Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 612 | 613 | (Page 614) | 615 | 616 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akimsalimia Katibu wa CCM tawi la Kijiji cha Mkurupita, Kata ya Ndomoni, Nora Lwambano wakati alipokuwa akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa kata hiyo kwa ajili ya kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata hiyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo. Waziri Chikawe alitoa msaada wa madaftari na kalamu kwa ajili ya kuzisaidia shule za Msingi na Sekondari katika kata hiyo. Chikawe pia aliwaomba wajumbe hao washiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Ndomoni, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo. Waziri Chikawe alitoa msaada wa madaftari na kalamu kwa ajili ya kuzisaidia shule za Msingi na Sekondari katika kata hiyo. Chikawe pia aliwaomba wajumbe hao washiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi madaftari na kalamu Diwani wa Kata ya Ndomoni, Rafael Saanane kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe yupo jimboni humo kwa ajili ya kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi wake kupitia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM za Kata, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata za Jimbo hilo. Aidha, Chikawe aliwaomba wajumbe wa kata za jimboni kwake kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
  Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Ndomoni, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakishirikiana kubeba maboksi ya madaftari na kalamu msaada uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nchingwea, Mathias Chikawe kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe pia alizungumza na wajumbe hao na kuwaomba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akishangiliwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Naipanga, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM wa Kata hiyo, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee wakati alipokuwa akiondoka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kata hiyo. Waziri Chikawe aliwaomba wajumbe hao kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa. Picha na Felix Mwagara.

  0 0

  Wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma wakitumbuiza katika onesho lao la kusherehekea kutimiza miaka 50 toka kuanza kwa bendi hiyo lililofanyika katika viwanja vya Sigara Chang'ombe jijini Dar es Salaam.kutoka kushoto ni Said Mabela, Othuman Kambi na Mustafa Pishuu.
  Wacharaza magita wa bendi ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao hilo. kushoto ni Said Mabela na Mustafa Pishuu.
  Waimbaji wa bendi ya Msondo Ngoma wakitoa budurani kwa mashabiki wako wakati wa onyesho la muendelezo wa wiki ya kutimiza miaka 50 ya bendi hiyo lililofanyika katika viwanja vya Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam. kutoka kushoto ni  Othuman Kambi, Shabani Dede na Juma Katundu.Picha na Burudan Blog.

  0 0

  Maiti ya Mwanaume anayekadirikiwa kuwa na Umri kati ya miaka 25-35, imeokotwa asubuhi ya leo katika Mfereji wa Maji uliopo jirani na kiwanda cha kukoboa Kahawa (Coffee Curing), maeneo ya Majengo Fire, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
   
   Baadhi ya wananchi wakishangaa maiti ya mwanaume huyo (haupo pichani) ambaye jina lake na wapi na chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana 
   Huu ndio mfereji ambako mwili wa mtu asiyejulikana ulikokutwa leo asubuhi
   Wananchi wakishiriki kuupakiza mwili huo kwenye gari la Polisi.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Jamii Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Nelly Msuya (wa kwanza kulia) akiwaongoza waandishi wa habari na kujionea sehemu utakapojengwa mtambo wa kuzailsha gesi na zinapojengwa maabara katika shule ya sekondari Manzese. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa ujenzi wa mtambo wa nishati endelevu inayohifadhi mazingira (Biogas) kutoka UN-HABITAT Phillemon Mutashubirwa.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese wakishiriki kuandaa eneo utakapojengwa mtambo wa kuzailsha gesi shuleni hapo.
  Baadhi wa wananchi wa mtaa wa Chakula bora wakifanya usafi kuzunguka maeneo ya shule ya sekondari Manzese. (Picha zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO)

