Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 610 | 611 | (Page 612) | 613 | 614 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti  akizungumza jambo wakati akifungua kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Na Mwandishi wetu
  Maafisa habari mbalimbali kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa kutoa taarifa kwa wananchi.

  Kongamano hilo linafuatia matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa.


  Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha ya kupata mwaliko. 

   Mwanasheria kutoka Taasisi Kitaifa ya Msaada wa Kisheria (National Organization of Legal Assistance-nola)  Bwana James Malenga akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kulia) akitoa msaada wa mabati kwa wananchi waliothiriwa na mafuriko jimboni kwake.  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kushoto) akitoa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Kitongoji cha Nyamagana ,Kata ya Bwawani kwaajili kuibua vipaji.


  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kushoto) akitoa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Kitongoji cha Kazamoyo,Kata ya Bwawani kwaajili kuibua vipaji.


  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kushoto) akitoa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Kitongoji cha Kazamoyo,Kata ya Bwawani kwaajili kuibua vipaji.

  Mbunge wa Arumeru Magharibi,mkoani Arusha,Godluck Ole Medeye(kulia) akikagua caravati linalowaondolea kero ya mawasiliano.Picha na woindeshizza blog

  0 0
 • 10/17/14--04:36: Article 3


 • 0 0

   Meneja wa Msanii wa Kimataifa T.I anayetarajiwa kuwasili chini , kwa ajiri ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Fiesta 2014 hapo kesho katika viwanja vya Lidaz Club jijini Dar, Jonson Geter wa kwanza kushoto akifafanua jambo moja ya swali lililoulizwa na mmoja  wasanii walioshiriki kwenye semina ya fursa ndogo ya Wasanii na wadau wa muziki iliyofanyika kwenye ukumbi wa Litle Theather,jijini Dar,Pichani kulia ni Prodyuza  mahiri wa Muziki wa hapa nchini anayemiliki studioo yake ya Bongo Records,P-Funk Majani.

  Aidha Uongozi wa msanii huyo T.I leo umeshiriki  kwenye semina ya fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze.
  Sehemu ya meza kuu iliyoshiriki semina ya fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze.
  Mwimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Skylight Band,Annet Kushaba akiuliza swali kwa uongozi wa msanii T.I kutoka nchini Marekani,kwenye fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze. 
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva atambulikae kwa jina la kisanii la  CPWA akiuliza swali kwenye semina ya fursa ndogo iliofanyika leo jjini dar.

   Msanii wa bongofleva ajulikanae kwa jinal a Witness akiuliza swali kwa uongozi wa msanii T.I kutoka nchini Marekani,kwenye fursa Ndogo ya wasanii na wadau wa muziki iliofanyika kwenye ukumbi wa Little Theather ,jijini Dar kuzungumzia Fursa zilizoko katika biashara ya Muziki, Mada iliyoongelewa ni namna ya kujiongeza kwa kuangalia fursa za mbalimbalizi zilizomo kwenye tasnia hiyo na wakati msanii anapokuwa kwenye kilele cha mafanikio.  Fursa 2014 inakaulimbiu ya Jitathmini Jiamini Jiongeze.  
   Baadhi ya wapenzi na wadau wa muziki walioshiriki senina ya fursa wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
   Baadhi ya wapenzi na wadau wa muziki walishiriki pia.Kulia ni Msanii kutoka kampuni ya NO Fake Zone Linah na Rechael kutoka THT.

  0 0


   Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanga makabrasha tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo masuala ya kujiendesha kiuchumi na mipango ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanajadiliwa.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza juu ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi. 

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara hiyo Mnazimmoja kuhusu uzinduzi wa chanjo ya kuzuia Surua na Rubella kwa watoto utakaofanyika kesho Oktoba 18 katika kijiji cha Uroa Mkoa Kusini Unguja.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Naibu Waziri wa Afya uliozungumiza uzinduzi wa chanjo ya kuzuia Surua na Rubella itakayoanza kesho kijiji cha Uroa.
   Mratibu wa chanjo Zanzibar Yussuf Haji Makame akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna chanjo hiyo itakavyoendeshwa nchi nzima kwa muda wa wiki moja kuanzia kesho. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Ikulu Bw. Peter Ilomo amewashauri watanzania kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ili kujiongezea kipato na hatimaye kuishi ya staha.

