Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 611 | 612 | (Page 613) | 614 | 615 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Wachezaji wa Stand United wakifanya mazoezi yao ya Mwisho kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini tayari kwa kuumana na Wenyeji wao Kagera Sugar kesho Jumamosi tarehe 18, 2014

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Jumla ya wachezaji 26 wa Timu ya Stand United ya Shinyanga wametua mjini Bukoba leo  kwa ajili ya kipute cha Ligi kuu ya  Vodacom msimu wa 2014-15 na  wenyeji wao Kagera Sugar wamefanya mazoezi yao kwa mara ya kwanza Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba.
  Wachezaji hao, wakiongozwa na Kocha Mkuu Emmanuel Massawe pamoja na viongozi wengine,  ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda Ligi na kesho Jumamosi inataka kuibana Timu ya Kagera Sugar ambao ndio wenyeji wao ambao pia wanashikilia nafasi ya sita kwenye Ligi hiyo ya Vodacom kwa msimu huu ulioanza hivi karibuni. 
  Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Kagera wanaingia wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 4 huku Stand United wakiwa nafasi ya 8 nao wakiwa wanalingana pointi na Kagera Sugar.


  0 0  0 0

  On Sunday, November 2, 2014, the Julius K. Nyerere Commemoration committee will convene its 6th Annual program commemorating the life and work of Julius Kambarage Nyerere at Gallery Serengeti, located at 7919 Central Avenue, Capitol Heights, MD 20743, 301.808.6987 from 5:00 – 7:00 pm. 
  The exciting program will feature DC’s own singer/ songwriter Luci Murphy; dancer/singer/songwriter Anna Mwalagho from Kenya, well-known to the Tanzanian community; griot and master storyteller Baba-C; Dr. John Rutayuga of Ukimwi Orphans Assistance; Alexander Valentin Rodriguez Salazar, 2nd Secretary of the Cuban Interest Section, and drummer/dancer/African cultural expert extraordinaire Melvin Deal. 
  The Gallery is an apt venue for this important program, with
  its phenomenal African art displays, operated by Wisson West, who spent some of his formative years in Tanzania and has been a supporter of the Julius K. Nyerere Commemorations since their inception. 
  Our keynoter is Elvira Williams, Executive Director of A.H.E.A.D., through which she, with her husband/ partner Dr. Irving Williams, has for 32 years been providing critical maternal and infant care services in Tanzania, that have vastly improved that nation’s infant mortality rate.
  Invitees include representatives from the Tanzanian Embassy, Gloria Minott of WPFW-FM, DC’s own René Henry, and have included Dr. Baruch ben Yehudah of Everlasting Life Health Complex, Mwiza Munthali of TransAfrica and Jessica Mushala of S.H.I.N.A. Inc. The program will also feature a Tanzanian style auction of African art.
  Who was Julius Kambarage Nyerere and why should we commemorate his life and work?  Simply put, he was a man who built a political career fighting poverty, ignorance and disease – and winning! 
  This program was begun by Leticia Nyerere (now MP, Tanzanian Parliament) and local activist/admirer Rick Tingling-Clemmons, in collaboration with a number of Tanzanians, to commemorate the life and work of Julius Kambarage Nyerere, the first President of Tanzania, who was a visionary leader – kind, astute, a dedicated educator who led the nation to adopt Swahili as a national language and embraced the title Mwalimu, Swahili for teacher, and implemented Ujamaa, Swahili for collective work and responsibility.  
  He authored several books; was a tactician and a pan-Africanist who materially supported many of his fellow African nations’ liberation movements. Nyerere – a great human being generally, and a great African in particular.
  Commemorating his life and continuing his work should be seen as one of the keys that will unlock the miseries of today’s woes as we fight against poverty, ignorance and disease the world over.

  We encourage you to attend this family-friendly life-affirming event!

  Donations: $25 in advance; $35 at the door.  Refreshments served

  [checks should be made out to Rick Tingling-Clemmons; put ‘Nyerere Commemoration’ in legend]
                                                                                  

  For more information, contact Rick Tingling-Clemmons at miricotc@gmail.com or 202.388.1111.

  0 0
 • 10/17/14--15:18: ngoma azipendazo ankal
 • Cassim Mganga - I Love you

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana ( Mb) akizungumza hapo siku ya Ijumaa wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliokuwa ukihitimisha Wiki ya Afrika ambayo hufanyika kuanzia Octoba 13 na kuhitimishwa Octoba 17 ya kila mwaka. ni Wiki ambayo Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na washirika wengine wa Maendeleo huitumia kujadiliana, kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala muhimu ya kijamii, kiuchumi, kimaendeleo pamoja na hali ya amani na usalama. Vile vile hujadiliana mafanikio ya utekelezaji wa masuala hayo muhimu pamoja na changamoto mbalimbali ambazo bado zinalikabili Bara hili na namna ya kuzitafutia ufumbuzi.
  Mhe. Pindi Chana ( Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akiwa na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi.