  0 0

  Kampuni ya simu za Mkononi ya Bharti Airtel yenye kufanya shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza mpango wa kuzindua huduma ya kutuma na kupokea pesa Afrika Mashariki. 
  Huduma hii ya kwanza barani Afrika itamwezesha Mteja wa Airtel kutuma , kupokea na kutoa pesa kutoka kwenye salio lake la Airtel Money Hatua ya awali ya huduma hii inategemea kuanza tarehe 1 November 2014 kwa kushirikisha nchi za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda ambapo huduma hii itaweza kupatikana kufatia kibali kutoka benki kuu ya serikali ya Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda cha kuendelea na uzinduzi wa mpango huu. 
  Hatua ya pili ya mwendelezo wa mpango huu kwa nchi nyingine za Afrika ambapo Airtel inaendesha biashara yake zinategemea kuanza mwakani. Akiongea wakati wa Mkutano wa Biashara kwa wakuu wa Makampuni katika nchi za Afrika Mashariki uliyofanyika Rwanda, Mkurugenzi na Mkuu wa kitengo cha Airtel Money bw, Chidi Okpala,alisema” hii ni hatua muhimu itakayowawezesha wateja wetu kuondoa vikwazo vya kutuma na kupokesa pesa nje ya mipaka ya nchi zao kiurahisi kuweza kufanya hivyo kwa kupitia huduma ya Airtel Money. 
  Huduma hii itatanua wigo, kutoa unafuu na kuleta urahisi kwa wafanyabiashara wadogo kufanya malipo ndani na nje ya mipaka ya nchi za Afrika Mashariki.” Aliongeza kwa kusema “huduma hii pia italeta fulsa za kibiashara, ni wazi kwamba huduma za kifedha kupitia simu ni muhimili mkuu katika ushirikiano wa huduma za kifedha na ndio dhamira ya serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania katika kuhakikisha inakuza shughuli za kibiashara ndani ya nchi za Afrika Mashariki.” Sambamba na hilo Hatua hii ya kwanza ya uzinduzi wa huduma hii pia itawawezesha wateja wa Benki ya Afrika nchini Kenya na Uganda kutuma na kupokea pesa katika nchi hizi mbili. 
   Huduma ya Airtel money ni huduma ya kifedha kupitia simu ya mkononi iliyo salama na rahisi inayowawezesha wateja kutuma pesa kutoka simu moja kwenda kwenye simu za mitandao yote, pia inamuwezesha mteja kununua muda wa maongezi kwaajili ya simu yake au kwa simu ya mtu mwingine. 
  Pia inawawezesha wateja kulipa ankra zao mbalimbali na kutoa pesa katika mashine za (ATM)’s Imekaririwa na jumuiya ya Afrika Masharika kwamba huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ni muhimu katika nchi hizi kutokana na urahisi, uharaka na inaokoa muda kwa wateja na wafanyabiashara. Uzinduzi wa huduma za kibunifu kama vile za mikopo, kuweka pesa, na kutoa huduma za bima zinazofanywa kwa kushirikiana na makampuni yanayotoa huduma za kibenki zimeleta mabadiliko chanya na kuongeza kasi ya ushirikiano wa kuvuka mipaka ya nchi.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigela(mwenye suti nyeusi)pamoja na Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City(kushoto)wakionesha hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 1/= kwa mashabiki wa timu yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na  Mkuu wa wilaya hiyo kwa niaba ya wadhamini wakuu wa ligi kuu Vodacom Tanzania hapo jana kabla ya mechi kuanza baina ya timu Mbeya City na  Azam FC,Ambapo Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli moja bila na anaeshuhudia kulia ni Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFU) Seleman Harub.  

    Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City akionesha kikombe chake
   mtanange ukiendelea katika ligi kuu ya vodakom katika
  uwanja wa sokoine
  Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli lao lililofungwa na  Aggrey Morris katika mzunguko wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya timu hiyo na Mbeya City hapo jana/juzi Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli 1-0.
  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke ofisini kwake vuga Mjini Zanzibar.
  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bwana Egon Kochanke akibadilisha mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika jitihada za kuimarisha ushirikiano kati ya Ujerumani na Zanzibar. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Mmoja wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku wa kuamkia leo katika tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
  Shaa na madansa wake wakilishambulia jukwaa. 
  Pichani kulia ni Msanii kutoka nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Kisanii Davido sambamba na Diamond Platnum kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014 usiku wa kuamkia leo.
  Msanii kutoka THT,Barnaba akiimba wimbo wake wa Wahalade sambamba na madansa wake kwenye jukwaa la fiesta 2014,katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
  Sehemu ya  umati wa watu waliokuwa wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.
  Ilikuwa ni shoo moja nzuri kutoka nyumba ya vipaji ya THT
  Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja.
  Anaitwa Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki  kuwa alifanyo shoo nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea kwenye kiti chake cha usanii.
    Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo
   Msanii kutoka nchini Marekani T.I akiwaimbisha mashabiki wake