  Bw. Ilomo alisema hayo Mjini Bagamoyo wakati wa semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa ajili ya Maafisa Rasilimali Watu kutoka wakala mbalimbali za Serikali

  Kutokana na mabadiliko kwenye sekta ya hifadhi ya jamii, PSPF ilianzisha Mpango wa Uchangiaji wa Hiari maarufu kama PSS ili kuweza kuwahudumia Watanzania wote ambao wanahitaji huduma za hifadhi ya jamii ambao walikosa fursa hiyo huko nyuma.

  “Mpango huu ni mkombozi kwani unazidi kukuongezea kipato na kukufanya uishi maisha yenye staha sasa na hata wakati wa ustaafu wako. Mpango huu pia unatoa ruksa kwa mtu asiye raia wa Tanzania lakini anafanyakazi hapa nchini kihalali kuwa mwanachama” alisema Bw. Ilomo.

  Akizungumzia juu ya ujio ya kanuni moja ya ukokotoaji wa mafao, Bw. Ilomo alisema, “Kuwepo kwa kanuni moja ya ukokotoaji mafao ni changamoto kwa  Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kwa kuwa kigezo kikubwa cha kuvutia wanachama kitakuwa ni ubora katika huduma na mafao ya muda mfupi. Hivyo, nawaagiza watendaji wote wa PSPF kuhakikisha mnatumia vyema fursa hii kutoa elimu sahihi kwa watendaji hawa muhimu katika utumishi wa umma hapa nchini”.

  Kutokana na Wizara ya Kazi na Ajira kutangaza kuwa Mifuko yote ya Hifadhi ya itakuwa ikitoa mafao yanayolingana, alisema wanachama wa PSPF waliokuwepo hadi tarehe 30/6/2014 watalipwa kwa utaratibu wa zamani na wote walioajiriwa kuanzia Julai 1, 2014 watalipwa mafao yao kwa mujibu wa kanuni mpya.

  Katibu Mkuu huyo kutoka ofisi ya Rais aliipongeza PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuongeza, “ Semina hizi ni muhimu kwani zinatoa fursa ya kuonana na wadau na kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kwa manufaa ya Mfuko na wanachama wake”.

  Awali akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliwahakikishia washiriki wote wa semina hiyo kwamba PSPF itahakikisha inafikia dira yeke ambayo ni kuwa mtoa huduma bora wa hifadhi ya jamii nchini, na kufanyakazi kwa mujibu wa dhima ya Mfuko ambayo ni kutoa huduma zenye ushindani katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wateja wake kwa kutumia watumishi wenye ari ya kazi na teknolojia inayofaa.

  Katika kuhakikisha inafikia dira yake na kuishi dhima yake, Bw. Mayingu aliahidi kwamba PSPF itaendelea kutekeleza majukumu yetu ya utendaji wa kila siku ikiongozwa na uwajibikaji, wajibu, muitikio, nidhamu, juhudi, uwazi na unyenyekevu kwa wote.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akizunfumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa maafisa rasilimali watu kutoka wakala za serikali iliyofanyika mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Alhamisi Oktoba 16, 2014.
  Katibu Mkuu Ikulu,Peter Ilomo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa maafisa rasilimali watu huko Bagamoyo mkoani Pwani, Alhamisi Oktoba 16, 2014. Warsha hiyo ililenga kuwapatia elimu waajiri kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwa wanachama wake.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kushoto) akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekeleza wa Miradi (PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa (wa pili kulia) mara baada ya kuhudhuria hivi karibuni maabara inayochambua miradi ya afya itakayoingia katika BRN. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Bw. Mahmoud Thabit Kombo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt, Mohammed Saleh Jidawi (kulia).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa), Hawa Ghasia akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Bw. Mahmoud Thabit Kombo wakati viongozi hao walipotembelea maabara inayochambua miradi ya afya itakayoingia katika BRN.
  Baadhi ya wawakilishi wa Wabia wa Maendeleo waliopo nchini wakifuatilia majadiliano jana jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea maabara ambayo inachambua miradi ya sekta ya afya itakayoingizwa katika BRN.
  Badhi ya washiriki wa maabara inayojadili miradi ya afya itakayoingizwa katika BRN wakifurahia zawadi waliyopewa na Waziri wa Afya (hayuko pichani) baada ya kundi lao kushinda katika uwasilishaji wa miradi ya afya itakayochambuliwa zaidi ili kuingia katika BRN.