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wakazi wote wa Mkoa wa Tanga ambao wanaendela na zoezi la ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili kwa awamu ya kwanza kuwa, Serikali imesikia kilio cha wananchi wake na hivyo inapenda kuwajulisha watendaji wote wa Serikali za mitaa ambao ndio wasajili kufungua vituo vya usajili saa 1.30 na kufunga saa 12.00 jioni.

  Kwa kuwa zoezi hili lilitakiwa kukamilika tarehe 17/10/2014, Serikali imeongeza siku za usajili kwa lengo la kuweza kuwasajili wananchi wote ambao hawajasajiliwa. Aidha, wananchi wote wanaoweza kujaza fomu za Utambuzi na Usajili, waruhusiwe kuzijaza na msajili aweze kuzihakiki fomu hizo mbele ya mwombaji.

  Kwa taarifa hii, Serikali inawahakikishia wananchi wote wa mkoa wa Tanga kuwa, wote watasajiliwa na hivyo inawaomba wote ambao hawajasajiliwa wajitokeze na kuwahi vituoni mapema kwa ajili ya kukamilisha zoezi la usajili wao. Napenda kuwahakikishia kuwa kila mtu mwenye stahili ya kusajiliwa atasajiliwa na kuwa kitambulisho cha Taifa ni haki ya msingi ya kila raia, mgeni mkaazi na mkimbizi mwenye umri wa miaka 18 na zaidi.

  Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

  Imetolewa na:-
  Mkurugenzi Mkuu
  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

  0 0
 • 10/17/14--23:35: HABARI NJEMA KWA WAKULIMA • 0 0

  Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama ‘Davido’ kuperform katika tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na Prime Promotion, October 18,2014.

  Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu , mheshimiwa D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Times Fm Radio na Times Fm Promotion.
  Times Fm Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura mahakamani hapo wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika tamasha hilo kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa kutoa kibali cha msanii huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini November 1 kwenye tamasha lililoandaliwa na Times Fm Radio,  Clouds Fm na Prime Times Promotion waliendelea na taratibu zote bila kujali zuio hilo la BASATA.

  Times Fm Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha madai yao dhidi ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni inayomsimamia Davido, HKN Music.
  Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu waliosababishiwa na walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.

  Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo October 18,2014 hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana Mahakamani hapo.

  Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza kuwa atakuja Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho linaloandaliwa na kituo hicho cha radio lililopewa jina la ‘The Climax’.

  0 0

  Mhe Spika wa Bunge Anne Makinda akiwa na Naibu Spika wa Majlis A'Shura Sheikh Abdullah Al Majaali aliempokea katika uwanja wa ndege wa Muscat International Airport.
  Mhe Spika akiwa na wenyeji wake pamoja na sehemu ya ujumbe wake.Wa kwanza Julia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Mhe Freeman Mbowe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge),Mhe William Lukuvi.Wa kwanza kushoto ni Mhe Ally Saleh Balozi wa Tanzania nchini Oman. Mhe Spika yuko katika ziara rasmi ya kibunge ya siku sita.
  Mhe Spika Anne Makinda wakati akipokelewa uwanjani Mara baada ya kuwasili.

  0 0


    Mwanamuziki kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Kisanii T.I akizungumza na Waandishi wa Habari jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa Sea Cliff hotel jijini Dar kuhusiana na onesho lake la kwanza atakalotumbuiza katika viwanja vya leaders Club,jijini Dar katika tamasha la Fiesta 2014,ambalo hufanyika kila mwaka mara moja,chini ya waandaji bingwa wa burudani hapa nchini kampuni ya Prime Time Promotions Lts sambamba na Clouds Media Group..
   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akitoa shukurani za dhati kabisa kwa wadau mbalimbali walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya tamasha la fiesta 2014, ambalo linatarajia kurindima usiku huu katika viwanja vya leaders Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo wasaniii mbalimbali wa ndani na nje pia watatumbuiza jukwaani,aidha kama vile haitoshi Msanii kutoka nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Davido amekiri wazi kuwa atatumbuiza usiku wa leo katika tamasha hilo,bila kikwazo chochote.
   Mwanamuziki kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Kisanii T.I (pichani kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa Sea Cliff hotel jijini Dar kuhusiana na onesho lake la kwanza atakalotumbuiza katika viwanja vya leaders Club,jijini Dar katika tamasha la Fiesta 2014,ambalo hufanyika kila mwaka mara moja,chini ya waandaji bingwa wa burudani hapa  nchini,Kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ikishirikiana na Clouds Media Group.
  Mwanamuziki kutoka Nigeria,ajulikanae kwa jina la Davido akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuwa atatumbuiza usiku wa leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 litakalofanyika usiku huu katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar.
  Mdau mkubwa wa mwanamuziki T.1 kutoka Dubai ,Rasheed Sazaf a.k.a Sazaf akipeana mkono na Mwanamuziki T.I jioni ya leo.