  0 0

  Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Meneja wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya mchezo wa Pool, kitita cha Dolla 5000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 8,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Pool kitita cha Dolla 2000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 3,400,000/= mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Wachezaji wa Taifa wa mchezo wa Safari Pool Tanzania, wakishangila wakiwa na kitita cha Dolla 2000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali za Silva mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
  Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles), Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akihutubia Jumuia ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu katika Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, lililoandaliwa na Vijana wa CCM wa Vyuo Vikuu, kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, leo, Oktoba 19, 2014.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika Kongangamano hilo la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Nape amewataka wasomi kutofumbia macho matatizo ndani ya CCM, badala yake wakati wakisifu  mema wawe mstari wa mbele kuyafichua na kuyakemea mapungufu ili chama kiende na wakati
  Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana nabaadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini humo leo mchana.
  Maaskofu wakimwekea mikono ya Baraka Askofu mwenzao, Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristu, waliohudhuria katika Sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo Oktoba 19, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Oktoba 19, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu na wanafamilia ya Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya sherehe za kuwekwa wakhfu zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, machana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu wakati akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, leo Oktoba 19, 2014. Picha na OMR.

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe Anne Semamba Makinda akipata maelezo toka kwa Katibu wa Bunge la Oman,Ali Nasser Al Mahrouqi ya namna mfumo wa kisasa wa uendeshaji Bunge ulivyo katika Bunge la Oman. Bunge hilo limeanza mfumo wa kutotoa hotuba/nyaraka kwa makaratasi na sasa wanatoa kwa njia ya mtandao (e-parliament).Wa pili kulia Mhe Sheikh Khalid Hilal All Maawali akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Mhe Mussa Zungu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na Spika wa Bunge la Oman Sheikh Khalid Al Maawali.Mhe William Lukuvi ambae pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge ni miongoni mwa wabunge nane wanaoambatana na Mheshimiwa Spika katika ziara rasmi ya kibunge nchini Oman.
  Mhe Spika Sheikh Khalid Al Maawali akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Spika Makinda kuhusu ukumbi wa Bunge la Majlis A'Shura.
  Mheshimiwa Spika Makinda akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Oman TV kuhusu ziara yake.
  Mheshimiwa Spika akimkabidhi zawadi ya picha ya mlango wa Zanzibar Spika wa Bunge la juu la Oman Majlis Doula, Mheshimiwa Dr Yahya Al Mandhary.Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania Oman Mheshimiwa Ally Saleh.
  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Wabunge wenzake waliomo katika msafara. Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

  0 0
 • 10/19/14--15:02: CHINA KUWEKEZA BAGAMOYO
 • Na John Gagarini, Bagamoyo
  JIMBO la Jilin nchini China limekubali kuwekeza hapa nchini kwenye eneo la Uwekezaji la (EPZ) la Kamal lililopo Kijiji cha Kerege kwa Kikwete wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

  Uwekezaji huo utafanyika baada ya ujio wa baadhi ya viongozi wa Jimbo hilo kutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji wilayani humo na kuonekana kuvutiwa na sehemu hiyo.

  Akizungumza jana mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa akiongozana na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na sekretarieti ya mkoa wa Pwani na kuvutiwa na eneo hilo la uwekezaji la EPZ, Naibu Gavana wa Jimbo hilo Zhoncheng Sui alisema ameridhika na eneo hilo.

  Sui alisema kuwa kutokana na urafiki wa kihistoria uliyopo kati ya Tanzania na China toka enzi za viongozi wa mataifa hayo Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Sung kumekuwa na ushirikiano ambao ni wa damu hivyo lazima udumishwe kwa ushirikiano wa kimaendeleo.

  “Tumeona mambo mengi ambayo tunaweza kushirikiana ambapo moja ni pale kwenye eneo la uwekezaji ambapo tutakuja kuwekeza hapo kwani kuna miuondombinu mizuri ya barabara, maji na umeme pia waiteni na wenzetu waliopo hapa Tanzania ili nao waje wajionee na kuangalia namna wanavyoweka kuwekeza kwenye mkoa huu wa Pwani,” alisema Sui.