  0 0

  pichani ni Mhe, Balozi Salome Sijaona (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wa Kampuni ya M.M.C wauzaji wa Kahawa ya Kilimanjaro Premium Brand kutoka Tanzania nchini Japan, na watumishi wengine wa Ubalozi, M.MC walifika  Ofisi za Ubalozi kuelezea mafanikio ya mauzo ya kahawa hii maalum ya Tanzania kwenye treini.

  Ujumbe wa M.M.C ulieleza kuwa siku ya kwanza ya kampeni hii maalum kwa Tanzania na Tokaido Shinkasen jumla ya vikombe vya kawahawa 9999 viliuzwa, na kumbe mauzo yanaongezeka siku baada ya siku.

  Kwa Tanzania imekuwa ni fursa nzuri ya kuitangaza nchi pamoja na vivutio vya utalii kama mlima Kilimanjaro na utamaduni wa michoro ya picha za Tingatinga.

  Ubalozi wa Tanzania
  Tokyo

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) (katikati) kuzungumza na watumishi katika hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda kwa kishindo katika Michezo ya SHIMIWI 2014.Kulia ni Mwenyekiti wa Michezo Utumishi Bw.Lumuli Mtaki.
  Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka Utumishi Bw.Hassan Ligoneko akimkabidhi kombe Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) wakati wa hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi iliyofanyika ukumbi wa Utumishi.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kuzipongeza timu zilizoshinda mashindano ya SHIMIWI yaliyomalizika mjini Morogoro hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Michezo wa Utumishi Bw.Lumuli Mtaki.


  0 0

  DSC_0209
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Jaji Francis Mtungi na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na Nyuma kabisa ni Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza.
  DSC_0232
  Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alipomtembelea leo na kufanya nae mazungumzo juu masuala mbalimbali ya maendeleo likiwemo suala la elimu na changamoto zake katika mkoa wa Dodoma.
  DSC_0237
  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph, Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza walipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake leo.


  0 0

  Jina: Deo  Mbasa 
  Vitu vilivyopotea ni begi lililokuwa na;
  1. Laptop aina ya Accer
  2. Simu kubwa ya Kirusi aina ya Oysters
  3. Vyeti vya masomo
       a) Cheti cha form four - NECTA
       b) Cheti cha form six - NECTA
       c) Cheti cha Chuo (Digrii ya Kwanza ya Elimu Jamii na Ualimu) -UDSM
  4. Vitambulisho mbalimbali ikiwemo kitambulisho cha Taifa.
  Vyeti na nyaraka zote zinasomeka kwa jina la Deo Mbasa Daudi.
  Mahali vilipopotelea ni maeneo ya Ofisi ya Posta Kijitonyama, jirani na TBC.
  Taarifa imetolewa Polisi Mabatini, Kijitonyama kwa RB Namba KJN/RB/9576/2014.
  Tafadhali naomba msaada wenu katika namba hizi;

  Mbasa
   0765 191 108 / 0716 646 177

  0 0

  Zoezi Ushirikiano imara limefunguliwa leo hii nchini Burundi katika mkoa wa Mwaro, Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi mhe.Prosper Bazombanza.

  Katika ufunguzi huo mhe Bazombanza amesema kuwa ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki umetokana na makubaliano ya wakuu wa nchi wanachama yaliyofanyika mwaka 2001,hivyo kuzitaka nchi shiriki kuenzi makubaliano hayo kwa kushiriki mara kwa mara katika mazoezi hayo. 