  0 0

   Kiungo wa timu ya Simba,Amri Kiemba akuchuana vikali na Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Andrey Coutinho wakati wa mtanange wa watani wa Jadi Yanga na Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
   Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga,Geilson Santos "Jaja" akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Simba wakati wa mtanange wa watani wa Jadi Yanga na Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.
   Golikipa wa Timu ya Simba,Manyika Peter Jr akinyaka vyema mpira mbele ya Washambuliaji wa Timu ya Yanga.
  Mchezaji wa Timu ya Simba Elias Maguri akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Yanga,Oscer Joshua katika mtanange wa watani wa Jadi Yanga na Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.


  0 0

   Ina nyumba mbili ndani kubwa na ndogo na zote zipo ndani ya fensi na kila moja inajitegemea luku yake na zote mbili system ya maji inafanya kazi safi kabisa na ndani kuna kisima cha maji cha umeme na kuna matanki mawili moja lina lita 5000 na lingine lita 2000 na maji yake yananyweka hayana chumvi.
  Nyumba kubwa ina vyumba vitatu kimoja masteroom na viwili single na kuna puplic toilet ipo ndani pia kuna store jiko sebure kubwaa na siting room kubwa, wakati nyumba ya nyuma ina chumba sebule na jiko pamoja na choo chake.
  Bei ni shilingi milioni 100 tu. Madalali hawatakiwi tafadhali
  Ukiihitaji mpigie Msafiri Kesi namba 0657040282

  0 0

  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Thomas Kashililah anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri kuwa Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza Jijini Dar es Salaam Jumatatu Oktoba 20,  2014. 

  Kwa tangazo hili waheshimiwa Wabunge wote mnaombwa kuwasili Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 19 Oktoba 2014.

  Kamati za Bunge katika vikao hivi vitakavyodumu hadi tarehe 2 Novemba 2014 zitapokea na kujadili pamoja na mambo mengine Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2014, Kukagua miradi mbalimbali, kutembelea Mamlaka ya Bandari, Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na kujadili Sheria ya VAT katika muktadha wa Sekta ya Elimu nchini. Pia zitapokea taarifa kuhusu Sheria ya mazingira inavyotekelezwa katika migodi ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, na North Mara, pamoja na kuijadili kwa ujumla taarifa ya CAG kuhusu ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu na mashirika ya umma kwa mwaka 2013.

  Aidha kutakuwa na maoni ya wadau kuhusu muswada ya Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2013 na kupokea taarifa kuhusu migogoro ya mipaka kati ya Hifadhi za Taifa za Saadani, Manyara, Tarangire, Mikumi, Ngorongoro, Ruaha na vijiji vinavyopakana na Hifadhi hizo.

  Imetolewa na Ofisi ya Bunge,

  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na

  Uhusiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam,


  18 Oktoba 2014


  0 0

  Balozi wa Tanzania  Ubeligiji (mwenye tai) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu vya Ubeligiji . Balozi Kamala kakutana na Watanzania hao Jumamosi jijini Brussels kuzungumzia maswala mbalimbali ikiwemo masomo na changamoto zake pamoja  na maendeleo ya nyumbani Tanzania.

  0 0
 • 10/18/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Mwasiti - Nalivua Pendo

  0 0

  President  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete presents to Kenyan photojournalist, Joseph Mathenge,  the top prize at this year’s CNN MultiChoice African Journalist 2014 Awards Ceremony held on Satuday night at the Mlimani City Conference hall in Dar es salaam. Looking on is Mathege's son, Geoff Kihato, also a photographer,  who helped his father capture the captivating images of  the Westgate Mall shoppers in Nairobi, Kenya, when the mall was attacked by unidentified gunmen in September 2013.
   Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa congratulates Mathenge as President Kikwete, Mathege's son Geoff Kihato and Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International,  (partially hidden) look on.