  Awali akimkaribisha naibu gavana wa Jimbo hilo la Jilin mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza alisema kuwa mkoa wa Pwani una mambo mengi ambayo wawekezaji wanaweza kuwekeza ikiwa ni pamoja na kwenye kilimo, uvuvi, utalii na mifugo.

  “Fursa zipo nyingi ndani ya mkoa wetu na hata miundombinu ya barabara, anga, bandari, uememe na reli viko vizuri kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji ambao una hitaji uwepo wa mawasiliano mazuri,” alisema Mahiza.

  Ujumbe huo ulikuwa na ziara ya siku moja wilayani Bagamoyo kutembelea maeneo ya uwekezaji kwenye ujenzi wa soko la kimataifa la samaki, eneo itakapojengwa bandari na eneo la uwekezaji la Kamal.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantumu Mahiza (katikati),Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Ahmed Kipozi (mwenye shati la kitenge) na Naibu Gavana wa Jimbo la Jilin nchini China Zongcheng Sui (pili kulia) wakiangalia bomba la maji ambalo limepasuka na kumwaga maji wakati ujumbe wa jimbo la China ulipotembelea jana eneo la uwekezaji la Kamal Kerege wilayani Bagamoyo.
  Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akiongea na Naibu Gavana wa Jimbo la Jilin nchini China Zhongcheng Sui alipotembelea wilaya ya Bagamoyo kuangalia maeneo ya uwekezaji.
  Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka jimbo la Jilin nchini China pamoja na watumishi wa wilaya ya Bagamoyo mara baada ya mkutano uliofanyika Oceanic Bay Hotel $ Resort mjini Bagamoyo.

  0 0


  0 0
 • 10/19/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Nay wa mitego Ft. Diamond platnumz - Muziki gani

  0 0

   Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Simon Delens, akizungumza wakati wa semina kuhusu utengenezaji wa bora wa matofali waliyowaandalia watengeneza matofali na wasambazaji wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Meneja Undelezaji Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Danford Semwenda, akitoa mada wakati wa semina kuhusu utengenezaji wa bora wa matofali waliyowaandalia watengeneza matofali na wasambazaji wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Meneja Afya, Usalama na ulinzi wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Alfred Anthony akizungumza wakati wa semina hiyo.
  Meneja Usambazaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Tumaini Joseph akizungumza wakati wa semina hiyo waliyowaandalia watengeneza matofali na wasambazaji wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Ofisa mahusiano na Huduma kwa Weteja wa Kampuni ya Twiga Cement (TPCC), Martha Haule (kushoto) akizungumza katika semina hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mmoja wa washiriki wa semina kuhusu utengenezaji bora wa matofali, Mary Kimaro (kulia) akipokea cheti kutoka kwa  Meneja Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya Twiga Cement (TPCC), Danford Semwenda mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo iliyoandaliwa na TPCC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja  Afya, Usalama na Ulinzi wa kampuni hiyo, Alfred Anthony.

  0 0

  Bi Rehema Salum Msambya pichani juu amepotea tokea tarehe 16/10/2014 maeneo ya Kigamboni - Kisota karibu na Shule ya Sekondari ya Abdu jumbe. 
  Siku hiyo alikuwa amevaa Dela Na Skintirt ya Rangi ya Blue. Bi Rehema ana Matatizo ya Akili. Yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kigamboni au kilicho karibu  au Apige simu namba
  0712 22 77 22
  0753 63 49 67
  0712 70 77 87
  0713 23 52 94

  0 0

  DSC_0135
  Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. 

  Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha mafunzo katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua uwanja zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ajali.

  Aidha amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na kuondoa tuhuma za rushwa.

  Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).

  washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
  DSC_0141
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph, akisalimiana naNaibu Kamishna waPolisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, mara baada ya kuwasili kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.


  0 0

   Kampuni ya SimbaNET (T) Linited ya jijini Dar es Salaam Jumamosi hii iliandaa bonanza la michezo lililowakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni hiyo na familia zao. Siku hiyo ilikuwa ni ya kula kunywa na kuchezo michezo ya aina mbalimbali ikiwepo soka, kuvutana kamba, kuogelea, muziki na michezo mbalimbali ya watoto. Kampuni ya Seree ndio walikuwa waandaaji wa tafrija hiyo iliyofanyika kwa mafanikio makubwa katika ufukwe wa Hoteli ya Bahai Beach.
   
   wafanyakazi na familia zao wakichukua kifuangua kinywa mara baada ya kuwasili bahari Beach Hotel.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  UNESCO-logo1
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati yake na mamlaka husika nchini Tanzania za kuwezeshwa kujengwa kwa bwawa la kufua umeme la Stiegler’s Gorge .