   Amesema ushiriki katika mazoezi haya unajenga kujiamini kwa majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwafanya wanajeshi wa Jumuiya hii kutambua kuwa wapo pamoja katika masuala ya ulinzi. Gwaride rasmi lilipita mbele ya mgeni rasmi kwa heshma huku Wakuu wa Majeshi na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakihudhuria sherehe hizo. 

   Kwa upande wa Tanzania sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali James Mwakibola pamoja na mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant Mutashobya ambaye kabla ya ufunguzi wa zoezi hili wakati wote alikuwa akivipokea vikundi kutoka Tanzania akianzia kupokea kikundi cha JWTZ kilichokwenda Burundi kwa njia ya barabara katika mpaka wa kabanga na baadaye kupokea kikundi cha wanamaji wa JWTZ kupitia mpaka wa Kagunga. 

   Zoezi ushirikiano imara ni moja ya mazoezi muhimu yanayolifanya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania kuendelea kuwa moja ya majeshi yenye weledi wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake kitaifa na kimataifa. Zoezi hilo linafanyika nchini Burundi kuanzia tarehe 13 hadi 26 Oct 2014 ambapo hushirikisha majeshi ya nchi za jumuiya ya afrika mashariki za Burundi,Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda. 

   Mazoezi ya pamoja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yameendelea kufanya majeshi katika ukanda huu kuwa na weledi kiutendaji hii ni kutokana na majeshi haya kubadilishana uzoefu katika Nyanja za kiulinzi na usalama. Wakati huohuo Tanzania imeteuliwa kuongoza zoezi hilo huku Brigedia Jenerali Joseph Cosmas Chengelela kuchukuwa jukumu la kuongoza kombaini ya vikundi vitakavyo shiriki zoezi hilo. 

  Akiongea mara baada ya ufunguzi, Mkuu wa zoezi kutoka Tanzanina Brigedia Jenerali Joseph Chengelela amesema ushiriki wa JWTZ katika mazoezi haya unalifanya JWTZ kuwa miongoni mwa majeshi bora katika ukanda huu kwani ni njia moja wapo ya kuwafanya maafisa na askari kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa majeshi mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Brigedia Jenerali Joseph Chengelela (kushoto)akimkabidhi bendera ya Afrika Mashariki msaidizi wa zoezi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa mgeni rasmi hayupo pichani siku ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
  Meja Jenerali James Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali Joseph Chengelela wa tano kulia na Mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
  Picha ya Pamoja ya maofisa wa serikali ya Burundi na Maafisa Wakuu wa Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI


  0 0


  0 0

   

  Ankal Michuzi, 
  Salam nyingi na hongera sana. Katika kuendeleza libeneke, nami nimeona sina budi kuunga mkono juhudi za kukuza lugha yetu kwa njia hii. Naomba nitangaze blogu mpya ya kawaida lakini yenye mambo yanayovutia sana kusoma na kufahamu.

  Blogu hii itajikita zaidi katika kuelezea mambo mbalimbali kwa muundo mwepesi na kwa Kiswahili ili kukuza uelewa wa mambo mengi katika jamii yetu ambayo yameachwa katika lugha ngumu za kisayansi na hivyo kuwanyima fursa watu wengi kuyafahamu kiundani.  Hivyo tutakuwa tukitoa uchambuzi wa mambo na “updates” au taarifa katika nyanja za sayansi,  saikolojia na elimu nyingine zenye kuvutia sana. 


  Ni matumaini yangu kwamba kupitia blog hii, wakubwa kwa wadogo watajifunza na pia kuchangia elimu mbalimbali zitakazowagusa au kuwavutia.    