  President Kikwete, Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa, Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International, share a group photo with Mathenge and son Geoff  Kihato during the ceremony.

  Mathenge was awarded the overall ‘CNN MultiChoice African Journalist of the Year’ Award for his work ‘Images of Terror’, which appeared in Kenyan daily print newspaper The Standard and was chosen from entries spanning 38 nations across the African continent.
  Mathenge said: “It’s a great honor, and I’m humbled to receive this award. All finalists who are here deserve this award. I hope it will motivate men, women and children of good will all over the world to fight terrorism. Memories fade with time, but pictures don’t. We felt it necessary to capture each and every moment so that generations to come may see the horror.”
  President Kikwete, Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa and Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International, presented Mathenge with the Award.
  Chairperson of the judging panel, Ferial Haffajee, said: “Joseph Mathenge’s photographs so eloquently captured one of Africa’s toughest 21st Century moments that they were worth a thousand words. That said, the quality of all the winners’ works made the contest a tightly run one.”
  Mathenge, winner in the Mohamed Amin Photography category, was among 28 finalists from 10 countries who attended the Awards ceremony as the culmination of a four day programme of workshops, media forums, networking, and sightseeing.
  Deborah Rayner, SVP International Newsgathering TV and Digital, CNN International, said: “This evening’s journalists represent the very best in African journalism. By entering these awards, they have proved they have the determination, professionalism and courage to showcase Africa’s stories to the world. I congratulate each and every one.”
  Nico Meyer, CEO MultiChoice Africa, said: “Congratulations to all the 2014 winners, we are proud to recognise your excellence in journalism and to reward you for your courage in telling stories that would have otherwise remained untold. We believe the CNN MultiChoice African Journalist Awards has had a profound effect on the African media landscape and as MultiChoice Africa we remain committed to recognising excellence in journalism throughout Africa. We applaud all the nominees and winners for contributing to Africa’s growth and success.”
  Imtiaz Patel, Group CEO of MultiChoice South Africa, congratulated all the winners of this year's Awards: “I would like to thank all of the journalists who have entered this competition and in doing so have helped further develop this award as a platform for excellence in journalism.  Your dedication and commitment to tell stories that reflect the reality of our world is very encouraging.  A special congratulation to the winners announced tonight.  Your work echoes a great future for the role of the journalists and serves to further strengthen the role of the media in Africa.  You are indeed all winners and an inspiration to us all – you have made us very proud.”
  Now in its 19th year, the Awards are supported by a range of prestigious sponsors:  Coca-Cola; Ecobank; GE Africa; IPP Media, Tanzania; Merck Sharp & Dohme (MSD) and A24 Media.
  The overall CNN MultiChoice African Journalist 2014 wins a substantial cash prize, and a visit to CNN Centre in Atlanta, to attend the three week CNN Journalism Fellowship. All finalists receive a cash prize, and iPad Air, with runner-ups receiving an iPad mini.
  Story credit: CNN

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana Jumamosi Oktoba 18, 2014 
   Maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha 
  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi ofisa kadeti Yusup kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko Monduli jana.
   Rais Joseph Kabila wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Mwamtemi baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika mafunzo ya porini wakati wa hafla ya kutunuku kmaisheni baada kumaliza mafunzo ya kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika Chuo cha kijeshi monduli leo.
    Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakisimama kikakamavu wakati nyimbo za taifa za nchi hizo zikipigwa  wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha. Picha na Fred Maro

  0 0

  More than 100 International Mediators, envoys and African Former Heads of State have confirmed to participate in the fifth retreat scheduled to be held in Arusha from 21st to 23rd October, 2014.
  The retreat, aimed at addressing threats and emerging challenges on the continent will, among other things,  device a coherent strategy to silence the guns and enhancing economical growth, justice, peace and stability in the continent.
  A statement issued by Tanzania Information Services in Dar-es-salaam yesterday said, the meeting is expected to adopt a long term and structural approach to Africa’s understanding and responding to violence and instability.
  “The retreat will attempt to answer one of the pertinent question of what are the long term response required to respond to Africa’s instability and address emerging threats of terrorism and climate change to peace, security and stability.” The statement said.
  The opening session of the retreat will include an introductory address by H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, UN Secretary General, Dr. Ban Ki-Moon  and AU Commission Chairperson Nkosazana Dlamini Zuma.
  This is the second event organized this year in response to the clarion call to silence the guns by the year 2020 following the retreat held in Durban South Africa in April 2014. That month also saw the AU Peace and Security Council holding a special session on the campaign against guns.
  Among the confirmed participants include Former President of South Africa, Thabo Mbeki, Former President of Mali, Alpha Omar Konare, Former President of Burundi, Pierre Buyoya and Former OAU Secretary General, Dr. Salim Ahmed Salim.
  The meeting will also draw participants from African Development Bank, UN, representatives from regional economical blocks, World Bank, League of Arab States, African bilateral partners, UN Security Council, European Union and team of Experts.
  Ambassador Augustine Mahiga, a former Tanzanian Permanent Representative to the UN in New York is among 23 experts who have been invited to attend the retreat in the tourism city of Arusha
  Issued by:
  The Director, Tanzania Information Services - MAELEZO,
  DAR ES SALAAM. 