  Ofisi za Shirika hilo zilizopo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki wametoa taarifa ya kukanusha maelezo yaliyoandikwa na gazeti la The Guardian (ref:http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=72984) kwamba yapo maafikiano kuhusu ujenzi wa bwawa hilo.

  Eneo la Stiegler’s Gorge lipo katika hifadhi ya Selou ambayo ni sehemu ya urithi wa kimataifa ambapo ujenzi wa miundombinu yoyote yenye athari kubwa katika hifadhi hiyo lazima kuwepo na maridhiano kati yake na mamlaka husika.

  Taarifa hiyo imesema taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo Oktoba 8, mwaka huu limeshutua shirika hilo. Taarifa hizo zilizokuwa ukurasa wa mbele zilisema kwamba Tanzania itavuna zaidi nishati ya umeme kutokana na maafikiano yake na UNESCO juu ya ujenzi wa wa bwawa hilo.

  Katika taarifa yake UNESCO imesema kwamba katika mkutano wa 36 wa kamati ya Urithi wa dunia (WHC) uliofanyika Saint-Petersburg mwaka 2012 na ule wa 37 uliofanyika Phnom Penh, mwaka 2013 na wa mwisho uliofanyika Doha mwaka huu ulieleza wazi mashaka yake juu ya athari ya ujenzi wa bwawa hilo katika hifadhi.

  Katika mikutano yote hiyo ilikubalika kwamba mamlaka zinaozohusika nchini kutofanya shughuli zozote za maendeleo ndani na kwenye mipaka ya hifadhi bila kupata kibali cha WHC kwa mujibu wa kifungu 172 cha makubaliano.

  Aidha kamati hiyo iliitaka mamlaka zinazohusika kutekeleza ushauri uliotolewa na kamati ya pamoja kati ya WHC na Muungano wa ushirikiano wa hifadhi ya asili (IUCN) wa kutengenezwa kwa mkakati kabambe wa menejimenti ya Ekolojia ya Selous. Aidha inatakiwa kutayarisha menejimenti hiyo kwa kuweka mipaka katika eneo la urithi wa dunia na kuonesha maeneo ambayo yanastahili kuingizwa katika hifadhi.

  Pia kufafanua mradi wa Stiegler's Gorge, hatua iliyofikiwa hasa katika maamuzi na kuhakikisha kwamba ufahamu kuhusu athari, gharama, manufaa na namna inavyofaa au kutofaa na pia kuwa na mpango mbadala kama haikuwezekana. Mambo yote hayo yanatakiwa kuzingatia umuhimu wa eneo hilo kwa jamii ya dunia na hivyo kuangalia vigezo vyote vya maeneo ya urithi .

  Katika maamuzi hayo pia Kamati ya Urithi ilifurahishwa na nia ya mamlaka husika za Tanzania kuendesha utafiti huo kwa mujibu wa makabaliano na vigezo stahiki ili kuelewa athari zake katika hifadhi hiyo ambayo ni urithi wa kimataifa, korido za mapito ya wanyama na nini kitatokea kwa korido la Selous-Niassa Corridor.

  Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, kamati hiyo ya Urithi wa Dunia (WHC) ilitarajia kupata taarifa za awali Februari Mosi mwakani. Aidha taarifa hiyo ilitakiwa kuwa na muhtasari wa hatua mbalimbali zinazchukuliwa na muda wake kuhusiana na hifadhi ya Selou kujiondoa katika urithi wa dunia ulio katika hatari ya kutoweka.

  Imeelezwa kuwa taarifa hiyo ndiyo itakuwa msingi wa majadiliano katika mkutano ujao wa WHC wa 39 utakaofanyika Bonn Ujerumani. Aidha taarifa hiyo imesema kutokana na vitu vyote kutokuwa bado kufanyika msimamo wa UNESCO unabaki kama ulivyo, kwamba hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na kinyume na hapo ni kukiuka makubaliano.

older | 1 | .... | 612 | 613 | (Page 614) | 615 | 616 | .... | 3278 | newer