  0 0

  Na. Ally Mataula – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. 
  Meya wa Halmashauri Manispaa ya Tabora Mhe. Gulam Hussein Dewji Remtullah amefikishwa mbele ya Baraza la Maadili kujibu tuhuma zinazomkabili. 
  Akisoma hati ya malalamiko mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Jaji (Mst.) Hamisi Msumi, Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Hassan Mayunga alilieleza Baraza hilo kuwa Mlalamikiwa akiwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa makusudi kabisa alikiuka Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kukiuka kifungu cha 6(a) na (d), 12(1) na 15 (b) vyote vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995. 
  Bw. Mayunga alilifafanulia Baraza kuwa Mhe. Gulam Hussein Dewji analalamikiwa kwa kujinufaisha binafsi kwa kutumia fedha kiasi cha shilingi 2,672,000/= mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa ajili ya safari ya nchini Marekani huku safari hiyo ikiwa imedhaminiwa na kugharamiwa na Wadhamini waliomualika kutembelea nchini Marekani mnamo Mwezi Aprili, 2011. Pia, Mhe Gulam Dewji analalamikiwa kuvunja Sheria ya Maadili makusudi kwa kipindi cha miaka minne yaani kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 kwa kutoa Tamko la uongo kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma huku akijua kuwa ni kosa kufanya hivyo. 
  Kosa lingine analolalamikiwa Mhe. Gulam Dewji ni kushindwa kutamka rasilimali zake ambazo ni pamoja na viwanja Na. 100 kitalu G, 158 Kitalu G, 637 kitalu D, 99 kitalu F, 206 kitalu C pamoja na nyumba moja iliyopo kwenye kiwanja Na. 42 kitalu G vyote vikiwa katika Manispaa ya Tabora. Aidha, Mali nyingine anazodaiwa kushindwa kuzitamka Mhe. Gulam Dewji ni pikipiki 422, duka moja, magari namba T 327 ADS Toyota Hilux, T 842 AWR Toyota Rav4, na T 110 CMW Toyota Rav4. 
   Bw. Mayunga alimaliza kumsomea hati ya malalamiko Mhe. Gulam Dewji kwa kulieleza Baraza kuwa kwa kufanya hayo na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu ni ukiukaji wa maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu cha 6(a) na (d), 12(1) na 15(b) vyote ni vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. 
   Aidha, Bw. Mayunga aliliomba Baraza la Maadili lenye mamlaka ya kisheria ya kufanya uchunguzi wa kina na kumtaka mlalamikiwa kutoa taarifa bayana kuhusu rasilimali zake na kutoa hati na kumbukumbu ambazo ziko chini ya udhibiti wake kuhusu rasilimali hizo kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria. 
  Naye Shahidi wa upande wa walalamikija Bw. Gerald Mwaitebele ambaye ni Mtumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi - Tabora alilieleza Baraza la Maadili kuwa Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma – Kanda ya Magharibi Tabora walipata tuhuma saba za ukiukaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya Mlalamikiwa kupitia vyombo vya habari. 
  Bw. Mwaitebele aliendelea kulieleza Baraza hilo kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa awali walifanikiwa kupata ushahidi kwa malalamiko matatu na mengine hawakuweza kupata ushahidi na hivyo kuamua kuyaacha. 
   Kwa mujibu wa Bw. Mwaitebele tuhuma ambazo waliweza kupata uthibitisho baada ya uchunguzi wa awali ni pamoja na kutumia madaraka vibaya kwa kujinufaisha fedha za Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, kutumia vibaya madaraka kwa kujitwalia mali ambazo ni viwanja na kutoa tamko la uongo kwa kushindwa kutaja mali zake yeye binafsi, mke pamoja na watoto wake. 
  Hata hivyo Mlalamikiwa Mhe. Gulam Hussein Dewji alikana malalamiko yote dhidi yake na Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Hamisi Msumi aliahirisha kusikiliza shauri hilo hadi tarehe nyingine itakayotangazwa hapo baadae. 
  Baraza la Maadili ni chombo cha kisheria chini ya fungu la 26 la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma lenye mamlaka ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko yanayohusu ukukaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya kiongozi yeyote. 
   Kwa mujibu wa fungu la 26 (8) linasema kuwa katika taarifa yake, Baraza linaweza kutoa mapendekezo kuhusu hatua za kiutawala, mashitaka ya jinai au hatua nyingine zozote za kuchukuliwa dhidi ya kiongozi husika kwa kadri litakavyoona inafaa.
   Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mhe. Gulam Hussein Dewji (aliyeshika chupa ya maji) akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutoka kuhojiwa na Baraza la Maadili juu ya tuhuma zinazomkabili kuhusu ukiukaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam.

