The American people through the United States Embassy in Dar es Salaam are proud to sponsor the visit to Tanzania of American singer Maya Azucena.  Ms. Azucena's visit from March 2 through 9 promotes cultural exchanges, women's empowerment and efforts against Gender Based Violence (GBV).  Maya Azucena is a women's rights activist and singer based in Brooklyn New York who has performed in several countries to promote the empowerment of women and girls, and raise global awareness against GBV. 


  U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt underscored that Maya Azucena's visit advances the United States' top priority to promote women's rights.  "As I have said previously, no nation which seeks to advance and develop, including my own can do so without welcoming the immense talents and contributions of women.  Every citizen has a responsibility to promote women's rights in their communities.  That is why promoting the rights and empowerment of women and girls is one of the United States' highest foreign policy priorities.  Maya Azucena's background is one of perseverance, hope, inspiration, and success.  Her messages of hope, healing, and women's rights through music have been welcomed in other nations."


  Maya Azucena is co-founder (along with Emmy-winning director Lisa Russell) of the multi-media website, MDGFive.com that uses all mediums of art to raise awareness for better maternal health. In addition to traveling and collaborating with international artists in Burma, China, the Philippines, Honduras, Tanzania, Sri Lanka, Russia, and others, she mentors teenagers and serves as a motivational speaker on the subjects of artistic entrepreneurship and achieving goals.


  Maya Azucena's visit to Tanzania is coordinated by Mega Mark Entertainment Marketing.  She will perform at Nyumbani Lounge on March 7 and at Triniti on March 8.  In addition, she will meet women and girls from Kiwohede Center for Women and Girls, and the Tanzania House of Talent.  She will also visit EngenderHealth's CHAMPION Project, a five-year initiative to increase men's involvement in preventing the spread of HIV in Tanzania supported by the United States Agency for International Development (USAID), a health clinic that is supported by USAID's MAISHA project and implemented by Jhpiego, an international non-profit health organization affiliated with Johns Hopkins University.  In all venues, she will engage in discussions with Tanzanian women to promote greater maternal health and raise awareness against gender based violence.  


older | 1 | .... | 60 | 61 | (Page 62) | 63 | 64 | .... | 3272 | newer