  0 0

   Timu ya Nyika stars wakimalizia kupiga kasia kwenye Ziwa Tanganyika ambao ni mabingwa wa Mkoa na watauwakilisha Mkoa kwenye mashindano ya kanda tarehe 6 Novemba jijini Mwanza
   Washiriki wanawake wakipiga kasia katika mashindano ya kupiga kasia kwa kutimia mitumbwi ndani ya ziwa Tanganyika
   Washindani wakijiandaa na mchuano
   Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno
  Kiongozi wa washindi wa kwanza kwa upande wa wanawake kutoka kikundi cha Katonga Beach akionyesha kitita chake kwa mashabiki
  Kiongozi wa kikundi cha wanaume cha Nyika Stars ambao ndo mabingwa wa Mkoa akionyesha kitita cha shilingi laki 9
  Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma
  KAMPUNI ya bia Tanzania(TBL)kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager imefanya uzinduzi wa mashindano ya mitumbwi ya  kupiga kasia kwa kanda ya ziwa leo Kigoma katika fukwe za eneo la ya Bangwe.

  Akizindua mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani maneno ametoa shukrani kwa uongozi wa bia ya balimi Lager kwa kuupa Mkoa wa Kigoma heshima ya kuwa wenyeji wa uzinduzi wa mashindano hayo kikanda.

  Maneno alisema kuwa mchezo siyo mpira pekee hata kupiga kasia pia ni mchezo pia kinachotakiwa ni wachezaji wote kuzingatia nidhamu na kufuata masharti na maelekezo pia aliwataka wadhamini kuongeza zawadi ili iwe kivutio kwa washiriki wengi kujitokeza mwakani.

  ''Nina waomba ndugu zangu mlioshinda katika vikundi vyenu fedha hizi tulizowapa isiwe ndiyo chanzo cha kwenda kulumbana bali mzitumie kwa uwekezaji na faida itakayopatikana katika uwekezaji huo ndo mgawane''alisema Mkuu wa Wilaya

  Alisema kupitia mashindano hayo ya mitumbwi yanayofanyika kila mwaka Mkoani hapa ni njia mojawapo ya kuwaweka watu pamoja kushirikiana na kuboresha maslahi yao pamoja biashara zao.

  Mashindano hayo yalishirikisha jinsia zote wanawake na wanaume,kikundi cha wanaume kiitwacho nyika Star kilifanikiwa kunyakua ubingwa wa kwanza na kuondoka na kitita cha shilingi laki tisa(900000)na upande wa wanawake kikundi kilichoongoza ni Katonga Beach nacho kiliondoka na kitita cha shilingi laki saba(700000).

  Naye mshindi wa pili kwa upande wa wanaume ni kikundi cha Kikumba  ambao walizawadiwa kiasi cha shilingi laki saba(700000)na upande wa wanawake nafasi ya pili ilikamatwa na kikundi cha warumona ambao walizawadiwa shilingi laki sita(600000).

  Mshindi wa tatu hadi nae kwa wanaume ambaye ni kikundi cha Mwakaye ameondoka na kitita cha shilingi laki nne na nusu(450000)na washindi wanne hadi wa kumi walizawadiwa kifuta jacho cha shilingi laki tatu ambao ni vikundi vya (4)Katonga A(5)Umoja(6)Kalalangabo(7)Tanganyika stars(8)Sigunga(9)Balimi(Bushabani).

  Kwa upande wanawake msindi wa tatu alipewa kitita cha shilingi laki tatu na mshindi wa nne hadi wa kumi walipewa kifuta jasho cha shilingi laki mbili na nusu(250000)kila kikundi ambao ni(4)Lembo)(5)Tanganyika(6)Fasta star(7)Mama Kikongwe(8)Kirasa(9)Mwamgongo(10)Upendo.

older | 1 | .... | 611 | 612 | (Page 613) | 614 | 615 | .... | 3286 | newer