  Shahidi upande wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Gerald Mwaitebele kushoto akizungumza na Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Filotheus Manula mara baada ya kutoa ushahidi wake kuhusu tuhuma za ukiukaji wa Sheria ya Maadili zinazomkabili Meya wa Manispaa ya Tabora  Mhe. Gulam Dewji mbele ya Baraza la Maadili katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam.


  0 0  0 0

  Mega sport.com

  Hakuna takwimu sahihi za mashabiki wa klabu kongwe nchini za Simba na Yanga ni wangapi, lakini si chini ya watu milioni 20, akili zao zitasimama kwa takriban dk 90 na kupata kiwewe cha huzuni au furaha wakati miamba hiyo itakapovaana hapo kesho Taifa.

  Joto la mechi hiyo tayari limepanda Zaidi ya nyuzi 90 huku kukiwa na hisia tofauti zikiwemo za udanganyifu wa wachezaji kuwa majeruhi ili kuteka akili za wapinzani.

  Tayari kuna taarifa Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu akiwemo nahodha, Nadir Haroub Canavaro, kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima na Mbrazil Genilson Santana (Jaja) ni majeruhi na huenda wasicheze.


  Na kama hiyo itakuwa kweli, basi itakuwa ni kicheko kwa wanamsimbazi kwani kwao itakuwa kama vile kuangusha silaha mikononi mwa waasi.

  Simba pia, imetangaza majeruhi wachezaji wake muhimu akiwepo kipa namba moja, Ivo Mapunda, kukiwa na habari kuumia kwake mwezi uliopita kidoleni, huenda asiwe golini na Husein Sharif “Casilas”, kipa mwingine, pia akioonekana majeruhi, akikokotwa katika kiti cha wagonjwa  wakati kikosi cha Simba kiliporejea kutoka Bondeni, Afrika ya Kusini kwa Mzee Madiba.

  Yanga inategemea bunduki zake chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo, ambaye yupo nyuma ya kiongozi wa lii (Mtibwa Sugar) akiwa na pointi sita.

  Simba, ikiwa chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri ambaye, anayejivunia rekodi ya kuchukua ubingwa msimu wa mwaka 1999/2010 bila ya kufungwa, itakuwa na kibarua kigumu cha kufufua matumaini ya mashabikin wake baada ya kuanza ligi kwa kususua, kwa kupata droo tatu ikiwa nyumbani (dhidi ya Coastal Union, Polisi Morogoro na Stand United).


   Aidha, faraja kwa Simba ni uwezekano wa kuwamo kikosini kwa mshambuliaji wake mahiri,Mganda Emmanuel Okwi, ambaye alisajili akitokea Yanga katika usajili wa dirisha dogo na kuzua mvutano baina ya timu hizo mbili juu ya uhalali wake wa uhamisho. Pia itamtegemea Amisi Tambwe, ambaye ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita.

  Aidha, kama ilivyo ada ya timu hizo zinapokutana, tayari hisia za uchawi zikiwa zinatawala ili kutafuta ushindi, kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
  Mara nyingi viongozi wa timu hizi hukanusha tuhuma za kujihusiha na uchawi kwa kudai kuwa ni uvumu na uzushi ambao upande mwingine wa upinzani huutoa ili kuweka akiba kuwa kama watafungwa basi ni kwa njia ya giza.

  Kwa kipindi hiki, nazi huwa adimu na silaha kubwa kwa kuumiza upande mwingine huku njiwa wakirushwa na hirizi kufukiwa sehemu za magoli.
  Hata utaratibu wa kuingia uwanjani, si ajabu kuvunjwa, kwa wachezaji kutokea katika majukwaa ya mashabiki, tena kwa mafungu.

  0 0


older | 1 | .... | 610 | 611 | (Page 612) | 613 | 614 | .... | 3284 | newer